سورة لقمان

Surat Luqman kwa Kiswahili

Msahafu

Mishary Rashid AlafasyPakua MP3Pakua PDF

Surat Luqman (لقمان) ni sura ya 31 katika Qur’ani na ina aya 34. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na iko katika juzuu ya 21.

Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat Luqman yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.

Surat Luqman kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

  1. الٓمٓ۝١

    Aliflammeem

    Alif Lam Mim (A.L.M.) .1

    Maelezo
    [1] Harufi hizi zimeanzia baadhi ya Sura kuashiria kuwa Qur'ani ni muujiza ulio tungwa na harufi kama harufi wanazo zitumia Waarabu katika maneno yao. Na juu ya hayo wao wameshindwa kuleta mfano wake. Na pia ni kwa ajili ya kuzindua watu wasikilize na watege sikio. Na washirikina walikuwa wamewafikiana kuwa wawe wanaropokwa maneno ya upuuzi tu ikisomwa Qur'ani wala wasiisikilize.
  2. تِلْكَ ءَايَـٰتُ ٱلْكِتَـٰبِ ٱلْحَكِيمِ۝٢

    Tilka ayatu alkitabi alhakeemi

    Hizi ni Aya za Kitabu chenye hikima.2

    Maelezo
    [2] Hizi Aya tukufu ni Aya za Qur'ani iliyo kusanya hikima na ukweli.
  3. هُدًى وَرَحْمَةً لِّلْمُحْسِنِينَ۝٣

    Hudan warahmatan lilmuhsineena

    Kuwa ni Uwongofu na Rehema kwa wafanyao wema!3

    Maelezo
    [3] Hizi Aya ni Uwongofu ulio kamilika, na Rehema iliyo kusanya kwa wenye kutenda mema.
  4. ٱلَّذِينَ يُقِيمُونَ ٱلصَّلَوٰةَ وَيُؤْتُونَ ٱلزَّكَوٰةَ وَهُم بِٱلْـَٔاخِرَةِ هُمْ يُوقِنُونَ۝٤

    Allatheena yuqeemoona alssalata wayutoona alzzakata wahum bialakhirati hum yooqinoona

    Wanao shika Swala, na wanatoa Zaka, nao wana yakini na Akhera.4

    Maelezo
    [4] Hao ndio wanao timiza Swala kwa njia ya ukamilifu kabisa, na wanawapa Zaka wanao istahiki; na wao wanayaamini maisha ya Akhera kwa imani yenye nguvu kabisa.
  5. أُو۟لَـٰٓئِكَ عَلَىٰ هُدًى مِّن رَّبِّهِمْ ۖ وَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْمُفْلِحُونَ۝٥

    Olaika ʿala hudan min rabbihim waolaika humu almuflihoona

    Hao ndio walio na uwongofu utokao kwa Mola wao Mlezi, na hao ndio wenye kufanikiwa.5

    Maelezo
    [5] Hao Waumini wanao tenda vyema vitendo vyao, wametua kwenye Uwongofu ulio wajia kutokana na Mola wao Mlezi. Na hao tu - si wengineo - ndio wenye kufuzu kikweli.
  6. وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يَشْتَرِى لَهْوَ ٱلْحَدِيثِ لِيُضِلَّ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ بِغَيْرِ عِلْمٍ وَيَتَّخِذَهَا هُزُوًا ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ مُّهِينٌ۝٦

    Wamina alnnasi man yashtaree lahwa alhadeethi liyudilla ʿan sabeeli Allahi bighayri ʿilmin wayattakhithaha huzuwan olaika lahum ʿathabun muheenun

    Na miongoni mwa watu wapo wanao nunua maneno ya upuuzi, ili wawapoteze watu na njia ya Mwenyezi Mungu pasipo kujua, na wanaichukulia ni maskhara. Hao watapata adhabu ya kuwafedhehesha.6

    Maelezo
    [6] Na miongoni mwa watu wapo ambao hununua maneno ya uwongo wawasimulie watu wapate kuwatenga na Uislamu na Qur'ani kwa kutojua dhambi zilio juu yao, na wanaifanyia maskhara Dini ya Mwenyezi Mungu na Ufunuo wake. Watendayo hayo watapata adhabu ya kuwatia unyonge na kuwadhalilisha.
  7. وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِ ءَايَـٰتُنَا وَلَّىٰ مُسْتَكْبِرًا كَأَن لَّمْ يَسْمَعْهَا كَأَنَّ فِىٓ أُذُنَيْهِ وَقْرًا ۖ فَبَشِّرْهُ بِعَذَابٍ أَلِيمٍ۝٧

    Waitha tutla ʿalayhi ayatuna walla mustakbiran kaan lam yasmaʿha kaanna fee othunayhi waqran fabashshirhu biʿathabin aleemin

    Na (mtu kama huyo) anapo somewa Aya zetu huzipa mgongo kwa kujivuna, kama kwamba hakuzisikia, kama kwamba masikioni mwake mna uziwi. Basi mbashirie kuwa atapata adhabu chungu.7

    Maelezo
    [7] Na mpotovu kama huyu akisomewa Aya za Mwenyezi Mungu huzipuuza kwa kiburi. Hali yake kwa haya ni hali ya ambaye hasikii, kama kwamba ana uziwi katika masikio yake. Basi mwonye kuwa hakika Mwenyezi Mungu amemuandalia adhabu yenye machungu makali.
  8. إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ لَهُمْ جَنَّـٰتُ ٱلنَّعِيمِ۝٨

