سورة المرسلات

Surat Al-Mursalat kwa Kiswahili

Wajumbe

Msahafu

Mishary Rashid AlafasyPakua MP3Pakua PDF

Surat Al-Mursalat (المرسلات) ni sura ya 77 katika Qur’ani na ina aya 50. Jina lake lina maana ya “Wajumbe”. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na iko katika juzuu ya 29.

Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat Al-Mursalat yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.

Surat Al-Mursalat kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

  1. وَٱلْمُرْسَلَـٰتِ عُرْفًا۝١

    Waalmursalati ʿurfan

    Naapa kwa zinazo tumwa kwa upole!1

    Maelezo
    [1] Naapa kwa Aya zilizo tumwa kwa ulimi wa Jibrili kumpelekea Muhammad kwa upole wa kawaida na kheri,
  2. فَٱلْعَـٰصِفَـٰتِ عَصْفًا۝٢

    Faalʿasifati ʿasfan

    Na zinazo vuma kwa kasi!2

    Maelezo
    [2] Na kwa Aya zenye kuzitwaa kwa nguvu dini nyengine zote za uwongo zikizipeperushia mbali,
  3. وَٱلنَّـٰشِرَٰتِ نَشْرًا۝٣

    Waalnnashirati nashran

    Na zikaeneza maeneo yote!3

    Maelezo
    [3] Na kwa Aya zenye kueneza hikima na uwongofu katika nyoyo za walimwengu kwa uenezi mkubwa mno,
  4. فَٱلْفَـٰرِقَـٰتِ فَرْقًا۝٤

    Faalfariqati farqan

    Na zinazo farikisha zikatawanya!4

    Maelezo
    [4] Na zenye kufarikisha baina ya kweli na uwongo kwa mfarakano ulio wazi kabisa,
  5. فَٱلْمُلْقِيَـٰتِ ذِكْرًا۝٥

    Faalmulqiyati thikran

    Na zinazo peleka mawaidha!5

    Maelezo
    [5] Na zenye kuwapa watu mawaidha ya kuwanufaisha,
  6. عُذْرًا أَوْ نُذْرًا۝٦

    ʿUthran aw nuthran

    Kwa kuudhuru au kuonya,6

    Maelezo
    [6] Ili iwe ni udhuru kwao na onyo wasiwe na hoja,
  7. إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَوَٰقِعٌ۝٧

    Innama tooʿadoona lawaqiʿun

    Hakika mnayo ahidiwa bila ya shaka yatakuwa!7

    Maelezo
    [7] Hakika haya mliyo ahidiwa ya kuja Kiyama kwa yakini yatatimia tu bila ya shaka yoyote.
  8. فَإِذَا ٱلنُّجُومُ طُمِسَتْ۝٨

    Faitha alnnujoomu tumisat

    Wakati nyota zitakapo futwa,8

    Maelezo
    [8] Basi nyota zitapo ondolewa kabisa,
  9. وَإِذَا ٱلسَّمَآءُ فُرِجَتْ۝٩

    Waitha alssamao furijat

    Na mbingu zitakapo pasuliwa,9

    Maelezo
    [9] Na mbingu zitapo pasuka,
  10. وَإِذَا ٱلْجِبَالُ نُسِفَتْ۝١٠

    Waitha aljibalu nusifat

    Na milima itakapo peperushwa,10

    Maelezo
    [10] Na milima ikavurugwa na ikapeperushiwa mbali na upepo,
  11. وَإِذَا ٱلرُّسُلُ أُقِّتَتْ۝١١

    Waitha alrrusulu oqqitat

    Na Mitume watakapo wekewa wakati wao,11

    Maelezo
    [11] Na Mitume wakawekewa wakati maalumu wahudhurie kwa ajili ya kuwatolea ushahidi kaumu zao.
  12. لِأَىِّ يَوْمٍ أُجِّلَتْ۝١٢

    Liayyi yawmin ojjilat

    Kwa siku gani hiyo wamewekewa muda huo?12

    Maelezo
    [12] Kwa ajili ya siku gani yametayarishwa mambo haya makubwa makubwa?
  13. لِيَوْمِ ٱلْفَصْلِ۝١٣

    Liyawmi alfasli

    Kwa siku ya kupambanua!13

    Maelezo
    [13] Kwa ajili ya siku watakapo pambanuliwa baina ya viumbe.
  14. وَمَآ أَدْرَىٰكَ مَا يَوْمُ ٱلْفَصْلِ۝١٤

    Wama adraka ma yawmu alfasli

    Na nini kitakacho kujuulisha siku ya kupambanua ni nini?14

    Maelezo
    [14] Na nini cha kukujuvya ina nini hiyo siku ya kupambanua?
  15. وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ۝١٥

