سورة المطففين

Surat Al-Mutaffifin kwa Kiswahili

Wapunjao

Msahafu

Mishary Rashid AlafasyPakua MP3Pakua PDF

Surat Al-Mutaffifin (المطففين) ni sura ya 83 katika Qur’ani na ina aya 36. Jina lake lina maana ya “Wapunjao”. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na iko katika juzuu ya 30.

Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat Al-Mutaffifin yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.

Surat Al-Mutaffifin kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

  1. وَيْلٌ لِّلْمُطَفِّفِينَ۝١

    Waylun lilmutaffifeena

    Ole wao hao wapunjao!1

    Maelezo
    [1] Wataangamia wanao punja,
  2. ٱلَّذِينَ إِذَا ٱكْتَالُوا۟ عَلَى ٱلنَّاسِ يَسْتَوْفُونَ۝٢

    Allatheena itha iktaloo ʿala alnnasi yastawfoona

    Ambao wanapo jipimia kwa watu hudai watimiziwe.2

    Maelezo
    [2] Ambao wakijipimia wenyewe kwa watu hujitwalia ya kutosha na kuzidi,
  3. وَإِذَا كَالُوهُمْ أَو وَّزَنُوهُمْ يُخْسِرُونَ۝٣

    Waitha kaloohum aw wazanoohum yukhsiroona

    Na wao wanapo wapimia watu kwa kipimo au mizani hupunguza.3

    Maelezo
    [3] Na wakiwapimia watu kwa vipimo au mizani huwapunguzia haki yao wanayo stahiki, kwa dhulma!
  4. أَلَا يَظُنُّ أُو۟لَـٰٓئِكَ أَنَّهُم مَّبْعُوثُونَ۝٤

    Ala yathunnu olaika annahum mabʿoothoona

    Kwani hawadhani hao kwamba watafufuliwa .4

    Maelezo
    [4] Hivyo haiwapitikii katika akili zao hawa wanao punja wenzao kwamba watakuja fufuliwa,
  5. لِيَوْمٍ عَظِيمٍ۝٥

    Liyawmin ʿatheemin

    Katika Siku iliyo kuu!5

    Maelezo
    [5] Katika siku ya vitisho vikuu?
  6. يَوْمَ يَقُومُ ٱلنَّاسُ لِرَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ۝٦

    Yawma yaqoomu alnnasu lirabbi alʿalameena

    Siku watapo msimamia watu Mola Mlezi wa walimwengu wote?6

    Maelezo
    [6] Siku watapo simama watu kwa amri ya Mola Mlezi wa walimwengu wote na hukumu yake?
  7. كَلَّآ إِنَّ كِتَـٰبَ ٱلْفُجَّارِ لَفِى سِجِّينٍ۝٧

    Kalla inna kitaba alfujjari lafee sijjeenin

    Hasha! Hakika maandiko ya wakosefu bila ya shaka yamo katika Sijjin.7

    Maelezo
    [7] Wacheni kupunja, na kughafilika na kufufuliwa! Kwani hakika waliyo andikiwa wakosefu katika a'mali zao mbovu, bila ya shaka yamo katika Sijjin.
  8. وَمَآ أَدْرَىٰكَ مَا سِجِّينٌ۝٨

    Wama adraka ma sijjeenun

    Unajua nini Sijjin?8

    Maelezo
    [8] Na nini kitakujuvya nini hiyo Sijjin?
  9. كِتَـٰبٌ مَّرْقُومٌ۝٩

    Kitabun marqoomun

    Kitabu kilicho andikwa.9

    Maelezo
    [9] Hicho ni Kitabu kilicho pigwa mistari baina ya maandishi yake.
  10. وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ۝١٠

    Waylun yawmaithin lilmukaththibeena

    Ole wao siku hiyo kwa wanao kadhibisha!10

    Maelezo
    [10] Wataangamia wanao kadhibisha siku itapo kuwa kufufuliwa na kuhisabiwa.
  11. ٱلَّذِينَ يُكَذِّبُونَ بِيَوْمِ ٱلدِّينِ۝١١

