سورة العلق

Surat Al-Alaq kwa Kiswahili

Pande la Damu

Msahafu

Mishary Rashid AlafasyPakua MP3Pakua PDF

Surat Al-Alaq (العلق) ni sura ya 96 katika Qur’ani na ina aya 19. Jina lake lina maana ya “Pande la Damu”. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na iko katika juzuu ya 30.

Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat Al-Alaq yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.

Surat Al-Alaq kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

  1. ٱقْرَأْ بِٱسْمِ رَبِّكَ ٱلَّذِى خَلَقَ۝١

    Iqra biismi rabbika allathee khalaqa

    Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba!1

    Maelezo
    [1] Ewe Muhammad! Soma unayo funuliwa kwa kufunguliwa kwa Jina la Mola wako Mlezi ambaye ni Yeye tu peke yake ndiye Mwenye uweza wa kuumba.
  2. خَلَقَ ٱلْإِنسَـٰنَ مِنْ عَلَقٍ۝٢

    Khalaqa alinsana min ʿalaqin

    Amemuumba binaadamu kwa tone la damu!2

    Maelezo
    [2] Amemuumba mtu kwa ukamilifu wa mwili wake na ilimu kutokana na kipande cha damu ambacho hakina chochote cha kupelekea kujiona bora.
  3. ٱقْرَأْ وَرَبُّكَ ٱلْأَكْرَمُ۝٣

    Iqra warabbuka alakramu

    Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote!3

    Maelezo
    [3] Endelea na kusoma, na Mola wako Mlezi aliye Karimu kushinda wote, atakutukuza wala hatakudharau.
  4. ٱلَّذِى عَلَّمَ بِٱلْقَلَمِ۝٤

    Allathee ʿallama bialqalami

    Ambaye amefundisha kwa kalamu.4

    Maelezo
    [4] Yeye ndiye ambaye aliye mfunza mtu kuandika kwa kalamu, na wala kwanza hakuwa anajua hayo.
  5. عَلَّمَ ٱلْإِنسَـٰنَ مَا لَمْ يَعْلَمْ۝٥

    ʿAllama alinsana ma lam yaʿlam

    Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui.5

    Maelezo
    [5] Amemfunza mtu yasiyo kuwa yanampitia katika mawazo yake.
  6. كَلَّآ إِنَّ ٱلْإِنسَـٰنَ لَيَطْغَىٰٓ۝٦

    Kalla inna alinsana layatgha

    Kwani! Hakika mtu bila ya shaka huwa jeuri.6

    Maelezo
    [6] Ni hakika kweli mtu hupindukia mpaka na hupanda kiburi mbele ya Mola wake Mlezi
  7. أَن رَّءَاهُ ٱسْتَغْنَىٰٓ۝٧

    An raahu istaghna

    Akijiona katajirika.7

    Maelezo
    [7] Anapo jiona si mhitaji, katajirika.
  8. إِنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ ٱلرُّجْعَىٰٓ۝٨

    Inna ila rabbika alrrujʿa

    Hakika kwa Mola wako Mlezi ndio marejeo.8

    Maelezo
    [8] Ewe Muhammad! Hakika ni kwa Mola wako Mlezi peke yake ndiyo yako marejeo ya wote kwa kufufuliwa na kulipwa.
  9. أَرَءَيْتَ ٱلَّذِى يَنْهَىٰ۝٩

    Araayta allathee yanha

    Umemwona yule anaye mkataza.9

    Maelezo
    [9] Je! Umemwona huyu jeuri
  10. عَبْدًا إِذَا صَلَّىٰٓ۝١٠

    ʿAbdan itha salla

    Mja anapo sali?10

    Maelezo
    [10] Anaye mzuia mja asisali anapo taka kusali?
  11. أَرَءَيْتَ إِن كَانَ عَلَى ٱلْهُدَىٰٓ۝١١

    Araayta in kana ʿala alhuda

    Umeona kama yeye yuko juu ya uwongofu?11

    Maelezo
    [11] Hebu niambie khabari za jeuri huyu kama yeye yumo katika uwongofu katika huku kuzuia kwake,
  12. أَوْ أَمَرَ بِٱلتَّقْوَىٰٓ۝١٢

