Surat Sad (ص) ni sura ya 38 katika Qur’ani na ina aya 88. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na iko katika juzuu ya 23.
Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat Sad yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.
Surat Sad kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
-
صٓ ۚ وَٱلْقُرْءَانِ ذِى ٱلذِّكْرِ١
Sad waalqurani thee alththikri
S'ad, Naapa kwa Qur'ani yenye mawaidha.1
Maelezo
[1] S'ad: Ni harufi iliyo anzia Sura hii kama zilivyo anzia baadhi ya Sura nyengine kwa mpango wa Qur'ani katika kuanzia kwa harufi moja moja. Naapa kwa Qur'ani yenye utukufu na shani kubwa kuwa hakika hii ni Kweli isiyo na shaka yoyote. -
بَلِ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ فِى عِزَّةٍ وَشِقَاقٍ٢
Bali allatheena kafaroo fee ʿizzatin washiqaqin
Lakini walio kufuru wamo katika majivuno na upinzani .2
Maelezo
[2] Lakini walio kufuru wamo katika majivuno, hawataki kufuata Haki, na wanawafanyia inda watu wa Haki. -
كَمْ أَهْلَكْنَا مِن قَبْلِهِم مِّن قَرْنٍ فَنَادَوا۟ وَّلَاتَ حِينَ مَنَاصٍ٣
Kam ahlakna min qablihim min qarnin fanadaw walata heena manasin
Mataifa mangapi tumeyaangamiza kabla yao, na wakapiga kelele, lakini wakati wa kuokoka ulikwisha pita.3
Maelezo
[3] Mataifa mengi tuliyateketeza kabla yao, wakapiga kelele kutaka msaada ilipo wafikia adhabu. Lakini huo haukuwa wakati wa kuiepuka adhabu. -
وَعَجِبُوٓا۟ أَن جَآءَهُم مُّنذِرٌ مِّنْهُمْ ۖ وَقَالَ ٱلْكَـٰفِرُونَ هَـٰذَا سَـٰحِرٌ كَذَّابٌ٤
Waʿajiboo an jaahum munthirun minhum waqala alkafiroona hatha sahirun kaththabun
Na walistaajabu kuwajia mwonyaji anaye tokana nao wenyewe, na makafiri wakasema: Huyu ni mchawi, mwongo.4
Maelezo
[4] Na walistaajabu watu hawa kuwa amewajia Mtume binaadamu kama wao, na wakasema hao wanao upinga Ujumbe wake: Huyu ni mdanganyifu, mwongo. -
أَجَعَلَ ٱلْـَٔالِهَةَ إِلَـٰهًا وَٰحِدًا ۖ إِنَّ هَـٰذَا لَشَىْءٌ عُجَابٌ٥
Ajaʿala alalihata ilahan wahidan inna hatha lashayon ʿujabun
Amewafanya miungu wote kuwa ni Mungu Mmoja tu? Hakika hili ni jambo la ajabu.5
Maelezo
[5] Ati amewafanya miungu yote kuwa ni Mungu mmoja tu! Ama hakika jambo hili ni la ajabu, mwisho wa kustaajabisha. -
وَٱنطَلَقَ ٱلْمَلَأُ مِنْهُمْ أَنِ ٱمْشُوا۟ وَٱصْبِرُوا۟ عَلَىٰٓ ءَالِهَتِكُمْ ۖ إِنَّ هَـٰذَا لَشَىْءٌ يُرَادُ٦
Waintalaqa almalao minhum ani imshoo waisbiroo ʿala alihatikum inna hatha lashayon yuradu
Na wakaondoka wakubwa wao wakiwaambia: Nendeni zenu na dumuni na miungu yenu, kwani hili ni jambo lililo pangwa.6
Maelezo
[6] Wakubwa wao wakakimbilia kuusiana wao kwa wao wakiambiana: Endeleeni na njia yenu hiyo hiyo, na shikilieni kuiabudu miungu yenu. Kwani hakika tumepangiwa jambo kubwa hili. -
مَا سَمِعْنَا بِهَـٰذَا فِى ٱلْمِلَّةِ ٱلْـَٔاخِرَةِ إِنْ هَـٰذَآ إِلَّا ٱخْتِلَـٰقٌ٧
Ma samiʿna bihatha fee almillati alakhirati in hatha illa ikhtilaqun
Sisi hatukusikia haya katika mila hii ya mwisho. Haya si chochote ila ni uzushi tu.7
Maelezo
[7] Hatujapata kusikia haya mambo ya Tawhidi, kumfanya Mungu mmoja tu, katika dini ya baba zetu tulio wawahi kuwaona. Haya si chochote ila ni uwongo tu ulio zuliwa. -
أَءُنزِلَ عَلَيْهِ ٱلذِّكْرُ مِنۢ بَيْنِنَا ۚ بَلْ هُمْ فِى شَكٍّ مِّن ذِكْرِى ۖ بَل لَّمَّا يَذُوقُوا۟ عَذَابِ٨
Aonzila ʿalayhi alththikru min baynina bal hum fee shakkin min thikree bal lamma yathooqoo ʿathabi
Ati yeye tu ndiye aliye teremshiwa mawaidha peke yake katika sisi? Lakini hao wana shaka na mawaidha yangu, bali hawajaionja adhabu yangu.8
Maelezo
[8] Basi katika sote sisi, amechaguliwa Muhammad tu peke yake kupewa hishima ya kuteremshiwa Qur'ani? -
أَمْ عِندَهُمْ خَزَآئِنُ رَحْمَةِ رَبِّكَ ٱلْعَزِيزِ ٱلْوَهَّابِ٩
Am ʿindahum khazainu rahmati rabbika alʿazeezi alwahhabi
Au wanazo wao khazina za rehema za Mola wako Mlezi, Mwenye nguvu, Mpaji?9
Maelezo
[9] Bali sisi tunawauliza hawa wanao kuhusudu: Kwani wao wanazo khazina za rehema ya Mola wako Mlezi Mwenye nguvu, Mwingi wa kutoa, hata wao wawe ndio wa kuteua nani wa kumpa Unabii kwa mujibu wa mapenzi ya nafsi zao? -
أَمْ لَهُم مُّلْكُ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا ۖ فَلْيَرْتَقُوا۟ فِى ٱلْأَسْبَـٰبِ١٠
Am lahum mulku alssamawati waalardi wama baynahuma falyartaqoo fee alasbabi
Au wao wana ufalme wa mbingu na ardhi na viliomo kati yao? Basi nawazipande njia za kwendea huko!10
Maelezo
[10] Tena tunawauliza: Kwani wao wanao ufalme wa mbingu na ardhi na viliomo baina yao? Ikiwa hivyo basi nawazipande ngazi mpaka wafikie pahala ambapo watakuwa wakitoa hukumu kama watakavyo, kama wanaweza! -
جُندٌ مَّا هُنَالِكَ مَهْزُومٌ مِّنَ ٱلْأَحْزَابِ١١
Jundun ma hunalika mahzoomun mina alahzabi
Hao ni askari watao shindwa miongoni mwa makundi yatayo shindwa.11
Maelezo
[11] Hao ni askari wanyonge walio shindwa, hapana hivi wala hivi, kama walivyo shindwa mfano kama wao walio jikusanya kuwapinga Manabii. -
