Surat As-Sajda (السجدة) ni sura ya 32 katika Qur’ani na ina aya 30. Jina lake lina maana ya “Kusujudu”. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na iko katika juzuu ya 21.
Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat As-Sajda yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.
Surat As-Sajda kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
-
الٓمٓ١
Aliflammeem
Alif Lam Mim (A.L.M.) .1
Maelezo
[1] Alif Lam Mim, ni harufi zilizo undiwa Qur'ani, kama yalivyo undiwa maneno yenu. Ikiwa mmeshindwa kuleta mfano wake hii, basi ni ushahidi kuwa hii inatokana na Mwenyezi Mungu, wala hakuisema mwanaadamu. -
تَنزِيلُ ٱلْكِتَـٰبِ لَا رَيْبَ فِيهِ مِن رَّبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ٢
Tanzeelu alkitabi la rayba feehi min rabbi alʿalameena
Huu ni mteremsho wa Kitabu kisicho kuwa na shaka yoyote kinacho toka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.2
Maelezo
[2] Huu ni uteremsho wa Qur'ani umetoka kwa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote. Na Yeye ndiye mwenye kupanga mambo yao. Hapana shaka yoyote kuwa hii imeteremka kutoka kwake. -
أَمْ يَقُولُونَ ٱفْتَرَىٰهُ ۚ بَلْ هُوَ ٱلْحَقُّ مِن رَّبِّكَ لِتُنذِرَ قَوْمًا مَّآ أَتَىٰهُم مِّن نَّذِيرٍ مِّن قَبْلِكَ لَعَلَّهُمْ يَهْتَدُونَ٣
Am yaqooloona iftarahu bal huwa alhaqqu min rabbika litunthira qawman ma atahum min natheerin min qablika laʿallahum yahtadoona
Au wanasema: Amekizua? Bali hichi ni Kweli iliyo toka kwa Mola wako Mlezi ili uwaonye watu wasio fikiwa na mwonyaji kabla yako; huenda wakaongoka.3
Maelezo
[3] Ati wanasema: Kaizua Muhammad, naye akamsingizia Mwenyezi Mungu! Haiwafalii wao kusema hayo. Kwani hii ni Haki, Kweli, iliyo teremka kutokana na Mola wako Mlezi, ili upate kuwakhofisha kwayo watu ambao hawajapata kujiwa na Mtume kabla yako, utaraji kwa onyo hili wapate kuongoka na waifuate Haki. -
ٱللَّهُ ٱلَّذِى خَلَقَ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِى سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ ٱسْتَوَىٰ عَلَى ٱلْعَرْشِ ۖ مَا لَكُم مِّن دُونِهِۦ مِن وَلِىٍّ وَلَا شَفِيعٍ ۚ أَفَلَا تَتَذَكَّرُونَ٤
Allahu allathee khalaqa alssamawati waalarda wama baynahuma fee sittati ayyamin thumma istawa ʿala alʿarshi ma lakum min doonihi min waliyyin wala shafeeʿin afala tatathakkaroona
Mwenyezi Mungu ndiye aliye umba mbingu na ardhi na viliomo baina yao kwa siku sita, na akatawala kwenye Kiti cha Enzi. Nyinyi hamna mlinzi wala mwombezi isipo kuwa Yeye tu. Basi, je, hamkumbuki?4
Maelezo
[4] Mwenyezi Mungu aliye umba mbingu na ardhi na vilio baina yao kwa siku sita, kisha akatawala juu ya Kiti cha Enzi, A'rshi, kwa utawala ulio laiki naye. Nyinyi hamna badala yake Yeye yeyote msaidizi wa kukunusuruni, wala mwombezi wa kukuombeeni. Basi je, mtaendelea kushikilia kuwa katika ukafiri na inda, wala msiwaidhike kwa mawaidha ya Mwenyezi Mungu? -