    Aw amara bialttaqwa

    Au anaamrisha uchamngu?12

    Maelezo
    [12] Au kwamba ndio anaamrisha uchamngu katika hayo anayo amrisha!
  13. أَرَءَيْتَ إِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰٓ۝١٣

    Araayta in kaththaba watawalla

    Umeona kama yeye akikanusha na anarudi nyuma?13

    Maelezo
    [13] Niambie khabari za huyu mwenye kukataza anapo yakadhibisha aliyo kuja nayo Mtume, na akapuuza Imani na vitendo vyema!
  14. أَلَمْ يَعْلَم بِأَنَّ ٱللَّهَ يَرَىٰ۝١٤

    Alam yaʿlam bianna Allaha yara

    Hajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anaona?14

    Maelezo
    [14] Hivyo hajui kwamba Mwenyezi Mungu anazijua vyema hali zake, naye atamlipa kwazo?
  15. كَلَّا لَئِن لَّمْ يَنتَهِ لَنَسْفَعًۢا بِٱلنَّاصِيَةِ۝١٥

    Kalla lain lam yantahi lanasfaʿan bialnnasiyati

    Kwani! Kama haachi, tutamkokota kwa shungi la nywele!15

    Maelezo
    [15] Kwa kumkemea huyu mwenye kuzuia, anaambiwa kama hakuacha hayo anayo yafanya, basi hapana shaka tutamkokota kwa nguvu tukimshika kwa shungi lake la nywele mpaka Motoni!
  16. نَاصِيَةٍ كَـٰذِبَةٍ خَاطِئَةٍ۝١٦

    Nasiyatin kathibatin khatiatin

    Shungi la uwongo, lenye makosa!16

    Maelezo
    [16] Hilo shungi lilio juu ya uso wake mwenye kuropokwa uwongo na mwenye athari za ukosefu!
  17. فَلْيَدْعُ نَادِيَهُۥ۝١٧

    Falyadʿu nadiyahu

    Basi na awaite wenzake!17

    Maelezo
    [17] Basi yeye awaite wenziwe na watu wa baraza lake wawe ndio wasaidizi duniani au Akhera.
  18. سَنَدْعُ ٱلزَّبَانِيَةَ۝١٨

    Sanadʿu alzzabaniyata

    Nasi tutawaita Mazabania!18

    Maelezo
    [18] Sisi tutawaita askari wetu wamsaidie Muhammad na walio pamoja naye, na wapambane na huyo mwenye kukanya na wasaidizi wawasukume kwenye Jahannamu!
  19. كَلَّا لَا تُطِعْهُ وَٱسْجُدْ وَٱقْتَرِب ۩۝١٩

    Kalla la tutiʿhu waosjud waiqtarib

    Hasha! Usimt'ii! Nawe sujudu na ujongee!19

    Maelezo
    [19] Kumnyamazisha huyu mwenye kuzuia, wewe usimkubalie kwa hayo anayo kukataza nayo, na dumu juu ya Swala zako, na endelea na sijida zako, na jijongeze kwa Mola wako Mlezi kwa hivyo.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Surat Al-Alaq maana yake ni nini?

Al-Alaq maana yake ni “Pande la Damu”.

Surat Al-Alaq iko katika juzuu ya ngapi?

Surat Al-Alaq iko katika juzuu ya 30.

Surat Al-Alaq ina aya ngapi?

Surat Al-Alaq ina aya 19.

Surat Al-Alaq ni ya Makka au ya Madina?

Surat Al-Alaq ni sura ya Makka.

Surat Al-Alaq ni sura ya ngapi katika Qur’ani?

Ni sura ya 96 katika Qur’ani.

Vyanzo

  • Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
  • Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
  • Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
  • Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
  • Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
  • Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.

Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.

Mipangilio ya kusoma

Fonti ya Qur’ani
Ukubwa wa Kiarabu
100%
Ukubwa wa tafsiri
100%
Mandhari

Ongeza kwenye skrini ya kwanza

ReadSurahFungua ReadSurah kutoka skrini ya kwanza, kwa skrini nzima. Sura ulizosoma hufunguka hata bila intaneti.

  1. Katika Safari, gusa kitufe cha kushiriki (Share). Kwenye iPhone mpya kiko kwenye menyu ya •••.
  2. Gusa “Add to Home Screen”. Huenda ukahitaji kusogeza chini.
  3. Gusa “Add”.