كَذَّبَتْ قَبْلَهُمْ قَوْمُ نُوحٍ وَعَادٌ وَفِرْعَوْنُ ذُو ٱلْأَوْتَادِ١٢
Kaththabat qablahum qawmu noohin waʿadun wafirʿawnu thoo alawtadi
Walikanusha kabla yao kaumu ya Nuhu, na kina A'adi na Firauni mwenye majengo.12
Maelezo
[12] Kabla ya hawa, walikadhibisha kaumu ya Nuhu, kina A'adi na Firauni aliye kuwa na majengo makubwa yaliyo simama imara kama milima, na kina Thamudi na Kaumu Lut'i na Kaumu ya Shuaibu, na watu wa Machakani, kwenye miti mingi iliyo shikamana. Hao ndio walio jumuika kuwapinga Mitume wao kama walivyo jumuika watu wako. -
وَثَمُودُ وَقَوْمُ لُوطٍ وَأَصْحَـٰبُ لْـَٔيْكَةِ ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ ٱلْأَحْزَابُ١٣
Wathamoodu waqawmu lootin waashabu alaykati olaika alahzabu
Na Thamud na kaumu Lut'i na watu wa Machakani. Hayo ndiyo makundi.13
Maelezo
[13] Na kina Thamudi na Kaumu Lut'i na Kaumu ya Shuaibu, na watu wa Machakani, kwenye miti mingi iliyo shikamana. Hao ndio walio jumuika kuwapinga Mitume wao kama walivyo jumuika watu wako. -
إِن كُلٌّ إِلَّا كَذَّبَ ٱلرُّسُلَ فَحَقَّ عِقَابِ١٤
In kullun illa kaththaba alrrusula fahaqqa ʿiqabi
Hao wote waliwakadhibisha Mitume; basi wakastahiki adhabu yangu.14
Maelezo
[14] Hapana mmoja katika hao wote ila alimkadhibisha Mtume wake, na kwa hivyo ikawashukia adhabu yangu. -
وَمَا يَنظُرُ هَـٰٓؤُلَآءِ إِلَّا صَيْحَةً وَٰحِدَةً مَّا لَهَا مِن فَوَاقٍ١٥
Wama yanthuru haolai illa sayhatan wahidatan ma laha min fawaqin
Na hawa hawangojei ila ukelele mmoja tu usio na muda.15
Maelezo
[15] Na hao walio jiunga kuwapinga Mitume hawangojei ila ukelele mmoja usio hitajia kukaririwa. -
وَقَالُوا۟ رَبَّنَا عَجِّل لَّنَا قِطَّنَا قَبْلَ يَوْمِ ٱلْحِسَابِ١٦
Waqaloo rabbana ʿajjil lana qittana qabla yawmi alhisabi
Na wao husema: Mola wetu Mlezi! Tuletee upesi sehemu yetu ya adhabu kabla ya Siku ya Hisabu.16
Maelezo
[16] Na makafiri husema kwa kejeli: Mola wetu Mlezi! Tuhimizie sehemu yetu ya adhabu kabla ya Siku ya Malipo. -
ٱصْبِرْ عَلَىٰ مَا يَقُولُونَ وَٱذْكُرْ عَبْدَنَا دَاوُۥدَ ذَا ٱلْأَيْدِ ۖ إِنَّهُۥٓ أَوَّابٌ١٧
Isbir ʿala ma yaqooloona waothkur ʿabdana dawooda tha alaydi innahu awwabun
Subiri kwa hayo wayasemayo, na umkumbuke mja wetu Daudi, mwenye nguvu. Hakika yeye alikuwa mwingi wa kutubia.17
Maelezo
[17] Ewe Muhammad! Yastahamilie hayo wanayo yasema juu yako washirikina. Na mkumbuke mja wetu, Daudi, mwenye nguvu katika Dini na dunia. Hakika yeye alikuwa mwingi wa kurejea kwa Mwenyezi Mungu katika hali zote. -
إِنَّا سَخَّرْنَا ٱلْجِبَالَ مَعَهُۥ يُسَبِّحْنَ بِٱلْعَشِىِّ وَٱلْإِشْرَاقِ١٨
Inna sakhkharna aljibala maʿahu yusabbihna bialʿashiyyi waalishraqi
Hakika tuliidhalilisha milima pamoja naye ikisabihi jioni na asubuhi pamoja naye.18
Maelezo
[18] Hakika Sisi tuliidhalilisha milima pamoja naye, yeye akichuma manufaa kutoka humo, na hiyo milima ikimtakasa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kila upungufu, wakati wa mwisho wa mchana na mwanzo wake. -
وَٱلطَّيْرَ مَحْشُورَةً ۖ كُلٌّ لَّهُۥٓ أَوَّابٌ١٩
Waalttayra mahshooratan kullun lahu awwabun
Na pia ndege walio kusanywa makundi kwa makundi; wote walikuwa wanyenyekevu kwake.19
Maelezo
[19] Na pia tukamdhalilishia ndege walio kusanywa kutokana na kila namna na kila pahali. Vyote hivyo, milima na ndege, vikimwitikia Daudi kama atakavyo, akivisarifu kama apendavyo kwa maslaha ya umma. -
وَشَدَدْنَا مُلْكَهُۥ وَءَاتَيْنَـٰهُ ٱلْحِكْمَةَ وَفَصْلَ ٱلْخِطَابِ٢٠
Washadadna mulkahu waataynahu alhikmata wafasla alkhitabi
Na tukautia nguvu ufalme wake, na tukampa hikima, na kukata hukumu.20
Maelezo
[20] Tukautia nguvu ufalme wake, na tukampa Unabii na kupambanua baina ya Haki na baat'ili. -
۞ وَهَلْ أَتَىٰكَ نَبَؤُا۟ ٱلْخَصْمِ إِذْ تَسَوَّرُوا۟ ٱلْمِحْرَابَ٢١
Wahal ataka nabao alkhasmi ith tasawwaroo almihraba
Na je! Imekufikia khabari ya wagombanao walipo pindukia ukuta kuingia chumbani?21
Maelezo
[21] Ewe Muhammad! Ati imekujia khabari ya makhasimu wagombanao, walio mjia Daudi kwa kupindukia kuta za mihrabuni palipo kuwa pahala pake pa ibada? Hawakupita mlangoni. -
إِذْ دَخَلُوا۟ عَلَىٰ دَاوُۥدَ فَفَزِعَ مِنْهُمْ ۖ قَالُوا۟ لَا تَخَفْ ۖ خَصْمَانِ بَغَىٰ بَعْضُنَا عَلَىٰ بَعْضٍ فَٱحْكُم بَيْنَنَا بِٱلْحَقِّ وَلَا تُشْطِطْ وَٱهْدِنَآ إِلَىٰ سَوَآءِ ٱلصِّرَٰطِ٢٢
Ith dakhaloo ʿala dawooda fafaziʿa minhum qaloo la takhaf khasmani bagha baʿduna ʿala baʿdin faohkum baynana bialhaqqi wala tushtit waihdina ila sawai alssirati
Walipo muingilia Daudi, naye akawaogopa. Wakasema: Usiogope! Sisi ni wagombanao wawili, mmoja wetu amemdhulumu mwenziwe. Basi tuhukumu kwa haki, wala usipendelee. Na utuongoe kwenye njia iliyo sawa.22
Maelezo
[22] Walipo muingilia Daudi, naye akawaogopa, akababaika. Wakasema: Usikhofu kitu. Sisi ni wenye kuzozana, tumedhulumiana. Basi tuhukumu kwa uadilifu wala usiupindukie huo uadilifu. Na tuongoze kwenye njia iliyo sawa sawa. -
