سورة فصلت

Surat Fussilat kwa Kiswahili

Zilizopambanuliwa

Msahafu

Mishary Rashid AlafasyPakua MP3Pakua PDF

Surat Fussilat (فصلت) ni sura ya 41 katika Qur’ani na ina aya 54. Jina lake lina maana ya “Zilizopambanuliwa”. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na inaenea katika juzuu za 24 na 25.

Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat Fussilat yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.

Surat Fussilat kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

  1. حمٓ۝١

    Hameem

    H'a Mim .1

    Maelezo
    [1] (H'a Mim) Hizi harufi mbili katika harufi za alifbete zilio fungulia Sura hii kama ilivyo ada ya Qur'ani katika Sura nyingi, ili kuzindua watu watanabahi, na pia kuonyesha dalili ya muujiza wa Qur'ani.
  2. تَنزِيلٌ مِّنَ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ۝٢

    Tanzeelun mina alrrahmani alrraheemi

    Uteremsho huu umetoka kwa Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.2

    Maelezo
    [2] Kitabu hichi ni mteremsho wa namna ya peke yake, kutokana na Mneemeshaji wa neema kubwa na neema ndogo.
  3. كِتَـٰبٌ فُصِّلَتْ ءَايَـٰتُهُۥ قُرْءَانًا عَرَبِيًّا لِّقَوْمٍ يَعْلَمُونَ۝٣

    Kitabun fussilat ayatuhu quranan ʿarabiyyan liqawmin yaʿlamoona

    Hichi ni Kitabu kilicho pambanuliwa Aya zake, cha kusomwa kwa Kiarabu kwa watu wanao jua.3

    Maelezo
    [3] Kitabu hichi ni namna ya peke yake kwa uzuri wake kwa matamshi na ibara yake ya utungaji, na kwa maana inavyo pambanua baina Haki na baat'ili, na bishara na onyo, na kuzitengeneza nafsi, na kupiga mifano, na kubainisha hukumu. Nacho kinasomwa kwa ulimi wa Kiarabu, chepesi kukifahamu kwa watu wanao jua.
  4. بَشِيرًا وَنَذِيرًا فَأَعْرَضَ أَكْثَرُهُمْ فَهُمْ لَا يَسْمَعُونَ۝٤

    Basheeran wanatheeran faaʿrada aktharuhum fahum la yasmaʿoona

    Kitoacho khabari njema, na chenye kuonya. Lakini wengi katika wao wamepuuza; kwa hivyo hawasikii.4

    Maelezo
    [4] Chenye kuwapa khabari njema Waumini wenye kutenda kuwa watapata neema iliyo andaliwa kwa ajili yao, na kuwakhofisha wanao kanusha kuwa watapata adhabu chungu iliyo andaliwa kwa ajili yao. Lakini wengi walikitupilia mbali, wala wasinafiike nacho, kama kwamba hawakusikia.
  5. وَقَالُوا۟ قُلُوبُنَا فِىٓ أَكِنَّةٍ مِّمَّا تَدْعُونَآ إِلَيْهِ وَفِىٓ ءَاذَانِنَا وَقْرٌ وَمِنۢ بَيْنِنَا وَبَيْنِكَ حِجَابٌ فَٱعْمَلْ إِنَّنَا عَـٰمِلُونَ۝٥

    Waqaloo quloobuna fee akinnatin mimma tadʿoona ilayhi wafee athanina waqrun wamin baynina wabaynika hijabun faiʿmal innana ʿamiloona

    Na wakasema: Nyoyo zetu zimo katika vifuniko kwa hayo unayo tuitia, na masikio yetu yana uziwi, na baina yetu na wewe lipo pazia. Basi wewe tenda, nasi tunatenda.5

    Maelezo
    [5] Na makafiri wakamwambia Mtume s.a.w.: Nyoyo zetu zimo katika vifuniko vizito kwa hayo unayo tuitia yaliyo khusu Tawhidi (Upweke) wa Mwenyezi Mungu. Na masikioni mwetu mna uziwi, basi hayasikii hayo unayo tulingania. Na baina yetu na wewe lipo pazia nene linalo tuzuia kukubali hayo uliyo tuletea. Basi fanya utakalo, na sisi tunafanya tutakalo.
  6. قُلْ إِنَّمَآ أَنَا۠ بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ يُوحَىٰٓ إِلَىَّ أَنَّمَآ إِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَٰحِدٌ فَٱسْتَقِيمُوٓا۟ إِلَيْهِ وَٱسْتَغْفِرُوهُ ۗ وَوَيْلٌ لِّلْمُشْرِكِينَ۝٦

    Qul innama ana basharun mithlukum yooha ilayya annama ilahukum ilahun wahidun faistaqeemoo ilayhi waistaghfiroohu wawaylun lilmushrikeena

    Sema: Hakika mimi ni mtu kama nyinyi; inafunuliwa kwangu ya kwamba Mungu wenu ni Mungu Mmoja tu. Basi nyookeni sawa kumwendea Yeye, na mumtake msamaha, na ole wao wanao mshirikisha!6

    Maelezo
    [6] Ewe Mtume! Waambie: Hakika mimi si chochote ila ni mtu mfano wenu nyinyi, napata Wahyi (Ufunuo) kutoka kwa Mwenyezi Mungu, kwamba wa kuabudiwa kwa haki na nyinyi ni Mungu Mmoja tu. Basi fuateni Njia Iliyo Nyooka ya kwendea kwake! Na mtake kwake msamaha kwa madhambi yenu. Na washirikina wasio toa Zaka kuwapa wanao stahiki watapata adhabu kali. Na wao tu, si wenginewe, ndio wanao kataa kuwa upo uhai wa Akhera.
  7. ٱلَّذِينَ لَا يُؤْتُونَ ٱلزَّكَوٰةَ وَهُم بِٱلْـَٔاخِرَةِ هُمْ كَـٰفِرُونَ۝٧

    Allatheena la yutoona alzzakata wahum bialakhirati hum kafiroona

    Ambao hawatoi Zaka na wanaikataa Akhera.7

    Maelezo
    [7] Na washirikina wasio toa Zaka kuwapa wanao stahiki watapata adhabu kali. Na wao tu, si wenginewe, ndio wanao kataa kuwa upo uhai wa Akhera.
  8. إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ لَهُمْ أَجْرٌ غَيْرُ مَمْنُونٍ۝٨

    Inna allatheena amanoo waʿamiloo alssalihati lahum ajrun ghayru mamnoonin

    Hakika wanao amini na wakatenda mema watakuwa na ujira usio na ukomo.8

    Maelezo
    [8] Hakika Waumini wanao tenda mema watapata malipo mazuri yasiyo katika.
  9. ۞ قُلْ أَئِنَّكُمْ لَتَكْفُرُونَ بِٱلَّذِى خَلَقَ ٱلْأَرْضَ فِى يَوْمَيْنِ وَتَجْعَلُونَ لَهُۥٓ أَندَادًا ۚ ذَٰلِكَ رَبُّ ٱلْعَـٰلَمِينَ۝٩

    Qul ainnakum latakfuroona biallathee khalaqa alarda fee yawmayni watajʿaloona lahu andadan thalika rabbu alʿalameena

    Sema: Hivyo nyinyi mnamkataa aliye umba ardhi katika siku mbili, na mnamfanyia washirika? Huyu ndiye Mola Mlezi wa walimwengu wote.9

