سورة الانسان

Surat Al-Insan kwa Kiswahili

Mwanadamu

Msahafu

Mishary Rashid AlafasyPakua MP3Pakua PDF

Surat Al-Insan (الانسان) ni sura ya 76 katika Qur’ani na ina aya 31. Jina lake lina maana ya “Mwanadamu”. Ni sura ya Madina, iliyoteremshwa Madina baada ya Hijra, na iko katika juzuu ya 29.

Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat Al-Insan yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.

Surat Al-Insan kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

  1. هَلْ أَتَىٰ عَلَى ٱلْإِنسَـٰنِ حِينٌ مِّنَ ٱلدَّهْرِ لَمْ يَكُن شَيْـًٔا مَّذْكُورًا۝١

    Hal ata ʿala alinsani heenun mina alddahri lam yakun shayan mathkooran

    Hakika kilimpitia binaadamu kipindi katika zama ambacho kwamba hakuwa kitu kinacho tajwa.1

    Maelezo
    [1] Hakika kimempitia mwanaadamu kipindi cha zama kabla hajapuliziwa roho, naye hata bado hakuwa ni kitu cha kutajika kwa jina lake, wala hajuulikani nini atakuwa.
  2. إِنَّا خَلَقْنَا ٱلْإِنسَـٰنَ مِن نُّطْفَةٍ أَمْشَاجٍ نَّبْتَلِيهِ فَجَعَلْنَـٰهُ سَمِيعًۢا بَصِيرًا۝٢

    Inna khalaqna alinsana min nutfatin amshajin nabtaleehi fajaʿalnahu sameeʿan baseeran

    Hakika Sisi tumemuumba mtu kutokana na mbegu ya uhai iliyo changanyika, tumfanyie mtihani. Kwa hivyo tukamfanya mwenye kusikia, mwenye kuona.2

    Maelezo
    [2] Hakika Sisi tumemuumba mwanaadamu naye ana sifa namna mbali mbali, kwa ajili ya kumtia mtihanini, majaribioni, baadaye. Kwa hivyo tukamjaalia awe anasikia na anaona, ili apate kuzisikia Aya na azione Ishara.
  3. إِنَّا هَدَيْنَـٰهُ ٱلسَّبِيلَ إِمَّا شَاكِرًا وَإِمَّا كَفُورًا۝٣

    Inna hadaynahu alssabeela imma shakiran waimma kafooran

    Hakika Sisi tumembainishia Njia. Ama ni mwenye kushukuru, au mwenye kukufuru.3

    Maelezo
    [3] Hakika Sisi tumembainishia Njia ya Uwongofu, ama awe Muumini au awe kafiri.
  4. إِنَّآ أَعْتَدْنَا لِلْكَـٰفِرِينَ سَلَـٰسِلَا۟ وَأَغْلَـٰلًا وَسَعِيرًا۝٤

    Inna aʿtadna lilkafireena salasila waaghlalan wasaʿeeran

    Hakika HaSisi tumewaandalia makafiri minyororo na pingu na Moto mkali.4

    Maelezo
    [4] Hakika Sisi tumewawekea tayari makafiri minyororo kuwafungia miguu yao, pingu za kuwafungia mikono na shingo, na moto unao waka.
  5. إِنَّ ٱلْأَبْرَارَ يَشْرَبُونَ مِن كَأْسٍ كَانَ مِزَاجُهَا كَافُورًا۝٥

    Inna alabrara yashraboona min kasin kana mizajuha kafooran

    Hakika watu wema watakunywa katika vinywaji vilivyo changanyika na kafuri!5

    Maelezo
    [5] Hakika walio kuwa wakweli katika Imani yao watakunywa mvinyo iliyo changanywa na maji ya kafuri.
  6. عَيْنًا يَشْرَبُ بِهَا عِبَادُ ٱللَّهِ يُفَجِّرُونَهَا تَفْجِيرًا۝٦

    ʿAynan yashrabu biha ʿibadu Allahi yufajjiroonaha tafjeeran

    Ni chemchem watakao inywa waja wa Mwenyezi Mungu, wakiifanya imiminike kwa wingi.6