إِنَّ هَـٰذَآ أَخِى لَهُۥ تِسْعٌ وَتِسْعُونَ نَعْجَةً وَلِىَ نَعْجَةٌ وَٰحِدَةٌ فَقَالَ أَكْفِلْنِيهَا وَعَزَّنِى فِى ٱلْخِطَابِ٢٣
Inna hatha akhee lahu tisʿun watisʿoona naʿjatan waliya naʿjatun wahidatun faqala akfilneeha waʿazzanee fee alkhitabi
Hakika huyu ndugu yangu ana kondoo wa kike tisiini na tisa; na mimi ninaye kondoo mke mmoja. Akasema: Nipe huyo nikufugie! Na amenishinda kwa maneno.23
Maelezo
[23] Mmoja wa hao wagombanao alisema: Hakika huyu ndugu yangu anao kondoo wa kike tisiini na tisa, na mimi ninaye kondoo mmoja tu. Akasema: Nache niwe nakuchungia kama ninavyo wachunga wangu. Na akanishinda katika usemi. -
قَالَ لَقَدْ ظَلَمَكَ بِسُؤَالِ نَعْجَتِكَ إِلَىٰ نِعَاجِهِۦ ۖ وَإِنَّ كَثِيرًا مِّنَ ٱلْخُلَطَآءِ لَيَبْغِى بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ إِلَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ وَقَلِيلٌ مَّا هُمْ ۗ وَظَنَّ دَاوُۥدُ أَنَّمَا فَتَنَّـٰهُ فَٱسْتَغْفَرَ رَبَّهُۥ وَخَرَّ رَاكِعًا وَأَنَابَ ۩٢٤
Qala laqad thalamaka bisuali naʿjatika ila niʿajihi wainna katheeran mina alkhulatai layabghee baʿduhum ʿala baʿdin illa allatheena amanoo waʿamiloo alssalihati waqaleelun ma hum wathanna dawoodu annama fatannahu faistaghfara rabbahu wakharra rakiʿan waanaba
Akasema: Kweli amekudhulumu kwa kumtaka kondoo wako mmoja kuongezea kwenye kondoo wake. Na hakika washirika wengi hudhulumiana wao kwa wao, isipo kuwa walio amini na wakatenda mema. Na hao ni wachache. Na Daudi akajua kuwa tumemfanyia mtihani. Basi akamwomba msamaha Mola wake Mlezi, na akaanguka kusujudu na kutubia.24
Maelezo
[24] Daudi akasema kabla hajasikia maneno ya yule mwenye ugomvi mwengine: Hakika huyo amekudhulumu kwa kumtaka kondoo wako amchanganye na wale wake. Na hakika wengi wenye kushirikiana hudhulumiana wao kwa wao, isipo kuwa wale ambao Imani yao imetulia katika nyoyo zao, na wakawa wanatenda mema. Na watu kama hao ni wachache, shida kupatikana. Na Daudi akajua kuwa jambo hili si chochote ila ni mtihani tuliyo mfanyia Sisi. Basi akaomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu, na akainama kurukuu kwa Mwenyezi Mungu, na akarejea kwa Mwenyezi Mungu kwa unyenyekevu. -
فَغَفَرْنَا لَهُۥ ذَٰلِكَ ۖ وَإِنَّ لَهُۥ عِندَنَا لَزُلْفَىٰ وَحُسْنَ مَـَٔابٍ٢٥
Faghafarna lahu thalika wainna lahu ʿindana lazulfa wahusna maabin
Basi tukamsamehe kwa hayo. Naye kwa hakika anao mkaribisho mkubwa na marejeo mazuri kwetu.25
Maelezo
[25] Na Sisi tukamsamehe kule kufanya haraka ya kutoa hukumu. Na hali yeye ana hadhi na marejeo mazuri kwetu. -
يَـٰدَاوُۥدُ إِنَّا جَعَلْنَـٰكَ خَلِيفَةً فِى ٱلْأَرْضِ فَٱحْكُم بَيْنَ ٱلنَّاسِ بِٱلْحَقِّ وَلَا تَتَّبِعِ ٱلْهَوَىٰ فَيُضِلَّكَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ ۚ إِنَّ ٱلَّذِينَ يَضِلُّونَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ لَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌۢ بِمَا نَسُوا۟ يَوْمَ ٱلْحِسَابِ٢٦
Ya dawoodu inna jaʿalnaka khaleefatan fee alardi faohkum bayna alnnasi bialhaqqi wala tattabiʿi alhawa fayudillaka ʿan sabeeli Allahi inna allatheena yadilloona ʿan sabeeli Allahi lahum ʿathabun shadeedun bima nasoo yawma alhisabi
Ewe Daudi! Hakika Sisi tumekufanya wewe uwe Khalifa katika nchi. Basi wahukumu watu kwa haki, wala usifuate matamanio yakakupoteza kwenye Njia ya Mwenyezi Mungu. Hakika wanao ipotea Njia ya Mwenyezi Mungu wakaiacha, watapata adhabu kali kwa sababu ya kusahau kwao Siku ya Hisabu.26
Maelezo
[26] Na Mwenyezi Mungu alimfunulia kwa kumwambia: Ewe Daudi! Hakika Sisi tumekufanya wewe uwe Khalifa, yaani Naibu, wetu katika ardhi. Basi wahukumu watu kwa sharia niliyo kupa, wala usiendeshe hukumu kufuata matamanio yao, yakakupotosha njia ya Mwenyezi Mungu. Hakika wendao pogo na njia ya Mwenyezi Mungu kwa kufuata matamanio yao wao watapata adhabu kali kwa kughafilika kwao na Siku ya Malipo. -
وَمَا خَلَقْنَا ٱلسَّمَآءَ وَٱلْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا بَـٰطِلًا ۚ ذَٰلِكَ ظَنُّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ ۚ فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ كَفَرُوا۟ مِنَ ٱلنَّارِ٢٧
Wama khalaqna alssamaa waalarda wama baynahuma batilan thalika thannu allatheena kafaroo fawaylun lillatheena kafaroo mina alnnari
Na hatukuziumba mbingu na ardhi na viliomo ndani yao bure. Hiyo ni dhana ya walio kufuru. Ole wao walio kufuru kwa Moto utao wapata.27
Maelezo
[27] Wala Sisi hatukuziumba mbingu na ardhi na viliomo baina yao kwa mchezo. Hayo ndiyo wanayo yadhania makafiri. Na kwa hivyo wakapitisha hukumu kwa mujibu wa pumbao zao. Basi hao walio kufuru watapata adhabu kali ya Moto. -
أَمْ نَجْعَلُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ كَٱلْمُفْسِدِينَ فِى ٱلْأَرْضِ أَمْ نَجْعَلُ ٱلْمُتَّقِينَ كَٱلْفُجَّارِ٢٨
Am najʿalu allatheena amanoo waʿamiloo alssalihati kaalmufsideena fee alardi am najʿalu almuttaqeena kaalfujjari