    Maelezo
    [9] Ewe Mtume! Waambie hawa washirikina: Ama nyinyi mnastaajabisha! Mnamkataa Mwenyezi Mungu aliye iumba ardhi kwa siku mbili, na huku juu ya hayo, mnamfanyia washirika wa kushirikiana naye huyo Muumba ardhi, Mmiliki wa walimwengu wote na Mlezi wao? Zimetajwa Siku moja au Siku nyingi katika Sura nyengine. Katika Surat Al-Hajj, Aya 47 Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: "Na kwa hakika siku moja kwa Mola wako Mlezi ni kama miaka elfu mnavyo hisabu nyinyi." Na katika Surat Assajdah, Aya 5 amesema Mtukufu: "Anapitisha mambo yote yaliyo baina ya mbingu na ardhi, kisha yanapanda kwake kwa siku moja tu ambayo kipimo chake ni miaka elfu mnayo hisabu." Na katika Surat Al-Ma'arij Mtukufu amesema: "Malaika na Roho hupanda kwake katika siku iliyo kadiri yake ni miaka elfu khamsini." Maoni ya kitaalamu: Vipimo vya wakati wanavyo vitumia watu vimefungamana na dunia na inavyo zunguka juu ya msumari-kati wake na kulizunguka jua. Mtu akitoka kwenye ardhi (dunia) akenda kwenye sayari nyengine za mbinguni vipimo hivyo vya nyakati vinabadilika kwa kuzidi au kwa kupungua. Na hizi Aya tukufu zinaonyesha ishara ya ukweli huu wa ki-ilimu, na ya kwamba zama au nyakati ni jambo la mlinganisho tu. Na bila ya shaka ipo miaka ya ki-ilimu ya Falaki ya kulinganisha yenye kumkinika kuifarikisha baina yao. Mwaka wa ki-jua wa duniani huhisabiwa kwa kupimwa wakati ambao dunia inachukua kulizunguka jua kwa ukamilifu mnamo siku 365, na ilhali sayari zilio karibu na jua kama U't'aarid (Mercury) humaliza safari yake ya kulizunguka jua mnamo siku 88, na upande mwengine sayari ya Blutu (Pluto) ambayo ndiyo sayari iliyo mbali mno na jua, na ndiyo inazunguka taratibu mno inachukua kuzunguka kwake mnamo miaka 250 kwa mujibu wa miaka yetu sisi.
  10. وَجَعَلَ فِيهَا رَوَٰسِىَ مِن فَوْقِهَا وَبَـٰرَكَ فِيهَا وَقَدَّرَ فِيهَآ أَقْوَٰتَهَا فِىٓ أَرْبَعَةِ أَيَّامٍ سَوَآءً لِّلسَّآئِلِينَ۝١٠

    Wajaʿala feeha rawasiya min fawqiha wabaraka feeha waqaddara feeha aqwataha fee arbaʿati ayyamin sawaan lilssaileena

    Na akaweka humo milima juu yake, na akabarikia humo na akakadiria humo chakula chake katika siku nne. Haya ni sawa kabisa kwa wanao uliza.10

    Maelezo
    [10] Naye Mwenyezi Mungu amesimamisha juu ya ardhi milima iliyo simama imara ili isiyumbe nanyi; na akakithirisha humo kheri nyingi, na akakadiria humo riziki kwa watu wake, kwa mujibu wa hikima yake, mnamo siku nne. Na nyinyi, juu ya haya, mnakwenda kumwekea washirika? Na Yeye amekadiria kila kitu bila ya upungufu wala kuzidi. Kufafanua huku katika uumbaji wa ardhi na vilio juu yake ni maelezo kwa hao wanao uliza.
  11. ثُمَّ ٱسْتَوَىٰٓ إِلَى ٱلسَّمَآءِ وَهِىَ دُخَانٌ فَقَالَ لَهَا وَلِلْأَرْضِ ٱئْتِيَا طَوْعًا أَوْ كَرْهًا قَالَتَآ أَتَيْنَا طَآئِعِينَ۝١١

    Thumma istawa ila alssamai wahiya dukhanun faqala laha walilardi itiya tawʿan aw karhan qalata atayna taiʿeena

    Kisha akazielekea mbingu, na zilikuwa moshi, akaziambia hizo na ardhi: Njooni, kwa khiari au kwa nguvu! Vyote viwili vikasema: Tumekuja nasi ni wat'iifu.11

    Maelezo
    [11] Kisha amekhusisha uweza wake na kuumba mbingu, nazo zilikuwa kama moshi, basi zikawapo. Na kuumba kwake mbingu na ardhi kwa mujibu wa mapendo yake ni jambo jepesi kwake, ni kama kukiambia kitu: Njoo ukipenda usipenda, nacho kikat'ii.
  12. فَقَضَىٰهُنَّ سَبْعَ سَمَـٰوَاتٍ فِى يَوْمَيْنِ وَأَوْحَىٰ فِى كُلِّ سَمَآءٍ أَمْرَهَا ۚ وَزَيَّنَّا ٱلسَّمَآءَ ٱلدُّنْيَا بِمَصَـٰبِيحَ وَحِفْظًا ۚ ذَٰلِكَ تَقْدِيرُ ٱلْعَزِيزِ ٱلْعَلِيمِ۝١٢

    Faqadahunna sabʿa samawatin fee yawmayni waawha fee kulli samain amraha wazayyanna alssamaa alddunya bimasabeeha wahifthan thalika taqdeeru alʿazeezi alʿaleemi

    Basi akazifanya mbingu saba kwa siku mbili, na akazipangia kila mbingu mambo yake. Na tukaipamba mbingu ya chini kwa mataa na kwa ulinzi. Hichi ndicho kipimo cha Mwenyezi Mungu Mwenye Kujua.12

    Maelezo
    [12] Na akatimiza kuumba mbingu saba mnamo siku mbili nyengine. Na akaweka katika kila mbingu alicho kiandalia na ilivyo pelekea hikima yake. Na akaipamba mbingu ya karibu na dunia kwa nyota zinazo ng'ara kama taa, kwa ajili ya uwongofu wasisikilize mashetani khabari za walio juu. Kuumba huko vilivyo ni mpango wa Mwenyezi Mungu asiye shindika, Mwenye kuzunguka kila kitu.
  13. فَإِنْ أَعْرَضُوا۟ فَقُلْ أَنذَرْتُكُمْ صَـٰعِقَةً مِّثْلَ صَـٰعِقَةِ عَادٍ وَثَمُودَ۝١٣

    Fain aʿradoo fuqul anthartukum saʿiqatan mithla saʿiqati ʿadin wathamooda

    Basi wakipuuza wewe sema: Nakuhadharisheni adhabu mfano wa adhabu ya A'di na Thamudi,13

    Maelezo
    [13] Basi washirikina wakipuuza Imani baada ya kuwekewa wazi dalili zake, wewe, Mtume, waambie: Nimekuonyeni msije kupatilizwa kwa adhabu kali kama iliyo wateketeza kina A'di na Thamudi.
  14. إِذْ جَآءَتْهُمُ ٱلرُّسُلُ مِنۢ بَيْنِ أَيْدِيهِمْ وَمِنْ خَلْفِهِمْ أَلَّا تَعْبُدُوٓا۟ إِلَّا ٱللَّهَ ۖ قَالُوا۟ لَوْ شَآءَ رَبُّنَا لَأَنزَلَ مَلَـٰٓئِكَةً فَإِنَّا بِمَآ أُرْسِلْتُم بِهِۦ كَـٰفِرُونَ۝١٤

    Ith jaathumu alrrusulu min bayni aydeehim wamin khalfihim alla taʿbudoo illa Allaha qaloo law shaa rabbuna laanzala malaikatan fainna bima orsiltum bihi kafiroona

    Walipo wajia Mitume mbele yao na nyuma yao wakawaambia: Msimuabudu ila Mwenyezi Mungu! Wakasema: Angeli taka Mola wetu Mlezi bila ya shaka angeli wateremsha Malaika. Basi sisi hakika tunayakataa hayo mliyo tumwa.14

