Surat An-Naba (النبإ) ni sura ya 78 katika Qur’ani na ina aya 40. Jina lake lina maana ya “Habari Kuu”. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na iko katika juzuu ya 30.
Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat An-Naba yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.
Surat An-Naba kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
-
عَمَّ يَتَسَآءَلُونَ١
ʿAmma yatasaaloona
WANAULIZANA nini?1
Maelezo
[1] Wanaulizana nini hao makafiri? -
عَنِ ٱلنَّبَإِ ٱلْعَظِيمِ٢
ʿAni alnnabai alʿatheemi
Ile khabari kuu!2
Maelezo
[2] Wanaulizana khabari kubwa, khabari ya kufufuliwa, -
ٱلَّذِى هُمْ فِيهِ مُخْتَلِفُونَ٣
Allathee hum feehi mukhtalifoona
Ambayo kwayo wanakhitalifiana.3
Maelezo
[3] Ambayo wao wamezama ndani yake kukhitalifiana baina ya wenye kuikataa na wenye kuitilia shaka. -
كَلَّا سَيَعْلَمُونَ٤
Kalla sayaʿlamoona
La! Karibu watakuja jua.4
Maelezo
[4] Kuwazuia kuulizana huko wanaambiwa kuwa watakuja ujua ukweli wa mambo hapo watapo ona kufufuliwa kumetokea khasa. -
ثُمَّ كَلَّا سَيَعْلَمُونَ٥
Thumma kalla sayaʿlamoona
Tena la! Karibu watakuja jua.5
Maelezo
[5] Tena kuwazuia, watakuja jua itapo wateremkia adhabu. -
أَلَمْ نَجْعَلِ ٱلْأَرْضَ مِهَـٰدًا٦
Alam najʿali alarda mihadan
kaKwani hatukuifanya ardhi ma tandiko?6
Maelezo
[6] Kwani wao hawaoni Ishara za uweza wetu kwamba Sisi tumeifanya ardhi imetandikwa upatikane utulivu juu yake na iwezekane kutembea juu yake? -
وَٱلْجِبَالَ أَوْتَادًا٧
Waaljibala awtadan
kama Na milima vigingi?7
Maelezo
[7] Na tukaifanya milima ni vigingi vya ardhi vya kuituliza? Sehemu ya gamba gumu lilio juu ya ardhi linfikilia kiasi ya kilomita 60 unene wake, na inazidi mikunjo, mifimbi, inapanda juu kuwa milima, na huteremka chini kuwa ni vina vya bahari; na hiyo hulingana kwa sababu ya uzito unao patikana kutokana na milima. Na kulingana huko hakuharibiki ila kwa kubugunyika, kwani gamba kavu la ardhi linazuiliwa na milima, kama vigingi vinavyo zuilia khema. (Rejea Maoni ya Wataalamu juu ya Aya 7 ya Surat Qaf). -
وَخَلَقْنَـٰكُمْ أَزْوَٰجًا٨
Wakhalaqnakum azwajan
Na tukakuumbeni kwa jozi?8
Maelezo
[8] Na tukakuumbeni kwa jozi, wanaume na wanawake? -
وَجَعَلْنَا نَوْمَكُمْ سُبَاتًا٩
Wajaʿalna nawmakum subatan
Na tukakufanya kulala kwenu ni mapumziko?9
Maelezo
[9] Na tukafanya kulala kwenu ni mapumziko ya machofu ya kazi? Kulala usingizi ni kusita nishat'i ya sehemu ya ubongo yenye kutambua na kuwa macho. Yaani gamba la ubongo, au kupunguka nishat'i yake kwa wingi, ukilinganisha na daraja za nishat'i ya sehemu za viungo vilio baki. Na kwa hivyo kunapunguka nguvu na joto la mwili, tena mwili hapo wakati wa usingizi hupata kutua na kupumzika baada ya kuhangaika viungo au akili au vyote viwili. Basi kazi za kimwili zote hupunguka isipo kuwa kazi za kusaga chakula, na kupitisha mkojo katika mafigo, na kutoka majasho katika ngozi, kwani yakisita hayo hupatikana madhara juu ya maisha ya mtu. Ama kuvuta pumzi huko nako hupunguka, na huwa ni kwa ndani zaidi, na huwa kwa kifua zaidi kuliko kwa tumbo. Na mpigo wa mishipa hupungua kasi kwa kunavyo tokana na moyo, na hudhoofika mkazano wa musulo (muscular tension), na kwa hivyo huwa taabu kupata harakati za kinyume. Na yote haya ni ili binaadamu apate kupumzika wakati wa kulala. -
