سورة الإنشقاق

Surat Al-Inshiqaq kwa Kiswahili

Kuchanika

Msahafu

Mishary Rashid AlafasyPakua MP3Pakua PDF

Surat Al-Inshiqaq (الإنشقاق) ni sura ya 84 katika Qur’ani na ina aya 25. Jina lake lina maana ya “Kuchanika”. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na iko katika juzuu ya 30.

Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat Al-Inshiqaq yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.

Surat Al-Inshiqaq kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

  1. إِذَا ٱلسَّمَآءُ ٱنشَقَّتْ۝١

    Itha alssamao inshaqqat

    Itapo chanika mbingu!1

    Maelezo
    [1] Mbingu itapo chanika, ikaamrishwa iondoke,
  2. وَأَذِنَتْ لِرَبِّهَا وَحُقَّتْ۝٢

    Waathinat lirabbiha wahuqqat

    Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza!2

    Maelezo
    [2] Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi na ikamt'ii, na ndio maelekeo yake isikie na kut'ii,
  3. وَإِذَا ٱلْأَرْضُ مُدَّتْ۝٣

    Waitha alardu muddat

    Na ardhi itakapo tanuliwa!3

    Maelezo
    [3] Na ardhi ikazidi upana wake kwa kulazwa milima na kuondolewa kifusi chake,
  4. وَأَلْقَتْ مَا فِيهَا وَتَخَلَّتْ۝٤

    Waalqat ma feeha watakhallat

    Na kuvitoa vilivyo kuwa ndani yake, ikawa tupu!4

    Maelezo
    [4] Na ardhi ikatoa nje maiti na khazina ziliyo kuwamo ndani yake, na ikaachana navyo vyote hivyo,
  5. وَأَذِنَتْ لِرَبِّهَا وَحُقَّتْ۝٥

    Waathinat lirabbiha wahuqqat

    Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza!5

    Maelezo
    [5] Na ikamwelekea Mola wake Mlezi kwa kuzidi kutanuka kwake na kutoa vilio kuwemo ndani yake na kuachana navyo, na hayo ni haki yake kuwa. Yakitokea yote hayo yaliyo tangulia kusimuliwa basi kila mtu atapata malipo ya vitendo vyake.
  6. يَـٰٓأَيُّهَا ٱلْإِنسَـٰنُ إِنَّكَ كَادِحٌ إِلَىٰ رَبِّكَ كَدْحًا فَمُلَـٰقِيهِ۝٦

    Ya ayyuha alinsanu innaka kadihun ila rabbika kadhan famulaqeehi

    Ewe mtu! Hakika wewe unajikusuru kwa juhudi kumwendea Mola wako Mlezi, basi utamkuta.6

    Maelezo
    [6] Ewe mtu! Hakika wewe unafanya juhudi katika vitendo vyako vikufikishie lengo lako. Basi utakuja kukutana na Mola wako Mlezi kwa a'mali yako, naye atakulipa kwayo.
  7. فَأَمَّا مَنْ أُوتِىَ كِتَـٰبَهُۥ بِيَمِينِهِۦ۝٧

    Faama man ootiya kitabahu biyameenihi

    Ama atakaye pewa daftari lake kwa mkono wa kulia!7

    Maelezo
    [7] Ama mwenye kupewa daftari la vitendo vyake kwa mkono wake wa kulia
  8. فَسَوْفَ يُحَاسَبُ حِسَابًا يَسِيرًا۝٨

    Fasawfa yuhasabu hisaban yaseeran

    Basi huyo atahisabiwa hisabu nyepesi!8

    Maelezo
    [8] Basi atahisabiwa kwa hisabu nyepesi,
  9. وَيَنقَلِبُ إِلَىٰٓ أَهْلِهِۦ مَسْرُورًا۝٩

    Wayanqalibu ila ahlihi masrooran

    Na arudi kwa ahali zake na furaha.9

    Maelezo
    [9] Na atarejea kwa jamaa zake Waumini naye furahani.
  10. وَأَمَّا مَنْ أُوتِىَ كِتَـٰبَهُۥ وَرَآءَ ظَهْرِهِۦ۝١٠

    Waamma man ootiya kitabahu waraa thahrihi

    Na ama atakaye pewa daftari lake kwa nyuma ya mgongo wake,10

    Maelezo
    [10] Ama mwenye kupewa daftari lake kwa mkono wa kushoto wake nyuma ya mgongo wake kwa kudharauliwa shani yake,
  11. فَسَوْفَ يَدْعُوا۟ ثُبُورًا۝١١

    Fasawfa yadʿoo thubooran

    Basi huyo ataomba kuteketea.11

    Maelezo
    [11] Huyo atatamani ajiue,
  12. وَيَصْلَىٰ سَعِيرًا۝١٢

    Wayasla saʿeeran

    Na ataingia Motoni.12

    Maelezo
    [12] Na ataingia Motoni aungulie mbali!
  13. إِنَّهُۥ كَانَ فِىٓ أَهْلِهِۦ مَسْرُورًا۝١٣

    Innahu kana fee ahlihi masrooran

    Hakika alikuwa furahani kati ya jamaa zake.13

    Maelezo
    [13] Kwani huyo hakika duniani alikuwa furahani kati ya jamaa zake akitanaamu na pumbao alilo kuwa nalo hata akapuuza a'mali ya kuitenda kwa mustakabali wake.
  14. إِنَّهُۥ ظَنَّ أَن لَّن يَحُورَ۝١٤

