سورة الأعلى

Surat Al-A’la kwa Kiswahili

Aliye Juu Kabisa

Msahafu

Mishary Rashid AlafasyPakua MP3Pakua PDF

Surat Al-A’la (الأعلى) ni sura ya 87 katika Qur’ani na ina aya 19. Jina lake lina maana ya “Aliye Juu Kabisa”. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na iko katika juzuu ya 30.

Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat Al-A’la yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.

Surat Al-A’la kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

  1. سَبِّحِ ٱسْمَ رَبِّكَ ٱلْأَعْلَى۝١

    Sabbihi isma rabbika alaʿla

    Litakase jina la Mola wako Mlezi aliye juu kabisa!1

    Maelezo
    [1] Litakase jina la Mola wako Mlezi lilio tukufu na kila kitu kisicho kuwa kinaelekeana nalo.
  2. ٱلَّذِى خَلَقَ فَسَوَّىٰ۝٢

    Allathee khalaqa fasawwa

    Aliye umba, na akaweka sawa!2

    Maelezo
    [2] Aliye umba kila kitu, na akajaalia uumbaji wote sawa sawa katika hukumu na kupangana.
  3. وَٱلَّذِى قَدَّرَ فَهَدَىٰ۝٣

    Waallathee qaddara fahada

    Na ambaye amekadiria na akaongoa,.3

    Maelezo
    [3] Na akakadiria kwa kila kitu kwa mujibu wa maslaha yake, na akakiongoza.
  4. وَٱلَّذِىٓ أَخْرَجَ ٱلْمَرْعَىٰ۝٤

    Waallathee akhraja almarʿa

    Na aliye otesha malisho!4

    Maelezo
    [4] Na ambaye akatoa kwenye ardhi mimea namna mbali mbali ya kuwalisha wanyama.
  5. فَجَعَلَهُۥ غُثَآءً أَحْوَىٰ۝٥

    Fajaʿalahu ghuthaan ahwa

    Kisha akayafanya makavu, meusi.5

    Maelezo
    [5] Na akaifanya mimea hiyo baada ya kuwa kijani imestawi, ikakauka na imekuwa myeusi!
  6. سَنُقْرِئُكَ فَلَا تَنسَىٰٓ۝٦

    Sanuqrioka fala tansa

    Tutakusomesha wala hutasahau!6

    Maelezo
    [6] Ewe Muhammad! Sisi tutakujaalia uwe ni mwenye kuisoma Qur'ani kwa ufunuo kutoka kwetu, na wala hutosahau utacho kihifadhi.
  7. إِلَّا مَا شَآءَ ٱللَّهُ ۚ إِنَّهُۥ يَعْلَمُ ٱلْجَهْرَ وَمَا يَخْفَىٰ۝٧

    Illa ma shaa Allahu innahu yaʿlamu aljahra wama yakhfa

    Ila akipenda Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye anayajua yaliyo dhaahiri na yaliyo fichikana.7

    Maelezo
    [7] Isipo kuwa anacho taka Mwenyezi Mungu ukisahau, kwani hakika Yeye Mtukufu anayajua wanayo yadhihirisha waja wake na wanayo yaficha, ikiwa maneno au vitendo.
  8. وَنُيَسِّرُكَ لِلْيُسْرَىٰ۝٨

    Wanuyassiruka lilyusra

    Na tutakusahilishia yawe mepesi.8

    Maelezo
    [8] Na tutakuwezesha kupita njia ya kufikilia kwa wepesi mambo yako yote.
  9. فَذَكِّرْ إِن نَّفَعَتِ ٱلذِّكْرَىٰ۝٩

    Fathakkir in nafaʿati alththikra

    Basi kumbusha, kama kukumbusha kunafaa.9

    Maelezo
    [9] Basi wakumbushe watu ikiwa kukumbusha kutaleta manufaa, kwani inavyo faa ndio kuwanafiisha.
  10. سَيَذَّكَّرُ مَن يَخْشَىٰ۝١٠

    Sayaththakkaru man yakhsha

    Atakumbuka mwenye kuogopa.10

    Maelezo
    [10] Watanafiika kwa ukumbusho wako wanao mwogopa Mwenyezi Mungu.
  11. وَيَتَجَنَّبُهَا ٱلْأَشْقَى۝١١

