سورة الفجر

Surat Al-Fajr kwa Kiswahili

Alfajiri

Msahafu

Mishary Rashid AlafasyPakua MP3Pakua PDF

Surat Al-Fajr (الفجر) ni sura ya 89 katika Qur’ani na ina aya 30. Jina lake lina maana ya “Alfajiri”. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na iko katika juzuu ya 30.

Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat Al-Fajr yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.

Surat Al-Fajr kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

  1. وَٱلْفَجْرِ۝١

    Waalfajri

    Naapa kwa alfajiri!1

    Maelezo
    [1] Naapa kwa mwangaza wa asubuhi unapo ufukuza usiku.
  2. وَلَيَالٍ عَشْرٍ۝٢

    Walayalin ʿashrin

    Na kwa masiku kumi!2

    Maelezo
    [2] Na kwa masiku kumi yaliyo tukuzwa na Mwenyezi Mungu. (Na hayo ni masiku kumi ya mwanzo wa Mwezi wa Alhaj, Mfungo Tatu).
  3. وَٱلشَّفْعِ وَٱلْوَتْرِ۝٣

    Waalshshafʿi waalwatri

    Na kwa viwili viwili na kimoja kimoja!3

    Maelezo
    [3] Na shafi' yaani hisabu inayo gawika kwa mbili, kama 4, 6, 8 n.k. na witri, yaani isiyo gawika kwa mbili, kama 1, 3, 5 n.k. katika kila kitu.
  4. وَٱلَّيْلِ إِذَا يَسْرِ۝٤

    Waallayli itha yasri

    Na kwa usiku unapo pita!4

    Maelezo
    [4] Na kwa usiku unapo pita kwa kwenda ulimwengu kwa namna ya ajabu.
  5. هَلْ فِى ذَٰلِكَ قَسَمٌ لِّذِى حِجْرٍ۝٥

    Hal fee thalika qasamun lithee hijrin

    Je! Hapana katika haya kiapo kwa mwenye akili?5

    Maelezo
    [5] Je! Katika vitu vilivyo tajwa vinavyo onekana kwa akili hapana kiapo cha kukinaisha?
  6. أَلَمْ تَرَ كَيْفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِعَادٍ۝٦

    Alam tara kayfa faʿala rabbuka biʿadin

    Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyo wafanya kina A'di?6

    Maelezo
    [6] Kwani hujui jinsi Mola wako Mlezi alivyo wateremshia adhabu yake kaumu ya Hud, ?
  7. إِرَمَ ذَاتِ ٱلْعِمَادِ۝٧

    Irama thati alʿimadi

    Wa Iram, wenye majumba marefu?7

    Maelezo
    [7] Watu wa Iram wenye majengo marefu?
  8. ٱلَّتِى لَمْ يُخْلَقْ مِثْلُهَا فِى ٱلْبِلَـٰدِ۝٨

    Allatee lam yukhlaq mithluha fee albiladi

    Ambao haukuumbwa mfano wake katika nchi?8

    Maelezo
    [8] Ambayo haikupata kujengwa mfano wake kwa umadhubuti na ujenzi katika nchi.
  9. وَثَمُودَ ٱلَّذِينَ جَابُوا۟ ٱلصَّخْرَ بِٱلْوَادِ۝٩

    Wathamooda allatheena jaboo alssakhra bialwadi

    Na Thamudi walio chonga majabali huko bondeni?9

    Maelezo
    [9] Kwani hukujua jinsi Mola wako Mlezi alivyo teremsha adhabu yake kwa Thamudi, kaumu ya Saleh, walio chonga majabali kujengea nyumba zao huko bondeni?
  10. وَفِرْعَوْنَ ذِى ٱلْأَوْتَادِ۝١٠

    Wafirʿawna thee alawtadi

    Na Firauni mwenye vigingi?10

    Maelezo
    [10] Au kwani hukujua vipi Mola wako Mlezi alivyo wateremshia adhabu yake Firauni mwenye majeshi yaliyo upa nguvu ufalme wake kama vigingi vinavyo simamisha makhema?
  11. ٱلَّذِينَ طَغَوْا۟ فِى ٱلْبِلَـٰدِ۝١١

    Allatheena taghaw fee albiladi

    Ambao walifanya jeuri katika nchi?11

    Maelezo
    [11] Ambao walipita mipaka katika nchi?
  12. فَأَكْثَرُوا۟ فِيهَا ٱلْفَسَادَ۝١٢

    Faaktharoo feeha alfasada

    Wakakithirisha humo ufisadi?12

    Maelezo
    [12] Na wakazidisha kufanya uharibifu kwa ukafiri na udhalimu?
  13. فَصَبَّ عَلَيْهِمْ رَبُّكَ سَوْطَ عَذَابٍ۝١٣

