Surat Yasin (يس) ni sura ya 36 katika Qur’ani na ina aya 83. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na inaenea katika juzuu za 22 na 23.
Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat Yasin yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.
Surat Yasin kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
-
يسٓ١
Yaseen
Ya-Sin (Y.S.).1
Maelezo
[1] Ya-Sin: Hizi ni harufi mbili zilizo anzia Sura hii kwa mujibu wa mpango wa Qur'ani katika kuanzia baadhi ya Sura kwa harufi moja moja. -
وَٱلْقُرْءَانِ ٱلْحَكِيمِ٢
Waalqurani alhakeemi
Kwa Haki ya Qur'ani yenye hikima!2
Maelezo
[2] Ninaapa kwa Qur'ani yenye kukusanya hikima na ilimu yenye manufaa. -
إِنَّكَ لَمِنَ ٱلْمُرْسَلِينَ٣
Innaka lamina almursaleena
Hakika wewe ni miongoni mwa walio tumwa!3
Maelezo
[3] Hakika wewe, Muhammad, ni katika wale ambao Mwenyezi Mungu amewatuma kwa watu wawapelekee Uwongofu na Dini ya Haki. -
عَلَىٰ صِرَٰطٍ مُّسْتَقِيمٍ٤
ʿAla siratin mustaqeemin
Juu ya Njia Iliyo Nyooka.4
Maelezo
[4] Juu ya Njia Iliyo Sawa, nayo ndiyo Dini ya Kiislamu. -
تَنزِيلَ ٱلْعَزِيزِ ٱلرَّحِيمِ٥
Tanzeela alʿazeezi alrraheemi
Uteremsho wa Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu.5
Maelezo
[5] Ni mteremsho wa Mwenye nguvu Mwenye kushinda kila kitu, ambaye hapana mtu awezae kumzuia chochote akitakacho. Mwenye kuwarehemu waja wake, kwa kuwatumia watu wa kuwaongoza njia ya kuokoka. -
لِتُنذِرَ قَوْمًا مَّآ أُنذِرَ ءَابَآؤُهُمْ فَهُمْ غَـٰفِلُونَ٦
Litunthira qawman ma onthira abaohum fahum ghafiloona
Ili uwaonye watu ambao baba zao hawakuonywa , basi wao wamekuwa wenye kughafilika.6
Maelezo
[6] Ili uwaonye watu ambao baba zao wa karibu hawakupata kuonywa, na kwa hivyo wamesahau yanayo wajibikia kwa Mwenyezi Mungu, na kwa nafsi zao, na kwa watu. -
لَقَدْ حَقَّ ٱلْقَوْلُ عَلَىٰٓ أَكْثَرِهِمْ فَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ٧
Laqad haqqa alqawlu ʿala aktharihim fahum la yuminoona
Bila ya shaka kauli imekwisha thibiti juu ya wengi katika wao, kwa hivyo hawaamini.7
Maelezo
[7] Sisi tulikwisha jua kuwa wengi wao hawatakhiari Imani. Basi yale tuliyo kuwa tunayajua yamewafikiana na yaliyo kwao. Basi haitakuwapo Imani kutoka kwao. -
إِنَّا جَعَلْنَا فِىٓ أَعْنَـٰقِهِمْ أَغْلَـٰلًا فَهِىَ إِلَى ٱلْأَذْقَانِ فَهُم مُّقْمَحُونَ٨
Inna jaʿalna fee aʿnaqihim aghlalan fahiya ila alathqani fahum muqmahoona
Tumeweka makongwa shingoni mwao, yakawafika videvuni. Kwa hivyo vichwa vyao viko juu tu.8
Maelezo
[8] Sisi tumewafanya hao wanao kakamia juu ya ukafiri ni kama walio tiwa minyororo shingoni mwao, ikawafika videvuni mwao. Na mikono yao ikawa imefungwa kwenye vichwa vyao, vikawa vimenyanyuka juu na macho yao yameinama. Basi hawawezi kuvizungusha vichwa vyao wapate kuona. -
وَجَعَلْنَا مِنۢ بَيْنِ أَيْدِيهِمْ سَدًّا وَمِنْ خَلْفِهِمْ سَدًّا فَأَغْشَيْنَـٰهُمْ فَهُمْ لَا يُبْصِرُونَ٩
Wajaʿalna min bayni aydeehim saddan wamin khalfihim saddan faaghshaynahum fahum la yubsiroona
Tumeweka kizuizi mbele yao, na kizuizi nyuma yao, na tumewafunika macho yao; kwa hivyo hawaoni.9
Maelezo
[9] Na tumewafanya wale walio zuwiwa wasione Ishara na dalili ni kama walio fungwa baina ya kuta mbili, na macho yao yakagubikwa, wasione yaliyo mbele yao wala yaliyo nyuma yao. -
وَسَوَآءٌ عَلَيْهِمْ ءَأَنذَرْتَهُمْ أَمْ لَمْ تُنذِرْهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ١٠
Wasawaon ʿalayhim aanthartahum am lam tunthirhum la yuminoona
Ni sawa sawa kwao ukiwaonya au usiwaonye, hawataamini.10
Maelezo
[10] Na ni sawa kwao ukiwahadharisha au ukito wahadharisha, hawaamini hao. -
إِنَّمَا تُنذِرُ مَنِ ٱتَّبَعَ ٱلذِّكْرَ وَخَشِىَ ٱلرَّحْمَـٰنَ بِٱلْغَيْبِ ۖ فَبَشِّرْهُ بِمَغْفِرَةٍ وَأَجْرٍ كَرِيمٍ١١
Innama tunthiru mani ittabaʿa alththikra wakhashiya alrrahmana bialghaybi fabashshirhu bimaghfiratin waajrin kareemin
Hakika wewe unamwonya mwenye kufuata ukumbusho, na akamcha Arrahman, Mwingi wa Rehema, kwa ghaibu. Basi mbashirie huyo msamaha na ujira mwema.11
Maelezo
[11] Hakika wanao nafiika kwa kuhadharisha kwako ni wale wanao ifuata Qur'ani na wakamkhofu Arrahman, ijapo kuwa hawamwoni. Basi watu hawa wape bishara njema kuwa Mwenyezi Mungu atawasamehe madhambi yao, na atawalipa malipo mema kwa vitendo vyao. -
إِنَّا نَحْنُ نُحْىِ ٱلْمَوْتَىٰ وَنَكْتُبُ مَا قَدَّمُوا۟ وَءَاثَـٰرَهُمْ ۚ وَكُلَّ شَىْءٍ أَحْصَيْنَـٰهُ فِىٓ إِمَامٍ مُّبِينٍ١٢
Inna nahnu nuhyee almawta wanaktubu ma qaddamoo waatharahum wakulla shayin ahsaynahu fee imamin mubeenin
Hakika Sisi tunawafufua wafu, na tunayaandika wanayo yatanguliza, na wanayo yaacha nyuma. Na kila kitu tumekihifadhi katika daftari asli lenye kubainisha.12
Maelezo
[12] Hakika Sisi tunawahuisha maiti, na tunayaandika yote waliyo yatenda na wakayakadimisha duniani, na walio yabakisha humo kuwa ni athari, mabaki, yao baada ya kufa kwao. Na kila kitu kimo katika Kitabu kilicho wazi. -
وَٱضْرِبْ لَهُم مَّثَلًا أَصْحَـٰبَ ٱلْقَرْيَةِ إِذْ جَآءَهَا ٱلْمُرْسَلُونَ١٣
Waidrib lahum mathalan ashaba alqaryati ith jaaha almursaloona
Na wapigie mfano wa wakaazi wa mji walipo wafikia walio tumwa.13
Maelezo
[13] Ewe Nabii! Watajie watu wako kisa cha mji mmoja Kwani hicho ni kama kisa chao. Waliwaendea Wajumbe walio tumwa ili wawahidi (awaongoze). Baadhi wa wafasiri wanasema mji huo ni Antiokia. -