    Inna allatheena amanoo waʿamiloo alssalihati lahum jannatu alnnaʿeemi

    Hakika walio amini na wakatenda mema watakuwa nazo Bustani za neema.8

    Maelezo
    [8] Hakika walio amini na wakatenda vitendo vyema watapata Bustani zenye neema.
  9. خَـٰلِدِينَ فِيهَا ۖ وَعْدَ ٱللَّهِ حَقًّا ۚ وَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلْحَكِيمُ۝٩

    Khalideena feeha waʿda Allahi haqqan wahuwa alʿazeezu alhakeemu

    Watadumu humo - ni ahadi ya Mwenyezi Mungu ya kweli. Na Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima.9

    Maelezo
    [9] Watabaki humo daima dawamu; Mwenyezi Mungu amewaahidi ahadi isiyo vunjika. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mshindi wa kila kitu, Mwenye hikima katika maneno yake na vitendo vyake.
  10. خَلَقَ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ بِغَيْرِ عَمَدٍ تَرَوْنَهَا ۖ وَأَلْقَىٰ فِى ٱلْأَرْضِ رَوَٰسِىَ أَن تَمِيدَ بِكُمْ وَبَثَّ فِيهَا مِن كُلِّ دَآبَّةٍ ۚ وَأَنزَلْنَا مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءً فَأَنۢبَتْنَا فِيهَا مِن كُلِّ زَوْجٍ كَرِيمٍ۝١٠

    Khalaqa alssamawati bighayri ʿamadin tarawnaha waalqa fee alardi rawasiya an tameeda bikum wabaththa feeha min kulli dabbatin waanzalna mina alssamai maan faanbatna feeha min kulli zawjin kareemin

    Ameziumba mbingu bila ya nguzo mnazo ziona; na ameweka katika ardhi milima ili ardhi isikuyumbisheni; na ametawanya humo kila namna ya wanyama; na tumeteremsha maji kutoka mbinguni, na tukaotesha katika ardhi mimea mizuri ya kila namna.10

    Maelezo
    [10] Mwenyezi Mungu ameziumba mbingu zisio na nguzo za nyinyi kuziona. Na juu ya ardhi ameweka milima iliyo simama imara, ili ardhi isikutingisheni. Na humo katika ardhi ametawanya kila namna ya wanyama wanao tambaa na kwenda. Na tumeteremsha maji kutoka mbinguni, na tukaotesha mimea ya kila namna nzuri yenye manufaa katika ardhi. Rejea uangalie maelezo ya kisayansi juu ya Aya 2, Sura ya Ar-Raa'd.
  11. هَـٰذَا خَلْقُ ٱللَّهِ فَأَرُونِى مَاذَا خَلَقَ ٱلَّذِينَ مِن دُونِهِۦ ۚ بَلِ ٱلظَّـٰلِمُونَ فِى ضَلَـٰلٍ مُّبِينٍ۝١١

    Hatha khalqu Allahi faaroonee matha khalaqa allatheena min doonihi bali alththalimoona fee dalalin mubeenin

    Huu ni uumbaji wa Mwenyezi Mungu. Basi nionyesheni wameumba nini hao wasio kuwa Yeye! Lakini madhaalimu wamo katika upotovu uliyo dhaahiri.11

    Maelezo
    [11] Hivi viumbe vya Mwenyezi Mungu vipo mbele yenu, basi hebu nionyesheni walicho umba hao mnao wafanya ni miungu badala yake Yeye hata wawe ni washirika wake! Bali madhaalimu - kwa ushirikina wao - wamo katika upotovu ulio wazi.
  12. وَلَقَدْ ءَاتَيْنَا لُقْمَـٰنَ ٱلْحِكْمَةَ أَنِ ٱشْكُرْ لِلَّهِ ۚ وَمَن يَشْكُرْ فَإِنَّمَا يَشْكُرُ لِنَفْسِهِۦ ۖ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَنِىٌّ حَمِيدٌ۝١٢

    Walaqad atayna luqmana alhikmata ani oshkur lillahi waman yashkur fainnama yashkuru linafsihi waman kafara fainna Allaha ghaniyyun hameedun

    Na tulimpa Luqman hikima, tukamwambia: Mshukuru Mwenyezi Mungu. Na mwenye kushukuru basi hakika anashukuru kwa manufaa ya nafsi yake. Na aliye kufuru, basi Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, Msifiwa.12

    Maelezo
    [12] Na hakika tulimpa Luqman hikima, na ilimu, na kauli ya kusibu. Tulimwambia: Mshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema aliyo kupa. Na mwenye kushukuru basi hakika huyo anaitafutia kheri nafsi yake. Na mwenye kuzikufuru neema, akazikataa, na asishukuru kwa ajili yake, basi kwa hakika Mwenyezi Mungu si mwenye kuihitaji shukra yake, na Yeye Mwenyezi Mungu ni Mwenye kustahiki sifa zote njema, na ingawa pasiwepo hata mmoja wa kumsifu.
  13. وَإِذْ قَالَ لُقْمَـٰنُ لِٱبْنِهِۦ وَهُوَ يَعِظُهُۥ يَـٰبُنَىَّ لَا تُشْرِكْ بِٱللَّهِ ۖ إِنَّ ٱلشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ۝١٣

    Waith qala luqmanu liibnihi wahuwa yaʿithuhu ya bunayya la tushrik biAllahi inna alshshirka lathulmun ʿatheemun

