سورة الطارق

Surat At-Tariq kwa Kiswahili

Kinachokuja Usiku

Msahafu

Mishary Rashid AlafasyPakua MP3Pakua PDF

Surat At-Tariq (الطارق) ni sura ya 86 katika Qur’ani na ina aya 17. Jina lake lina maana ya “Kinachokuja Usiku”. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na iko katika juzuu ya 30.

Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat At-Tariq yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.

Surat At-Tariq kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

  1. وَٱلسَّمَآءِ وَٱلطَّارِقِ۝١

    Waalssamai waalttariqi

    Naapa kwa mbingu na Kinacho kuja usiku!1

    Maelezo
    [1] Naapa kwa mbingu na nyota inayo tokeza usiku!
  2. وَمَآ أَدْرَىٰكَ مَا ٱلطَّارِقُ۝٢

    Wama adraka ma alttariqu

    Na nini kitakacho kujuulisha ni nini hicho Kinacho kuja usiku?2

    Maelezo
    [2] Na kitu gani kitakujuvya ukweli wa nyota hii? Ni hiyo inayotoa mwanga wake katika giza.
  3. ٱلنَّجْمُ ٱلثَّاقِبُ۝٣

    Alnnajmu alththaqibu

    Ni Nyota yenye mwanga mkali.3

    Maelezo
    [3] Na kitu gani kitakujuvya ukweli wa nyota hii? Ni hiyo inayotoa mwanga wake katika giza.
  4. إِن كُلُّ نَفْسٍ لَّمَّا عَلَيْهَا حَافِظٌ۝٤

    In kullu nafsin lamma ʿalayha hafithun

    Hapana nafsi ila inayo mwangalizi.4

    Maelezo
    [4] Hapana nafsi ila inayo mlinzi wa kuiangalia na kudhibiti vitendo vyake.
  5. فَلْيَنظُرِ ٱلْإِنسَـٰنُ مِمَّ خُلِقَ۝٥

    Falyanthuri alinsanu mimma khuliqa

    Hebu naajitazame mwanaadamu ameumbwa kwa kitu gani?5

    Maelezo
    [5] Basi naafikiri mtu, yeye kaumbwa kutokana na nini?
  6. خُلِقَ مِن مَّآءٍ دَافِقٍ۝٦

    Khuliqa min main dafiqin

    Ameumbwa kwa maji yatokayo kwa kuchupa!6

    Maelezo
    [6] Ameumbwa mtu kutokana na maji yanayo toka kwa nguvu.
  7. يَخْرُجُ مِنۢ بَيْنِ ٱلصُّلْبِ وَٱلتَّرَآئِبِ۝٧

    Yakhruju min bayni alssulbi waalttaraibi

    Yatokayo baina ya mifupa ya mgongo na mbavu.7

    Maelezo
    [7] Maji haya yanatoka baina ya uti wa mgongo na mbavu za mwanamume na mwanamke. S'ULB ni sehemu za uti wa mgongo; na TARAAIB ni mafupa ya vifua, yaani mbavu. Masomo ya watoto wanapo kuwa ndani ya matumbo ya mama zao (Embryology). yamedhihirisha kuwa viini vya vyombo vya uzazi na mkojo katika mtoto ndani ya tumbo la mama yake vinadhihiri baina ya khalaya (cells) za mishipa itakayo kuwa mafupa ya uti wa mgongo, na baina ya khalaya zitakazo kuwa mafupa ya kifua. Mafigo hubakia pahala pake, na kokwa huteremka kwenye pahala pake pa kawaida katika pumbu wakati wa kuzaliwa. Na juu ya kuteremka kokwa chini mishipa inayo inywesha damu maisha yake yote inatokana na mishipa ya mafigo. Hali kadhaalika mishipa ya Navo inayo peleka kuhisi na ikasaidia kuzalisha vitu vya uhai na yaliyo khusiana na hayo kama maji yanayo toka kwenye mshipa wa kifua wa kumi unao tokana na ubongo wa uti wa mgongo kwenye kipingili cha kumi na kumi na moja. Yaliyo wazi kutokana na hayo ni kwamba vyombo vya uzazi na vinavyo lisha vyombo hivyo, na vyombo vya damu, vipo katika kiwiliwili baina ya uti wa mgongo na mbavu.
  8. إِنَّهُۥ عَلَىٰ رَجْعِهِۦ لَقَادِرٌ۝٨

