سورة الصافات

Surat As-Saffat kwa Kiswahili

Wanaojipanga Safu

Msahafu

Mishary Rashid AlafasyPakua MP3Pakua PDF

Surat As-Saffat (الصافات) ni sura ya 37 katika Qur’ani na ina aya 182. Jina lake lina maana ya “Wanaojipanga Safu”. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na iko katika juzuu ya 23.

Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat As-Saffat yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.

Surat As-Saffat kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

  1. وَٱلصَّـٰٓفَّـٰتِ صَفًّا۝١

    Waalssaffati saffan

    Naapa kwa wanao jipanga kwa safu.1

    Maelezo
    [1] Naapa kwa mataifa katika viumbe vyangu, walio jipanga wenyewe kwa safu zilio sawa katika msimamo wa ibada na ut'iifu.
  2. فَٱلزَّٰجِرَٰتِ زَجْرًا۝٢

    Faalzzajirati zajran

    Na kwa wenye kukataza mabaya.2

    Maelezo
    [2] Na kwa wanao zuia wanao pindukia mipaka kwa mzuio mkali, nidhamu ibakie, na ulimwengu uhifadhiwe.
  3. فَٱلتَّـٰلِيَـٰتِ ذِكْرًا۝٣

    Faalttaliyati thikran

    Na kwa wenye kusoma Ukumbusho.3

    Maelezo
    [3] Na kwa wenye kusoma Aya, na wanamdhukuru Mwenyezi Mungu kwa dhikri ya Tasbihi, Kumtakasa, na Kumhimidi, kumsifu.
  4. إِنَّ إِلَـٰهَكُمْ لَوَٰحِدٌ۝٤

    Inna ilahakum lawahidun

    Hakika Mungu wenu bila ya shaka ni Mmoja.4

    Maelezo
    [4] Hakika Mungu wenu anaye faa kuabudiwa bila ya shaka ni Mmoja tu. Hana mshirika wake, kwa dhati, wala kitendo, wala sifa.
  5. رَّبُّ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا وَرَبُّ ٱلْمَشَـٰرِقِ۝٥

    Rabbu alssamawati waalardi wama baynahuma warabbu almashariqi

    Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, na yaliyomo kati yao, na ni Mola Mlezi wa mashariki zote.5

    Maelezo
    [5] Yeye - peke yake - ndiye Muumba mbingu na ardhi na viliomo baina yao, na ndiye Mwenye kupanga mambo, na ndiye Mwenye kutawala mashariki za kila chenye mashariki. Mwenyezi Mungu ndiye Muumba mbingu saba na viliomo baina yao, navyo ni hivyo vyombo vya mbinguni na nyota zake. Naye ndiye Mwenye kusimamisha, Mwenye kulinda vile vile juu ya mwahali zinapo chomozea jua na nyota zote. Na Yeye ndiye anaye vionyesha hivyo kila siku katika pahala huko upeo wa macho, kila siku pahala mbali na vilipo dhihiri siku iliyo tangulia. Na hayo ni kwa mwendo wa mpango wa jua maalumu kwa inavyo zunguka dunia juu ya msumari-kati wake kutoka magharibi kwendea mashariki kila siku na wakati huo huo inavyo lizunguka jua katika njia yake katika falaki. Na jua na nyota huonekana na wakaazi wa ardhi kila siku kama zinachomoza mwahala mbali mbali. Na kila ardhi ikigeuza mahala pake katika safari yake katika mbingu linaonekana jua linachomoza pahala pengine. Ukiliangalia jua kwa utulivu kuanzia mwishoni wa mwezi wa Machi, yaani linapo kuwa jua lipo kati ya mstari wa Ikweta mwanzo wa musimu wa Rabii, yaani Spring, kwa nusu ya kaskazini ya dunia, utaliona linachomoza pahala katika mashariki juu ya upeo wa macho. Kwa mwenye kupeleleza kila siku ikipita ataona kuchomoza kwake kunajongelea kaskazini. Na mwishoni mwa mwezi wa Juni utaona linachomozea mwisho wa kukaribia kaskazini. Kisha baada ya hapo utaliona jua linarejea linafuata kugeuka kule kule mpaka mwisho wa Septemba (wakati wa kuwa sawa wakati wa Khariif yaani Autumn) utaliona jua linachomoza pale pale lilipo chomoza mwanzo wa Machi. Kisha litaendelea kuelekea kusini kuchomoza kwake mpaka mwisho wa Desemba linakuwa linachomoza karibu kabisa na kusini. Baada ya hapo huanza tena kurejea kuelekea kaskazini mpaka limalize safari yake ya kufika kati sawa katika Rabii ya pili. Na safari hii yote inachukua siku 365 na robo siku. Na inaonekana kuwa nyota nazo zinachomoza mwahala mbali mbali katika upeo wa macho inapo kuwa dunia imo katika safari yake ya mbinguni, na khasa nyota za buruji (au vituo) 12 vinavyo pitiwa na jua katika mwendo wake wa mwaka.
  6. إِنَّا زَيَّنَّا ٱلسَّمَآءَ ٱلدُّنْيَا بِزِينَةٍ ٱلْكَوَاكِبِ۝٦

    Inna zayyanna alssamaa alddunya bizeenatin alkawakibi

    Hakika Sisi tumeipamba mbingu ya karibu kwa pambo la nyota.6

    Maelezo
    [6] Sisi tumeipamba hii mbingu ya karibu na watu wa duniani kwa mapambo, nayo ni hizo nyota zinazong'ara, zenye ukubwa mbali mbali, na mwahala pao mbali mbali kwenye anga la ulimwengu kama ionekanavyo kwa macho.
  7. وَحِفْظًا مِّن كُلِّ شَيْطَـٰنٍ مَّارِدٍ۝٧

    Wahifthan min kulli shaytanin maridin

    Na kulinda na kila shet'ani a'si.7

    Maelezo
    [7] Na tukaihifadhi hiyo mbingu na kila shetani jabari aliye a'si.
  8. لَّا يَسَّمَّعُونَ إِلَى ٱلْمَلَإِ ٱلْأَعْلَىٰ وَيُقْذَفُونَ مِن كُلِّ جَانِبٍ۝٨

    La yassammaʿoona ila almalai alaʿla wayuqthafoona min kulli janibin

    Wasiweze kuwasikiliza viumbe watukufu. Na wanafukuzwa huko kila upande.8

    Maelezo
    [8] Hao majabari wa kishetani hawawezi kusikiliza yanayo pita katika ulimwengu wa Malaika. Na wao hupopolewa kwa kila kinacho faa cha kuwazuia.
  9. دُحُورًا ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ وَاصِبٌ۝٩

    Duhooran walahum ʿathabun wasibun

    Wakifurushwa. Na wanayo adhabu ya kudumu.9

    Maelezo
    [9] Hufukuzwa hao kwa nguvu wasifikilie kuweza kusikiliza khabari za mbinguni. Na Akhera watapata adhabu kali ya kudumu.
  10. إِلَّا مَنْ خَطِفَ ٱلْخَطْفَةَ فَأَتْبَعَهُۥ شِهَابٌ ثَاقِبٌ۝١٠

    Illa man khatifa alkhatfata faatbaʿahu shihabun thaqibun

    Isipo kuwa anaye nyakua kitu kidogo, na mara humfwatia kimondo kinacho ng'ara.10

    Maelezo
    [10] Isipo kuwa anaye lipata neno moja hivi katika khabari za mbinguni kwa kuibia. Na huyo naye tunamwandama kwa mwenge wa moto unao murika anga kwa mwangaza wake, ukamuunguzilia mbali.
  11. فَٱسْتَفْتِهِمْ أَهُمْ أَشَدُّ خَلْقًا أَم مَّنْ خَلَقْنَآ ۚ إِنَّا خَلَقْنَـٰهُم مِّن طِينٍ لَّازِبٍۭ۝١١

    Faistaftihim ahum ashaddu khalqan am man khalaqna inna khalaqnahum min teenin lazibin

    Hebu waulize: Je! Wao ni wenye umbo gumu zaidi au hao wengine tulio waumba. Hakika Sisi tuliwaumba wao kwa udongo unao nata.11

    Maelezo
    [11] Ewe Nabii! Hebu waulize hao wanao kanya kufufuliwa wanao ona hayawi hayo: Je! Kwani kuwaumba wao hawa ni kugumu zaidi au kuziumba mbingu, na ardhi, na nyota, na vyenginevyo, tulivyo viumba Sisi?
  12. بَلْ عَجِبْتَ وَيَسْخَرُونَ۝١٢

    Bal ʿajibta wayaskharoona

    Bali unastaajabu, na wao wanafanya maskhara.12

    Maelezo
    [12] Hakika Sisi tumewaumba wao kutokana na udongo unao gandana. Basi kwa nini wanaona ajabu kurejezwa tena wao?
  13. وَإِذَا ذُكِّرُوا۟ لَا يَذْكُرُونَ۝١٣

    Waitha thukkiroo la yathkuroona

    Na wanapo kumbushwa hawakumbuki.13

    Maelezo
    [13] Na wanapo kabiliwa kwa dalili za uweza wa Mwenyezi Mungu kufufua, hata hawazishughulikii wakanufaika kwa hizo dalili.
  14. وَإِذَا رَأَوْا۟ ءَايَةً يَسْتَسْخِرُونَ۝١٤

    Waitha raaw ayatan yastaskhiroona

    Na wanapo ona Ishara, wanafanya maskhara.14

    Maelezo
    [14] Na wanapo ona ushahidi wa kuonyesha uweza wa Mwenyezi Mungu huitana wapate kupita mipaka katika kumkejeli.
  15. وَقَالُوٓا۟ إِنْ هَـٰذَآ إِلَّا سِحْرٌ مُّبِينٌ۝١٥

    Waqaloo in hatha illa sihrun mubeenun

    Na husema: Haya si chochote ila ni uchawi tu ulio dhaahiri.15

    Maelezo
    [15] Na makafiri husema juu ya Ishara zinazo onyesha uweza wa Mwenyezi Mungu: Haya tunayo yaona si chochote ila ni uchawi tu.
  16. أَءِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَـٰمًا أَءِنَّا لَمَبْعُوثُونَ۝١٦

    Aitha mitna wakunna turaban waʿithaman ainna lamabʿoothoona

    Ati tukisha kufa na tukawa udongo na mifupa ndio kweli tutafufuliwa?16

    Maelezo
    [16] Hivyo sisi tukisha kufa tukawa udongo na mafupa tutatolewa tena makaburini kwetu tuwe wahai?
  17. أَوَءَابَآؤُنَا ٱلْأَوَّلُونَ۝١٧

    Awaabaona alawwaloona

    Hata baba zetu wa zamani?17

    Maelezo
    [17] Sisi tuwe wahai, na pia watafufuliwa baba zetu wa zamani walio kufa kabla yetu, na wakapotea, na wakateketea?
  18. قُلْ نَعَمْ وَأَنتُمْ دَٰخِرُونَ۝١٨

    Qul naʿam waantum dakhiroona

    Sema: Naam! Hali nanyi ni madhalili.18

    Maelezo
    [18] Ewe Nabii! Waambie: Ndio mtafufuliwa nyote, nanyi ni madhalili na wanyonge.
  19. فَإِنَّمَا هِىَ زَجْرَةٌ وَٰحِدَةٌ فَإِذَا هُمْ يَنظُرُونَ۝١٩