    Na Luqman alipo mwambia mwanawe kwa kumpa mawaidha: Ewe mwanangu! Usimshirikishe Mwenyezi Mungu. Kwani hakika ushirikina bila ya shaka ni dhulma iliyo kubwa.13

    Maelezo
    [13] Taja pale Luqman alipo mwambia mwanawe: Ewe mwanangu! Usimshirikishe Mwenyezi Mungu na yeyote. Hakika kumshirikisha Mwenyezi Mungu ni dhulma kubwa, kuwaweka sawa Mwenye kustahiki na asiye stahiki. Waarabu walikuwa wanawajua watu wawili kwa jina hili. Mmoja wapo ni Luqman bin A'adi. Nao walikuwa wakimtukuza cheo kwa werevu wake, uraisi, ujuzi, ufasihi na ujanja. Na walikithiri sana kumtaja na kumpigia mithali, kama inavyo onekana katika vitabu vya Kiarabu vingi. Ama mwengine ni huyo anaye itwa Luqman Alhakim, (Mwenye hikima), aliye kuwa mashuhuri kwa hikima yake na mifano yake, na ambaye Sura hii ya Qur'ani imeitwa kwa jina lake. Na hikima zake zilikuwa zimeenea kwa Waarabu. Ibn Hisham amesimulia kwamba Suwaid bin Ass'amit alifika Makka. Naye alikuwa mtu mtukufu kwa watu wake. Mtume s.a.w. akamtaka asilimu. Suwaid akasema: Huenda labda uliyo nayo wewe ndiyo kama niliyo nayo mimi. Mtume s.a.w. akasema: Nini ulicho nacho? Akasema: Majalla ya Luqman. Mtume s.a.w. akasema: Nisomee. Akamsomea. Tena akasema: Hakika haya maneno mazuri. Na niliyo nayo mimi ni bora zaidi, nayo ni Qur'ani aliyo niteremshia Mwenyezi Mungu, nayo ni Uwongofu na Nuru. Mtume s.a.w. akamsomea Qur'ani na akamtaka asilimu. Na pia Imam Malik ametaja kwa wingi hikima za Luqman katika kitabu chake, Al Muwatt'a. Na baadhi ya vitabu vya Tafsiri ya Qur'ani na Adab (maandishi ya ufasihi wa lugha) vimetaja namna mbali mbali katika hikima hizo. Kisha baadae ikakusanywa mithali kwa visa katika kitabu chenye jina la Mithali za Luqman. Lakini kwa sababu ya udhaifu wa mpango wake, na wingi wa makosa ya nahau na sarfu, na kuwa kutopokewa kitabu cha jina hili katika vitabu vya Waarabu wa kale, yatilia nguvu kuwa hichi kimezuliwa tu katika zama za mwisho. Na maoni yanayo gongana juu ya uhakika wa Luqman Al-hakim: ni kuwa yeye ni Mnubi katika watu wa Abla au Uhabeshi, au mtu mweusi wa Sudan ya Misri, au ni Muibrani. Na wengi walio mtaja wanakubaliana kuwa hakuwa Nabii. Wachache tu ndio wanasema kuwa alikuwa Nabii. Na tunalo weza kutambua katika yaliyo tajwa ni kuwa hakuwa Mwaarabu, kwa sababu wote wamewafikiana kwa hayo. Na kwamba alikuwa ni mtu mwenye hikima, na hakuwa Nabii, na kwamba ameingiza miongoni mwa Waarabu hikima mpya zikawa zinatajwa mara nyingi kama ilivyo onekana baadae katika vitabu.
  14. وَوَصَّيْنَا ٱلْإِنسَـٰنَ بِوَٰلِدَيْهِ حَمَلَتْهُ أُمُّهُۥ وَهْنًا عَلَىٰ وَهْنٍ وَفِصَـٰلُهُۥ فِى عَامَيْنِ أَنِ ٱشْكُرْ لِى وَلِوَٰلِدَيْكَ إِلَىَّ ٱلْمَصِيرُ۝١٤

    Wawassayna alinsana biwalidayhi hamalathu ommuhu wahnan ʿala wahnin wafisaluhu fee ʿamayni ani oshkur lee waliwalidayka ilayya almaseeru

    Na tumemuusia mtu kwa wazazi wake wawili. Mama yake ameichukua mimba yake kwa udhaifu juu ya udhaifu, na kumwachisha ziwa baada ya miaka miwili. (Tumemuusia): Nishukuru Mimi na wazazi wako. Ni kwangu Mimi ndiyo marudio.14

    Maelezo
    [14] Na tumemuamrisha mtu awafanyie wema wazazi wake, na mama yake ampe fungu kubwa zaidi. Kwani yeye alimbeba katika mimba kwa udhaifu unao zidi kila siku kidogo kidogo. Na tena kamnyonyesha muda wa miaka miwili ndipo alipo muachisha ziwa. Na tumemuusia: Mshukuru Mwenyezi Mungu na wazazi wako. Kwa Mwenyezi Mungu ndio marejeo kwa ajili ya hisabu na malipo.
  15. وَإِن جَـٰهَدَاكَ عَلَىٰٓ أَن تُشْرِكَ بِى مَا لَيْسَ لَكَ بِهِۦ عِلْمٌ فَلَا تُطِعْهُمَا ۖ وَصَاحِبْهُمَا فِى ٱلدُّنْيَا مَعْرُوفًا ۖ وَٱتَّبِعْ سَبِيلَ مَنْ أَنَابَ إِلَىَّ ۚ ثُمَّ إِلَىَّ مَرْجِعُكُمْ فَأُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ۝١٥