وَجَعَلْنَا ٱلَّيْلَ لِبَاسًا١٠
Wajaʿalna allayla libasan
Na tukaufanya usiku ni nguo?10
Maelezo
[10] Na tumeufanya usiku ni sitara kwenu kwa kiza kinacho kufunikeni. -
وَجَعَلْنَا ٱلنَّهَارَ مَعَاشًا١١
Wajaʿalna alnnahara maʿashan
Na tukaufanya mchana ni wa kuchumia maisha?11
Maelezo
[11] Na tumeufanya mchana ni wakati wa kuhangaika kwenu kutafuta cha kukusaidieni katika maisha yenu. -
وَبَنَيْنَا فَوْقَكُمْ سَبْعًا شِدَادًا١٢
Wabanayna fawqakum sabʿan shidadan
Na tukajenga juu yenu saba zenye nguvu?12
Maelezo
[12] Na tumesimamisha juu yenu mbingu saba zenye nguvu madhubuti. -
وَجَعَلْنَا سِرَاجًا وَهَّاجًا١٣
Wajaʿalna sirajan wahhajan
Na tukaifanya taa yenye mwanga na joto;13
Maelezo
[13] Na Sisi tumeliumba jua lenye mwangaza na linalo waka. Makusudio ya Assiraj Alwahhaaj, Taa yenye mwanga na joto, ni Jua. Na hayo kama ilivyo thibiti katika sayansi kuwa daraja ya joto la uso wake inafika daraja 6000. Ama kati yake daraja yake inazidi daraja 30 milioni kwa sababu ya mdidimizo mkubwa unao patikana juu ya madda ziliomo ndani yake. Na jua linatoa nishat'i hizi zifuatazo: 9 katika 100 ya miale ya Ultraviolet rays, 46 katika 100 ya miale ya mwangaza, 45 katika 100 miale ya joto, au Infra red rays. Na kwa hivyo hii Aya tukufu imeliita kuwa ni Taa yenye mwangaza na joto. -
وَأَنزَلْنَا مِنَ ٱلْمُعْصِرَٰتِ مَآءً ثَجَّاجًا١٤
Waanzalna mina almuʿsirati maan thajjajan
Na tukateremsha maji yanayo anguka kwa kasi kutoka mawinguni,14
Maelezo
[14] Na tumeteremsha kutokana na mawingu yaliyo karibia kunyesha maji yenye kumiminika kwa nguvu. Mvua ndio kitu pekee kinacho toka asli yake maji matamu katika ardhi. Na asli ya mvua ni kukusanyika vijisehemu vya maji yanayo panda kutoka baharini, na maziwa na mito, yakakusanyika kama mawingu na yakageuka chembe za mvua au vipande vya barafu, na khatimaye yakaanguka kwa sura ya mvua au theluji. -
لِّنُخْرِجَ بِهِۦ حَبًّا وَنَبَاتًا١٥
Linukhrija bihi habban wanabatan
Ili tutoe kwayo nafaka na mimea.15
Maelezo
[15] Ili tutoe kwa maji haya nafaka na mimea kuwa ni chakula kwa ajili ya watu na wanyama. -
وَجَنَّـٰتٍ أَلْفَافًا١٦
Wajannatin alfafan
Na mabustani yenye miti iliyo kamatana.16
Maelezo
[16] Na mabustani yenye miti iliyo fungamana na matawi yake yameingiliana. -
إِنَّ يَوْمَ ٱلْفَصْلِ كَانَ مِيقَـٰتًا١٧
Inna yawma alfasli kana meeqatan
Hakika siku ya uamuzi imewekewa wakati wake,17
Maelezo
[17] Hakika siku ya uamuzi baina ya viumbe imewekewa miadi ilio kwisha kadiriwa kwa ajili ya kufufuliwa. -
يَوْمَ يُنفَخُ فِى ٱلصُّورِ فَتَأْتُونَ أَفْوَاجًا١٨
Yawma yunfakhu fee alssoori fatatoona afwajan
Siku litapo pulizwa barugumu, nanyi mtakuja kwa makundi,18
Maelezo
[18] Siku litakapo pulizwa barugumu na kufufuliwa watu, mtakuja kwenye mkutano makundi kwa makundi. -
وَفُتِحَتِ ٱلسَّمَآءُ فَكَانَتْ أَبْوَٰبًا١٩
Wafutihati alssamao fakanat abwaban
Na mbingu zitafunguliwa, ziwe milango.19
Maelezo
[19] Na mbingu zitapasuliwa kila upande hata zitakuwa ni milango milango. -
وَسُيِّرَتِ ٱلْجِبَالُ فَكَانَتْ سَرَابًا٢٠
Wasuyyirati aljibalu fakanat saraban