    Maelezo
    [14] Walijiwa A'di na Thamudi na hiyo adhabu walipo watokelea Mitume pande zote. Hawakuacha njia ya kuwaongoza ila waliipitia, na wakawaambia: Msimuabudu ila Mwenyezi Mungu. Wao wakasema: Lau Mwenyezi Mungu angeli taka kumtuma Mtume basi angeli tuteremshia Malaika. Basi sisi hakika tunakataa hayo ya Tawhidi na mengineyo mliyo kuja nayo nyinyi.
  15. فَأَمَّا عَادٌ فَٱسْتَكْبَرُوا۟ فِى ٱلْأَرْضِ بِغَيْرِ ٱلْحَقِّ وَقَالُوا۟ مَنْ أَشَدُّ مِنَّا قُوَّةً ۖ أَوَلَمْ يَرَوْا۟ أَنَّ ٱللَّهَ ٱلَّذِى خَلَقَهُمْ هُوَ أَشَدُّ مِنْهُمْ قُوَّةً ۖ وَكَانُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَا يَجْحَدُونَ۝١٥

    Faamma ʿadun faistakbaroo fee alardi bighayri alhaqqi waqaloo man ashaddu minna quwwatan awalam yaraw anna Allaha allathee khalaqahum huwa ashaddu minhum quwwatan wakanoo biayatina yajhadoona

    Ama kina A'di walijivuna katika nchi bila ya haki, na wakasema: Nani aliye kuwa na nguvu kushinda sisi? Kwani wao hawakuona kwamba Mwenyezi Mungu aliye waumba ni Mwenye nguvu kushinda wao? Na wao wakawa wanazikataa Ishara zetu!15

    Maelezo
    [15] Ama kina A'di walipandwa na kiburi katika nchi bila ya haki ya kuwa na kiburi hicho. Na walisema kwa kughurika na nafsi zao: Nani huyo anaye tushinda sisi kwa nguvu? Ama ajabu watu hawa! Wanasema hayo na wao hawaoni kwamba Mwenyezi Mungu aliye waumba ana nguvu zaidi kuwashinda wao? Na wao walikuwa wakizikanya Ishara zetu!
  16. فَأَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ رِيحًا صَرْصَرًا فِىٓ أَيَّامٍ نَّحِسَاتٍ لِّنُذِيقَهُمْ عَذَابَ ٱلْخِزْىِ فِى ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا ۖ وَلَعَذَابُ ٱلْـَٔاخِرَةِ أَخْزَىٰ ۖ وَهُمْ لَا يُنصَرُونَ۝١٦

    Faarsalna ʿalayhim reehan sarsaran fee ayyamin nahisatin linutheeqahum ʿathaba alkhizyi fee alhayati alddunya walaʿathabu alakhirati akhza wahum la yunsaroona

    Basi tuliwapelekea upepo wa kimbunga katika siku za ukorofi, ili tuwaonjeshe adhabu ya kuwahizi katika uhai wa duniani, na bila ya shaka adhabu ya Akhera ina hizaya zaidi, na wala wao hawatanusuriwa.16

    Maelezo
    [16] Tukawapelekea upepo wenye sauti kali katika siku korofi, ili tuwaonjeshe adhabu ya kuwafanya wawe madhalili wanyonge katika maisha ya duniani. Na ninaapa kuwa bila ya shaka adhabu ya Akhera itakuwa ya hizaya zaidi, wala wao siku hiyo hawatapata wa kuwasaidia.
  17. وَأَمَّا ثَمُودُ فَهَدَيْنَـٰهُمْ فَٱسْتَحَبُّوا۟ ٱلْعَمَىٰ عَلَى ٱلْهُدَىٰ فَأَخَذَتْهُمْ صَـٰعِقَةُ ٱلْعَذَابِ ٱلْهُونِ بِمَا كَانُوا۟ يَكْسِبُونَ۝١٧

    Waamma thamoodu fahadaynahum faistahabboo alʿama ʿala alhuda faakhathathum saʿiqatu alʿathabi alhooni bima kanoo yaksiboona

    Na ama Thamudi tuliwaongoza, lakini walipenda upofu kuliko uwongofu. Basi uliwachukua moto wa adhabu ya kuwafedhehi kwa sababu ya yale waliyo kuwa wakiyachuma.17

    Maelezo
    [17] Na ama kina Thamudi tuliwabainishia njia ya kheri na njia ya shari. Lakini wao walikhiari upotovu kuliko uwongofu, ikawatwaa radi iliyo waunguza kwa madhila na unyonge, kwa sababu ya madhambi waliyo yachuma.
  18. وَنَجَّيْنَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَكَانُوا۟ يَتَّقُونَ۝١٨

    Wanajjayna allatheena amanoo wakanoo yattaqoona

    Na tukawaokoa walio amini na wakawa wanamcha-mngu.18

    Maelezo
    [18] Na tukawaokoa kutokana na adhabu hii wale walio amini, na wakawa wanamcha Mwenyezi Mungu na wanaiogopa adhabu yake.
  19. وَيَوْمَ يُحْشَرُ أَعْدَآءُ ٱللَّهِ إِلَى ٱلنَّارِ فَهُمْ يُوزَعُونَ۝١٩

    Wayawma yuhsharu aʿdao Allahi ila alnnari fahum yoozaʿoona

    Na siku watakapo kusanywa maadui wa Mwenyezi Mungu kwenye Moto, nao wakikgawanywa kwa makundi.19

    Maelezo
    [19] Ewe Nabii! Siku watakapo kusanywa maadui wa Mwenyezi Mungu kupelekwa Motoni, wakawa wa mwanzo wao wanakutana na wa mwisho wao, ili ipate hoja ilazimike juu ya wote,
  20. حَتَّىٰٓ إِذَا مَا جَآءُوهَا شَهِدَ عَلَيْهِمْ سَمْعُهُمْ وَأَبْصَـٰرُهُمْ وَجُلُودُهُم بِمَا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ۝٢٠

    Hatta itha ma jaooha shahida ʿalayhim samʿuhum waabsaruhum wajulooduhum bima kanoo yaʿmaloona

    Hata watakapo ufikia Moto yatawashuhudia masikio yao, na macho yao na ngozi zao kwa waliyo kuwa wakiyatenda.20

    Maelezo
    [20] Mpaka watakapo ufikilia Moto na wakaulizwa juu ya madhambi waliyo yatenda duniani, na wao wakakataa, yakawashuhudilia masikio yao, na macho yao, na ngozi zao kwa waliyo yatenda wao,
  21. وَقَالُوا۟ لِجُلُودِهِمْ لِمَ شَهِدتُّمْ عَلَيْنَا ۖ قَالُوٓا۟ أَنطَقَنَا ٱللَّهُ ٱلَّذِىٓ أَنطَقَ كُلَّ شَىْءٍ وَهُوَ خَلَقَكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ۝٢١

    Waqaloo lijuloodihim lima shahidtum ʿalayna qaloo antaqana Allahu allathee antaqa kulla shayin wahuwa khalaqakum awwala marratin wailayhi turjaʿoona

    Na wao wataziambia ngozi zao: Kwa nini mmetushuhudilia? Nazo zitasema: Ametutamkisha Mwenyezi Mungu ambaye ametamkisha kila kitu! Na Yeye ndiye aliye kuumbeni mara ya kwanza, na kwake Yeye tu mtarejeshwa.21

    Maelezo
    [21] Na hao maadui wa Mwenyezi Mungu wakaziambia ngozi zao: Kwa nini mmetushuhudilia? Na ngozi zitasema: Ametutamkisha Mwenyezi Mungu aliye tamkisha kila kitu. Na Yeye ndiye aliye kuumbeni hapo mwanzo kabla hamjawa chochote. Na kwake Yeye, peke yake, ndio mtarejea baada ya kufufuliwa, akuhisabieni mliyo kwisha yatanguliza katika vitendo.
  22. وَمَا كُنتُمْ تَسْتَتِرُونَ أَن يَشْهَدَ عَلَيْكُمْ سَمْعُكُمْ وَلَآ أَبْصَـٰرُكُمْ وَلَا جُلُودُكُمْ وَلَـٰكِن ظَنَنتُمْ أَنَّ ٱللَّهَ لَا يَعْلَمُ كَثِيرًا مِّمَّا تَعْمَلُونَ۝٢٢