يُدَبِّرُ ٱلْأَمْرَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ إِلَى ٱلْأَرْضِ ثُمَّ يَعْرُجُ إِلَيْهِ فِى يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُۥٓ أَلْفَ سَنَةٍ مِّمَّا تَعُدُّونَ٥
Yudabbiru alamra mina alssamai ila alardi thumma yaʿruju ilayhi fee yawmin kana miqdaruhu alfa sanatin mimma taʿuddoona
Anapitisha mambo yote yalio baina mbingu na ardhi, kisha yanapanda kwake kwa siku ambayo kipimo chake ni miaka elfu kwa mnavyo hisabu nyinyi.5
Maelezo
[5] Yeye huyaendesha mambo ya uumbaji katika mbingu na ardhi, kisha amri yake hupanda kwenda kwake kwa siku ambayo kadiri yake ni kama miaka elfu kwa mujibu wa miaka ya duniani mnayo ihisabu nyinyi. -
ذَٰلِكَ عَـٰلِمُ ٱلْغَيْبِ وَٱلشَّهَـٰدَةِ ٱلْعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ٦
Thalika ʿalimu alghaybi waalshshahadati alʿazeezu alrraheemu
Huyu ndiye Mwenye kuyajua yasiyo onekana na yanayo onekana. Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu.6
Maelezo
[6] Huyo ndiye aliye sifika kwa kuumba na kutawala na kupanga, Mwenye kuyajua ya ghaibu ya viumbe vyote na wanayo yaona, ambaye amri yake ni yenye kushinda, Mkunjufu wa rehema, -
ٱلَّذِىٓ أَحْسَنَ كُلَّ شَىْءٍ خَلَقَهُۥ ۖ وَبَدَأَ خَلْقَ ٱلْإِنسَـٰنِ مِن طِينٍ٧
Allathee ahsana kulla shayin khalaqahu wabadaa khalqa alinsani min teenin
Ambaye ametengeneza vizuri umbo la kila kitu; na akaanzisha kumuumba mtu kwa udongo.7
Maelezo
[7] Aliye umba kila kitu kwa ustadi, kwa mujibu wa inavyo hitajia hikima yake, na akaanza kumuumba mtu wa mwanzo kwa udongo, -
ثُمَّ جَعَلَ نَسْلَهُۥ مِن سُلَـٰلَةٍ مِّن مَّآءٍ مَّهِينٍ٨
Thumma jaʿala naslahu min sulalatin min main maheenin
Na kisha akajaalia uzao wake utokane na kizazi cha maji madhaifu.8
Maelezo
[8] Kisha akawafanya dhuriya zake wa namna mbali mbali kutokana na maji machache, dhaifu, yasiyo tamanika kwa kawaida. Katika Aya hii tukufu "utokane na kizazi cha maji dhaifu". Neno la Kiarabu lilio tumiwa ni "Mahiin". Neno hili likitumiwa kwa mtu lina maana ya "dhaif", mnyonge, na pia lina maana ya "chache". Basi kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Min maain mahiin" maana yake ni "kutokana na maji machache dhaifu" , ndiyo ya kudharauliwa. Mfano wa hayo ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Au mimi si bora kuliko huyu aliye (mahiin) mnyonge wala hawezi kusema waziwazi?" (Azzukhruf: 43.52). Na neno "Mahana al-ibila" maana yake "Kamkama maziwa ngamia". Kwa hivyo basi hapana ubaya kulifasiri neno hili Mahiin katika Aya hii kwa maana ya maji yanayo toka kwa kuchupa, au kumiminika, (kama yanavyo toka maziwa kwenye chuchu) au machache. -
ثُمَّ سَوَّىٰهُ وَنَفَخَ فِيهِ مِن رُّوحِهِۦ ۖ وَجَعَلَ لَكُمُ ٱلسَّمْعَ وَٱلْأَبْصَـٰرَ وَٱلْأَفْـِٔدَةَ ۚ قَلِيلًا مَّا تَشْكُرُونَ٩