    Maelezo
    [6] Hiyo ni chemchem wanayo inywa waja wa Mwenyezi Mungu, na wanaipitisha watakapo kwa sahala.
  7. يُوفُونَ بِٱلنَّذْرِ وَيَخَافُونَ يَوْمًا كَانَ شَرُّهُۥ مُسْتَطِيرًا۝٧

    Yoofoona bialnnathri wayakhafoona yawman kana sharruhu mustateeran

    Wanatimiza ahadi,na wanaiogopa siku ambayo shari yake inaenea sana,7

    Maelezo
    [7] Wanatekeleza yaliyo wajibikia , na wanaikhofu Siku kubwa hiyo ambayo madhara yake yataenea kote kote,
  8. وَيُطْعِمُونَ ٱلطَّعَامَ عَلَىٰ حُبِّهِۦ مِسْكِينًا وَيَتِيمًا وَأَسِيرًا۝٨

    Wayutʿimona alttaʿama ʿala hubbihi miskeenan wayateeman waaseeran

    Na huwalisha chakula, juu ya kukipenda kwake, masikini, na yatima, na wafungwa.8

    Maelezo
    [8] Na huwalisha chakula mafakiri wasio weza kazi, na watoto walio fiwa na wazee wao, na wafungwa wasio miliki kitu, ijapo kuwa wao wenyewe hao watoaji wanakipenda hicho wanacho kitoa, na wanakihitajia.
  9. إِنَّمَا نُطْعِمُكُمْ لِوَجْهِ ٱللَّهِ لَا نُرِيدُ مِنكُمْ جَزَآءً وَلَا شُكُورًا۝٩

    Innama nutʿimukum liwajhi Allahi la nureedu minkum jazaan wala shukooran

    Hakika sisi tunakulisheni kwa wajihi wa Mwenyezi Mungu. Hatutaki kwenu malipo wala shukrani.9

    Maelezo
    [9] Na hujiambia nafsi zao: Hakika sisi tunakulisheni kwa ajili ya kutaka thawa;bu za Mwenyezi Mungu. Sisi hatutaki kwenu malipo au zawadi, wala hatutaki kushukuriwa na kusifiwa.
  10. إِنَّا نَخَافُ مِن رَّبِّنَا يَوْمًا عَبُوسًا قَمْطَرِيرًا۝١٠

    Inna nakhafu min rabbina yawman ʿaboosan qamtareeran

    Hakika sisi tunaiogopa kwa Mola wetu Mlezi hiyo siku yenye shida na taabu.10

    Maelezo
    [10] Hakika sisi tunakhofu kwa Mola wetu Mlezi hiyo siku ya kumletea msiba atakaye kuwapo siku hiyo, na siku ya watu kukunja nyuso zao na vipaji vyao.
  11. فَوَقَىٰهُمُ ٱللَّهُ شَرَّ ذَٰلِكَ ٱلْيَوْمِ وَلَقَّىٰهُمْ نَضْرَةً وَسُرُورًا۝١١

    Fawaqahumu Allahu sharra thalika alyawmi walaqqahum nadratan wasurooran

    Basi Mwenyezi Mungu atwalinda na shari ya siku hiyo, na atawakutanisha na raha na furaha.11

    Maelezo
    [11] Basi Mwenyezi Mungu akawalinda na shida za siku hiyo, na badala ya mkunjo wa wenye maasi, akawapa nyuso za kupendeza, na ukunjufu na furaha katika nyoyo zao,
  12. وَجَزَىٰهُم بِمَا صَبَرُوا۟ جَنَّةً وَحَرِيرًا۝١٢

    Wajazahum bima sabaroo jannatan wahareeran

    Na atawajazi Bustani za Peponi na maguo ya hariri kwa vile walivyo subiri.12

    Maelezo
    [12] Na akawajazi kwa ile subira yao Pepo imeenea furaha, na nguo zake ni hariri laini.
  13. مُّتَّكِـِٔينَ فِيهَا عَلَى ٱلْأَرَآئِكِ ۖ لَا يَرَوْنَ فِيهَا شَمْسًا وَلَا زَمْهَرِيرًا۝١٣

    Muttakieena feeha ʿala alaraiki la yarawna feeha shamsan wala zamhareeran

    Humo wataegemea juu ya viti vya enzi, hawataona humo jua kali wala baridi kali.13