Je! Tuwafanye walio amini na wakatenda mema kama wafanyao uharibifu katika nchi? Au tuwafanye wachamngu kama waovu?28
Maelezo
[28] Inaelekeana vipi na hikima yetu na uadilifu wetu tuwafanye sawa baina ya Waumini wenye kutenda mema, na wale wanao fanya uharibifu katika ardhi? Au yaelekea vipi tuwaweke sawa baina ya wenye kuikhofu adhabu yetu na wakaiogopa ikabu yetu na wale walio waasi wakenda kinyume na hukumu zetu? -
كِتَـٰبٌ أَنزَلْنَـٰهُ إِلَيْكَ مُبَـٰرَكٌ لِّيَدَّبَّرُوٓا۟ ءَايَـٰتِهِۦ وَلِيَتَذَكَّرَ أُو۟لُوا۟ ٱلْأَلْبَـٰبِ٢٩
Kitabun anzalnahu ilayka mubarakun liyaddabbaroo ayatihi waliyatathakkara oloo alalbabi
Na hiki Kitabu, tumekuteremshia wewe, kimebarikiwa, ili wazizingatie Aya zake, na wawaidhike wenye akili.29
Maelezo
[29] Ewe Muhammad! Hichi tulicho kuteremshia ni Kitabu chenye manufaa mengi, ili wenye akili nzuri na nyoyo za kufahamu wapate kuzielewa Aya zake, na wawaidhike kwazo. -
وَوَهَبْنَا لِدَاوُۥدَ سُلَيْمَـٰنَ ۚ نِعْمَ ٱلْعَبْدُ ۖ إِنَّهُۥٓ أَوَّابٌ٣٠
Wawahabna lidawooda sulaymana niʿma alʿabdu innahu awwabun
Na Daudi tukamtunukia Suleiman. Alikuwa mja mwema. Na hakika alikuwa mwingi wa kutubia.30
Maelezo
[30] Na Daudi tulimtunukia mwana, aitwaye Suleiman, mwenye kustahiki sifa nzuri, ambaye anafaa kuitwa, "Mja mwema kweli". Kwa sababu yeye alikuwa mwingi mno wa kurejea kwa Mwenyezi Mungu katika kila hali. -
إِذْ عُرِضَ عَلَيْهِ بِٱلْعَشِىِّ ٱلصَّـٰفِنَـٰتُ ٱلْجِيَادُ٣١
Ith ʿurida ʿalayhi bialʿashiyyi alssafinatu aljiyadu
Alipo pelekewa jioni farasi wasimamao kidete, tayari kutoka shoti;31
Maelezo
[31] Na hebu taja katika khabari za Suleiman kuwa alipelekewa alasiri farasi wa asli ambao hutulia wanapo simama, na huenda mbio wanapo kwenda. -
فَقَالَ إِنِّىٓ أَحْبَبْتُ حُبَّ ٱلْخَيْرِ عَن ذِكْرِ رَبِّى حَتَّىٰ تَوَارَتْ بِٱلْحِجَابِ٣٢
Faqala innee ahbabtu hubba alkhayri ʿan thikri rabbee hatta tawarat bialhijabi
Basi akasema: Navipenda vitu vizuri kwa kumkumbuka Mola wangu Mlezi. Kisha wakafichikana nyuma ya boma.32
Maelezo
[32] Suleiman akasema: Hakika mimi nimenyweshwa mapenzi ya farasi, kwa sababu hawa ni katika matayarisho ya mambo ya kheri, nayo ni Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Mapenzi haya yametokana na kumkumbuka Mola wangu Mlezi. Na hakusita kushughulika kuwaangalia mpaka wakapotea machoni mwake. -
رُدُّوهَا عَلَىَّ ۖ فَطَفِقَ مَسْحًۢا بِٱلسُّوقِ وَٱلْأَعْنَاقِ٣٣
Ruddooha ʿalayya fatafiqa mashan bialssooqi waalaʿnaqi
Nirudishieni! Akaanza kuwapapasa miguu na shingo.33
Maelezo
[33] Akaamrisha warudishwe tena kwake apate kujua hali yao. Akaingia kuwapapasa miundi ya miguu yao na shingo zao kwa upole na mapenzi juu yao. -
وَلَقَدْ فَتَنَّا سُلَيْمَـٰنَ وَأَلْقَيْنَا عَلَىٰ كُرْسِيِّهِۦ جَسَدًا ثُمَّ أَنَابَ٣٤
Walaqad fatanna sulaymana waalqayna ʿala kursiyyihi jasadan thumma anaba
Na tulimtia mtihanini Suleiman, na tukauweka mwili juu ya kiti chake, kisha akarejea kwa kutubu.34
Maelezo
[34] Na hakika Sisi tulimfanyia mtihani Suleiman ili asighurike na heba ya ufalme. Tukaweka juu ya kiti chake kiwiliwili kisicho weza kuendesha mambo. Akautambua mtihani, akarejea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na akatubu. -
قَالَ رَبِّ ٱغْفِرْ لِى وَهَبْ لِى مُلْكًا لَّا يَنۢبَغِى لِأَحَدٍ مِّنۢ بَعْدِىٓ ۖ إِنَّكَ أَنتَ ٱلْوَهَّابُ٣٥
Qala rabbi ighfir lee wahab lee mulkan la yanbaghee liahadin min baʿdee innaka anta alwahhabu
Akasema: Mola wangu Mlezi! Nisamehe na unipe ufalme usio mwelekea yeyote baada yangu. Hakika Wewe ndiye Mpaji.35
Maelezo
[35] Suleiman alimwomba Mola wake Mlezi kwa kurejea kwake: Mola wangu Mlezi! Nighufirie yaliyo toka kwangu kwa ghafla, na unitunukie ufalme usio elekea yeyote kuupata baada yangu. Hakika Wewe ndiye Mwingi wa kutunukia, na ndiye Mwingi wa kutoa. -
فَسَخَّرْنَا لَهُ ٱلرِّيحَ تَجْرِى بِأَمْرِهِۦ رُخَآءً حَيْثُ أَصَابَ٣٦
Fasakhkharna lahu alrreeha tajree biamrihi rukhaan haythu asaba
Basi tukaufanya upepo umtumikie, ukenda kwa amri yake, popote alipo taka kufika.36
Maelezo
[36] Tukamdhalilishia upepo, ukenda kama anavyo taka maridhawa, kokote aliko kusudia na kutaka. -
وَٱلشَّيَـٰطِينَ كُلَّ بَنَّآءٍ وَغَوَّاصٍ٣٧
Waalshshayateena kulla bannain waghawwasin
Na tukayafanya mashet'ani yamtumikie, wote wajenzi na wapiga mbizi.37
Maelezo
[37] Na tukamdhalilishia kila mjenzi na mpiga mbizi katika bahari kuu miongoni mwa mashetani maasi. -
وَءَاخَرِينَ مُقَرَّنِينَ فِى ٱلْأَصْفَادِ٣٨
Waakhareena muqarraneena fee alasfadi
Na wengine wafungwao kwa minyororo.38
Maelezo
[38] Na wengine katika hao mashetani wamefungwa wao kwa wao kwa minyororo, kuwazuia na wenginewe wasifanye ufisadi wao. -
هَـٰذَا عَطَآؤُنَا فَٱمْنُنْ أَوْ أَمْسِكْ بِغَيْرِ حِسَابٍ٣٩
Hatha ʿataona faomnun aw amsik bighayri hisabin
Hichi ndicho kipawa chetu. Basi toa au zuia, bila ya hisabu.39
Maelezo