    Wayatajannabuha alashqa

    Na atajitenga mbali nayo mpotovu,11

    Maelezo
    [11] Na atajitenga na ukumbusho mpotovu anaye shikilia kufanya inda na ukafiri.
  12. ٱلَّذِى يَصْلَى ٱلنَّارَ ٱلْكُبْرَىٰ۝١٢

    Allathee yasla alnnara alkubra

    Ambaye atauingia Moto mkubwa.12

    Maelezo
    [12] Ambaye ataingia kwenye Moto mkubwa ulio andaliwa kuwa ndio malipo yake.
  13. ثُمَّ لَا يَمُوتُ فِيهَا وَلَا يَحْيَىٰ۝١٣

    Thumma la yamootu feeha wala yahya

    Tena humo hatakufa wala hawi hai.13

    Maelezo
    [13] Tena hatokufa huko Motoni akapumzika kwa kifo, wala hawi hai kwa uhai wa kustarehe nao.
  14. قَدْ أَفْلَحَ مَن تَزَكَّىٰ۝١٤

    Qad aflaha man tazakka

    Hakika amekwisha fanikiwa aliye jitakasa.14

    Maelezo
    [14] Hakika amefuzu mwenye kujisafisha na ukafiri na maasi.
  15. وَذَكَرَ ٱسْمَ رَبِّهِۦ فَصَلَّىٰ۝١٥

    Wathakara isma rabbihi fasalla

    Na akakumbuka jina la Mola wake Mlezi, na akaswali.15

    Maelezo
    [15] Na akalikumbuka jina la Muumba wake kwa moyo wake na ulimi wake, na akaswali kwa unyenyekevu kama itakikanavyo.
  16. بَلْ تُؤْثِرُونَ ٱلْحَيَوٰةَ ٱلدُّنْيَا۝١٦

    Bal tuthiroona alhayata alddunya

    Lakini nyinyi mnakhiari maisha ya dunia!16

    Maelezo
    [16] Bali nyinyi hamfanyi hayo yanayo pelekea kufanikiwa, lakini katika hima zenu mnatanguliza maisha ya duniani kuliko ya Akhera.
  17. وَٱلْـَٔاخِرَةُ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰٓ۝١٧

    Waalakhiratu khayrun waabqa

    Na Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi.17

    Maelezo
    [17] Na Akhera ni bora kuliko dunia, kwa usafi wa neema zake, na ni yenye kubaki na kudumu zaidi.
  18. إِنَّ هَـٰذَا لَفِى ٱلصُّحُفِ ٱلْأُولَىٰ۝١٨

    Inna hatha lafee alssuhufi aloola

    Hakika haya yamo katika Vitabu vya mwanzo,18

    Maelezo
    [18] Hakika haya yote yaliyo tajwa katika Sura hii bila ya shaka yamethibitishwa katika Vitabu vya zamani,
  19. صُحُفِ إِبْرَٰهِيمَ وَمُوسَىٰ۝١٩

    Suhufi ibraheema wamoosa

    Vitabu vya Ibrahimu na Musa.19

    Maelezo
    [19] Vitabu vya Ibrahimu na Musa; kwani haya yamewafikiana na mafunzo ya dini zote na yamesajiliwa katika Vitabu vya mbinguni.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Surat Al-A’la maana yake ni nini?

Al-A’la maana yake ni “Aliye Juu Kabisa”.

Surat Al-A’la iko katika juzuu ya ngapi?

Surat Al-A’la iko katika juzuu ya 30.

Surat Al-A’la ina aya ngapi?

Surat Al-A’la ina aya 19.

Surat Al-A’la ni ya Makka au ya Madina?

Surat Al-A’la ni sura ya Makka.

Surat Al-A’la ni sura ya ngapi katika Qur’ani?

Ni sura ya 87 katika Qur’ani.

Vyanzo

  • Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
  • Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
  • Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
  • Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
  • Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
  • Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.

Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.

Mipangilio ya kusoma

Fonti ya Qur’ani
Ukubwa wa Kiarabu
100%
Ukubwa wa tafsiri
100%
Mandhari

Ongeza kwenye skrini ya kwanza

ReadSurahFungua ReadSurah kutoka skrini ya kwanza, kwa skrini nzima. Sura ulizosoma hufunguka hata bila intaneti.

  1. Katika Safari, gusa kitufe cha kushiriki (Share). Kwenye iPhone mpya kiko kwenye menyu ya •••.
  2. Gusa “Add to Home Screen”. Huenda ukahitaji kusogeza chini.
  3. Gusa “Add”.