إِذْ أَرْسَلْنَآ إِلَيْهِمُ ٱثْنَيْنِ فَكَذَّبُوهُمَا فَعَزَّزْنَا بِثَالِثٍ فَقَالُوٓا۟ إِنَّآ إِلَيْكُم مُّرْسَلُونَ١٤
Ith arsalna ilayhimu ithnayni fakaththaboohuma faʿazzazna bithalithin faqaloo inna ilaykum mursaloona
Tulipo watumia wawili, wakawakanusha. Basi tukawazidishia nguvu kwa mwingine wa tatu. Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwenu.14
Maelezo
[14] Tuliwatuma wajumbe wawili, wakawakadhibisha. Tukawaongeza nguvu kwa kumpeleka mwengine wa tatu. Basi hawa watatu wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwenu! -
قَالُوا۟ مَآ أَنتُمْ إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُنَا وَمَآ أَنزَلَ ٱلرَّحْمَـٰنُ مِن شَىْءٍ إِنْ أَنتُمْ إِلَّا تَكْذِبُونَ١٥
Qaloo ma antum illa basharun mithluna wama anzala alrrahmanu min shayin in antum illa takthiboona
Wakasema: Nyinyi si chochote ila ni watu kama sisi. Na Mwingi wa Rehema hakuteremsha kitu. Nyinyi mnasema uwongo tu.15
Maelezo
[15] Wale watu wa mji wakasema kuwajibu: Nyinyi si chochote ila ni wanaadamu kama sisi. Na Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema hakuteremsha wahyi wowote kwa mwanaadamu. Nyinyi ni watu mnao sema yasiyo kuwapo. -
قَالُوا۟ رَبُّنَا يَعْلَمُ إِنَّآ إِلَيْكُمْ لَمُرْسَلُونَ١٦
Qaloo rabbuna yaʿlamu inna ilaykum lamursaloona
Wakasema: Mola wetu Mlezi anajua kwamba hakika sisi tumetumwa kwenu.16
Maelezo
[16] Wale Wajumbe wakasema: Mola wetu Mlezi aliye tutuma anajua kuwa hakika sisi bila ya shaka tumetumwa kwenu. -
وَمَا عَلَيْنَآ إِلَّا ٱلْبَلَـٰغُ ٱلْمُبِينُ١٧
Wama ʿalayna illa albalaghu almubeenu
Wala si juu yetu ila kufikisha ujumbe ulio wazi.17
Maelezo
[17] Na sisi hatuna waajibu wowote ila kufikilisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu ufike kwa uwazi. -
قَالُوٓا۟ إِنَّا تَطَيَّرْنَا بِكُمْ ۖ لَئِن لَّمْ تَنتَهُوا۟ لَنَرْجُمَنَّكُمْ وَلَيَمَسَّنَّكُم مِّنَّا عَذَابٌ أَلِيمٌ١٨
Qaloo inna tatayyarna bikum lain lam tantahoo lanarjumannakum walayamassannakum minna ʿathabun aleemun
Wakasema: Sisi tumeagua kuwa nyinyi ni wakorofi. Ikiwa hamtaacha basi kwa yakini tutakupigeni mawe, na mtapata adhabu chungu kutoka kwetu.18
Maelezo
[18] Wana mji wale wakasema: Sisi tunaona kuwa nyinyi mnatuletea ukorofi. Na tunaapa, lau kuwa hamsiti na huo wito wenu hapana shaka tutakupopoeni kwa mawe, na hapana shaka mtapata kwetu adhabu kali yenye kutia uchungu. -
قَالُوا۟ طَـٰٓئِرُكُم مَّعَكُمْ ۚ أَئِن ذُكِّرْتُم ۚ بَلْ أَنتُمْ قَوْمٌ مُّسْرِفُونَ١٩
Qaloo tairukum maʿakum ain thukkirtum bal antum qawmun musrifoona
Wakasema: Ukorofi wenu mnao wenyewe! Je! Ni kwa kuwa mnakumbushwa? Ama nyinyi ni watu walio pindukia mipaka.19
Maelezo
[19] Wale Wajumbe wakasema: Ukorofi mnao nyinyi wenyewe, kwa hizo kufuru zenu. Badala ya kuwaidhika kwa mambo yenye kheri kwenu wenyewe, mnatutuhumu sisi kuwa ni wakorofi, na mnatutishia kutupa adhabu chungu? Lakini nyinyi ni watu mlio pindukia mipaka ya Haki na Uadilifu. -
وَجَآءَ مِنْ أَقْصَا ٱلْمَدِينَةِ رَجُلٌ يَسْعَىٰ قَالَ يَـٰقَوْمِ ٱتَّبِعُوا۟ ٱلْمُرْسَلِينَ٢٠
Wajaa min aqsa almadeenati rajulun yasʿa qala ya qawmi ittabiʿoo almursaleena
Na akaja mtu mbio kutokea upande wa mbali wa mjini, akasema: Enyi watu wangu! Wafuateni hawa walio tumwa.20
Maelezo
[20] Akaja mtu kutoka huko mwisho wa mji akiwakimbilia wale wanamji, akawaambia: Wafuateni hawa walio tumwa kwenu na Mwenyezi Mungu. -
ٱتَّبِعُوا۟ مَن لَّا يَسْـَٔلُكُمْ أَجْرًا وَهُم مُّهْتَدُونَ٢١
Ittabiʿoo man la yasalukum ajran wahum muhtadoona
Wafuateni ambao hawakutakini ujira, hali ya kuwa wenyewe wameongoka.21
Maelezo
[21] Wafuateni watu wasio taka kwenu ujira wowote kwa kukunasihini na kukuongozeni, na hali wao wenyewe wameongoka, na nyinyi mtapata manufaa kwa kufuata njia ya kheri na mafanikio! -
وَمَا لِىَ لَآ أَعْبُدُ ٱلَّذِى فَطَرَنِى وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ٢٢
Wama liya la aʿbudu allathee fataranee wailayhi turjaʿoona
NA KWA NINI nisimuabudu yule aliye niumba na kwake mtarejeshwa?22
Maelezo
[22] Na kitu gani cha kunizuia hata nisimuabudu yule aliye niumba, na ambaye kwake Yeye, si kwa mwenginewe, ndio mtarejea? -
ءَأَتَّخِذُ مِن دُونِهِۦٓ ءَالِهَةً إِن يُرِدْنِ ٱلرَّحْمَـٰنُ بِضُرٍّ لَّا تُغْنِ عَنِّى شَفَـٰعَتُهُمْ شَيْـًٔا وَلَا يُنقِذُونِ٢٣
Aattakhithu min doonihi alihatan in yuridni alrrahmanu bidurrin la tughni ʿannee shafaʿatuhum shayan wala yunqithooni
Je! Niishike miungu mingine badala yake? Arrahmani, Mwingi wa Rehema, akinitakia madhara uombezi wa hao hautanifaa kitu, wala hawataniokoa.23
Maelezo
[23] Je! Niishike kwa kuiabudu badala ya Mwenyezi Mungu, miungu mingine isiyo nifaa kitu kuniombea kwao, pindi Mwenyezi Mungu akinitakia madhara? Wala hawataniokoa nayo yakinishukia hayo madhara. -
إِنِّىٓ إِذًا لَّفِى ضَلَـٰلٍ مُّبِينٍ٢٤
Innee ithan lafee dalalin mubeenin
Basi hakika mimi hapo nitakuwa katika upotovu ulio dhaahiri.24
Maelezo
[24] Basi hakika mimi nikiiabudu miungu mingine badala yake Yeye, nitakuwa katika upotovu ulio dhaahiri. -
إِنِّىٓ ءَامَنتُ بِرَبِّكُمْ فَٱسْمَعُونِ٢٥
Innee amantu birabbikum faismaʿooni
Hakika mimi nimemuamini Mola wenu Mlezi, basi nisikilizeni!25
Maelezo
[25] Hakika mimi ninamsadiki Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni, na ndiye Mwenye kutawala mambo yenu. Basi nisikilezeni na mnit'ii. -
