سورة الزلزلة

Surat Az-Zalzala kwa Kiswahili

Tetemeko la Ardhi

Msahafu

Mishary Rashid AlafasyPakua MP3Pakua PDF

Surat Az-Zalzala (الزلزلة) ni sura ya 99 katika Qur’ani na ina aya 8. Jina lake lina maana ya “Tetemeko la Ardhi”. Ni sura ya Madina, iliyoteremshwa Madina baada ya Hijra, na iko katika juzuu ya 30.

Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat Az-Zalzala yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.

Surat Az-Zalzala kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

  1. إِذَا زُلْزِلَتِ ٱلْأَرْضُ زِلْزَالَهَا۝١

    Itha zulzilati alardu zilzalaha

    Itakapo tetemeshwa ardhi kwa mtetemeko wake!1

    Maelezo
    [1] Ikitisika ardhi kwa mtikiso mkubwa, na ikasukika kwa ukomo wa kutisika na kusukika kunako mkinika na ikaweza kuchukua!
  2. وَأَخْرَجَتِ ٱلْأَرْضُ أَثْقَالَهَا۝٢

    Waakhrajati alardu athqalaha

    Na itakapo toa ardhi mizigo yake!2

    Maelezo
    [2] Na ardhi ikatoa yote yaliomo katika ndani ya tumbo lake, ikiwa khazina au maiti walio kwisha zikwa!
  3. وَقَالَ ٱلْإِنسَـٰنُ مَا لَهَا۝٣

    Waqala alinsanu ma laha

    Na mtu akasema: Ina nini?3

    Maelezo
    [3] Na binaadamu akasema kwa kushtuka na khofu: Ardhi hii ina nini hata inatikisika hivi, na inatoa vilivyomo tumboni mwake, ndio Saa imefika?
  4. يَوْمَئِذٍ تُحَدِّثُ أَخْبَارَهَا۝٤

    Yawmaithin tuhaddithu akhbaraha

    Siku hiyo itahadithia khabari zake.4

    Maelezo
    [4] Siku hiyo ardhi itamsimulia mtu khabari zake zilio mshitua,
  5. بِأَنَّ رَبَّكَ أَوْحَىٰ لَهَا۝٥

    Bianna rabbaka awha laha

    Kwa sababu Mola wake Mlezi ameifunulia!5

    Maelezo
    [5] Kwani Mlezi wake na Muumba wake atakuwa kaifunulia, kaipa Wahyi, na kaiamuru itetemeke na ijisuke suke, ndio ikafanya upesi kutekeleza amri.
  6. يَوْمَئِذٍ يَصْدُرُ ٱلنَّاسُ أَشْتَاتًا لِّيُرَوْا۟ أَعْمَـٰلَهُمْ۝٦

    Yawmaithin yasduru alnnasu ashtatan liyuraw aʿmalahum

    Siku hiyo watu watatoka kwa mfarakano wakaonyweshwe vitendo vyao!6

    Maelezo
    [6] Siku hiyo watu watatoka makaburini mbio, nao wamo katika mtafaruku, wapate kuziona hisabu zao na malipo yao aliyo waahidi Mwenyezi Mungu.
  7. فَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ خَيْرًا يَرَهُۥ۝٧

    Faman yaʿmal mithqala tharratin khayran yarahu

    Basi anaye tenda chembe ya wema, atauona!7

    Maelezo
    [7] Basi mwenye kufanya hata kitu chenye uzito wa punje ya mchanga cha kheri ataiona katika daftari lake, na atapata malipo yake.
  8. وَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ شَرًّا يَرَهُۥ۝٨

    Waman yaʿmal mithqala tharratin sharran yarahu

    Na anaye tenda chembe ya uovu atauona!8

    Maelezo
    [8] Na mwenye kufanya shari ya uzito wa chembe ya mchanga ataiona kadhaalika, na atapata malipo yake. Wala Mola wako Mlezi hatamdhulumu yeyote.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Surat Az-Zalzala maana yake ni nini?

Az-Zalzala maana yake ni “Tetemeko la Ardhi”.

Surat Az-Zalzala iko katika juzuu ya ngapi?

Surat Az-Zalzala iko katika juzuu ya 30.

Surat Az-Zalzala ina aya ngapi?

Surat Az-Zalzala ina aya 8.

Surat Az-Zalzala ni ya Makka au ya Madina?

Surat Az-Zalzala ni sura ya Madina.

Surat Az-Zalzala ni sura ya ngapi katika Qur’ani?

Ni sura ya 99 katika Qur’ani.

Vyanzo

  • Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
  • Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
  • Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
  • Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
  • Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
  • Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.

Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.

Mipangilio ya kusoma

Fonti ya Qur’ani
Ukubwa wa Kiarabu
100%
Ukubwa wa tafsiri
100%
Mandhari

Ongeza kwenye skrini ya kwanza

ReadSurahFungua ReadSurah kutoka skrini ya kwanza, kwa skrini nzima. Sura ulizosoma hufunguka hata bila intaneti.

  1. Katika Safari, gusa kitufe cha kushiriki (Share). Kwenye iPhone mpya kiko kwenye menyu ya •••.
  2. Gusa “Add to Home Screen”. Huenda ukahitaji kusogeza chini.
  3. Gusa “Add”.