Surat Al-Infitar (الإنفطار) ni sura ya 82 katika Qur’ani na ina aya 19. Jina lake lina maana ya “Kupasuka”. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na iko katika juzuu ya 30.
Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat Al-Infitar yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.
Surat Al-Infitar kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
-
إِذَا ٱلسَّمَآءُ ٱنفَطَرَتْ١
Itha alssamao infatarat
Mbingu itapo chanika!1
Maelezo
[1] Itakapo pasuka mbingu, -
وَإِذَا ٱلْكَوَاكِبُ ٱنتَثَرَتْ٢
Waitha alkawakibu intatharat
Na nyota zitapo tawanyika!2
Maelezo
[2] Na nyota zitakapo pukutika na kutawanyika, -
وَإِذَا ٱلْبِحَارُ فُجِّرَتْ٣
Waitha albiharu fujjirat
Na bahari zitakapo pasuliwa!3
Maelezo
[3] Na bahari zikafurika na kuingiliana kwa kuondoka viziwizi baina yao, -
وَإِذَا ٱلْقُبُورُ بُعْثِرَتْ٤
Waitha alqubooru buʿthirat
Na makaburi yatapo fukuliwa!4
Maelezo
[4] Na makaburi yakafunuliwa na wakatoka maiti walio kuwamo, -
عَلِمَتْ نَفْسٌ مَّا قَدَّمَتْ وَأَخَّرَتْ٥
ʿAlimat nafsun ma qaddamat waakhkharat
Hapo kila nafsi itajua ilicho tanguliza, na ilicho bakisha nyuma.5
Maelezo
[5] Hapo basi kila nafsi itajua nini kheri au shari iliyo tanguliza na iliyo chelewesha. -
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلْإِنسَـٰنُ مَا غَرَّكَ بِرَبِّكَ ٱلْكَرِيمِ٦
Ya ayyuha alinsanu ma gharraka birabbika alkareemi
Ewe mwanaadamu! Nini kilicho kughuri ukamwacha Mola wako Mlezi Mtukufu?6
Maelezo
[6] Ewe mwanaadamu! Kitu gani kilicho kukhadaa wewe na Mola wako Mlezi Mtukufu hata ukafanya jeuri ya kwenda kumuasi? (Ni dhaahiri kuwa Sayyid Abdulla bin Ali bin Nassir aliye tunga utenzi wa Kiswahili maarufu uitwao Al Inkishaf aliiwaza Aya hii alipo tunga ubeti huu: Moyo wangu nini huzundukani Likughurielo hela ni nni? Hunelezi nami kalibaini Liwapo na sura nisikataye ) -
ٱلَّذِى خَلَقَكَ فَسَوَّىٰكَ فَعَدَلَكَ٧
Allathee khalaqaka fasawwaka faʿadalaka
Aliye kuumba, akakuweka sawa, akakunyoosha!7
Maelezo
[7] Mungu wako huyo ndiye aliye kuumba nawe hukuwa chochote, akakuumba na viungo vya kukuletea manufaa, akakufanya umenyooka kwa umbo sawa sawa. -
فِىٓ أَىِّ صُورَةٍ مَّا شَآءَ رَكَّبَكَ٨
Fee ayyi sooratin ma shaa rakkabaka
Katika sura yoyote aliyo ipenda akakujenga.8
Maelezo
[8] Akakujenga na akakuleta katika sura yoyote aliyo itaka. -
كَلَّا بَلْ تُكَذِّبُونَ بِٱلدِّينِ٩
Kalla bal tukaththiboona bialddeeni
Sivyo hivyo! Bali nyinyi mnaikanusha Siku ya Malipo.9
Maelezo
[9] Hamwachi? Bali nyinyi mnakadhibisha malipo ya Siku ya Kiyama! -
وَإِنَّ عَلَيْكُمْ لَحَـٰفِظِينَ١٠
Wainna ʿalaykum lahafitheena
Na hakika bila ya shaka wapo walinzi juu yenu,10
Maelezo
[10] Na hakika wapo juu yenu Malaika walinzi, ambao ni waheshimiwa kwetu, -
كِرَامًا كَـٰتِبِينَ١١