    Wama kuntum tastatiroona an yashhada ʿalaykum samʿukum wala absarukum wala juloodukum walakin thanantum anna Allaha la yaʿlamu katheeran mimma taʿmaloona

    Na hamkuwa wenye kujificha hata masikio yenu, na macho yenu, na ngozi zenu, zisikushuhudilieni. Lakini mlidhani kwamba Mwenyezi Mungu hayajui mengi katika mliyo kuwa mkiyatenda.22

    Maelezo
    [22] Wala nyinyi hamkuwa mkiweza kuficha vitendo vyenu viovu hata viungo vyenu visivione na ikawa macho yenu, na masikio yenu na ngozi zenu, vyote hivyo vikakushuhudilieni. Lakini nyinyi mlikuwa mkidhani kuwa Mwenyezi Mungu hajui mengi katika vitendo vyenu, kwa sababu mkivifanya kwa uficho.
  23. وَذَٰلِكُمْ ظَنُّكُمُ ٱلَّذِى ظَنَنتُم بِرَبِّكُمْ أَرْدَىٰكُمْ فَأَصْبَحْتُم مِّنَ ٱلْخَـٰسِرِينَ۝٢٣

    Wathalikum thannukumu allathee thanantum birabbikum ardakum faasbahtum mina alkhasireena

    Basi hiyo dhana yenu mliyo kuwa mkimdhania Mola wenu Mlezi. Imekuangamizeni; na mmekuwa miongoni mwa walio khasiri.23

    Maelezo
    [23] Lakini dhana mbovu mliyo kuwa mkimdhania Mola wenu Mlezi imekuhilikini, na kwa hivyo mmekuwa Siku ya Kiyama katika wenye kukhasiri vibaya mno.
  24. فَإِن يَصْبِرُوا۟ فَٱلنَّارُ مَثْوًى لَّهُمْ ۖ وَإِن يَسْتَعْتِبُوا۟ فَمَا هُم مِّنَ ٱلْمُعْتَبِينَ۝٢٤

    Fain yasbiroo faalnnaru mathwan lahum wain yastaʿtiboo fama hum mina almuʿtabeena

    Basi wakisubiri Moto ndio maskani yao. Na wakiomba radhi hawakubaliwi.24

    Maelezo
    [24] Basi hata wakijizuia machungu yao, Moto ndio mwisho wao, na makaazi yao ya daima. Na wakitaka kumridhi Mwenyezi Mungu sasa hawakubaliwi hayo matakwa yao.
  25. ۞ وَقَيَّضْنَا لَهُمْ قُرَنَآءَ فَزَيَّنُوا۟ لَهُم مَّا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَحَقَّ عَلَيْهِمُ ٱلْقَوْلُ فِىٓ أُمَمٍ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِم مِّنَ ٱلْجِنِّ وَٱلْإِنسِ ۖ إِنَّهُمْ كَانُوا۟ خَـٰسِرِينَ۝٢٥

    Waqayyadna lahum quranaa fazayyanoo lahum ma bayna aydeehim wama khalfahum wahaqqa ʿalayhimu alqawlu fee omamin qad khalat min qablihim mina aljinni waalinsi innahum kanoo khasireena

    Na tukawawekea marafiki, na wakawapambia yaliyo mbele yao na nyuma yao. Basi ikawathibitikia kauli wawe pamoja na mataifa yaliyo pita kabla yao, miongoni mwa majini na watu. Hakika hao wamekuwa ni wenye kukhasirika.25

    Maelezo
    [25] Nasi tumewaandalia duniani marafiki waharibifu, na wao wakawazainishia mbele yao mambo ya Akhera, basi wakawaghuri kwamba ati hakuna kufufuliwa wala kuhisabiwa, na wakawapambia pia mambo ya duniani ili wastarehe nayo. Na neno la adhabu lilio wapata mataifa yaliyo kwisha pita miongoni mwa majini na watu walio kuwa kama wao, likawathibitikia na wao kwa sababu ya kukhiari kwao upotovu badala ya uwongofu. Hakika watu hao wote walikuwa katika walio khasiri khasara iliyo timia.
  26. وَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لَا تَسْمَعُوا۟ لِهَـٰذَا ٱلْقُرْءَانِ وَٱلْغَوْا۟ فِيهِ لَعَلَّكُمْ تَغْلِبُونَ۝٢٦

    Waqala allatheena kafaroo la tasmaʿoo lihatha alqurani wailghaw feehi laʿallakum taghliboona

    Na walio kufuru walisema: Msiisikilize Qur'ani hii, na timueni zogo, huenda mkashinda.26

    Maelezo
    [26] Makafiri wakaambizana wenyewe kwa wenyewe: Msiisikilize hii Qur'ani, na inapo somwa nyie leteni porojo lisio kuwa na maana, ili pasiwepo mtu wa kuisikia wala kunafiika kwayo, asaa kwa hivyo mkamshinda Muhammad.
  27. فَلَنُذِيقَنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ عَذَابًا شَدِيدًا وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَسْوَأَ ٱلَّذِى كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ۝٢٧

    Falanutheeqanna allatheena kafaroo ʿathaban shadeedan walanajziyannahum aswaa allathee kanoo yaʿmaloona

    Basi hapana shaka tutawaonjesha hao walio kufuru adhabu kali, na hapana shaka tutawalipa malipo mabaya ya yale waliyo kuwa wakiyafanya.27

    Maelezo
    [27] Tunaapa: Bila ya shaka tutawaonjesha walio kufuru adhabu kali kwa vitendo vyao, na khasa kwa hivi kuipiga vita Qur'ani. Na bila ya shaka tutawalipa malipo maovu kabisa kwa vitendo vyao.
  28. ذَٰلِكَ جَزَآءُ أَعْدَآءِ ٱللَّهِ ٱلنَّارُ ۖ لَهُمْ فِيهَا دَارُ ٱلْخُلْدِ ۖ جَزَآءًۢ بِمَا كَانُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَا يَجْحَدُونَ۝٢٨

    Thalika jazao aʿdai Allahi alnnaru lahum feeha daru alkhuldi jazaan bima kanoo biayatina yajhadoona

    Hayo ndiyo malipo ya Maadui wa Mwenyezi Mungu - Moto! Humo watakuwa na maskani ya kudumu, ndiyo malipo yao kwa sababu walikuwa wakizikataa Ishara zetu.28

    Maelezo
    [28] Hizo adhabu zilizo tajwa ni malipo wanayo stahiki maadui wa Mwenyezi Mungu - Moto walio andaliwa katika makaazi ya kuishi milele, kuwa ni malipo kwa kule kuzikataa mfululizo Ishara za Mwenyezi Mungu na hoja zake.
  29. وَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ رَبَّنَآ أَرِنَا ٱلَّذَيْنِ أَضَلَّانَا مِنَ ٱلْجِنِّ وَٱلْإِنسِ نَجْعَلْهُمَا تَحْتَ أَقْدَامِنَا لِيَكُونَا مِنَ ٱلْأَسْفَلِينَ۝٢٩

    Waqala allatheena kafaroo rabbana arina allathayni adallana mina aljinni waalinsi najʿalhuma tahta aqdamina liyakoona mina alasfaleena

    Na walio kufuru watasema: Mola wetu Mlezi! Tuonyeshe walio tupoteza miongoni mwa majini na watu ili tuwaweke chini ya miguu yetu, wapate kuwa miongoni wa walio chini kabisa.29

    Maelezo
    [29] Na makafiri watasema, nao wamo Motoni: Mola wetu Mlezi! Tuonyeshe hayo makundi ya majini na watu walio tupoteza ili tuwaweke chini ya nyayo zetu, wawe katika watu wa chini kabisa.
  30. إِنَّ ٱلَّذِينَ قَالُوا۟ رَبُّنَا ٱللَّهُ ثُمَّ ٱسْتَقَـٰمُوا۟ تَتَنَزَّلُ عَلَيْهِمُ ٱلْمَلَـٰٓئِكَةُ أَلَّا تَخَافُوا۟ وَلَا تَحْزَنُوا۟ وَأَبْشِرُوا۟ بِٱلْجَنَّةِ ٱلَّتِى كُنتُمْ تُوعَدُونَ۝٣٠