    Maelezo
    [13] Wakiegemea huko Peponi juu ya makochi, hawaoni joto la jua, wala shida ya baridi.
  14. وَدَانِيَةً عَلَيْهِمْ ظِلَـٰلُهَا وَذُلِّلَتْ قُطُوفُهَا تَذْلِيلًا۝١٤

    Wadaniyatan ʿalayhim thilaluha wathullilat qutoofuha tathleelan

    Na vivuli vyake vitakuwa karibu yao, na mashada ya matunda yataning'inia mpaka chini.14

    Maelezo
    [14] Na Pepo ambayo vivuli vya miti yake vimeenea kote kote, na matunda yake mepesi kuyachuma.
  15. وَيُطَافُ عَلَيْهِم بِـَٔانِيَةٍ مِّن فِضَّةٍ وَأَكْوَابٍ كَانَتْ قَوَارِيرَا۠۝١٥

    Wayutafu ʿalayhim bianiyatin min fiddatin waakwabin kanat qawareera

    Na watapitishiwa vyombo vya fedha na vikombe vya vigae,15

    Maelezo
    [15] Na wakiwazungukia watumishi wao kwa bilauri za kunywea zilio fanywa kwa fedha, lakini unaona kiliomo ndani kama kwamba ni kigae,
  16. قَوَارِيرَا۟ مِن فِضَّةٍ قَدَّرُوهَا تَقْدِيرًا۝١٦

    Qawareera min fiddatin qaddarooha taqdeeran

    Vya fedha safi kama kiyoo, wamevipima kwa vipimo.16

    Maelezo
    [16] Na vinapimwa vinywaji kwa kadiri wanavyo penda wanywaji.
  17. وَيُسْقَوْنَ فِيهَا كَأْسًا كَانَ مِزَاجُهَا زَنجَبِيلًا۝١٧

    Wayusqawna feeha kasan kana mizajuha zanjabeelan

    Na humo watanyweshwa kinywaji kilicho changanyika na tangawizi.17

    Maelezo
    [17] Na watu wema hupewa kunywa huko Peponi mvinyo inayo fanana na sharubati ya tangawizi kwa utamu.
  18. عَيْنًا فِيهَا تُسَمَّىٰ سَلْسَبِيلًا۝١٨

    ʿAynan feeha tusamma salsabeelan

    Hiyo ni chemchem iliyo humo inaitwa Salsabil.18

    Maelezo
    [18] Hiyo ni kutokana na chemchem ya Peponi inayo itwa Salsabil, kwa sababu ya wepesi wa unywaji wake na uzuri wake.
  19. ۞ وَيَطُوفُ عَلَيْهِمْ وِلْدَٰنٌ مُّخَلَّدُونَ إِذَا رَأَيْتَهُمْ حَسِبْتَهُمْ لُؤْلُؤًا مَّنثُورًا۝١٩

    Wayatoofu ʿalayhim wildanun mukhalladoona itha raaytahum hasibtahum luluan manthooran

    Na watawazungukia kuwatumikia wavulana wasio pevuka, ukiwaona utawafikiri ni lulu zilizo tawanywa.19

    Maelezo
    [19] Na watakuwa wanawazunguka vijana ambao hawabadiliki hali yao, kwa furaha na sururi. Ukiwaona wanapo zunguka kwa wepesi na uchangamfu, utawadhania kwa uzuri wao na usafi wa rangi zao, kama lulu zilizo tandazwa mbele yako zinang'ara.
  20. وَإِذَا رَأَيْتَ ثَمَّ رَأَيْتَ نَعِيمًا وَمُلْكًا كَبِيرًا۝٢٠

    Waitha raayta thamma raayta naʿeeman wamulkan kabeeran

    Na utakapo yaona, utakuwa umeona neema na ufalme mkubwa.20

    Maelezo
    [20] Na ukitazama popote katika hiyo Pepo utaona neema kubwa, na ufalme ulio tanda.
  21. عَـٰلِيَهُمْ ثِيَابُ سُندُسٍ خُضْرٌ وَإِسْتَبْرَقٌ ۖ وَحُلُّوٓا۟ أَسَاوِرَ مِن فِضَّةٍ وَسَقَىٰهُمْ رَبُّهُمْ شَرَابًا طَهُورًا۝٢١

