Surat Al-Layl (الليل) ni sura ya 92 katika Qur’ani na ina aya 21. Jina lake lina maana ya “Usiku”. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na iko katika juzuu ya 30.
Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat Al-Layl yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.
Surat Al-Layl kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
-
وَٱلَّيْلِ إِذَا يَغْشَىٰ١
Waallayli itha yaghsha
Naapa kwa usiku unapo funika!1
Maelezo
[1] Naapa kwa usiku kinapo enea kiza chake! -
وَٱلنَّهَارِ إِذَا تَجَلَّىٰ٢
Waalnnahari itha tajalla
Na mchana unapo dhihiri!2
Maelezo
[2] Na naapa kwa mchana unapo zagaa mwangaza wake! -
وَمَا خَلَقَ ٱلذَّكَرَ وَٱلْأُنثَىٰٓ٣
Wama khalaqa alththakara waalontha
Na kwa Aliye umba dume na jike!3
Maelezo
[3] Na naapa kwa Mjuzi aliye umba viwili viwili, dume na jike, katika kila vinavyo zaliwa! -
إِنَّ سَعْيَكُمْ لَشَتَّىٰ٤
Inna saʿyakum lashatta
Hakika juhudi zenu bila ya shaka ni mbali mbali.4
Maelezo
[4] Hakika juhudi zenu bila ya shaka zimekhitalifiana; kwani wapo wenye kubahatika katika juhudi zao, na wako wasio bahatika. -
فَأَمَّا مَنْ أَعْطَىٰ وَٱتَّقَىٰ٥
Faamma man aʿta waittaqa
Ama mwenye kutoa na akamchamngu!5
Maelezo
[5] Ama mwenye kutoa katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na akamkhofu Mola wake Mlezi, na kwa hivyo akaepuka anayo yakataza, -
وَصَدَّقَ بِٱلْحُسْنَىٰ٦
Wasaddaqa bialhusna
Na akaliwafiki lilio jema!6
Maelezo
[6] Na akayakinika kufuata fadhila njema, nayo ni Imani kumuamini Mwenyezi Mungu kwa kumjua, -
فَسَنُيَسِّرُهُۥ لِلْيُسْرَىٰ٧
Fasanuyassiruhu lilyusra
Tutamsahilishia yawe mepesi.7
Maelezo
[7] Basi Sisi tutamtengenezea awe katika khulka ya wepesi na raha kwa kumwongoza kwenye njia ya kheri. -
وَأَمَّا مَنۢ بَخِلَ وَٱسْتَغْنَىٰ٨
Waamma man bakhila waistaghna
Na ama mwenye kufanya ubakhili, na asiwe na haja ya wenzake!8
Maelezo
[8] Ama mwenye kufanya ubakhili kwa mali yake asitoe haki ya Mwenyezi Mungu iliomo humo, na akawa hana haja na yatokayo kwa Mwenyezi Mungu, -
وَكَذَّبَ بِٱلْحُسْنَىٰ٩
Wakaththaba bialhusna
Na akakanusha lilio jema!9
Maelezo
[9] Na akakadhibisha khulka nzuri, -
فَسَنُيَسِّرُهُۥ لِلْعُسْرَىٰ١٠
Fasanuyassiruhu lilʿusra
Tutamsahilishia yawe mazito!10
Maelezo
[10] Basi huyo tutamtengenezea khulka ambayo inapelekea uzito na mashaka ya milele. -
وَمَا يُغْنِى عَنْهُ مَالُهُۥٓ إِذَا تَرَدَّىٰٓ١١
Wama yughnee ʿanhu maluhu itha taradda
Na mali yake yatamfaa nini atapo kuwa anadidimia?11
Maelezo
[11] Na kitu gani katika adhabu ambacho hayo mali yake yataweza kumkinga nacho, atapo teketea yeye mwenyewe mzima? -
إِنَّ عَلَيْنَا لَلْهُدَىٰ١٢
Inna ʿalayna lalhuda
Hakika ni juu yetu kuonyesha uwongofu.12
Maelezo