    Fainnama hiya zajratun wahidatun faitha hum yanthuroona

    Huko utapigwa ukelele mmoja tu! Na hapo ndio wataona!19

    Maelezo
    [19] Kwani hakika kufufuliwa ni Ukelele mmoja tu, mara wote watakuwa wahai wakiyaona waliyo ahidiwa.
  20. وَقَالُوا۟ يَـٰوَيْلَنَا هَـٰذَا يَوْمُ ٱلدِّينِ۝٢٠

    Waqaloo ya waylana hatha yawmu alddeeni

    Watasema: Ole wetu! Hii ndiyo Siku ya Malipo.20

    Maelezo
    [20] Na washirikina watasema: Ee msiba wetu huu! Hii ndiyo Siku ya Hisabu na Malipo kwa a'mali zilio tendwa!
  21. هَـٰذَا يَوْمُ ٱلْفَصْلِ ٱلَّذِى كُنتُم بِهِۦ تُكَذِّبُونَ۝٢١

    Hatha yawmu alfasli allathee kuntum bihi tukaththiboona

    Hii ndiyo Siku ya Hukumu mliyo kuwa mkiikadhibisha.21

    Maelezo
    [21] Watajibiwa: Hii ndiyo Siku ya Hukumu na kufarikisha vitendo, mliyo kuwa mkiikadhibisha.
  22. ۞ ٱحْشُرُوا۟ ٱلَّذِينَ ظَلَمُوا۟ وَأَزْوَٰجَهُمْ وَمَا كَانُوا۟ يَعْبُدُونَ۝٢٢

    Ohshuroo allatheena thalamoo waazwajahum wama kanoo yaʿbudoona

    Wakusanyeni walio dhulumu, na wake zao, na hao walio kuwa wakiwaabudu.22

    Maelezo
    [22] Enyi Malaika wangu! Wakusanyeni walio jidhulumu nafsi zao kwa kufuru, pamoja na wake zao wa kikafiri, na miungu yao waliyo kuwa wakiiabudu badala ya Mwenyezi Mungu, yakiwa masanamu au watu, na waonyesheni njia ya kwendea Motoni waingie humo.
  23. مِن دُونِ ٱللَّهِ فَٱهْدُوهُمْ إِلَىٰ صِرَٰطِ ٱلْجَحِيمِ۝٢٣

    Min dooni Allahi faihdoohum ila sirati aljaheemi

    Badala ya Mwenyezi Mungu. Waongozeni njia ya Jahannamu!23

    Maelezo
    [23] Enyi Malaika wangu! Wakusanyeni walio jidhulumu nafsi zao kwa kufuru, pamoja na wake zao wa kikafiri, na miungu yao waliyo kuwa wakiiabudu badala ya Mwenyezi Mungu, yakiwa masanamu au watu, na waonyesheni njia ya kwendea Motoni waingie humo.
  24. وَقِفُوهُمْ ۖ إِنَّهُم مَّسْـُٔولُونَ۝٢٤

    Waqifoohum innahum masooloona

    Na wasimamisheni. Hakika hao watasailiwa:24

    Maelezo
    [24] Na wazuieni hapo hapo; kwani wao hakika watahojiwa juu ya imani zao na vitendo vyao.
  25. مَا لَكُمْ لَا تَنَاصَرُونَ۝٢٥

    Ma lakum la tanasaroona

    Mna nini? Mbona hamsaidiani?25

    Maelezo
    [25] Enyi washirikina! Mna nini? Mbona hamsaidiani kama mlivyo kuwa mkisaidiana nyinyi kwa nyinyi duniani?
  26. بَلْ هُمُ ٱلْيَوْمَ مُسْتَسْلِمُونَ۝٢٦

    Bal humu alyawma mustaslimoona

    Bali hii leo, watasalimu amri.26

    Maelezo
    [26] Leo hii hawasaidiani, bali leo wanaongozwa tu, wamekwisha salimu amri.
  27. وَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَسَآءَلُونَ۝٢٧

    Waaqbala baʿduhum ʿala baʿdin yatasaaloona

    Watakabiliana wao kwa wao kuulizana.27

    Maelezo
    [27] Watakuwa wakikabiliana kulaumiana na kusutana, na wakiulizana khabari za mwisho wao muovu.
  28. قَالُوٓا۟ إِنَّكُمْ كُنتُمْ تَأْتُونَنَا عَنِ ٱلْيَمِينِ۝٢٨

    Qaloo innakum kuntum tatoonana ʿani alyameeni

    Watasema: Kwa hakika nyinyi mlikuwa mkitujia upande wa kulia.28

    Maelezo
    [28] Wanyonge watawaambia walio jipa ukubwa: Nyinyi mlikuwa mkitujia upande tulio udhania ni wa kheri na mafanikio, ili mtugeuze njia tuache Haki twende kwenye upotovu.
  29. قَالُوا۟ بَل لَّمْ تَكُونُوا۟ مُؤْمِنِينَ۝٢٩

    Qaloo bal lam takoonoo mumineena

    Watasema (wakubwa): Bali nyinyi wenyewe hamkuwa Waumini.29

    Maelezo
    [29] Watasema walio jipa ukubwa: Sisi hatukukugeuzeni njia, lakini nyinyi wenyewe mliikataa Imani, na mkaipuuza kwa khiari yenu.
  30. وَمَا كَانَ لَنَا عَلَيْكُم مِّن سُلْطَـٰنٍۭ ۖ بَلْ كُنتُمْ قَوْمًا طَـٰغِينَ۝٣٠

    Wama kana lana ʿalaykum min sultanin bal kuntum qawman tagheena

    Sisi hatukuwa na mamlaka juu yenu, bali nyinyi wenyewe mlikuwa wapotovu.30

    Maelezo
    [30] Na sisi hatukuwa na madaraka juu yenu hata tuweze kukunyang'anyeni uweza wenu wa kukhiari. Bali nyinyi wenyewe mlikuwa watu mlio iacha Haki.
  31. فَحَقَّ عَلَيْنَا قَوْلُ رَبِّنَآ ۖ إِنَّا لَذَآئِقُونَ۝٣١

    Fahaqqa ʿalayna qawlu rabbina inna lathaiqoona

    Basi hukumu ya Mola wetu Mlezi imekwisha tuthibitikia. Hakika bila ya shaka tutaonja tu adhabu.31

    Maelezo
    [31] Basi neno la Mola wetu Mlezi limethibiti juu yetu. Hakika hapana shaka sisi tutaionja adhabu ya Siku ya Kiyama.
  32. فَأَغْوَيْنَـٰكُمْ إِنَّا كُنَّا غَـٰوِينَ۝٣٢

    Faaghwaynakum inna kunna ghaweena

    Tulikupotezeni kwa sababu sisi wenyewe tulikuwa wapotovu.32

    Maelezo
    [32] Tukakuiteni kwenye maasi na upotovu na nyinyi mkaitikia wito wetu. Kazi yetu ni kufanya hila ya kuwaita watu wafuate upotovu tulio nao. Basi hatuna lawama.
  33. فَإِنَّهُمْ يَوْمَئِذٍ فِى ٱلْعَذَابِ مُشْتَرِكُونَ۝٣٣

    Fainnahum yawmaithin fee alʿathabi mushtarikoona

    Basi wao kwa hakika siku hiyo watashirikiana katika adhabu pamoja.33

    Maelezo
    [33] Kwani hakika wafuasi na wenye kufuatwa wote watashiriki pamoja katika adhabu ya Siku ya Kiyama.
  34. إِنَّا كَذَٰلِكَ نَفْعَلُ بِٱلْمُجْرِمِينَ۝٣٤

    Inna kathalika nafʿalu bialmujrimeena

    Hivyo ndivyo tutakavyo wafanyia wakosefu.34

    Maelezo
    [34] Hakika mfano wa adhabu hiyo Sisi tunawapa wale walio fanya makosa katika Haki ya Mwenyezi Mungu kwa ushirikina na kutenda maasi.
  35. إِنَّهُمْ كَانُوٓا۟ إِذَا قِيلَ لَهُمْ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا ٱللَّهُ يَسْتَكْبِرُونَ۝٣٥

    Innahum kanoo itha qeela lahum la ilaha illa Allahu yastakbiroona

    Wao walipo kuwa wakiambiwa La ilaha illa 'Llahu Hapana mungu ila Mwenyezi Mungu tu, wakijivuna.35

    Maelezo
    [35] Hakika watu hao walikuwa wakiambiwa: La ilaha illa 'Llah, Hapana mungu ila Mwenyezi Mungu tu, wakakataa kukiri kwa kiburi na majivuno.
  36. وَيَقُولُونَ أَئِنَّا لَتَارِكُوٓا۟ ءَالِهَتِنَا لِشَاعِرٍ مَّجْنُونٍۭ۝٣٦

    Wayaqooloona ainna latarikoo alihatina lishaʿirin majnoonin

    Na wakisema: Hivyo sisi tuiache miungu yetu kwa ajili ya huyu mtunga mashairi mwendawazimu?36

    Maelezo
    [36] Na husema: Sisi tuache kuabudu miungu yetu kwa kufuata kauli ya mtunga mashairi aliye zugwa asiye kuwa na akili?
  37. بَلْ جَآءَ بِٱلْحَقِّ وَصَدَّقَ ٱلْمُرْسَلِينَ۝٣٧

    Bal jaa bialhaqqi wasaddaqa almursaleena

    Bali huyu amekuja kwa Haki, na amewasadikisha Mitume.37

    Maelezo
    [37] Bali Mtume wao amewaletea Tawhidi, Imani ya Mwenyezi Mungu Mmoja, ambayo ndiyo wito wa Mitume wote, naye akasadikisha kwa hivyo wito wa hao Mitume.
  38. إِنَّكُمْ لَذَآئِقُوا۟ ٱلْعَذَابِ ٱلْأَلِيمِ۝٣٨

    Innakum lathaiqoo alʿathabi alaleemi

    Hakika nyinyi bila ya shaka mtaionja adhabu chungu.38

    Maelezo
    [38] Enyi washirikina! Hakika nyinyi hapana shaka mtaionja adhabu kali ya Akhera.
  39. وَمَا تُجْزَوْنَ إِلَّا مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ۝٣٩

    Wama tujzawna illa ma kuntum taʿmaloona

    Wala hamlipwi ila hayo mliyo kuwa mkiyafanya.39

    Maelezo
    [39] Na hamtapata malipo Akhera ila malipo ya vitendo vyenu vya duniani.
  40. إِلَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلْمُخْلَصِينَ۝٤٠

    Illa ʿibada Allahi almukhlaseena

    Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio khitariwa.40

    Maelezo
    [40] Ila waja wangu walio safika; hao hawataionja adhabu kwa sababu wao ni watu wa Imani na ut'iifu.
  41. أُو۟لَـٰٓئِكَ لَهُمْ رِزْقٌ مَّعْلُومٌ۝٤١

    Olaika lahum rizqun maʿloomun

    Hao ndio watakao pata riziki maalumu,41

    Maelezo
    [41] Hawa watu wa ikhlasi watapata Akhera riziki maalumu kwa Mwenyezi Mungu.
  42. فَوَٰكِهُ ۖ وَهُم مُّكْرَمُونَ۝٤٢