[39] Na akamfunulia kwa wahyi : Haya tuliyo kuneemesha kwayo ni kipawa kilicho toka kwetu. Yaani ni Sisi tulio kupa. Basi mpe umtakaye, na mnyime umtakaye. Hapana hisabu juu yako kwa kutoa au kunyima. -
وَإِنَّ لَهُۥ عِندَنَا لَزُلْفَىٰ وَحُسْنَ مَـَٔابٍ٤٠
Wainna lahu ʿindana lazulfa wahusna maabin
Na hakika yeye kwetu Sisi ana cheo cha kukaribishwa kwetu, na pahala pazuri pa kurejea.40
Maelezo
[40] Hakika Suleiman kwetu Sisi ana ukaribisho mkubwa, na marejeo mazuri. -
وَٱذْكُرْ عَبْدَنَآ أَيُّوبَ إِذْ نَادَىٰ رَبَّهُۥٓ أَنِّى مَسَّنِىَ ٱلشَّيْطَـٰنُ بِنُصْبٍ وَعَذَابٍ٤١
Waothkur ʿabdana ayyooba ith nada rabbahu annee massaniya alshshaytanu binusbin waʿathabin
Na mkumbuke mja wetu Ayubu alipo mwita Mola wake Mlezi akasema: Kwa hakika Shet'ani amenifikishia udhia na adhabu.41
Maelezo
[41] Ewe Muhammad! Mkumbuke mja wetu Ayubu alipo mwomba Mola wake Mlezi kwa kusema: Hakika Shetani amenipatisha taabu na machungu. -
ٱرْكُضْ بِرِجْلِكَ ۖ هَـٰذَا مُغْتَسَلٌۢ بَارِدٌ وَشَرَابٌ٤٢
Orkud birijlika hatha mughtasalun baridun washarabun
(Akaambiwa:) Piga-piga ardhi kwa mguu wako! Basi haya maji baridi ya kuogea na ya kunywa.42
Maelezo
[42] Tukamuitikia na tukamwambia: Ipige ardhi kwa mguu wako, yatatimbuka maji baridi, utakoga na utakunywa hayo, na kwa hivyo yatakuondokea machofu na adhabu. -
وَوَهَبْنَا لَهُۥٓ أَهْلَهُۥ وَمِثْلَهُم مَّعَهُمْ رَحْمَةً مِّنَّا وَذِكْرَىٰ لِأُو۟لِى ٱلْأَلْبَـٰبِ٤٣
Wawahabna lahu ahlahu wamithlahum maʿahum rahmatan minna wathikra liolee alalbabi
Na tukampa ahali zake na wengine kama wao pamoja nao, kuwa ni rehema itokayo kwetu, na iwe kumbusho kwa watu wenye akili.43
Maelezo
[43] Tukamkusanyia watu wake walio kuwa wametapanyika mbali naye siku zile za mateso yake. Na tukamzidishia wenginewe kama wale. Na tulifanya hayo kuwa ni rehema kutokana nasi, na ili yawe ni mawaidha kwa wenye akili, wapate kujua kuwa matokeo ya subira ni faraji. -
وَخُذْ بِيَدِكَ ضِغْثًا فَٱضْرِب بِّهِۦ وَلَا تَحْنَثْ ۗ إِنَّا وَجَدْنَـٰهُ صَابِرًا ۚ نِّعْمَ ٱلْعَبْدُ ۖ إِنَّهُۥٓ أَوَّابٌ٤٤
Wakhuth biyadika dighthan faidrib bihi wala tahnath inna wajadnahu sabiran niʿma alʿabdu innahu awwabun
Na shika kicha cha vijiti tu mkononi mwako, kisha ndio upigie nacho, wala usivunje kiapo. Hakika tulimkuta mwenye subira, mbora wa waja, kwa hakika alikuwa mwingi wa kutubu.44
Maelezo
[44] Ayubu alikuwa kaapa kuwa atampiga mmoja wapo katika ahali zake fimbo kadhaa wa kadhaa. Mwenyezi Mungu alimhalalishia aondoe kiapo chake kwa kuchukua kifungu cha fimbo idadi ile ile alio apia kuwa atampigia. Basi kwa kile kifungu cha fimbo ampige aliye apa kuwa atampiga, na hapo yamini yake itakuwa imetimia kwa uchache wa machungu. Mwenyezi Mungu ndiye aliye mneemesha kwa neema hizi, kwa sababu Mwenyezi Mungu alimwona kuwa ni mtu aliye vumilia masaibu yake. Kwa hivyo amestahiki sifa. Mbora wa kusifiwa kwa ibada ni yeye, kwa sababu yeye ni mwingi mno wa kurejea kwa Mwenyezi Mungu katika kila jambo. -
وَٱذْكُرْ عِبَـٰدَنَآ إِبْرَٰهِيمَ وَإِسْحَـٰقَ وَيَعْقُوبَ أُو۟لِى ٱلْأَيْدِى وَٱلْأَبْصَـٰرِ٤٥
Waothkur ʿibadana ibraheema waishaqa wayaʿqooba olee alaydee waalabsari
Na wakumbuke waja wetu, Ibrahim na Is-haqa na Yaa'qubu walio kuwa na nguvu na busara.45
Maelezo
[45] Na mkumbuke mja wetu Ibrahim, na Is-haqa, na Yaa'qubu, wenye nguvu katika Dini na dunia, na wenye busara ya mwangaza. -
إِنَّآ أَخْلَصْنَـٰهُم بِخَالِصَةٍ ذِكْرَى ٱلدَّارِ٤٦
Inna akhlasnahum bikhalisatin thikra alddari
Sisi tumewakhusisha wao kwa sifa ya ukumbusho wa Akhera.46
Maelezo
[46] Hakika Sisi tumewakhusisha wao kwa sifa, nayo ni kuwa wanaikumbuka Nyumba ya Akhera, wao wanaikumbuka nao wanakumbukwa kwayo. -
وَإِنَّهُمْ عِندَنَا لَمِنَ ٱلْمُصْطَفَيْنَ ٱلْأَخْيَارِ٤٧
Wainnahum ʿindana lamina almustafayna alakhyari
Na hakika wao kwetu sisi ni wateuliwa walio bora.47
Maelezo
[47] Na hakika wao kwetu Sisi ni wenye kukhitariwa walio bora. -
وَٱذْكُرْ إِسْمَـٰعِيلَ وَٱلْيَسَعَ وَذَا ٱلْكِفْلِ ۖ وَكُلٌّ مِّنَ ٱلْأَخْيَارِ٤٨
Waothkur ismaʿeela wailyasaʿa watha alkifli wakullun mina alakhyari
Na mkumbuke Ismail na Alyasaa na Dhulkifli, na wote hao ni katika walio bora.48
Maelezo
[48] Na mkumbuke Ismail, na Alyasaa, na Dhalkifli - na wote hao ni miongoni mwa walio bora. -
هَـٰذَا ذِكْرٌ ۚ وَإِنَّ لِلْمُتَّقِينَ لَحُسْنَ مَـَٔابٍ٤٩
Hatha thikrun wainna lilmuttaqeena lahusna maabin
Huu ni ukumbusho. Na hakika wachamngu wana marudio mazuri.49
Maelezo
[49] Haya tuliyo kusimulia ni khabari za baadhi ya Mitume ili kukukumbusha wewe na kuwakumbusha watu wako. Na hakika wachamngu walio jikinga na kumuasi Mwenyezi Mungu Mtukufu watapata marejeo mazuri na natija njema. -
جَنَّـٰتِ عَدْنٍ مُّفَتَّحَةً لَّهُمُ ٱلْأَبْوَٰبُ٥٠
Jannati ʿadnin mufattahatan lahumu alabwabu
Bustani za milele zitazo funguliwa milango yao kwa ajili yao.50
Maelezo
[50] Wameandaliwa bustani za milele zilizo funguliwa milango yao hapana wa kuwazuia wasiingie humo. -
