Surat Al-Fil (الفيل) ni sura ya 105 katika Qur’ani na ina aya 5. Jina lake lina maana ya “Tembo”. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na iko katika juzuu ya 30.
Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat Al-Fil yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.
Surat Al-Fil kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
-
أَلَمْ تَرَ كَيْفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِأَصْحَـٰبِ ٱلْفِيلِ١
Alam tara kayfa faʿala rabbuka biashabi alfeeli
Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyo watenda wale wenye tembo?1
Maelezo
[1] Hakika, ewe Muhammad, unajua kwa ujuzi usio ingiliwa na shaka yoyote, alivyo fanya Mola wako Mlezi kuwafanyia wale watu wenye tembo (ndovu), wakataka kuishambulia Nyumba takatifu ya Al-Kaaba. -
أَلَمْ يَجْعَلْ كَيْدَهُمْ فِى تَضْلِيلٍ٢
Alam yajʿal kaydahum fee tadleelin
Kwani hakujaalia vitimbi vyao kuharibika?2
Maelezo
[2] Unajua ya kwamba hakika Mwenyezi Mungu amejaalia juhudi yao kutaka kuibomoa Al-Kaaba ivize na ipotelee mbali. Juhudi yao ikapeperuka, na wao wasipate makusudio yao. -
وَأَرْسَلَ عَلَيْهِمْ طَيْرًا أَبَابِيلَ٣
Waarsala ʿalayhim tayran ababeela
Na akawapelekea ndege makundi kwa makundi,3
Maelezo
[3] Na Mwenyezi Mungu aliwasalitisha na majeshi ya ndege yaliyo watokea makundi kwa makundi yakifuatana, na yakawazunguka kila upande. -
تَرْمِيهِم بِحِجَارَةٍ مِّن سِجِّيلٍ٤
Tarmeehim bihijaratin min sijjeelin
Wakiwatupia mawe ya udongo wa Motoni,4
Maelezo
[4] Wakiwatupia mawe kutoka Jahannamu. -
فَجَعَلَهُمْ كَعَصْفٍ مَّأْكُولٍۭ٥
Fajaʿalahum kaʿasfin makoolin
Akawafanya kama majani yaliyo liwa!5
Maelezo
[5] Akawafanya kama majani ya mimea yaliyo sibiwa yakatilifu.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Surat Al-Fil maana yake ni nini?
Al-Fil maana yake ni “Tembo”.
Surat Al-Fil iko katika juzuu ya ngapi?
Surat Al-Fil iko katika juzuu ya 30.
Surat Al-Fil ina aya ngapi?
Surat Al-Fil ina aya 5.
Surat Al-Fil ni ya Makka au ya Madina?
Surat Al-Fil ni sura ya Makka.
Surat Al-Fil ni sura ya ngapi katika Qur’ani?
Ni sura ya 105 katika Qur’ani.
Vyanzo
- Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
- Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
- Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
- Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
- Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
- Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.
Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.