سورة الواقعة

Surat Al-Waqi’a kwa Kiswahili

Tukio

Msahafu

Mishary Rashid AlafasyPakua MP3Pakua PDF

Surat Al-Waqi’a (الواقعة) ni sura ya 56 katika Qur’ani na ina aya 96. Jina lake lina maana ya “Tukio”. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na iko katika juzuu ya 27.

Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat Al-Waqi’a yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.

Surat Al-Waqi’a kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

  1. إِذَا وَقَعَتِ ٱلْوَاقِعَةُ۝١

    Itha waqaʿati alwaqiʿatu

    Litakapo tukia hilo Tukio .1

    Maelezo
    [1] Kitakapo tukia Kiyama
  2. لَيْسَ لِوَقْعَتِهَا كَاذِبَةٌ۝٢

    Laysa liwaqʿatiha kathibatun

    Hapana cha kukanusha kutukia kwake.2

    Maelezo
    [2] Haitotokea nafsi yoyote ya kukadhibisha.
  3. خَافِضَةٌ رَّافِعَةٌ۝٣

    Khafidatun rafiʿatun

    Literemshalo linyanyualo!3

    Maelezo
    [3] Kiyama hicho kitawateremsha chini walio waovu, na kitawanyanyua juu walio wema.
  4. إِذَا رُجَّتِ ٱلْأَرْضُ رَجًّا۝٤

    Itha rujjati alardu rajjan

    Itakapo tikiswa ardhi kwa mtikiso!4

    Maelezo
    [4] Ardhi itakapo tikiswa, na ikatetemeshwa kwa nguvu.
  5. وَبُسَّتِ ٱلْجِبَالُ بَسًّا۝٥

    Wabussati aljibalu bassan

    Na milima itapo sagwasagwa!5

    Maelezo
    [5] Na milima ikavurugwa teketeke,
  6. فَكَانَتْ هَبَآءً مُّنۢبَثًّا۝٦

    Fakanat habaan munbaththan

    Iwe mavumbi yanayo peperushwa!6

    Maelezo
    [6] Ikawa vumbi la kupeperushwa, Aya hizi tukufu zinaeleza hadi gani vitakuwa vitisho vitavyo uteremkia ulimwengu kitapo fika Kiyama. Na katika vitisho hivyo ni hayo masaibu ya dunia yatakayo athiri ardhi na mat'abaka yake. Kwani hii ardhi tunayo ishi juu ya mgongo wake si yenye kutulia na kukaa sawa kwa utimilivu. Kwani hiyo imeundwa kwa mat'abaka ya majabali yaliyo ingiliana ovyo. Huenda baadhi yao yakateremka yakaachana na mengineyo yaliyo jirani nayo. Na huwa hiyo inayo itwa kupasuka kwa mat'abaka ya ardhi, Geological cleavage kama inavyo tokea katika maeneo kadhaa wa kadhaa. Mpasuko huu ulikuwa na ungali kuwa ndio asili ya chini kabisa ya zilzala, mitetemeko, mikubwa kwa kuathirika na nguvu za kudidimiza na kuvuta zinazo fuatana na mat'abaka ya ardhi yanapo vunjika. Basi mizani ya utulivu ya nguvu hizi inapo geuka kwa kuathirika na mambo mengineyo ya nje huenda zikafunguka nguvu za mtikiso mkubwa ndio ikatokea mitetemeko na mitikisiko ya ardhi, ambayo hubomoa kila kitu kiliopo juu ya ardhi karibu na ilipo anzia hiyo zilzala. Na hapo tena hutokea uharibifu mkubwa mno. Na hayo maelezo ya kisayansi hayageuzi kitu, wala hayako mbali na nadhari ya kidini. Kwani hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu huenda akajaalia sababu za maumbile za kawaida zikajumuika kwa njia tusiyo izoea sisi ili zikiingiliana kwa njia ya kutisha ndio sababu ya kuharibika dunia. Hapo maelezo ya kisayansi yanafuatana na Aya zenye kuonya kwa vitisho hivyo vikuu. Na yote hayo yanatokana kwa Mwenyezi Mungu. Na hutokea kwa idhini yake Mwenyezi Mungu kutimiza hukumu yake katika dunia yetu.
  7. وَكُنتُمْ أَزْوَٰجًا ثَلَـٰثَةً۝٧

    Wakuntum azwajan thalathatan

    Na nyinyi mtakuwa namna tatu: .7

    Maelezo
    [7] Na mkawa nyote siku hiyo namna tatu kwa mujibu wa vitendo vyenu;
  8. فَأَصْحَـٰبُ ٱلْمَيْمَنَةِ مَآ أَصْحَـٰبُ ٱلْمَيْمَنَةِ۝٨

    Faashabu almaymanati ma ashabu almaymanati

    Basi watakuwepo wa kuliani; je, ni wepi wa kuliani?8

    Maelezo
    [8] Basi watu wa mkono wa kulia, watu wa cheo kilio bora, utukufu ulioje huo wa hali yao!
  9. وَأَصْحَـٰبُ ٱلْمَشْـَٔمَةِ مَآ أَصْحَـٰبُ ٱلْمَشْـَٔمَةِ۝٩

    Waashabu almashamati ma ashabu almashamati

    Na wa kushotoni; je, ni wepi wa kushotoni?9

    Maelezo
    [9] Na watu wa kushotoni, hao ni watu wa cheo duni, uovu ulioje wa hali yao!
  10. وَٱلسَّـٰبِقُونَ ٱلسَّـٰبِقُونَ۝١٠