    Wain jahadaka ʿala an tushrika bee ma laysa laka bihi ʿilmun fala tutiʿhuma wasahibhuma fee alddunya maʿroofan waittabiʿ sabeela man anaba ilayya thumma ilayya marjiʿukum faonabbiokum bima kuntum taʿmaloona

    Na pindi wakikushikilia kunishirikisha na ambayo huna ilimu nayo, basi usiwat'ii. Lakini kaa nao kwa wema duniani, nawe ishike njia ya anaye elekea kwangu. Kisha marejeo yenu ni kwangu Mimi, na Mimi nitakuambieni mliyo kuwa mkiyatenda.15

    Maelezo
    [15] Na ikiwa wazazi wako wakikushikilia kwa juhudi umshirikishe Mwenyezi Mungu na vitu usivyo vijua kuwa vinastahiki kuabudiwa, basi usiwakubalie. Lakini endelea na kusuhubiana nao duniani kwa wema na ihsani. Na fuata njia ya wanao rejea kwangu kwa Tawhidi, Imani ya Mwenyezi Mungu Mmoja, na Ikhlasi, usafi wa niya na vitendo. Kisha nyote mtarejea kwangu, na nitakupeni khabari ya mliyo kuwa mkiyatenda, ya kheri na shari, ili nipate kukulipeni kwayo.
  16. يَـٰبُنَىَّ إِنَّهَآ إِن تَكُ مِثْقَالَ حَبَّةٍ مِّنْ خَرْدَلٍ فَتَكُن فِى صَخْرَةٍ أَوْ فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ أَوْ فِى ٱلْأَرْضِ يَأْتِ بِهَا ٱللَّهُ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَطِيفٌ خَبِيرٌ۝١٦

    Ya bunayya innaha in taku mithqala habbatin min khardalin fatakun fee sakhratin aw fee alssamawati aw fee alardi yati biha Allahu inna Allaha lateefun khabeerun

    Ewe mwanangu! Kikiwapo kitu cha uzito wa chembe ya khardali kikawa ndani ya jabali au ndani ya mbingu au ndani ya ardhi, basi Mwenyezi Mungu atakileta. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa yaliyo fichika, Mwenye khabari za yote.16

    Maelezo
    [16] Ewe mwanangu! Hakika wema au ubaya kwa mtu, hata ukiwa, mathalan, kwa udogo wake kama chembe ya khardali, iliyoko pahali palipo fichikana kabisa, kama ndani ya jabali, au ndani ya mbingu, au chini ya ardhi, Mwenyezi Mungu ataufichua na autolee hisabu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa yaliyo fichika, hakifichikani kitu hata kidogo kwake, ni Mwenye khabari ya kujua hakika ya kila kitu.
  17. يَـٰبُنَىَّ أَقِمِ ٱلصَّلَوٰةَ وَأْمُرْ بِٱلْمَعْرُوفِ وَٱنْهَ عَنِ ٱلْمُنكَرِ وَٱصْبِرْ عَلَىٰ مَآ أَصَابَكَ ۖ إِنَّ ذَٰلِكَ مِنْ عَزْمِ ٱلْأُمُورِ۝١٧

    Ya bunayya aqimi alssalata wamur bialmaʿroofi wainha ʿani almunkari waisbir ʿala ma asabaka inna thalika min ʿazmi alomoori

    Ewe mwanangu! Shika Swala, na amrisha mema, na kataza maovu, na subiri kwa yanayo kupata. Hayo ni katika mambo ya kuazimiwa.17

    Maelezo
    [17] Ewe mwanangu! Zihifadhi Swala, na amrisha kila wema, na kataza kila baya, na stahamili kwa shida zinazo kusibu. Hakika anayo usia Mwenyezi Mungu ni katika mambo ambayo yanahitajia kufanyiwa hima na kuyashikilia.
  18. وَلَا تُصَعِّرْ خَدَّكَ لِلنَّاسِ وَلَا تَمْشِ فِى ٱلْأَرْضِ مَرَحًا ۖ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ كُلَّ مُخْتَالٍ فَخُورٍ۝١٨

    Wala tusaʿʿir khaddaka lilnnasi wala tamshi fee alardi marahan inna Allaha la yuhibbu kulla mukhtalin fakhoorin

    Wala usiwabeuwe watu, wala usitembee katika nchi kwa maringo. Hakika Mwenyezi Mungu hampendi kila anaye jivuna na kujifakhirisha.18

    Maelezo
    [18] Wala usiwageuzie watu uso wako kwa takaburi, wala usitembee katika nchi kwa kujiona na majivuno. Hakika Mwenyezi Mungu hampendi kila mwenye kuringa na kujiona.
  19. وَٱقْصِدْ فِى مَشْيِكَ وَٱغْضُضْ مِن صَوْتِكَ ۚ إِنَّ أَنكَرَ ٱلْأَصْوَٰتِ لَصَوْتُ ٱلْحَمِيرِ۝١٩

    Waiqsid fee mashyika waoghdud min sawtika inna ankara alaswati lasawtu alhameeri

    Na ushike mwendo wa katikati, na teremsha sauti yako. Hakika katika sauti mbaya zote bila ya shaka iliyo zidi ni sauti ya punda.19