قِيلَ ٱدْخُلِ ٱلْجَنَّةَ ۖ قَالَ يَـٰلَيْتَ قَوْمِى يَعْلَمُونَ٢٦
Qeela odkhuli aljannata qala ya layta qawmee yaʿlamoona
Akaambiwa: Ingia Peponi! Akasema: Laiti kuwa watu wangu wangeli jua26
Maelezo
[26] Kuwa ni malipo ya Imani yake na wito wake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ataambiwa: Ingia Peponi! Naye, hali yuko katika kivuli cha neema na hishima, atasema: Laiti kuwa watu wangu wangeli jua alivyo nighufiria Mola wangu Mlezi na kunipa hishima, nao wakaamini kama nilivyo amini mimi. -
بِمَا غَفَرَ لِى رَبِّى وَجَعَلَنِى مِنَ ٱلْمُكْرَمِينَ٢٧
Bima ghafara lee rabbee wajaʿalanee mina almukrameena
Jinsi Mola wangu Mlezi alivyo nisamehe, na akanifanya miongoni mwa walio hishimiwa.27
Maelezo
[27] Kuwa ni malipo ya Imani yake na wito wake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ataambiwa: Ingia Peponi! Naye, hali yuko katika kivuli cha neema na hishima, atasema: Laiti kuwa watu wangu wangeli jua alivyo nighufiria Mola wangu Mlezi na kunipa hishima, nao wakaamini kama nilivyo amini mimi. -
۞ وَمَآ أَنزَلْنَا عَلَىٰ قَوْمِهِۦ مِنۢ بَعْدِهِۦ مِن جُندٍ مِّنَ ٱلسَّمَآءِ وَمَا كُنَّا مُنزِلِينَ٢٨
Wama anzalna ʿala qawmihi min baʿdihi min jundin mina alssamai wama kunna munzileena
Na hatukuwateremshia kaumu yake baada yake jeshi kutoka mbinguni, wala si wenye kuteremsha.28
Maelezo
[28] Na Sisi hatukawaangamiza kwa kuwapelekea maaskari kutoka mbinguni. Wala huo sio mtindo wetu kupeleka majeshi tunapo yahiliki mataifa. -
إِن كَانَتْ إِلَّا صَيْحَةً وَٰحِدَةً فَإِذَا هُمْ خَـٰمِدُونَ٢٩
In kanat illa sayhatan wahidatan faitha hum khamidoona
Hakukuwa ila ukelele mmoja tu; na mara walizimwa!29
Maelezo
[29] Kuteketezwa kwao hakukuwa ila ni kwa ukelele mmoja tu tulio wapelekea. Na mara wao wakawa ni maiti, kama moto ulio zimwa. -
يَـٰحَسْرَةً عَلَى ٱلْعِبَادِ ۚ مَا يَأْتِيهِم مِّن رَّسُولٍ إِلَّا كَانُوا۟ بِهِۦ يَسْتَهْزِءُونَ٣٠
Ya hasratan ʿala alʿibadi ma yateehim min rasoolin illa kanoo bihi yastahzioona
Nawasikitikia waja wangu. Hawajii Mtume ila wao humkejeli.30
Maelezo
[30] Ee khasara yao, inayo faa kusikitikiwa! Hatuwapelekei waja wangu Mtume ila wao huwa wakimfanyia maskhara. -
أَلَمْ يَرَوْا۟ كَمْ أَهْلَكْنَا قَبْلَهُم مِّنَ ٱلْقُرُونِ أَنَّهُمْ إِلَيْهِمْ لَا يَرْجِعُونَ٣١
Alam yaraw kam ahlakna qablahum mina alqurooni annahum ilayhim la yarjiʿoona
Je! Hawaoni umma ngapi tulizo ziangamiza kabla yao? Hakika hao hawarejei tena kwao.31
Maelezo
[31] Kwani wao hawayazingatii mataifa mengi yaliyo tangulia tuliyo yahiliki? Hakika hao hawarejei tena kwenye maisha yao ya duniani. -
وَإِن كُلٌّ لَّمَّا جَمِيعٌ لَّدَيْنَا مُحْضَرُونَ٣٢
Wain kullun lamma jameeʿun ladayna muhdaroona
Na hapana mmoja ila wote watakusanywa waletwe mbele yetu.32
Maelezo
[32] Hapana katika mataifa yaliyo tangulia na yajayo ila wote watakusanywa mbele yetu, nao wamelazimishwa kuhudhuria mbele yetu. -
وَءَايَةٌ لَّهُمُ ٱلْأَرْضُ ٱلْمَيْتَةُ أَحْيَيْنَـٰهَا وَأَخْرَجْنَا مِنْهَا حَبًّا فَمِنْهُ يَأْكُلُونَ٣٣
Waayatun lahumu alardu almaytatu ahyaynaha waakhrajna minha habban faminhu yakuloona
Na Ishara hiyo kwao - ardhi iliyo kufa, nasi tukaifufua, na tukatoa ndani yake nafaka, wakawa wanazila!33
Maelezo
[33] Na dalili kwao ya uweza wetu wa kufufua ni kuangalia vipi ardhi yenye ukame tunavyo ihuisha kwa maji, na kutoa ndani yake nafaka wanazo zila. -
وَجَعَلْنَا فِيهَا جَنَّـٰتٍ مِّن نَّخِيلٍ وَأَعْنَـٰبٍ وَفَجَّرْنَا فِيهَا مِنَ ٱلْعُيُونِ٣٤
Wajaʿalna feeha jannatin min nakheelin waaʿnabin wafajjarna feeha mina alʿuyooni
Na tukafanya ndani yake mabustani ya mitende na mizabibu, na tukatimbua chemchem ndani yake,34
Maelezo
[34] Na humo tukafanya vitalu na mabustani ya mitende na mizabibu, na tukapasua humo chemchem ya kumwagia maji kwenye miti yake, na ikatoa matunda, na wao wakala katika hayo. Na hayo si kazi ya mikono yao. Basi kwa nini hawatoi haki ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yao kwa kumuamini na kumshukuru? -
لِيَأْكُلُوا۟ مِن ثَمَرِهِۦ وَمَا عَمِلَتْهُ أَيْدِيهِمْ ۖ أَفَلَا يَشْكُرُونَ٣٥
Liyakuloo min thamarihi wama ʿamilathu aydeehim afala yashkuroona
Ili wale matunda yake, na hayo hayakufanywa na mikono yao! Basi je, hawashukuru?35
Maelezo
[35] Na humo tukafanya vitalu na mabustani ya mitende na mizabibu, na tukapasua humo chemchem ya kumwagia maji kwenye miti yake, na ikatoa matunda, na wao wakala katika hayo. Na hayo si kazi ya mikono yao. Basi kwa nini hawatoi haki ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yao kwa kumuamini na kumshukuru? -
سُبْحَـٰنَ ٱلَّذِى خَلَقَ ٱلْأَزْوَٰجَ كُلَّهَا مِمَّا تُنۢبِتُ ٱلْأَرْضُ وَمِنْ أَنفُسِهِمْ وَمِمَّا لَا يَعْلَمُونَ٣٦
Subhana allathee khalaqa alazwaja kullaha mimma tunbitu alardu wamin anfusihim wamimma la yaʿlamoona
Subhana, Ametakasika, aliye umba dume na jike vyote katika vinavyo mea katika ardhi na katika nafsi zao, na katika wasivyo vijua.36
Maelezo
[36] Wa kutakasika ni Mwenyezi Mungu aliye umba kila kitu kwa mpango wa ume na uke, katika mimea na katika nafsi zao watu, na katika vitu ambavyo watu hawavijui. Hii harufi Min , yaani "Katika" katika Aya hii ni ya kubainisha. Maana yake Mwenyezi Mungu Mtukufu ameumba madume na majike katika viumbe vyake vyote, sawa sawa katika mimea, na wanyama, na wanaadamu na vyenginevyo ambavyo watu hawavijui na hawavioni. -
