سورة النازعات
Surat An-Nazi’at kwa Kiswahili
Wanaong’oa
- 79
- Aya 46
- Sura ya Makka
- Juzuu 30
- Kurasa 583–584
Surat An-Nazi’at (النازعات) ni sura ya 79 katika Qur’ani na ina aya 46. Jina lake lina maana ya “Wanaong’oa”. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na iko katika juzuu ya 30.
Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat An-Nazi’at yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.
Surat An-Nazi’at kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
-
وَٱلنَّـٰزِعَـٰتِ غَرْقًا١
Waalnnaziʿati gharqan
Naapa kwa wanao komoa kwa nguvu!1
Maelezo
[1] Ninaapa kwa kila kilicho pewa uwezo wa kuving'oa vitu kutokana na pahala pao kwa nguvu, -
وَٱلنَّـٰشِطَـٰتِ نَشْطًا٢
Waalnnashitati nashtan
Na kwa wanao toa kwa upole!2
Maelezo
[2] Na kwa kila kilicho pewa uwezo wa kuvitoa vitu kwa utaratibu na ulaini, -
وَٱلسَّـٰبِحَـٰتِ سَبْحًا٣
Waalssabihati sabhan
Na wanao ogelea!3
Maelezo
[3] Na kwa kila kilicho pewa mbio za kutekeleza kazi yake kwa sahala na wepesi. -
فَٱلسَّـٰبِقَـٰتِ سَبْقًا٤
Faalssabiqati sabqan
Wakishindana mbio!4
Maelezo
[4] Na kwa vinavyo shindania kutimiza waajibu ulio twikwa juu yao kushindania kwa juhudi, -
فَٱلْمُدَبِّرَٰتِ أَمْرًا٥
Faalmudabbirati amran
Wakidabiri mambo.5
Maelezo
[5] Na vinavyo dabiri, kupanga, mambo na kuyaendesha kwa mujibu wa vilivyo khusishwa, -
يَوْمَ تَرْجُفُ ٱلرَّاجِفَةُ٦
Yawma tarjufu alrrajifatu
Siku kitapo tetemeka cha kutetemeka!6
Maelezo
[6] Bila ya shaka Saa ya Kiyama itafika; hiyo siku ambayo mpulizo wa mwanzo wa barugumu utavitikisa viumbe vyote, -
تَتْبَعُهَا ٱلرَّادِفَةُ٧
Tatbaʿuha alrradifatu
Kifuate cha kufuatia.7
Maelezo
[7] Na mpulizo huo utafuatiwa na wa pili ambao ndio utakao kuwa wa kufufuliwa watu. -
قُلُوبٌ يَوْمَئِذٍ وَاجِفَةٌ٨
Quloobun yawmaithin wajifatun
Siku hiyo nyoyo zitapiga piga!8
Maelezo
[8] Siku hiyo nyoyo zitapapatika kwa khofu. -
أَبْصَـٰرُهَا خَـٰشِعَةٌ٩
Absaruha khashiʿatun
Macho yatainama chini!9
Maelezo
[9] Macho ya watu yatakuwa na huzuni, manyonge. -
يَقُولُونَ أَءِنَّا لَمَرْدُودُونَ فِى ٱلْحَافِرَةِ١٠
Yaqooloona ainna lamardoodoona fee alhafirati
Sasa wanasema: Ati kweli tutarudishwa kwenye hali ya kwanza?10
Maelezo
[10] Watu hawa husema duniani kwa kukanya kufufuliwa: Ati tutarudishwa sisi baada ya kwisha kufa, tuumbwe tena kama tulivyo kuwa? -
أَءِذَا كُنَّا عِظَـٰمًا نَّخِرَةً١١
Aitha kunna ʿithaman nakhiratan
Hata tukiwa mifupa iliyo bunguliwa?11
Maelezo
[11] Tukisha kuwa mafupa yaliyo chakaa, ati tutarejeshwa tufufuliwe upya? -
قَالُوا۟ تِلْكَ إِذًا كَرَّةٌ خَاسِرَةٌ١٢
Qaloo tilka ithan karratun khasiratun
Wanasema: Basi marejeo hayo ni yenye khasara!12
Maelezo
[12] Wanasema, kwa kukanya na kejeli: Kurejea huko kama kukitokea basi ni marejeo ya khasara, na sisi si watu wa kukhasiri. -
فَإِنَّمَا هِىَ زَجْرَةٌ وَٰحِدَةٌ١٣
