سورة البروج

Surat Al-Buruj kwa Kiswahili

Vituo vya Nyota

Msahafu

Mishary Rashid AlafasyPakua MP3Pakua PDF

Surat Al-Buruj (البروج) ni sura ya 85 katika Qur’ani na ina aya 22. Jina lake lina maana ya “Vituo vya Nyota”. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na iko katika juzuu ya 30.

Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat Al-Buruj yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.

Surat Al-Buruj kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

  1. وَٱلسَّمَآءِ ذَاتِ ٱلْبُرُوجِ۝١

    Waalssamai thati alburooji

    Naapa kwa mbingu yenye Buruji!1

    Maelezo
    [1] Naapa kwa mbingu yenye Buruj au Manaazil, njia au vituo ambavyo nyota hupitia katika nyendo zake, Buruuj au Manaazil ndio huu mkusanyiko wa nyota unao onekana kwa sura namna mbali mbali mbinguni. Hizo Buruuj zimegawika sehemu kumi na mbili ambazo ardhi inazipitia inapo lizunguka jua.
  2. وَٱلْيَوْمِ ٱلْمَوْعُودِ۝٢

    Waalyawmi almawʿoodi

    Na kwa siku iliyo ahidiwa!2

    Maelezo
    [2] Na kwa Siku iliyo ahidiwa kuwa ndiyo Siku ya Hisabu na Malipo,
  3. وَشَاهِدٍ وَمَشْهُودٍ۝٣

    Washahidin wamashhoodin

    Na kwa shahidi na kinacho shuhudiwa!3

    Maelezo
    [3] Na kwa viumbe watao hudhuria Siku hiyo wakaona vitisho na ajabu zitakazo kuwepo,
  4. قُتِلَ أَصْحَـٰبُ ٱلْأُخْدُودِ۝٤

    Qutila ashabu alukhdoodi

    Wameangamizwa watu wa makhandaki.4

    Maelezo
    [4] Hakika Mwenyezi Mungu amewalaani watu walio chimba khandaki katika ardhi,
  5. ٱلنَّارِ ذَاتِ ٱلْوَقُودِ۝٥

    Alnnari thati alwaqoodi

    Yenye moto wenye kuni nyingi!5

    Maelezo
    [5] Wakawasha moto kuwatumbukiza ndani yake Waumini ili kuwatesa,
  6. إِذْ هُمْ عَلَيْهَا قُعُودٌ۝٦

    Ith hum ʿalayha quʿoodun

    Walipo kuwa wamekaa hapo!6

    Maelezo
    [6] Na wao wamekaa ukingoni mwake wakishuhudia mateso yanayo wapata Waumini.
  7. وَهُمْ عَلَىٰ مَا يَفْعَلُونَ بِٱلْمُؤْمِنِينَ شُهُودٌ۝٧

    Wahum ʿala ma yafʿaloona bialmumineena shuhoodun

    Na wao ni mashahidi wa yale waliyo kuwa wakiwafanyia Waumini.7

    Maelezo
    [7] Na wao wapo hapo wamehudhuria kwenye mateso wanayo watendea Waumini.
  8. وَمَا نَقَمُوا۟ مِنْهُمْ إِلَّآ أَن يُؤْمِنُوا۟ بِٱللَّهِ ٱلْعَزِيزِ ٱلْحَمِيدِ۝٨

    Wama naqamoo minhum illa an yuminoo biAllahi alʿazeezi alhameedi

    Nao hawakuona baya lolote kwao ila kuwa wakimuamini Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Msifiwa!8

    Maelezo
    [8] Na hapana walilo lichukia kwa hao Waumini ila ni kuwa wakimuamini Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu ambaye adhabu yake huogopwa, Msifiwa anaye tarajiwa thawabu zake.
  9. ٱلَّذِى لَهُۥ مُلْكُ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۚ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ شَهِيدٌ۝٩

    Allathee lahu mulku alssamawati waalardi waAllahu ʿala kulli shayin shaheedun

    Ambaye anao ufalme wa mbingu na ardhi; na Mwenyezi Mungu ni shaahidi wa kila kitu.9

    Maelezo
    [9] Ambaye, peke yake, ndiye Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi. Na Mwenyezi Mungu ni shahidi anashuhudia yote wayatendayo Waumini na makafiri na atawalipa kwayo.
  10. إِنَّ ٱلَّذِينَ فَتَنُوا۟ ٱلْمُؤْمِنِينَ وَٱلْمُؤْمِنَـٰتِ ثُمَّ لَمْ يَتُوبُوا۟ فَلَهُمْ عَذَابُ جَهَنَّمَ وَلَهُمْ عَذَابُ ٱلْحَرِيقِ۝١٠

    Inna allatheena fatanoo almumineena waalmuminati thumma lam yatooboo falahum ʿathabu jahannama walahum ʿathabu alhareeqi

    Hakika walio wafitini Waumini wanaume na Waumini wanawake, kisha hawakutubu, basi watapata adhabu ya Jahannamu na watapata adhabu ya kuungua.10

    Maelezo
    [10] Hakika walio watia matatani Waumini wanaume na Waumini wanawake kwa maudhi na kuwaadhibu kwa moto, kisha wasitubu na kurejea nyuma watapata Akhera adhabu ya Jahannamu kwa ukafiri wao, na watapata adhabu ya kuunguzwa kwa kule kuwaunguza moto Waumini.
  11. إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ لَهُمْ جَنَّـٰتٌ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَـٰرُ ۚ ذَٰلِكَ ٱلْفَوْزُ ٱلْكَبِيرُ۝١١

    Inna allatheena amanoo waʿamiloo alssalihati lahum jannatun tajree min tahtiha alanharu thalika alfawzu alkabeeru

