سورة العاديات
Surat Al-Adiyat kwa Kiswahili
Farasi Wendao Mbio
- 100
- Aya 11
- Sura ya Makka
- Juzuu 30
- Kurasa 599–600
Surat Al-Adiyat (العاديات) ni sura ya 100 katika Qur’ani na ina aya 11. Jina lake lina maana ya “Farasi Wendao Mbio”. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na iko katika juzuu ya 30.
Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat Al-Adiyat yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.
Surat Al-Adiyat kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
-
وَٱلْعَـٰدِيَـٰتِ ضَبْحًا١
Waalʿadiyati dabhan
Naapa kwa farasi wendao mbio wakipumua,1
Maelezo
[1] Ninaapa kwa farasi wa Jihadi wendao mbio, na huku pumzi zao zinasikilizana kwa sauti inayo itwa "Dh'abh'an". -
فَٱلْمُورِيَـٰتِ قَدْحًا٢
Faalmooriyati qadhan
Na wakitoa moto kwa kupiga kwato zao chini,2
Maelezo
[2] Na kwa farasi hao ambao hutoa cheche za moto zinapo gonga kwato zao kwenye ardhi wanapo kwenda. -
فَٱلْمُغِيرَٰتِ صُبْحًا٣
Faalmugheerati subhan
Wakishambulia wakati wa asubuhi,3
Maelezo
[3] Na kwa farasi hao wanao washambulia maadui asubuhi kabla jua halijachomoza; -
فَأَثَرْنَ بِهِۦ نَقْعًا٤
Faatharna bihi naqʿan
Huku wakitimua vumbi,4
Maelezo
[4] Wakatimua mavumbia mengi, farasi hao, kati ya makundi ya maadui! -
فَوَسَطْنَ بِهِۦ جَمْعًا٥
Fawasatna bihi jamʿan
Na wakijitoma kati ya kundi,5
Maelezo
[5] Ikawa vumbi limewagubika maadui hata wakaingiwa kiwewe na kufazaika. -
إِنَّ ٱلْإِنسَـٰنَ لِرَبِّهِۦ لَكَنُودٌ٦
Inna alinsana lirabbihi lakanoodun
Hakika mwanaadamu ni mtovu wa fadhila kwa Mola wake Mlezi!6
Maelezo
[6] Hakika mwanaadamu ni mwingi wa kuzikufuru neema za Mola wake Mlezi ambazo hazikadiriki. -
وَإِنَّهُۥ عَلَىٰ ذَٰلِكَ لَشَهِيدٌ٧
Wainnahu ʿala thalika lashaheedun
Na hakika yeye mwenyewe bila ya shaka ni shahidi wa hayo!7
Maelezo
[7] Na hakika yeye mwenyewe bila ya shaka atakuwa mwingi wa kuja jishuhudia huko Akhera kwa kuungama madhambi yake. -
وَإِنَّهُۥ لِحُبِّ ٱلْخَيْرِ لَشَدِيدٌ٨
Wainnahu lihubbi alkhayri lashadeedun
Naye hakika bila ya shaka ana nguvu za kupenda mali!8
Maelezo
[8] Na hakika yeye kwa uchoyo na kuyapenda mali alio nayo, ni bakhili, hatoi kama inavyo mwajibikia katika mali yake. -
۞ أَفَلَا يَعْلَمُ إِذَا بُعْثِرَ مَا فِى ٱلْقُبُورِ٩
Afala yaʿlamu itha buʿthira ma fee alquboori
Kwani hajui watakapo fufuliwa waliomo makaburini?9
Maelezo
[9] Kwani hajui mwisho wa hali yake, hata hajui wakitolewa maiti waliomo makaburini, -
وَحُصِّلَ مَا فِى ٱلصُّدُورِ١٠
Wahussila ma fee alssudoori
Na yakakusanywa yaliomo vifuani?10
Maelezo
[10] Na vikakusanywa viliomo vifuani navyo vimekwisha sajiliwa katika madaftari yao, yakiwa mema au mabaya waliyo yatenda? -
إِنَّ رَبَّهُم بِهِمْ يَوْمَئِذٍ لَّخَبِيرٌۢ١١
Inna rabbahum bihim yawmaithin lakhabeerun
Kuwa hakika Mola wao Mlezi siku hiyo bila ya shaka atakuwa na khabari zao wote!11
Maelezo
[11] Kwamba hakika Mlezi wao na Muumba wao bila ya shaka anajua vyema vitendo vyao na malipo yao Siku ya Kufufuliwa na Kulipwa.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Surat Al-Adiyat maana yake ni nini?
Al-Adiyat maana yake ni “Farasi Wendao Mbio”.
Surat Al-Adiyat iko katika juzuu ya ngapi?
Surat Al-Adiyat iko katika juzuu ya 30.
Surat Al-Adiyat ina aya ngapi?
Surat Al-Adiyat ina aya 11.
Surat Al-Adiyat ni ya Makka au ya Madina?
Surat Al-Adiyat ni sura ya Makka.
Surat Al-Adiyat ni sura ya ngapi katika Qur’ani?
Ni sura ya 100 katika Qur’ani.
Vyanzo
- Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
- Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
- Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
- Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
- Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
- Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.
Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.