    Waylun yawmaithin lilmukaththibeena

    Ole wao, siku hiyo hao wanao kanusha!15

    Maelezo
    [15] Ni maangamio ya milele siku hiyo kwa hao wanao kadhibisha walio waahidi Mitume!
  16. أَلَمْ نُهْلِكِ ٱلْأَوَّلِينَ۝١٦

    Alam nuhliki alawwaleena

    Kwani hatukuwaangamiza walio tangulia?16

    Maelezo
    [16] Kwani hatukuwaangamiza mataifa ya zamani yaliyo kadhibisha,
  17. ثُمَّ نُتْبِعُهُمُ ٱلْـَٔاخِرِينَ۝١٧

    Thumma nutbiʿuhumu alakhireena

    Kisha tukawafuatilizia walio fuatia?17

    Maelezo
    [17] Na kisha tukawafuatilizia hao wenginewe tukawateketeza hali kadhaalika,
  18. كَذَٰلِكَ نَفْعَلُ بِٱلْمُجْرِمِينَ۝١٨

    Kathalika nafʿalu bialmujrimeena

    Ndio kama hivi tuwatendavyo wakosefu!18

    Maelezo
    [18] Kwa madhambi waliyo yafanya na walivyo mkataa Mwenyezi Mungu?
  19. وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ۝١٩

    Waylun yawmaithin lilmukaththibeena

    Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!19

    Maelezo
    [19] Siku hiyo ni siku ya kuteketezwa walio kadhibisha, kama tulivyo waahidi.
  20. أَلَمْ نَخْلُقكُّم مِّن مَّآءٍ مَّهِينٍ۝٢٠

    Alam nakhluqkum min main maheenin

    Kwani hatukukuumbeni kwa maji ya kudharauliwa?20

    Maelezo
    [20] Kwani hatukukuumbeni kutokana na maji yaliyo dhalili, nayo ni manii,
  21. فَجَعَلْنَـٰهُ فِى قَرَارٍ مَّكِينٍ۝٢١

    Fajaʿalnahu fee qararin makeenin

    Kisha tukayaweka mahali pa utulivu madhubuti?21

    Maelezo
    [21] Na tukayaweka maji haya katika pahala patulivu,
  22. إِلَىٰ قَدَرٍ مَّعْلُومٍ۝٢٢

    Ila qadarin maʿloomin

    Mpaka muda maalumu?22

    Maelezo
    [22] Mpaka kutimilia kuumbwa kwake na kutengenezwa kwake kwa muda anao ujua Mwenyezi Mungu.
  23. فَقَدَرْنَا فَنِعْمَ ٱلْقَـٰدِرُونَ۝٢٣

    Faqadarna faniʿma alqadiroona

    Tukakadiria na Sisi ni wabora wa kukadiria.23

    Maelezo
    [23] Nasi tukaweka vipimo katika kuumbwa kwake, na kutengenezwa kwake, na kutoka kwake. Basi wabora wa kupima na kukadiria ni Sisi.
  24. وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ۝٢٤

    Waylun yawmaithin lilmukaththibeena

    Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!24

    Maelezo
    [24] Ole wao hao wanao kadhibisha neema za kuumba na kukadiria.
  25. أَلَمْ نَجْعَلِ ٱلْأَرْضَ كِفَاتًا۝٢٥

    Alam najʿali alarda kifatan

    Kwani hatukuifanya ardhi yenye kukusanya25

    Maelezo
    [25] Kwani hatukuifanya ardhi kuwa imekusanya juu ya mgongo wake
  26. أَحْيَآءً وَأَمْوَٰتًا۝٢٦

    Ahyaan waamwatan

    Walio hai na maiti?26

    Maelezo
    [26] Viumbe vilivyo hai visio hisabika, na vilio kufa visio kadirika,
  27. وَجَعَلْنَا فِيهَا رَوَٰسِىَ شَـٰمِخَـٰتٍ وَأَسْقَيْنَـٰكُم مَّآءً فُرَاتًا۝٢٧

    Wajaʿalna feeha rawasiya shamikhatin waasqaynakum maan furatan

    Na ndani yake tukaweka milima mirefu yenye kuthibiti, na tunakunywesheni maji matamu?27

    Maelezo
    [27] Na tukaweka milima iliyo thibiti imara mirefu, na tukakunywesheni maji matamu?
  28. وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ۝٢٨

    Waylun yawmaithin lilmukaththibeena

    Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!28

    Maelezo
    [28] Wataangamia siku hiyo hao wanao kadhibisha neema hizi!
  29. ٱنطَلِقُوٓا۟ إِلَىٰ مَا كُنتُم بِهِۦ تُكَذِّبُونَ۝٢٩