مُتَّكِـِٔينَ فِيهَا يَدْعُونَ فِيهَا بِفَـٰكِهَةٍ كَثِيرَةٍ وَشَرَابٍ٥١
Muttakieena feeha yadʿoona feeha bifakihatin katheeratin washarabin
Humo wataegemea matakia, wawe wanaagiza humo matunda mengi na vinywaji.51
Maelezo
[51] Watakuwa wamekaa humo wakiegemea juu ya makochi na vitanda kama wafanyavyo wenye taanusi, wakistarehe kwa kutaka matunda ya kila namna na vinywaji. -
۞ وَعِندَهُمْ قَـٰصِرَٰتُ ٱلطَّرْفِ أَتْرَابٌ٥٢
Waʿindahum qasiratu alttarfi atrabun
Na pamoja nao wake zao wenye kutuliza macho, hirimu zao.52
Maelezo
[52] Na huko Peponi watakuwa na wake ambao macho yao hayawatazami ila waume zao tu, hawawaangalii wengineo, nao ni wa miaka sawa na waume zao. Kwa hivyo wameelekeana kuwafikiana. -
هَـٰذَا مَا تُوعَدُونَ لِيَوْمِ ٱلْحِسَابِ٥٣
Hatha ma tooʿadoona liyawmi alhisabi
aya ndiyo mliyo ahidiwa kwa Siku ya Hisabu.53
Maelezo
[53] Raha hii ndiyo mliyo ahidiwa kuipata Siku ya Kiyama. -
إِنَّ هَـٰذَا لَرِزْقُنَا مَا لَهُۥ مِن نَّفَادٍ٥٤
Inna hatha larizquna ma lahu min nafadin
Hakika hii ndiyo riziki yetu isiyo malizika.54
Maelezo
[54] Hakika haya bila ya shaka ni tunayo yatoa Sisi, na wala hayana ukomo. -
هَـٰذَا ۚ وَإِنَّ لِلطَّـٰغِينَ لَشَرَّ مَـَٔابٍ٥٥
Hatha wainna lilttagheena lasharra maabin
Ndio hivi! Na hakika wenye kuasi bila ya shaka watapata marudio maovu kabisa;55
Maelezo
[55] Neema hizi ni malipo ya wachamngu. Na hakika majabari wenye kuwaasi Manabii wao bila ya shaka watakuwa na marejeo na mwisho muovu. -
جَهَنَّمَ يَصْلَوْنَهَا فَبِئْسَ ٱلْمِهَادُ٥٦
Jahannama yaslawnaha fabisa almihadu
Nayo ni Jahannamu! Wataingia humo. Nacho hicho ni kitanda kiovu mno cha kulalia.56
Maelezo
[56] Na mwisho huo ni Jahannamu watakayo iingia, na moto wake uwatese. Na malalio maovu mno hayo! -
هَـٰذَا فَلْيَذُوقُوهُ حَمِيمٌ وَغَسَّاقٌ٥٧
Hatha falyathooqoohu hameemun waghassaqun
Ndio hivi! Basi na wayaonje maji ya moto na ya usaha!57
Maelezo
[57] Haya maji ya moto, mwisho wa umoto, na usaha wa watu wa Jahannamu wataamrishwa wayaonje. -
وَءَاخَرُ مِن شَكْلِهِۦٓ أَزْوَٰجٌ٥٨
Waakharu min shaklihi azwajun
Na adhabu nyenginezo za namna hii.58
Maelezo
[58] Na adhabu nyengine mfano wa hizi, za namna kwa namna zilizo changanyika. -
هَـٰذَا فَوْجٌ مُّقْتَحِمٌ مَّعَكُمْ ۖ لَا مَرْحَبًۢا بِهِمْ ۚ إِنَّهُمْ صَالُوا۟ ٱلنَّارِ٥٩
Hatha fawjun muqtahimun maʿakum la marhaban bihim innahum saloo alnnari
Hili ndilo kundi litakalo ingia pamoja nanyi. Hapana makaribisho mema kwao. Hakika hao wanaingia Motoni.59
Maelezo
[59] Na majabari, wale marais wa washirikina, wataambiwa: Hawa chungu ya watu wanao ingia Motoni pamoja nanyi kwa kusukumana na kwa shida, ni wafwasi wenu. Wale marais watasema: Hawana mapokezi mema hao! Hakika hao wanaingia Motoni wapate kuteseka kwa mvukuto wake. -
قَالُوا۟ بَلْ أَنتُمْ لَا مَرْحَبًۢا بِكُمْ ۖ أَنتُمْ قَدَّمْتُمُوهُ لَنَا ۖ فَبِئْسَ ٱلْقَرَارُ٦٠
Qaloo bal antum la marhaban bikum antum qaddamtumoohu lana fabisa alqararu
Waseme: Lakini nyinyi! Hamna mapokezi mazuri! Nyinyi ndio mlio tusabibisha haya, napo ni pahala paovu kabisa!60
Maelezo
[60] Na wafwasi hao watasema: Bali nyinyi ndio mnastahiki zaidi hayo maapizo mnayo tuapizia sisi, kwani nyinyi ndio mlio tuletea adhabu hii kwa vile mlivyo tudanganya na mkatuitia ukafirini, nasi tukakufuru kwa sababu yenu. Basi nyumba ovu kabisa ya kukaa ni Jahannamu! -
قَالُوا۟ رَبَّنَا مَن قَدَّمَ لَنَا هَـٰذَا فَزِدْهُ عَذَابًا ضِعْفًا فِى ٱلنَّارِ٦١
Qaloo rabbana man qaddama lana hatha fazidhu ʿathaban diʿfan fee alnnari
Waseme: Mola wetu Mlezi! Aliye tusabibisha haya mzidishie adhabu mara mbili Motoni.61
Maelezo
[61] Wafwasi watasema: Ewe Mola wetu Mlezi! Aliye kuwa ni sababu ya adhabu hii, mzidishie adhabu mara mbili katika Moto. -
وَقَالُوا۟ مَا لَنَا لَا نَرَىٰ رِجَالًا كُنَّا نَعُدُّهُم مِّنَ ٱلْأَشْرَارِ٦٢
Waqaloo ma lana la nara rijalan kunna naʿudduhum mina alashrari
Watasema: Tuna nini hata hatuwaoni wale watu ambao tukiwahisabu ndio katika waovu?62
Maelezo
[62] Na watu wa Motoni watasema: Mbona hatuwaoni wale watu ambao tulikuwa duniani tukiwahisabu kuwa ndio katika waovu, na wa duni, wasio kuwa na jema lolote? Na watu hao ni wale mafakiri wa Kiislamu. -
أَتَّخَذْنَـٰهُمْ سِخْرِيًّا أَمْ زَاغَتْ عَنْهُمُ ٱلْأَبْصَـٰرُ٦٣
Attakhathnahum sikhriyyan am zaghat ʿanhumu alabsaru
Tulikosea tulipo wafanyia maskhara, au macho yetu tu hayawaoni ?63
Maelezo
[63] Imekuwaje kuwa sisi tukiwakejeli na wala hawakuingia Motoni pamoja nasi? Au wamekwisha ingia na macho yetu yakazibwa tusiwaone tu? -
إِنَّ ذَٰلِكَ لَحَقٌّ تَخَاصُمُ أَهْلِ ٱلنَّارِ٦٤
Inna thalika lahaqqun takhasumu ahli alnnari
Hakika hayo bila ya shaka ndiyo makhasimiano ya watu wa Motoni.64
Maelezo
[64] Hakika hayo tuliyo yataja ya hadithi ya watu wa Motoni ni kweli ambayo haina budi kutokea, nayo ni ya kugombana kwa watu wa Motoni wao kwa wao. -
قُلْ إِنَّمَآ أَنَا۠ مُنذِرٌ ۖ وَمَا مِنْ إِلَـٰهٍ إِلَّا ٱللَّهُ ٱلْوَٰحِدُ ٱلْقَهَّارُ٦٥