    Maelezo
    [19] Na nenda mwendo wa wastani, si mbio mbio mno wala taratibu mno. Na teremsha sauti yako. Kwani hapana sauti mbaya kama sauti ya punda. Inaanzia kwa mngurumo unao ghasi, na inaishia kwa ukenje unao kera.
  20. أَلَمْ تَرَوْا۟ أَنَّ ٱللَّهَ سَخَّرَ لَكُم مَّا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَمَا فِى ٱلْأَرْضِ وَأَسْبَغَ عَلَيْكُمْ نِعَمَهُۥ ظَـٰهِرَةً وَبَاطِنَةً ۗ وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يُجَـٰدِلُ فِى ٱللَّهِ بِغَيْرِ عِلْمٍ وَلَا هُدًى وَلَا كِتَـٰبٍ مُّنِيرٍ۝٢٠

    Alam taraw anna Allaha sakhkhara lakum ma fee alssamawati wama fee alardi waasbagha ʿalaykum niʿamahu thahiratan wabatinatan wamina alnnasi man yujadilu fee Allahi bighayri ʿilmin wala hudan wala kitabin muneerin

    Kwani hamwoni ya kwamba Mwenyezi Mungu amevifanya vikutumikieni viliomo mbinguni na kwenye ardhi, na akakujalizieni neema zake, za dhaahiri na za siri? Na miongoni mwa watu wapo wanao bishana juu ya Mwenyezi Mungu pasipo ilimu, wala uwongofu, wala Kitabu chenye nuru.20

    Maelezo
    [20] Mmeona kwamba Mwenyezi Mungu amekudhalilishieni viliomo mbinguni kama jua, na mwezi, na nyota na vyenginevyo; na viliomo katika ardhi, kama mito, na matunda, na wanyama. Naye amekutimizieni neema zake zilio dhaahiri na zilio sitirika, msizo ziona. Na miongoni mwa watu, wapo wanao jadiliana juu ya dhati ya Mwenyezi Mungu na sifa zake bila ya dalili wala uwongozi ulio pokewa kutokana na Nabii au Wahyi (ufunuo) wenye kumurika kwa mwangaza njia ya Haki.
  21. وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ٱتَّبِعُوا۟ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ قَالُوا۟ بَلْ نَتَّبِعُ مَا وَجَدْنَا عَلَيْهِ ءَابَآءَنَآ ۚ أَوَلَوْ كَانَ ٱلشَّيْطَـٰنُ يَدْعُوهُمْ إِلَىٰ عَذَابِ ٱلسَّعِيرِ۝٢١

    Waitha qeela lahumu ittabiʿoo ma anzala Allahu qaloo bal nattabiʿu ma wajadna ʿalayhi abaana awalaw kana alshshaytanu yadʿoohum ila ʿathabi alssaʿeeri

    Na wanapo ambiwa: Fuateni aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, husema: Bali tunafuata tuliyo wakuta nayo baba zetu. Je! Ijapo kuwa Shet'ani anawaita kwenye adhabu ya Moto uwakao?21

    Maelezo
    [21] Na pindi wakiambiwa: Fuateni Haki na Uwongofu alio uteremsha Mwenyezi Mungu, wao husema: Bali sisi tunafuata tuliyo wakuta nao baba zetu. Je! Wanawafuata hao, ijapo kuwa Shetani ndio anawaitia wende kwenye upotovu utakao waingizia Motoni?
  22. ۞ وَمَن يُسْلِمْ وَجْهَهُۥٓ إِلَى ٱللَّهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ فَقَدِ ٱسْتَمْسَكَ بِٱلْعُرْوَةِ ٱلْوُثْقَىٰ ۗ وَإِلَى ٱللَّهِ عَـٰقِبَةُ ٱلْأُمُورِ۝٢٢

    Waman yuslim wajhahu ila Allahi wahuwa muhsinun faqadi istamsaka bialʿurwati alwuthqa waila Allahi ʿaqibatu alomoori

    Na mwenye kuuelekeza uso wake kwa Mwenyezi Mungu, naye akawa anafanya wema, basi huyo hakika amekwisha kamata fundo lilio madhubuti. Na mwisho wa mambo yote ni kwa Mwenyezi Mungu.22

    Maelezo
    [22] Na mwenye kumuelekea Mwenyezi Mungu kwa moyo wake na uso wake, na akamwakilisha Yeye mambo yake yote, naye akawa ni mwenye kutenda vitendo vyema, basi amefungamana na sababu za nguvu kabisa za kumfikisha kwenye radhi ya Mwenyezi Mungu. Na kwake Yeye, Subhanahu, ndio marejeo ya mambo yote.
  23. وَمَن كَفَرَ فَلَا يَحْزُنكَ كُفْرُهُۥٓ ۚ إِلَيْنَا مَرْجِعُهُمْ فَنُنَبِّئُهُم بِمَا عَمِلُوٓا۟ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمٌۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ۝٢٣

    Waman kafara fala yahzunka kufruhu ilayna marjiʿuhum fanunabbiohum bima ʿamiloo inna Allaha ʿaleemun bithati alssudoori

    Na anaye kufuru, isikuhuzunishe kufuru yake. Kwetu ndio marudio yao, na hapo tutawaambia waliyo yatenda. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani.23