    Hakika walio amini na wakatenda mema watapata Bustani zenye mito ipitayo kati yake. Huko ndiko kufuzu kukubwa.11

    Maelezo
    [11] Hakika hao walio kusanya kwenye Imani ya Mwenyezi Mungu vitendo vyema watapata Mabustani yapitayo mito kati yake. Neema hiyo waliyo lipwa ni kufuzu kukubwa.
  12. إِنَّ بَطْشَ رَبِّكَ لَشَدِيدٌ۝١٢

    Inna batsha rabbika lashadeedun

    Hakika kutesa kwa Mola wako Mlezi ni kukali.12

    Maelezo
    [12] Hakika mshiko wa Mola wako Mlezi kuwashika majabari umefika ukomo kwa ukali wake
  13. إِنَّهُۥ هُوَ يُبْدِئُ وَيُعِيدُ۝١٣

    Innahu huwa yubdio wayuʿeedu

    Yeye ndiye anaye anzisha na ndiye anaye rejeza tena,13

    Maelezo
    [13] Ni Yeye peke yake ndiye Mwenye kuanza kuumba, na kisha ni Yeye anaye rejeza tena,
  14. وَهُوَ ٱلْغَفُورُ ٱلْوَدُودُ۝١٤

    Wahuwa alghafooru alwadoodu

    Naye ni Mwenye kusamehe, Mwenye mapenzi,14

    Maelezo
    [14] Na Yeye ni Mwingi wa msamaha kwa mwenye kutubu na akarejea, na Mwingi wa mapenzi kwa mwenye kumpenda na akamt'ii.
  15. ذُو ٱلْعَرْشِ ٱلْمَجِيدُ۝١٥

    Thoo alʿarshi almajeedi

    Mwenye Kiti cha Enzi, Mtukufu,15

    Maelezo
    [15] Yeye ndiye Mwenye Kiti cha Enzi na Mwenye kukimiliki, na Mkuu kwa dhati yake na sifa zake.
  16. فَعَّالٌ لِّمَا يُرِيدُ۝١٦

    Faʿʿalun lima yureedu

    Atendaye ayatakayo.16

    Maelezo
    [16] Ni Mtendaji kwa alitakalo, na hendi kinyume na uweza wake yeyote anaye taka.
  17. هَلْ أَتَىٰكَ حَدِيثُ ٱلْجُنُودِ۝١٧

    Hal ataka hadeethu aljunoodi

    Je! Zimekuwasilia khabari za majeshi?17

    Maelezo
    [17] Je! Imekujia, ewe Muhammad, hadithi ya kile kikundi kilicho a'si katika mataifa yaliyo kwisha pita?
  18. فِرْعَوْنَ وَثَمُودَ۝١٨

    Firʿawna wathamooda

    Ya Firauni na Thamudi?18

    Maelezo
    [18] Kaumu ya Firauni na Thamudi na yaliyo washukia katika malipo ya kushikilia kwao upotovu?
  19. بَلِ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ فِى تَكْذِيبٍ۝١٩

    Bali allatheena kafaroo fee taktheebin

    Lakini walio kufuru wamo katika kukadhibisha.19

    Maelezo
    [19] Bali hao makafiri katika kaumu yako ni shadidi zaidi katika kukukadhibisha kuliko hawa walivyo wakadhibisha Mitume wao.
  20. وَٱللَّهُ مِن وَرَآئِهِم مُّحِيطٌۢ۝٢٠

    WaAllahu min waraihim muheetun

    Na Mwenyezi Mungu nyuma yao amewazunguka.20

    Maelezo
    [20] Na Mwenyezi Mungu anawaweza hao, na anawajua vilivyo.
  21. بَلْ هُوَ قُرْءَانٌ مَّجِيدٌ۝٢١

    Bal huwa quranun majeedun

    Bali hii ni Qur'ani tukufu21

    Maelezo
    [21] Bali hii ulio waletea ni Qur'ani tukufu inadhihirisha hoja za ukweli wako.
  22. فِى لَوْحٍ مَّحْفُوظٍۭ۝٢٢

    Fee lawhin mahfoothin

    Katika Ubao Ulio Hifadhiwa.22

    Maelezo
    [22] Imo katika Ubao Ulio Hifadhiwa, hapana uwezo unao weza kuipotoa au kuigeuza

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Surat Al-Buruj maana yake ni nini?

Al-Buruj maana yake ni “Vituo vya Nyota”.

Surat Al-Buruj iko katika juzuu ya ngapi?

Surat Al-Buruj iko katika juzuu ya 30.

Surat Al-Buruj ina aya ngapi?

Surat Al-Buruj ina aya 22.

Surat Al-Buruj ni ya Makka au ya Madina?

Surat Al-Buruj ni sura ya Makka.

Surat Al-Buruj ni sura ya ngapi katika Qur’ani?

Ni sura ya 85 katika Qur’ani.

Vyanzo

  • Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
  • Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
  • Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
  • Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
  • Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
  • Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.

Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.

Mipangilio ya kusoma

Fonti ya Qur’ani
Ukubwa wa Kiarabu
100%
Ukubwa wa tafsiri
100%
Mandhari

Ongeza kwenye skrini ya kwanza

ReadSurahFungua ReadSurah kutoka skrini ya kwanza, kwa skrini nzima. Sura ulizosoma hufunguka hata bila intaneti.

  1. Katika Safari, gusa kitufe cha kushiriki (Share). Kwenye iPhone mpya kiko kwenye menyu ya •••.
  2. Gusa “Add to Home Screen”. Huenda ukahitaji kusogeza chini.
  3. Gusa “Add”.