    Inna allatheena qaloo rabbuna Allahu thumma istaqamoo tatanazzalu ʿalayhimu almalaikatu alla takhafoo wala tahzanoo waabshiroo bialjannati allatee kuntum tooʿadoona

    Hakika walio sema: Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu! Kisha wakanyooka sawa, hao huwateremkia Malaika wakawaambia: Msiogope, wala msihuzunike; nanyi furahini kwa Pepo mliyo kuwa mkiahidiwa.30

    Maelezo
    [30] Hakika walio sema: Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu, kwa kuukubali Upweke wake, kisha wakasimama sawa sawa juu ya sharia zake, Malaika watawateremkia mara kwa mara wakiwaambia: Msikhofu kukuteremkieni shari, wala msihuzunike kuwa mtakosa kheri, na furahini kuwa mtapata Pepo mliyo ahidiwa kwa ndimi za Manabii na Mitume.
  31. نَحْنُ أَوْلِيَآؤُكُمْ فِى ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا وَفِى ٱلْـَٔاخِرَةِ ۖ وَلَكُمْ فِيهَا مَا تَشْتَهِىٓ أَنفُسُكُمْ وَلَكُمْ فِيهَا مَا تَدَّعُونَ۝٣١

    Nahnu awliyaokum fee alhayati alddunya wafee alakhirati walakum feeha ma tashtahee anfusukum walakum feeha ma taddaʿoona

    Sisi ni vipenzi vyenu katika maisha ya dunia na katika Akhera, na humo mtapata kinacho tamaniwa na nafsi zenu, na humo mtapata mtakavyo vitaka.31

    Maelezo
    [31] Na Malaika watawaambia: Sisi ni wasaidizi wenu katika maisha ya duniani kwa kukuungeni mkono, na Akhera kwa kukuombeeni shafaa na kukutukuzeni. Na huko Akhera mtapata kila cha ladha na kizuri kinacho pendwa na nafsi zenu, na mtapata kila mnacho kitamani kuwa ni takrima, na maamkio yanayo toka kwa Mola Mlezi Mkunjufu wa maghfira na rehema.
  32. نُزُلًا مِّنْ غَفُورٍ رَّحِيمٍ۝٣٢

    Nuzulan min ghafoorin raheemin

    Ni takrima itokayo kwa Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.32

    Maelezo
    [32] Na Malaika watawaambia: Sisi ni wasaidizi wenu katika maisha ya duniani kwa kukuungeni mkono, na Akhera kwa kukuombeeni shafaa na kukutukuzeni. Na huko Akhera mtapata kila cha ladha na kizuri kinacho pendwa na nafsi zenu, na mtapata kila mnacho kitamani kuwa ni takrima, na maamkio yanayo toka kwa Mola Mlezi Mkunjufu wa maghfira na rehema.
  33. وَمَنْ أَحْسَنُ قَوْلًا مِّمَّن دَعَآ إِلَى ٱللَّهِ وَعَمِلَ صَـٰلِحًا وَقَالَ إِنَّنِى مِنَ ٱلْمُسْلِمِينَ۝٣٣

    Waman ahsanu qawlan mimman daʿa ila Allahi waʿamila salihan waqala innanee mina almuslimeena

    Na ni nani mbora wa kusema kuliko aitaye kwa Mwenyezi Mungu na akatenda mema, na akasema: Hakika mimi ni katika Waislamu?33

    Maelezo
    [33] Hapana mwenye kauli nzuri zaidi kuliko mwenye kulingania Tawhid ya Mwenyezi Mungu na ut'iifu wake, na pamoja na hayo, akatenda vitendo vyema, na akasema kwa kuungama itikadi yake: Hakika mimi ni miongoni mwa Waislamu, yaani wenye kunyenyekea amri za Mwenyezi Mungu.
  34. وَلَا تَسْتَوِى ٱلْحَسَنَةُ وَلَا ٱلسَّيِّئَةُ ۚ ٱدْفَعْ بِٱلَّتِى هِىَ أَحْسَنُ فَإِذَا ٱلَّذِى بَيْنَكَ وَبَيْنَهُۥ عَدَٰوَةٌ كَأَنَّهُۥ وَلِىٌّ حَمِيمٌ۝٣٤

    Wala tastawee alhasanatu wala alssayyiatu idfaʿ biallatee hiya ahsanu faitha allathee baynaka wabaynahu ʿadawatun kaannahu waliyyun hameemun

    Mema na maovu hayalingani. Pinga uovu kwa lilio jema zaidi. Hapo yule ambaye baina yako naye pana uadui atakuwa kama rafiki jamaa wa kukuonea uchungu.34

    Maelezo
    [34] Haziwezi kuwa sawa tabia njema na tabia mbovu. Pinga uovu ukikujia kutokana na adui kwa tabia iliyo bora kuliko yake. Hapo matokeo yake ni huyo ambaye uliye kuwa na uadui naye atakuja kuwa kama mwenzio wa kukunusuru mwenye moyo safi.
  35. وَمَا يُلَقَّىٰهَآ إِلَّا ٱلَّذِينَ صَبَرُوا۟ وَمَا يُلَقَّىٰهَآ إِلَّا ذُو حَظٍّ عَظِيمٍ۝٣٥

    Wama yulaqqaha illa allatheena sabaroo wama yulaqqaha illa thoo haththin ʿatheemin

    Lakini hawapewi wema huu ila wanao subiri, wala hawapewi ila wenye bahati kubwa.35

    Maelezo
    [35] Na hawaruzukiwi tabia hii, ya kulipa wema kwa uovu, ila wale wenye khulka ya kusubiri, na hawaruzukiwi hayo ila wenye fungu kubwa la tabia ya wema na ukamilifu wa nafsi.
  36. وَإِمَّا يَنزَغَنَّكَ مِنَ ٱلشَّيْطَـٰنِ نَزْغٌ فَٱسْتَعِذْ بِٱللَّهِ ۖ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلْعَلِيمُ۝٣٦

    Waimma yanzaghannaka mina alshshaytani nazghun faistaʿith biAllahi innahu huwa alssameeʿu alʿaleemu

    Na Shet'ani akikuchochea kwa uchochezi wewe jikinge kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.36

    Maelezo
    [36] Na akitokea Shetani akakutia wasiwasi kukuachisha hayo uliyo amrishwa, ewe unaye semezwa, basi jilinde naye kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu kusikia kwake na kujua kwake kumezunguka kila kitu. Na Yeye atakulinda naye.
  37. وَمِنْ ءَايَـٰتِهِ ٱلَّيْلُ وَٱلنَّهَارُ وَٱلشَّمْسُ وَٱلْقَمَرُ ۚ لَا تَسْجُدُوا۟ لِلشَّمْسِ وَلَا لِلْقَمَرِ وَٱسْجُدُوا۟ لِلَّهِ ٱلَّذِى خَلَقَهُنَّ إِن كُنتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ۝٣٧

    Wamin ayatihi allaylu waalnnaharu waalshshamsu waalqamaru la tasjudoo lilshshamsi wala lilqamari waosjudoo lillahi alathee khalaqahunna in kuntum iyyahu taʿbudoona

    Na katika Ishara zake ni usiku na mchana, na jua na mwezi. Basi msilisujudie jua wala mwezi, bali msujudieni Mwenyezi Mungu aliye viumba, ikiwa nyinyi mnamuabudu Yeye tu.37