    ʿaliyahum thiyabu sundusin khudrun waistabraqun wahulloo asawira min fiddatin wasaqahum rabbuhum sharaban tahooran

    Juu yao zipo nguo za hariri laini za kijani kibichi, na hariri nzito ya at'ilasi. Na watavikwa vikuku vya fedha, na Mola wao Mlezi atawanywesha kinywaji safi kabisa.21

    Maelezo
    [21] Juu yao zipo nguo za hariri nyepesi za kijani, na nguo za hariri nzito. Na mapambo yao yaliomo mikononi mwao ni vikuku vya fedha. Na Mola wao Mlezi atawanywesha kinywaji kingine kilio safi, hakina uchafu wala najisi.
  22. إِنَّ هَـٰذَا كَانَ لَكُمْ جَزَآءً وَكَانَ سَعْيُكُم مَّشْكُورًا۝٢٢

    Inna hatha kana lakum jazaan wakana saʿyukum mashkooran

    Hakika haya ni malipo yenu; na juhudi zenu zimekubaliwa.22

    Maelezo
    [22] Hakika neema hizi ameziandaa kwa kukulipeni kwa vitendo vyenu. Na hizo juhudi zenu duniani ni zenye kusifika kwa Mwenyezi Mungu, na zinampendeza, na zimekubaliwa.
  23. إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا عَلَيْكَ ٱلْقُرْءَانَ تَنزِيلًا۝٢٣

    Inna nahnu nazzalna ʿalayka alqurana tanzeelan

    Hakika Sisi tumekuteremshia Qur'ani kidogo kidogo.23

    Maelezo
    [23] Hakika Sisi, kwa rehema yetu na hikima yetu, tumekuteremshia wewe Qur'ani kwa njia ya kukutuza moyo wako, na uweze daima kuihifadhi, basi huto isahau kabisa.
  24. فَٱصْبِرْ لِحُكْمِ رَبِّكَ وَلَا تُطِعْ مِنْهُمْ ءَاثِمًا أَوْ كَفُورًا۝٢٤

    Faisbir lihukmi rabbika wala tutiʿ minhum athiman aw kafooran

    Basi ngojea hukumu ya Mola wako Mlezi wala usimt'ii miongoni mwao mwenye dhambi au mwenye kufuru.24

    Maelezo
    [24] Basi subiri, uivumilie hikima ya Mola wako Mlezi kwa kuakhirisha kushinda kwako kuwashinda maadui zako, na wewe ukapata mitihani kwa maudhi yao. Wala usiwat'ii washirikina, wingi wa madhambi, walio zama katika ukafiri.
  25. وَٱذْكُرِ ٱسْمَ رَبِّكَ بُكْرَةً وَأَصِيلًا۝٢٥

    Waothkuri isma rabbika bukratan waaseelan

    Na likumbuke jina la Mola wako Mlezi asubuhi na jioni;25

    Maelezo
    [25] Na dumisha kumkumbuka na kumtaja Mola wako Mlezi, na sali alfajiri mapema, na adhuhuri, na alasiri jioni,
  26. وَمِنَ ٱلَّيْلِ فَٱسْجُدْ لَهُۥ وَسَبِّحْهُ لَيْلًا طَوِيلًا۝٢٦

    Wamina allayli faosjud lahu wasabbihhu laylan taweelan

    Na usiku msujudie Yeye, na umtakase usiku, wakati mrefu.26

    Maelezo
    [26] Na usiku sali magharibi na isha. Na fanya ibada za usiku kwa muda mrefu.
  27. إِنَّ هَـٰٓؤُلَآءِ يُحِبُّونَ ٱلْعَاجِلَةَ وَيَذَرُونَ وَرَآءَهُمْ يَوْمًا ثَقِيلًا۝٢٧

    Inna haolai yuhibboona alʿajilata wayatharoona waraahum yawman thaqeelan

    Kwa hakika watu hawa wanapenda maisha ya kidunia, na wanaiacha nyuma yao siku nzito.27