    Waalssabiqoona alssabiqoona

    Na wa mbele watakuwa mbele.10

    Maelezo
    [10] Na walio tangulia mbele katika mambo ya kheri duniani ndio watakuwa mbele katika vyeo vya Akhera.
  11. أُو۟لَـٰٓئِكَ ٱلْمُقَرَّبُونَ۝١١

    Olaika almuqarraboona

    Hao ndio watakao karibishwa11

    Maelezo
    [11] Hao ndio walio karibishwa mbele kwa Mwenyezi Mungu. Mola wao Mlezi atawatia katika Bustani zenye neema.
  12. فِى جَنَّـٰتِ ٱلنَّعِيمِ۝١٢

    Fee jannati alnnaʿeemi

    Katika Bustani zenye neema.12

    Maelezo
    [12] Mola wao Mlezi atawatia katika Bustani zenye neema.
  13. ثُلَّةٌ مِّنَ ٱلْأَوَّلِينَ۝١٣

    Thullatun mina alawwaleena

    Fungu kubwa katika wa mwanzo,13

    Maelezo
    [13] Hawa walio karibishwa mbele ni kundi la wengi katika mataifa yaliyo tangulia na Manabii wao,
  14. وَقَلِيلٌ مِّنَ ٱلْـَٔاخِرِينَ۝١٤

    Waqaleelun mina alakhireena

    Na wachache katika wa mwisho.14

    Maelezo
    [14] Na wachache katika umma wa Muhammad ukiwalinganisha na hao.
  15. عَلَىٰ سُرُرٍ مَّوْضُونَةٍ۝١٥

    ʿAla sururin mawdoonatin

    Watakuwa juu ya viti vya fakhari vilivyo tonewa.15

    Maelezo
    [15] Juu ya viti au vitanda vilivyo nakishiwa kwa nakshi za vito vya thamani,
  16. مُّتَّكِـِٔينَ عَلَيْهَا مُتَقَـٰبِلِينَ۝١٦

    Muttakieena ʿalayha mutaqabileena

    Wakiviegemea wakielekeana.16

    Maelezo
    [16] wakivitegemea kwa raha na utulivu huku wakielekezana nyuso kwa ziada ya mahaba.
  17. يَطُوفُ عَلَيْهِمْ وِلْدَٰنٌ مُّخَلَّدُونَ۝١٧

    Yatoofu ʿalayhim wildanun mukhalladoona

    Wakitumikiwa na wavulana wa ujana wa milele,17

    Maelezo
    [17] Wakiwazungukia kwa kuwakhudumia vijana watakao baki milele hivyo hivyo,
  18. بِأَكْوَابٍ وَأَبَارِيقَ وَكَأْسٍ مِّن مَّعِينٍ۝١٨

    Biakwabin waabareeqa wakasin min maʿeenin

    Kwa vikombe na mabirika na bilauri za vinywaji kutoka chemchem safi.18

    Maelezo
    [18] Nao wamechukua vikombe na mabirika yaliyo jaa vinywaji vya Peponi, na bilauri zenye mvinyo kutoka chemchem zinazo miminika,
  19. لَّا يُصَدَّعُونَ عَنْهَا وَلَا يُنزِفُونَ۝١٩

    La yusaddaʿoona ʿanha wala yunzifoona

    Hawataumwa kichwa kwa vinywaji hivyo wala hawatoleweshwa.19

    Maelezo
    [19] Vinywaji hivyo haviwaletei kuumwa kichwa wala kutokwa akili kwa ulevi.
  20. وَفَـٰكِهَةٍ مِّمَّا يَتَخَيَّرُونَ۝٢٠

    Wafakihatin mimma yatakhayyaroona

    Na matunda wayapendayo,20

    Maelezo
    [20] Na matunda ya kila namna wanayo yapenda na wanayo yaona;
  21. وَلَحْمِ طَيْرٍ مِّمَّا يَشْتَهُونَ۝٢١

    Walahmi tayrin mimma yashtahoona

    Na nyama za ndege kama wanavyo tamani.21

    Maelezo
    [21] Na nyama za ndege kama zinavyo tamani nafsi zao.
  22. وَحُورٌ عِينٌ۝٢٢

    Wahoorun ʿeenun

    Na Mahurulaini,22

    Maelezo
    [22] Na wanawake wenye macho ya vikombe,
  23. كَأَمْثَـٰلِ ٱللُّؤْلُؤِ ٱلْمَكْنُونِ۝٢٣

    Kaamthali allului almaknooni

    Walio kama mfano wa lulu zilio hifadhiwa.23

    Maelezo
    [23] Kama mfano wa lulu zilio hifadhiwa katika chaza, kwa usafi wao na urembo wao.
  24. جَزَآءًۢ بِمَا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ۝٢٤

    Jazaan bima kanoo yaʿmaloona

    Ni malipo kwa waliyo kuwa wakiyatenda.24

    Maelezo
    [24] Watapewa haya kuwa ni malipo kwa mambo mema waliyo kuwa wakiyatenda duniani.
  25. لَا يَسْمَعُونَ فِيهَا لَغْوًا وَلَا تَأْثِيمًا۝٢٥