    Innahu thanna an lan yahoora

    Huyo hakika alidhani kuwa hatarejea tena.14

    Maelezo
    [14] Hakika huyo alidhani kuwa kabisa hatorejea kwa Mwenyezi Mungu akamhisabu.
  15. بَلَىٰٓ إِنَّ رَبَّهُۥ كَانَ بِهِۦ بَصِيرًا۝١٥

    Bala inna rabbahu kana bihi baseeran

    Kwani? Hakika Mola wake Mlezi alikuwa akimwona!15

    Maelezo
    [15] Bali atarejea, na atahisabiwa! Kwani Mola wake Mlezi alikuwa anamwona vyema yeye na vitendo vyake.
  16. فَلَآ أُقْسِمُ بِٱلشَّفَقِ۝١٦

    Fala oqsimu bialshshafaqi

    Basi ninaapa kwa wekundu wa jua linapo kuchwa,16

    Maelezo
    [16] Basi naapa kiapo cha mkazo kwa wekundu wa mbingu baada ya kuchwa jua!
  17. وَٱلَّيْلِ وَمَا وَسَقَ۝١٧

    Waallayli wama wasaqa

    Na kwa usiku na unavyo vikusanya,17

    Maelezo
    [17] Na kwa usiku na unavyo vikusanya vyote katika giza lake, wanaadamu, wanyama na vyenginevyo!
  18. وَٱلْقَمَرِ إِذَا ٱتَّسَقَ۝١٨

    Waalqamari itha ittasaqa

    Na kwa mwezi unapo pevuka,18

    Maelezo
    [18] Na mwezi unapo kamilika kupevuka na kutimia nuru yake,
  19. لَتَرْكَبُنَّ طَبَقًا عَن طَبَقٍ۝١٩

    Latarkabunna tabaqan ʿan tabaqin

    Lazima mtapanda t'abaka kwa t'abaka!19

    Maelezo
    [19] Hapana shaka yoyote mtakutana na hali baada ya hali, baadhi yake zina shida zaidi kuliko nyenginezo, za kufa na kufufuliwa na vitisho vya Kiyama.
  20. فَمَا لَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ۝٢٠

    Fama lahum la yuminoona

    Basi wana nini hawaamini?20

    Maelezo
    [20] Wana nini hawa makafiri yanayo wazuia wasimuamini Mwenyezi Mungu na kufufuliwa baada ya kuwekwa wazi dalili zake zote za kuwajibika kwake?
  21. وَإِذَا قُرِئَ عَلَيْهِمُ ٱلْقُرْءَانُ لَا يَسْجُدُونَ ۩۝٢١

    Waitha quria ʿalayhimu alquranu la yasjudoona

    Na wanapo somewa Qur'ani hawasujudu?21

    Maelezo
    [21] Na pindi wakizisikia Aya za Qur'ani hawasujudu wakanyenyekea?
  22. بَلِ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ يُكَذِّبُونَ۝٢٢

    Bali allatheena kafaroo yukaththiboona

    Bali walio kufuru wanakanusha tu.22

    Maelezo
    [22] Bali watu hawa, kwa ukafiri wao, wanakanusha kwa inadi na kutakabari kuikataa Haki!
  23. وَٱللَّهُ أَعْلَمُ بِمَا يُوعُونَ۝٢٣

    WaAllahu aʿlamu bima yooʿoona

    Na Mwenyezi Mungu anajua wanayo yadhamiria.23

    Maelezo
    [23] Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua kabisa hayo wanayo yadhamiria katika nyoyo zao.
  24. فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ۝٢٤

    Fabashshirhum biʿathabin aleemin

    Basi wabashirie adhabu chungu!24

    Maelezo
    [24] Basi wabashirie, kwa kejeli, kuwa watapata adhabu ya kutia uchungu.
  25. إِلَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ لَهُمْ أَجْرٌ غَيْرُ مَمْنُونٍۭ۝٢٥

    Illa allatheena amanoo waʿamiloo alssalihati lahum ajrun ghayru mamnoonin

    Isipo kuwa wale walio amini na wakatenda mema; hao watakuwa na ujira usio malizika.25

    Maelezo
    [25] Lakini walio amini na wakatenda mema watapata, kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ujira usio wakatikia na wala usio kuwa na hisabu juu yao.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Surat Al-Inshiqaq maana yake ni nini?

Al-Inshiqaq maana yake ni “Kuchanika”.

Surat Al-Inshiqaq iko katika juzuu ya ngapi?

Surat Al-Inshiqaq iko katika juzuu ya 30.

Surat Al-Inshiqaq ina aya ngapi?

Surat Al-Inshiqaq ina aya 25.

Surat Al-Inshiqaq ni ya Makka au ya Madina?

Surat Al-Inshiqaq ni sura ya Makka.

Surat Al-Inshiqaq ni sura ya ngapi katika Qur’ani?

Ni sura ya 84 katika Qur’ani.

Vyanzo

  • Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
  • Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
  • Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
  • Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
  • Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
  • Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.

Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.

Mipangilio ya kusoma

Fonti ya Qur’ani
Ukubwa wa Kiarabu
100%
Ukubwa wa tafsiri
100%
Mandhari

Ongeza kwenye skrini ya kwanza

ReadSurahFungua ReadSurah kutoka skrini ya kwanza, kwa skrini nzima. Sura ulizosoma hufunguka hata bila intaneti.

  1. Katika Safari, gusa kitufe cha kushiriki (Share). Kwenye iPhone mpya kiko kwenye menyu ya •••.
  2. Gusa “Add to Home Screen”. Huenda ukahitaji kusogeza chini.
  3. Gusa “Add”.