    Innahu ʿala rajʿihi laqadirun

    Hakika Yeye ana uweza wa kumrudisha.8

    Maelezo
    [8] Hakika Mwenyezi Mungu aliye muumba hivi hapo mwanzo, bila ya shaka ni Muweza wa kumuumba tena baada ya kufa kwake.
  9. يَوْمَ تُبْلَى ٱلسَّرَآئِرُ۝٩

    Yawma tubla alssarairu

    Siku zitakapo dhihirishwa siri.9

    Maelezo
    [9] Siku dhamiri zitapo fanyiwa mtihani, na zitengwe mbali mbali baina ya ziliyo kuwa nzuri na ziliyo kuwa mbovu.
  10. فَمَا لَهُۥ مِن قُوَّةٍ وَلَا نَاصِرٍ۝١٠

    Fama lahu min quwwatin wala nasirin

    Basi hatakuwa na nguvu wala msaidizi.10

    Maelezo
    [10] Basi hapana mtu wakati huo ataye kuwa na nguvu ya kujikinga nafsi yake, wala hatakuwa na msaidizi wa kumnusuru.
  11. وَٱلسَّمَآءِ ذَاتِ ٱلرَّجْعِ۝١١

    Waalssamai thati alrrajʿi

    Naapa kwa mbingu yenye marejeo!11

    Maelezo
    [11] Naapa kwa mbingu yenye mvua inayo rejea na kuja mara kwa mara!
  12. وَٱلْأَرْضِ ذَاتِ ٱلصَّدْعِ۝١٢

    Waalardi thati alssadʿi

    Na kwa ardhi inayo pasuka!12

    Maelezo
    [12] Na ardhi inayo pasuka kwa kuchipuka mimea!
  13. إِنَّهُۥ لَقَوْلٌ فَصْلٌ۝١٣

    Innahu laqawlun faslun

    Hakika hii ni kauli ya kupambanua.13

    Maelezo
    [13] Hakika hii Qur'ani ni yenye kupambanua baina ya kweli na uwongo.
  14. وَمَا هُوَ بِٱلْهَزْلِ۝١٤

    Wama huwa bialhazli

    Wala si mzaha.14

    Maelezo
    [14] Wala haina nuksani yoyote ya mchezo au maskhara.
  15. إِنَّهُمْ يَكِيدُونَ كَيْدًا۝١٥

    Innahum yakeedoona kaydan

    Hakika wao wanapanga mpango.15

    Maelezo
    [15] Hakika hao wanao ikadhibisha Qur'ani wanaipangia njama kutaka kuiharibia, njama zenye kufikia ukomo!
  16. وَأَكِيدُ كَيْدًا۝١٦

    Waakeedu kaydan

    Na Mimi napanga mpango.16

    Maelezo
    [16] Lakini Mimi nitawalipa, na nitavipambanisha hivyo vitimbi vyao kwa vitimbi madhubuti ambavyo hawataweza kujikinga navyo.
  17. فَمَهِّلِ ٱلْكَـٰفِرِينَ أَمْهِلْهُمْ رُوَيْدًۢا۝١٧

    Famahhili alkafireena amhilhum ruwaydan

    Basi wape muhula makafiri - wape muhula pole pole.17

    Maelezo
    [17] Basi wangojee hao makafiri! Wape muhula wa karibu mpaka nikuamrishe amri gani kali ya kuwatendea.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Surat At-Tariq maana yake ni nini?

At-Tariq maana yake ni “Kinachokuja Usiku”.

Surat At-Tariq iko katika juzuu ya ngapi?

Surat At-Tariq iko katika juzuu ya 30.

Surat At-Tariq ina aya ngapi?

Surat At-Tariq ina aya 17.

Surat At-Tariq ni ya Makka au ya Madina?

Surat At-Tariq ni sura ya Makka.

Surat At-Tariq ni sura ya ngapi katika Qur’ani?

Ni sura ya 86 katika Qur’ani.

Vyanzo

  • Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
  • Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
  • Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
  • Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
  • Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
  • Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.

Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.

Mipangilio ya kusoma

Fonti ya Qur’ani
Ukubwa wa Kiarabu
100%
Ukubwa wa tafsiri
100%
Mandhari

Ongeza kwenye skrini ya kwanza

ReadSurahFungua ReadSurah kutoka skrini ya kwanza, kwa skrini nzima. Sura ulizosoma hufunguka hata bila intaneti.

  1. Katika Safari, gusa kitufe cha kushiriki (Share). Kwenye iPhone mpya kiko kwenye menyu ya •••.
  2. Gusa “Add to Home Screen”. Huenda ukahitaji kusogeza chini.
  3. Gusa “Add”.