وَءَايَةٌ لَّهُمُ ٱلَّيْلُ نَسْلَخُ مِنْهُ ٱلنَّهَارَ فَإِذَا هُم مُّظْلِمُونَ٣٧
Waayatun lahumu allaylu naslakhu minhu alnnahara faitha hum muthlimoona
Na usiku ni Ishara kwao. Tunauvua humo mchana, mara wao wanakuwa gizani.37
Maelezo
[37] Na Ishara pia ya kuwepo Mwenyezi Mungu na uweza wake, ni huu usiku ambao tunautoa ndani yake mchana, kama kuivua nguo inayo sitiri. Mara utaona watu wamo gizani lilio wazunguka kila upande. -
وَٱلشَّمْسُ تَجْرِى لِمُسْتَقَرٍّ لَّهَا ۚ ذَٰلِكَ تَقْدِيرُ ٱلْعَزِيزِ ٱلْعَلِيمِ٣٨
Waalshshamsu tajree limustaqarrin laha thalika taqdeeru alʿazeezi alʿaleemi
Na jua linakwenda kwa kiwango chake. Hayo ni makadirio ya Mwenye nguvu, Mwenye kujua.38
Maelezo
[38] Na jua linakwenda katika njia yake maalumu. Mwenyezi Mungu amekwisha kadiria kwa zama na mahala. Huo ndio mpango wake Mwenye kushinda kwa uweza wake, Mwenye kuvizunguka vitu vyote kwa ujuzi wake. -
وَٱلْقَمَرَ قَدَّرْنَـٰهُ مَنَازِلَ حَتَّىٰ عَادَ كَٱلْعُرْجُونِ ٱلْقَدِيمِ٣٩
Waalqamara qaddarnahu manazila hatta ʿada kaalʿurjooni alqadeemi
Na mwezi tumeupimia vituo, mpaka unakuwa kama karara kongwe.39
Maelezo
[39] Na mwezi kwa mpango wetu tumeujaalia una vituo vyake. Mwanzo wa mwezi unakuwa mdogo na mwembamba. Kisha kila usiku unazidi kukua mpaka unatimia kuwa mbaamwezi. Tena unaingia kupungua vile vile, mpaka ukawa kama karara la mtende linapo kuwa kongwe limepindana na limekuwa manjano. -
لَا ٱلشَّمْسُ يَنۢبَغِى لَهَآ أَن تُدْرِكَ ٱلْقَمَرَ وَلَا ٱلَّيْلُ سَابِقُ ٱلنَّهَارِ ۚ وَكُلٌّ فِى فَلَكٍ يَسْبَحُونَ٤٠
La alshshamsu yanbaghee laha an tudrika alqamara wala allaylu sabiqu alnnahari wakullun fee falakin yasbahoona
Haliwi jua kuufikia mwezi, wala usiku kuupita mchana. Na vyote vinaogelea katika njia zao.40
Maelezo
[40] Haipelekei jua likaacha sharia zake likakutana na mwezi, na likaingia katika njia zake. Wala usiku hauwi kuushinda mchana ukauzuia usije, bali vyote viwili hivyo hupeana zamu. Na vyote, jua na mwezi, na vyenginevyo vyote vinaogelea katika njia zao za mbinguni, wala haviachi njia. Hakika Aya hizi tukufu zinabainisha ukweli wa ki-ilimu ambao wataalamu walikuwa hawaujui ila mwanzo wa karne ya kumi na nne ya kuzaliwa Nabii Isa. Na jua ni moja katika nyota za mbinguni, nalo kama nyota zilizo baki lina mwendo wake wenyewe. Lakini linakhitalifiana na nyota nyengine kwa kuwa lipo karibu na dunia, na kwa kuwa lina kundi la sayari na miezi ya mikia na sayari ndogo ndogo zinazo lifuata daima, na zinat'ii mvuto wake. Kwa hivyo zinakuwa hizo zinazunguka kwa kufuatana kwa utungo kama sura ya yai. Na mkusanyo wote huu unakwenda angani pamoja na jua kwa mvuto wake. Kwa ufupi jua, na ardhi, na mwezi na sayari zote na vyombo vyote hivyo vinakwenda angani kwa mbio maalumu, na kuelekea jiha maalumu. Na yaonekana kuwa jua na mkusanyo wote huo wake, na nyota zilizo karibu nalo zipo katika mkusanyo ulio tanda katika mbingu inayo itwa kwa Kiarabu Sadiimu almajarrah, au kwa Kiingereza Nebula course. Na imebainika kwa masomo ya kisasa sehemu zote za hiyo Nebula zinaizunguka kati yake kwa mbio ya kunasibiana na kinyume cha umbali wake kutoka hapo kati. Pia imeonakana kuwa jua na ardhi na sayari zake na nyota zilio karibu nayo, vyote hivyo vinakwenda mbio, na upande maalumu. Mbio zake zinafika kilomita 700 kila nukta moja. Na kunatimia kuzunguka kwake kukizunguka hicho kituo cha kati kwa kiasi ya miaka milioni 200 ya muangaza. Na kiini cha maneno ni kuwa Aya tukufu iliyo taja kuwa jua linakwenda kwa kiwango chake, hawakujua wataalamu uzuri wake wa ndani mpaka katika mwanzo wa karne hii. Wala hayamkini jua kuupata mwezi, kwani kila kimojapo kinakwenda katika njia zake mbali mbali, basi ni muhali kukutana, kama ilivyo kuwa ni muhali kupitana usiku na mchana. Hayo ingeli takikana ardhi izunguke juu ya msumari-kati wake kutoka mashariki kwendea magharibi, kinyume na ilivyo hivi sasa kutoka magharibi kwendea mashariki. Na mwezi katika kuizunguka kwake ardhi, na ardhi kulizunguka jua, huenda pamoja na mkusanyo wa nyota unao itwa Manaazil Alqamar au Lunar system. Na katika robo ya mwanzo na ya mwisho wa mwezi huonekana sura yake kama karara kongwe au kole lilio kauka, linapo kuwa kongwe na kunyauka. -
وَءَايَةٌ لَّهُمْ أَنَّا حَمَلْنَا ذُرِّيَّتَهُمْ فِى ٱلْفُلْكِ ٱلْمَشْحُونِ٤١
Waayatun lahum anna hamalna thurriyyatahum fee alfulki almashhooni
Na ni Ishara kwao kwamba Sisi tuliwapakia dhuriya zao katika jahazi ilio sheheni.41
Maelezo
[41] Na Ishara nyengine kwao ni kuwa Sisi tuliwapakia wanaadamu katika jahazi ilio jaa bidhaa zao na riziki zao. -
وَخَلَقْنَا لَهُم مِّن مِّثْلِهِۦ مَا يَرْكَبُونَ٤٢
Wakhalaqna lahum min mithlihi ma yarkaboona
Na tukawaumbia kutoka mfano wake wanavyo vipanda.42
Maelezo
[42] Na tukawaumbia mfano wa hiyo marikebu na vyenginevyo wanavyo vipanda kadhaalika. -
وَإِن نَّشَأْ نُغْرِقْهُمْ فَلَا صَرِيخَ لَهُمْ وَلَا هُمْ يُنقَذُونَ٤٣
Wain nasha nughriqhum fala sareekha lahum wala hum yunqathoona
Na tukitaka tunawazamisha, wala hapana wa kuwasaidia, wala hawaokolewi,43
Maelezo
[43] Na tukitaka kuwazamisha, tunawazamisha. Na wala hawapati wa kuwaopoa, wala hawapati wa kuwaokoa wasiangamie. -