    Maelezo
    [27] Hakika hawa makafiri wanaipenda dunia, na wanaifadhilisha kuliko Akhera. Na wanaiacha migongoni mwao siku yenye misiba mikubwa, na vitisho vikali. Wala wao hawajui nini cha kuwaokoa wao na hayo!
  28. نَّحْنُ خَلَقْنَـٰهُمْ وَشَدَدْنَآ أَسْرَهُمْ ۖ وَإِذَا شِئْنَا بَدَّلْنَآ أَمْثَـٰلَهُمْ تَبْدِيلًا۝٢٨

    Nahnu khalaqnahum washadadna asrahum waitha shina baddalna amthalahum tabdeelan

    Sisi tumewaumba, na tukavitia nguvu viungo vyao. Na tukitaka tutawabadilisha mfano wao wawe badala yao.28

    Maelezo
    [28] Sisi tumewaumba wao, na tumefanya kwa hikima kuumbwa kwao. Na tukitaka tutawateketeza wao na tutawaleta mfano ya wao badala yao, ambao hao watakuja kumt'ii Mwenyezi Mungu kinyume na wao.
  29. إِنَّ هَـٰذِهِۦ تَذْكِرَةٌ ۖ فَمَن شَآءَ ٱتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِۦ سَبِيلًا۝٢٩

    Inna hathihi tathkiratun faman shaa ittakhatha ila rabbihi sabeelan

    Hakika haya ni mawaidha; basi anaye taka atashika Njia ya kwenda kwa Mola wake Mlezi.29

    Maelezo
    [29] Hakika Sura hii ni mawaidha kwa walimwengu wote. Basi mwenye kutaka atafuata njia ya Imani na uchamngu kwendea kwa Mola wake Mlezi imfikishe kwenye maghfira yake na Pepo yake.
  30. وَمَا تَشَآءُونَ إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًا۝٣٠

    Wama tashaoona illa an yashaa Allahu inna Allaha kana ʿaleeman hakeeman

    Wala hamwezi kutaka ila atakapo Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye ilimu, Mwenye hikima.30

    Maelezo
    [30] Wala nyinyi hamwezi kutaka kitu chochote ila wakati anapo taka Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuzijua hali zenu, Mwenye hikima kwa anayo yataka na akayakhiari.
  31. يُدْخِلُ مَن يَشَآءُ فِى رَحْمَتِهِۦ ۚ وَٱلظَّـٰلِمِينَ أَعَدَّ لَهُمْ عَذَابًا أَلِيمًۢا۝٣١

    Yudkhilu man yashao fee rahmatihi waalththalimeena aʿadda lahum ʿathaban aleeman

    Humuingiza amtakaye katika rehema yake. Na wenye kudhulumu amewawekea adhabu iliyo chungu.31

    Maelezo
    [31] Humuingiza amtakaye katika Pepo yake. Basi kuingia Peponi ni kwa fadhila na rehema ya Mwenyezi Mungu. Naye amewadhalilisha wenye kudhulumu, amewatengenezea adhabu iliyo chungu.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Surat Al-Insan maana yake ni nini?

Al-Insan maana yake ni “Mwanadamu”.

Surat Al-Insan iko katika juzuu ya ngapi?

Surat Al-Insan iko katika juzuu ya 29.

Surat Al-Insan ina aya ngapi?

Surat Al-Insan ina aya 31.

Surat Al-Insan ni ya Makka au ya Madina?

Surat Al-Insan ni sura ya Madina.

Surat Al-Insan ni sura ya ngapi katika Qur’ani?

Ni sura ya 76 katika Qur’ani.

Vyanzo

  • Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
  • Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
  • Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
  • Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
  • Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
  • Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.

Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.

Mipangilio ya kusoma

Fonti ya Qur’ani
Ukubwa wa Kiarabu
100%
Ukubwa wa tafsiri
100%
Mandhari

Ongeza kwenye skrini ya kwanza

ReadSurahFungua ReadSurah kutoka skrini ya kwanza, kwa skrini nzima. Sura ulizosoma hufunguka hata bila intaneti.

  1. Katika Safari, gusa kitufe cha kushiriki (Share). Kwenye iPhone mpya kiko kwenye menyu ya •••.
  2. Gusa “Add to Home Screen”. Huenda ukahitaji kusogeza chini.
  3. Gusa “Add”.