    La yasmaʿoona feeha laghwan wala tatheeman

    Humo hawatasikia porojo wala maneno ya dhambi,25

    Maelezo
    [25] Huko Peponi hawatasikia maneno yasiyo kuwa na maana, wala masimulizi ya kumtia dhambini mwenye kuyasikia.
  26. إِلَّا قِيلًا سَلَـٰمًا سَلَـٰمًا۝٢٦

    Illa qeelan salaman salaman

    Isipo kuwa maneno ya Salama, Salama.26

    Maelezo
    [26] Ila watalo sikia ni kauli ya wao kwa wao: Tunakusalimuni kwa Salama.
  27. وَأَصْحَـٰبُ ٱلْيَمِينِ مَآ أَصْحَـٰبُ ٱلْيَمِينِ۝٢٧

    Waashabu alyameeni ma ashabu alyameeni

    Na wale wa mkono wa kulia, ni yepi yatakuwa ya wa kuliani?27

    Maelezo
    [27] Na watu wa mkono wa kulia, hapana ajuaye nini malipo ya watu wa kuliani.
  28. فِى سِدْرٍ مَّخْضُودٍ۝٢٨

    Fee sidrin makhdoodin

    Katika mikunazi isiyo na miba,28

    Maelezo
    [28] Katika miti ya mikunazi iliyo katwa miba yake,
  29. وَطَلْحٍ مَّنضُودٍ۝٢٩

    Watalhin mandoodin

    Na migomba iliyo pangiliwa,29

    Maelezo
    [29] Na migomba iliyo pangika na ndizi zake zimepandana juu ya mikungu,
  30. وَظِلٍّ مَّمْدُودٍ۝٣٠

    Wathillin mamdoodin

    Na kivuli kilicho tanda,30

    Maelezo
    [30] Na kivuli kilicho enea wala hakiondoki,
  31. وَمَآءٍ مَّسْكُوبٍ۝٣١

    Wamain maskoobin

    Na maji yanayo miminika,31

    Maelezo
    [31] Na maji yanayo miminika karibu yao popote wayatakapo,
  32. وَفَـٰكِهَةٍ كَثِيرَةٍ۝٣٢

    Wafakihatin katheeratin

    Na matunda mengi,32

    Maelezo
    [32] Na matunda ya namna nyingi na kabila nyingi yasiyo tindikia wakati wowote,
  33. لَّا مَقْطُوعَةٍ وَلَا مَمْنُوعَةٍ۝٣٣

    La maqtooʿatin wala mamnooʿatin

    Hayatindikii wala hayakatazwi,33

    Maelezo
    [33] Wala hazuiwiliwi ayatakayo,
  34. وَفُرُشٍ مَّرْفُوعَةٍ۝٣٤

    Wafurushin marfooʿatin

    Na matandiko yaliyo nyanyuliwa.34

    Maelezo
    [34] Na matandiko yaliyo nyanyuliwa ya starehe.
  35. إِنَّآ أَنشَأْنَـٰهُنَّ إِنشَآءً۝٣٥

    Inna anshanahunna inshaan

    Hakika Sisi tutawaumba (Mahurulaini) upya,35

    Maelezo
    [35] Hakika Sisi tulianza kuwaumba Mahurulaini mwanzo,
  36. فَجَعَلْنَـٰهُنَّ أَبْكَارًا۝٣٦

    Fajaʿalnahunna abkaran

    Na tutawafanya vijana,36

    Maelezo
    [36] Na tukawafanya kuwa ni vijana,
  37. عُرُبًا أَتْرَابًا۝٣٧

    ʿUruban atraban

    Wanapendana na waume zao, hirimu moja.37

    Maelezo
    [37] Wenye kupendwa na waume zao, wenye umri ulio karibiana,
  38. لِّأَصْحَـٰبِ ٱلْيَمِينِ۝٣٨

    Liashabi alyameeni

    Kwa ajili ya watu wa kuliani.38

    Maelezo
    [38] Wa tayari kwa neema ya watu wa kuliani.
  39. ثُلَّةٌ مِّنَ ٱلْأَوَّلِينَ۝٣٩

    Thullatun mina alawwaleena

    Fungu kubwa katika wa mwanzo,39

    Maelezo
    [39] Watu wa kulia ni wengi katika mataifu yaliyo kwisha tangulia,
  40. وَثُلَّةٌ مِّنَ ٱلْـَٔاخِرِينَ۝٤٠

    Wathullatun mina alakhireena

    Na fungu kubwa katika wa mwisho.40

    Maelezo
    [40] Na kikundi kikubwa katika umma wa Muhammad.
  41. وَأَصْحَـٰبُ ٱلشِّمَالِ مَآ أَصْحَـٰبُ ٱلشِّمَالِ۝٤١

    Waashabu alshshimali ma ashabu alshshimali

    Na watu wa kushotoni; je ni yepi ya wa kushotoni?41

    Maelezo
    [41] Na watu wa kushoto, hapana anaye jua nini adhabu ya watu wa kushoto.
  42. فِى سَمُومٍ وَحَمِيمٍ۝٤٢

    Fee samoomin wahameemin

    Katika upepo wa moto, na maji yanayo chemka,42

    Maelezo
    [42] Watakuwa kwenye upepo umoto utakao wazunguka, unao penya katika tundu za mwili, na maji yaliyo chemshwa motoni wayanywe na wamiminiwe vichwani,
  43. وَظِلٍّ مِّن يَحْمُومٍ۝٤٣