    Maelezo
    [23] Na asiye mtakasia Mwenyezi Mungu dhati yake na nafsi yake, basi usikuhuzunishe upinzani wake na mapuuza yake. Kwetu Sisi peke yetu ndio marejeo yao Siku ya Kiyama. Hapo tutawaonyesha vitendo vyao. Kwani Sisi tumezunguka kwa kuvijua viliomo ndani ya nafsi zao, seuze vitendo vyao vya dhaahiri.
  24. نُمَتِّعُهُمْ قَلِيلًا ثُمَّ نَضْطَرُّهُمْ إِلَىٰ عَذَابٍ غَلِيظٍ۝٢٤

    Numattiʿuhum qaleelan thumma nadtarruhum ila ʿathabin ghaleethin

    Tunawastarehesha kwa uchache, kisha tutawasukuma kwenye adhabu ngumu.24

    Maelezo
    [24] Tunawastarehesha kwa muda mchache katika dunia yao, kisha tutawalazimisha kwenda kwenye adhabu kali isiyo stahimilika.
  25. وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ لَيَقُولُنَّ ٱللَّهُ ۚ قُلِ ٱلْحَمْدُ لِلَّهِ ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ۝٢٥

    Walain saaltahum man khalaqa alssamawati waalarda layaqoolunna Allahu quli alhamdu lillahi bal aktharuhum la yaʿlamoona

    Na ukiwauliza: Nani aliye ziumba mbingu na ardhi? Bila ya shaka watasema: Mwenyezi Mungu. Wewe sema: Alhamdulillahi! Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu. Lakini wengi wao hawajui.25

    Maelezo
    [25] Ewe Nabii! Nakuapia ya kuwa ukiwauliza: Nani aliye umba mbingu na ardhi? Hapana shaka watasema: Ni Mwenyezi Mungu. Sema: Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, aliye ziweka dalili za Upweke wake hata zikaubomoa ushirikina wao wa kumshirikisha na wenginewe katika ibada. Na lakini wengi wao hawajui ya kuwa kwa kukiri kwao huku, basi wamesimamisha hoja ya kuwapinga wenyewe kwa ubovu wa itikadi yao.
  26. لِلَّهِ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلْغَنِىُّ ٱلْحَمِيدُ۝٢٦

    Lillahi ma fee alssamawati waalardi inna Allaha huwa alghaniyyu alhameedu

    Ni vya Mwenyezi Mungu vyote viliomo mbinguni na katika ardhi. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mkwasi, Mwenye kusifiwa.26

    Maelezo
    [26] Viliomo katika mbingu na ardhi ni vya Mwenyezi Mungu, kwa kuviumba, na kuvikadiria, na kuvipanga. Basi vipi wao wanaacha kumuabudu Yeye? Na Mwenyezi Mungu Aliye takasika si mhitaji wa viumbe vyake wala ibada yao. Yeye ni Msifiwa kwa dhati yake. Ni mwenye kustahiki kusifiwa na waja wake.
  27. وَلَوْ أَنَّمَا فِى ٱلْأَرْضِ مِن شَجَرَةٍ أَقْلَـٰمٌ وَٱلْبَحْرُ يَمُدُّهُۥ مِنۢ بَعْدِهِۦ سَبْعَةُ أَبْحُرٍ مَّا نَفِدَتْ كَلِمَـٰتُ ٱللَّهِ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ۝٢٧

    Walaw annama fee alardi min shajaratin aqlamun waalbahru yamudduhu min baʿdihi sabʿatu abhurin ma nafidat kalimatu Allahi inna Allaha ʿazeezun hakeemun

    Na lau kuwa miti yote iliyomo duniani ikawa ni kalamu, na bahari (ikawa wino), na ikaongezewa juu yake bahari nyengine saba, maneno ya Mwenyezi Mungu yasingeli kwisha. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima.27

    Maelezo
    [27] Na lau kuwa miti yote ya duniani ikageuka kalamu, na maji yote ya baharini kwa wingi wake yakageuka wino, kuandikia maneno ya Mwenyezi Mungu, basi zingeli kwisha kalamu na wino ukamalizika kabla ya kumalizika maneno ya Mwenyezi Mungu. Kwani hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, hashindwi na chochote, Mwenye hikima hakimfutu kitu katika ujuzi wake na hikima yake. Basi hayeshi maneno yake na hikima yake.
  28. مَّا خَلْقُكُمْ وَلَا بَعْثُكُمْ إِلَّا كَنَفْسٍ وَٰحِدَةٍ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ سَمِيعٌۢ بَصِيرٌ۝٢٨

    Ma khalqukum wala baʿthukum illa kanafsin wahidatin inna Allaha sameeʿun baseerun

    Hakukuwa kuumbwa kwenu, wala kufufuliwa kwenu ila ni kama nafsi moja tu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia Mwenye kuona.28

    Maelezo
    [28] Kukuumbeni nyinyi hapo mwanzo na kukufufueni baada ya kufa, mbele ya uweza wa Mwenyezi Mungu si chochote ila ni kama kumuumba na kumfufua mtu mmoja tu. Hakika Mwenyezi Mungu anaisikia kauli ya washirikina wanapo sema ati: Hakuna kufufuliwa. Naye ni Mwenye kuviona vitendo vyao, naye atawalipa kwavyo.
  29. أَلَمْ تَرَ أَنَّ ٱللَّهَ يُولِجُ ٱلَّيْلَ فِى ٱلنَّهَارِ وَيُولِجُ ٱلنَّهَارَ فِى ٱلَّيْلِ وَسَخَّرَ ٱلشَّمْسَ وَٱلْقَمَرَ كُلٌّ يَجْرِىٓ إِلَىٰٓ أَجَلٍ مُّسَمًّى وَأَنَّ ٱللَّهَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ۝٢٩