    Maelezo
    [37] Na katika dalili za uweza wake Mwenyezi Mungu Mtukufu ni huu usiku na mchana, na jua na mwezi. Msilisujudie jua wala mwezi, kwani hivyo ni katika Ishara zake tu. Bali msujudieni Yeye Mwenyezi Mungu peke yake, aliye umba jua, na mwezi, na usiku, na mchana, ikiwa nyinyi kweli mnamuabudu Yeye peke yake.
  38. فَإِنِ ٱسْتَكْبَرُوا۟ فَٱلَّذِينَ عِندَ رَبِّكَ يُسَبِّحُونَ لَهُۥ بِٱلَّيْلِ وَٱلنَّهَارِ وَهُمْ لَا يَسْـَٔمُونَ ۩۝٣٨

    Faini istakbaroo faallatheena ʿinda rabbika yusabbihoona lahu biallayli waalnnahari wahum la yasamoona

    Na ikiwa watajivuna, basi hao walioko kwa Mola wako Mlezi wanamtakasa Yeye usiku na mchana, na wao hawachoki.38

    Maelezo
    [38] Ikiwa washirikina watajiona wakubwa hawafai kufuata amri yako, basi wewe usiudhike. Kwani hao walio kwa Mola wako Mlezi kwenye utakatifu wake, nao ni Malaika, wanamtakasa Yeye na kila upungufu katika kila wakati, usiku na mchana, wakimsafia ibada Yeye tu, wala hawachoki kumsabihi.
  39. وَمِنْ ءَايَـٰتِهِۦٓ أَنَّكَ تَرَى ٱلْأَرْضَ خَـٰشِعَةً فَإِذَآ أَنزَلْنَا عَلَيْهَا ٱلْمَآءَ ٱهْتَزَّتْ وَرَبَتْ ۚ إِنَّ ٱلَّذِىٓ أَحْيَاهَا لَمُحْىِ ٱلْمَوْتَىٰٓ ۚ إِنَّهُۥ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ۝٣٩

    Wamin ayatihi annaka tara alarda khashiʿatan faitha anzalna ʿalayha almaa ihtazzat warabat inna allathee ahyaha lamuhyee almawta innahu ʿala kulli shayin qadeerun

    Na katika Ishara zake ni kwamba unaiona ardhi nyonge, lakini tunapo iteremshia maji mara unaiona inataharaki na kuumuka. Bila ya shaka aliye ihuisha ardhi ndiye atakaye huisha wafu. Hakika Yeye ni Muweza wa kila kitu.39

    Maelezo
    [39] Na katika dalili za uweza wake, Mtukufu, ni kwamba unaona, wewe unaye weza kuona, ardhi kavu. Tukiiteremshia maji inatikisika kwa mimea, na inaumuka na kuja juu. Hakika huyo aliye ihuisha ardhi iliyo kwisha kufa ndiye aliye elekea kuhuisha wafu katika hayawani. Yeye ni mtimilivu wa uweza juu ya kila kitu. Aya hii inabainisha kwamba mawadi za mbolea ambazo ni chumvi chumvi zisio na uhai, pindi zipatapo maji ya mvua, huyayuka, na kwa hivyo husahilika kufikilia kwenye mbegu za mimea na mizizi yake. Hapo hugeuka kuingia katika khalaya (Cells) na mifumo na viungo vilio hai. Na kwa hivyo vinaonekana kuwa ni hai. Na ukubwa wake hukua na kuzidi kwa kuingiana na kukuzwa na mimea.
  40. إِنَّ ٱلَّذِينَ يُلْحِدُونَ فِىٓ ءَايَـٰتِنَا لَا يَخْفَوْنَ عَلَيْنَآ ۗ أَفَمَن يُلْقَىٰ فِى ٱلنَّارِ خَيْرٌ أَم مَّن يَأْتِىٓ ءَامِنًا يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ ۚ ٱعْمَلُوا۟ مَا شِئْتُمْ ۖ إِنَّهُۥ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ۝٤٠

    Inna allatheena yulhidoona fee ayatina la yakhfawna ʿalayna afaman yulqa fee alnnari khayrun am man yatee aminan yawma alqiyamati iʿmaloo ma shitum innahu bima taʿmaloona baseerun

    Hakika wale wanao upotoa ukweli uliomo katika Ishara zetu hawatufichikii Sisi. Je! Atakaye tupwa Motoni ni bora au atakaye kuja kwa amani Siku ya Kiyama? Tendeni mpendavyo, kwa hakika Yeye anayaona mnayo yatenda.40

    Maelezo
    [40] Hakika hao wanao iacha Njia iliyo sawa kwa mintarafu ya Ishara zetu na wakaitupilia mbali kwa kuikadhibisha, mambo yao hayatupotei Sisi wala hayo wanayo yakusudia. Nasi tutawalipa kama wanavyo stahiki. Kwani anaye tupwa katika Moto ni bora au yule anaye kuja naye hali katulia Siku ya Kiyama kwa kuokoka kwake na kila ovu? Kabisa hao hawalingani. Waambie kwa kuwaahidi: Fanyeni mtakavyo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuzunguka kila kitu kwa jicho lake, naye atamlipa kila mmoja kwa a'mali yake.
  41. إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ بِٱلذِّكْرِ لَمَّا جَآءَهُمْ ۖ وَإِنَّهُۥ لَكِتَـٰبٌ عَزِيزٌ۝٤١

    Inna allatheena kafaroo bialththikri lamma jaahum wainnahu lakitabun ʿazeezun

    Kwa hakika wanayo yakataa mawaidha haya yanapo wajia (wataangamia), na haya bila ya shaka ni Kitabu chenye nguvu na utukufu.41

    Maelezo
    [41] Hakika wanao ikataa Qur'ani Tukufu inapo wajia bila ya kuzingatia, watapata adhabu ambayo hapana mtu anaye weza kuikadiria. Wao wameipinga Qur'ani nacho hakika ni Kitabu kisicho kuwa na mfano, kinamshinda kila mwenye kukipinga, hakiingiliwi na upotofu usio kuwa na asli kwake kwa upande wowote ule, kimeteremka kwa kukufuatana kutokana na Mungu aliye takasika na upuuzi, Msifiwa kwa wingi wa sifa kwa neema alizo zitoa.
  42. لَّا يَأْتِيهِ ٱلْبَـٰطِلُ مِنۢ بَيْنِ يَدَيْهِ وَلَا مِنْ خَلْفِهِۦ ۖ تَنزِيلٌ مِّنْ حَكِيمٍ حَمِيدٍ۝٤٢

    La yateehi albatilu min bayni yadayhi wala min khalfihi tanzeelun min hakeemin hameedin

    Hautakifikia upotovu mbele yake wala nyuma yake. Kimeteremshwa na Mwenye hikima, Msifiwa.42

    Maelezo
    [42] Hakika wanao ikataa Qur'ani Tukufu inapo wajia bila ya kuzingatia, watapata adhabu ambayo hapana mtu anaye weza kuikadiria. Wao wameipinga Qur'ani nacho hakika ni Kitabu kisicho kuwa na mfano, kinamshinda kila mwenye kukipinga, hakiingiliwi na upotofu usio kuwa na asli kwake kwa upande wowote ule, kimeteremka kwa kukufuatana kutokana na Mungu aliye takasika na upuuzi, Msifiwa kwa wingi wa sifa kwa neema alizo zitoa.
  43. مَّا يُقَالُ لَكَ إِلَّا مَا قَدْ قِيلَ لِلرُّسُلِ مِن قَبْلِكَ ۚ إِنَّ رَبَّكَ لَذُو مَغْفِرَةٍ وَذُو عِقَابٍ أَلِيمٍ۝٤٣

    Ma yuqalu laka illa ma qad qeela lilrrusuli min qablika inna rabbaka lathoo maghfiratin wathoo ʿiqabin aleemin

    Huambiwi ila yale yale waliyo ambiwa Mitume wa kabla yako. Hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka ni Mwenye maghfira, na ni Mwenye adhabu chungu.43