    Fawakihu wahum mukramoona

    Matunda, nao watahishimiwa.42

    Maelezo
    [42] Matunda ya namna mbali mbali. Nao watastareheshwa na kutukuzwa,
  43. فِى جَنَّـٰتِ ٱلنَّعِيمِ۝٤٣

    Fee jannati alnnaʿeemi

    Katika Bustani za neema.43

    Maelezo
    [43] Katika Bustani zenye neema.
  44. عَلَىٰ سُرُرٍ مُّتَقَـٰبِلِينَ۝٤٤

    ʿAla sururin mutaqabileena

    Wako juu ya viti wamekabiliana.44

    Maelezo
    [44] Wakikaa humo juu ya viti wakikabiliana.
  45. يُطَافُ عَلَيْهِم بِكَأْسٍ مِّن مَّعِينٍۭ۝٤٥

    Yutafu ʿalayhim bikasin min maʿeenin

    Wanazungushiwa kikombe chenye kinywaji cha chemchem.45

    Maelezo
    [45] Watawazungukia watoto na chombo chenye kinywaji kilicho toka kwenye chemchem zisio katika.
  46. بَيْضَآءَ لَذَّةٍ لِّلشَّـٰرِبِينَ۝٤٦

    Baydaa laththatin lilshsharibeena

    Kinywaji cheupe, kitamu kwa wanywao.46

    Maelezo
    [46] Kinywaji chenyewe ni cheupe kinapo changanywa, na kitamu kwa wenye kukinywa.
  47. لَا فِيهَا غَوْلٌ وَلَا هُمْ عَنْهَا يُنزَفُونَ۝٤٧

    La feeha ghawlun wala hum ʿanha yunzafoona

    Hakina madhara, wala hakiwaleweshi.47

    Maelezo
    [47] Hakiwaumizi kichwa na kuwaletea ghururi, wala kwa kukinywa hicho haiwapotei akili yao kidogo kidogo, yaani hakileweshi.
  48. وَعِندَهُمْ قَـٰصِرَٰتُ ٱلطَّرْفِ عِينٌ۝٤٨

    Waʿindahum qasiratu alttarfi ʿeenun

    Na watakuwa nao wanawake wenye macho ya staha mazuri.48

    Maelezo
    [48] Na watu hawa wat'iifu walioko Peponi watakuwa nao mahuruleini walio safi, wema, macho yao hayawatazami ila waume zao tu, basi hawayatafuti matamanio maovu, jicho la mwema haliangalii ila mema.
  49. كَأَنَّهُنَّ بَيْضٌ مَّكْنُونٌ۝٤٩

    Kaannahunna baydun maknoonun

    Hao wanawake kama mayai yaliyo hifadhika.49

    Maelezo
    [49] Hao wanawake wenye macho ya staha ni kama mayai ya mbuni, yaliyo hifadhiwa na mbawa zake. Basi hayaguswi na mikono, wala hayapati vumbi.
  50. فَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَسَآءَلُونَ۝٥٠

    Faaqbala baʿduhum ʿala baʿdin yatasaaloona

    Waingie kuulizana wenyewe kwa wenyewe.50

    Maelezo
    [50] Hao watu wema watakuwa wakiingia kuulizana hali, na walikuwaje duniani?
  51. قَالَ قَآئِلٌ مِّنْهُمْ إِنِّى كَانَ لِى قَرِينٌ۝٥١

    Qala qailun minhum innee kana lee qareenun

    Aseme msemaji mmoja miongoni mwao: Hakika mimi nalikuwa na rafiki.51

    Maelezo
    [51] Hapo mmoja wao atasema: Mimi nalikuwa na rafiki katika washirikina, akijadiliana nami katika mambo ya Dini na yaliyo kuja katika Qur'ani.
  52. يَقُولُ أَءِنَّكَ لَمِنَ ٱلْمُصَدِّقِينَ۝٥٢

    Yaqoolu ainnaka lamina almusaddiqeena

    Aliye kuwa akinambia: Hivyo wewe ni katika wanao sadiki.52

    Maelezo
    [52] Akisema: Ati wewe ni katika hao wanao sadiki kuwa kupo kufufuliwa na kuhisabiwa na kulipwa baada ya kufa?
  53. أَءِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَـٰمًا أَءِنَّا لَمَدِينُونَ۝٥٣

    Aitha mitna wakunna turaban waʿithaman ainna lamadeenoona

    Ati tukisha kufa tukawa udongo na mafupa, ndio tutalipwa na kuhisabiwa?53

    Maelezo
    [53] Ati baada ya kwisha teketea, tukawa udongo na mafupa, tutakuja kuwa hai mara nyengine, tuhisabiwe na tulipwe kwa vitendo tulivyo kwisha vitenda?
  54. قَالَ هَلْ أَنتُم مُّطَّلِعُونَ۝٥٤

    Qala hal antum muttaliʿoona

    Atasema: Je! Nyie mnawaona?54

    Maelezo
    [54] Muumini awaambie wenzie alio kaa nao: Enyi watu wa Peponi, mnawaona watu wa Motoni nipate kumwona rafiki yangu?
  55. فَٱطَّلَعَ فَرَءَاهُ فِى سَوَآءِ ٱلْجَحِيمِ۝٥٥

    Faittalaʿa faraahu fee sawai aljaheemi

    Basi atachungulia amwone katikati ya Jahannamu.55

    Maelezo
    [55] Jicho lake lipige duru kuelekea Motoni, na huko amwone sahibu yake wa zamani yuko katikati akiadhibika kwa Moto.
  56. قَالَ تَٱللَّهِ إِن كِدتَّ لَتُرْدِينِ۝٥٦

    Qala taAllahi in kidta laturdeeni

    Atasema: Wallahi! Ulikaribia kunipoteza.56

    Maelezo
    [56] Akimwona aseme: Wallahi! Ulikaribia kule duniani kunihilikisha lau ningeli kufuata katika ukafiri wako na maasiya yako!
  57. وَلَوْلَا نِعْمَةُ رَبِّى لَكُنتُ مِنَ ٱلْمُحْضَرِينَ۝٥٧

    Walawla niʿmatu rabbee lakuntu mina almuhdareena

    Na lau kuwa si neema ya Mola wangu Mlezi bila ya shaka ningeli kuwa miongoni mwa walio hudhurishwa.57

    Maelezo
    [57] Na lau kuwa si neema ya Mola wangu Mlezi kwa hidaya yake na kuniwezesha kwake nikamuamini Mwenyezi Mungu na kufufuka, basi ningeli kuwa mfano wako wewe katika walio hudhurishwa katika hiyo adhabu.
  58. أَفَمَا نَحْنُ بِمَيِّتِينَ۝٥٨

    Afama nahnu bimayyiteena

    Je! Sisi hatutakufa,58

    Maelezo
    [58] Je! Sisi tutakaa milele tukineemeka katika Pepo, wala hatufi kabisa isipo kuwa kule kufa kwetu mara ya kwanza duniani, na wala hatuadhibiwi baada ya kwisha ingia Peponi?
  59. إِلَّا مَوْتَتَنَا ٱلْأُولَىٰ وَمَا نَحْنُ بِمُعَذَّبِينَ۝٥٩

    Illa mawtatana aloola wama nahnu bimuʿaththabeena

    Isipo kuwa kifo chetu cha kwanza? Wala sisi hatutaadhibiwa.59

    Maelezo
    [59] Je! Sisi tutakaa milele tukineemeka katika Pepo, wala hatufi kabisa isipo kuwa kule kufa kwetu mara ya kwanza duniani, na wala hatuadhibiwi baada ya kwisha ingia Peponi?
  60. إِنَّ هَـٰذَا لَهُوَ ٱلْفَوْزُ ٱلْعَظِيمُ۝٦٠

    Inna hatha lahuwa alfawzu alʿatheemu

    Hakika huku bila ya shaka ndiko kufuzu kukubwa.60

    Maelezo
    [60] Hakika haya aliyo tupa Mwenyezi Mungu katika ukarimu wa Peponi bila ya shaka ndiyo kufuzu kukubwa, na kuvuka kukuu na hiyo adhabu tuliyo kuwa tunatahadhari nayo tangu duniani.
  61. لِمِثْلِ هَـٰذَا فَلْيَعْمَلِ ٱلْعَـٰمِلُونَ۝٦١

    Limithli hatha falyaʿmali alʿamiloona

    Kwa mfano wa haya nawatende watendao.61

    Maelezo
    [61] Ili wapate ukarimu wa Akhera kama walio bahatika kuupata Waumini, basi nawafanye kazi duniani hao wafanyao kazi, ili wapate kama walio pata wao.
  62. أَذَٰلِكَ خَيْرٌ نُّزُلًا أَمْ شَجَرَةُ ٱلزَّقُّومِ۝٦٢

    Athalika khayrun nuzulan am shajaratu alzzaqqoomi

    Je! Kukaribishwa hivi si ndio bora, au mti wa Zaqqum?62

    Maelezo
    [62] Je! Hiyo riziki maalumu iliyo andaliwa kwa sababu ya watu wa Peponi ni bora, au mti wa Zaqqum ulio andaliwa kwa ajili ya watu wa Motoni?
  63. إِنَّا جَعَلْنَـٰهَا فِتْنَةً لِّلظَّـٰلِمِينَ۝٦٣

    Inna jaʿalnaha fitnatan lilththalimeena

    Hakika Sisi tumeufanya huo kuwa ni mateso kwa walio dhulumu.63

    Maelezo
    [63] Hakika Sisi tumeujaalia mti huu uwe ni mtihani na adhabu ya Akhera kwa ajili ya washirikina.
  64. إِنَّهَا شَجَرَةٌ تَخْرُجُ فِىٓ أَصْلِ ٱلْجَحِيمِ۝٦٤

    Innaha shajaratun takhruju fee asli aljaheemi

    Hakika huo ni mti unao toka katikati ya Jahannamu.64

    Maelezo
    [64] Hakika huo ni mti ulioko katikati ya Jahannamu, umekulia huko Motoni, na umeumbwa kutokana na huko huko.
  65. طَلْعُهَا كَأَنَّهُۥ رُءُوسُ ٱلشَّيَـٰطِينِ۝٦٥

    Talʿuha kaannahu ruoosu alshshayateeni

    Mashada ya matunda yake kama kwamba vichwa vya mashet'ani.65

    Maelezo
    [65] Matunda yake mabaya kuyatazama, yana sura ya kukirihisha, macho hayapendi kuyatazama, kama vichwa vya mashetani ambavyo kwa hakika watu hawajaviona, lakini mtu humpitikia tu katika dhana jinsi ya ubaya wake.
  66. فَإِنَّهُمْ لَـَٔاكِلُونَ مِنْهَا فَمَالِـُٔونَ مِنْهَا ٱلْبُطُونَ۝٦٦

    Fainnahum laakiloona minha famalioona minha albutoona

    Basi hakika bila ya shaka hao watayala hayo, na wajaze matumbo.66

    Maelezo
    [66] Na wao watakuwa wanakula matunda ya mti huo, na wajaze matumbo yao kwayo. Kwani hawanacho kinginecho cha kukila.
  67. ثُمَّ إِنَّ لَهُمْ عَلَيْهَا لَشَوْبًا مِّنْ حَمِيمٍ۝٦٧