Kiraman katibeena
Waandishi wenye hishima,11
Maelezo
[11] Wanasajili vitendo vyenu vyote mvitendavyo, vya kheri na shari. -
يَعْلَمُونَ مَا تَفْعَلُونَ١٢
Yaʿlamoona ma tafʿaloona
Wanayajua mnayo yatenda.12
Maelezo
[12] Wanayajua mnayo yafanya ya kheri na ya shari -
إِنَّ ٱلْأَبْرَارَ لَفِى نَعِيمٍ١٣
Inna alabrara lafee naʿeemin
Hakika wema bila ya shaka watakuwa katika neema,13
Maelezo
[13] Hakika wale walio ni wa kweli katika Imani yao wapo katika neema kubwa. -
وَإِنَّ ٱلْفُجَّارَ لَفِى جَحِيمٍ١٤
Wainna alfujjara lafee jaheemin
Na hakika waovu bila ya shaka watakuwa Motoni;14
Maelezo
[14] Na hakika walio iacha amri ya Mwenyezi bila ya shaka watakuwa katika Moto unao unguza, -
يَصْلَوْنَهَا يَوْمَ ٱلدِّينِ١٥
Yaslawnaha yawma alddeeni
Wataingia humo Siku ya Malipo.15
Maelezo
[15] Wataingia humo Siku ya Malipo. -
وَمَا هُمْ عَنْهَا بِغَآئِبِينَ١٦
Wama hum ʿanha bighaibeena
Na hawatoacha kuwamo humo.16
Maelezo
[16] Na wala hawatatoka katika Jahannamu! -
وَمَآ أَدْرَىٰكَ مَا يَوْمُ ٱلدِّينِ١٧
Wama adraka ma yawmu alddeeni
Na nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani?17
Maelezo
[17] Na nini kitakujuvya ni nini hiyo Siku ya Malipo, na mambo yake yamepindukia ujuzi wako na fikra zako? -
ثُمَّ مَآ أَدْرَىٰكَ مَا يَوْمُ ٱلدِّينِ١٨
Thumma ma adraka ma yawmu alddeeni
Tena nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani?18
Maelezo
[18] Tena ni nini kitacho kujuvya ni nini hiyo Siku ya Malipo kwa vitisho vyake na shida zake? -
يَوْمَ لَا تَمْلِكُ نَفْسٌ لِّنَفْسٍ شَيْـًٔا ۖ وَٱلْأَمْرُ يَوْمَئِذٍ لِّلَّهِ١٩
Yawma la tamliku nafsun linafsin shayan waalamru yawmaithin lillahi
Siku ambayo nafsi haitakuwa na madaraka yoyote juu ya nafsi; na amri yote siku hiyo ni ya Mwenyezi Mungu tu.19
Maelezo
[19] Siku ambayo nafsi haitakuwa na mamlaka yoyote juu ya nafsi ya kuifaa au kuidhuru; na amri yote siku hiyo itakuwa ni ya Mwenyezi Mungu peke yake!
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Surat Al-Infitar maana yake ni nini?
Al-Infitar maana yake ni “Kupasuka”.
Surat Al-Infitar iko katika juzuu ya ngapi?
Surat Al-Infitar iko katika juzuu ya 30.
Surat Al-Infitar ina aya ngapi?
Surat Al-Infitar ina aya 19.
Surat Al-Infitar ni ya Makka au ya Madina?
Surat Al-Infitar ni sura ya Makka.
Surat Al-Infitar ni sura ya ngapi katika Qur’ani?
Ni sura ya 82 katika Qur’ani.
Vyanzo
- Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
- Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
- Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
- Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
- Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
- Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.
Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.