Surat Abasa (عبس) ni sura ya 80 katika Qur’ani na ina aya 42. Jina lake lina maana ya “Alikunja Uso”. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na iko katika juzuu ya 30.
Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat Abasa yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.
Surat Abasa kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
-
عَبَسَ وَتَوَلَّىٰٓ١
ʿAbasa watawalla
Alikunja kipaji na akageuka!1
Maelezo
[1] Uso wake ulitaghayari kwa kuchukia na akageuka, -
أَن جَآءَهُ ٱلْأَعْمَىٰ٢
An jaahu alaʿma
Kwa sababu alimjia kipofu!2
Maelezo
[2] Kwa sababu kamjia kipofu anamuuliza khabari ya Dini yake. -
وَمَا يُدْرِيكَ لَعَلَّهُۥ يَزَّكَّىٰٓ٣
Wama yudreeka laʿallahu yazzakka
Na nini kitakujuulisha pengine yeye atatakasika?3
Maelezo
[3] Na wewe unajuaje, pengine huyo kipofu atatakasika kwa atayo yapata kwako, -
أَوْ يَذَّكَّرُ فَتَنفَعَهُ ٱلذِّكْرَىٰٓ٤
Aw yaththakkaru fatanfaʿahu alththikra
Au atawaidhika, na mawaidha yamfae?4
Maelezo
[4] Au atawaidhika na mawaidha yamfae. -
أَمَّا مَنِ ٱسْتَغْنَىٰ٥
Amma mani istaghna
Ama ajionaye hana haja!5
Maelezo
[5] Ama yule anaye jiona ametosheka kwa mali yake na nguvu zake, -
فَأَنتَ لَهُۥ تَصَدَّىٰ٦
Faanta lahu tasadda
Wewe ndio unamshughulikia?6
Maelezo
[6] Wewe ndio unamkabili na unamshughulikia kumfikishia wito wako. -
وَمَا عَلَيْكَ أَلَّا يَزَّكَّىٰ٧
Wama ʿalayka alla yazzakka
Na si juu yako kama hakutakasika.7
Maelezo
[7] Na wewe una lawama gani ikiwa yeye hakutakasika kwa Imani? -
وَأَمَّا مَن جَآءَكَ يَسْعَىٰ٨
Waamma man jaaka yasʿa
Ama anaye kujia kwa juhudi .8
Maelezo
[8] Ama anaye kukimbilia kutafuta ilimu na uwongofu, -
وَهُوَ يَخْشَىٰ٩
Wahuwa yakhsha
Naye anaogopa!9
Maelezo
[9] Naye anamkhofu Mwenyezi Mungu . -
فَأَنتَ عَنْهُ تَلَهَّىٰ١٠
Faanta ʿanhu talahha
Ndio wewe unampuuza?10
Maelezo
[10] Wewe unampuuza. -
كَلَّآ إِنَّهَا تَذْكِرَةٌ١١
Kalla innaha tathkiratun
Sivyo hivyo! Huku ni kukumbushana.11
Maelezo
[11] Hakika Aya hizi ni mawaidha. -
فَمَن شَآءَ ذَكَرَهُۥ١٢
Faman shaa thakarahu
Basi anaye penda akumbuke.12
Maelezo
[12] Mwenye kutaka atawaidhika kwa Qur'ani. -
فِى صُحُفٍ مُّكَرَّمَةٍ١٣
Fee suhufin mukarramatin
Yamo katika kurasa zilizo hishimiwa,13
Maelezo
[13] Nayo Qur'ani imo katika kurasa zilizo tukuzwa kwa Mwenyezi Mungu, -
مَّرْفُوعَةٍ مُّطَهَّرَةٍۭ١٤
Marfooʿatin mutahharatin
Zilizo inuliwa, zilizo takaswa.14
Maelezo
[14] Zina cheo cha juu, na pahala palipo tukuka, zimetakasika na kila upungufu. -
بِأَيْدِى سَفَرَةٍ١٥
Biaydee safaratin
Zimo mikononi mwa Malaika waandishi,15
Maelezo
[15] Katika mikono ya Malaika ambao Mwenyezi Mungu amewafanya ndio mabalozi baina yake na Mitume wake; -
كِرَامٍۭ بَرَرَةٍ١٦
Kiramin bararatin
Watukufu, wema.16
Maelezo
[16] Walio bora, wema. -
قُتِلَ ٱلْإِنسَـٰنُ مَآ أَكْفَرَهُۥ١٧
Qutila alinsanu ma akfarahu
Ameangamia mwanaadamu! Nini kinacho mkufurisha?17
