سورة الغاشية
Surat Al-Ghashiya kwa Kiswahili
Tukio Linalogubika
- 88
- Aya 26
- Sura ya Makka
- Juzuu 30
- Ukurasa 592
Surat Al-Ghashiya (الغاشية) ni sura ya 88 katika Qur’ani na ina aya 26. Jina lake lina maana ya “Tukio Linalogubika”. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na iko katika juzuu ya 30.
Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat Al-Ghashiya yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.
Surat Al-Ghashiya kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
-
هَلْ أَتَىٰكَ حَدِيثُ ٱلْغَـٰشِيَةِ١
Hal ataka hadeethu alghashiyati
Je! Imekufikia khabari ya msiba wa kufudikiza?1
Maelezo
[1] Je! Ewe Muhammad! Imepata kukujia hadithi ya Kiyama ambacho kwa vitisho vyake kitawafanya watu wazimie? -
وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ خَـٰشِعَةٌ٢
Wujoohun yawmaithin khashiʿatun
Siku hiyo nyuso zitainama!2
Maelezo
[2] Siku hiyo ya Kiyama zitakuwepo nyuso zimedhalilika, -
عَامِلَةٌ نَّاصِبَةٌ٣
ʿamilatun nasibatun
Zikifanya kazi, nazo taabani.3
Maelezo
[3] Zimechoka, taabani kwa shughuli na mashaka ya Motoni, -
تَصْلَىٰ نَارًا حَامِيَةً٤
Tasla naran hamiyatan
Ziingie katika Moto unao waka .4
Maelezo
[4] Zinaingia kwenye Moto unao waka kwa nguvu! -
تُسْقَىٰ مِنْ عَيْنٍ ءَانِيَةٍ٥
Tusqa min ʿaynin aniyatin
Zikinyweshwa kutoka chemchem inayo chemka.5
Maelezo
[5] Wananywesha maji yanayo toka kwenye chemchem inayo tokota. -
لَّيْسَ لَهُمْ طَعَامٌ إِلَّا مِن ضَرِيعٍ٦
Laysa lahum taʿamun illa min dareeʿin
Hawatakuwa na chakula isipo kuwa kichungu chenye miba.6
Maelezo
[6] Hawana chakula ila chakula kiovu kabisa, anaadhibika mwenye kukila. -
لَّا يُسْمِنُ وَلَا يُغْنِى مِن جُوعٍ٧
La yusminu wala yughnee min jooʿin
Hakinenepeshi wala hakiondoi njaa.7
Maelezo
[7] Hakileti nafuu yoyote katika mwili, wala hakiondoi njaa. -
وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ نَّاعِمَةٌ٨
Wujoohun yawmaithin naʿimatun
Siku hiyo nyuso nyengine zitakuwa kunjufu.8
Maelezo
[8] Na pia zitakuwapo nyuso zenye kutoa nuru Siku ya Kiyama, kwa malipo ya vitendo vyao walivyo fanya duniani. -
لِّسَعْيِهَا رَاضِيَةٌ٩
Lisaʿyiha radiyatun
Zitakuwa radhi kwa juhudi yao!9
Maelezo
[9] Hao watakuwa wameridhia kwa watayo yapata katika Pepo iliyo juu kwa pahala na cheo. -
فِى جَنَّةٍ عَالِيَةٍ١٠
Fee jannatin ʿaliyatin
Katika Bustani ya juu.10
Maelezo
[10] Katika Pepo iliyo juu kwa pahala na cheo. -
لَّا تَسْمَعُ فِيهَا لَـٰغِيَةً١١
La tasmaʿu feeha laghiyatan
Hawatasikia humo upuuzi.Humo imo chemchem inayo miminika.11
Maelezo
[11] Humo halisikilizani neno la upuuzi. -
فِيهَا عَيْنٌ جَارِيَةٌ١٢
Feeha ʿaynun jariyatun
Humo imo chemchem inayo miminika.12
Maelezo
[12] Humo mna chemchem isiyo katika. -
فِيهَا سُرُرٌ مَّرْفُوعَةٌ١٣
Feeha sururun marfooʿatun
Humo vimo viti vilivyo nyanyuliwa,13
Maelezo
[13] Humo vitakuwamo viti vilivyo nyanyuliwa kwa cheo na kwa hakika, kama ni ziada ya neema. -
وَأَكْوَابٌ مَّوْضُوعَةٌ١٤
Waakwabun mawdooʿatun
Na bilauri zilizo pangwa,14
Maelezo
[14] Na bilauri (gilasi) zilio wekwa mbele yao, -
وَنَمَارِقُ مَصْفُوفَةٌ١٥