    Wathillin min yahmoomin

    Na kivuli cha moshi mweusi,43

    Maelezo
    [43] Na katika kivuli cha kiza cheusi cha moshi umoto,
  44. لَّا بَارِدٍ وَلَا كَرِيمٍ۝٤٤

    La baridin wala kareemin

    Si cha kuburudisha wala kustarehesha.44

    Maelezo
    [44] Hapana ubaridi wa kupunguza joto la hewa, wala huruma ya kuwaletea nafuu wanapo vuta pumzi.
  45. إِنَّهُمْ كَانُوا۟ قَبْلَ ذَٰلِكَ مُتْرَفِينَ۝٤٥

    Innahum kanoo qabla thalika mutrafeena

    Hakika hao walikuwa kabla ya haya wakiishi maisha ya anasa.45

    Maelezo
    [45] Hakika hao kabla ya haya walikuwa wamepita kiasi katika kustarehea neema za duniani, wamepumbaa hawataki kumt'ii Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  46. وَكَانُوا۟ يُصِرُّونَ عَلَى ٱلْحِنثِ ٱلْعَظِيمِ۝٤٦

    Wakanoo yusirroona ʿala alhinthi alʿatheemi

    Na walikuwa wakishikilia kufanya madhambi makubwa,46

    Maelezo
    [46] Na walikuwa wameshikilia daima kufanya dhambi kubwa kabisa, kwani waliapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba kabisa Mwenyezi Mungu hatamfufua aliye kufa.
  47. وَكَانُوا۟ يَقُولُونَ أَئِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَـٰمًا أَءِنَّا لَمَبْعُوثُونَ۝٤٧

    Wakanoo yaqooloona aitha mitna wakunna turaban waʿithaman ainna lamabʿoothoona

    Na walikuwa wakisema: Tutakapo kufa na tukawa udongo na mafupa, ati ndio tutafufuliwa?47

    Maelezo
    [47] Na walikuwa wakisema kwa kukanusha kurejea tena: Ati tutafufuliwa baada ya kwisha kufa, na baadhi ya miili yetu ikisha kuwa udongo na mengine mifupa iliyo chakaa? Ati sisi tutarudishwa tuwe hai mara ya pili?
  48. أَوَءَابَآؤُنَا ٱلْأَوَّلُونَ۝٤٨

    Awa abaona alawwaloona

    Au baba zetu wa zamani?48

    Maelezo
    [48] Ati tutafufuliwa sisi na baba zetu wa zamani walio kwisha kuwa udongo ulio tapanyika na umepotea katika ardhi?
  49. قُلْ إِنَّ ٱلْأَوَّلِينَ وَٱلْـَٔاخِرِينَ۝٤٩

    Qul inna alawwaleena waalakhireena

    Sema: Hakika wa zamani na wa mwisho49

    Maelezo
    [49] Waambie kwa kuwajibu kukanusha kwao: Hakika wa zamani na wa mwisho, ambao nyinyi ni katika jumla ya hao,
  50. لَمَجْمُوعُونَ إِلَىٰ مِيقَـٰتِ يَوْمٍ مَّعْلُومٍ۝٥٠

    Lamajmooʿoona ila meeqati yawmin maʿloomin

    Bila ya shaka watakusanywa kwa wakati wa siku maalumu.50

    Maelezo
    [50] Nyote mtakusanywa katika wakati wa siku malumu, na wala hamtoipita.
  51. ثُمَّ إِنَّكُمْ أَيُّهَا ٱلضَّآلُّونَ ٱلْمُكَذِّبُونَ۝٥١

    Thumma innakum ayyuha alddalloona almukaththiboona

    Kisha nyinyi, mlio potea, mnao kanusha,51

    Maelezo
    [51] Kisha nyinyi, enyi mnao ipinga Njia ya Uwongofu, mnao kanusha kufufuliwa,
  52. لَـَٔاكِلُونَ مِن شَجَرٍ مِّن زَقُّومٍ۝٥٢

    Laakiloona min shajarin min zaqqoomin

    Kwa yakini mtakula mti wa Zaqqumu.52

    Maelezo
    [52] Bila ya shaka mtakula mti wa Zaqqumu katika Jahannamu, na mtayajaza matumbo yenu kwa shida ya njaa.
  53. فَمَالِـُٔونَ مِنْهَا ٱلْبُطُونَ۝٥٣

    Famalioona minha albutoona

    Na kwa mti huo mtajaza matumbo.53

    Maelezo
    [53] Na mtayajaza matumbo yenu kwa shida ya njaa.
  54. فَشَـٰرِبُونَ عَلَيْهِ مِنَ ٱلْحَمِيمِ۝٥٤

    Fashariboona ʿalayhi mina alhameemi

    Na juu yake mtakunywa maji yanayo chemka.54

    Maelezo
    [54] Mtakunywa juu ya mlicho kila maji yenye kutokota, yasiyo ondoa kiu,
  55. فَشَـٰرِبُونَ شُرْبَ ٱلْهِيمِ۝٥٥

    Fashariboona shurba alheemi

    Tena mtakunywa kama wanavyo kunywa ngamia wenye kiu.55

    Maelezo
    [55] Na mtakunywa kwa wingi na pupa kama anavyo kunywa ngamia mwenye kiu kisicho katika kiu chake kwa maji.
  56. هَـٰذَا نُزُلُهُمْ يَوْمَ ٱلدِّينِ۝٥٦