    Thumma inna lahum ʿalayha lashawban min hameemin

    Kisha juu yake wanyweshwe mchanganyo wa maji yamoto yaliyo chemka.67

    Maelezo
    [67] Kisha washirikina hao juu ya kula mti wa Zaqqum watapewa maji yaliyo changanywa, yamoto, ya kuwababua nyuso zao, na kukatakata matumbo yao.
  68. ثُمَّ إِنَّ مَرْجِعَهُمْ لَإِلَى ٱلْجَحِيمِ۝٦٨

    Thumma inna marjiʿahum laila aljaheemi

    Kisha hakika marejeo yao bila ya shaka yatakuwa kwenye Jahannamu.68

    Maelezo
    [68] Tena mwisho wao ni Motoni. Wao watakuwa katika adhabu ya milele. Wataletwa kutoka Motoni waje kula mti wa Zaqqum kisha wanyweshe kinywaji hicho, na tena warejeshwe mahala pao katika Jahannamu.
  69. إِنَّهُمْ أَلْفَوْا۟ ءَابَآءَهُمْ ضَآلِّينَ۝٦٩

    Innahum alfaw abaahum dalleena

    Hakika waliwakuta baba zao wamepotea.69

    Maelezo
    [69] Wao waliwakuta baba zao wamepotoka, na wao wakafanya haraka kufuata zile zile nyayo za baba zao. Wakawa mbioni kwendea njia yao, wakifuata tu wala hawachungui, kama walio timuliwa na wakihimizwa wende mbio mbio kuwafuata hao baba zao bila ya kupima wala kuzingatia.
  70. فَهُمْ عَلَىٰٓ ءَاثَـٰرِهِمْ يُهْرَعُونَ۝٧٠

    Fahum ʿala atharihim yuhraʿoona

    Na wao wakafanya haraka kufuata nyayo zao.70

    Maelezo
    [70] Wao waliwakuta baba zao wamepotoka, na wao wakafanya haraka kufuata zile zile nyayo za baba zao. Wakawa mbioni kwendea njia yao, wakifuata tu wala hawachungui, kama walio timuliwa na wakihimizwa wende mbio mbio kuwafuata hao baba zao bila ya kupima wala kuzingatia.
  71. وَلَقَدْ ضَلَّ قَبْلَهُمْ أَكْثَرُ ٱلْأَوَّلِينَ۝٧١

    Walaqad dalla qablahum aktharu alawwaleena

    Na wao wakafanya haraka kufuata nyayo zao.71

    Maelezo
    [71] Na hakika walipotea njia ya sawa na njia ya Imani wengi katika mataifa yaliyo kwisha tangulia kabla ya hawa washirikina wa Makka.
  72. وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا فِيهِم مُّنذِرِينَ۝٧٢

    Walaqad arsalna feehim munthireena

    Na Sisi hakika tuliwapelekea waonyaji.72

    Maelezo
    [72] Na bila ya shaka Sisi tuliyatumia Mitume hayo mataifa yaliyo tangulia ili wawaonye na wawahadharishe na adhabu ya Mwenyezi Mungu, nao wakawakadhibisha.
  73. فَٱنظُرْ كَيْفَ كَانَ عَـٰقِبَةُ ٱلْمُنذَرِينَ۝٧٣

    Faonthur kayfa kana ʿaqibatu almunthareena

    Basi hebu angalia ulikuje mwisho wa walioonywa.73

    Maelezo
    [73] Basi angalia, ewe uliye jaaliwa kuangalia, ulikuwaje mwisho wa walio onywa na Mitume? Bila ya shaka waliteketezwa, wakawa ni mazingatio kwa watu.
  74. إِلَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلْمُخْلَصِينَ۝٧٤

    Illa ʿibada Allahi almukhlaseena

    Isipokuwa waja wa Mwenyezi Mungu waliokhitariwa.74

    Maelezo
    [74] Lakini walikuwapo Waumini ambao aliwakhitari Mwenyezi Mungu wamuabudu Yeye, ili wapate fadhila za ukarimu wake. Basi hao walizipata thawabu zake, na wakaepukana na adhabu yake.
  75. وَلَقَدْ نَادَىٰنَا نُوحٌ فَلَنِعْمَ ٱلْمُجِيبُونَ۝٧٥

    Walaqad nadana noohun falaniʿma almujeeboona

    Na hakika Nuhu alitwita, na Sisi ni bora wa waitikiaji.75

    Maelezo
    [75] Na hakika Nuhu alitwita alipo kwisha kata tamaa na watu wake, basi na Sisi tukawa ni wabora wa kuitikia wito wake, tulipo muitikia ombi lake, na tukawaangamiza watu wake kwa tofani.
  76. وَنَجَّيْنَـٰهُ وَأَهْلَهُۥ مِنَ ٱلْكَرْبِ ٱلْعَظِيمِ۝٧٦

    Wanajjaynahu waahlahu mina alkarbi alʿatheemi

    Na tulimwokoa yeye na ahali zake kutokana na msiba mkubwa.76

    Maelezo
    [76] Na tukamwokoa Nuhu na walio amini pamoja naye, wasizame na kuteketea kwa tofani.
  77. وَجَعَلْنَا ذُرِّيَّتَهُۥ هُمُ ٱلْبَاقِينَ۝٧٧

    Wajaʿalna thurriyyatahu humu albaqeena

    Na tuliwajaalia dhuriya zake ndio wenye kubakia.77

    Maelezo
    [77] Tukawajaalia vizazi vya Nuhu ndio walio bakia katika ardhi baada ya kuteketea watu wake.
  78. وَتَرَكْنَا عَلَيْهِ فِى ٱلْـَٔاخِرِينَ۝٧٨

    Watarakna ʿalayhi fee alakhireena

    Na tukamwachia (sifa njema) kwa walio kuja baadaye.78

    Maelezo
    [78] Na tukamwachilia Nuhu kutajwa kwa wema na watu walio kuja baada yake wakimdhukuru mpaka Siku ya Kiyama.
  79. سَلَـٰمٌ عَلَىٰ نُوحٍ فِى ٱلْعَـٰلَمِينَ۝٧٩

    Salamun ʿala noohin fee alʿalameena

    Iwe salama kwa Nuhu ulimwenguni kote!79

    Maelezo
    [79] Maamkio ya Salama na Amani kumuamkia Nuhu kutokana na Malaika, na watu, na majini.
  80. إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلْمُحْسِنِينَ۝٨٠

    Inna kathalika najzee almuhsineena

    Kwa hakika hivi ndivyo tunavyo walipa wanao fanya mema.80

    Maelezo
    [80] Hakika Sisi huwalipa walio tenda mema mfano wa haya. Basi aliingia katika Jihadi kulinyanyua Neno letu, na akavumilia maudhi kwa ajili yetu.
  81. إِنَّهُۥ مِنْ عِبَادِنَا ٱلْمُؤْمِنِينَ۝٨١

    Innahu min ʿibadina almumineena

    Hakika yeye ni katika waja wetu walio amini.81

    Maelezo
    [81] Hakika yeye ni miongoni mwa waja wetu walio tuamini, na wakatimiza ahadi yetu, na wakaufikisha Ujumbe wetu.
  82. ثُمَّ أَغْرَقْنَا ٱلْـَٔاخَرِينَ۝٨٢

    Thumma aghraqna alakhareena

    Kisha tukawazamisha wale wengine.82

    Maelezo
    [82] Kisha tukawazamisha wenginewe katika makafiri wa kaumu yake.
  83. ۞ وَإِنَّ مِن شِيعَتِهِۦ لَإِبْرَٰهِيمَ۝٨٣

    Wainna min sheeʿatihi laibraheema

    Na hakika Ibrahim alikuwa katika kundi lake,83

    Maelezo
    [83] Na hakika bila ya shaka Ibrahim alikuwa akifuata ile ile njia yake na mwenendo wake katika kuitia Tawhidi, Imani
  84. إِذْ جَآءَ رَبَّهُۥ بِقَلْبٍ سَلِيمٍ۝٨٤

    Ith jaa rabbahu biqalbin saleemin

    Alipo mjia Mola wake Mlezi kwa moyo mzima.84

    Maelezo
    [84] Alipo mkabili Mola wake Mlezi kwa moyo ulio kuwa nadhifu hauna ushirikina, umemsafia ibada Yeye tu.
  85. إِذْ قَالَ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِۦ مَاذَا تَعْبُدُونَ۝٨٥

    Ith qala liabeehi waqawmihi matha taʿbudoona

    Alimwambia baba yake na watu wake: Mnaabudu nini?85

    Maelezo
    [85] Alipo chukia kuwa baba yake na watu wake wanaabudu masanamu, akawaambia: Ni nini haya masanamu mnayo yaabudu?
  86. أَئِفْكًا ءَالِهَةً دُونَ ٱللَّهِ تُرِيدُونَ۝٨٦

    Aifkan alihatan doona Allahi tureedoona

    Kwa kuzua tu mnataka miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu?86

    Maelezo
    [86] Si mnazua uwongo tu ulio wazi kwa haya myatendayo, kwa kuwa mnamuabudu asiye kuwa Mwenyezi Mungu? Na si mnataka kuzua uzushi huu bila ya udhuru wowote ila kupenda kwenu tu?
  87. فَمَا ظَنُّكُم بِرَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ۝٨٧

    Fama thannukum birabbi alʿalameena

    Mnamdhania nini Mola Mlezi wa walimwengu wote?87

    Maelezo
    [87] Mnamdhania nini huyo ambaye ndiye Mwenye haki ya kuabudiwa kwa kuwa Yeye ndiye Muumba walimwengu wote, mtapo kutana naye na hali nyinyi mmemfanyia washirika wenginewe katika ibada?
  88. فَنَظَرَ نَظْرَةً فِى ٱلنُّجُومِ۝٨٨

    Fanathara nathratan fee alnnujoomi

    Kisha akapiga jicho kutazama nyota.88

    Maelezo
    [88] Basi akazitupia jicho nyota kuzitazama ili apate kuona dalili ya Muumba ulimwengu. Akaziona zinageuka, zinabadilika
  89. فَقَالَ إِنِّى سَقِيمٌ۝٨٩

    Faqala innee saqeemun

    Akasema: Hakika mimi ni mgonjwa!89

    Maelezo
    [89] Akajikhofia nafsi yake asiwe ana upotovu na maradhi ya itikadi.
  90. فَتَوَلَّوْا۟ عَنْهُ مُدْبِرِينَ۝٩٠

    Fatawallaw ʿanhu mudbireena

    Nao wakamwacha, wakampa kisogo.90

    Maelezo
    [90] Watu wake wakamwachilia mbali, na wakapuuza maneno yake.
  91. فَرَاغَ إِلَىٰٓ ءَالِهَتِهِمْ فَقَالَ أَلَا تَأْكُلُونَ۝٩١

    Faragha ila alihatihim faqala ala takuloona

    Basi akaiendea miungu yao kwa siri, akaiambia: Mbona hamli?91

    Maelezo
    [91] Akayaendea kwa haraka yale masanamu kwa kificho, na akayapa chakula ambacho wale washirikina walikiweka mbele yao ili nao wapate baraka yao kwa mujibu wa madai yao. Akasema kwa maskhara na kejeli: Mbona hamli?
  92. مَا لَكُمْ لَا تَنطِقُونَ۝٩٢

    Ma lakum la tantiqoona

    Mna nini hata hamsemi?92

    Maelezo
    [92] Mna nini hata mmeshindwa kusema lolote, hata ndio au sio?
  93. فَرَاغَ عَلَيْهِمْ ضَرْبًۢا بِٱلْيَمِينِ۝٩٣