Fainnama hiya zajratun wahidatun
Kwa hakika hayo ni ukelele mmoja tu,13
Maelezo
[13] Msidhani kurejea huko ni kuzito. Kwani hayo ni ukelele mmoja tu, -
فَإِذَا هُم بِٱلسَّاهِرَةِ١٤
Faitha hum bialssahirati
Mara watakuwa kwenye uwanda wa mkutano!14
Maelezo
[14] Mara maiti wote watahudhurishwa kwenye ardhi ya mkusanyiko! -
هَلْ أَتَىٰكَ حَدِيثُ مُوسَىٰٓ١٥
Hal ataka hadeethu moosa
Je! Imekufikia hadithi ya Musa?15
Maelezo
[15] Ewe Muhammad! Imekufikilia hadithi ya Musa, -
إِذْ نَادَىٰهُ رَبُّهُۥ بِٱلْوَادِ ٱلْمُقَدَّسِ طُوًى١٦
Ith nadahu rabbuhu bialwadi almuqaddasi tuwan
Mola wake Mlezi alipo mwita katika bonde takatifu la T'uwaa, akamwambia:16
Maelezo
[16] Alipo mwita Mola wake Mlezi katika bonde lilio takaswa, linalo itwa "T'uwa"? -
ٱذْهَبْ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ إِنَّهُۥ طَغَىٰ١٧
Ithhab ila firʿawna innahu tagha
Nenda kwa Firauni. Hakika yeye amezidi jeuri17
Maelezo
[17] Akaambiwa: Nenda kwa Firauni aliye pindukia mpaka katika udhalimu. -
فَقُلْ هَل لَّكَ إِلَىٰٓ أَن تَزَكَّىٰ١٨
Faqul hal laka ila an tazakka
Umwambie: Je! Unapenda kujitakasa?18
Maelezo
[18] Umwambie: Je! Huelekei kut'ahirika? -
وَأَهْدِيَكَ إِلَىٰ رَبِّكَ فَتَخْشَىٰ١٩
Waahdiyaka ila rabbika fatakhsha
Nami nitakuongoa ufike kwa Mola wako Mlezi, upate kumcha.19
Maelezo
[19] Na mimi nikuongoze upate kumjua Mola wako Mlezi, umwogope. -
فَأَرَىٰهُ ٱلْـَٔايَةَ ٱلْكُبْرَىٰ٢٠
Faarahu alayata alkubra
Basi alimwonyesha Ishara kubwa.20
Maelezo
[20] Musa akamwonyesha Firauni miujiza mikubwa. -
فَكَذَّبَ وَعَصَىٰ٢١
Fakaththaba waʿasa
Lakini aliikadhibisha na akaasi.21
Maelezo
[21] Lakini Firauni alimkadhibisha Musa kwa aliyo kuja nayo, na akamuasi kwa aliyo mwitia. -
ثُمَّ أَدْبَرَ يَسْعَىٰ٢٢
Thumma adbara yasʿa
Kisha alirudi nyuma, akaingia kufanya juhudi.22
Maelezo
[22] Kisha akamgeuzia mgongo, akenda kujitahidi kumpinga. -
فَحَشَرَ فَنَادَىٰ٢٣
Fahashara fanada
Akakusanya watu akanadi.23
Maelezo
[23] Akawakusanya wachawi, na akawaita watu, -
فَقَالَ أَنَا۠ رَبُّكُمُ ٱلْأَعْلَىٰ٢٤
Faqala ana rabbukumu alaʿla
Akasema: Mimi ndiye Mola wenu Mlezi mkuu kabisa.24
Maelezo
[24] Akasema: Mimi ndiye Mola wenu Mlezi aliye mkubwa kabisa. -
فَأَخَذَهُ ٱللَّهُ نَكَالَ ٱلْـَٔاخِرَةِ وَٱلْأُولَىٰٓ٢٥
Faakhathahu Allahu nakala alakhirati waaloola
Basi hapo Mwenyezi Mungu akamshika kumuadhibu kwa la mwisho na la mwanzo.25
Maelezo
[25] Mwenyezi Mungu akampa adhabu kwa kauli yake ya mwisho, nayo ni vile kusema: Mimi ndiye Mola wenu Mlezi aliye mkubwa kabisa. Na akampa adhabu kwa kauli yake ya mwanzo, nayo ni kumkadhibisha Musa a.s. -
إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَعِبْرَةً لِّمَن يَخْشَىٰٓ٢٦
Inna fee thalika laʿibratan liman yakhsha
Kwa hakika katika haya yapo mazingatio kwa wanao ogopa.26
Maelezo
