سورة الفاتحة

Surat Al-Fatiha kwa Kiswahili

Ufunguzi

Msahafu

Mishary Rashid AlafasyPakua MP3Pakua PDF

Surat Al-Fatiha (الفاتحة) ni sura ya kwanza katika Qur’ani na ina aya 7. Jina lake lina maana ya “Ufunguzi”. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na iko katika juzuu ya 1.

Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat Al-Fatiha yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.

Surat Al-Fatiha kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi

  1. بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ۝١

    Bismi Allahi alrrahmani alrraheemi

    KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU .1

    Maelezo
    [1] Sura inaanza kwa Jina la Mwenyezi Mungu ambaye hapana anayefaa kuabudiwa ila Yeye aliye sifika kwa kila sifa za ukamilifu, na ametakasika na kila la upungufu. Yeye ndiye Mwenye rehema ambaye ananeemesha kwa neema kubwa na ndogo, na za kuwapa wote, na za kuwapa walio khusika. Na Yeye ndiye mwenye kusifika kwa sifa ya Rehema yenye kudumu. (Kauli ya mwanzo aliyo semezwa Mtume s.a.w. na kuamrishwa na Mwenyezi Mungu ni "Iqra` bismi Rabbika", yaani: "Soma kwa jina la Mola wako Mlezi!" Naye Mtume s.a.w. amesema: "Jambo lolote lisilo anziwa kwa Bismillahi ni pungufu." Kila Sura ya Qur'ani, isipo kuwa Sura Attawba, imeanziwa kwa Bismillahi Rrahmani Rrahim.)
  2. ٱلْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ۝٢

    Alhamdu lillahi rabbi alʿalameena

    Sifa njema zote ni za Mwenyeezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote;2

    Maelezo
    [2] Sifa njema za namna yote na katika kila hali ni za Mwenyezi Mungu pekee. Na tunamsifu Yeye kwa sifa zote kwa sababu Yeye ndiye mwenye kuviumba viumbe vyote na mwenye kuviangalia na kuvilea. (Neno Rabb, kwa Kiarabu, lina maana ya Ubwana na Ulezi na Utengenezaji. Ndiyo tukatumia Mola Mlezi. Neno Baba lina upungufu.)
  3. ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ۝٣

    Alrrahmani alrraheemi

    Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu;3

    Maelezo
    [3] Na Yeye ndiye Mwenye rehema ya kudumu, na rehema inatokana naye. Ananeemesha kwa neema zote ndogo na kubwa. (Arrahman ni jina lake Mwenyezi Mungu tu, na hafai mtu kuitwa hivyo.)
  4. مَـٰلِكِ يَوْمِ ٱلدِّينِ۝٤

    Maliki yawmi alddeeni

    Mwenye kumiliki siku ya malipo.4

    Maelezo
    [4] Na Yeye peke yake ndiye Mwenye kumiliki Siku ya Malipo na Hisabu, yaani Siku ya Kiyama, anafanya atakavyo wala hapana mwenye kushirikiana naye walau kwa kuonekana tu.
  5. إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ۝٥

    Iyyaka naʿbudu waiyyaka nastaʿeenu

    Wewe tu tunakuabudu, na wewe tu tunakuomba msaada.5

    Maelezo
    [5] Hatumuabudu yeyote ila Wewe tu, wala hatutaki msaada kwa yeyote ila kwako tu.
  6. ٱهْدِنَا ٱلصِّرَٰطَ ٱلْمُسْتَقِيمَ۝٦

    Ihdina alssirata almustaqeema

    Tuongoe njia iliyonyooka.6

    Maelezo
    [6] Tunakuomba utuwafikishe kuendea Njia ya haki, na kheri na mafanikio.
  7. صِرَٰطَ ٱلَّذِينَ أَنْعَمْتَ عَلَيْهِمْ غَيْرِ ٱلْمَغْضُوبِ عَلَيْهِمْ وَلَا ٱلضَّآلِّينَ۝٧

    Sirata allatheena anʿamta ʿalayhim ghayri almaghdoobi ʿalayhim wala alddalleena

    Njia ya ulio waneemesha, siyo ya walio kasirikiwa, wala walio potea.7

    Maelezo
    [7] Na njia hiyo ndiyo ya waja wako ulio wawezesha kukuamini Wewe, na ukawajaalia neema ya uwongofu na radhi, sio njia ya walio stahiki kupata ghadhabu zako na wakaiwacha njia ya haki na kheri, kwa sababu hao wameitupa imani kukuamini Wewe na kuelekea kwenye uwongofu wako. (Hapana katika Vitabu vyote vitakatifu, vya dini zote, dua inayo lingana na hii kwa uzuri wake, na utimilivu wake. Baada ya kumsifu Mwenyezi Mungu kwa Rehema yake isio na ukomo wala kipimo, na kumshukuru Mola Mwenye kuviumba na kuviangalia na kuvilea kwa huruma viumbe vyote, na kuhakikisha kuwa tunajua kuwa hapana Mungu ila Yeye tu wa kuabudiwa na kuombwa msaada, na kuwa hapana wa kumuingilia katika Ufalme wake na Uwezo wake wa kulipa hisabu kwa kila alitendalo mtu, hapo tena ndio tunaomba. Na tunaomba nini? Si mkate wa kula, wala riziki yoyote, wala jambo lolote la manufaa ya kimwili duniani, bali tunaomba Uwongofu kwenye Njia Iliyo Nyooka, Njia ya kumwendea Yeye Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema. Tunaomba tusiendee njia waliyo ifuata wale walio kasirikiwa na Mwenyezi Mungu, kwa kuwa walifunzwa wakajua, lakini kwa chuki na jeuri wakakataa kuongoka, wala sio njia ya wale ambao labda kwa ujinga wamepotea. Hiyo kwa mukhtasari ndiyo Dua ambayo Waislamu, wanafunzwa waiombe, na wanaiomba mara kadhaa wa kadhaa katika Sala zao, na katika kila fursa inapo tokea.)

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Surat Al-Fatiha maana yake ni nini?

Al-Fatiha maana yake ni “Ufunguzi”.

Surat Al-Fatiha iko katika juzuu ya ngapi?

Surat Al-Fatiha iko katika juzuu ya 1.

Surat Al-Fatiha ina aya ngapi?

Surat Al-Fatiha ina aya 7.

Surat Al-Fatiha ni ya Makka au ya Madina?

Surat Al-Fatiha ni sura ya Makka.

Surat Al-Fatiha ni sura ya ngapi katika Qur’ani?

Ni sura ya kwanza katika Qur’ani.

Vyanzo

  • Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
  • Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
  • Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
  • Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
  • Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
  • Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.

Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.

Mipangilio ya kusoma

Fonti ya Qur’ani
Ukubwa wa Kiarabu
100%
Ukubwa wa tafsiri
100%
Mandhari

Ongeza kwenye skrini ya kwanza

ReadSurahFungua ReadSurah kutoka skrini ya kwanza, kwa skrini nzima. Sura ulizosoma hufunguka hata bila intaneti.

  1. Katika Safari, gusa kitufe cha kushiriki (Share). Kwenye iPhone mpya kiko kwenye menyu ya •••.
  2. Gusa “Add to Home Screen”. Huenda ukahitaji kusogeza chini.
  3. Gusa “Add”.