[12] Hakika ni juu yetu, Sisi, kwa kufuatana na hikima yetu, ndio tuwabainishie viumbe njia ya uwongofu. -
وَإِنَّ لَنَا لَلْـَٔاخِرَةَ وَٱلْأُولَىٰ١٣
Wainna lana lalakhirata waaloola
Na hakika ni yetu Sisi Akhera na dunia.13
Maelezo
[13] Na juu yetu Sisi peke yetu, bila ya shaka, hili jambo la kuendesha yaliomo duniani na Akhera. -
فَأَنذَرْتُكُمْ نَارًا تَلَظَّىٰ١٤
Faanthartukum naran talaththa
Basi nakuonyeni na Moto unao waka!14
Maelezo
[14] Ndio maana tukakutieni khofu ya Moto unao waka na kuripuka! -
لَا يَصْلَىٰهَآ إِلَّا ٱلْأَشْقَى١٥
La yaslaha illa alashqa
Hatauingia ila mwovu kabisa!15
Maelezo
[15] Hawauingii kwa kudumu ila kafiri -
ٱلَّذِى كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ١٦
Allathee kaththaba watawalla
Anaye kadhibisha na kupa mgongo.16
Maelezo
[16] Aliye ikadhibisha Haki na akazipuuza Ishara za Mola wake Mlezi. -
وَسَيُجَنَّبُهَا ٱلْأَتْقَى١٧
Wasayujannabuha alatqa
Na mchamngu ataepushwa nao,17
Maelezo
[17] Na atakuwa mbali na huo Moto aliye mwingi wa kujikinga na ukafiri na maasi, -
ٱلَّذِى يُؤْتِى مَالَهُۥ يَتَزَكَّىٰ١٨
Allathee yutee malahu yatazakka
Ambaye hutoa mali yake kwa ajili ya kujitakasa.18
Maelezo
[18] Amabye hutoa mali yake wakati wa nafasi ili kujisafisha na uchafu wa ubakhili, na najsi ya uchoyo. -
وَمَا لِأَحَدٍ عِندَهُۥ مِن نِّعْمَةٍ تُجْزَىٰٓ١٩
Wama liahadin ʿindahu min niʿmatin tujza
Na wala si kwa kuwa yupo yeyote aliye mfanyia hisani ndio anamlipa.19
Maelezo
[19] Na mtoaji huyu si kama anaye mtu yeyote ambaye ndio anamlipa kwa neema aliyo mfanyia zamani, -
إِلَّا ٱبْتِغَآءَ وَجْهِ رَبِّهِ ٱلْأَعْلَىٰ٢٠
Illa ibtighaa wajhi rabbihi alaʿla
Ila ni kutaka radhi ya Mola wake Mlezi aliye juu kabisa.20
Maelezo
[20] Bali anatoa hicho kwa kutafuta radhi ya Mola wake Mlezi Mtukufu tu. -
وَلَسَوْفَ يَرْضَىٰ٢١
Walasawfa yarda
Naye atakuja ridhika!21
Maelezo
[21] Na bila ya shaka atakuja pata kutoka kwa Mola wake Mlezi anacho kitaka kwa njia za ukamilifu kabisa, hata itimie radhi kwake.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Surat Al-Layl maana yake ni nini?
Al-Layl maana yake ni “Usiku”.
Surat Al-Layl iko katika juzuu ya ngapi?
Surat Al-Layl iko katika juzuu ya 30.
Surat Al-Layl ina aya ngapi?
Surat Al-Layl ina aya 21.
Surat Al-Layl ni ya Makka au ya Madina?
Surat Al-Layl ni sura ya Makka.
Surat Al-Layl ni sura ya ngapi katika Qur’ani?
Ni sura ya 92 katika Qur’ani.
Vyanzo
- Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
- Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
- Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
- Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
- Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
- Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.
Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.