    Intaliqoo ila ma kuntum bihi tukaththiboona

    Nendeni kwenye adhabu mliyo kuwa mkiikanusha!29

    Maelezo
    [29] Siku ya kupambanua wataambiwa makafiri: Nendeni huko Motoni mliko kuwa mkikukanusha.
  30. ٱنطَلِقُوٓا۟ إِلَىٰ ظِلٍّ ذِى ثَلَـٰثِ شُعَبٍ۝٣٠

    Intaliqoo ila thillin thee thalathi shuʿabin

    Nendeni kwenye kivuli chenye mapande matatu!30

    Maelezo
    [30] Nendeni kwenye joto la moshi wa Jahannamu ulio gawika kwa ukubwa wake mapande matatu.
  31. لَّا ظَلِيلٍ وَلَا يُغْنِى مِنَ ٱللَّهَبِ۝٣١

    La thaleelin wala yughnee mina allahabi

    Hakikingi moto, wala hakiwaepushi na mwako.31

    Maelezo
    [31] Hapana cha kujikinga na joto la siku hiyo, wala kivuli hicho hakipunguzi joto la mwako hata kidogo.
  32. إِنَّهَا تَرْمِى بِشَرَرٍ كَٱلْقَصْرِ۝٣٢

    Innaha tarmee bishararin kaalqasri

    Hakika Moto huo unatoa macheche kama majumba!32

    Maelezo
    [32] Moto huo hutupa macheche yenye ukubwa kama majumba,
  33. كَأَنَّهُۥ جِمَـٰلَتٌ صُفْرٌ۝٣٣

    Kaannahu jimalatun sufrun

    Kama kwamba ni ngamia wa rangi ya manjano!33

    Maelezo
    [33] Au utaona hayo macheche kama ngamia weusi wenye kuingia rangi ya manjano.
  34. وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ۝٣٤

    Waylun yawmaithin lilmukaththibeena

    Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!34

    Maelezo
    [34] Wataangamia siku hiyo wanao kanusha kwamba hizi ndizo sifa za Moto.
  35. هَـٰذَا يَوْمُ لَا يَنطِقُونَ۝٣٥

    Hatha yawmu la yantiqoona

    Hii ni siku ambayo hawatatamka kitu,35

    Maelezo
    [35] Haya uliyo simuliwa yatatokea katika siku ambayo hawatatamka kitu cha kuwanufaisha,
  36. وَلَا يُؤْذَنُ لَهُمْ فَيَعْتَذِرُونَ۝٣٦

    Wala yuthanu lahum fayaʿtathiroona

    Wala hawataruhusiwa kutoa udhuru.36

    Maelezo
    [36] Wala hawatakuwa na idhini ya kutamka, wala hawatatoa udhuru, kwani hawana udhuru.
  37. وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ۝٣٧

    Waylun yawmaithin lilmukaththibeena

    Ole wao siku hiyo hao walio kanusha!37

    Maelezo
    [37] Wataangamia siku hiyo wanayo ikadhibisha siku hii.
  38. هَـٰذَا يَوْمُ ٱلْفَصْلِ ۖ جَمَعْنَـٰكُمْ وَٱلْأَوَّلِينَ۝٣٨

    Hatha yawmu alfasli jamaʿnakum waalawwaleena

    Hii ndiyo siku ya kupambanua. Tumekukusanyeni nyinyi na walio tangulia.38

    Maelezo
    [38] Hii ndiyo siku ya kufafanua baina ya mwenye ukweli, na mwenye uwongo, kwa kuwa kila mmoja atalipwa kwa mujibu wa anavyo stahiki. Enyi mnao mkadhibisha Muhammad! Tumekujaalieni nyinyi na walio kutangulieni walio kadhibisha mfano wenu,
  39. فَإِن كَانَ لَكُمْ كَيْدٌ فَكِيدُونِ۝٣٩

    Fain kana lakum kaydun fakeedooni

    kiwa mnayo hila, nifanyieni hila Mimi!39

    Maelezo
    [39] Kama mnayo hila ya kujikinga na adhabu basi fanyeni hila hiyo. Basi njooni muepukane na adhabu yangu.
  40. وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ۝٤٠

    Waylun yawmaithin lilmukaththibeena

    Ole wao siku hiyo hao walio kanusha!40

    Maelezo
    [40] Wataangamia siku hiyo wanayo ikadhibisha ahadi ya Mwenyezi Mungu.
  41. إِنَّ ٱلْمُتَّقِينَ فِى ظِلَـٰلٍ وَعُيُونٍ۝٤١

