سورة القارعة

Surat Al-Qari’a kwa Kiswahili

Janga Kubwa

Msahafu

Mishary Rashid AlafasyPakua MP3Pakua PDF

Surat Al-Qari’a (القارعة) ni sura ya 101 katika Qur’ani na ina aya 11. Jina lake lina maana ya “Janga Kubwa”. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na iko katika juzuu ya 30.

Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat Al-Qari’a yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.

Surat Al-Qari’a kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

  1. ٱلْقَارِعَةُ۝١

    Alqariʿatu

    Inayo gonga!1

    Maelezo
    [1] AL-QAARIA'H, Inayo gonga, ni Kiyama, ambacho kinaanza kwa mpulizo wa mwanzo wa barugumu, na kinaishia itapo katwa hukumu baina ya watu.
  2. مَا ٱلْقَارِعَةُ۝٢

    Ma alqariʿatu

    Nini Inayo gonga?2

    Maelezo
    [2] Kitu gani kilicho cha ajabu zaidi katika ukuu wake, na khatari zake na kitisho chake!
  3. وَمَآ أَدْرَىٰكَ مَا ٱلْقَارِعَةُ۝٣

    Wama adraka ma alqariʿatu

    Na nini kitacho kujuilisha nini Inayo gonga?3

    Maelezo
    [3] Na kitu gani kitacho kujuulisha hali ya AL-QAARIA'H katika kitisho chake juu ya nafsi za watu?
  4. يَوْمَ يَكُونُ ٱلنَّاسُ كَٱلْفَرَاشِ ٱلْمَبْثُوثِ۝٤

    Yawma yakoonu alnnasu kaalfarashi almabthoothi

    Siku ambayo watu watakuwa kama nondo walio tawanyika;4

    Maelezo
    [4] Siku hiyo watu watakuwa kama vipepeo kwa wingi na kuhangaika kulia na kushoto, madhaifu na wanyonge!
  5. وَتَكُونُ ٱلْجِبَالُ كَٱلْعِهْنِ ٱلْمَنفُوشِ۝٥

    Watakoonu aljibalu kaalʿihni almanfooshi

    Na milima itakuwa kama sufi zilizo chambuliwa!5

    Maelezo
    [5] Na milima itakuwa kama sufi iliyo tiwa rangi na kuchambuliwa kwa kutapanyika vipande mbali mbali na kupeperuka katika anga huku na huku.
  6. فَأَمَّا مَن ثَقُلَتْ مَوَٰزِينُهُۥ۝٦

    Faamma man thaqulat mawazeenuhu

    Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito,6

    Maelezo
    [6] Ama yule ambaye mizani yake itakuwa nzito, mema yake yakapindukia kuliko maovu yake,
  7. فَهُوَ فِى عِيشَةٍ رَّاضِيَةٍ۝٧

    Fahuwa fee ʿeeshatin radiyatin

    Huyo atakuwa katika maisha ya kupendeza.7

    Maelezo
    [7] Basi huyo atakuwa na maisha yatayo mridhisha mwenyewe, na nafsi yake itue.
  8. وَأَمَّا مَنْ خَفَّتْ مَوَٰزِينُهُۥ۝٨

    Waamma man khaffat mawazeenuhu

    Na yule ambaye mizani yake itakuwa khafifu,8

    Maelezo
    [8] Na ama ambaye mizani yake itakuwa nyepesi, na maovu yake yakazidi kuliko mema yake,
  9. فَأُمُّهُۥ هَاوِيَةٌ۝٩

    Faommuhu hawiyatun

    Huyo maskani yake yatakuwa Moto wa Hawiya!9

    Maelezo
    [9] Basi makaazi yake yatakuwa Jahannamu.
  10. وَمَآ أَدْرَىٰكَ مَا هِيَهْ۝١٠

    Wama adraka ma hiyah

    Na nini kitacho kujuilisha nini hiyo?10

    Maelezo
    [10] Na nini cha kukujuulisha ni nini Hawiya?
  11. نَارٌ حَامِيَةٌۢ۝١١

    Narun hamiyatun

    Ni Moto mkali!11

    Maelezo
    [11] Moto ulio mkali, hapana moto unao fikilia ukali wake, hata ukichochewa vipi na kutiwa kuni gani!

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Surat Al-Qari’a maana yake ni nini?

Al-Qari’a maana yake ni “Janga Kubwa”.

Surat Al-Qari’a iko katika juzuu ya ngapi?

Surat Al-Qari’a iko katika juzuu ya 30.

Surat Al-Qari’a ina aya ngapi?

Surat Al-Qari’a ina aya 11.

Surat Al-Qari’a ni ya Makka au ya Madina?

Surat Al-Qari’a ni sura ya Makka.

Surat Al-Qari’a ni sura ya ngapi katika Qur’ani?

Ni sura ya 101 katika Qur’ani.

Vyanzo

  • Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
  • Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
  • Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
  • Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
  • Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
  • Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.

Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.

Mipangilio ya kusoma

Fonti ya Qur’ani
Ukubwa wa Kiarabu
100%
Ukubwa wa tafsiri
100%
Mandhari

Ongeza kwenye skrini ya kwanza

ReadSurahFungua ReadSurah kutoka skrini ya kwanza, kwa skrini nzima. Sura ulizosoma hufunguka hata bila intaneti.

  1. Katika Safari, gusa kitufe cha kushiriki (Share). Kwenye iPhone mpya kiko kwenye menyu ya •••.
  2. Gusa “Add to Home Screen”. Huenda ukahitaji kusogeza chini.
  3. Gusa “Add”.