Thumma sawwahu wanafakha feehi min roohihi wajaʿala lakumu alssamʿa waalabsara waalafidata qaleelan ma tashkuroona
Kisha akamtengeneza, na akampulizia roho yake, na akakujaalieni kusikia na kuona, na nyoyo za kufahamu. Ni uchache mnavyo shukuru.9
Maelezo
[9] Kisha akamsimamisha na kumkuza, na akamtia ndani yake siri yake aliyo mkhusisha nayo, na akakupeni masikio, na macho, na akili, mpate kusikia na kuona na kufahamu. Nanyi hamshukuru ila kwa uchache. -
وَقَالُوٓا۟ أَءِذَا ضَلَلْنَا فِى ٱلْأَرْضِ أَءِنَّا لَفِى خَلْقٍ جَدِيدٍۭ ۚ بَلْ هُم بِلِقَآءِ رَبِّهِمْ كَـٰفِرُونَ١٠
Waqaloo aitha dalalna fee alardi ainna lafee khalqin jadeedin bal hum biliqai rabbihim kafiroona
Nao husema: Tutapo kwisha potea chini ya ardhi, ni kweli tutarudishwa katika umbo jipya? Bali wao wanakanusha kwamba watakutana na Mola wao Mlezi.10
Maelezo
[10] Na wanao kanya kufufuliwa wakasema: Ati sisi tukisha kuwa mchanga, ulio changanyika na mchanga wa ardhi, usibagulike, ndio kweli tutarejea kwa umbo jipya? Hao hakika si kama wanakanya kufufuliwa tu, bali wanakadhibisha yote yatayo kuwako Akhera. -
۞ قُلْ يَتَوَفَّىٰكُم مَّلَكُ ٱلْمَوْتِ ٱلَّذِى وُكِّلَ بِكُمْ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُمْ تُرْجَعُونَ١١
Qul yatawaffakum malaku almawti allathee wukkila bikum thumma ila rabbikum turjaʿoona
Sema: Atakufisheni Malaika wa mauti aliye wakilishwa juu yenu; kisha mtarejeshwa kwa Mola wenu Mlezi.11
Maelezo
[11] Sema: Atakufisheni Malaika wa mauti, aliyewakilishwa kuzikamata roho zenu utapo kwisha muda wenu. Kisha kwa Mwenyezi Mungu peke yake ndio mtarejea. -
وَلَوْ تَرَىٰٓ إِذِ ٱلْمُجْرِمُونَ نَاكِسُوا۟ رُءُوسِهِمْ عِندَ رَبِّهِمْ رَبَّنَآ أَبْصَرْنَا وَسَمِعْنَا فَٱرْجِعْنَا نَعْمَلْ صَـٰلِحًا إِنَّا مُوقِنُونَ١٢
Walaw tara ithi almujrimoona nakisoo ruoosihim ʿinda rabbihim rabbana absarna wasamiʿna faarjiʿna naʿmal salihan inna mooqinoona
Na ungeli waona wakosefu wanvyo inamisha vichwa vyao mbele ya Mola wao Mlezi, (wakisema): Mola wetu Mlezi! Tumesha ona, na tumesha sikia. Turejeshe tukatende mema, kwani hakika sisi tumekwisha kuwa na yakini sasa.12
Maelezo
[12] Lau kuwa umejaaliwa kuwaona wakosefu kwenye msimamo wa hisabu ungeli ona ajabu. Pale wale wakosefu wenye kujivuna watavyo inamisha vichwa vyao kwa hizaya inayo tokana na Mola wao Mlezi, nao watasema kwa unyonge: Ewe Mola wetu Mlezi! Tumekwisha yaona tuliyo kuwa na upofu nayo, na tumekwisha yasikia tuliyo kuwa na uziwi nayo, basi turejeshe duniani tupate tenda mema ambayo tuliyo kuwa hatuyatendi. Hakika sasa hivi sisi tumeyakinika na walio kuja nayo Mitume wako. -
وَلَوْ شِئْنَا لَـَٔاتَيْنَا كُلَّ نَفْسٍ هُدَىٰهَا وَلَـٰكِنْ حَقَّ ٱلْقَوْلُ مِنِّى لَأَمْلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنَ ٱلْجِنَّةِ وَٱلنَّاسِ أَجْمَعِينَ١٣
Walaw shina laatayna kulla nafsin hudaha walakin haqqa alqawlu minnee laamlaanna jahannama mina aljinnati waalnnasi ajmaʿeena
