سورة التكوير

Surat At-Takwir kwa Kiswahili

Kukunjwa

Msahafu

Mishary Rashid AlafasyPakua MP3Pakua PDF

Surat At-Takwir (التكوير) ni sura ya 81 katika Qur’ani na ina aya 29. Jina lake lina maana ya “Kukunjwa”. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na iko katika juzuu ya 30.

Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat At-Takwir yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.

Surat At-Takwir kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

  1. إِذَا ٱلشَّمْسُ كُوِّرَتْ۝١

    Itha alshshamsu kuwwirat

    Jua litakapo kunjwa!1

    Maelezo
    [1] Jua litakapo kunjwa na mwangaza wake ukafutwa,
  2. وَإِذَا ٱلنُّجُومُ ٱنكَدَرَتْ۝٢

    Waitha alnnujoomu inkadarat

    Na nyota zikazimwa!2

    Maelezo
    [2] Na nyota ikazimwa nuru yao,
  3. وَإِذَا ٱلْجِبَالُ سُيِّرَتْ۝٣

    Waitha aljibalu suyyirat

    Na milima ikaondolewa!3

    Maelezo
    [3] Na milima ikaondoshwa hapo ilipo,
  4. وَإِذَا ٱلْعِشَارُ عُطِّلَتْ۝٤

    Waitha alʿisharu ʿuttilat

    Na ngamia wenye mimba pevu watakapo achwa wasishughulikiwe,4

    Maelezo
    [4] Na ambao wa kuchukua mimba wakaharibu mimba zao,
  5. وَإِذَا ٱلْوُحُوشُ حُشِرَتْ۝٥

    Waitha alwuhooshu hushirat

    Na wanyama wa mwituni wakakusanywa!5

    Maelezo
    [5] Na nyama mwitu wakusanywe kutoka vichakani mwao na mashimoni mwao, hawajijui hawajitambui kwa wingi wa kufazaika.
  6. وَإِذَا ٱلْبِحَارُ سُجِّرَتْ۝٦

    Waitha albiharu sujjirat

    Na bahari zikawaka moto!6

    Maelezo
    [6] Na bahari zikawa zinawaka moto,
  7. وَإِذَا ٱلنُّفُوسُ زُوِّجَتْ۝٧

    Waitha alnnufoosu zuwwijat

    Na nafsi zikaunganishwa!7

    Maelezo
    [7] Na roho zikaunganishwa na viwiliwili vyao,
  8. وَإِذَا ٱلْمَوْءُۥدَةُ سُئِلَتْ۝٨

    Waitha almawoodatu suilat

    Na msichana aliye zikwa hai atapo ulizwa!8

    Maelezo
    [8] Na mtoto wa kike aliye zikwa hai, akaulizwa kwa kumliwaza yeye, na kumshutumu aliye mzika hai,
  9. بِأَىِّ ذَنۢبٍ قُتِلَتْ۝٩

    Biayyi thanbin qutilat

    Kwa kosa gani aliuliwa?9

    Maelezo
    [9] Kwa makosa gani kauliwa, naye hana dhambi? (Ilikuwa ada ya makafiri wa Kiarabu kabla ya Uislamu kuwazika watoto wao wa kike nao wahai! Baadhi ya Mabaniani wanawauwa watoto wao wa kike hata hivi leo huko India!!)
  10. وَإِذَا ٱلصُّحُفُ نُشِرَتْ۝١٠

    Waitha alssuhufu nushirat

    Na madaftari yatakapo enezwa,10

    Maelezo
    [10] Na nyaraka zilizo andikwa ndani vitendo vya watu zikakunjuliwa wakati wa hisabu.
  11. وَإِذَا ٱلسَّمَآءُ كُشِطَتْ۝١١

    Waitha alssamao kushitat

    Na mbingu itapo tanduliwa,11

    Maelezo
    [11] Na mbingu itapo ondoshwa pahala pake,
  12. وَإِذَا ٱلْجَحِيمُ سُعِّرَتْ۝١٢