Wanamariqu masfoofatun
Na matakia safu safu,15
Maelezo
[15] Na mito na matakia yalio pangwa kwa safu. -
وَزَرَابِىُّ مَبْثُوثَةٌ١٦
Wazarabiyyu mabthoothatun
Na mazulia yaliyo tandikwa.16
Maelezo
[16] Na mazulia mengi yaliyo tandazwa hapo barazani. -
أَفَلَا يَنظُرُونَ إِلَى ٱلْإِبِلِ كَيْفَ خُلِقَتْ١٧
Afala yanthuroona ila alibili kayfa khuliqat
Je! Hawamtazami ngamia jinsi alivyo umbwa?17
Maelezo
[17] Je! Wanapuuza kuzingatia Ishara, basi hebu na wamuangalie ngamia, vipi alivyo umbwa kwa namna ya peke yake kwa uweza wa Mwenyezi Mungu? Katika kuumbwa ngamia zipo Ishara na miujiza yenye kuthibitisha uweza wa Mwenyezi Mungu ambao yafaa wenye kuzingatia wauzingatie. Katika sifa zake zinazo onekana ni hizo zinazo mfanya kweli awe ni jahazi ya jangwani. Macho yake yamenyanyuka yako juu ya kichwa, na yanaelekea nyuma, na tena yana kope za kuyakinga na mchanga na vumbi. Kadhaalika pua na masikio yamefunikwa na nywele kwa sababu hiyo hiyo. Ukivuma mdharuba wa mchanga pua hufunga na masikio hupinda, juu ya kuwa tokea hapo ni madogo na si yenye kudhihiri mno, ukilinganisha na mwili wake. Ama miguu ni mirefu kwa kusaidia wepesi wa kwenda, pamoja na kunasibiana na urefu wa shingo yake. Ama nyayo ni pana zimetanda kwa ukhafifu ili kumwezesha ngamia kwenda juu ya mchanga laini. Na ngamia kwa jumla chini ya kifua chake na chini ya viungo vyake vya miguu pana kama mito inayo msaidia ngamia kupiga magoti na kulala juu ya ardhi ngumu na imoto, kama vile vile pande zote mbili za mkia wake yapo manyoya marefu ya kumlinda sehemu zake za nyuma na vitu vya kumuudhi. Ama vipawa alivyo pewa ngamia kwa ajili ya kazi yake ni vya ajabu zaidi. Siku za baridi hahitajii maji, bali anaweza asinywe maji muda wa miezi miwili mfululizo, ikiwa chakula kimajimaji na laini, au wiki mbili ikiwa kikavu. Pia anaweza kustahamili kiu hata siku za joto muda wa wiki au wiki mbili, na hupungua muda huo zaidi ya thuluthi mbili ya uzito wake. Na anapo yapata maji huyagugumia maji kwa wingi mno arejeshe uzito wake wa zamani kwa dakika chache tu. Na ngamia hayarimbiki maji katika tumbo lake kama ilivyo kuwa ikidhaniwa, bali katika mfumo wa mwili wake, na huyatumia kwa uangalifu mkubwa mno. Kwa hivyo kabisa hapumui kama anavyo pumua mbwa, mathalan, wala hatoi pumzi kwa mdomo wake, wala hatoki majasho kwenye ngozi yake ila kwa uchache kabisa. Na hayo ni kuwa daraja ya joto ya mwili wake inakuwa chini sana asubuhi mapema. Kisha hupanda kidogo kidogo zaidi ya daraja sita kabla ya kuhitajia kuipoza kwa jasho na kutoa mvuke. Na juu ya maji mengi mno yanayo toka katika mwili baada ya kiu kirefu kwa hakika uzito wa damu hauathiriki ila kwa kiasi tu, na kwa hivyo kiu hakina athari kitu juu yake. Na imethibiti mafuta ya nunudu yaliyo khaziniwa kwa ajili ya nishat'i yanamkifu kumkinga na machungu ya njaa, lakini hayamfaidishi sana kwa haja ya maji ambayo ni lazima kwa mwili wake. Na bado wataalamu wangali wanagundua mapya katika ngamia kila wakichungua ya kuhakikisha hadhi aliyo mpa Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwa atazamwe katika uumbaji wake wa muujiza. -
