سورة الهمزة

Surat Al-Humaza kwa Kiswahili

Msengenyaji

Msahafu

Mishary Rashid AlafasyPakua MP3Pakua PDF

Surat Al-Humaza (الهمزة) ni sura ya 104 katika Qur’ani na ina aya 9. Jina lake lina maana ya “Msengenyaji”. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na iko katika juzuu ya 30.

Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat Al-Humaza yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.

Surat Al-Humaza kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

  1. وَيْلٌ لِّكُلِّ هُمَزَةٍ لُّمَزَةٍ۝١

    Waylun likulli humazatin lumazatin

    Ole wake kila safihi, msengenyaji!1

    Maelezo
    [1] Atapata adhabu kali na maangamio huyo ambaye mtindo wake ni kuwafedhehi watu kwa kauli au kwa ishara, au kuwasengenya kuwavunjia hishima zao.
  2. ٱلَّذِى جَمَعَ مَالًا وَعَدَّدَهُۥ۝٢

    Allathee jamaʿa malan waʿaddadahu

    Aliye kusanya mali na kuyahisabu.2

    Maelezo
    [2] Ambaye amekusanya chungu ya mali na akawa kazi yake kuyahisabu tu, kwa kuona ladha huko kuhisabu.
  3. يَحْسَبُ أَنَّ مَالَهُۥٓ أَخْلَدَهُۥ۝٣

    Yahsabu anna malahu akhladahu

    Anadhani ya kuwa mali yake yatambakisha milele!3

    Maelezo
    [3] Anadhani huyo kuwa mali yake yatamweka milele duniani, na yatamkinga na hayo anayo yachukia?
  4. كَلَّا ۖ لَيُنۢبَذَنَّ فِى ٱلْحُطَمَةِ۝٤

    Kalla layunbathanna fee alhutamati

    Hasha! Atavurumishwa katika H'ut'ama.4

    Maelezo
    [4] Na aache dhana hiyo! Wallahi! Hapana shaka yoyote kwa vitendo vyake viovu hivyo atakuja tumbukizwa katika Moto unao vuruga kila kinacho tupwa humo!
  5. وَمَآ أَدْرَىٰكَ مَا ٱلْحُطَمَةُ۝٥

    Wama adraka ma alhutamatu

    Na nani atakujuvya ni nini H'ut'ama?5

    Maelezo
    [5] Na kitu gani kitacho kujuvya nini ukweli wa Moto huu wa H'ut'ama?
  6. نَارُ ٱللَّهِ ٱلْمُوقَدَةُ۝٦

    Naru Allahi almooqadatu

    Moto wa Mwenyezi Mungu ulio washwa.6

    Maelezo
    [6] Moto wa Mwenyezi Mungu ulio washwa kwa amri yake, na daima unawaka!
  7. ٱلَّتِى تَطَّلِعُ عَلَى ٱلْأَفْـِٔدَةِ۝٧

    Allatee tattaliʿu ʿala alafidati

    Ambao unapanda nyoyoni.7

    Maelezo
    [7] Ambao unafikilia nyoyoni na kuzizunguka nyoyo.
  8. إِنَّهَا عَلَيْهِم مُّؤْصَدَةٌ۝٨

    lnnaha ʿalayhim musadatun

    Hakika huo utafungiwa nao8

    Maelezo
    [8] Huo utakuwa umefungwa milango yake, na wao watakuwa wamefungwa humo ndani
  9. فِى عَمَدٍ مُّمَدَّدَةٍۭ۝٩

    Fee ʿamadin mumaddadatin

    Kwenye nguzo zilio nyooshwa.9

    Maelezo
    [9] Kwenye maguzo yaliyo nyooka. Hawawezi kutaharaki, wala kutoka.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Surat Al-Humaza maana yake ni nini?

Al-Humaza maana yake ni “Msengenyaji”.

Surat Al-Humaza iko katika juzuu ya ngapi?

Surat Al-Humaza iko katika juzuu ya 30.

Surat Al-Humaza ina aya ngapi?

Surat Al-Humaza ina aya 9.

Surat Al-Humaza ni ya Makka au ya Madina?

Surat Al-Humaza ni sura ya Makka.

Surat Al-Humaza ni sura ya ngapi katika Qur’ani?

Ni sura ya 104 katika Qur’ani.

Vyanzo

  • Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
  • Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
  • Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
  • Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
  • Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
  • Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.

Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.

Mipangilio ya kusoma

Fonti ya Qur’ani
Ukubwa wa Kiarabu
100%
Ukubwa wa tafsiri
100%
Mandhari

Ongeza kwenye skrini ya kwanza

ReadSurahFungua ReadSurah kutoka skrini ya kwanza, kwa skrini nzima. Sura ulizosoma hufunguka hata bila intaneti.

  1. Katika Safari, gusa kitufe cha kushiriki (Share). Kwenye iPhone mpya kiko kwenye menyu ya •••.
  2. Gusa “Add to Home Screen”. Huenda ukahitaji kusogeza chini.
  3. Gusa “Add”.