Na milima itaondolewa na itakuwa kama sarabi.20
Maelezo
[20] Na milima itaondolewa baada ya kung'olewa mwahala mwake, na kuvurugwa, ikawa unaiona kama sura ya milima na hali hiyo ni kifusi tu kilicho rindikwa, kama uonavyo mangati, sarabi, unaona kama sura ya maji nayo si maji. -
إِنَّ جَهَنَّمَ كَانَتْ مِرْصَادًا٢١
Inna jahannama kanat mirsadan
Hakika Jahannamu inangojea!21
Maelezo
[21] Hakika Jahannamu imekuwa kama ni kitu kinacho ngojea, walinzi wake wanawangojea watu watakao kuja kuingia. -
لِّلطَّـٰغِينَ مَـَٔابًا٢٢
Lilttagheena maaban
Kwa walio asi ndio makaazi yao,22
Maelezo
[22] Yawe ni marejeo na mafikio kwa wenye kupindukia mipaka ya Mwenyezi Mungu. -
لَّـٰبِثِينَ فِيهَآ أَحْقَابًا٢٣
Labitheena feeha ahqaban
Wakae humo karne baada ya karne,23
Maelezo
[23] Watakaa humo dahari baada ya dahari. -
لَّا يَذُوقُونَ فِيهَا بَرْدًا وَلَا شَرَابًا٢٤
La yathooqoona feeha bardan wala sharaban
Hawataonja humo chochote kibaridi wala kinywaji,24
Maelezo
[24] Hawataonja humo hata chembe ya upepo wa kuburudisha joto lake, wala kinywaji cha kupoza kiu chao. -
إِلَّا حَمِيمًا وَغَسَّاقًا٢٥
Illa hameeman waghassaqan
Ila maji yamoto sana na usaha,25
Maelezo
[25] Lakini watakunywa maji yalio pita ukomo kwa umoto wake, na usaha unao miminika kutokana na ngozi za watu wa Motoni. -
جَزَآءً وِفَاقًا٢٦
Jazaan wifaqan
Ndio jaza muwafaka.26
Maelezo
[26] Malipo ya kuwafikiana na vitendo vyao viovu. -
إِنَّهُمْ كَانُوا۟ لَا يَرْجُونَ حِسَابًا٢٧
Innahum kanoo la yarjoona hisaban
Hakika hao hawakuwa wakitaraji kuwa kuna hisabu.27
Maelezo
[27] Kwani hao hawakutaraji kuwa itakuwapo kuhisabiwa, hata watende ya kuwaokoa humo. -
وَكَذَّبُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَا كِذَّابًا٢٨
Wakaththaboo biayatina kiththaban
Na wakikanusha Aya zetu kwa nguvu.28
Maelezo
[28] Wakazikadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu zenye kuthibitisha kufufuliwa kwa mkadhibisho mkali. -
وَكُلَّ شَىْءٍ أَحْصَيْنَـٰهُ كِتَـٰبًا٢٩
Wakulla shayin ahsaynahu kitaban
Na kila kitu Sisi tumekidhibiti kwa kukiandika.29
Maelezo
[29] Na kila kitu tumekidhibiti kwa kukiandika. -
فَذُوقُوا۟ فَلَن نَّزِيدَكُمْ إِلَّا عَذَابًا٣٠
Fathooqoo falan nazeedakum illa ʿathaban
Basi onjeni! Nasi hatutakuzidishieni ila adhabu!30
Maelezo
[30] Basi onjeni, wala hampati kwetu ila kuzidishiwa adhabu tu. -
إِنَّ لِلْمُتَّقِينَ مَفَازًا٣١
Inna lilmuttaqeena mafazan
Hakika wachamngu wanastahiki kufuzu,31
Maelezo
[31] Hakika wenye kumcha Mola wao Mlezi watapata kuokoka na adhabu, na wataipata Pepo, -
حَدَآئِقَ وَأَعْنَـٰبًا٣٢
Hadaiqa waaʿnaban
Mabustani na mizabibu,32
Maelezo
[32] Na mabustani yenye matunda, na mizabibu mizuri, -
وَكَوَاعِبَ أَتْرَابًا٣٣
Wakawaʿiba atraban
Na wake walio lingana nao,33
Maelezo
[33] Na wanawari walio watipwatipwa wa hirimu yao, -
وَكَأْسًا دِهَاقًا٣٤
Wakasan dihaqan
Na bilauri zilizo jaa,34
Maelezo
[34] Na bilauri safi zilizo jaa pomoni, -
لَّا يَسْمَعُونَ فِيهَا لَغْوًا وَلَا كِذَّٰبًا٣٥
La yasmaʿoona feeha laghwan wala kiththaban
Hawatasikia humo upuuzi wala uwongo,35
Maelezo
[35] Hawasikii huko Peponi upuuzi wala uwongo. -
جَزَآءً مِّن رَّبِّكَ عَطَآءً حِسَابًا٣٦