Qul innama ana munthirun wama min ilahin illa Allahu alwahidu alqahharu
Sema: Hakika mimi ni mwonyaji tu; na hapana mungu ila Mwenyezi Mungu Mmoja, Mtenda nguvu,65
Maelezo
[65] Ewe Muhammad! Waambie washirikina: Hakika mimi ni mwenye kukuonyeni na adhabu ya Mwenyezi Mungu, na hapana wa kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu Mmoja ambaye hana mshirika wake, Mtenda nguvu, Mwenye kumshinda kila mwenye madaraka. -
رَبُّ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا ٱلْعَزِيزُ ٱلْغَفَّـٰرُ٦٦
Rabbu alssamawati waalardi wama baynahuma alʿazeezu alghaffaru
Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na viliomo baina yake, Mwenye nguvu, Mwenye kusamehe.66
Maelezo
[66] Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na viliomo baina yao, Mwenye nguvu asiye shindika, Mwenye kusamehe, akazifuta dhambi za mwenye kumuamini. -
قُلْ هُوَ نَبَؤٌا۟ عَظِيمٌ٦٧
Qul huwa nabaon ʿatheemun
Sema: Hii ni khabari kubwa kabisa.67
Maelezo
[67] Ewe Muhammad! Waambie: Haya ninayo kuambieni ni khabari kubwa, ambazo nyinyi mnazipuuza. Msizikanye! -
أَنتُمْ عَنْهُ مُعْرِضُونَ٦٨
Antum ʿanhu muʿridoona
Ambayo nyinyi mnaipuuza.68
Maelezo
[68] Ewe Muhammad! Waambie: Haya ninayo kuambieni ni khabari kubwa, ambazo nyinyi mnazipuuza. Msizikanye! -
مَا كَانَ لِىَ مِنْ عِلْمٍۭ بِٱلْمَلَإِ ٱلْأَعْلَىٰٓ إِذْ يَخْتَصِمُونَ٦٩
Ma kana liya min ʿilmin bialmalai alaʿla ith yakhtasimoona
Sikuwa na ilimu ya mambo ya viumbe wakuu watukufu walipo kuwa wakishindana.69
Maelezo
[69] Mimi sikuwa nikijua khabari za watukufu walio juu walipo kuwa wakizozana juu ya shauri ya Adam, kwa sababu mimi sikupitia njia za kupata ilimu zilizo zowewa na watu za kusoma vitabu au kupokea masomo kwa wataalamu. Njia yangu mimi ya kujua ni kwa kufunuliwa kwa Wahyi. -
إِن يُوحَىٰٓ إِلَىَّ إِلَّآ أَنَّمَآ أَنَا۠ نَذِيرٌ مُّبِينٌ٧٠
In yooha ilayya illa annama ana natheerun mubeenun
Haikufunuliwa kwangu isipo kuwa ya kwamba hakika mimi ni mwonyaji dhaahiri.70
Maelezo
[70] Na mimi sikufunuliwa kwa Wahyi ila kwamba hakika mimi ni Mtume wa kukufikishieni Ujumbe wa Mola wangu Mlezi kwa njia iliyo wazi kabisa. -
إِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَـٰٓئِكَةِ إِنِّى خَـٰلِقٌۢ بَشَرًا مِّن طِينٍ٧١
Ith qala rabbuka lilmalaikati innee khaliqun basharan min teenin
Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Hakika Mimi nitaumba mtu kutokana na udongo.71
Maelezo
[71] Watajie pale alipo sema Mola wako Mlezi kuwaambia Malaika: Mimi nataka umba mtu, naye ni Adam a.s., kutokana na udongo. -
فَإِذَا سَوَّيْتُهُۥ وَنَفَخْتُ فِيهِ مِن رُّوحِى فَقَعُوا۟ لَهُۥ سَـٰجِدِينَ٧٢
Faitha sawwaytuhu wanafakhtu feehi min roohee faqaʿoo lahu sajideena
Na nitakapo mkamilisha na kumpulizia roho inayo tokana nami, basi muangukieni kwa kumt'ii.72
Maelezo
[72] Nikisha timiza kumuumba na nikampulizia siri ya uhai, nayo ni roho, muangukieni kwa kusujudu sijida ya kumtukuza na kumuamkia. -
فَسَجَدَ ٱلْمَلَـٰٓئِكَةُ كُلُّهُمْ أَجْمَعُونَ٧٣
Fasajada almalaikatu kulluhum ajmaʿoona
Basi Malaika wakat'ii wote pamoja.73
Maelezo
[73] Malaika wote wakafanya kama walivyo amrishwa, wakamuangukia wakisujudu, isipo kuwa Iblisi. Yeye hakusujudu, na akajiona bora na akapanda kiburi, na akawa miongoni mwa makafiri. -
إِلَّآ إِبْلِيسَ ٱسْتَكْبَرَ وَكَانَ مِنَ ٱلْكَـٰفِرِينَ٧٤
Illa ibleesa istakbara wakana mina alkafireena
Isipo kuwa Iblisi; alijivuna na akawa katika makafiri.74
Maelezo
[74] Malaika wote wakafanya kama walivyo amrishwa, wakamuangukia wakisujudu, isipo kuwa Iblisi. Yeye hakusujudu, na akajiona bora na akapanda kiburi, na akawa miongoni mwa makafiri. -
قَالَ يَـٰٓإِبْلِيسُ مَا مَنَعَكَ أَن تَسْجُدَ لِمَا خَلَقْتُ بِيَدَىَّ ۖ أَسْتَكْبَرْتَ أَمْ كُنتَ مِنَ ٱلْعَالِينَ٧٥
Qala ya ibleesu ma manaʿaka an tasjuda lima khalaqtu biyadayya astakbarta am kunta mina alʿaleena
Mwenyezi Mungu akamwambia: Ewe Iblisi! Kipi kilicho kuzuia kumt'ii yule niliye muumba kwa mikono yangu? Je! Umejiona mkubwa, au umekuwa katika wakuu kweli?75
Maelezo
[75] Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: Ewe Iblisi! Nini kilicho kuzuilia kumsujudia niliye muumba Mimi mwenyewe bila ya kuingiliwa na yeyote kati yake! Umejiona mkubwa hali nawe si mkubwa, au hakika wewe nafsi yako ni katika walio shinda ukubwa? -
قَالَ أَنَا۠ خَيْرٌ مِّنْهُ ۖ خَلَقْتَنِى مِن نَّارٍ وَخَلَقْتَهُۥ مِن طِينٍ٧٦
Qala ana khayrun minhu khalaqtanee min narin wakhalaqtahu min teenin
Akasema: Mimi ni bora kuliko yeye. Umeniumba kwa moto, na yeye umemuumba kwa udongo.76
Maelezo
[76] Iblisi akasema: Mimi ni bora kuliko Adam; kwani Wewe umeniumba kwa moto, na yeye umemuumba kwa udongo. Basi vipi mimi nimsujudie yeye? -
قَالَ فَٱخْرُجْ مِنْهَا فَإِنَّكَ رَجِيمٌ٧٧
Qala faokhruj minha fainnaka rajeemun
Akasema: Basi toka humo, kwani hakika wewe umelaanika.77
Maelezo