    Fasabba ʿalayhim rabbuka sawta ʿathabin

    Basi Mola wako Mlezi aliwapiga mjeledi wa adhabu.13

    Maelezo
    [13] Basi Mola wako Mlezi aliwateremshia adhabu kali ya kuwaunguza.
  14. إِنَّ رَبَّكَ لَبِٱلْمِرْصَادِ۝١٤

    Inna rabbaka labialmirsadi

    Hakika Mola wako Mlezi yupo kwenye mavizio anawavizia.14

    Maelezo
    [14] Hakika Mola wako Mlezi anaviangalia vitendo vya watu, na anawahisabia, na atakuja kuwalipa kwavyo.
  15. فَأَمَّا ٱلْإِنسَـٰنُ إِذَا مَا ٱبْتَلَىٰهُ رَبُّهُۥ فَأَكْرَمَهُۥ وَنَعَّمَهُۥ فَيَقُولُ رَبِّىٓ أَكْرَمَنِ۝١٥

    Faamma alinsanu itha ma ibtalahu rabbuhu faakramahu wanaʿʿamahu fayaqoolu rabbee akramani

    Ama mtu anapo jaribiwa na Mola wake Mlezi, akamkirimu na akamneemesha, husema: Mola wangu Mlezi amenikirimu!15

    Maelezo
    [15] Ama mtu akijaribiwa na Mola wake Mlezi na akamkirimu, na akamneemesha kwa mali na cheo na nguvu, basi husema kwa kughurika na hayo: Mola wangu Mlezi amenitukuza kwa kuwa ninastahiki haya!
  16. وَأَمَّآ إِذَا مَا ٱبْتَلَىٰهُ فَقَدَرَ عَلَيْهِ رِزْقَهُۥ فَيَقُولُ رَبِّىٓ أَهَـٰنَنِ۝١٦

    Waamma itha ma ibtalahu faqadara ʿalayhi rizqahu fayaqoolu rabbee ahanani

    Na ama anapo mjaribu akampunguzia riziki yake, husema: Mola wangu Mlezi amenitia unyonge!16

    Maelezo
    [16] Na pindi Mola wake Mlezi akimjaribu mtu kwa kumdhikisha riziki, basi hughafilika na hikima ya hayo na husema: Mola wangu Mlezi kanidhalilisha!
  17. كَلَّا ۖ بَل لَّا تُكْرِمُونَ ٱلْيَتِيمَ۝١٧

    Kalla bal la tukrimoona alyateema

    Sivyo hivyo! Bali nyinyi hamuwakirimu mayatima,17

    Maelezo
    [17] Wacheni mtindo huo! Mambo siyo hayo kama msemavyo; bali nyinyi hamumkirimu yatima;
  18. وَلَا تَحَـٰٓضُّونَ عَلَىٰ طَعَامِ ٱلْمِسْكِينِ۝١٨

    Wala tahaddoona ʿala taʿami almiskeeni

    Wala hamhimizani kulisha masikini;18

    Maelezo
    [18] Wala hamhimizani kuwalisha masikini;
  19. وَتَأْكُلُونَ ٱلتُّرَاثَ أَكْلًا لَّمًّا۝١٩

    Watakuloona altturatha aklan lamman

    Na mnakula urithi kwa ulaji wa pupa,19

    Maelezo
    [19] Na mnakula mali ya urithi kwa pupa, hamchagui linalo faa na lisilo faa.
  20. وَتُحِبُّونَ ٱلْمَالَ حُبًّا جَمًّا۝٢٠

    Watuhibboona almala hubban jamman

    Na mnapenda mali pendo la kupita kiasi.20

    Maelezo
    [20] Na mnayapenda mali mno, yanayo kupelekeeni kupapatika katika kuyakusanya na ubakhili wa kuyatumia.
  21. كَلَّآ إِذَا دُكَّتِ ٱلْأَرْضُ دَكًّا دَكًّا۝٢١

    Kalla itha dukkati alardu dakkan dakkan

    Sivyo hivyo! Itakapo vunjwa ardhi vipande vipande,21

    Maelezo
    [21] Wacheni vitendo hivyo! Kwani inakungojeeni siku itapo lazwa ardhi iwe sawa sawa,
  22. وَجَآءَ رَبُّكَ وَٱلْمَلَكُ صَفًّا صَفًّا۝٢٢

    Wajaa rabbuka waalmalaku saffan saffan

    Na akaja Mola wako Mlezi na Malaika safu safu,22

    Maelezo
    [22] Na aje Mola wako Mlezi kama anavyo stahiki kuja kwake Subhanahu na Malaika waje kwa safu safu;
  23. وَجِا۟ىٓءَ يَوْمَئِذٍۭ بِجَهَنَّمَ ۚ يَوْمَئِذٍ يَتَذَكَّرُ ٱلْإِنسَـٰنُ وَأَنَّىٰ لَهُ ٱلذِّكْرَىٰ۝٢٣