    Waitha aljaheemu suʿʿirat

    Na Jahannamu itapo chochewa,12

    Maelezo
    [12] Na Moto ukawashwa kwa mwako mkali,
  13. وَإِذَا ٱلْجَنَّةُ أُزْلِفَتْ۝١٣

    Waitha aljannatu ozlifat

    Na Pepo ikasogezwa,13

    Maelezo
    [13] Na Pepo ikajongezwa ikawa karibu,
  14. عَلِمَتْ نَفْسٌ مَّآ أَحْضَرَتْ۝١٤

    ʿAlimat nafsun ma ahdarat

    Kila nafsi itajua ilicho kihudhurisha.14

    Maelezo
    [14] Yatakapo tokea yote hayo, basi hapo tena kila nafsi itajua nini iliyo tanguliza, ikiwa kheri au shari.
  15. فَلَآ أُقْسِمُ بِٱلْخُنَّسِ۝١٥

    Fala oqsimu bialkhunnasi

    Naapa kwa nyota zinapo rejea nyuma,15

    Maelezo
    [15] Naapa kiapo cha mkazo kwa nyota ambazo zinanywea zinapo chomoza, na hapo mwanga wake huwa khafifu,
  16. ٱلْجَوَارِ ٱلْكُنَّسِ۝١٦

    Aljawari alkunnasi

    Zinazo kwenda, kisha zikajificha,16

    Maelezo
    [16] Zenye kwenda na hujificha wakati wa kuchwa kwake, kama paa wanapo jificha kwenye mapango yao.
  17. وَٱلَّيْلِ إِذَا عَسْعَسَ۝١٧

    Waallayli itha ʿasʿasa

    Na kwa usiku unapo pungua,17

    Maelezo
    [17] Na kwa usiku linapo pungua giza lake wakati unapo malizika.
  18. وَٱلصُّبْحِ إِذَا تَنَفَّسَ۝١٨

    Waalssubhi itha tanaffasa

    Na kwa asubuhi inapo pambazuka,18

    Maelezo
    [18] Na kwa asubuhi unapo anza mwangaza wake na ukavuma upepo wake,
  19. إِنَّهُۥ لَقَوْلُ رَسُولٍ كَرِيمٍ۝١٩

    Innahu laqawlu rasoolin kareemin

    Kwamba hakika bila ya shaka hii ni kauli ya Mjumbe mtukufu,19

    Maelezo
    [19] Hakika Qur'ani bila ya shaka ni kauli ya Mjumbe anaye toka kwa Mwenyezi Mungu, naye ni mwenye kuhishimiwa kwake,
  20. ذِى قُوَّةٍ عِندَ ذِى ٱلْعَرْشِ مَكِينٍ۝٢٠

    Thee quwwatin ʿinda thee alʿarshi makeenin

    Mwenye nguvu na mwenye cheo kwa huyo Mwenye Kiti cha Enzi,20

    Maelezo
    [20] Mwenye nguvu katika kutekeleza waajibu wake, mwenye cheo na daraja mbele ya Mwenyezi Mungu Mwenye Kiti cha Enzi.
  21. مُّطَاعٍ ثَمَّ أَمِينٍ۝٢١

    Mutaʿin thamma ameenin

    Anaye t'iiwa, tena muaminifu.21

    Maelezo
    [21] Tena ni mwenye kut'iiwa, na muaminifu wa kuchukua wahyi miongoni wa walio juu.
  22. وَمَا صَاحِبُكُم بِمَجْنُونٍ۝٢٢

    Wama sahibukum bimajnoonin

    Na wala huyu mwenzenu hana wazimu.22

    Maelezo
    [22] Na huyo Mtume wenu ambaye ni mwenzenu, mnaye mjua kuwa ana akili timamu, si mwendawazimu.
  23. وَلَقَدْ رَءَاهُ بِٱلْأُفُقِ ٱلْمُبِينِ۝٢٣

