Surat Al-Balad (البلد) ni sura ya 90 katika Qur’ani na ina aya 20. Jina lake lina maana ya “Mji”. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na iko katika juzuu ya 30.
Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat Al-Balad yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.
Surat Al-Balad kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
-
لَآ أُقْسِمُ بِهَـٰذَا ٱلْبَلَدِ١
La oqsimu bihatha albaladi
Naapa kwa Mji huu!1
Maelezo
[1] Naapa kiapo cha mkazo kwa mji wa Makka, mji mtakatifu; -
وَأَنتَ حِلٌّۢ بِهَـٰذَا ٱلْبَلَدِ٢
Waanta hillun bihatha albaladi
Nawe unaukaa Mji huu.2
Maelezo
[2] Na wewe unaishi katika mji huu, unauzidisha utukufu wake na cheo chake. -
وَوَالِدٍ وَمَا وَلَدَ٣
Wawalidin wama walada
Na naapa kwa mzazi na alicho kizaa.3
Maelezo
[3] Na naapa kwa mzazi na anacho kizaa, na kwa hao wawili ndio jinsi inahifadhika na maendeleo yanabakia. -
لَقَدْ خَلَقْنَا ٱلْإِنسَـٰنَ فِى كَبَدٍ٤
Laqad khalaqna alinsana fee kabadin
Hakika tumemuumba mtu katika taabu.4
Maelezo
[4] Hakika Sisi tumemuumba mtu katika mashaka na taabu tangu mwanzo wake mpaka kumalizika mambo yake. -
أَيَحْسَبُ أَن لَّن يَقْدِرَ عَلَيْهِ أَحَدٌ٥
Ayahsabu an lan yaqdira ʿalayhi ahadun
Ati anadhani hapana yeyote ataye muweza?5
Maelezo
[5] Je! Anadhani mtu aliye umbwa katika mashaka haya kuwa hapana awezae kumdhalilisha? -
يَقُولُ أَهْلَكْتُ مَالًا لُّبَدًا٦
Yaqoolu ahlaktu malan lubadan
Anasema: Nimeteketeza chungu ya mali.6
Maelezo
[6] Anasema: Nimetumia katika kupambana na Muhammad s.a.w. na kuupinga wito wake mali mengi ukiyakusanya pamoja. -
أَيَحْسَبُ أَن لَّمْ يَرَهُۥٓ أَحَدٌ٧
Ayahsabu an lam yarahu ahadun
Ati anadhani ya kuwa hapana yeyote anaye mwona?7
Maelezo
[7] Ati anadhani kwamba mambo yake hayo yamefichikana, hayajui yeyote hata huyo aliye muumba? -
أَلَمْ نَجْعَل لَّهُۥ عَيْنَيْنِ٨
Alam najʿal lahu ʿaynayni
Kwani hatukumpa macho mawili?8
Maelezo
[8] Kwani Sisi hatukumuumba na macho mawili ya kutazamia,? -
وَلِسَانًا وَشَفَتَيْنِ٩
Walisanan washafatayni
Na ulimi, na midomo miwili?9
Maelezo
[9] Na ulimi na midomo miwili ili aweze kutamka na kusema sawa? -
وَهَدَيْنَـٰهُ ٱلنَّجْدَيْنِ١٠
Wahadaynahu alnnajdayni
Na tukambainishia zote njia mbili?10
Maelezo
[10] Na tukamwonyesha njia ya kheri na ya shari, na tukamtengenezea aweze kuchagua mojawapo? -
فَلَا ٱقْتَحَمَ ٱلْعَقَبَةَ١١
Fala iqtahama alʿaqabata
Lakini hakujitoma kwenye njia ya vikwazo vya milimani.11
Maelezo
[11] Basi huyo hakunafiika kwa tuliyo mtengenezea, wala hakuivuka njia ya milimani inayo mzuia asifikie uwokovu, nayo ni choyo wa nafsi yake. -
وَمَآ أَدْرَىٰكَ مَا ٱلْعَقَبَةُ١٢
Wama adraka ma alʿaqabatu
Na nini kitakujuvya ni nini njia ya vikwazo vya milimani?12
Maelezo
[12] Na kitu gani kitakufunza nini huko kujitoma kwenye njia ya milimani? -
فَكُّ رَقَبَةٍ١٣
Fakku raqabatin
Kumkomboa mtumwa;13
Maelezo
[13] Kumkomboa mtu kutokana na utumwa, -
أَوْ إِطْعَـٰمٌ فِى يَوْمٍ ذِى مَسْغَبَةٍ١٤
Aw itʿamun fee yawmin thee masghabatin
Au kumlisha siku ya njaa14
Maelezo
[14] Au kumlisha siku ya njaa -
يَتِيمًا ذَا مَقْرَبَةٍ١٥
Yateeman tha maqrabatin
Yatima aliye jamaa,15
Maelezo
[15] Yatima aliye jamaa wa kumliwaza kwa ujamaa na ufakiri. -
أَوْ مِسْكِينًا ذَا مَتْرَبَةٍ١٦
Aw miskeenan tha matrabatin
Au masikini aliye vumbini.16
Maelezo
[16] Au masikini mwingi wa haja na kufakirika. -
ثُمَّ كَانَ مِنَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَتَوَاصَوْا۟ بِٱلصَّبْرِ وَتَوَاصَوْا۟ بِٱلْمَرْحَمَةِ١٧
Thumma kana mina allatheena amanoo watawasaw bialssabri watawasaw bialmarhamati
Tena awe miongoni mwa walio amini na wakausiana kusubiri na wakausiana kuhurumiana.17
Maelezo
[17] Tena awe pamoja na hayo miongoni mwa wenye Imani wanao usiana na wenzao kwa subira na kuoneana huruma. -
أُو۟لَـٰٓئِكَ أَصْحَـٰبُ ٱلْمَيْمَنَةِ١٨
Olaika ashabu almaymanati
Hao ndio watu wa kheri wa kuliani.18
Maelezo
[18] Hao wanao sifika kwa sifa hizi, ndio watu wa kheri, wa mkono wa kulia. -
وَٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَا هُمْ أَصْحَـٰبُ ٱلْمَشْـَٔمَةِ١٩
Waallatheena kafaroo biayatina hum ashabu almashamati
Lakini walio zikataa Ishara zetu, hao ndio watu wa shari wa kushotoni.19
Maelezo
[19] Na walio zikataa dalili tulizo zisimamisha kuthibitisha Haki kutoka na Kitabu na hoja zake, hao ndio wapotovu watu waovu walio kosa kheri na watapata adhabu. -
عَلَيْهِمْ نَارٌ مُّؤْصَدَةٌۢ٢٠
ʿAlayhim narun musadatun
Juu yao utakuwa Moto ulio fungiwa kila upande.20
Maelezo
[20] Juu yao utakuwa Moto ulio bebeana na milango yake ikafungwa.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Surat Al-Balad maana yake ni nini?
Al-Balad maana yake ni “Mji”.
Surat Al-Balad iko katika juzuu ya ngapi?
Surat Al-Balad iko katika juzuu ya 30.
Surat Al-Balad ina aya ngapi?
Surat Al-Balad ina aya 20.
Surat Al-Balad ni ya Makka au ya Madina?
Surat Al-Balad ni sura ya Makka.
Surat Al-Balad ni sura ya ngapi katika Qur’ani?
Ni sura ya 90 katika Qur’ani.
Vyanzo
- Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
- Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
- Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
- Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
- Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
- Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.
Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.