Na lau tungeli taka tunge mpa kila mtu uwongofu wake. Lakini imekwisha kuwa kauli iliyo toka kwangu : Kwa yakini nitaijaza Jahannamu kwa wote hawa, majini na watu.13
Maelezo
[13] Na lau kuwa tunataka tungeli mpa kila mtu uwongofu wake, lakini kauli yangu ilikwisha tangulia, nayo ni: Bila ya shaka nitaijaza Jahannamu kwa wote hawa majini na watu. Kwa kuwa tulijua kuwa wengi wao watakhiari upotovu. -
فَذُوقُوا۟ بِمَا نَسِيتُمْ لِقَآءَ يَوْمِكُمْ هَـٰذَآ إِنَّا نَسِينَـٰكُمْ ۖ وَذُوقُوا۟ عَذَابَ ٱلْخُلْدِ بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ١٤
Fathooqoo bima naseetum liqaa yawmikum hatha inna naseenakum wathooqoo ʿathaba alkhuldi bima kuntum taʿmaloona
Basi onjeni kwa vile mlivyo usahau mkutano wa Siku yenu hii. Na Sisi hakika tunakusahauni. Basi onjeni adhabu ya milele kwa yale mliyo kuwa mkiyatenda.14
Maelezo
[14] Basi ionjeni adhabu kwa vile mlivyo ghafilika na kukutana nami hii leo. Hakika Sisi tunakuacheni katika adhabu kama watu walio sahauliwa. Na onjeni adhabu ya milele isiyo katika, kwa sababu ya ukafiri wenu na uasi wenu. -
إِنَّمَا يُؤْمِنُ بِـَٔايَـٰتِنَا ٱلَّذِينَ إِذَا ذُكِّرُوا۟ بِهَا خَرُّوا۟ سُجَّدًا وَسَبَّحُوا۟ بِحَمْدِ رَبِّهِمْ وَهُمْ لَا يَسْتَكْبِرُونَ ۩١٥
Innama yuminu biayatina allatheena itha thukkiroo biha kharroo sujjadan wasabbahoo bihamdi rabbihim wahum la yastakbiroona
Hakika wanao ziamini Aya zetu ni hao tu ambao wakikumbushwa hizo, basi wao huanguka kusujudu, na humsabihi Mola wao Mlezi kwa kumhimidi, nao hawajivuni.15
Maelezo
[15] Hakika wanazisadiki Ishara zetu wale ambao wanapo waidhiwa kwazo huanguka chini kwa kumsujudia Mwenyezi Mungu, na wakamtakasa Mola wao Mlezi na kila upungufu, na wakamsifu kwa kila ukamilifu. Na wala wao hawatakabari wakakataa kuzifuata Ishara hizi. -
تَتَجَافَىٰ جُنُوبُهُمْ عَنِ ٱلْمَضَاجِعِ يَدْعُونَ رَبَّهُمْ خَوْفًا وَطَمَعًا وَمِمَّا رَزَقْنَـٰهُمْ يُنفِقُونَ١٦
Tatajafa junoobuhum ʿani almadajiʿi yadʿoona rabbahum khawfan watamaʿan wamimma razaqnahum yunfiqoona
Mbavu zao zinaachana na vitanda kwa kumwomba Mola wao Mlezi kwa khofu na kutumaini, na hutoa kutokana na tulivyo waruzuku.16
Maelezo
[16] Mbavu zao zinabambatuka na vitanda vyao, yaani wanaacha usingizi wao, kwa kumwomba Mola wao Mlezi kwa kuikhofu ghadhabu yake, na kutumai rehema yake; na ambao kutokana na mali tuliyo wapa wanatoa kwa ajili ya mambo ya kheri. -
فَلَا تَعْلَمُ نَفْسٌ مَّآ أُخْفِىَ لَهُم مِّن قُرَّةِ أَعْيُنٍ جَزَآءًۢ بِمَا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ١٧
Fala taʿlamu nafsun ma okhfiya lahum min qurrati aʿyunin jazaan bima kanoo yaʿmaloona
Nafsi yoyote haijui waliyo fichiwa katika hayo yanayo furahisha macho - ni malipo ya yale waliyo kuwa wakiyatenda.17
Maelezo