    Walaqad raahu bialofuqi almubeeni

    Na hakika yeye alimwona kwenye upeo wa macho ulio safi.23

    Maelezo
    [23] Na ninaapa kuwa Muhammad s.a.w. bila ya shaka alimwona Jibrili katika upeo wa macho kwa mujibu wa inavyo onekana.
  24. وَمَا هُوَ عَلَى ٱلْغَيْبِ بِضَنِينٍ۝٢٤

    Wama huwa ʿala alghaybi bidaneenin

    Wala yeye si bakhili kwa mambo ya ghaibu.24

    Maelezo
    [24] Na Muhammad si bakhili wa kufikisha wahyi na kuwafunza watu.
  25. وَمَا هُوَ بِقَوْلِ شَيْطَـٰنٍ رَّجِيمٍ۝٢٥

    Wama huwa biqawli shaytanin rajeemin

    Wala hii si kauli ya Shetani maluuni.25

    Maelezo
    [25] Wala huu wahyi (ufunuo) ulio teremshwa juu yake si kauli ya Shetani aliye fukuzwa kutoka kwenye rehema ya Mwenyezi Mungu.
  26. فَأَيْنَ تَذْهَبُونَ۝٢٦

    Faayna tathhaboona

    Basi mnakwenda wapi?26

    Maelezo
    [26] Basi njia gani iliyo ya uwongofu zaidi kuliko hii mnayo ifuata?
  27. إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ لِّلْعَـٰلَمِينَ۝٢٧

    In huwa illa thikrun lilʿalameena

    Haikuwa hii ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote.27

    Maelezo
    [27] Qur'ani si chochote ila ni ukumbusho na mawaidha kwa walimwengu wote.
  28. لِمَن شَآءَ مِنكُمْ أَن يَسْتَقِيمَ۝٢٨

    Liman shaa minkum an yastaqeema

    Kwa yule miongoni mwenu anaye taka kwenda sawa.28

    Maelezo
    [28] Kwa anaye taka, miongoni mwenu, kusimama sawa kufikilia haki na kweli.
  29. وَمَا تَشَآءُونَ إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُ رَبُّ ٱلْعَـٰلَمِينَ۝٢٩

    Wama tashaoona illa an yashaa Allahu rabbu alʿalameena

    Wala nyinyi hamtataka isipo kuwa atake Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote.29

    Maelezo
    [29] Na nyinyi hamwezi kutaka kitu ila anapo taka Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Surat At-Takwir maana yake ni nini?

At-Takwir maana yake ni “Kukunjwa”.

Surat At-Takwir iko katika juzuu ya ngapi?

Surat At-Takwir iko katika juzuu ya 30.

Surat At-Takwir ina aya ngapi?

Surat At-Takwir ina aya 29.

Surat At-Takwir ni ya Makka au ya Madina?

Surat At-Takwir ni sura ya Makka.

Surat At-Takwir ni sura ya ngapi katika Qur’ani?

Ni sura ya 81 katika Qur’ani.

Vyanzo

  • Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
  • Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
  • Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
  • Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
  • Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
  • Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.

Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.

Mipangilio ya kusoma

Fonti ya Qur’ani
Ukubwa wa Kiarabu
100%
Ukubwa wa tafsiri
100%
Mandhari

Ongeza kwenye skrini ya kwanza

ReadSurahFungua ReadSurah kutoka skrini ya kwanza, kwa skrini nzima. Sura ulizosoma hufunguka hata bila intaneti.

  1. Katika Safari, gusa kitufe cha kushiriki (Share). Kwenye iPhone mpya kiko kwenye menyu ya •••.
  2. Gusa “Add to Home Screen”. Huenda ukahitaji kusogeza chini.
  3. Gusa “Add”.