سورة التين

Surat At-Tin kwa Kiswahili

Tini

Msahafu

Mishary Rashid AlafasyPakua MP3Pakua PDF

Surat At-Tin (التين) ni sura ya 95 katika Qur’ani na ina aya 8. Jina lake lina maana ya “Tini”. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na iko katika juzuu ya 30.

Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat At-Tin yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.

Surat At-Tin kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi

بِّسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

  1. وَٱلتِّينِ وَٱلزَّيْتُونِ۝١

    Waaltteeni waalzzaytooni

    Naapa kwa tini na zaituni!1

    Maelezo
    [1] Naapa kwa tini na zaituni, kwa baraka zao na ubora wa manufaa yao.
  2. وَطُورِ سِينِينَ۝٢

    Watoori seeneena

    Na kwa Mlima wa Sinai!2

    Maelezo
    [2] Na kwa mlima ambao juu yake ndio Mwenyezi Mungu alimsemeza Musa.
  3. وَهَـٰذَا ٱلْبَلَدِ ٱلْأَمِينِ۝٣

    Wahatha albaladi alameeni

    Na kwa mji huu wenye amani!3

    Maelezo
    [3] Na kwa huu mji mtukufu wa Makka, ambao anaushuhudia utukufu wake mwenye kwenda uzuru, na anapata amani mwenye kuuingia.
  4. لَقَدْ خَلَقْنَا ٱلْإِنسَـٰنَ فِىٓ أَحْسَنِ تَقْوِيمٍ۝٤

    Laqad khalaqna alinsana fee ahsani taqweemin

    Bila ya shaka tumemuumba mtu kwa umbo lilio bora kabisa.4

    Maelezo
    [4] Kwa hakika bila ya shaka yoyote Sisi tumemuumba mtu amesimama sawa kwa umbo bora kabisa lilio nyooka, na akasifika kwa sifa nzuri kabisa.
  5. ثُمَّ رَدَدْنَـٰهُ أَسْفَلَ سَـٰفِلِينَ۝٥

    Thumma radadnahu asfala safileena

    Kisha tukamrudisha kuwa chini kuliko walio chini!5

    Maelezo
    [5] Kisha tukamteremsha cheo mpaka akawa ni wa chini kabisa katika hao walioko chini, kwa kuacha kufanya waajibu wa hayo tuliyo muumbia.
  6. إِلَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ فَلَهُمْ أَجْرٌ غَيْرُ مَمْنُونٍ۝٦

    Illa allatheena amanoo waʿamiloo alssalihati falahum ajrun ghayru mamnoonin

    Lakini wale walio amini na wakatenda mema, hao watapata ujira usio kwisha.6

    Maelezo
    [6] Lakini walio amini na wakatenda vitendo vyema, hao basi watapata ujira usio wakatikia wala kuwapungukia.
  7. فَمَا يُكَذِّبُكَ بَعْدُ بِٱلدِّينِ۝٧

    Fama yukaththibuka baʿdu bialddeeni

    Basi ni kipi baadaye kitacho kukukadhibishia malipo?7

    Maelezo
    [7] Basi kitu gani kinacho kupelekea kukadhibisha kufufuliwa na kulipwa baada ya kuwekwa wazi uweza wetu wa hayo?
  8. أَلَيْسَ ٱللَّهُ بِأَحْكَمِ ٱلْحَـٰكِمِينَ۝٨

    Alaysa Allahu biahkami alhakimeena

    Kwani Mwenyezi Mungu si muadilifu kuliko mahakimu wote?8

    Maelezo
    [8] Kwani Mwenyezi Mungu aliye yatenda hayo tuliyo kueleza si muadilifu kuliko mahakimu wote kwa kufanya na kupanga?

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Surat At-Tin maana yake ni nini?

At-Tin maana yake ni “Tini”.

Surat At-Tin iko katika juzuu ya ngapi?

Surat At-Tin iko katika juzuu ya 30.

Surat At-Tin ina aya ngapi?

Surat At-Tin ina aya 8.

Surat At-Tin ni ya Makka au ya Madina?

Surat At-Tin ni sura ya Makka.

Surat At-Tin ni sura ya ngapi katika Qur’ani?

Ni sura ya 95 katika Qur’ani.

Vyanzo

  • Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
  • Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
  • Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
  • Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
  • Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
  • Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.

Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.

Mipangilio ya kusoma

Fonti ya Qur’ani
Ukubwa wa Kiarabu
100%
Ukubwa wa tafsiri
100%
Mandhari

Ongeza kwenye skrini ya kwanza

ReadSurahFungua ReadSurah kutoka skrini ya kwanza, kwa skrini nzima. Sura ulizosoma hufunguka hata bila intaneti.

  1. Katika Safari, gusa kitufe cha kushiriki (Share). Kwenye iPhone mpya kiko kwenye menyu ya •••.
  2. Gusa “Add to Home Screen”. Huenda ukahitaji kusogeza chini.
  3. Gusa “Add”.