Surat Ad-Duha (الضحى) ni sura ya 93 katika Qur’ani na ina aya 11. Jina lake lina maana ya “Asubuhi”. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na iko katika juzuu ya 30.
Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat Ad-Duha yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.
Surat Ad-Duha kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
-
وَٱلضُّحَىٰ١
Waaldduha
Naapa kwa mchana!1
Maelezo
[1] Naapa kwa wakati wa kupanda juu jua, na ni wakati wa uchangamfu na kazi! -
وَٱلَّيْلِ إِذَا سَجَىٰ٢
Waallayli itha saja
Na kwa usiku unapo tanda!2
Maelezo
[2] Na naapa kwa usiku unapo tulia na ukatanda kote kiza chake! -
مَا وَدَّعَكَ رَبُّكَ وَمَا قَلَىٰ٣
Ma waddaʿaka rabbuka wama qala
Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukasirika nawe.3
Maelezo
[3] Ewe Muhammad! Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukuchukia. -
وَلَلْـَٔاخِرَةُ خَيْرٌ لَّكَ مِنَ ٱلْأُولَىٰ٤
Walalakhiratu khayrun laka mina aloola
Na bila ya shaka wakati ujao utakuwa bora kwako kuliko ulio tangulia.4
Maelezo
[4] Na matokeo ya mambo yako, mwisho wake, yatakuwa bora kuliko mwanzo wake. -
وَلَسَوْفَ يُعْطِيكَ رَبُّكَ فَتَرْضَىٰٓ٥
Walasawfa yuʿteeka rabbuka fatarda
Na Mola wako Mlezi atakupa mpaka uridhike.5
Maelezo
[5] Na ninaapa kuwa bila ya shaka hapo Mola wako Mlezi atakupa kheri za duniani na Akhera hata utaridhia. -
أَلَمْ يَجِدْكَ يَتِيمًا فَـَٔاوَىٰ٦
Alam yajidka yateeman faawa
Kwani hakukukuta yatima akakupa makaazi?6
Maelezo
[6] Kwani hakukukuta wewe yatima unahitaji wa kukutunza naye akakupa makaazi ya kukuhifadhi kwa mwenye kukuangalia vyema kwa mambo yako? -
وَوَجَدَكَ ضَآلًّا فَهَدَىٰ٧
Wawajadaka dallan fahada
Na akakukuta umepotea akakuongoa?7
Maelezo
[7] Na akakuona umebabaika hukukinaika na itikadi zilizo kuzunguka, naye akakuongoa kwenye Njia ya Haki? -
وَوَجَدَكَ عَآئِلًا فَأَغْنَىٰ٨
Wawajadaka ʿailan faaghna
Akakukuta mhitaji akakutosheleza?8
Maelezo
[8] Akakukuta fakiri wa mali naye akakutajirisha kwa kukupa riziki? -
فَأَمَّا ٱلْيَتِيمَ فَلَا تَقْهَرْ٩
Faamma alyateema fala taqhar
Basi yatima usimwonee!9
Maelezo
[9] Ikiwa hii ndiyo hali yetu nawe, basi yatima usimdhili, -
وَأَمَّا ٱلسَّآئِلَ فَلَا تَنْهَرْ١٠
Waamma alssaila fala tanhar
Na anaye omba au kuuliza usimkaripie!10
Maelezo
[10] Na mwenye kuomba au kuuliza usimjibu kwa ukavu, -
وَأَمَّا بِنِعْمَةِ رَبِّكَ فَحَدِّثْ١١
Waamma biniʿmati rabbika fahaddith
Na neema za Mola wako Mlezi zisimlie.11
Maelezo
[11] Na ama neema za Mola wako Mlezi zitangaze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kuwa ndio kudhihirisha neema.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Surat Ad-Duha maana yake ni nini?
Ad-Duha maana yake ni “Asubuhi”.
Surat Ad-Duha iko katika juzuu ya ngapi?
Surat Ad-Duha iko katika juzuu ya 30.
Surat Ad-Duha ina aya ngapi?
Surat Ad-Duha ina aya 11.
Surat Ad-Duha ni ya Makka au ya Madina?
Surat Ad-Duha ni sura ya Makka.
Surat Ad-Duha ni sura ya ngapi katika Qur’ani?
Ni sura ya 93 katika Qur’ani.
Vyanzo
- Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
- Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
- Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
- Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
- Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
- Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.
Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.