    Hatha nuzuluhum yawma alddeeni

    Hiyo ndiyo karamu yao Siku ya Malipo.56

    Maelezo
    [56] Hayo yaliyo tajwa ya mateso mbali mbali ndio karamu yao waliyo andaliwa kwa siku ya malipo.
  57. نَحْنُ خَلَقْنَـٰكُمْ فَلَوْلَا تُصَدِّقُونَ۝٥٧

    Nahnu khalaqnakum falawla tusaddiqoona

    Sisi tumekuumbeni; basi hamsadiki?57

    Maelezo
    [57] Sisi tulianza kukuumbeni mlipo kuwa si chochote, basi hebu hamkiri uweza wetu wa kukurejesheni tena baada ya kukufufueni?
  58. أَفَرَءَيْتُم مَّا تُمْنُونَ۝٥٨

    Afaraaytum ma tumnoona

    Je! Mnaiona mbegu ya uzazi mnayo idondokeza?58

    Maelezo
    [58] Hamuangalii manii mnayo itia katika tumbo la uzazi?
  59. ءَأَنتُمْ تَخْلُقُونَهُۥٓ أَمْ نَحْنُ ٱلْخَـٰلِقُونَ۝٥٩

    Aantum takhluqoonahu am nahnu alkhaliqoona

    Je! Mnaiumba nyinyi, au ni Sisi ndio Waumbaji?59

    Maelezo
    [59] Ni nyinyi ndio mwenye uweza juu yake na kuilea mpaka ikawa mtu, au ni Sisi ndio twenye makadara hayo?
  60. نَحْنُ قَدَّرْنَا بَيْنَكُمُ ٱلْمَوْتَ وَمَا نَحْنُ بِمَسْبُوقِينَ۝٦٠

    Nahnu qaddarna baynakumu almawta wama nahnu bimasbooqeena

    Sisi tumekuwekeeni mauti; na wala Sisi hatushindwi60

    Maelezo
    [60] Sisi tumekuhukumieni mauti, na tumeweka wakati makhsuri wa kufa kwenu. Na wala Sisi si wenye kushindwa kukubadilisheni sura zenu,
  61. عَلَىٰٓ أَن نُّبَدِّلَ أَمْثَـٰلَكُمْ وَنُنشِئَكُمْ فِى مَا لَا تَعْلَمُونَ۝٦١

    ʿAla an nubaddila amthalakum wanunshiakum fee ma la taʿlamoona

    Kuwaleta wengine badala yenu na kukuumbeni nyinyi kwa umbo msilo lijua.61

    Maelezo
    [61] Na wala Sisi si wenye kushindwa kukubadilisheni sura zenu, na kuzileta nyengine, na tukakuumbeni katika umbo jengine na sura nyengine msiyo ijua.
  62. وَلَقَدْ عَلِمْتُمُ ٱلنَّشْأَةَ ٱلْأُولَىٰ فَلَوْلَا تَذَكَّرُونَ۝٦٢

    Walaqad ʿalimtumu alnnashata aloola falawla tathakkaroona

    Na bila ya shaka mlikwisha jua umbo la kwanza, basi kwa nini hamkumbuki?62

    Maelezo
    [62] Bila ya shaka mmekwisha yakinika kuwa Mwenyezi Mungu alikuumbeni mara ya kwanza, basi je, hamkumbuki kwamba Mwenye kuweza hayo ni Mweza zaidi wa kufanya tena.
  63. أَفَرَءَيْتُم مَّا تَحْرُثُونَ۝٦٣

    Afaraaytum ma tahruthoona

    Je! Mnaona makulima mnayo yapanda?63

    Maelezo
    [63] Je! Hamuangalii mbegu mnayo ipanda katika ardhi?
  64. ءَأَنتُمْ تَزْرَعُونَهُۥٓ أَمْ نَحْنُ ٱلزَّٰرِعُونَ۝٦٤

    Aantum tazraʿoonahu am nahnu alzzariʿoona

    Je! Ni nyinyi mnayo yaotesha au ni Sisi ndio wenye kuotesha?64

    Maelezo
    [64] Ni nyinyi mnao ifanya imee au ni Sisi peke yetu ndio tunaifanya imee?
  65. لَوْ نَشَآءُ لَجَعَلْنَـٰهُ حُطَـٰمًا فَظَلْتُمْ تَفَكَّهُونَ۝٦٥

    Law nashao lajaʿalnahu hutaman fathaltum tafakkahoona

    Tungeli taka tungeli yafanya yakawa mapepe, mkabaki mnastaajabu,65

    Maelezo
    [65] Tungeli taka tungeli ifanya mimea hiyo iwe mabua na mapepe yaliyo katika katika kabla haijapevuka, mkawa mkistaajabu tu kwa uovu ulio isibu,
  66. إِنَّا لَمُغْرَمُونَ۝٦٦

    Inna lamughramoona

    Mkisema: Hakika sisi tumegharimika;66

    Maelezo
    [66] Huku mkisema: Hakika sisi tumepata khasara baada ya juhudi yetu.
  67. بَلْ نَحْنُ مَحْرُومُونَ۝٦٧