    Alam tara anna Allaha yooliju allayla fee alnnahari wayooliju alnnahara fee allayli wasakhkhara alshshamsa waalqamara kullun yajree ila ajalin musamman waanna Allaha bima taʿmaloona khabeerun

    Kwani huoni kwamba Mwenyezi Mungu huuingiza usiku katika mchana, na huuingiza mchana katika usiku, na amedhalilisha jua na mwezi? Vyote hivyo vinakwenda mpaka wakati ulio wekwa. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda.29

    Maelezo
    [29] Je! Huangalii, ewe mwenye jukumu, kwa maangalio ya mwenye kuzingatia, ya kwamba hakika Mwenyezi Mungu huupunguza wakati wa usiku kwa kadri ya anavyo uongeza mchana? Na anaupunguza mchana kwa kadri ya anavyo uzidisha usiku? Naye amedhalilisha jua na mwezi kwa ajili ya maslaha yenu, na amefanya hayo yafuate mpango wa peke yao. Basi kila moja katika hayo huenda katika njia maalumu ya mbinguni wala haigeuki. Na mwendo huo unaendelea mpaka Siku ya Kiyama. Na hakika Yeye, Subhanahu, anazo khabari za yote myatendayo, na ni Mwenye kukulipeni kwayo.
  30. ذَٰلِكَ بِأَنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلْحَقُّ وَأَنَّ مَا يَدْعُونَ مِن دُونِهِ ٱلْبَـٰطِلُ وَأَنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلْعَلِىُّ ٱلْكَبِيرُ۝٣٠

    Thalika bianna Allaha huwa alhaqqu waanna ma yadʿoona min doonihi albatilu waanna Allaha huwa alʿaliyyu alkabeeru

    Hivi ni kwa sababu hakika Mwenyezi Mungu ndiye wa kweli, na hakika wanacho kiomba ni cha uwongo. Na kwamba hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mtukufu na ndiye Mkubwa.30

    Maelezo
    [30] Hayo yaliyo tajwa ni katika ajabu za uundaji wa Mwenyezi Mungu na uweza wake, kwa sababu muundaji wake ni Mungu aliye thibiti Ungu wake, Mwenye kustahiki peke yake kuabudiwa, na kwamba miungu yote mnayo iabudu badala yake ni miungu ya uwongo. Na hakika Mwenyezi Mungu, peke yake, ndiye Mtukufu wa shani, Mkubwa wa utawala.
  31. أَلَمْ تَرَ أَنَّ ٱلْفُلْكَ تَجْرِى فِى ٱلْبَحْرِ بِنِعْمَتِ ٱللَّهِ لِيُرِيَكُم مِّنْ ءَايَـٰتِهِۦٓ ۚ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَـٰتٍ لِّكُلِّ صَبَّارٍ شَكُورٍ۝٣١

    Alam tara anna alfulka tajree fee albahri biniʿmati Allahi liyuriyakum min ayatihi inna fee thalika laayatin likulli sabbarin shakoorin

    Kwani huoni kwamba marikebu hupita baharini zikichukua neema za Mwenyezi Mungu, ili kukuonyesheni baadhi ya Ishara zake? Hakika katika haya zipo Ishara kwa kila mwenye kusubiri, mwenye kushukuru.31

    Maelezo
    [31] Ewe mtu! Huzitazami marikebu, vyombo vinavyo kwenda baharini kwa rehema ya Mwenyezi Mungu, vikichukua ndani yake bidhaa za kukupeni manufaa, ili Mwenyezi Mungu akuonyesheni baadhi ya maajabu ya uundaji wake, na dalili za uweza wake? Hakika katika hayo zimo Ishara kwa kila mwenye kuvumilia mitihani yake, mwenye kuzishukuru kwa neema zake.
  32. وَإِذَا غَشِيَهُم مَّوْجٌ كَٱلظُّلَلِ دَعَوُا۟ ٱللَّهَ مُخْلِصِينَ لَهُ ٱلدِّينَ فَلَمَّا نَجَّىٰهُمْ إِلَى ٱلْبَرِّ فَمِنْهُم مُّقْتَصِدٌ ۚ وَمَا يَجْحَدُ بِـَٔايَـٰتِنَآ إِلَّا كُلُّ خَتَّارٍ كَفُورٍ۝٣٢

    Waitha ghashiyahum mawjun kaalththulali daʿawoo Allaha mukhliseena lahu alddeena falamma najjahum ila albarri faminhum muqtasidun wama yajhadu biayatina illa kullu khattarin kafoorin

    Na wimbi linapo wafunika kama wingu, wao humwomba Mwenyezi Mungu kwa kumsafia dini. Lakini anapo waokoa wakafika nchi kavu, wapo baadhi yao huenda mwendo wa sawa. Wala hazikanushi Ishara zetu ila aliye khaini kafiri mkubwa.32