    Maelezo
    [43] Ewe Muhammad! Huambiwi wewe na maadui wako ila kama walivyo ambiwa Mitume wa kabla yako na maadui wao, nayo ni matusi na kuambiwa mwongo. Hakika Muumba wako na Mlezi wako ana msamaha mwingi, na ni Mwenye kuadhibu kwa machungu makubwa. Basi Yeye humghufiria mwenye kutubu kwake, na humtesa mwenye kushikilia na inda yake.
  44. وَلَوْ جَعَلْنَـٰهُ قُرْءَانًا أَعْجَمِيًّا لَّقَالُوا۟ لَوْلَا فُصِّلَتْ ءَايَـٰتُهُۥٓ ۖ ءَا۬عْجَمِىٌّ وَعَرَبِىٌّ ۗ قُلْ هُوَ لِلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ هُدًى وَشِفَآءٌ ۖ وَٱلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ فِىٓ ءَاذَانِهِمْ وَقْرٌ وَهُوَ عَلَيْهِمْ عَمًى ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ يُنَادَوْنَ مِن مَّكَانٍۭ بَعِيدٍ۝٤٤

    Walaw jaʿalnahu quranan aʿjamiyyan laqaloo lawla fussilat ayatuhu aaʿjamiyyun waʿarabiyyun qul huwa lillatheena amanoo hudan washifaon waallatheena la yuminoona fee athanihim waqrun wahuwa ʿalayhim ʿaman olaika yunadawna min makanin baʿeedin

    Na lau tungeli ifanya Qur'ani kwa lugha ya kigeni wangeli sema: Kwanini Aya zake haziku pambanuliwa? Yawaje lugha ya kigeni na Mtume Mwaarabu? Sema: Hii Qur'ani ni uwongofu na poza kwa wenye kuamini. Na wasio amini umo uziwi katika masikio yao, nayo kwao imezibwa hawaioni. Hao wanaitwa nao wako pahala mbali.44

    Maelezo
    [44] Na lau tungeli ifanya Qur'ani kwa lugha ya kigeni, kama walivyo pendekeza baadhi ya hao wanao kera, basi bila ya shaka wangeli sema: Lau zingeli bainishwa Aya zake kwa ulimi tunao ufahamu! Kitabu hichi cha lugha ya kigeni, na huyu mkhubiri wake ni Mwaarabu! Yawaje haya? Ewe Mtume! Waambie: Hii Qur'ani ni hivyo hivyo kama walivyo teremshiwa Waumini, si wengineo, kuwa ni Uwongofu na Poza kwa Waumini; kiwaokoe na ubabaishi, na kiwaponyeshe na shaka shaka. Na wasio amini wamekuwa kama katika masikio yao pana kizuizi, uziwi, nayo hii Qur'ani kwao wao ni upofu, hawaoni chochote ndani yake ila fitna tu. Hao makafiri ni kama wanao itwa waiamini kwa umbali kabisa. Hawausikii wito huo.
  45. وَلَقَدْ ءَاتَيْنَا مُوسَى ٱلْكِتَـٰبَ فَٱخْتُلِفَ فِيهِ ۗ وَلَوْلَا كَلِمَةٌ سَبَقَتْ مِن رَّبِّكَ لَقُضِىَ بَيْنَهُمْ ۚ وَإِنَّهُمْ لَفِى شَكٍّ مِّنْهُ مُرِيبٍ۝٤٥

    Walaqad atayna moosa alkitaba faikhtulifa feehi walawla kalimatun sabaqat min rabbika laqudiya baynahum wainnahum lafee shakkin minhu mureebin

    Na hakika tulimpa Musa Kitabu, lakini pakatokea khitilafu kati yake. Na lau kuwa halikwisha tangulia neno la Mola wako Mlezi wangeli hukumiwa. Na hakika wao wamo katika shaka yenye kuwatia wasiwasi.45

    Maelezo
    [45] Ninaapa: Kwa hakika tulimpa Musa Taurati, na watu wake wakakhitalifiana kwayo. Na lau ingeli kuwa hukumu ya Mola wako Mlezi haikuakhirishwa, ewe Muhammad, mpaka muda maalumu kwake, basi hapana shaka pange amuliwa hukumu baina yako na hao kwa kuwang'olea mbali wanao kanusha. Na hakika makafiri katika kaumu yako wamo katika shaka na Qur'ani, na hiyo inawatia dhiki na wasiwasi.
  46. مَّنْ عَمِلَ صَـٰلِحًا فَلِنَفْسِهِۦ ۖ وَمَنْ أَسَآءَ فَعَلَيْهَا ۗ وَمَا رَبُّكَ بِظَلَّـٰمٍ لِّلْعَبِيدِ۝٤٦

    Man ʿamila salihan falinafsihi waman asaa faʿalayha wama rabbuka bithallamin lilʿabeedi

    Anaye tenda mema basi anajitendea mwenyewe nafsi yake, na mwenye kutenda uovu basi ni juu ya nafsi yake vile vile; wala Mola wako Mlezi si mwenye kuwadhulumu waja.46

    Maelezo
    [46] Mwenye kutenda vitendo vyema ujira wake ataupata mwenyewe, na mwenye kutenda uovu madhambi yake yatakuwa juu yake. Na Mola wako Mlezi si mwenye kuwadhulumu waja wake, hata amtese mtu kwa dhambi za mwengine.
  47. ۞ إِلَيْهِ يُرَدُّ عِلْمُ ٱلسَّاعَةِ ۚ وَمَا تَخْرُجُ مِن ثَمَرَٰتٍ مِّنْ أَكْمَامِهَا وَمَا تَحْمِلُ مِنْ أُنثَىٰ وَلَا تَضَعُ إِلَّا بِعِلْمِهِۦ ۚ وَيَوْمَ يُنَادِيهِمْ أَيْنَ شُرَكَآءِى قَالُوٓا۟ ءَاذَنَّـٰكَ مَا مِنَّا مِن شَهِيدٍ۝٤٧

    Ilayhi yuraddu ʿilmu alssaʿati wama takhruju min thamaratin min akmamiha wama tahmilu min ontha wala tadaʿu illa biʿilmihi wayawma yunadeehim ayna shurakaee qaloo athannaka ma minna min shaheedin

    UJUZI wa kuijua Saa ya Kiyama unarudishwa kwake tu Mwenyezi Mungu. Na matunda hayatoki katika mafumba yake, wala mwanamke hachukui mimba, wala hazai, ila kwa kujua kwake. Na siku atakayo waita, akawaambia: Wako wapi washirika wangu? Hapo watasema: Tunakiri kwako ya kwamba hapana miongoni mwetu anaye shuhudia hayo.47

    Maelezo
    [47] Kwa Mwenyezi Mungu peke yake ndio unarejea ujuzi wa kusimama Saa ya Kiyama. Matunda hayatoki kwenye vifuniko vyake, wala mwanamke hachukui mimba wala hazai ila awe Yeye anajua. Na kumbuka siku ambayo Mwenyezi Mungu atawaita washirikina, kwa kuwakebehi, awaambie: Wako wapi hao washirika wangu mlio kuwa mkiwaomba badala yangu? Watasema kwa kutaadhari: Ewe Mwenyezi Mungu! Tunakujuvya kuwa sisi hatuna wa kushuhudia kuwa wewe una mshirika yeyote.
  48. وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا۟ يَدْعُونَ مِن قَبْلُ ۖ وَظَنُّوا۟ مَا لَهُم مِّن مَّحِيصٍ۝٤٨

    Wadalla ʿanhum ma kanoo yadʿoona min qablu wathannoo ma lahum min maheesin

    Na wakawapotea wale walio kuwa wakiwaomba hapo kwanza, na wakawa na yakini kuwa hawana pa kukimbilia.48

    Maelezo
    [48] Na hao miungu ya ushirikina walio kuwa wakiwaabudu watawapotea, na waliyakinika kuwa hawana pa kukimbilia.
  49. لَّا يَسْـَٔمُ ٱلْإِنسَـٰنُ مِن دُعَآءِ ٱلْخَيْرِ وَإِن مَّسَّهُ ٱلشَّرُّ فَيَـُٔوسٌ قَنُوطٌ۝٤٩

