سورة البينة
Surat Al-Bayyina kwa Kiswahili
Hoja Iliyo Wazi
- 98
- Aya 8
- Sura ya Madina
- Juzuu 30
- Kurasa 598–599
Surat Al-Bayyina (البينة) ni sura ya 98 katika Qur’ani na ina aya 8. Jina lake lina maana ya “Hoja Iliyo Wazi”. Ni sura ya Madina, iliyoteremshwa Madina baada ya Hijra, na iko katika juzuu ya 30.
Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat Al-Bayyina yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.
Surat Al-Bayyina kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
-
لَمْ يَكُنِ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ مِنْ أَهْلِ ٱلْكِتَـٰبِ وَٱلْمُشْرِكِينَ مُنفَكِّينَ حَتَّىٰ تَأْتِيَهُمُ ٱلْبَيِّنَةُ١
Lam yakuni allatheena kafaroo min ahli alkitabi waalmushrikeena munfakkeena hatta tatiyahumu albayyinatu
Hawakuwa walio kufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu na washirikina waache walio nayo mpaka iwajie bayana!1
Maelezo
[1] Hawakuwa walio mkataa Mwenyezi Mungu na Mtume wake miongoni mwa Mayahudi na Wakristo, na miongoni mwa washirikina, waache kughafilika kwao na ujinga wao kuto ijua Haki mpaka iwajie hoja ya kukata. -
رَسُولٌ مِّنَ ٱللَّهِ يَتْلُوا۟ صُحُفًا مُّطَهَّرَةً٢
Rasoolun mina Allahi yatloo suhufan mutahharatan
Yaani Mtume aliye toka kwa Mwenyezi Mungu anaye wasomea kurasa zilizo takasika!2
Maelezo
[2] Na hoja hiyo ni Mtume aliye tumwa kutokana na Mwenyezi Mungu awasomee kurasa zilizo takasika na upotovu, -
فِيهَا كُتُبٌ قَيِّمَةٌ٣
Feeha kutubun qayyimatun
Ndani yake mna maandiko yaliyo nyooka.3
Maelezo
[3] Ndani yake zimo hukumu zilizo sawa zenye kutamka kwa haki na kwa yaliyo ndiyo. -
وَمَا تَفَرَّقَ ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْكِتَـٰبَ إِلَّا مِنۢ بَعْدِ مَا جَآءَتْهُمُ ٱلْبَيِّنَةُ٤
Wama tafarraqa allatheena ootoo alkitaba illa min baʿdi ma jaathumu albayyinatu
Wala hawakufarikiana walio pewa Kitabu ila baada ya kuwajia hiyo bayana.4
Maelezo
[4] Wala hawakufarikiana walio pewa Kitabu katika Mayahudi na Wakristo, ila baada ya kuwajia hiyo hoja iliyo wazi yenye kuonyesha ya kwamba Muhammad ndiye huyo Mtume wa Mwenyezi Mungu aliye ahidiwa katika Vitabu vyao. -
وَمَآ أُمِرُوٓا۟ إِلَّا لِيَعْبُدُوا۟ ٱللَّهَ مُخْلِصِينَ لَهُ ٱلدِّينَ حُنَفَآءَ وَيُقِيمُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ وَيُؤْتُوا۟ ٱلزَّكَوٰةَ ۚ وَذَٰلِكَ دِينُ ٱلْقَيِّمَةِ٥
Wama omiroo illa liyaʿbudoo Allaha mukhliseena lahu alddeena hunafaa wayuqeemoo alssalata wayutoo alzzakata wathalika deenu alqayyimati
Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia Dini, wawe waongofu, na washike Swala, na watoe Zaka. Na hiyo ndiyo Dini madhubuti.5
Maelezo
[5] Na hawakulazimishwa jambo katika walio lazimishwa ila iwe ibada yao kwa Mwenyezi Mungu ni kumsafia Yeye Dini, waache upotovu wasimame sawa kwenye Haki, na wazihifadhi Swala, na watoe Zaka. Na hiyo ndiyo Mila Iliyo Nyooka. -
إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ مِنْ أَهْلِ ٱلْكِتَـٰبِ وَٱلْمُشْرِكِينَ فِى نَارِ جَهَنَّمَ خَـٰلِدِينَ فِيهَآ ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ هُمْ شَرُّ ٱلْبَرِيَّةِ٦
Inna allatheena kafaroo min ahli alkitabi waalmushrikeena fee nari jahannama khalideena feeha olaika hum sharru albariyyati
Hakika walio kufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu na washirikina wataingia katika Moto wa Jahannamu wadumu milele humo. Hao ndio viumbe waovu kabisa.6
Maelezo
[6] Hakika wale walio kufuru katika Watu wa Kitabu na washirikina wataingia katika Moto wa Jahannamu, wala hawatatoka humo. Hao ndio waovu wa viumbe kwa itikadi na vitendo. -
إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ أُو۟لَـٰٓئِكَ هُمْ خَيْرُ ٱلْبَرِيَّةِ٧
Inna allatheena amanoo waʿamiloo alssalihati olaika hum khayru albariyyati
Hakika walio amini na wakatenda mema, hao ndio bora wa viumbe.7
Maelezo
[7] Hakika wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na wakatenda vitendo vyema, hao ndio bora ya viumbe kwa itikadi na vitendo. -
جَزَآؤُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ جَنَّـٰتُ عَدْنٍ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَـٰرُ خَـٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدًا ۖ رَّضِىَ ٱللَّهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا۟ عَنْهُ ۚ ذَٰلِكَ لِمَنْ خَشِىَ رَبَّهُۥ٨
Jazaohum ʿinda rabbihim jannatu ʿadnin tajree min tahtiha alanharu khalideena feeha abadan radiya Allahu ʿanhum waradoo ʿanhu thalika liman khashiya rabbahu
Malipo yao kwa Mola wao Mlezi ni Bustani za daima, zipitazo mito kati yake. Wakae humo milele. Mwenyezi Mungu yu radhi nao, na wao waradhi naye. Hayo ni kwa anaye mwogopa Mola wake Mlezi.8
Maelezo
[8] Malipo yao Akhera kwa Imani na vitendo vyema walivyo vitanguliza, ni Mabustani ya kudumu yenye kupitiwa na mito kati yake, watakaa humo milele. Mwenyezi Mungu amepokea a'mali zao, na wao watamshukuru kwa hisani yake aliyo wafanyia. Hiyo ndiyo jaza ya mwenye kuiogopa adhabu ya Mola wake Mlezi, akaamini na akatenda mema.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Surat Al-Bayyina maana yake ni nini?
Al-Bayyina maana yake ni “Hoja Iliyo Wazi”.
Surat Al-Bayyina iko katika juzuu ya ngapi?
Surat Al-Bayyina iko katika juzuu ya 30.
Surat Al-Bayyina ina aya ngapi?
Surat Al-Bayyina ina aya 8.
Surat Al-Bayyina ni ya Makka au ya Madina?
Surat Al-Bayyina ni sura ya Madina.
Surat Al-Bayyina ni sura ya ngapi katika Qur’ani?
Ni sura ya 98 katika Qur’ani.
Vyanzo
- Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
- Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
- Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
- Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
- Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
- Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.
Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.