[17] Na hapana mtu yeyote anaye jua kiasi cha Mwenyezi Mungu alicho muandalia na akawafichia katika neema kubwa kubwa, na ambazo ni za kupoza macho yao, kuwa ni malipo kwa waliyo kuwa wanayachuma ya ut'iifu na vitendo. -
أَفَمَن كَانَ مُؤْمِنًا كَمَن كَانَ فَاسِقًا ۚ لَّا يَسْتَوُۥنَ١٨
Afaman kana muminan kaman kana fasiqan la yastawoona
Ati aliye Muumini atakuwa sawa na aliye mpotovu? Hawawi sawa.18
Maelezo
[18] Kwani watu watakuwa sawa katika malipo yao, na hali wamekhitalifiana katika vitendo vyao? Je! Aliye kuwa mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu ni kama mwenye kumkataa na akamuasi? Hasha! Hawawi sawa! -
أَمَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ فَلَهُمْ جَنَّـٰتُ ٱلْمَأْوَىٰ نُزُلًۢا بِمَا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ١٩
Amma allatheena amanoo waʿamiloo alssalihati falahum jannatu almawa nuzulan bima kanoo yaʿmaloona
Ama walio amini na wakatenda mema, watakuwa nazo Bustani za makaazi mazuri. Ndio pa kufikia kwa waliyo kuwa wakiyatenda.19
Maelezo
[19] Ama walio amini na wakatenda mema watapata Bustani za Utulivu ziwe ndio maskani zao, kuwa ni ukarimu watao kirimiwa kwa waliyo kuwa wakiyatenda. -
وَأَمَّا ٱلَّذِينَ فَسَقُوا۟ فَمَأْوَىٰهُمُ ٱلنَّارُ ۖ كُلَّمَآ أَرَادُوٓا۟ أَن يَخْرُجُوا۟ مِنْهَآ أُعِيدُوا۟ فِيهَا وَقِيلَ لَهُمْ ذُوقُوا۟ عَذَابَ ٱلنَّارِ ٱلَّذِى كُنتُم بِهِۦ تُكَذِّبُونَ٢٠
Waamma allatheena fasaqoo famawahumu alnnaru kullama aradoo an yakhrujoo minha oʿeedoo feeha waqeela lahum thooqoo ʿathaba alnnari allathee kuntum bihi tukaththiboona
Na ama wale walio tenda uovu, basi makaazi yao ni Motoni. Kila wakitaka kutoka humo watarudishwa humo humo. Na wataambiwa: Onjeni adhabu ya Moto ambayo mliyo kuwa mkiikanusha.20
Maelezo
[20] Ama wale walio toka nje ya ut'iifu wa Mwenyezi Mungu kwa kufuru zao, makaazi yao aliyo watayarishia ni Motoni. Kila wakijaribu kutoka watarudishwa huko huko. Na wataambiwa: Onjeni adhabu ya Moto ambayo mlipo kuwa duniani mkishikilia kuikadhibisha. -
وَلَنُذِيقَنَّهُم مِّنَ ٱلْعَذَابِ ٱلْأَدْنَىٰ دُونَ ٱلْعَذَابِ ٱلْأَكْبَرِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ٢١
Walanutheeqannahum mina alʿathabi aladna doona alʿathabi alakbari laʿallahum yarjiʿoona
Na tutawaonjesha adhabu khafifu kabla ya adhabu kubwa, huenda labda watarejea.21
Maelezo
[21] Na tunaapa: Hapana shaka tutawaonjesha duniani adhabu duni kabla hawajaifikia hiyo adhabu kubwa kabisa, nayo ni kudumu milele katika Moto. Huenda pengine watakao adhibiwa kwa hiyo adhabu duni watatubia, waache ukafiri wao. -
وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن ذُكِّرَ بِـَٔايَـٰتِ رَبِّهِۦ ثُمَّ أَعْرَضَ عَنْهَآ ۚ إِنَّا مِنَ ٱلْمُجْرِمِينَ مُنتَقِمُونَ٢٢
Waman athlamu mimman thukkira biayati rabbihi thumma aʿrada ʿanha inna mina almujrimeena muntaqimoona
Na ni nani dhaalimu mkubwa kuliko yule anaye kumbushwa kwa Ishara za Mola wake Mlezi, kisha akazikataa? Hakika Sisi tutajilipiza kwa wakosefu.22