    Inna almuttaqeena fee thilalin waʿuyoonin

    Hakika wachamngu watakuwa katika vivuli na chemchem,41

    Maelezo
    [41] Hakika wachamngu wenye kujikinga na adhabu ya Mwenyezi Mungu watakuwa katika kivuli kikubwa, na chemchem zinazo miminika,
  42. وَفَوَٰكِهَ مِمَّا يَشْتَهُونَ۝٤٢

    Wafawakiha mimma yashtahoona

    Na matunda wanayo yapenda,42

    Maelezo
    [42] Na matunda wanayo yaonea ladha, na wanayo yapenda,
  43. كُلُوا۟ وَٱشْرَبُوا۟ هَنِيٓـًٔۢا بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ۝٤٣

    Kuloo waishraboo haneean bima kuntum taʿmaloona

    Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa yale mliyo kuwa mkiyatenda.43

    Maelezo
    [43] Wataambiwa kwa kuamkiwa na kukirimiwa: Kuleni na mnywe chakula na vinywaji kwa starehe kwa sababu ya vitendo vyema mlivyo kuwa mkivitenda duniani.
  44. إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلْمُحْسِنِينَ۝٤٤

    Inna kathalika najzee almuhsineena

    Hakika ndio kama hivyo tunavyo walipa watendao mema.44

    Maelezo
    [44] Hakika Sisi huwalipa mfano wa malipo hayo matukufu watu wema.
  45. وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ۝٤٥

    Waylun yawmaithin lilmukaththibeena

    Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!45

    Maelezo
    [45] Wataangamia siku hiyo wanayo ikadhibisha Pepo.
  46. كُلُوا۟ وَتَمَتَّعُوا۟ قَلِيلًا إِنَّكُم مُّجْرِمُونَ۝٤٦

    Kuloo watamattaʿoo qaleelan innakum mujrimoona

    Kuleni na mjifurahishe kidogo tu. Hakika nyinyi ni wakosefu!46

    Maelezo
    [46] Na makafiri wataambiwa: Kuleni na mjistareheshe kwa starehe isiyo baki muda mrefu, kwani hakika nyinyi ni wakosefu kwa kumshirikisha kwenu Mwenyezi Mungu.
  47. وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ۝٤٧

    Waylun yawmaithin lilmukaththibeena

    Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!47

    Maelezo
    [47] Wataangamia siku hiyo wanao ikadhibisha neema.
  48. وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ٱرْكَعُوا۟ لَا يَرْكَعُونَ۝٤٨

    Waitha qeela lahumu irkaʿoo la yarkaʿoona

    Na wakiambiwa: Inameni! Hawainami.48

    Maelezo
    [48] Na wakiambiwa: Swalini kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na mnyenyekeeni Yeye, hawanyenyekei wala hawaswali; bali hushikilia kiburi chao!
  49. وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ۝٤٩

    Waylun yawmaithin lilmukaththibeena

    Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!49

    Maelezo
    [49] Wataangamia siku wanao kadhibisha amri za Mwenyezi Mungu na makatazo yake.
  50. فَبِأَىِّ حَدِيثٍۭ بَعْدَهُۥ يُؤْمِنُونَ۝٥٠

    Fabiayyi hadeethin baʿdahu yuminoona

    Basi maneno gani baada ya haya watayaamini?50

    Maelezo
    [50] Basi maneno gani hawa watayaamini ikiwa hawaiamini Qur'ani, na hali hii ni muujiza ulio toka mbinguni?

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Surat Al-Mursalat maana yake ni nini?

Al-Mursalat maana yake ni “Wajumbe”.

Surat Al-Mursalat iko katika juzuu ya ngapi?

Surat Al-Mursalat iko katika juzuu ya 29.

Surat Al-Mursalat ina aya ngapi?

Surat Al-Mursalat ina aya 50.

Surat Al-Mursalat ni ya Makka au ya Madina?

Surat Al-Mursalat ni sura ya Makka.

Surat Al-Mursalat ni sura ya ngapi katika Qur’ani?

Ni sura ya 77 katika Qur’ani.

Vyanzo

  • Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
  • Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
  • Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
  • Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
  • Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
  • Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.

Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.

Mipangilio ya kusoma

Fonti ya Qur’ani
Ukubwa wa Kiarabu
100%
Ukubwa wa tafsiri
100%
Mandhari

Ongeza kwenye skrini ya kwanza

ReadSurahFungua ReadSurah kutoka skrini ya kwanza, kwa skrini nzima. Sura ulizosoma hufunguka hata bila intaneti.

  1. Katika Safari, gusa kitufe cha kushiriki (Share). Kwenye iPhone mpya kiko kwenye menyu ya •••.
  2. Gusa “Add to Home Screen”. Huenda ukahitaji kusogeza chini.
  3. Gusa “Add”.