سورة قريش

Surat Quraish kwa Kiswahili

Msahafu

Mishary Rashid AlafasyPakua MP3Pakua PDF

Surat Quraish (قريش) ni sura ya 106 katika Qur’ani na ina aya 4. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na iko katika juzuu ya 30.

Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat Quraish yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.

Surat Quraish kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

  1. لِإِيلَـٰفِ قُرَيْشٍ۝١

    Lieelafi qurayshin

    Kwa walivyo zoea Maqureshi,1

    Maelezo
    [1] Hebu staajabuni kwa yanayo walazimu Makureshi! Kuwalazimu safari za musimu wa baridi kwenda Yaman,
  2. إِۦلَـٰفِهِمْ رِحْلَةَ ٱلشِّتَآءِ وَٱلصَّيْفِ۝٢

    Eelafihim rihlata alshshitai waalssayfi

    Kuzoea kwao safari za siku za baridi na siku za joto.2

    Maelezo
    [2] Na safari za musimu wa joto kwenda Shamu, kufanya biashara na kutafuta riziki kwa utulivu na amani. (Hizo safari za biashara za Yaman ndizo zilizo waleta Waarabu Afrika Mashariki kwa maelfu ya miaka, na zikauleta Uislamu pande za Afrika kabla ya kuenea Arabuni. Kwani nchi za Afrika Mashariki zilikaliwa na Waarabu kwa maelfu ya miaka. Soma Periplus of the Erythrean Sea, na East Africa and Its Invaders ya Prof. Coupland, na vitabu vya Sir John Gray na Dr. L.W. Hollingsworth.)
  3. فَلْيَعْبُدُوا۟ رَبَّ هَـٰذَا ٱلْبَيْتِ۝٣

    Falyaʿbudoo rabba hatha albayti

    Basi nawamuabudu Mola Mlezi wa Nyumba hii,3

    Maelezo
    [3] Basi wamtakasie ibada Mola Mlezi wa Nyumba hii aliye wawezesha kuzifanya hizi safari mbili.
  4. ٱلَّذِىٓ أَطْعَمَهُم مِّن جُوعٍ وَءَامَنَهُم مِّنْ خَوْفٍۭ۝٤

    Allathee atʿamahum min jooʿin waamanahum min khawfin

    Ambaye anawalisha wasipate njaa, na anawalinda na khofu.4

    Maelezo
    [4] Ambaye anawalisha wasione njaa, na hali wao wamo katika bonde lisio na makulima, na akawalinda na khofu na watu wengine pembezoni mwao wananyakuliwa.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Surat Quraish iko katika juzuu ya ngapi?

Surat Quraish iko katika juzuu ya 30.

Surat Quraish ina aya ngapi?

Surat Quraish ina aya 4.

Surat Quraish ni ya Makka au ya Madina?

Surat Quraish ni sura ya Makka.

Surat Quraish ni sura ya ngapi katika Qur’ani?

Ni sura ya 106 katika Qur’ani.

Vyanzo

  • Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
  • Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
  • Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
  • Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
  • Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
  • Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.

Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.

Mipangilio ya kusoma

Fonti ya Qur’ani
Ukubwa wa Kiarabu
100%
Ukubwa wa tafsiri
100%
Mandhari

Ongeza kwenye skrini ya kwanza

ReadSurahFungua ReadSurah kutoka skrini ya kwanza, kwa skrini nzima. Sura ulizosoma hufunguka hata bila intaneti.

  1. Katika Safari, gusa kitufe cha kushiriki (Share). Kwenye iPhone mpya kiko kwenye menyu ya •••.
  2. Gusa “Add to Home Screen”. Huenda ukahitaji kusogeza chini.
  3. Gusa “Add”.