    Allatheena yukaththiboona biyawmi alddeeni

    Ambao wanaikadhibisha Siku ya Malipo.11

    Maelezo
    [11] Ambao wanaikanusha Siku ya Malipo.
  12. وَمَا يُكَذِّبُ بِهِۦٓ إِلَّا كُلُّ مُعْتَدٍ أَثِيمٍ۝١٢

    Wama yukaththibu bihi illa kullu muʿtadin atheemin

    Wala haikadhibishi ila kila mwenye kuruka mipaka, mwenye dhambi.12

    Maelezo
    [12] Na wala haikanushi Siku ya Malipo ila kila mwenye kupindukia mipaka mwingi wa madhambi.
  13. إِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِ ءَايَـٰتُنَا قَالَ أَسَـٰطِيرُ ٱلْأَوَّلِينَ۝١٣

    Itha tutla ʿalayhi ayatuna qala asateeru alawwaleena

    Anapo somewa Aya zetu husema: Ni visa vya watu wa kale!13

    Maelezo
    [13] Na akisomewa Aya za Mwenyezi Mungu zenye kutaja kuwepo malipo husema: Huo ni uwongo wa walio tangulia!
  14. كَلَّا ۖ بَلْ ۜ رَانَ عَلَىٰ قُلُوبِهِم مَّا كَانُوا۟ يَكْسِبُونَ۝١٤

    Kalla bal rana ʿala quloobihim ma kanoo yaksiboona

    Hasha! Bali yametia kutu juu ya nyoyo zao hao walio kuwa wakiyachuma.14

    Maelezo
    [14] Ewe uliye kiuka mipaka! Wacha kauli hiyo potovu. Bali nyoyo za wenye kupindukia mipaka imegubikwa na ukafiri na maasi waliyo yatenda.
  15. كَلَّآ إِنَّهُمْ عَن رَّبِّهِمْ يَوْمَئِذٍ لَّمَحْجُوبُونَ۝١٥

    Kalla innahum ʿan rabbihim yawmaithin lamahjooboona

    Hasha! Hakika hao siku hiyo bila ya shaka watazuiliwa na neema za Mola wao Mlezi.15

    Maelezo
    [15] Hakika ni kweli kuwa hao wanao kadhibisha watazuiliwa siku hiyo rehema ya Mwenyezi Mungu kwa sababu ya maasi waliyo yachuma.
  16. ثُمَّ إِنَّهُمْ لَصَالُوا۟ ٱلْجَحِيمِ۝١٦

    Thumma innahum lasaloo aljaheemi

    Kisha wataingia Motoni!16

    Maelezo
    [16] Kisha hakika hao bila ya shaka wataingia Motoni.
  17. ثُمَّ يُقَالُ هَـٰذَا ٱلَّذِى كُنتُم بِهِۦ تُكَذِّبُونَ۝١٧

    Thumma yuqalu hatha allathee kuntum bihi tukaththiboona

    Kisha waambiwe: Haya ndiyo mliyo kuwa mkiyakadhabisha.17

    Maelezo
    [17] Kisha wataambiwa kwa kuwakebehi: Hii basi ndiyo adhabu inayo kuteremkieni ambayo mlikuwa mkiikanusha duniani!
  18. كَلَّآ إِنَّ كِتَـٰبَ ٱلْأَبْرَارِ لَفِى عِلِّيِّينَ۝١٨

    Kalla inna kitaba alabrari lafee ʿilliyyeena

    Hasha! Hakika maandiko ya watu wema bila ya shaka yamo katika I'liyyin.18

    Maelezo
    [18] Ni hakika kuwa vitendo vya watu wema bila ya shaka vimeandikwa katika I'liyyin.
  19. وَمَآ أَدْرَىٰكَ مَا عِلِّيُّونَ۝١٩

    Wama adraka ma ʿilliyyoona

    Na nini kitakacho kujuvya nini I'liyyin?19

    Maelezo
    [19] Na nini cha kukujuvya nini I'liyyin?
  20. كِتَـٰبٌ مَّرْقُومٌ۝٢٠