Maelezo
[22] Na hapana mtu yeyote aliye zidi udhaalimu kuidhulumu Haki na kuidhulumu nafsi yake, kuliko mtu anaye kumbushwa kwa Ishara za Mwenyezi Mungu na hoja zilizo wazi, kisha akaacha kuziamini juu ya kuwa ni wazi dhaahiri. Hakika Sisi tutajilipizia juu ya kila mkosefu! -
وَلَقَدْ ءَاتَيْنَا مُوسَى ٱلْكِتَـٰبَ فَلَا تَكُن فِى مِرْيَةٍ مِّن لِّقَآئِهِۦ ۖ وَجَعَلْنَـٰهُ هُدًى لِّبَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ٢٣
Walaqad atayna moosa alkitaba fala takun fee miryatin min liqaihi wajaʿalnahu hudan libanee israeela
Hakika Sisi tulikwisha mpa Musa Kitabu. Basi usiwe na shaka kuwa kakipokea. Na tukakifanya kuwa ni uwongofu kwa Wana wa Israili.23
Maelezo
[23] Na Sisi tulikwisha mpa Musa Taurati. Basi usiwe na shaka na kupokea kwa Musa Kitabu hicho. Na tumekijaalia Kitabu alicho teremshiwa Musa kiwe ni uwongofu kwa Wana wa Israili. -
وَجَعَلْنَا مِنْهُمْ أَئِمَّةً يَهْدُونَ بِأَمْرِنَا لَمَّا صَبَرُوا۟ ۖ وَكَانُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَا يُوقِنُونَ٢٤
Wajaʿalna minhum aimmatan yahdoona biamrina lamma sabaroo wakanoo biayatina yooqinoona
Na tukawafanya miongoni mwao waongozi wanao ongoa watu kwa amri yetu, walipo subiri na wakawa na yakini na Ishara zetu.24
Maelezo
[24] Na kutokana na Wana wa Israili tumejaalia wawepo Maimamu, waongozi, wa Dini, wasimame kuwaongoa watu, kwa kuitikia amri yetu kwa vile walivyo vumilia kuyatenda yaliomo katika Taurati, na wakawa wanazisadiki Ishara zetu ukomo wa kusadiki. -
إِنَّ رَبَّكَ هُوَ يَفْصِلُ بَيْنَهُمْ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ فِيمَا كَانُوا۟ فِيهِ يَخْتَلِفُونَ٢٥
Inna rabbaka huwa yafsilu baynahum yawma alqiyamati feema kanoo feehi yakhtalifoona
Hakika Mola wako Mlezi ndiye atakaye fafanua baina yao Siku ya Kiyama katika waliyo kuwa wakikhitalifiana.25
Maelezo
[25] Hakika Mola wako Mlezi ndiye peke yake atakaye hukumu baina ya Manabii na kaumu zao Siku ya Kiyama katika mambo wanayo khitalifiana. -
أَوَلَمْ يَهْدِ لَهُمْ كَمْ أَهْلَكْنَا مِن قَبْلِهِم مِّنَ ٱلْقُرُونِ يَمْشُونَ فِى مَسَـٰكِنِهِمْ ۚ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَـٰتٍ ۖ أَفَلَا يَسْمَعُونَ٢٦
Awalam yahdi lahum kam ahlakna min qablihim mina alqurooni yamshoona fee masakinihim inna fee thalika laayatin afala yasmaʿoona
Je! Haijawabainikia kwamba kaumu ngapi tuliziangamiza kabla yao, nao wanapita katika maskani zao hizo? Hakika katika hayo zipo Ishara. Basi, je, hawasikii?26
Maelezo
[26] Je! Kwani Mwenyezi Mungu aliwaacha walio wakadhibisha Mitume wao, na hakuwabainishia kwamba Yeye aliwahilikisha wengi katika kaumu zilizo watangulia, na wao wanapita kwenye majumba yao, na wanatembea kwenye maskani zao? Hakika katika hayo pana mawaidha ya kuwaonyesha Haki. Wao wameingiwa na uziwi, hawasikii mawaidha haya. -