إِلَّا رَحْمَةً مِّنَّا وَمَتَـٰعًا إِلَىٰ حِينٍ٤٤
Illa rahmatan minna wamataʿan ila heenin
Isipo kuwa kwa rehema zitokazo kwetu na starehe kwa muda.44
Maelezo
[44] Lakini Sisi hatuwazamishi, kwa sababu ya rehema inayo tokana nasi, na ili tuwastareheshe kwa muda ulio kwisha kadiriwa. -
وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ٱتَّقُوا۟ مَا بَيْنَ أَيْدِيكُمْ وَمَا خَلْفَكُمْ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ٤٥
Waitha qeela lahumu ittaqoo ma bayna aydeekum wama khalfakum laʿallakum turhamoona
Na wanapo ambiwa: Jilindeni na yalioko mbele yenu na yalioko nyuma yenu, ili mpate kurehemewa45
Maelezo
[45] Na wanapo ambiwa: Yaogopeni mfano wa yaliyo wapata mataifa yaliyo kwisha pita kwa kukadhibisha kwao, na iogopeni adhabu ya Akhera ambayo itakupateni kwa kushikilia kwenu ukafiri, kwa kutaraji kuwa asaa Mola wenu Mlezi akakurehemuni mkimcha Yeye, wao hupuuza. -
وَمَا تَأْتِيهِم مِّنْ ءَايَةٍ مِّنْ ءَايَـٰتِ رَبِّهِمْ إِلَّا كَانُوا۟ عَنْهَا مُعْرِضِينَ٤٦
Wama tateehim min ayatin min ayati rabbihim illa kanoo ʿanha muʿrideena
Na haiwafikii Ishara yoyote katika Ishara za Mola wao Mlezi ila wao huwa ni wenye kuipuuza.46
Maelezo
[46] Na haiwajii hoja katika hoja za Mola wao Mlezi, yenye kuonyesha Upweke wa Mwenyezi Mungu na uweza wake, ila wao huipa nyongo, hawaijali. -
وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ أَنفِقُوا۟ مِمَّا رَزَقَكُمُ ٱللَّهُ قَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لِلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ أَنُطْعِمُ مَن لَّوْ يَشَآءُ ٱللَّهُ أَطْعَمَهُۥٓ إِنْ أَنتُمْ إِلَّا فِى ضَلَـٰلٍ مُّبِينٍ٤٧
Waitha qeela lahum anfiqoo mimma razaqakumu Allahu qala allatheena kafaroo lillatheena amanoo anutʿimu man law yashao Allahu atʿamahu in antum illa fee dalalin mubeenin
Na wanapo ambiwa: Toeni katika aliyo kupeni Mwenyezi Mungu, walio kufuru huwaambia walio amini: Je! Tuwalishe ambao Mwenyezi Mungu angependa angeli walisha mwenyewe? Nyinyi hammo ila katika upotofu ulio dhaahiri.47
Maelezo
[47] Na wakiambiwa: Wapeni mafakiri kutokana na hicho alicho kuruzukuni Mwenyezi Mungu, makafiri huwaambia Waumini: Je! Tuwalishe watu ambao Mwenyezi Mungu Mwenyewe angeli taka angeli walisha? Hivyo inakuwa tunamfanyia inda Mwenyezi Mungu kwenda kinyume na mapenzi yake! Nyinyi mnao taka tutoe, si chochote ila mmo katika upofu ulio wazi, hamuioni Haki. -
وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَـٰذَا ٱلْوَعْدُ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ٤٨
Wayaqooloona mata hatha alwaʿdu in kuntum sadiqeena
Na wanasema: Ahadi hii itatokea lini, ikiwa nyinyi ni wakweli?48
Maelezo
[48] Na huwaambia Waumini kwa kuwafanyia kejeli: Lini yatatokea hayo mlio tuahidi, kama nyinyi mnasema kweli katika mnayo ahidi? -
مَا يَنظُرُونَ إِلَّا صَيْحَةً وَٰحِدَةً تَأْخُذُهُمْ وَهُمْ يَخِصِّمُونَ٤٩
Ma yanthuroona illa sayhatan wahidatan takhuthuhum wahum yakhissimoona
Hawangojei ila ukelele mmoja tu utakao wachukua nao wamo kuzozana.49
Maelezo
[49] Hawangojei ila sauti moja tu, iwamalize kwa ghafla, nao wakizozana katika mambo ya kidunia, wameghafilika na Akhera. -
فَلَا يَسْتَطِيعُونَ تَوْصِيَةً وَلَآ إِلَىٰٓ أَهْلِهِمْ يَرْجِعُونَ٥٠
Fala yastateeʿoona tawsiyatan wala ila ahlihim yarjiʿoona
Basi hawataweza kuusia, wala kwa watu wao hawarejei.50
Maelezo
[50] Kwa upesi wa hayo yatakayo wateremkia, hawatowahi kuusia chochote, wala kurejea kwa ahali zao. -
وَنُفِخَ فِى ٱلصُّورِ فَإِذَا هُم مِّنَ ٱلْأَجْدَاثِ إِلَىٰ رَبِّهِمْ يَنسِلُونَ٥١
Wanufikha fee alssoori faitha hum mina alajdathi ila rabbihim yansiloona
Na litapulizwa barugumu, mara watatoka makaburini wakikimbilia kwa Mola wao Mlezi.51
Maelezo
[51] Na barugumu litapulizwa kwa mpulizo wa kufufua watu. Mara watu watatoka makaburini mwao wakikimbilia kwenda kukutana na Mwenyezi Mungu. Na hilo barugumu, na kupulizwa kwake, ni katika anayo yajua Mwenyezi Mungu Yeye peke yake. -
قَالُوا۟ يَـٰوَيْلَنَا مَنۢ بَعَثَنَا مِن مَّرْقَدِنَا ۜ ۗ هَـٰذَا مَا وَعَدَ ٱلرَّحْمَـٰنُ وَصَدَقَ ٱلْمُرْسَلُونَ٥٢
Qaloo ya waylana man baʿathana min marqadina hatha ma waʿada alrrahmanu wasadaqa almursaloona
Watasema: Ole wetu! Nani aliye tufufua kwenye malazi yetu? Haya ndiyo aliyo yaahidi Mwingi wa Rehema na wakasema kweli Mitume.52
Maelezo
[52] Watasema watakao fufuliwa kutoka makaburini: Balaa gani lilio tushukia! Nani aliye tuamsha tukauwacha usingizi wetu? Jawabu ya suala lao itawajia: Hii ndiyo siku ya kufufuliwa aliyo waahidia Arrahaman, Mwingi wa Rehema, waja wake, na Mitume wakaisemea kweli kwa waliyo yasimulia. -
إِن كَانَتْ إِلَّا صَيْحَةً وَٰحِدَةً فَإِذَا هُمْ جَمِيعٌ لَّدَيْنَا مُحْضَرُونَ٥٣
In kanat illa sayhatan wahidatan faitha hum jameeʿun ladayna muhdaroona
Haitakuwa ila ukelele mmoja tu, mara wote watahudhuruishwa mbele yetu.53
Maelezo
[53] Wito wao wa kuwatoa hautakuwa ila ukelele mmoja tu, mara wote watakusanywa mbele yetu wahudhurishwe ili tuwahisabie. -
فَٱلْيَوْمَ لَا تُظْلَمُ نَفْسٌ شَيْـًٔا وَلَا تُجْزَوْنَ إِلَّا مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ٥٤
Faalyawma la tuthlamu nafsun shayan wala tujzawna illa ma kuntum taʿmaloona
Basi leo nafsi yoyote haitadhulumiwa kitu, wala hamtalipwa ila yale mliyo kuwa mkiyatenda.54
Maelezo