    Bal nahnu mahroomoona

    Bali sisi tumenyimwa.67

    Maelezo
    [67] Bali sisi hatuna bahati, tumenyimwa riziki.
  68. أَفَرَءَيْتُمُ ٱلْمَآءَ ٱلَّذِى تَشْرَبُونَ۝٦٨

    Afaraaytumu almaa allathee tashraboona

    Je! Mnayaona maji mnayo yanywa?68

    Maelezo
    [68] Je! Hamyaoni maji matamu mnayo yanywa?
  69. ءَأَنتُمْ أَنزَلْتُمُوهُ مِنَ ٱلْمُزْنِ أَمْ نَحْنُ ٱلْمُنزِلُونَ۝٦٩

    Aantum anzaltumoohu mina almuzni am nahnu almunziloona

    Je! Ni nyinyi mnayo yateremsha kutoka mawinguni au ni Sisi ndio wenye kuyateremsha?69

    Maelezo
    [69] Ni nyinyi mnayo yateremsha kutoka mawinguni, au ni Sisi ndio Wenye kuyateremsha kuwa ni rehema juu yenu? Katika Kiarabu limetajwa neno Almuzni. Maana yake ni mawingu yanayo leta mvua. Na kitendo cha kunyesha mvua kinahitajia mambo yaliyo khusiana na hali ya hewa maalumu ambayo mwanaadamu hana mamlaka nayo, au kuyaleta kwa juhudi zake. Kwa mfano zinahitajiwa pepo zinazo kwenda kwa mkondo zilizo baridi juu ya nyengine zilizo za joto, au hali za kuondoka utulivu katika anga. Na watu wamejaribu kuinyesha mvua kwa mawingu yanayo pita kwa njia ya ufundi, lakini juhudi hizo mpaka sasa ni majaribio, na lilio thibiti katika sayansi ni kufuzu kwa majaribio hayo ni kudogo mno, na hata hivyo kunalazimu ziwepo hali maalumu za maumbile zinazo saidia.
  70. لَوْ نَشَآءُ جَعَلْنَـٰهُ أُجَاجًا فَلَوْلَا تَشْكُرُونَ۝٧٠

    Law nashao jaʿalnahu ojajan falawla tashkuroona

    Tungeli penda tungeli yafanya ya chumvi. Basi mbona hamshukuru?70

    Maelezo
    [70] Lau tungeli taka tungeli yafanya hayo maji yakawa ya chumvi yasiyo nyweka. Basi mbona hamumshukuru Mwenyezi Mungu aliye yajaalia matamu yenye kunyweka?
  71. أَفَرَءَيْتُمُ ٱلنَّارَ ٱلَّتِى تُورُونَ۝٧١

    Afaraaytumu alnnara allatee tooroona

    Je! Mnauona moto mnao uwasha?71

    Maelezo
    [71] Je! Hamuuoni moto huo mnao uasha?
  72. ءَأَنتُمْ أَنشَأْتُمْ شَجَرَتَهَآ أَمْ نَحْنُ ٱلْمُنشِـُٔونَ۝٧٢

    Aantum anshatum shajarataha am nahnu almunshioona

    Ni nyinyi mlio uumba mti wake au Sisi ndio Waumbaji?72

    Maelezo
    [72] Ni nyinyi ndio mlio uotesha mti wake, na mkautia ndani ya huo mti moto, au ni Sisi ndio tulio uumbia hivyo, kadhaalika?
  73. نَحْنُ جَعَلْنَـٰهَا تَذْكِرَةً وَمَتَـٰعًا لِّلْمُقْوِينَ۝٧٣

    Nahnu jaʿalnaha tathkiratan wamataʿan lilmuqweena

    Sisi tumeufanya uwe ni ukumbusho na manufaa kwa walioko nyikani.73

    Maelezo
    [73] Sisi tumeufanya huu moto uwe ni ukumbusho wa Moto wa Jahannamu mtapo uona, na uwe ni manufaa kwa wasafiri wa msitu na nyika, wakinafiika kwa kupikia chakula chao na kuotea moto wakati wa baridi.
  74. فَسَبِّحْ بِٱسْمِ رَبِّكَ ٱلْعَظِيمِ۝٧٤

    Fasabbih biismi rabbika alʿatheemi

    Basi litakase jina la Mola wako Mlezi aliye Mkuu.74

    Maelezo
    [74] Basi dumisha kusabihi, kutakasa, kwa kulidhukuru jina la Mola wako Mlezi aliye Mkubwa, kwa kumtakasa na kumshukuru kwa neema hizi nzuri.
  75. ۞ فَلَآ أُقْسِمُ بِمَوَٰقِعِ ٱلنُّجُومِ۝٧٥

    Fala oqsimu bimawaqiʿi alnnujoomi

    Basi naapa kwa maanguko ya nyota,75

    Maelezo
    [75] Basi ninaapa kweli kwa maangukio ya nyota pale zinapo tua mwisho wa usiku wakati wa Tahajudi, ibada za usiku, na kustaghafiru.
  76. وَإِنَّهُۥ لَقَسَمٌ لَّوْ تَعْلَمُونَ عَظِيمٌ۝٧٦