    Faragha ʿalayhim darban bialyameeni

    Kisha akaigeukia kuipiga kwa mkono wa kulia.93

    Maelezo
    [93] Akayaingilia yale masanamu kuyapiga kwa mkono wa kulia, kwa kuwa ndio wenye nguvu, akayabomoa.
  94. فَأَقْبَلُوٓا۟ إِلَيْهِ يَزِفُّونَ۝٩٤

    Faaqbaloo ilayhi yaziffoona

    Basi wakamjia upesi upesi.94

    Maelezo
    [94] Walipo baini kwamba kuvunjwa miungu yao ni kwa kitendo cha Ibrahim, basi walimkimbilia ili wamtese kwa alivyo watendea miungu yao.
  95. قَالَ أَتَعْبُدُونَ مَا تَنْحِتُونَ۝٩٥

    Qala ataʿbudoona ma tanhitoona

    Akasema: Hivyo mnaviabudu vitu mnavyo vichonga wenyewe95

    Maelezo
    [95] Ibrahim akawaambia kwa kuwahizi: Hivyo nyinyi mnaabudu mawe mliyo yachonga nyinyi wenyewe kwa mikono yenu? Akili zenu zimekwenda wapi?
  96. وَٱللَّهُ خَلَقَكُمْ وَمَا تَعْمَلُونَ۝٩٦

    WaAllahu khalaqakum wama taʿmaloona

    Na hali Mwenyezi Mungu ndiye aliye kuumbeni nyinyi na hivyo mnavyo vifanya!96

    Maelezo
    [96] Na Mwenyezi Mungu ndiye aliye kuumbeni, na akayaumba hata hayo masanamu mnayo yaunda kwa mikono yenu. Basi Yeye peke yake ndiye Mwenye kustahiki kuabudiwa.
  97. قَالُوا۟ ٱبْنُوا۟ لَهُۥ بُنْيَـٰنًا فَأَلْقُوهُ فِى ٱلْجَحِيمِ۝٩٧

    Qaloo ibnoo lahu bunyanan faalqoohu fee aljaheemi

    Wakasema: Mjengeeni jengo, na kisha mtupeni motoni humo!97

    Maelezo
    [97] Hoja ilipo wapata wale wanao abudu masanamu, wakaona hawana ila waingie kutumia nguvu; wakaazimia kumchoma moto. Basi waliambizana: Mjengeeni jengo, na mlijaze moto, na mtupeni katikati yake!
  98. فَأَرَادُوا۟ بِهِۦ كَيْدًا فَجَعَلْنَـٰهُمُ ٱلْأَسْفَلِينَ۝٩٨

    Faaradoo bihi kaydan fajaʿalnahumu alasfaleena

    Basi walitaka kumfanyia vitimbi, lakini tukawafanya wao ndio wa chini.98

    Maelezo
    [98] Kwa haya walikusudia kumteketeza, lakini Mwenyezi Mungu alimwokoa na ule moto baada ya wao kwisha mtumbukiza humo. Hadhi yake ikawa juu kwa utukufu ule, na Mwenyezi Mungu akawafanya wao ndio watu wa chini.
  99. وَقَالَ إِنِّى ذَاهِبٌ إِلَىٰ رَبِّى سَيَهْدِينِ۝٩٩

    Waqala innee thahibun ila rabbee sayahdeeni

    Na akasema: Hakika mimi nahama, nakwenda kwa Mola wangu Mlezi; Yeye ataniongoa.99

    Maelezo
    [99] Ibrahim alipo kata tamaa nao, kuwa hawaamini tena, alisema: Mimi ninahama kwendea pahala alipo niamrisha Mola wangu Mlezi nende. Mola wangu Mlezi atanihidi aniongoze mpaka nifike pahala pa utulivu, penye amani, na nchi nzuri.
  100. رَبِّ هَبْ لِى مِنَ ٱلصَّـٰلِحِينَ۝١٠٠

    Rabbi hab lee mina alssaliheena

    Ewe Mola wangu Mlezi! Nitunukie aliye miongoni mwa watenda mema.100

    Maelezo
    [100] Ewe Mola wangu Mlezi! Nipe dhuriya walio wema wa vitendo, wasimamie hii kazi ya wito kuwaitia watu kwako Wewe, baada yangu.
  101. فَبَشَّرْنَـٰهُ بِغُلَـٰمٍ حَلِيمٍ۝١٠١

    Fabashsharnahu bighulamin haleemin

    Basi tukambashiria mwana aliye mpole.101

    Maelezo
    [101] Malaika wakampa bishara ya kwamba atapata mwana atakaye pambwa kwa akili na upole.
  102. فَلَمَّا بَلَغَ مَعَهُ ٱلسَّعْىَ قَالَ يَـٰبُنَىَّ إِنِّىٓ أَرَىٰ فِى ٱلْمَنَامِ أَنِّىٓ أَذْبَحُكَ فَٱنظُرْ مَاذَا تَرَىٰ ۚ قَالَ يَـٰٓأَبَتِ ٱفْعَلْ مَا تُؤْمَرُ ۖ سَتَجِدُنِىٓ إِن شَآءَ ٱللَّهُ مِنَ ٱلصَّـٰبِرِينَ۝١٠٢

    Falamma balagha maʿahu alssaʿya qala ya bunayya innee ara fee almanami annee athbahuka faonthur matha tara qala ya abati ifʿal ma tumaru satajidunee in shaa Allahu mina alssabireena

    Basi alipo fika makamo ya kwenda na kurudi pamoja naye, alimwambia: Ewe mwanangu! Hakika mimi nimeona usingizini kuwa ninakuchinja. Basi angalia wewe, waonaje? Akasema: Ewe baba yangu! Tenda unavyo amrishwa, utanikuta mimi, Inshallah, katika wanao subiri.102

    Maelezo
    [102] Akazaliwa huyo mwana, na alipo kuwa kijana wa kwenda naye baba yake katika kutafuta haja za maisha, Ibrahim alipewa mtihani kwa ndoto aliyo iota. Ibrahim akasema: Ewe mwanangu! Hakika mimi nimeona usingizini ufunuo kutokana na Mwenyezi Mungu ananitaka nikuchinje! Basi wewe tazama unaonaje? Yule mwana mwema alisema: Ewe baba yangu! Tekeleza amri ya Mola wako Mlezi. Utaniona mimi katika wanao subiri, Inshallah!
  103. فَلَمَّآ أَسْلَمَا وَتَلَّهُۥ لِلْجَبِينِ۝١٠٣

    Falamma aslama watallahu liljabeeni

    Basi wote wawili walipo jisalimisha, na akamlaza juu ya kipaji.103

    Maelezo
    [103] Yule baba na mwanawe walipo iridhia hukumu ya Mwenyezi Mungu, na akamweka juu ya fungu la mchanga na akamlaza juu yake, kipaji chake kikawa juu ya ardhi, akawa tayari kumchinja.
  104. وَنَـٰدَيْنَـٰهُ أَن يَـٰٓإِبْرَٰهِيمُ۝١٠٤

    Wanadaynahu an ya ibraheemu

    Tulimwita: Ewe Ibrahim!.104

    Maelezo
    [104] Na Mwenyezi Mungu akajua umadhubuti wa Ibrahim na mwanawe katika majaribio, Mwenyezi Mungu alimwita Ibrahim kwa wito wa kirafiki: Ewe Ibrahim! Hakika umeuitikia kwa utulivu huo ufunuo wa ndoto, na wala hukusitasita katika kufuata amri. Basi haya yanakutosha. Sisi tunakupunguzia haya majaribio yetu kuwa ni malipo kwa wema wako, kama tunavyo walipa walio wema kwa wema wao.
  105. قَدْ صَدَّقْتَ ٱلرُّءْيَآ ۚ إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلْمُحْسِنِينَ۝١٠٥

    Qad saddaqta alrruya inna kathalika najzee almuhsineena

    Umekwisha itimiliza ndoto. Hakika hivi ndivyo tunavyo walipa wanao tenda mema.105

    Maelezo
    [105] Na Mwenyezi Mungu akajua umadhubuti wa Ibrahim na mwanawe katika majaribio, Mwenyezi Mungu alimwita Ibrahim kwa wito wa kirafiki: Ewe Ibrahim! Hakika umeuitikia kwa utulivu huo ufunuo wa ndoto, na wala hukusitasita katika kufuata amri. Basi haya yanakutosha. Sisi tunakupunguzia haya majaribio yetu kuwa ni malipo kwa wema wako, kama tunavyo walipa walio wema kwa wema wao.
  106. إِنَّ هَـٰذَا لَهُوَ ٱلْبَلَـٰٓؤُا۟ ٱلْمُبِينُ۝١٠٦

    Inna hatha lahuwa albalao almubeenu

    Hakika haya ni majaribio yaliyo dhaahiri.106

    Maelezo
    [106] Hakika majaribio haya tuliyo mjaribia Ibrahim na mwanawe bila ya shaka ni majaribio yaliyo dhihirisha undani wa Imani yao na yakini yao kwa Mola Mlezi wa walimwengu.
  107. وَفَدَيْنَـٰهُ بِذِبْحٍ عَظِيمٍ۝١٠٧

    Wafadaynahu bithibhin ʿatheemin

    Basi tukamtolea fidia kwa dhabihu mtukufu.107

    Maelezo
    [107] Na tukamkomboa kwa mhanga wenye cheo kikubwa, kwa kuwa hayo ni kwa amri ya Mwenyezi Mungu.
  108. وَتَرَكْنَا عَلَيْهِ فِى ٱلْـَٔاخِرِينَ۝١٠٨

    Watarakna ʿalayhi fee alakhireena

    Na tukamwachia (sifa njema) kwa watu walio kuja baadaye.108

    Maelezo
    [108] Na tukaacha atajike kwa sifa nzuri katika ndimi za walio kuja baada yake.
  109. سَلَـٰمٌ عَلَىٰٓ إِبْرَٰهِيمَ۝١٠٩

    Salamun ʿala ibraheema

    Iwe salama kwa Ibrahim!.109

    Maelezo
    [109] Maamkio ya amani na salama kwa Ibrahim!
  110. كَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلْمُحْسِنِينَ۝١١٠

    Kathalika najzee almuhsineena

    Hivi ndivyo tunavyo walipa wanao fanya mema.110

    Maelezo
    [110] Mfano wa malipo kama haya ya kuwakinga na balaa ndivyo tunavyo walipa walio wema katika kufuata amri za Mwenyezi Mungu.
  111. إِنَّهُۥ مِنْ عِبَادِنَا ٱلْمُؤْمِنِينَ۝١١١

    Innahu min ʿibadina almumineena

    Hakika yeye ni katika waja wetu walio amini.111

    Maelezo
    [111] Hakika Ibrahim ni katika waja wetu wanao ifuata Haki.
  112. وَبَشَّرْنَـٰهُ بِإِسْحَـٰقَ نَبِيًّا مِّنَ ٱلصَّـٰلِحِينَ۝١١٢