    Maelezo
    [32] Hawa makafiri wanao mkataa Mwenyezi Mungu wakipanda marikebu, na bahari ikawachafukia, na mawimbi yakaja juu mpaka wakaona yatawafunika, na wakawa yakini watazama bila ya muhali, humkimbilia Mwenyezi Mungu, wakimwomba kwa ikhlasi na unyenyekevu, awaokoe. Basi akisha waokoa wakafika nchi kavu wapo kati yao wachache wanao kumbuka ahadi yao, na wakenda mwendo wa sawa. Na wapo kati yao, nao ndio wengi, walio sahau fadhila za Mola wao Mlezi, na wakaendelea na kumkataa. Na wala hakatai fadhila za Mola wake Mlezi na hisani yake ila kila mtu aliye mwingi wa ukhaini, aliye pita mpaka kumkanya Mola wake Mlezi.
  33. يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ ٱتَّقُوا۟ رَبَّكُمْ وَٱخْشَوْا۟ يَوْمًا لَّا يَجْزِى وَالِدٌ عَن وَلَدِهِۦ وَلَا مَوْلُودٌ هُوَ جَازٍ عَن وَالِدِهِۦ شَيْـًٔا ۚ إِنَّ وَعْدَ ٱللَّهِ حَقٌّ ۖ فَلَا تَغُرَّنَّكُمُ ٱلْحَيَوٰةُ ٱلدُّنْيَا وَلَا يَغُرَّنَّكُم بِٱللَّهِ ٱلْغَرُورُ۝٣٣

    Ya ayyuha alnnasu ittaqoo rabbakum waikhshaw yawman la yajzee walidun ʿan waladihi wala mawloodun huwa jazin ʿan walidihi shayan inna waʿda Allahi haqqun fala taghurrannakumu alhayatu alddunya wala yaghurrannakum biAllahi algharooru

    Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi, na iogopeni siku ambayo mzazi hatamfaa mwana, wala mwana hatamfaa mzazi kwa lolote. Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli. Basi yasikudanganyeni maisha ya dunia, wala asikudanganyeni na Mwenyezi Mungu mdanganyifu.33

    Maelezo
    [33] Enyi watu! Fanyeni aliyo kuamrisheni Mola wenu Mlezi, na wacheni aliyo kukatazeni. Na tahadharini na adhabu yake ya Siku ya Kiyama, Siku ambayo kwamba mzazi hatamfaa mwanawe kwa lolote, wala mwana hatamfaa mzazi wake kwa lolote. Hakika Siku hii ndiyo aliyo iahidi Mwenyezi Mungu. Na ahadi yake ni ya kweli, hayendi kinyume. Basi yasikupumbazeni mapambo ya dunia na uzuri wake, mkaacha kujitayarisha kwa ajili ya Siku hiyo. Wala msikhadaike na uchochezi wa Shetani, ukakuachisheni kumuelekea Mwenyezi Mungu na kumt'ii.
  34. إِنَّ ٱللَّهَ عِندَهُۥ عِلْمُ ٱلسَّاعَةِ وَيُنَزِّلُ ٱلْغَيْثَ وَيَعْلَمُ مَا فِى ٱلْأَرْحَامِ ۖ وَمَا تَدْرِى نَفْسٌ مَّاذَا تَكْسِبُ غَدًا ۖ وَمَا تَدْرِى نَفْسٌۢ بِأَىِّ أَرْضٍ تَمُوتُ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌۢ۝٣٤

    Inna Allaha ʿindahu ʿilmu alssaʿati wayunazzilu alghaytha wayaʿlamu ma fee alarhami wama tadree nafsun matha taksibu ghadan wama tadree nafsun biayyi ardin tamootu inna Allaha ʿaleemun khabeerun

    Hakika kuijua Saa (ya Kiyama) kuko kwa Mwenyezi Mungu. Na Yeye ndiye anaye iteremsha mvua. Na anavijua viliomo ndani ya matumbo ya uzazi. Na haijui nafsi yoyote itachuma nini kesho. Wala nafsi yoyote haijui itafia nchi gani. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujua, Mwenye khabari.34

    Maelezo
    [34] Hakika ujuzi wa Saa ya Kiyama uko kwa Mwenyezi Mungu umethibiti. Basi hapana anaye ijua isipo kuwa Yeye tu. Na Yeye huteremsha mvua kwa wakati wake alio uweka. Na anavijua viliomo ndani ya matumbo ya uzazi, kama wanaume, au wanawake, hivyo viliomo vimetimia au havikutimia mimba. Wala hapana mtu ajuaye, mwema na muovu, atapata nini kesho, kama kheri au shari. Wala hapana mtu ajuaye pahala gani duniani itamfika ajali yake ya kufa. Kwa hakika Mwenyezi Mungu ndiye aliye timia ujuzi wake na kuwa na khabari ya kila kitu. Wala hapana yeyote awezae kujua siri yake.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Surat Luqman iko katika juzuu ya ngapi?

Surat Luqman iko katika juzuu ya 21.

Surat Luqman ina aya ngapi?

Surat Luqman ina aya 34.

Surat Luqman ni ya Makka au ya Madina?

Surat Luqman ni sura ya Makka.

Surat Luqman ni sura ya ngapi katika Qur’ani?

Ni sura ya 31 katika Qur’ani.

Vyanzo

  • Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
  • Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
  • Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
  • Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
  • Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
  • Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.

Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.

Mipangilio ya kusoma

Fonti ya Qur’ani
Ukubwa wa Kiarabu
100%
Ukubwa wa tafsiri
100%
Mandhari

Ongeza kwenye skrini ya kwanza

ReadSurahFungua ReadSurah kutoka skrini ya kwanza, kwa skrini nzima. Sura ulizosoma hufunguka hata bila intaneti.

  1. Katika Safari, gusa kitufe cha kushiriki (Share). Kwenye iPhone mpya kiko kwenye menyu ya •••.
  2. Gusa “Add to Home Screen”. Huenda ukahitaji kusogeza chini.
  3. Gusa “Add”.