    Wainnahu laqasamun law taʿlamoona ʿatheemun

    Na hakika bila ya shaka hichi ni kiapo kikubwa, laiti mngeli jua!76

    Maelezo
    [76] Na hakika bila ya shaka hicho ni kiapo kikubwa chenye maana ya kufikia mbali, lau kuwa mnafikiri makusudio yake. Aya mbili hizi zinabainisha hadi ya umuhimu wa kiapo hichi kikubwa. Kwani nyota ni vitu vyenye kutoa mwangaza wenyewe, na nyota ya karibu mno kwetu sisi, nayo ni jua, ni kiasi ya masafa ya miaka 500 ya mwangaza. Na nyota ifuatayo kwa ukaribu iko mbali nasi kwa kiasi cha miaka 4 ya mwangaza takriban. Basi nguvu tunazo zitumia kutokana na jua ndizo zinazo tuwezesha kuishi. Lau kuwa umbali wa jua kutokana na ardhi ni duni ya hivyo au zaidi ya hivyo basi hapana shaka kuwa maisha yangeli kuwa taabu, bali ni muhali. Kadhaalika ukubwa wa nyota unakhitalifiana. Zipo nyota kubwa mno hata ukubwa wake unaweza kukusanya hii ardhi na jua juu ya umbali wao. Vipo vikundi vya nyota vinavyo itwa A'naqiid vinaogelea angani zikivuka Njia ya Maziwa The Milky Way mara kwa mara. Wakati wa kupita kwake zikasadifiana kukutana na kikundi cha jua na zikagongana basi hakika hapo itakuwa ndio maangamizo na kumalizika kwa kweli. Hata ikikaribia nyota moja katika nyota zitokazo kwenye jua basi hayo pia yataleta kuharibika mizani na kupelekea maangamizo na kumalizika ulimwengu. Kwa hivyo basi hakika Ishara za mazingatio na uweza wa Mwenyezi Mungu zinaonekana katika ulimwengu huu alio uumba Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala na akaupanga.
  77. إِنَّهُۥ لَقُرْءَانٌ كَرِيمٌ۝٧٧

    Innahu laquranun kareemun

    Hakika hii bila ya shaka ni Qur'ani Tukufu,77

    Maelezo
    [77] Hakika hii bila ya shaka ni Qur'ani yenye manufaa mengi,
  78. فِى كِتَـٰبٍ مَّكْنُونٍ۝٧٨

    Fee kitabin maknoonin

    Katika Kitabu kilicho hifadhiwa.78

    Maelezo
    [78] Imo katika ubao ulio hifadhiwa Al-lauhu-lmahfudh, usio karibiwa na yeyote ila Malaika walio karibishwa kwa Mwenyezi Mungu. (Kwa watumiaji Computer wanaweza kukisia kuwa hiyo Al-lauhu-lmahfudh ni kama Disk iliyomo ndani ya Computer na haigusi mtu, na Misahafu tunayo iona, na kuisoma, ni kama yapigwayo chapa kutoka hiyo Disk.)
  79. لَّا يَمَسُّهُۥٓ إِلَّا ٱلْمُطَهَّرُونَ۝٧٩

    La yamassuhu illa almutahharoona

    Hapana akigusaye ila walio takaswa.79

    Maelezo
    [79] Hawaigusi Qur'ani Tukufu ila walio t'ahirika na najisi na hadathi, vitengua udhu;
  80. تَنزِيلٌ مِّن رَّبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ۝٨٠

    Tanzeelun min rabbi alʿalameena

    Ni uteremsho unao toka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.80

    Maelezo
    [80] imeteremshwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa viumbe vyote.
  81. أَفَبِهَـٰذَا ٱلْحَدِيثِ أَنتُم مُّدْهِنُونَ۝٨١

    Afabihatha alhadeethi antum mudhinoona

    Ni maneno haya ndiyo nyinyi mnayapuuza?81

    Maelezo
    [81] Je! Mnapuuza? Ni Qur'ani hii tukufu ndio nyinyi mnaidharau?
  82. وَتَجْعَلُونَ رِزْقَكُمْ أَنَّكُمْ تُكَذِّبُونَ۝٨٢

    Watajʿaloona rizqakum annakum tukaththiboona

    Na badala ya kushukuru kwa riziki yenu mnafanya kuwa mnakadhibisha?82

    Maelezo
    [82] Na badala ya kuishukuru riziki yenu ndio mna ikadhibisha?
  83. فَلَوْلَآ إِذَا بَلَغَتِ ٱلْحُلْقُومَ۝٨٣

    Falawla itha balaghati alhulqooma

    Yawaje basi itakapo fika roho kwenye koo,83

    Maelezo
    [83] Basi je! Ikifika roho ya mmoja wenu kwenye mapitio ya pumzi,
  84. وَأَنتُمْ حِينَئِذٍ تَنظُرُونَ۝٨٤

    Waantum heenaithin tanthuroona

    Na nyinyi wakati huo mnatazama!84

    Maelezo
    [84] Na nyinyi inapo fika roho kwenye koo nanyi mnamwangalia huyo anaye kufa,
  85. وَنَحْنُ أَقْرَبُ إِلَيْهِ مِنكُمْ وَلَـٰكِن لَّا تُبْصِرُونَ۝٨٥

    Wanahnu aqrabu ilayhi minkum walakin la tubsiroona

    Na Sisi tuko karibu zaidi naye kuliko nyinyi.85

    Maelezo
    [85] Na Sisi tuko karibu zaidi kwa huyo aliye kabiliwa na mauti na tunaijua zaidi hali yake kuliko nyinyi, lakini nyinyi hamjui hayo wala hamhisi.
  86. فَلَوْلَآ إِن كُنتُمْ غَيْرَ مَدِينِينَ۝٨٦