    La yasamu alinsanu min duʿai alkhayri wain massahu alshsharru fayaoosun qanootun

    Mwanaadamu hachoki kuomba dua za kheri, na inapo mpata shari, mara huvunjika moyo akakata tamaa.49

    Maelezo
    [49] Mwanaadamu hachoki kumwomba Mola wake Mlezi kwa kheri za kidunia. Ikimpata shari basi huwa mwingi wa kuikatia tamaa kheri, na kuvunjika moyo hadi, ya kwamba Mwenyezi Mungu hamwitikii dua yake.
  50. وَلَئِنْ أَذَقْنَـٰهُ رَحْمَةً مِّنَّا مِنۢ بَعْدِ ضَرَّآءَ مَسَّتْهُ لَيَقُولَنَّ هَـٰذَا لِى وَمَآ أَظُنُّ ٱلسَّاعَةَ قَآئِمَةً وَلَئِن رُّجِعْتُ إِلَىٰ رَبِّىٓ إِنَّ لِى عِندَهُۥ لَلْحُسْنَىٰ ۚ فَلَنُنَبِّئَنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ بِمَا عَمِلُوا۟ وَلَنُذِيقَنَّهُم مِّنْ عَذَابٍ غَلِيظٍ۝٥٠

    Walain athaqnahu rahmatan minna min baʿdi darraa massathu layaqoolanna hatha lee wama athunnu alssaʿata qaimatan walain rujiʿtu ila rabbee inna lee ʿindahu lalhusna falanunabbianna allatheena kafaroo bima ʿamiloo walanutheeqannahum min ʿathabin ghaleethin

    Na pindi tukimwonjesha rehema itokayo kwetu baada ya kumgusa dhara, bila ya shaka husema: Haya nayastahiki mimi, wala sidhani kuwa Kiyama kitakuja. Na hata nikirudishwa kwa Mola wangu Mlezi bila ya shaka nina mema yangu kwake! Basi kwa yakini tutawaelezea walio kufuru hayo waliyo yatenda, na kwa yakini tutawaonjesha adhabu ngumu.50

    Maelezo
    [50] Tunaapa: Tukimwonjesha mtu neema, kwa fadhila yetu, baada ya dhara kubwa iliyo msibu bila ya shaka husema: Hii neema niliyo ipata ni haki yangu mimi. Wala sidhani kuwa Kiyama kitakuja. Na ninaapa ikitokea nikarejeshwa kwa Mola wangu Mlezi basi na huko kwake bila ya shaka nitapata malipo mema. Lakini Sisi tunaapa: Hapana shaka tutawalipa walio kufuru, Siku ya Kiyama, kwa vitendo vyao! Na hapana shaka tutawaonjesha adhabu kali iliyo rindikwa juu kwa juu!
  51. وَإِذَآ أَنْعَمْنَا عَلَى ٱلْإِنسَـٰنِ أَعْرَضَ وَنَـَٔا بِجَانِبِهِۦ وَإِذَا مَسَّهُ ٱلشَّرُّ فَذُو دُعَآءٍ عَرِيضٍ۝٥١

    Waitha anʿamna ʿala alinsani aʿrada wanaa bijanibihi waitha massahu alshsharru fathoo duʿain ʿareedin

    Na tukimneemesha mwanaadamu hugeuka na kujitenga upande, na inapo mgusa shari, huwa na madua marefu marefu.51

    Maelezo
    [51] Na tukimneemesha mtu huacha kutushukuru, na akajitenga mbali na Dini yetu. Na tukimwonjesha shari basi huwa mwingi wa kuomba madua.
  52. قُلْ أَرَءَيْتُمْ إِن كَانَ مِنْ عِندِ ٱللَّهِ ثُمَّ كَفَرْتُم بِهِۦ مَنْ أَضَلُّ مِمَّنْ هُوَ فِى شِقَاقٍۭ بَعِيدٍ۝٥٢

    Qul araaytum in kana min ʿindi Allahi thumma kafartum bihi man adallu mimman huwa fee shiqaqin baʿeedin

    Sema: Mnaonaje! Ikiwa haya yanatoka kwa Mwenyezi Mungu, nanyi ikawa ndio mmeyakataa, ni nani aliye potea zaidi kuliko aliye katika upinzani wa mbali?52

    Maelezo
    [52] Ewe Muhammad! Waambie: Hebu nambieni; ikiwa hii Qur'ani imetoka kwa Mwenyezi Mungu nanyi mkawa mnaikataa, basi nani aliye kuwa mbali mno na Ukweli kuliko huyo aliye kinyume na Haki?
  53. سَنُرِيهِمْ ءَايَـٰتِنَا فِى ٱلْـَٔافَاقِ وَفِىٓ أَنفُسِهِمْ حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُ ٱلْحَقُّ ۗ أَوَلَمْ يَكْفِ بِرَبِّكَ أَنَّهُۥ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ شَهِيدٌ۝٥٣

    Sanureehim ayatina fee alafaqi wafee anfusihim hatta yatabayyana lahum annahu alhaqqu awalam yakfi birabbika annahu ʿala kulli shayin shaheedun

    Tutawaonyesha Ishara zetu katika upeo wa mbali na katika nafsi zao wenyewe mpaka iwabainikie kwamba haya ni kweli. Je! Haikutoshi kwamba Mola wako Mlezi kuwa Yeye ni Shahidi wa kila kitu?53

    Maelezo
    [53] Karibuni hivi tutawaonyesha hao wanao zikataa Ishara zetu zenye kuonyesha ukweli wako katika pande za mbinguni na ardhi, na katika nafsi zao wenyewe, mpaka yawadhihirikie ya kwamba uliyo waletea ni Haki tupu si vinginevyo. Je! Wanakataa kuwa Sisi tunawaletea Ishara hizo? Je! Haitoshi kuwa Mola wako Mlezi ni Mwenye kukizunguka kila kitu?
  54. أَلَآ إِنَّهُمْ فِى مِرْيَةٍ مِّن لِّقَآءِ رَبِّهِمْ ۗ أَلَآ إِنَّهُۥ بِكُلِّ شَىْءٍ مُّحِيطٌۢ۝٥٤

    Ala innahum fee miryatin min liqai rabbihim ala innahu bikulli shayin muheetun

    Ama wao wamo katika shaka ya kukutana na Mola wao Mlezi! Ama hakika Yeye amekizunguka kila kitu.54

    Maelezo
    [54] Ama hakika hawa makafiri wamo katika shaka kubwa kukutana na Mola wao Mlezi, kwa sababu ya kuwa hawaamini kufufuliwa. Ama hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kukizunguka kila kitu kwa ujuzi wake na uweza wake.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Surat Fussilat maana yake ni nini?

Fussilat maana yake ni “Zilizopambanuliwa”.

Surat Fussilat iko katika juzuu ya ngapi?

Surat Fussilat inaenea katika juzuu za 24 na 25.

Surat Fussilat ina aya ngapi?

Surat Fussilat ina aya 54.

Surat Fussilat ni ya Makka au ya Madina?

Surat Fussilat ni sura ya Makka.

Surat Fussilat ni sura ya ngapi katika Qur’ani?

Ni sura ya 41 katika Qur’ani.

Vyanzo

  • Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
  • Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
  • Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
  • Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
  • Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
  • Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.

Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.

Mipangilio ya kusoma

Fonti ya Qur’ani
Ukubwa wa Kiarabu
100%
Ukubwa wa tafsiri
100%
Mandhari

Ongeza kwenye skrini ya kwanza

ReadSurahFungua ReadSurah kutoka skrini ya kwanza, kwa skrini nzima. Sura ulizosoma hufunguka hata bila intaneti.

  1. Katika Safari, gusa kitufe cha kushiriki (Share). Kwenye iPhone mpya kiko kwenye menyu ya •••.
  2. Gusa “Add to Home Screen”. Huenda ukahitaji kusogeza chini.
  3. Gusa “Add”.