[77] Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa kumlipa Iblisi kwa kiburi chake cha kukataa amri ya Mola wake Mlezi, alimwambia: Basi toka kwenye kundi la watukufu walio juu, kwani wewe umekwisha fukuzwa kutokana na rehema yangu! -
وَإِنَّ عَلَيْكَ لَعْنَتِىٓ إِلَىٰ يَوْمِ ٱلدِّينِ٧٨
Wainna ʿalayka laʿnatee ila yawmi alddeeni
Na hakika laana yangu itakuwa juu yako mpaka Siku ya Malipo.78
Maelezo
[78] Na hakika wewe umetengwa mbali na kila kheri mpaka Siku ya Malipo. Hapo utalipwa kwa sababu ya kunikufuru Mimi na kunifanyia kiburi. -
قَالَ رَبِّ فَأَنظِرْنِىٓ إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ٧٩
Qala rabbi faanthirnee ila yawmi yubʿathoona
Akasema: Mola wangu Mlezi! Nipe muhula mpaka siku watayo fufuliwa viumbe.79
Maelezo
[79] Iblisi akasema: Mola Mlezi! Nipe muhula, wala usinifishe mpaka Siku ya kufufuliwa viumbe. -
قَالَ فَإِنَّكَ مِنَ ٱلْمُنظَرِينَ٨٠
Qala fainnaka mina almunthareena
Mwenyezi Mungu akasema: Basi umekwisha kuwa miongoni mwa walio pewa muhula,80
Maelezo
[80] Akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Basi wewe utaakhirishwa, utapewa muhula, mpaka siku ya wakati tunao ujua Sisi, nao ni kumalizika dunia. -
إِلَىٰ يَوْمِ ٱلْوَقْتِ ٱلْمَعْلُومِ٨١
Ila yawmi alwaqti almaʿloomi
Mpaka siku ya wakati maalumu.81
Maelezo
[81] Akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Basi wewe utaakhirishwa, utapewa muhula, mpaka siku ya wakati tunao ujua Sisi, nao ni kumalizika dunia. -
قَالَ فَبِعِزَّتِكَ لَأُغْوِيَنَّهُمْ أَجْمَعِينَ٨٢
Qala fabiʿizzatika laoghwiyannahum ajmaʿeena
Akasema (Iblisi): Naapa kwa utukufu wako, bila ya shaka nitawapoteza wote,82
Maelezo
[82] Iblisi akasema: Basi naapa kwa Ukubwa wako na Utukufu wako, kwa yakini nitawapoteza watu wote, isipo kuwa waja wako ulio wateuwa kwa ajili ya kukut'ii Wewe. Hao sina madaraka nao. -
إِلَّا عِبَادَكَ مِنْهُمُ ٱلْمُخْلَصِينَ٨٣
Illa ʿibadaka minhumu almukhlaseena
Isipo kuwa wale waja wako miongoni mwao walio khitariwa.83
Maelezo
[83] Isipo kuwa waja wako ulio wateuwa kwa ajili ya kukut'ii Wewe. Hao sina madaraka nao. -
قَالَ فَٱلْحَقُّ وَٱلْحَقَّ أَقُولُ٨٤
Qala faalhaqqu waalhaqqa aqoolu
kasema: Haki! Na haki ninaisema.84
Maelezo
[84] Akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Haki ndiyo yamini yangu na kiapo changu; na wala sisemi ila Haki. Bila ya shaka nitaijaza Jahannamu kwa jinsi yako ya kishetani na watakao kufuata katika vizazi vya Adam wote. Hapana khitilafu kwangu baina ya wafuasi na wanao fuatwa. -
لَأَمْلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنكَ وَمِمَّن تَبِعَكَ مِنْهُمْ أَجْمَعِينَ٨٥
Laamlaanna jahannama minka wamimman tabiʿaka minhum ajmaʿeena
Bila ya shaka nitaijaza Jahannamu kwa wewe na kwa hao wote wenye kukufuata miongoni mwao.85
Maelezo
[85] Akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Haki ndiyo yamini yangu na kiapo changu; na wala sisemi ila Haki. Bila ya shaka nitaijaza Jahannamu kwa jinsi yako ya kishetani na watakao kufuata katika vizazi vya Adam wote. Hapana khitilafu kwangu baina ya wafuasi na wanao fuatwa. -
قُلْ مَآ أَسْـَٔلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ وَمَآ أَنَا۠ مِنَ ٱلْمُتَكَلِّفِينَ٨٦
Qul ma asalukum ʿalayhi min ajrin wama ana mina almutakallifeena
Sema (Ewe Mtume) : Sikuombeni ujira juu ya haya, wala mimi si katika wadanganyifu.86
Maelezo
[86] Ewe Muhammad! Waambie umma wako: Mimi sikuombeni ujira kwa ajili ya haya niliyo amrishwa nikufikishieni yaliyomo katika Qur'ani na Wahyi. Wala mimi si katika hao wanao jipamba na yasiyo kuwa yao, hata nijidai Unabii. -
إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ لِّلْعَـٰلَمِينَ٨٧
In huwa illa thikrun lilʿalameena
Hayakuwa haya ila ni mawaidha kwa walimwengu wote.87
Maelezo
[87] Haikuwa Qur'ani ila ni ukumbusho na mawaidha kwa walimwengu wote. -
وَلَتَعْلَمُنَّ نَبَأَهُۥ بَعْدَ حِينٍۭ٨٨
Walataʿlamunna nabaahu baʿda heenin
Na bila ya shaka mtajua khabari zake baada ya muda.88
Maelezo
[88] Na hapana shaka nyinyi, mnao ikadhibisha Qur'ani, mtakuja jua karibuni hivi ukweli uliomo ndani yake wa ahadi, na maonyo, na khabari za mambo yatakayo kuja, na Ishara za ulimwengu.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Surat Sad iko katika juzuu ya ngapi?
Surat Sad iko katika juzuu ya 23.
Surat Sad ina aya ngapi?
Surat Sad ina aya 88.
Surat Sad ni ya Makka au ya Madina?
Surat Sad ni sura ya Makka.
Surat Sad ni sura ya ngapi katika Qur’ani?
Ni sura ya 38 katika Qur’ani.
Vyanzo
- Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
- Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
- Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
- Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
- Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
- Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.
Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.