Jazaan min rabbika ʿataan hisaban
Malipo kutoka kwa Mola wako Mlezi, kipawa cha kutosha.36
Maelezo
[36] Ni malipo kutokana na Mola wako Mlezi, kwa fadhila yake na ihsani ya kutosha. -
رَّبِّ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا ٱلرَّحْمَـٰنِ ۖ لَا يَمْلِكُونَ مِنْهُ خِطَابًا٣٧
Rabbi alssamawati waalardi wama baynahuma alrrahmani la yamlikoona minhu khitaban
Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilio baina yao, Arrahman, Mwingi wa rehema; hawamiliki usemi mbele yake!37
Maelezo
[37] Mola Mlezi wa mbinguni na duniani na vilio baina yao, ambaye rehema yake imeenea juu ya kila kitu. Hapana yeyote mwenye madaraka ya kusema mbele yake. -
يَوْمَ يَقُومُ ٱلرُّوحُ وَٱلْمَلَـٰٓئِكَةُ صَفًّا ۖ لَّا يَتَكَلَّمُونَ إِلَّا مَنْ أَذِنَ لَهُ ٱلرَّحْمَـٰنُ وَقَالَ صَوَابًا٣٨
Yawma yaqoomu alrroohu waalmalaikatu saffan la yatakallamoona illa man athina lahu alrrahmanu waqala sawaban
Siku atakapo simama Roho na Malaika kwa safu. Hawatasema ila Mwingi wa rehema aliye mruhusu, na atasema yaliyo sawa tu.38
Maelezo
[38] Siku atakapo simama Jibrili na Malaika walio teuliwa nao wamenyenyekea, hasemi mmoja wao ila akipewa idhini na Arrahman, Mwingi wa rehema, kuwa aseme, naye atasema lilio sawa tu. -
ذَٰلِكَ ٱلْيَوْمُ ٱلْحَقُّ ۖ فَمَن شَآءَ ٱتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِۦ مَـَٔابًا٣٩
Thalika alyawmu alhaqqu faman shaa ittakhatha ila rabbihi maaban
Hiyo ndiyo Siku ya haki. Basi anaye taka na ashike njia arejee kwa Mola wake Mlezi39
Maelezo
[39] Hiyo ndiyo siku isiyo na shaka. Basi atakaye na ashike njia ya kwenda kwa Mola wake Mlezi arejee kwa Imani, na a'mali njema. -
إِنَّآ أَنذَرْنَـٰكُمْ عَذَابًا قَرِيبًا يَوْمَ يَنظُرُ ٱلْمَرْءُ مَا قَدَّمَتْ يَدَاهُ وَيَقُولُ ٱلْكَافِرُ يَـٰلَيْتَنِى كُنتُ تُرَٰبًۢا٤٠
Inna antharnakum ʿathaban qareeban yawma yanthuru almaro ma qaddamat yadahu wayaqoolu alkafiru ya laytanee kuntu turaban
Hakika tumekuhadharisheni adhabu iliyo karibu kufika; Siku ambayo mtu atakapo ona yaliyo tangulizwa na mikono yake; na kafiri atasema: Laiti ningeli kuwa udongo!40
Maelezo
[40] Hakika Sisi tumekuhadharisheni na adhabu itakayo tokea karibu, siku atakapo angalia mtu vitendo vyake vilivyo tangulizwa na mikono yake, na atakapo sema kafiri kwa kutamani kuokoka: Laiti ningeli bakia udongo baada ya kufa, nisifufuliwe wala nisihisabiwe!
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Surat An-Naba maana yake ni nini?
An-Naba maana yake ni “Habari Kuu”.
Surat An-Naba iko katika juzuu ya ngapi?
Surat An-Naba iko katika juzuu ya 30.
Surat An-Naba ina aya ngapi?
Surat An-Naba ina aya 40.
Surat An-Naba ni ya Makka au ya Madina?
Surat An-Naba ni sura ya Makka.
Surat An-Naba ni sura ya ngapi katika Qur’ani?
Ni sura ya 78 katika Qur’ani.
Vyanzo
- Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
- Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
- Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
- Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
- Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
- Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.
Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.