    Kitabun marqoomun

    Kitabu kilicho andikwa.20

    Maelezo
    [20] Hicho ni Kitabu kilicho andikwa wazi maandishi yake,
  21. يَشْهَدُهُ ٱلْمُقَرَّبُونَ۝٢١

    Yashhaduhu almuqarraboona

    Wanakishuhudia walio karibishwa.21

    Maelezo
    [21] Wanakihudhurisha na kukihifadhi Malaika walio kurubishwa.
  22. إِنَّ ٱلْأَبْرَارَ لَفِى نَعِيمٍ۝٢٢

    Inna alabrara lafee naʿeemin

    Hakika watu wema bila ya shaka watakuwa katika neema.22

    Maelezo
    [22] Hakika watu wema bila ya shaka watakuwa katika neema za Peponi,
  23. عَلَى ٱلْأَرَآئِكِ يَنظُرُونَ۝٢٣

    ʿAla alaraiki yanthuroona

    Wakae juu ya viti vya enzi wakiangalia.23

    Maelezo
    [23] Juu ya viti vya enzi, wakiziangalia neema na ukarimu alio wakirimu Mwenyezi Mungu.
  24. تَعْرِفُ فِى وُجُوهِهِمْ نَضْرَةَ ٱلنَّعِيمِ۝٢٤

    Taʿrifu fee wujoohihim nadrata alnnaʿeemi

    Utatambua katika nyuso zao mng'aro wa neema,24

    Maelezo
    [24] Utaona katika nyuso zao uchangamfu na mng'aro wa neema.
  25. يُسْقَوْنَ مِن رَّحِيقٍ مَّخْتُومٍ۝٢٥

    Yusqawna min raheeqin makhtoomin

    Watanyweshwa kinywaji safi kiliyo tiwa muhuri,25

    Maelezo
    [25] Wakinyweshwa kinywaji safi kilicho hifadhiwa;
  26. خِتَـٰمُهُۥ مِسْكٌ ۚ وَفِى ذَٰلِكَ فَلْيَتَنَافَسِ ٱلْمُتَنَـٰفِسُونَ۝٢٦

    Khitamuhu miskun wafee thalika falyatanafasi almutanafisoona

    Muhuri wake ni miski. Na katika hayo washindanie wenye kushindana.26

    Maelezo
    [26] Kuhifadhiwa huko hakukuzidisha ila uzuri wake. Na kupata neema hizo, basi, na washindanie wanao shindana.
  27. وَمِزَاجُهُۥ مِن تَسْنِيمٍ۝٢٧

    Wamizajuhu min tasneemin

    Na mchanganyiko wake ni Tasniim,27

    Maelezo
    [27] Cha kuchanganyia kinywaji hicho ni maji ya Tasniim ya Peponi,
  28. عَيْنًا يَشْرَبُ بِهَا ٱلْمُقَرَّبُونَ۝٢٨

    ʿAynan yashrabu biha almuqarraboona

    Chemchem watakayo inywa walio kurubishwa.28

    Maelezo
    [28] Nayo ni chemchem wanao inywa walio kurubishwa si wengineo, katika watu wa Peponi.
  29. إِنَّ ٱلَّذِينَ أَجْرَمُوا۟ كَانُوا۟ مِنَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ يَضْحَكُونَ۝٢٩

    Inna allatheena ajramoo kanoo mina allatheena amanoo yadhakoona

    Kwa hakika wale walio kuwa wakosefu walikuwa wakiwacheka walio amini.29

    Maelezo
    [29] Wale walio kuwa wakibeba madhambi kuipingia Dini walikuwa wakiwacheka kuwakejeli Waumini duniani.
  30. وَإِذَا مَرُّوا۟ بِهِمْ يَتَغَامَزُونَ۝٣٠

    Waitha marroo bihim yataghamazoona

    Na wanapo pita karibu yao wakikonyezana.30

    Maelezo
    [30] Na wakipita Waumini mbele yao basi wao hukonyezana kwa kuwabeza.
  31. وَإِذَا ٱنقَلَبُوٓا۟ إِلَىٰٓ أَهْلِهِمُ ٱنقَلَبُوا۟ فَكِهِينَ۝٣١