[54] Basi katika hii siku ya leo haipungukiwi nafsi na chochote katika ujira wake kwa kazi iliyo tenda. Na wala hamtopata isipo kuwa jaza ya mliyo kuwa mkiyatenda, ikiwa ni kheri au shari. -
إِنَّ أَصْحَـٰبَ ٱلْجَنَّةِ ٱلْيَوْمَ فِى شُغُلٍ فَـٰكِهُونَ٥٥
Inna ashaba aljannati alyawma fee shughulin fakihoona
Hakika watu wa Peponi leo wamo shughulini, wamefurahi.55
Maelezo
[55] Hakika watu wa Peponi hii leo watakuwa wameshughulika kwa neema walizo nazo, wakistaajabia na kufurahia. -
هُمْ وَأَزْوَٰجُهُمْ فِى ظِلَـٰلٍ عَلَى ٱلْأَرَآئِكِ مُتَّكِـُٔونَ٥٦
Hum waazwajuhum fee thilalin ʿala alaraiki muttakioona
Wao na wake zao wamo katika vivuli wameegemea juu ya viti vya fakhari.56
Maelezo
[56] Wao na wake zao wamo katika vivuli vilivyo enea, wameegemea juu ya viti vilivyo pambwa. -
لَهُمْ فِيهَا فَـٰكِهَةٌ وَلَهُم مَّا يَدَّعُونَ٥٧
Lahum feeha fakihatun walahum ma yaddaʿoona
Watapata humo kila namna ya matunda na watapata kila watakacho kitaka.57
Maelezo
[57] Wao na wake zao wamo katika vivuli vilivyo enea, wameegemea juu ya viti vilivyo pambwa. -
سَلَـٰمٌ قَوْلًا مِّن رَّبٍّ رَّحِيمٍ٥٨
Salamun qawlan min rabbin raheemin
"Salama!" Hiyo ndiyo kauli itokayo kwa Mola Mlezi Mwenye kurehemu.58
Maelezo
[58] Wataambiwa: "Salama", kuwa ni kauli iliyo toka kwa Mola Mlezi Mwenye kurehemu. -
وَٱمْتَـٰزُوا۟ ٱلْيَوْمَ أَيُّهَا ٱلْمُجْرِمُونَ٥٩
Waimtazoo alyawma ayyuha almujrimoona
Na enyi wakosefu! Jitengeni leo!59
Maelezo
[59] Na wataambiwa wakosefu siku hii ya leo: Jitengeni mbali na Waumini. -
۞ أَلَمْ أَعْهَدْ إِلَيْكُمْ يَـٰبَنِىٓ ءَادَمَ أَن لَّا تَعْبُدُوا۟ ٱلشَّيْطَـٰنَ ۖ إِنَّهُۥ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ٦٠
Alam aʿhad ilaykum ya banee adama an la taʿbudoo alshshaytana innahu lakum ʿaduwwun mubeenun
Je! Sikuagana nanyi, enyi wanaadamu, kuwa msimuabudu Shet'ani? Hakika yeye ni adui dhaahiri kwenu.60
Maelezo
[60] Enyi wanaadamu! Sikukuusieni kuwa msimfuate Shetani kwa ut'iifu kama kwamba ni mungu wa kuabudiwa. Hakika yeye ni adui yenu, aliye dhihirisha uadui wake. -
وَأَنِ ٱعْبُدُونِى ۚ هَـٰذَا صِرَٰطٌ مُّسْتَقِيمٌ٦١
Waani oʿbudoonee hatha siratun mustaqeemun
Na ya kwamba mniabudu Mimi? Hii ndiyo Njia Iliyo Nyooka.61
Maelezo
[61] Na nyinyi mniabudu Mimi peke yangu, kwani kuniabudu Mimi tu ndiyo Njia kuu katika kusimamisha Dini sawa. -
وَلَقَدْ أَضَلَّ مِنكُمْ جِبِلًّا كَثِيرًا ۖ أَفَلَمْ تَكُونُوا۟ تَعْقِلُونَ٦٢
Walaqad adalla minkum jibillan katheeran afalam takoonoo taʿqiloona
Na bila ya shaka yeye amekwisha lipoteza kundi kubwa miongoni mwenu. Je, hamkuwa mkifikiri?62
Maelezo
[62] Na Shetani amewapotoa viumbe wengi kati yenu. Nyinyi mmeghafilika na hayo. Basi hamkuwa mkifikiri mlipo mt'ii yeye? -
هَـٰذِهِۦ جَهَنَّمُ ٱلَّتِى كُنتُمْ تُوعَدُونَ٦٣
Hathihi jahannamu allatee kuntum tooʿadoona
Hii basi ndiyo Jahannamu mliyo kuwa mkiahidiwa.63
Maelezo
[63] Wataambiwa: Hii ndiyo Jahannamu mliyo kuwa mkiahidiwa mlipo kuwa duniani. Ndiyo jaza ya ukafiri wenu. -
ٱصْلَوْهَا ٱلْيَوْمَ بِمَا كُنتُمْ تَكْفُرُونَ٦٤
Islawha alyawma bima kuntum takfuroona
Ingieni leo kwa vile mlivyo kuwa mkikufuru.64
Maelezo
[64] Ingieni! Na hilikini kwa joto lake hii leo kwa ukafiri wenu! -
ٱلْيَوْمَ نَخْتِمُ عَلَىٰٓ أَفْوَٰهِهِمْ وَتُكَلِّمُنَآ أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُم بِمَا كَانُوا۟ يَكْسِبُونَ٦٥
Alyawma nakhtimu ʿala afwahihim watukallimuna aydeehim watashhadu arjuluhum bima kanoo yaksiboona
Leo tunaviziba vinywa vyao, na iseme nasi mikono yao, na itoe ushahidi miguu yao kwa waliyo kuwa wakiyachuma.65
Maelezo
[65] Leo vitazibwa vinywa vyao, basi havito tamka kitu. Mikono yao ndiyo itakayo sema nasi, na miguu yao itatamka kwa kutoa ushahidi juu yao kwa waliyo kuwa wakiyafanya. -
وَلَوْ نَشَآءُ لَطَمَسْنَا عَلَىٰٓ أَعْيُنِهِمْ فَٱسْتَبَقُوا۟ ٱلصِّرَٰطَ فَأَنَّىٰ يُبْصِرُونَ٦٦
Walaw nashao latamasna ʿala aʿyunihim faistabaqoo alssirata faanna yubsiroona
Na tungeli penda tungeli yafutilia mbali macho yao, wakawa wanaiwania njia. Lakini wange ionaje?66
Maelezo
[66] Na tungeli taka kuwatia upofu duniani tungeli watia upofu, wakawa wanaipapasa njia ya kupita wasiweze kuiona. Wataionaje nasi tumewapofoa! -
وَلَوْ نَشَآءُ لَمَسَخْنَـٰهُمْ عَلَىٰ مَكَانَتِهِمْ فَمَا ٱسْتَطَـٰعُوا۟ مُضِيًّا وَلَا يَرْجِعُونَ٦٧
Walaw nashao lamasakhnahum ʿala makanatihim fama istataʿoo mudiyyan wala yarjiʿoona
Na tungeli taka tunge wageuza sura hapo hapo walipo, basi wasinge weza kwenda wala kurudi.67
Maelezo
[67] Na lau tungeli taka kuzigeuza sura zao tungeli zigeuza zikawa mbaya, juu ya kuwa wana nguvu na vyeo. Hata wasinge weza kwenda mbele wala kurudi nyuma, kwa kuwa inge kuwa tumevunja nguvu zao. -
وَمَن نُّعَمِّرْهُ نُنَكِّسْهُ فِى ٱلْخَلْقِ ۖ أَفَلَا يَعْقِلُونَ٦٨
Waman nuʿammirhu nunakkishu fee alkhalqi afala yaʿqiloona
Na tunaye mzeesha tunamrudisha nyuma katika umbo. Basi je! hawazingatii?68
Maelezo