وَإِلَى ٱلسَّمَآءِ كَيْفَ رُفِعَتْ١٨
Waila alssamai kayfa rufiʿat
Na mbingu jinsi ilivyo inuliwa?18
Maelezo
[18] Na waizingatie mbingu wanayo iona daima, vipi ilivyo nyanyuliwa huko mbali bila ya nguzo! -
وَإِلَى ٱلْجِبَالِ كَيْفَ نُصِبَتْ١٩
Waila aljibali kayfa nusibat
Na milima jinsi ilivyo thibitishwa?19
Maelezo
[19] Na milima wanayo ikwea mpaka wakafika vileleni kwake, vipi ilivyo simamishwa kwa urefu, imeshikamana na ardhi, haiyumbi wala haitikisiki! -
وَإِلَى ٱلْأَرْضِ كَيْفَ سُطِحَتْ٢٠
Waila alardi kayfa sutihat
Na ardhi jinsi ilivyo tandazwa?20
Maelezo
[20] Na ardhi wanayo ikalia na kuyendea juu yake, vipi ilivyo kunjuliwa na kutandazwa! Mara nyingi katika Qur'ani tukufu inatajwa kuwa ardhi "imekunjuliwa". Na makusudio ya hayo ni kuwa ardhi ijapo kuwa ni duara kama mpira kwa sura yake, lakini inavyo onekana kwa watazamao ni kuwa imekunjuliwa. Na haya hayagongani na yaliyo thibitishwa na sayansi katika jambo lolote. -
فَذَكِّرْ إِنَّمَآ أَنتَ مُذَكِّرٌ٢١
Fathakkir innama anta muthakkirun
Basi kumbusha! Hakika wewe ni Mkumbushaji.21
Maelezo
[21] Basi kumbusha kwa wito wako, kwani kazi yako muhimu ni kufikisha wito tu. -
لَّسْتَ عَلَيْهِم بِمُصَيْطِرٍ٢٢
Lasta ʿalayhim bimusaytirin
Wewe si mwenye kuwatawalia.22
Maelezo
[22] Hukuwa mtawala juu yao. -
إِلَّا مَن تَوَلَّىٰ وَكَفَرَ٢٣
Illa man tawalla wakafara
Lakini anaye rudi nyuma na kukataa,23
Maelezo
[23] Lakini miongoni mwao ataye puuza na akakataa, -
فَيُعَذِّبُهُ ٱللَّهُ ٱلْعَذَابَ ٱلْأَكْبَرَ٢٤
Fayuʿaththibuhu Allahu alʿathaba alakbara
Basi Mwenyezi Mungu atamuadhibu kwa adhabu iliyo kubwa kabisa!24
Maelezo
[24] Basi Mwenyezi Mungu atampa adhabu iliyo kubwa kabisa, isiyo kuwa na ya kuipita. -
إِنَّ إِلَيْنَآ إِيَابَهُمْ٢٥
Inna ilayna iyabahum
Hakika ni kwetu Sisi ndio marejeo yao.25
Maelezo
[25] Hakika ni kwetu Sisi marejeo yao kwa kifo na kufufuliwa, wala hapana penginepo isipo kuwa kwetu. -
ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا حِسَابَهُم٢٦
Thumma inna ʿalayna hisabahum
Kisha hakika ni juu yetu Sisi hisabu yao!26
Maelezo
[26] Tena ni juu yetu Sisi tu peke yetu kuwahisabia na kuwalipa.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Surat Al-Ghashiya maana yake ni nini?
Al-Ghashiya maana yake ni “Tukio Linalogubika”.
Surat Al-Ghashiya iko katika juzuu ya ngapi?
Surat Al-Ghashiya iko katika juzuu ya 30.
Surat Al-Ghashiya ina aya ngapi?
Surat Al-Ghashiya ina aya 26.
Surat Al-Ghashiya ni ya Makka au ya Madina?
Surat Al-Ghashiya ni sura ya Makka.
Surat Al-Ghashiya ni sura ya ngapi katika Qur’ani?
Ni sura ya 88 katika Qur’ani.
Vyanzo
- Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
- Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
- Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
- Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
- Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
- Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.
Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.