[26] Hakika katika hadithi hiyo yapo mawaidha kwa mwenye kumkhofu Mwenyezi Mungu. -
ءَأَنتُمْ أَشَدُّ خَلْقًا أَمِ ٱلسَّمَآءُ ۚ بَنَىٰهَا٢٧
Aantum ashaddu khalqan ami alssamao banaha
Je! Ni vigumu zaidi kukuumbeni nyinyi au mbingu? Yeye ndiye aliye ijenga!27
Maelezo
[27] Enyi mnao kanya kufufuliwa! Kukuumbeni nyinyi ni taabu zaidi au kuziumba mbingu, kuzikusanya sehemu zake zilio tawanyika mbali mbali, -
رَفَعَ سَمْكَهَا فَسَوَّىٰهَا٢٨
Rafaʿa samkaha fasawwaha
Akainua kimo chake, na akaitengeneza vizuri.28
Maelezo
[28] Na kunyanyua kimo chake, na zikakaa sawa hazina tafauti wala ila? -
وَأَغْطَشَ لَيْلَهَا وَأَخْرَجَ ضُحَىٰهَا٢٩
Waaghtasha laylaha waakhraja duhaha
Na akautia giza usiku wake, na akautokeza mchana wake29
Maelezo
[29] Na akatia kiza katika usiku wake, na akautokeza mchana wake ukawa na mwangaza? -
وَٱلْأَرْضَ بَعْدَ ذَٰلِكَ دَحَىٰهَآ٣٠
Waalarda baʿda thalika dahaha
Na juu ya hivyo ameitandaza ardhi.30
Maelezo
[30] Na ardhi baada ya hayo akaikunjua, na akaisawazisha, ikasilihi kukaliwa na watu wake? -
أَخْرَجَ مِنْهَا مَآءَهَا وَمَرْعَىٰهَا٣١
Akhraja minha maaha wamarʿaha
Akatoa ndani yake maji yake na malisho yake,31
Maelezo
[31] Akatoa ndani yake maji yake yanayo tibuka katika chemchem zake, na ikamiminika mito yake, na ikawa na mimea yake ya chakula kwa ajili ya watu na wanyama; -
وَٱلْجِبَالَ أَرْسَىٰهَا٣٢
Waaljibala arsaha
Na milima akaisimamisha,32
Maelezo
[32] Na milima akaithibitisha imara -
مَتَـٰعًا لَّكُمْ وَلِأَنْعَـٰمِكُمْ٣٣
Mataʿan lakum walianʿamikum
Kwa nafuu yenu na mifugo yenu.33
Maelezo
[33] Kwa ajili ya manufaa yenu na wanyama wenu mnao wafuga! -
فَإِذَا جَآءَتِ ٱلطَّآمَّةُ ٱلْكُبْرَىٰ٣٤
Faitha jaati alttammatu alkubra
Basi itakapo fika hiyo balaa kubwa,34
Maelezo
[34] Kitakapo fika Kiyama ambacho vitisho vyake vitaenea kote, -
يَوْمَ يَتَذَكَّرُ ٱلْإِنسَـٰنُ مَا سَعَىٰ٣٥
Yawma yatathakkaru alinsanu ma saʿa
Siku ambayo mtu atakumbuka aliyo yafanya,35
Maelezo
[35] Siku atakapo kumbuka mtu vitendo vyake vya kheri au shari, -
وَبُرِّزَتِ ٱلْجَحِيمُ لِمَن يَرَىٰ٣٦
Waburrizati aljaheemu liman yara
Na Jahannamu itadhihirishwa kwa mwenye kuona,36
Maelezo
[36] Na Jahannamu ikadhihirishwa wazi, akaiona kila mwenye macho kuwa ndio malipo, -
فَأَمَّا مَن طَغَىٰ٣٧
Faamma man tagha
Basi ama yule aliye zidi ujeuri,37
Maelezo
[37] Basi ama mwenye kupita mpaka kwa maasi yake, -
وَءَاثَرَ ٱلْحَيَوٰةَ ٱلدُّنْيَا٣٨
Waathara alhayata alddunya
Na akakhiari maisha ya dunia,38
Maelezo
[38] Na akajichagulia nafsi yake maisha yanayo pita njia, -
فَإِنَّ ٱلْجَحِيمَ هِىَ ٱلْمَأْوَىٰ٣٩
Fainna aljaheema hiya almawa
Kwa hakika Jahannamu ndiyo makaazi yake!39
Maelezo
[39] Basi Moto wa Jahannamu unao babua upepo wake ndio makaazi yake wala hana mengineyo. -
وَأَمَّا مَنْ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِۦ وَنَهَى ٱلنَّفْسَ عَنِ ٱلْهَوَىٰ٤٠