    Wajeea yawmaithin bijahannama yawmaithin yatathakkaru alinsanu waanna lahu alththikra

    Na ikaletwa Jahannamu siku hiyo, siku hiyo mtu atakumbuka! Lakini kukumbuka huko kutamfaa nini?23

    Maelezo
    [23] Na siku hiyo iletwe Jahannamu, nyumba ya adhabu, siku hiyo yatapo tokea hayo mwanaadamu atakumbuka aliyo yaharibu - lakini wapi! Kukumbuka huko kumfae nini, na wakati umekwisha pita?
  24. يَقُولُ يَـٰلَيْتَنِى قَدَّمْتُ لِحَيَاتِى۝٢٤

    Yaqoolu ya laytanee qaddamtu lihayatee

    Atasema: Laiti ningeli jitangulizia kwa uhai wangu!24

    Maelezo
    [24] Atasema kwa majuto: Laiti ningeli jitangulizia katika dunia vitendo vyema vya kunifaa katika maisha ya Akhera!
  25. فَيَوْمَئِذٍ لَّا يُعَذِّبُ عَذَابَهُۥٓ أَحَدٌ۝٢٥

    Fayawmaithin la yuʿaththibu ʿathabahu ahadun

    Basi siku hiyo hataadhibu yeyote namna ya kuadhibu kwake.25

    Maelezo
    [25] Siku hiyo zitakuwa hali hizi, haadhibu mtu kama adhabu ya Mwenyezi Mungu, wala hafungi mtu kama afungavyo Yeye.
  26. وَلَا يُوثِقُ وَثَاقَهُۥٓ أَحَدٌ۝٢٦

    Wala yoothiqu wathaqahu ahadun

    Wala hatafunga yeyote kama kufunga kwake.26

    Maelezo
    [26] Siku hiyo zitakuwa hali hizi, haadhibu mtu kama adhabu ya Mwenyezi Mungu, wala hafungi mtu kama afungavyo Yeye.
  27. يَـٰٓأَيَّتُهَا ٱلنَّفْسُ ٱلْمُطْمَئِنَّةُ۝٢٧

    Ya ayyatuha alnnafsu almutmainnatu

    Ewe nafsi iliyo tua!27

    Maelezo
    [27] Ewe nafsi uliye tulia juu ya Haki!
  28. ٱرْجِعِىٓ إِلَىٰ رَبِّكِ رَاضِيَةً مَّرْضِيَّةً۝٢٨

    Irjiʿee ila rabbiki radiyatan mardiyyatan

    Rejea kwa Mola wako Mlezi umeridhika, na umemridhisha.28

    Maelezo
    [28] Rejea kwenye radhi ya Mola wako Mlezi nawe uradhi kwa neema ulio pewa, nawe umemridhisha kwa a'mali uliyo ikadimisha.
  29. فَٱدْخُلِى فِى عِبَـٰدِى۝٢٩

    Faodkhulee fee ʿibadee

    Basi ingia miongoni mwa waja wangu,29

    Maelezo
    [29] Basi ingia katika kundi la waja wangu walio wema!
  30. وَٱدْخُلِى جَنَّتِى۝٣٠

    Waodkhulee jannatee

    Na ingia katika Pepo yangu.30

    Maelezo
    [30] Na ingia katika Pepo yangu, nyumba ya neema ya milele!

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Surat Al-Fajr maana yake ni nini?

Al-Fajr maana yake ni “Alfajiri”.

Surat Al-Fajr iko katika juzuu ya ngapi?

Surat Al-Fajr iko katika juzuu ya 30.

Surat Al-Fajr ina aya ngapi?

Surat Al-Fajr ina aya 30.

Surat Al-Fajr ni ya Makka au ya Madina?

Surat Al-Fajr ni sura ya Makka.

Surat Al-Fajr ni sura ya ngapi katika Qur’ani?

Ni sura ya 89 katika Qur’ani.

Vyanzo

  • Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
  • Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
  • Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
  • Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
  • Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
  • Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.

Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.

Mipangilio ya kusoma

Fonti ya Qur’ani
Ukubwa wa Kiarabu
100%
Ukubwa wa tafsiri
100%
Mandhari

Ongeza kwenye skrini ya kwanza

ReadSurahFungua ReadSurah kutoka skrini ya kwanza, kwa skrini nzima. Sura ulizosoma hufunguka hata bila intaneti.

  1. Katika Safari, gusa kitufe cha kushiriki (Share). Kwenye iPhone mpya kiko kwenye menyu ya •••.
  2. Gusa “Add to Home Screen”. Huenda ukahitaji kusogeza chini.
  3. Gusa “Add”.