Surat Ash-Sharh (الشرح) ni sura ya 94 katika Qur’ani na ina aya 8. Jina lake lina maana ya “Faraja”. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na iko katika juzuu ya 30.
Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat Ash-Sharh yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.
Surat Ash-Sharh kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
-
أَلَمْ نَشْرَحْ لَكَ صَدْرَكَ١
Alam nashrah laka sadraka
Hatukukunjulia kifua chako?1
Maelezo
[1] Hakika tumekukunjulia kifua chako kwa kuwa tulitia ndani yake Uwongofu na Imani. -
وَوَضَعْنَا عَنكَ وِزْرَكَ٢
Wawadaʿna ʿanka wizraka
Na tukakuondolea mzigo wako!2
Maelezo
[2] Na tumekupunguzia mizigo iliyo kuwa mizito juu ya mgongo wako, kwa kukuunga mkono na kukusahilishia mambo yako, -
ٱلَّذِىٓ أَنقَضَ ظَهْرَكَ٣
Allathee anqada thahraka
Ulio vunja mgongo wako?3
Maelezo
[3] Ambayo yalikuwa ni mazito juu ya mgongo wako. -
وَرَفَعْنَا لَكَ ذِكْرَكَ٤
Warafaʿna laka thikraka
Na tukakunyanyulia utajo wako?4
Maelezo
[4] Na tumelitukuza jina lako, tukalifanya linatajwa na ulimi wa kila Muumini pamoja na jina letu. -
فَإِنَّ مَعَ ٱلْعُسْرِ يُسْرًا٥
Fainna maʿa alʿusri yusran
Basi kwa hakika pamoja na uzito upo wepesi!5
Maelezo
[5] Hizo ni baadhi ya neema zetu juu yako. Basi kuwa na yakini na uweza wa Mwenyezi Mtukufu, kwani pamoja na uzito upo wepesi mwingi unao kuja nao. -
إِنَّ مَعَ ٱلْعُسْرِ يُسْرًا٦
Inna maʿa alʿusri yusran
Hakika pamoja na uzito upo wepesi.6
Maelezo
[6] Hakika pamoja na uzito (wakati huo huo ijapo kuwa wewe hujui), upo wepesi mwingi vile vile. -
فَإِذَا فَرَغْتَ فَٱنصَبْ٧
Faitha faraghta fainsab
Na ukipata faragha, fanya juhudi.7
Maelezo
[7] Basi ukipata nafasi katika kazi ya kuwalingania watu, na mambo yaliyo khusiana na Jihadi, endelea na jitihada ya ibada na jishughulishe nafsi yako katika hayo. -
وَإِلَىٰ رَبِّكَ فَٱرْغَب٨
Waila rabbika fairghab
Na Mola wako Mlezi ndio mshughulikie.8
Maelezo
[8] Kwa Mola wako Mlezi tu ndio uelekee kwa kumwomba na kumhitajia.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Surat Ash-Sharh maana yake ni nini?
Ash-Sharh maana yake ni “Faraja”.
Surat Ash-Sharh iko katika juzuu ya ngapi?
Surat Ash-Sharh iko katika juzuu ya 30.
Surat Ash-Sharh ina aya ngapi?
Surat Ash-Sharh ina aya 8.
Surat Ash-Sharh ni ya Makka au ya Madina?
Surat Ash-Sharh ni sura ya Makka.
Surat Ash-Sharh ni sura ya ngapi katika Qur’ani?
Ni sura ya 94 katika Qur’ani.
Vyanzo
- Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
- Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
- Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
- Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
- Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
- Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.
Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.