    Falawla in kuntum ghayra madeeneena

    Na lau kuwa nyinyi hamumo katika mamlaka yangu,86

    Maelezo
    [86] Basi je! Ikiwa nyinyi si wenye kunyenyekea kwa Ungu wetu,
  87. تَرْجِعُونَهَآ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ۝٨٧

    Tarjiʿoonaha in kuntum sadiqeena

    Kwanini hamuirudishi hiyo roho, ikiwa nyinyi mnasema kweli?87

    Maelezo
    [87] Mrudishieni roho yake huyo aliye kabiliwa na mauti ikiwa nyinyi mwasema kweli kwamba nyinyi mnazo nguvu na hamshindwi.
  88. فَأَمَّآ إِن كَانَ مِنَ ٱلْمُقَرَّبِينَ۝٨٨

    Faamma in kana mina almuqarrabeena

    Basi akiwa miongoni mwa walio karibishwa,88

    Maelezo
    [88] Ama akiwa huyo aliye kabiliwa na mauti ni katika walio tangulia walio karibishwa ,
  89. فَرَوْحٌ وَرَيْحَانٌ وَجَنَّتُ نَعِيمٍ۝٨٩

    Farawhun warayhanun wajannatu naʿeemin

    Basi ni raha, na manukato, na Bustani zenye neema.89

    Maelezo
    [89] Basi mwisho wake ni raha, na rehema, na riziki njema, na Pepo yenye neema.
  90. وَأَمَّآ إِن كَانَ مِنْ أَصْحَـٰبِ ٱلْيَمِينِ۝٩٠

    Waamma in kana min ashabi alyameeni

    Na akiwa katika watu wa upande wa kulia,90

    Maelezo
    [90] Ama akiwa katika watu wa mkono wa kulia,
  91. فَسَلَـٰمٌ لَّكَ مِنْ أَصْحَـٰبِ ٱلْيَمِينِ۝٩١

    Fasalamun laka min ashabi alyameeni

    Basi ni Salamu kwako uliye miongoni mwa watu wa upande wa kulia.91

    Maelezo
    [91] Basi ataambiwa kwa maamkio na takrima: Unapewa salamu kutokana na watu wa kuliani.
  92. وَأَمَّآ إِن كَانَ مِنَ ٱلْمُكَذِّبِينَ ٱلضَّآلِّينَ۝٩٢

    Waamma in kana mina almukaththibeena alddalleena

    Na ama akiwa katika walio kadhibisha wapotovu,92

    Maelezo
    [92] Na ama akiwa ni katika wa kushoto, wanao kanusha, walio wapotovu,
  93. فَنُزُلٌ مِّنْ حَمِيمٍ۝٩٣

    Fanuzulun min hameemin

    Basi karamu yake ni maji yanayo chemka,93

    Maelezo
    [93] Basi atakirimiwa maji ya moto hadi ya kuchemka,
  94. وَتَصْلِيَةُ جَحِيمٍ۝٩٤

    Watasliyatu jaheemin

    Na kutiwa Motoni.94

    Maelezo
    [94] Na kubabuliwa na moto wa mwisho wa ukali.
  95. إِنَّ هَـٰذَا لَهُوَ حَقُّ ٱلْيَقِينِ۝٩٥

    Inna hatha lahuwa haqqu alyaqeeni

    Hakika hii ndiyo haki yenye yakini.95

    Maelezo
    [95] Hakika haya yaliyo tajwa katika Sura hii tukufu bila ya shaka ni kiini cha yakini iliyo thibiti, isiyo ingiliwa na shaka.
  96. فَسَبِّحْ بِٱسْمِ رَبِّكَ ٱلْعَظِيمِ۝٩٦

    Fasabbih biismi rabbika alʿatheemi

    Basi litakase jina la Mola wako Mlezi aliye Mkubwa.96

    Maelezo
    [96] Tanguliza tasbihi kwa kumdhukuru Mola wako Mlezi aliye Mkubwa, kwa kumtakasa na kumshukuru kwa neema zake.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Surat Al-Waqi’a maana yake ni nini?

Al-Waqi’a maana yake ni “Tukio”.

Surat Al-Waqi’a iko katika juzuu ya ngapi?

Surat Al-Waqi’a iko katika juzuu ya 27.

Surat Al-Waqi’a ina aya ngapi?

Surat Al-Waqi’a ina aya 96.

Surat Al-Waqi’a ni ya Makka au ya Madina?

Surat Al-Waqi’a ni sura ya Makka.

Surat Al-Waqi’a ni sura ya ngapi katika Qur’ani?

Ni sura ya 56 katika Qur’ani.

Vyanzo

  • Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
  • Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
  • Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
  • Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
  • Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
  • Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.

Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.

Mipangilio ya kusoma

Fonti ya Qur’ani
Ukubwa wa Kiarabu
100%
Ukubwa wa tafsiri
100%
Mandhari

Ongeza kwenye skrini ya kwanza

ReadSurahFungua ReadSurah kutoka skrini ya kwanza, kwa skrini nzima. Sura ulizosoma hufunguka hata bila intaneti.

  1. Katika Safari, gusa kitufe cha kushiriki (Share). Kwenye iPhone mpya kiko kwenye menyu ya •••.
  2. Gusa “Add to Home Screen”. Huenda ukahitaji kusogeza chini.
  3. Gusa “Add”.