    Waitha inqalaboo ila ahlihimu inqalaboo fakiheena

    Na wanapo rudi kwa watu wao hurudi nao wamefurahi.31

    Maelezo
    [31] Na hao wakosefu wakirejea kwa ahali zao hurejea kwa furaha na kuona ladha kwa vile kuwakejeli Waumini.
  32. وَإِذَا رَأَوْهُمْ قَالُوٓا۟ إِنَّ هَـٰٓؤُلَآءِ لَضَآلُّونَ۝٣٢

    Waitha raawhum qaloo inna haolai ladalloona

    Na wanapo waona husema: Hakika hawa ndio khasa walio potea.32

    Maelezo
    [32] Na wakiwaona Waumini husema: Ama hakika hawa wamepotea kweli kwa kumuamini Muhammad.
  33. وَمَآ أُرْسِلُوا۟ عَلَيْهِمْ حَـٰفِظِينَ۝٣٣

    Wama orsiloo ʿalayhim hafitheena

    Na wao hawakutumwa wawe walinzi juu yao.33

    Maelezo
    [33] Wala hao wakosefu hawakutumwa wawe wa kuwahukumu Waumini kwa kuwaongoza au kuwapoteza, wala kuwa ni walinzi wa vitendo vyao.
  34. فَٱلْيَوْمَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ مِنَ ٱلْكُفَّارِ يَضْحَكُونَ۝٣٤

    Faalyawma allatheena amanoo mina alkuffari yadhakoona

    Basi leo walio amini ndio watawacheka makafiri,34

    Maelezo
    [34] Basi Siku ya Malipo walio amini watakuwa ndio wa kuwacheka hao makafiri kwa kuwalipizia kile kicheko chao na kejeli yao ya duniani.
  35. عَلَى ٱلْأَرَآئِكِ يَنظُرُونَ۝٣٥

    ʿAla alaraiki yanthuroona

    Nao wako juu ya viti vya enzi wakiangalia.35

    Maelezo
    [35] Ilhali wako juu ya vitanda na matakia watakuwa Waumini wakiziangalia neema za Mwenyezi Mungu alizo wapa.
  36. هَلْ ثُوِّبَ ٱلْكُفَّارُ مَا كَانُوا۟ يَفْعَلُونَ۝٣٦

    Hal thuwwiba alkuffaru ma kanoo yafʿaloona

    Je! makafiri wamelipwa malipo ya yale waliyo kuwa wakiyatenda?36

    Maelezo
    [36] Je! Makafiri watalipwa huko Akhera kwa waliyo yatenda duniani?

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Surat Al-Mutaffifin maana yake ni nini?

Al-Mutaffifin maana yake ni “Wapunjao”.

Surat Al-Mutaffifin iko katika juzuu ya ngapi?

Surat Al-Mutaffifin iko katika juzuu ya 30.

Surat Al-Mutaffifin ina aya ngapi?

Surat Al-Mutaffifin ina aya 36.

Surat Al-Mutaffifin ni ya Makka au ya Madina?

Surat Al-Mutaffifin ni sura ya Makka.

Surat Al-Mutaffifin ni sura ya ngapi katika Qur’ani?

Ni sura ya 83 katika Qur’ani.

Vyanzo

  • Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
  • Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
  • Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
  • Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
  • Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
  • Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.

Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.

Mipangilio ya kusoma

Fonti ya Qur’ani
Ukubwa wa Kiarabu
100%
Ukubwa wa tafsiri
100%
Mandhari

Ongeza kwenye skrini ya kwanza

ReadSurahFungua ReadSurah kutoka skrini ya kwanza, kwa skrini nzima. Sura ulizosoma hufunguka hata bila intaneti.

  1. Katika Safari, gusa kitufe cha kushiriki (Share). Kwenye iPhone mpya kiko kwenye menyu ya •••.
  2. Gusa “Add to Home Screen”. Huenda ukahitaji kusogeza chini.
  3. Gusa “Add”.