[68] Na tunaye mfanyia umri wake ukawa mrefu, tunamrudisha, kutoka nguvu akawa dhaifu. Basi je hawayazingatii haya wakayatia akilini ya uweza wetu kuyafanya haya, na wao wakajua kuwa dunia ni nyumba ya kupita ina mwisho wake, na kuwa Akhera ndiyo nyumba ya kubaki na kudumu? Na tunaye mfanyia umri wake uwe mrefu tunamrejesha awe kinyume na alivyo kuwa. Yaani baada ya kuwa na nguvu anakuwa dhaifu. Hayo ni kwa kuwa maisha ya mwanaadamu yanapitia vipindi vitatu, kukua, kutimia kukua; na ukongwe unaanza kwa kunywea kwa mafigo, ini, Ghudda Ddarqiya au Thyroid gland, na Pancreas, yaani Dongoronya. Na haya huleta athari katika kudhoofika mwili wote. Mishipa ya damu nayo huanza kukacha na kunywea, na kwa hivyo hupunguka damu inayo kwenda katika viungo vyote vya mwili, basi ndio huzidi udhaifu juu ya udhaifu. Na katika sababu za kukonga ni kuzidi nguvu za kubomoka kuliko kujengeka katika mwili, yaani Metabolism. Na hayo ni kwa kuwa Khalaya au Cells, za mwili zote zimo katika hali ya kugeuka, na pia Khalaya za damu, isipo kuwa Khalaya za ubongo wa kichwani na wa katika mifupa. Hizo hazigeuki muda wote wa uhai. Ikiwa kiasi ya kuundika upya ni sawa ya kiasi cha kuharibika, basi hapana madhara yanayo tokea. Lakini ikiwa kuharibika ni kukubwa kuliko kujengeka katika kiungo chochote basi hapo hudhihiri madhara kwenye kiungo hicho. Na kwa hivyo kila umri ukiwa mkubwa kiasi cha kujengeka kinapungua na kinazidi kiasi cha kubomoka kwa Khalaya, na kunadhihiri kunywea, na kupungua nguvu kote. Na hukhitalifiana kiasi cha kujengeka kwa mnasaba wa kubomoka kwa kukhitalifiana namna ya mfumo (Nasiij, Texture). Katika hayo yanayo dhihiri kama ngozi iliyo funika mwili, na zilio funika paipu za kusaga chakula, na paipu za Ghudad, Glands, zinachakaa kwa upesi zaidi kila miaka ya binaadamu ikipita. Na hii ni sababu ya kuonekana upesi alama za kuzeeka. -
وَمَا عَلَّمْنَـٰهُ ٱلشِّعْرَ وَمَا يَنۢبَغِى لَهُۥٓ ۚ إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ وَقُرْءَانٌ مُّبِينٌ٦٩
Wama ʿallamnahu alshshiʿra wama yanbaghee lahu in huwa illa thikrun waquranun mubeenun
Wala hatukumfundisha (Muhammad) mashairi, wala hayatakikani kwake hayo. Haukuwa huu ila ni ukumbusho na Qur'ani inayo bainisha.69
Maelezo
[69] Na Sisi hatukumfunza Mtume kutunga mashairi. Wala haifai hivyo, kwa kuzingatia pahala pake na cheo chake awe mtungaji mashairi! Hii Qur'ani iliyo teremka juu yake si chochote ila ni mawaidha, na Kitabu cha mbinguni kilio wazi. Hakikhusiani kabisa na mashairi. -
لِّيُنذِرَ مَن كَانَ حَيًّا وَيَحِقَّ ٱلْقَوْلُ عَلَى ٱلْكَـٰفِرِينَ٧٠
Liyunthira man kana hayyan wayahiqqa alqawlu ʿala alkafireena
Ili imwonye aliye hai, na neno litimie juu ya makafiri.70
Maelezo
[70] Hii Qur'ani ni kumtia khofu mwenye moyo ulio hai ulio nawirika kwa akili. Na ipite hukumu ya adhabu kuwashukia wanao ipinga Qur'ani, wenye kukataa uwongofu wake. -
أَوَلَمْ يَرَوْا۟ أَنَّا خَلَقْنَا لَهُم مِّمَّا عَمِلَتْ أَيْدِينَآ أَنْعَـٰمًا فَهُمْ لَهَا مَـٰلِكُونَ٧١
Awalam yaraw anna khalaqna lahum mimma ʿamilat aydeena anʿaman fahum laha malikoona
Je! Hawaoni kwamba tumewaumbia kutokana na iliyo fanya mikono yetu wanyama wa mifugo, na wao wakawa wenye kuwamiliki.71
Maelezo
[71] Je! Makafiri wameingiwa na upofu hata hawaoni kwamba Sisi tumewaumbia kutokana na iliyo fanya kudra yetu nyama hoa, wanyama wa mifugo, na wao wamekuwa wanawamiliki, wanawatumilia kama wapendavyo? Ngamia, kondoo, mbuzi na ng'ombe. -
وَذَلَّلْنَـٰهَا لَهُمْ فَمِنْهَا رَكُوبُهُمْ وَمِنْهَا يَأْكُلُونَ٧٢
Wathallalnaha lahum faminha rakoobuhum waminha yakuloona
Na Sisi tukawadhalilishia. Basi baadhi yao wako wanao wapanda, na baadhi yao wanawala.72
Maelezo
[72] Na hao wanyama tumewafanya wawatumikie. Wengine basi wanawapanda, na wengine wanawala. -
وَلَهُمْ فِيهَا مَنَـٰفِعُ وَمَشَارِبُ ۖ أَفَلَا يَشْكُرُونَ٧٣
Walahum feeha manafiʿu wamasharibu afala yashkuroona
Na wao wanapata kwao manufaa na vinywaji. Basi je, hawashukuru?73
Maelezo
[73] Na wanapata kwa hao vitu vya kuwapa manufaa, kama sufi, na manyoya, na nywele, na ngozi, na mafupa, na vinywaji kutokana na maziwa yao. Je! Wanasahau neema hizi hata wamekuwa hawamshukuru aliye waneemesha? -
وَٱتَّخَذُوا۟ مِن دُونِ ٱللَّهِ ءَالِهَةً لَّعَلَّهُمْ يُنصَرُونَ٧٤
Waittakhathoo min dooni Allahi alihatan laʿallahum yunsaroona
Na wameishika miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu ili ati wapate kusaidiwa!74
Maelezo
[74] Na washirikina wamefanya miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu wakiwaabudu kwa kutaraji kuwa ati watawasaidia. -
لَا يَسْتَطِيعُونَ نَصْرَهُمْ وَهُمْ لَهُمْ جُندٌ مُّحْضَرُونَ٧٥
La yastateeʿoona nasrahum wahum lahum jundun muhdaroona
Hawataweza kuwasaidia. Bali hao ndio watakuwa askari wao watakao hudhurishwa.75
Maelezo
[75] Hiyo miungu ya uwongo haiwezi kuwasaidia kwa lolote Mwenyezi Mungu akiwatakia madhara. Kwani miungu hiyo haiwezi kunafiisha wala kudhuru. Bali wao kwa hiyo miungu isiyo weza kitu, ni kama askari walio tayarishwa kwa ajili ya kuwakhudumia na wa kuwalinda na madhara. -
فَلَا يَحْزُنكَ قَوْلُهُمْ ۘ إِنَّا نَعْلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعْلِنُونَ٧٦
Fala yahzunka qawluhum inna naʿlamu ma yusirroona wama yuʿlinoona
Basi maneno yao yasikuhuzunishe. Hakika Sisi tunayajua wanayo yaweka siri na wanayo yatangaza.76
Maelezo
[76] Basi yasikuhuzunishe maneno yao kumkhusu Mwenyezi Mungu kwa kumkufuru, na kukukhusu wewe kwa kukwambia mwongo. Hakika Sisi tunayajua wanayo yaficha na wanayo yatangaza. Nasi tutawalipa kwa hayo. -
أَوَلَمْ يَرَ ٱلْإِنسَـٰنُ أَنَّا خَلَقْنَـٰهُ مِن نُّطْفَةٍ فَإِذَا هُوَ خَصِيمٌ مُّبِينٌ٧٧