Waama man khafa maqama rabbihi wanaha alnnafsa ʿani alhawa
Na ama yule anaye ogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi, na akajizuilia nafsi yake na matamanio,40
Maelezo
[40] Na ama mwenye kukhofu ukubwa na utukufu wa Mola wake Mlezi, na akaizuia nafsi yake na matamanio ya kumpumbaza, -
فَإِنَّ ٱلْجَنَّةَ هِىَ ٱلْمَأْوَىٰ٤١
Fainna aljannata hiya almawa
Basi huyo, Pepo itakuwa ndiyo makaazi yake!41
Maelezo
[41] Basi huyo nyumba ya neema ya Peponi ndio makaazi yake, wala hana penginepo. -
يَسْـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلسَّاعَةِ أَيَّانَ مُرْسَىٰهَا٤٢
Yasaloonaka ʿani alssaʿati ayyana mursaha
Wanakuuliza Saa (ya Kiyama) itakuwa lini?42
Maelezo
[42] Ewe Muhammad! Wanakuuliza, ati, khabari za Saa ya Kiyama, itakuwa lini? -
فِيمَ أَنتَ مِن ذِكْرَىٰهَآ٤٣
Feema anta min thikraha
Una nini wewe hata uitaje?43
Maelezo
[43] Ujuzi wa hayo hauko kwako hata uwatajie. -
إِلَىٰ رَبِّكَ مُنتَهَىٰهَآ٤٤
Ila rabbika muntahaha
Kwa Mola wako Mlezi ndio mwisho wake.44
Maelezo
[44] Ujuzi wa hayo uko kwa Mola wako Mlezi tu, si kwa mwenginewe. (Nabii Isa a.s. ambaye Wakristo wanasema ni Mwana wa Mungu, au ndiye Mungu, pia anasimuliwa katika Biblia kuwa hakuijua Saa na Siku ya Kiyama. Injili ya Mathayo inanukulu maneno ya Yesu: "Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake.") -
إِنَّمَآ أَنتَ مُنذِرُ مَن يَخْشَىٰهَا٤٥
Innama anta munthiru man yakhshaha
Kwa hakika wewe ni mwonyaji tu kwa mwenye kuikhofu.45
Maelezo
[45] Kwani waajibu wako ni kuwaonya wanao khofu si kuwatangazia wakati wake. -
كَأَنَّهُمْ يَوْمَ يَرَوْنَهَا لَمْ يَلْبَثُوٓا۟ إِلَّا عَشِيَّةً أَوْ ضُحَىٰهَا٤٦
Kaannahum yawma yarawnaha lam yalbathoo illa ʿashiyyatan aw duhaha
Ni kama kwamba wao siku watapo iona (hiyo Saa) hawakukaa ila jioni moja tu, au mchana wake.46
Maelezo
[46] Na wao siku watakayo iona hiyo Saa ya Kiyama ni kama kwamba hawakuishi duniani zaidi kuliko jioni moja tu, au mchana wake.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Surat An-Nazi’at maana yake ni nini?
An-Nazi’at maana yake ni “Wanaong’oa”.
Surat An-Nazi’at iko katika juzuu ya ngapi?
Surat An-Nazi’at iko katika juzuu ya 30.
Surat An-Nazi’at ina aya ngapi?
Surat An-Nazi’at ina aya 46.
Surat An-Nazi’at ni ya Makka au ya Madina?
Surat An-Nazi’at ni sura ya Makka.
Surat An-Nazi’at ni sura ya ngapi katika Qur’ani?
Ni sura ya 79 katika Qur’ani.
Vyanzo
- Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
- Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
- Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
- Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
- Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
- Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.
Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.