    Wabashsharnahu biishaqa nabiyyan mina alssaliheena

    Na tukambashiria kuzaliwa Is-haqa, naye ni Nabii miongoni mwa watu wema.112

    Maelezo
    [112] Na kwa amri yetu, Malaika walimbashiria kuwa ataruzukiwa mwana, Is-haqa juu ya kukata tamaa na kuwa mkewe ni tasa. Na kwamba yeye hakika atakuwa Nabii miongoni mwa walio wema.
  113. وَبَـٰرَكْنَا عَلَيْهِ وَعَلَىٰٓ إِسْحَـٰقَ ۚ وَمِن ذُرِّيَّتِهِمَا مُحْسِنٌ وَظَالِمٌ لِّنَفْسِهِۦ مُبِينٌ۝١١٣

    Wabarakna ʿalayhi waʿala ishaqa wamin thurriyyatihima muhsinun wathalimun linafsihi mubeenun

    Na tukambarikia yeye na Is-haqa. Na miongoni mwa dhuriya zao walitokea wema na wenye kudhulumu nafsi zao waziwazi.113

    Maelezo
    [113] Nasi tukamtunukia yeye na mwanawe baraka na kheri duniani na Akhera. Na miongoni mwa vizazi vyao watatokea watakao jifanyia wema nafsi zao kwa Imani na ut'iifu, na watakao jidhulumu kwa upotovu wa ukafiri na maasi.
  114. وَلَقَدْ مَنَنَّا عَلَىٰ مُوسَىٰ وَهَـٰرُونَ۝١١٤

    Walaqad mananna ʿala moosa waharoona

    Na kwa hakika tuliwafanyia hisani Musa na Haruni.114

    Maelezo
    [114] Na bila ya shaka tuliwaneemesha Musa na Haruni kwa kuwapa Unabii na neema kubwa kubwa.
  115. وَنَجَّيْنَـٰهُمَا وَقَوْمَهُمَا مِنَ ٱلْكَرْبِ ٱلْعَظِيمِ۝١١٥

    Wanajjaynahuma waqawmahuma mina alkarbi alʿatheemi

    Na tukawaokoa wao na watu wao kutokana na dhiki kubwa.115

    Maelezo
    [115] Na tukawaokoa wao na watu wao kutokana na dhiki kubwa iliyo kuwa iwashukie kutokana na Firauni na kaumu yake.
  116. وَنَصَرْنَـٰهُمْ فَكَانُوا۟ هُمُ ٱلْغَـٰلِبِينَ۝١١٦

    Wanasarnahum fakanoo humu alghalibeena

    Na tukawanusuru; na wakawa wao ndio wenye kushinda.116

    Maelezo
    [116] Na Sisi tukawanusuru na adui zao, wakawa wao ndio wenye kushinda.
  117. وَءَاتَيْنَـٰهُمَا ٱلْكِتَـٰبَ ٱلْمُسْتَبِينَ۝١١٧

    Waataynahuma alkitaba almustabeena

    Na tukawapa wawili hao Kitabu kinacho bainisha.117

    Maelezo
    [117] Na tukampa Musa na Haruni Kitabu kilicho wazi chenye kubainisha hukumu za Dini, nacho ni Taurati.
  118. وَهَدَيْنَـٰهُمَا ٱلصِّرَٰطَ ٱلْمُسْتَقِيمَ۝١١٨

    Wahadaynahuma alssirata almustaqeema

    Na tukawaongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka.118

    Maelezo
    [118] Na tukawaongoza waifuate Njia iliyo sawa.
  119. وَتَرَكْنَا عَلَيْهِمَا فِى ٱلْـَٔاخِرِينَ۝١١٩

    Watarakna ʿalayhima fee alakhireena

    Na tukawaongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka.119

    Maelezo
    [119] Na tukabakisha sifa njema za kutajika wote wawili hao kwa watu wengineo walio kuja baada yao.
  120. سَلَـٰمٌ عَلَىٰ مُوسَىٰ وَهَـٰرُونَ۝١٢٠

    Salamun ʿala moosa waharoona

    Iwe salama kwa Musa na Haruni!.120

    Maelezo
    [120] Maamkio ya Amani na Salama kwa Musa na Haruni.
  121. إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلْمُحْسِنِينَ۝١٢١

    Inna kathalika najzee almuhsineena

    Hakika hivyo ndivyo tunavyo walipa walio wema.121

    Maelezo
    [121] Hakika mfano wa malipo tuliyo mjazi Musa na Haruni ndivyo tunavyo wajazi wote walio wema.
  122. إِنَّهُمَا مِنْ عِبَادِنَا ٱلْمُؤْمِنِينَ۝١٢٢

    Innahuma min ʿibadina almumineena

    Hakika wawili hao ni katika waja wetu walio amini.122

    Maelezo
    [122] Hakika wawili hao ni katika waja wetu wenye kuifuata Haki.
  123. وَإِنَّ إِلْيَاسَ لَمِنَ ٱلْمُرْسَلِينَ۝١٢٣

    Wainna ilyasa lamina almursaleena

    Na hakika Ilyas bila ya shaka alikuwa miongoni mwa Mitume.123

    Maelezo
    [123] Na hakika Ilyas ni katika hao tulio watuma kwenda waongoa watu wao.
  124. إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِۦٓ أَلَا تَتَّقُونَ۝١٢٤

    Ith qala liqawmihi ala tattaqoona

    Alipo waambia watu wake: Hamwogopi?.124

    Maelezo
    [124] Ilyas alipo waambia watu wake, nao walikuwa wakiyaabudu masanamu yao: Je! Mnaendelea juu ya makosa yenu, na wala hamumkhofu Mwenyezi Mungu mkajikinga na adhabu yake?
  125. أَتَدْعُونَ بَعْلًا وَتَذَرُونَ أَحْسَنَ ٱلْخَـٰلِقِينَ۝١٢٥

    Atadʿoona baʿlan watatharoona ahsana alkhaliqeena

    Mnamwomba Baa'li na mnamwacha Mbora wa waumbaji,.125

    Maelezo
    [125] Mnaliabudu sanamu linalo itwa Baa'li, na mkaacha kumuabudu Mwenyezi Mungu aliye uumba ulimwengu na akaufanya mzuri uumbaji wake?
  126. ٱللَّهَ رَبَّكُمْ وَرَبَّ ءَابَآئِكُمُ ٱلْأَوَّلِينَ۝١٢٦

    Allaha rabbakum warabba abaikumu alawwaleena

    Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu na Mola Mlezi wa baba zenu wa zamani?.126

    Maelezo
    [126] Mwenyezi Mungu amekuumbeni na amekuhifadhini nyinyi na baba zenu wa zamani. Yeye basi ndiye Mwenye haki ya kuabudiwa.
  127. فَكَذَّبُوهُ فَإِنَّهُمْ لَمُحْضَرُونَ۝١٢٧

    Fakaththaboohu fainnahum lamuhdaroona

    Wakamkadhibisha. Basi kwa hakika watahudhurishwa;.127

    Maelezo
    [127] Lakini walimkadhibisha, basi jaza yao ni kuhudhurishwa kwenye Moto Siku ya Kiyama.
  128. إِلَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلْمُخْلَصِينَ۝١٢٨

    Illa ʿibada Allahi almukhlaseena

    Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio safishwa.128

    Maelezo
    [128] Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio safisha Imani yao. Hao basi ndio wenye kufuzu.
  129. وَتَرَكْنَا عَلَيْهِ فِى ٱلْـَٔاخِرِينَ۝١٢٩

    Watarakna ʿalayhi fee alakhireena

    Na tumemwachia (sifa nzuri) kwa walio kuja baadaye.129

    Maelezo
    [129] Na tukamjaalia awe anatajwa kwa wema na ndimi za walio kuja baada yake.
  130. سَلَـٰمٌ عَلَىٰٓ إِلْ يَاسِينَ۝١٣٠

    Salamun ʿala il yaseena

    Iwe salama kwa Ilyas.130

    Maelezo
    [130] Salamu juu ya Ilyasi, au juu yake yeye na watu wake, kwa kuwa kawashinda.
  131. إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلْمُحْسِنِينَ۝١٣١

    Inna kathalika najzee almuhsineena

    Hakika hivyo ndivyo tunavyo walipa walio wema.131

    Maelezo
    [131] Hakika mfano wa malipo tuliyo mlipa Ilyas tunamlipa kila aliye mwema kwa sababu ya wema wake.
  132. إِنَّهُۥ مِنْ عِبَادِنَا ٱلْمُؤْمِنِينَ۝١٣٢

    Innahu min ʿibadina almumineena

    Hakika yeye ni katika waja wetu walio amini.132

    Maelezo
    [132] Hakika Ilyas ni katika waja wetu walio amini.
  133. وَإِنَّ لُوطًا لَّمِنَ ٱلْمُرْسَلِينَ۝١٣٣

    Wainna lootan lamina almursaleena

    Na hakika Lut'i bila ya shaka ni miongoni mwa Mitume.133

    Maelezo
    [133] Na hakika Lut'i ni katika Mitume tulio watuma ili afikishe Ujumbe wetu kwa watu.
  134. إِذْ نَجَّيْنَـٰهُ وَأَهْلَهُۥٓ أَجْمَعِينَ۝١٣٤

    Ith najjaynahu waahlahu ajmaʿeena

    Tulipo mwokoa yeye na ahali zake wote,.134

    Maelezo
    [134] Kwa hakika Sisi tumemwokoa yeye na ahali zake wote kutokana na adhabu iliyo wasibu watu wake.
  135. إِلَّا عَجُوزًا فِى ٱلْغَـٰبِرِينَ۝١٣٥

    Illa ʿajoozan fee alghabireena

    Isipo kuwa mwanamke mkongwe katika wale walio bakia nyuma.135

    Maelezo
    [135] Ila mkewe mkongwe. Yeye bila ya shaka aliteketea pamoja na walio teketea.
  136. ثُمَّ دَمَّرْنَا ٱلْـَٔاخَرِينَ۝١٣٦

    Thumma dammarna alakhareena

    Kisha tukawaangamiza wale wengineo.136

    Maelezo
    [136] Kisha tukawaangamiza wote isipo kuwa Lut'i na walio muamini.
  137. وَإِنَّكُمْ لَتَمُرُّونَ عَلَيْهِم مُّصْبِحِينَ۝١٣٧

    Wainnakum latamurroona ʿalayhim musbiheena

    Na hakika nyinyi mnawapitia wakati wa asubuhi,.137

    Maelezo
    [137] Na hakika nyinyi, watu wa Makka, mnayapitia majumba ya hao kaumu Lut'i katika safari zenu za kwendea Sham asubuhi au usiku. Je! Mmepotelewa na akili zenu hata hamwezi kuzingatia yaliyo wapitia hao kuwa ni malipo ya ukanushaji wao?
  138. وَبِٱلَّيْلِ ۗ أَفَلَا تَعْقِلُونَ۝١٣٨

    Wabiallayli afala taʿqiloona

    Na usiku. Basi je! Hamyatii akilini?.138

    Maelezo
    [138] Na hakika nyinyi, watu wa Makka, mnayapitia majumba ya hao kaumu Lut'i katika safari zenu za kwendea Sham asubuhi au usiku. Je! Mmepotelewa na akili zenu hata hamwezi kuzingatia yaliyo wapitia hao kuwa ni malipo ya ukanushaji wao?
  139. وَإِنَّ يُونُسَ لَمِنَ ٱلْمُرْسَلِينَ۝١٣٩