Awalam yara alinsanu anna khalaqnahu min nutfatin faitha huwa khaseemun mubeenun
Kwani mwanaadamu haoni ya kwamba Sisi tumemuumba yeye kutokana na tone la manii? Kisha sasa yeye ndio amekuwa ndiye mgomvi wa dhaahiri!77
Maelezo
[77] Je! Binaadamu anakataa kuwepo Mwenyezi Mungu na uweza wake, na haoni yeye kwamba Sisi, baada ya kuwa hata hayupo, tulimuumba kutokana na tone la manii dhalili? Na sasa amekuwa mkali wa kutukhasimu kwa uwazi kabisa? -
وَضَرَبَ لَنَا مَثَلًا وَنَسِىَ خَلْقَهُۥ ۖ قَالَ مَن يُحْىِ ٱلْعِظَـٰمَ وَهِىَ رَمِيمٌ٧٨
Wadaraba lana mathalan wanasiya khalqahu qala man yuhyee alʿithama wahiya rameemun
Na akatupigia mfano, na akasahau kuumbwa kwake, akasema: Ni nani huyo atakaye ihuisha mifupa nayo imekwisha mung'unyika?78
Maelezo
[78] Tena huyu mpingaji aliye dhaahiri ametupigia mfano ambao kwao anakanya uweza wetu kufufua mafupa baada ya kuoza na kusagika. Na amesahau kuwa Sisi tulimuumba yeye, naye hata hakuwepo aslani. Akasema kwa kukanya na kuona haliwezi kuwa hilo: Ni nani huyo atakaye yafufua mafupa nayo yamekwisha mung'unyika? -
قُلْ يُحْيِيهَا ٱلَّذِىٓ أَنشَأَهَآ أَوَّلَ مَرَّةٍ ۖ وَهُوَ بِكُلِّ خَلْقٍ عَلِيمٌ٧٩
Qul yuhyeeha allathee anshaaha awwala marratin wahuwa bikulli khalqin ʿaleemun
Sema: Ataihuisha huyo huyo aliye iumba hapo mara ya mwanzo. Na Yeye ni Mjuzi wa kila kuumba.79
Maelezo
[79] Ewe Muhammad! Sema: Atayafufua yule yule aliye yaumba hapo mara ya kwanza. Kwani aliye anza anao uweza wa kufanya tena. Naye ni Mkubwa wa kujua kila alicho kiumba. Basi haemewi Yeye na kukusanya vipande vipande baada ya kutawanyika. -
ٱلَّذِى جَعَلَ لَكُم مِّنَ ٱلشَّجَرِ ٱلْأَخْضَرِ نَارًا فَإِذَآ أَنتُم مِّنْهُ تُوقِدُونَ٨٠
Allathee jaʿala lakum mina alshshajari alakhdari naran faitha antum minhu tooqidoona
Aliye kujaalieni kupata moto kutokana na mti wa kijani nanyi mkawa kwa huo mnawasha.80
Maelezo
[80] Aliye kuumbieni moto kutoka mti mbichi, baada ya kwisha kauka. Nguvu za jua zinaingia ndani ya mimea kwa wasita wa mwangaza. Khalaya zenye madda ya kijani katika mimea Chlorophyl ndizo zinafyonza Carbon dioxide kutokana na hewa, na hii huchanganyika na maji yanayo fonzwa na mimea, na kufanyika Carbohydrates kwa kuathiriwa na nguvu zinazo tokana na mwangaza wa jua. Tena hufanyika mbao, kuni, ambazo sehemu kubwa ni muundo wa kimyaa wa Carbon na Hydrogen na Oxygen. Na kutokana na kuni hizi hufanyika makaa haya ya miti tuyatumiayo. Ukiyachoma makaa hutoka nguvu zilizo kuwamo ndani yake kwa ajili ya kupikia, na kwa kazi nyingi nyenginezo. Na makaa ya mawe si chochote ila ni hiyo hiyo mimea na miti iliyo kuwa na kufanyika kama ilivyo elezwa, na kisha ikazikika kwa njia fulani na kugeuka baada ya kupita mamilioni ya miaka kuwa makaa ya mawe, kwa kuathirika na hali za geology kama joto au mdidimizo au menginewe. Na yapasa kuzingatia kuwa kutajwa katika Aya hii "mti wa kijani" si bure, bali ni ishara ya hiyo Chlorophyll ya kijani ambayo ni lazima kwa ajili ya kuimeza Carbon dioxide katika mimea. -
أَوَلَيْسَ ٱلَّذِى خَلَقَ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ بِقَـٰدِرٍ عَلَىٰٓ أَن يَخْلُقَ مِثْلَهُم ۚ بَلَىٰ وَهُوَ ٱلْخَلَّـٰقُ ٱلْعَلِيمُ٨١
Awalaysa allathee khalaqa alssamawati waalarda biqadirin ʿala an yakhluqa mithlahum bala wahuwa alkhallaqu alʿaleemu
Kwani aliye ziumba mbingu na ardhi hawezi kuwaumba mfano wao? Kwani! Naye ndiye Muumbaji Mkuu, Mjuzi.81
Maelezo
[81] Kwani hao wamepotelewa na akili zao hata hawajui kwamba aliye ziumba mbingu na ardhi, juu ya ukubwa wao, ni Muweza vile vile kurejesha kuwaumba wanaadamu ambao ni wadogo na hali yao ni dhaifu? Kwani? Yeye ni Muweza sana, na Yeye ni Mwingi wa kuumba, ambaye ujuzi wake umeenea kila kitu. -
إِنَّمَآ أَمْرُهُۥٓ إِذَآ أَرَادَ شَيْـًٔا أَن يَقُولَ لَهُۥ كُن فَيَكُونُ٨٢
Innama amruhu itha arada shayan an yaqoola lahu kun fayakoonu
Hakika amri yake anapo taka kitu ni kukiambia tu: Kuwa! Na kikawa.82
Maelezo
[82] Hakika shani yake katika kuumba anapo taka kiwe kitu ni kukiambia tu: Kuwa! Kikawa, na hutokea hapo hapo! -
فَسُبْحَـٰنَ ٱلَّذِى بِيَدِهِۦ مَلَكُوتُ كُلِّ شَىْءٍ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ٨٣
Fasubhana allathee biyadihi malakootu kulli shayin wailayhi turjaʿoona
Basi Ametakasika yule ambaye mkononi mwake umo Ufalme wa kila kitu; na kwake Yeye mtarejeshwa.83
Maelezo
[83] Basi Mtukufu ametakasika na kila kisicho laiki na dhati yake, yule ambaye katika kudra yake upo Ufalme wa kila kitu, kwa kuumba, na kupanga, na kuendesha - Kwake Yeye peke yake mtarejeshwa, akuhisabuni kwa a'mali zenu.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Surat Yasin iko katika juzuu ya ngapi?
Surat Yasin inaenea katika juzuu za 22 na 23.
Surat Yasin ina aya ngapi?
Surat Yasin ina aya 83.
Surat Yasin ni ya Makka au ya Madina?
Surat Yasin ni sura ya Makka.
Surat Yasin ni sura ya ngapi katika Qur’ani?
Ni sura ya 36 katika Qur’ani.
Vyanzo
- Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
- Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
- Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
- Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
- Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
- Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.
Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.