أَوَلَمْ يَرَوْا۟ أَنَّا نَسُوقُ ٱلْمَآءَ إِلَى ٱلْأَرْضِ ٱلْجُرُزِ فَنُخْرِجُ بِهِۦ زَرْعًا تَأْكُلُ مِنْهُ أَنْعَـٰمُهُمْ وَأَنفُسُهُمْ ۖ أَفَلَا يُبْصِرُونَ٢٧
Awalam yaraw anna nasooqu almaa ila alardi aljuruzi fanukhriju bihi zarʿan takulu minhu anʿamuhum waanfusuhum afala yubsiroona
Je! Hawaoni ya kwamba tunayapeleka maji kwenye ardhi kavu, kisha kwayo tunaitoa mimea wanayo kula wanyama wao na wao wenyewe? Je! Hawaoni?27
Maelezo
[27] Wameingia upofu, na wala hawaoni ya kwamba hakika Sisi tunapeleka mvua na mito kwenye ardhi za ukame ambazo hazimei mimea, na tukaziotesha mazao yake, wakala wanyama wao, na wao wenyewe wakala nafaka zake na matunda yake? Wamepofuka, na kwa hivyo hawazioni dalili za Mwenyezi Mungu za kuwafufua wafu. -
وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَـٰذَا ٱلْفَتْحُ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ٢٨
Wayaqooloona mata hatha alfathu in kuntum sadiqeena
Wanasema: Ushindi huu ni lini, kama mnasema kweli?28
Maelezo
[28] Na washirikina wanakwambia wewe na Waumini: Wakati gani Mwenyezi Mungu atakufungulieni mpate ushindi? Twambieni wakati wake ikiwa nyinyi ni wasema kweli. -
قُلْ يَوْمَ ٱلْفَتْحِ لَا يَنفَعُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓا۟ إِيمَـٰنُهُمْ وَلَا هُمْ يُنظَرُونَ٢٩
Qul yawma alfathi la yanfaʿu allatheena kafaroo eemanuhum wala hum yuntharoona
Sema: Siku ya Ushindi, wale walio kufuru imani yao haitawafaa kitu, wala wao hawatapewa muhula.29
Maelezo
[29] Waambie: Siku ya hukumu na kufafanua ikikufikilieni, walio kufuru haitowafaa kitu imani yao, wala hawatapewa muhula hata chembe ya hiyo adhabu wanayo istahiki. -
فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ وَٱنتَظِرْ إِنَّهُم مُّنتَظِرُونَ٣٠
Faaʿrid ʿanhum waintathir innahum muntathiroona
Basi wapuuze, nawe ngonja; hakika wao wanangoja.30
Maelezo
[30] Na ikiwa kufanya maskhara kama hivi ndio mtindo wao, basi wapuuzilie mbali. Na wewe ngojea ukweli aliyo kuahidi Mola wako Mlezi juu yao, kwani wao wanakungojea ushindwe.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Surat As-Sajda maana yake ni nini?
As-Sajda maana yake ni “Kusujudu”.
Surat As-Sajda iko katika juzuu ya ngapi?
Surat As-Sajda iko katika juzuu ya 21.
Surat As-Sajda ina aya ngapi?
Surat As-Sajda ina aya 30.
Surat As-Sajda ni ya Makka au ya Madina?
Surat As-Sajda ni sura ya Makka.
Surat As-Sajda ni sura ya ngapi katika Qur’ani?
Ni sura ya 32 katika Qur’ani.
Vyanzo
- Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
- Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
- Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
- Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
- Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
- Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.
Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.