    Wainna yoonusa lamina almursaleena

    Na hakika Yunus alikuwa miongoni mwa Mitume.139

    Maelezo
    [139] Na hakika Yunus ni miongoni mwa tulio watuma wawafikishie Ujumbe wetu watu.
  140. إِذْ أَبَقَ إِلَى ٱلْفُلْكِ ٱلْمَشْحُونِ۝١٤٠

    Ith abaqa ila alfulki almashhooni

    Alipo kimbia katika jahazi lilio sheheni.140

    Maelezo
    [140] Alipo wahama watu wake bila ya amri ya Mola wake Mlezi, akaliendea jahazi ambalo lilio kwisha sheheni pomoni, akalipanda. Jahazi likapatikana na mambo ikawajibikia lazima mmoja katika abiria atoswe kupunguza shehena yake. Kura ikamuangukia Yunus, akashindwa kwa kura. Akatoswa baharini kwa mujibu wa ada yao zama zile.
  141. فَسَاهَمَ فَكَانَ مِنَ ٱلْمُدْحَضِينَ۝١٤١

    Fasahama fakana mina almudhadeena

    Akaingia katika kupigiwa kura, na akawa katika walio shindwa.141

    Maelezo
    [141] Alipo wahama watu wake bila ya amri ya Mola wake Mlezi, akaliendea jahazi ambalo lilio kwisha sheheni pomoni, akalipanda. Jahazi likapatikana na mambo ikawajibikia lazima mmoja katika abiria atoswe kupunguza shehena yake. Kura ikamuangukia Yunus, akashindwa kwa kura. Akatoswa baharini kwa mujibu wa ada yao zama zile.
  142. فَٱلْتَقَمَهُ ٱلْحُوتُ وَهُوَ مُلِيمٌ۝١٤٢

    Failtaqamahu alhootu wahuwa muleemun

    Samaki akammeza hali ya kuwa ni mwenye kulaumiwa.142

    Maelezo
    [142] Samaki akammeza, naye hakika alistahiki lawama kwa kuikimbia kazi yake ya Daa'wa, Wito, kuwaitia watu wafuate Haki, na kuacha kuwasubiria wale walio kwenda kinyume naye..
  143. فَلَوْلَآ أَنَّهُۥ كَانَ مِنَ ٱلْمُسَبِّحِينَ۝١٤٣

    Falawla annahu kana mina almusabbiheena

    Na ingeli kuwa hakuwa katika wanao mtakasa Mwenyezi Mungu,.143

    Maelezo
    [143] Na lau kuwa Yunus hakuwa katika wanao mtakasa Mwenyezi Mungu, wanao dumu kumdhukuru, angeli kufa ndani ya samaki, wala asingeli toka humo mpaka siku ya kufufuliwa.
  144. لَلَبِثَ فِى بَطْنِهِۦٓ إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ۝١٤٤

    Lalabitha fee batnihi ila yawmi yubʿathoona

    Bila ya shaka angeli kaa ndani yake mpaka siku ya kufufuliwa.144

    Maelezo
    [144] Na lau kuwa Yunus hakuwa katika wanao mtakasa Mwenyezi Mungu, wanao dumu kumdhukuru, angeli kufa ndani ya samaki, wala asingeli toka humo mpaka siku ya kufufuliwa.
  145. ۞ فَنَبَذْنَـٰهُ بِٱلْعَرَآءِ وَهُوَ سَقِيمٌ۝١٤٥

    Fanabathnahu bialʿarai wahuwa saqeemun

    Lakini tulimtupa ufukweni patupu, hali yu mgonjwa.145

    Maelezo
    [145] Tukamtupa pahali patupu kwenye nchi pasipo kuwa na miti wala majumba, naye ni mgonjwa kwa yaliyo mpata. Yaliyo mtokea Sayyidna Yunus a.s. ni muujiza. Lakini nayo si muhali kutokea mtu kumezwa na samaki, na akabakia yuhai ndani yake kwa muda fulani. Mawili yaweza kuwa - Kwanza, ni kuwa huyo samaki ni namna asiye kuwa na meno katika kabila ya nyangumi wakubwa kabisa, kama nyangumi wanao onekana sana katika Bahari ya Kati (Mediterranean). Urefu wake huweza kufika Mita 20. Alibaki Yunus katika mpandikizi wa kinywa chake huyo nyangumi mpaka alipo mtema kwenye ufukwe mtupu, kwani koo ya nyangumi ni nyembamba hawezi kupita mtu. Pili, yaweza kuwa huyo samaki ni namna ya wenye meno pia, kama nyangumi wa ambari, na ambaye pia urefu wake hufika mita 20. Hawa mara kadhaa wa kadhaa huonekana katika Bahari ya Kati. Nyangumi hao yawezekana kwa kawaida kuwameza wanyama wakubwa wanao pita urefu wa mita tatu.
  146. وَأَنۢبَتْنَا عَلَيْهِ شَجَرَةً مِّن يَقْطِينٍ۝١٤٦

    Waanbatna ʿalayhi shajaratan min yaqteenin

    Na tukauotesha juu yake mmea wa kabila ya mung'unye.146

    Maelezo
    [146] Tukauotesha mmea wa kutambaa, usio simama juu ya kigogo, ukamfunika na kumkinga na madhara ya hali ya hewa.
  147. وَأَرْسَلْنَـٰهُ إِلَىٰ مِا۟ئَةِ أَلْفٍ أَوْ يَزِيدُونَ۝١٤٧

    Waarsalnahu ila miati alfin aw yazeedoona

    Na tulimtuma kwa watu laki moja au zaidi.147

    Maelezo
    [147] Hata alipo pata nafuu kutokana na yaliyo msibu, tukamtuma awaendee watu wengi. Wanasema walio waona kuwa wanapata laki moja au zaidi.
  148. فَـَٔامَنُوا۟ فَمَتَّعْنَـٰهُمْ إِلَىٰ حِينٍ۝١٤٨

    Faamanoo famattaʿnahum ila heenin

    Basi wakaamini, na tukawastarehesha kwa muda.148

    Maelezo
    [148] Wakauwitikia wito wake, nasi tukawakunjulia neema zetu kwa muda maalumu.
  149. فَٱسْتَفْتِهِمْ أَلِرَبِّكَ ٱلْبَنَاتُ وَلَهُمُ ٱلْبَنُونَ۝١٤٩

    Faistaftihim alirabbika albanatu walahumu albanoona

    Basi waulize: Ati Mola wako Mlezi ndiye mwenye watoto wa kike, na wao wanao watoto wa kiume?.149

    Maelezo
    [149] Ewe Nabii! Waulize watu wako: Ati Mwenyezi Mungu aliye kuumba ana watoto wa kike kinyume na wao; na wao ndio wana watoto wanaume kinyuma na Yeye?
  150. أَمْ خَلَقْنَا ٱلْمَلَـٰٓئِكَةَ إِنَـٰثًا وَهُمْ شَـٰهِدُونَ۝١٥٠

    Am khalaqna almalaikata inathan wahum shahidoona

    Au tumewaumba Malaika kuwa ni wanawake, na wao wakashuhudia?.150

    Maelezo
    [150] Ati tumewaumba Malaika kuwa ni wanawake, na wao hao makafiri waliona kwa macho yao kuumba kwao, na ndio wakasimulia walio yaona?
  151. أَلَآ إِنَّهُم مِّنْ إِفْكِهِمْ لَيَقُولُونَ۝١٥١

    Ala innahum min ifkihim layaqooloona

    Ati ni kwa uzushi wao ndio wanasema:.151

    Maelezo
    [151] Ewe mwenye kusikia! Yazingatie maneno yao. Hakika wao kwa uwongo wao wanasema: Mwenyezi Mungu amezaa! Na hali Yeye ametakasika na upungufu kama huo wa kuwa mzazi au kuzaliwa. Na hakika bila ya shaka hao ni waongo kwa usemi huo, kwa ushahidi wa dalili nyingi za Upweke wake.
  152. وَلَدَ ٱللَّهُ وَإِنَّهُمْ لَكَـٰذِبُونَ۝١٥٢

    Walada Allahu wainnahum lakathiboona

    Mwenyezi Mungu amezaa! Ama hakika bila ya shaka hao ni waongo!.152

    Maelezo
    [152] Ewe mwenye kusikia! Yazingatie maneno yao. Hakika wao kwa uwongo wao wanasema: Mwenyezi Mungu amezaa! Na hali Yeye ametakasika na upungufu kama huo wa kuwa mzazi au kuzaliwa. Na hakika bila ya shaka hao ni waongo kwa usemi huo, kwa ushahidi wa dalili nyingi za Upweke wake.
  153. أَصْطَفَى ٱلْبَنَاتِ عَلَى ٱلْبَنِينَ۝١٥٣

    Astafa albanati ʿala albaneena

    Ati amekhiari watoto wa kike kuliko wanaume?.153

    Maelezo
    [153] Ati Yeye amejichagulia mwenyewe mabinti ambao kwa madai yenu ndio mnawachukia kuliko watoto wa kiume ambao mnawapenda, na hali Yeye ndiye Mwenye kuwaumba wote, watoto wa kike na wa kiume?
  154. مَا لَكُمْ كَيْفَ تَحْكُمُونَ۝١٥٤

    Ma lakum kayfa tahkumoona

    Mna nini? Mnahukumu vipi nyinyi?.154

    Maelezo
    [154] Ni nini lilio kusibuni hata mkakata hukumu bila ya ushahidi? Vipi mnahukumu hivyo na hali ni upotovu ulio wazi?
  155. أَفَلَا تَذَكَّرُونَ۝١٥٥

    Afala tathakkaroona

    Hamkumbuki?.155

    Maelezo
    [155] Je! Mmesahau dalili za uweza wake na kutakasika kwake, ndio msikumbuke mpaka mkaingia katika upotovu?
  156. أَمْ لَكُمْ سُلْطَـٰنٌ مُّبِينٌ۝١٥٦

    Am lakum sultanun mubeenun

    Au mnayo hoja iliyo wazi?.156

    Maelezo
    [156] Hebu nyinyi mnazo nguvu za ushahidi wa kubainisha wa kuthibitisha hayo mnayo yadai?
  157. فَأْتُوا۟ بِكِتَـٰبِكُمْ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ۝١٥٧

    Fatoo bikitabikum in kuntum sadiqeena

    Basi leteni Kitabu chenu kama mnasema kweli.157

    Maelezo
    [157] Basi leteni hoja zenu, ikiwa mnazo hoja za katika Kitabu cha mbinguni, kama nyinyi ni wakweli katika hayo myasemayo na mnayo yahukumia.
  158. وَجَعَلُوا۟ بَيْنَهُۥ وَبَيْنَ ٱلْجِنَّةِ نَسَبًا ۚ وَلَقَدْ عَلِمَتِ ٱلْجِنَّةُ إِنَّهُمْ لَمُحْضَرُونَ۝١٥٨

    Wajaʿaloo baynahu wabayna aljinnati nasaban walaqad ʿalimati aljinnatu innahum lamuhdaroona

    Na wameweka makhusiano ya nasaba baina yake na majini; na majini wamekwisha jua bila ya shaka kuwa wao watahudhurishwa.158

    Maelezo
    [158] Wakashikilia katika itikadi zao, na wakazua baina ya Mwenyezi Mungu na majini, ambao hawawaoni, kuwa ati yapo makhusiano ya nasaba. Na bila ya shaka hao majini walikwisha jua kuwa makafiri watahudhurishwa mbele ya Mwenyezi Mungu ili wapate malipo yao yasiyo kimbilika.
  159. سُبْحَـٰنَ ٱللَّهِ عَمَّا يَصِفُونَ۝١٥٩

