Surat Ash-Shams (الشمس) ni sura ya 91 katika Qur’ani na ina aya 15. Jina lake lina maana ya “Jua”. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na iko katika juzuu ya 30.
Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat Ash-Shams yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.
Surat Ash-Shams kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
-
وَٱلشَّمْسِ وَضُحَىٰهَا١
Waalshshamsi waduhaha
Naapa kwa jua na mwangaza wake!1
Maelezo
[1] Naapa kwa jua na mwangaza wake na kuchomoza kwake na kwa joto lake! -
وَٱلْقَمَرِ إِذَا تَلَىٰهَا٢
Waalqamari itha talaha
Na kwa mwezi unapo lifuatia!2
Maelezo
[2] Na kwa mwezi unapo lifuata na likawa nyuma yake kwa kutoa mwangaza baada ya kuchwa jua, -
وَٱلنَّهَارِ إِذَا جَلَّىٰهَا٣
Waalnnahari itha jallaha
Na kwa mchana unapo lidhihirisha!3
Maelezo
[3] Na kwa mchana unapo lidhihirisha jua, likaonekana wazi halikufichikana. -
وَٱلَّيْلِ إِذَا يَغْشَىٰهَا٤
Waallayli itha yaghshaha
Na kwa usiku unapo lifunika!4
Maelezo
[4] Na kwa usiku unapo lifunika jua, ukawa mwangaza wake hauonekani. -
وَٱلسَّمَآءِ وَمَا بَنَىٰهَا٥
Waalssamai wama banaha
Na kwa mbingu na kwa aliye ijenga!5
Maelezo
[5] Na kwa mbingu na kwa Mweza Mtukufu aliye inyanyua na akaijenga kwa hikima yake. -
وَٱلْأَرْضِ وَمَا طَحَىٰهَا٦
Waalardi wama tahaha
Na kwa ardhi na kwa aliye itandaza!6
Maelezo
[6] Na kwa ardhi na kwa Mweza Mtukufu aliye ikunjua kwa kila upande, na akaitengeneza kwa ajili ya utulivu, na akaifanya kama tandiko. -
وَنَفْسٍ وَمَا سَوَّىٰهَا٧
Wanafsin wama sawwaha
Na kwa nafsi na kwa aliye itengeneza!7
Maelezo
[7] Na kwa nafsi, na aliye iumba na akaiweka sawa, kwa kuipa nguvu, -
فَأَلْهَمَهَا فُجُورَهَا وَتَقْوَىٰهَا٨
Faalhamaha fujooraha wataqwaha
Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake!8
Maelezo
[8] Akaifunza jema na baya, na akaipa uweza wa kutenda itakayo katika hayo, -
قَدْ أَفْلَحَ مَن زَكَّىٰهَا٩
Qad aflaha man zakkaha
Hakika amefanikiwa aliye itakasa!9
Maelezo
[9] Hakika amefuzu mwenye kuisafisha nafsi yake kwa ut'iifu na vitendo vya kheri. -
وَقَدْ خَابَ مَن دَسَّىٰهَا١٠
Waqad khaba man dassaha
Na hakika amekhasiri aliye iviza.10
Maelezo
[10] Na hakika amekhasiri mwenye kuzificha fadhila zake, na akayaua matayarisho aliyo umbwa nayo ya kutenda kheri. -
كَذَّبَتْ ثَمُودُ بِطَغْوَىٰهَآ١١
Kaththabat thamoodu bitaghwaha
Kina Thamudi walikadhibisha kwa sababu ya upotofu wao,11
Maelezo
[11] Kina Thamudi walimkanusha Nabii wao kwa upotovu wao na jeuri zao, -
إِذِ ٱنۢبَعَثَ أَشْقَىٰهَا١٢
Ithi inbaʿatha ashqaha
Alipo simama mwovu wao mkubwa,12
Maelezo
[12] Alipo gutuka mwovu wao mkubwa kabisa kutaka kumchinja ngamia. -
فَقَالَ لَهُمْ رَسُولُ ٱللَّهِ نَاقَةَ ٱللَّهِ وَسُقْيَـٰهَا١٣
Faqala lahum rasoolu Allahi naqata Allahi wasuqyaha
Hapo Mtume wa Mwenyezi Mungu alipo waambia: Huyu ni ngamia wa Mwenyezi Mungu, mwacheni anywe maji fungu lake.13
Maelezo
[13] Saleh, Mtume wa Mwenyezi Mungu, akawaambia: Mwachilieni huyu ngamia wa Mwenyezi Mungu ale maridhawa katika ardhi ya Mwenyezi Mungu, na tahadharini msimzuie maji katika siku yake aliyo wekewa. -
فَكَذَّبُوهُ فَعَقَرُوهَا فَدَمْدَمَ عَلَيْهِمْ رَبُّهُم بِذَنۢبِهِمْ فَسَوَّىٰهَا١٤
Fakaththaboohu faʿaqarooha fadamdama ʿalayhim rabbuhum bithanbihim fasawwaha
Lakini walimkadhibisha na wakamchinja ngamia, kwa hivyo Mola wao Mlezi aliwaangamiza kwa sababu ya dhambi zao na akawafuta kabisa.14
Maelezo
[14] Wakamkadhibisha Mtume wao katika hilo onyo lake, wakamchinja. Mola wao Mlezi akazibomoa nyumba zao kwa sababu ya dhambi zao; akazisawazisha na ardhi! -
وَلَا يَخَافُ عُقْبَـٰهَا١٥
Wala yakhafu ʿuqbaha
Wala Yeye haogopi matokeo yake.15
Maelezo
[15] Wala Yeye Mwenyezi Mungu hakhofu matokeo ya adhabu hiyo, kwani hiyo ni malipo ya haki kwa yale waliyo yatenda.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Surat Ash-Shams maana yake ni nini?
Ash-Shams maana yake ni “Jua”.
Surat Ash-Shams iko katika juzuu ya ngapi?
Surat Ash-Shams iko katika juzuu ya 30.
Surat Ash-Shams ina aya ngapi?
Surat Ash-Shams ina aya 15.
Surat Ash-Shams ni ya Makka au ya Madina?
Surat Ash-Shams ni sura ya Makka.
Surat Ash-Shams ni sura ya ngapi katika Qur’ani?
Ni sura ya 91 katika Qur’ani.
Vyanzo
- Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
- Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
- Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
- Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
- Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
- Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.
Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.