سورة التكاثر

Surat At-Takathur kwa Kiswahili

Kushindana kwa Wingi wa Mali

Msahafu

Mishary Rashid AlafasyPakua MP3Pakua PDF

Surat At-Takathur (التكاثر) ni sura ya 102 katika Qur’ani na ina aya 8. Jina lake lina maana ya “Kushindana kwa Wingi wa Mali”. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na iko katika juzuu ya 30.

Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat At-Takathur yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.

Surat At-Takathur kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

  1. أَلْهَىٰكُمُ ٱلتَّكَاثُرُ۝١

    Alhakumu alttakathuru

    Kumekushughulisheni kutafuta wingi,1

    Maelezo
    [1] Yamekushughulisheni mkaacha kutimiza yaliyo waajibu na ya ut'iifu kule kujitapa kwenu kwa wana na wafwasi, na kujifakhiri kwa mali, na hisabu, na nasaba, mpaka yakusibuni mauti!
  2. حَتَّىٰ زُرْتُمُ ٱلْمَقَابِرَ۝٢

    Hatta zurtumu almaqabira

    Mpaka mje makaburini!2

    Maelezo
    [2] Mpaka yakusibuni mauti!
  3. كَلَّا سَوْفَ تَعْلَمُونَ۝٣

    Kalla sawfa taʿlamoona

    Sivyo hivyo! Mtakuja jua!3

    Maelezo
    [3] Hakika mtakuja jua matokeo ya upumbavu wenu na mapuuza yenu.
  4. ثُمَّ كَلَّا سَوْفَ تَعْلَمُونَ۝٤

    Thumma kalla sawfa taʿlamoona

    Tena sivyo hivyo! Mtakuja jua!4

    Maelezo
    [4] Na hakika bila ya shaka mtakuja jua natija ya hayo!
  5. كَلَّا لَوْ تَعْلَمُونَ عِلْمَ ٱلْيَقِينِ۝٥

    Kalla law taʿlamoona ʿilma alyaqeeni

    Sivyo hivyo! Lau mngeli jua kwa ujuzi wa yakini,5

    Maelezo
    [5] Ama kwa hakika lau mngeli jua kwa yakini uovu wa mwisho wenu bila ya shaka mngeli ogopa huko kushindania kurindika mali, na mngeli jitengenezea Akhera yenu.
  6. لَتَرَوُنَّ ٱلْجَحِيمَ۝٦

    Latarawunna aljaheema

    Basi bila ya shaka mtaiona Jahannamu!6

    Maelezo
    [6] Nakuapieni na nakutilieni mkazo, enyi watu, kwamba hakika nyinyi mtakuja ushuhudia Moto unao waka.
  7. ثُمَّ لَتَرَوُنَّهَا عَيْنَ ٱلْيَقِينِ۝٧

    Thumma latarawunnaha ʿayna alyaqeeni

    Tena, bila ya shaka, mtaiona kwa jicho la yakini.7

    Maelezo
    [7] Kisha ninaapa na natilia mkazo kwamba mtauona wazi na kwa yakini.
  8. ثُمَّ لَتُسْـَٔلُنَّ يَوْمَئِذٍ عَنِ ٱلنَّعِيمِ۝٨

    Thumma latusalunna yawmaithin ʿani alnnaʿeemi

    Tena bila ya shaka mtaulizwa siku hiyo juu ya neema.8

    Maelezo
    [8] Tena naapa na natilia mkazo kwamba hakika nyinyi mtahisabiwa kwa neema mlizo deka nazo na mkazistarehea.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Surat At-Takathur maana yake ni nini?

At-Takathur maana yake ni “Kushindana kwa Wingi wa Mali”.

Surat At-Takathur iko katika juzuu ya ngapi?

Surat At-Takathur iko katika juzuu ya 30.

Surat At-Takathur ina aya ngapi?

Surat At-Takathur ina aya 8.

Surat At-Takathur ni ya Makka au ya Madina?

Surat At-Takathur ni sura ya Makka.

Surat At-Takathur ni sura ya ngapi katika Qur’ani?

Ni sura ya 102 katika Qur’ani.

Vyanzo

  • Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
  • Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
  • Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
  • Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
  • Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
  • Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.

Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.

Mipangilio ya kusoma

Fonti ya Qur’ani
Ukubwa wa Kiarabu
100%
Ukubwa wa tafsiri
100%
Mandhari

Ongeza kwenye skrini ya kwanza

ReadSurahFungua ReadSurah kutoka skrini ya kwanza, kwa skrini nzima. Sura ulizosoma hufunguka hata bila intaneti.

  1. Katika Safari, gusa kitufe cha kushiriki (Share). Kwenye iPhone mpya kiko kwenye menyu ya •••.
  2. Gusa “Add to Home Screen”. Huenda ukahitaji kusogeza chini.
  3. Gusa “Add”.