    Subhana Allahi ʿamma yasifoona

    Subhana 'Llah Ametakasika Mwenyezi Mungu na hayo wanayo msingizia.159

    Maelezo
    [159] Mwenyezi Mungu Mtukufu ametakasika na hizo sifa za kuemewa na za upungufu wanazo mzulia kuwa anazo.
  160. إِلَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلْمُخْلَصِينَ۝١٦٠

    Illa ʿibada Allahi almukhlaseena

    Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio safishwa.160

    Maelezo
    [160] Lakini waja wa Mwenyezi Mungu walio khitariwa wakasafishwa hawana makosa ya huo uzushi wa makafiri.
  161. فَإِنَّكُمْ وَمَا تَعْبُدُونَ۝١٦١

    Fainnakum wama taʿbudoona

    Basi hakika nyinyi na mnao waabudu.161

    Maelezo
    [161] Enyi makafiri! Hakika nyinyi, na hao mnao waabudu badala ya Mwenyezi Mungu - Nyinyi kwa kuwaabudu kwenu badala yake Yeye, hamtampoteza yeyote kwa upotovu wenu. Isipo kuwa yule ambaye tangu hapo Mwenyezi Mungu Mtukufu anamjua ni katika watu wa Motoni, na huko ataingia.
  162. مَآ أَنتُمْ عَلَيْهِ بِفَـٰتِنِينَ۝١٦٢

    Ma antum ʿalayhi bifatineena

    Hamwezi kuwapoteza.162

    Maelezo
    [162] Enyi makafiri! Hakika nyinyi, na hao mnao waabudu badala ya Mwenyezi Mungu - Nyinyi kwa kuwaabudu kwenu badala yake Yeye, hamtampoteza yeyote kwa upotovu wenu.
  163. إِلَّا مَنْ هُوَ صَالِ ٱلْجَحِيمِ۝١٦٣

    Illa man huwa sali aljaheemi

    Isipo kuwa yule atakaye ingia Motoni.163

    Maelezo
    [163] Isipo kuwa yule ambaye tangu hapo Mwenyezi Mungu Mtukufu anamjua ni katika watu wa Motoni, na huko ataingia.
  164. وَمَا مِنَّآ إِلَّا لَهُۥ مَقَامٌ مَّعْلُومٌ۝١٦٤

    Wama minna illa lahu maqamun maʿloomun

    Na hapana katika sisi ila anapo mahali pake maalumu.164

    Maelezo
    [164] Na Malaika kuwania kuwa wao ni waja wa Mwenyezi Mungu, wakasema: Hapana yeyote katika sisi ila ana cheo chake maalumu katika ujuzi, na ibada, na wala hakikiuki hicho.
  165. وَإِنَّا لَنَحْنُ ٱلصَّآفُّونَ۝١٦٥

    Wainna lanahnu alssaffoona

    Na hakika bila ya shaka sisi ndio wajipangao safu.165

    Maelezo
    [165] Na sisi tumejipanga safu wenyewe katika misimamo ya kutumika daima.
  166. وَإِنَّا لَنَحْنُ ٱلْمُسَبِّحُونَ۝١٦٦

    Wainna lanahnu almusabbihoona

    Na hakika sisi ndio wenye kusabihi kutakasa.166

    Maelezo
    [166] Na hakika sisi bila ya shaka yoyote ndio wenye kumtakasa Mwenyezi Mungu na kila lisilo kuwa na maelekeo naye katika kila hali.
  167. وَإِن كَانُوا۟ لَيَقُولُونَ۝١٦٧

    Wain kanoo layaqooloona

    Na walikuwapo walio kuwa wakisema:.167

    Maelezo
    [167] Na walikuwapo makafiri wa Makka kabla ya kuteuliwa Mtume s.a.w. ambao wakisema:
  168. لَوْ أَنَّ عِندَنَا ذِكْرًا مِّنَ ٱلْأَوَّلِينَ۝١٦٨

    Law anna ʿindana thikran mina alawwaleena

    Tungeli kuwa na Ukumbusho kama wa watu wa zamani,.168

    Maelezo
    [168] Lau kuwa sisi tungeli kuwa na Kitabu kama Vitabu vya watu wa zamani, yaani kama Taurati na Injili, nasi bila ya shaka tungeli kuwa waja wa Mwenyezi Mungu wenye kumsafia ibada Yeye.
  169. لَكُنَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلْمُخْلَصِينَ۝١٦٩

    Lakunna ʿibada Allahi almukhlaseena

    Bila ya shaka tungeli kuwa ni waja wa Mwenyezi Mungu wenye ikhlasi.169

    Maelezo
    [169] Nasi bila ya shaka tungeli kuwa waja wa Mwenyezi Mungu wenye kumsafia ibada Yeye.
  170. فَكَفَرُوا۟ بِهِۦ ۖ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ۝١٧٠

    Fakafaroo bihi fasawfa yaʿlamoona

    Lakini waliukataa. Basi watakuja jua.170

    Maelezo
    [170] Na Kitabu kikawajia, nao wakakikataa. Basi watakuja jua nini matokeo ya kukataa kwao.
  171. وَلَقَدْ سَبَقَتْ كَلِمَتُنَا لِعِبَادِنَا ٱلْمُرْسَلِينَ۝١٧١

    Walaqad sabaqat kalimatuna liʿibadina almursaleena

    Na bila ya shaka neno letu lilikwisha tangulia kwa waja wetu walio tumwa.171

    Maelezo
    [171] Ninaapa! Hukumu yetu kwa Mitume tulio watuma imekwisha tolewa mbele, ya kwamba ushindi na matokeo mema ni yao wao dhidi ya makafiri.
  172. إِنَّهُمْ لَهُمُ ٱلْمَنصُورُونَ۝١٧٢

    Innahum lahumu almansooroona

    Ya kuwa wao bila ya shaka ndio watakao nusuriwa.172

    Maelezo
    [172] Ninaapa! Hukumu yetu kwa Mitume tulio watuma imekwisha tolewa mbele, ya kwamba ushindi na matokeo mema ni yao wao dhidi ya makafiri.
  173. وَإِنَّ جُندَنَا لَهُمُ ٱلْغَـٰلِبُونَ۝١٧٣

    Wainna jundana lahumu alghaliboona

    Na kwamba jeshi letu ndilo litakalo shinda.173

    Maelezo
    [173] Na kwamba wafuasi wetu na wasaidizi wetu ndio peke yao watakao washinda walio kengeuka.
  174. فَتَوَلَّ عَنْهُمْ حَتَّىٰ حِينٍ۝١٧٤

    Fatawalla ʿanhum hatta heenin

    Basi waachilie mbali kwa mda.174

    Maelezo
    [174] Basi waachilie mbali, nawe ngoja mpaka wakati ujao. Kwani Sisi tutakupa wewe matokeo mema, na manusura, na ushindi.
  175. وَأَبْصِرْهُمْ فَسَوْفَ يُبْصِرُونَ۝١٧٥

    Waabsirhum fasawfa yubsiroona

    Na watazame, nao wataona.175

    Maelezo
    [175] Nawe watazame, na uangalie vyema adhabu gani na mateso yatakayo wapata kwa kwenda kinyume nawe na kukukadhibisha. Basi watakuja ona kwa macho yao zitakavyo shindwa safu zao, na wataona nusura ya Mwenyezi Mungu inavyo wafikia Waumini.
  176. أَفَبِعَذَابِنَا يَسْتَعْجِلُونَ۝١٧٦

    Afabiʿathabina yastaʿjiloona

    Je! Wanaihimiza adhabu yetu?.176

    Maelezo
    [176] Je! Wamepoteza akili zao nini, hata wakawa wanaihimiza adhabu yetu?
  177. فَإِذَا نَزَلَ بِسَاحَتِهِمْ فَسَآءَ صَبَاحُ ٱلْمُنذَرِينَ۝١٧٧

    Faitha nazala bisahatihim fasaa sabahu almunthareena

    Basi itakapo shuka uwanjani kwao, itakuwa asubuhi mbaya kwa walio onywa.177

    Maelezo
    [177] Basi adhabu hiyo itakapo teremka kwenye uwanja wao mpana, itakuwa asubuhi ovu kweli hiyo kwa hao walio onywa na adhabu.
  178. وَتَوَلَّ عَنْهُمْ حَتَّىٰ حِينٍ۝١٧٨

    Watawalla ʿanhum hatta heenin

    Na waache kwa muda.178

    Maelezo
    [178] Na waachilie mbali mpaka mambo yatakapo waishia.
  179. وَأَبْصِرْ فَسَوْفَ يُبْصِرُونَ۝١٧٩

    Waabsir fasawfa yubsiroona

    Na tazama, na wao wataona.179

    Maelezo
    [179] Na yaangalie yatakayo wafika wao na yatakayo kufika wewe. Wao watakuja yaona hayo wanayo yahimiza.
  180. سُبْحَـٰنَ رَبِّكَ رَبِّ ٱلْعِزَّةِ عَمَّا يَصِفُونَ۝١٨٠

    Subhana rabbika rabbi alʿizzati ʿamma yasifoona

    Subhana Rabbi'l'Izzat Ametakasika Mola Mlezi Mwenye enzi na yale wanayo mzulia.180

    Maelezo
    [180] Mwenyezi Mungu, aliye kuumba wewe na aliye ziumba nguvu na ushindi, ametakasika na huo uzushi wanao muambatisha naye.
  181. وَسَلَـٰمٌ عَلَى ٱلْمُرْسَلِينَ۝١٨١

    Wasalamun ʿala almursaleena

    Na Salamu juu ya Mitume.181

    Maelezo
    [181] Na salamu zishuke juu ya Mitume wapenzi walio safika.
  182. وَٱلْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ۝١٨٢

    Waalhamdu lillahi rabbi alʿalameena

    Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote.182

    Maelezo
    [182] Na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu peke yake, Muumba wa viumbe vyote, na Mwenye kuwaangalia makhaluku wote.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Surat As-Saffat maana yake ni nini?

As-Saffat maana yake ni “Wanaojipanga Safu”.

Surat As-Saffat iko katika juzuu ya ngapi?

Surat As-Saffat iko katika juzuu ya 23.

Surat As-Saffat ina aya ngapi?

Surat As-Saffat ina aya 182.

Surat As-Saffat ni ya Makka au ya Madina?

Surat As-Saffat ni sura ya Makka.

Surat As-Saffat ni sura ya ngapi katika Qur’ani?

Ni sura ya 37 katika Qur’ani.

Vyanzo

  • Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
  • Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
  • Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
  • Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
  • Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
  • Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.

Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.

Mipangilio ya kusoma

Fonti ya Qur’ani
Ukubwa wa Kiarabu
100%
Ukubwa wa tafsiri
100%
Mandhari

Ongeza kwenye skrini ya kwanza

ReadSurahFungua ReadSurah kutoka skrini ya kwanza, kwa skrini nzima. Sura ulizosoma hufunguka hata bila intaneti.

  1. Katika Safari, gusa kitufe cha kushiriki (Share). Kwenye iPhone mpya kiko kwenye menyu ya •••.
  2. Gusa “Add to Home Screen”. Huenda ukahitaji kusogeza chini.
  3. Gusa “Add”.