Maelezo
[17] Ameangamia mwanaadamu! Nini kilicho mfanya akufuru na hali Mwenyezi Mungu amemfanyia hisani zote hizi? -
مِنْ أَىِّ شَىْءٍ خَلَقَهُۥ١٨
Min ayyi shayin khalaqahu
Kwa kitu gani amemuumba?18
Maelezo
[18] Hakumbuki yeye kaumbwa kutokana na nini? -
مِن نُّطْفَةٍ خَلَقَهُۥ فَقَدَّرَهُۥ١٩
Min nutfatin khalaqahu faqaddarahu
Kwa tone la manii, akamuumba na akamkadiria.19
Maelezo
[19] Kutokana na maji ya kudharauliwa Yeye Mwenyezi Mungu alimwanzisha kumuumba akamjaalia apitie daraja mbali mbali za kukua. -
ثُمَّ ٱلسَّبِيلَ يَسَّرَهُۥ٢٠
Thumma alssabeela yassarahu
Kisha akamsahilishia njia.20
Maelezo
[20] Kisha akamfanyia nyepesi njia ya kufikia Imani, na akamfunza njia hiyo. -
ثُمَّ أَمَاتَهُۥ فَأَقْبَرَهُۥ٢١
Thumma amatahu faaqbarahu
Kisha akamfisha, akamtia kaburini.21
Maelezo
[21] Kisha akamfisha na akamtukuza kwa kumtia kaburini. -
ثُمَّ إِذَا شَآءَ أَنشَرَهُۥ٢٢
Thumma itha shaa ansharahu
Kisha apendapo atamfufua.22
Maelezo
[22] Na tena akipenda atamhuisha baada ya kufa kwake. -
كَلَّا لَمَّا يَقْضِ مَآ أَمَرَهُۥ٢٣
Kalla lamma yaqdi ma amarahu
La! Hajamaliza aliyo muamuru.23
Maelezo
[23] Ni kweli mwanaadamu, juu ya kuwa umri wake mrefu duniani, hakutimiza aliyo amrishwa na Mwenyezi Mungu katika mambo ya Imani na ut'iifu. -
فَلْيَنظُرِ ٱلْإِنسَـٰنُ إِلَىٰ طَعَامِهِۦٓ٢٤
Falyanthuri alinsanu ila taʿamihi
Hebu mtu na atazame chakula chake.24
Maelezo
[24] Hebu mtu na aangalie shani ya chakula chake - vipi tulivyo kipanga na kumsahilishia! -
أَنَّا صَبَبْنَا ٱلْمَآءَ صَبًّا٢٥
Anna sababna almaa sabban
Hakika Sisi tumemimina maji kwa nguvu,25
Maelezo
[25] Ni Sisi tumeiteremsha mvua kutoka mbinguni, ikateremka. -
ثُمَّ شَقَقْنَا ٱلْأَرْضَ شَقًّا٢٦
Thumma shaqaqna alarda shaqqan
Tena tukaipasua pasua ardhi kwa nguvu,26
Maelezo
[26] Tena tukaipasua pasua ardhi kwa ajili ya mimea. -
فَأَنۢبَتْنَا فِيهَا حَبًّا٢٧
Faanbatna feeha habban
Kisha tukaotesha humo nafaka,27
Maelezo
[27] Tukaotesha humo nafaka ambazo watu huzila na huweka akiba. -
وَعِنَبًا وَقَضْبًا٢٨
Waʿinaban waqadban
Na zabibu, na mimea ya majani,28
Maelezo
[28] Na mizabibu na mimea ya majani inayo liwa mibichi. -
وَزَيْتُونًا وَنَخْلًا٢٩
Wazaytoonan wanakhlan
Na mizaituni, na mitende,29
Maelezo
[29] Na mizaituni mizuri, na mitende yenye kuzaa, -
وَحَدَآئِقَ غُلْبًا٣٠
Wahadaiqa ghulban
Na bustani zenye miti iliyo songana baraabara,30
Maelezo
[30] Na mabustani yaliyo songamana matawi ya miti yake, -
وَفَـٰكِهَةً وَأَبًّا٣١
Wafakihatan waabban
Na matunda, na malisho ya wanyama;31
Maelezo
[31] Na matunda ya kustaladhi nayo, na malisha ya kula nyama hoa (mifugo). -
مَّتَـٰعًا لَّكُمْ وَلِأَنْعَـٰمِكُمْ٣٢
Mataʿan lakum walianʿamikum
Kwa manufaa yenu na mifugo yenu.32
Maelezo
[32] Tumeotesha yote hayo kwa ajili ya faida yenu na wanyama wenu wa kufuga. -
فَإِذَا جَآءَتِ ٱلصَّآخَّةُ٣٣
Faitha jaati alssakhkhatu
Basi utakapo kuja ukelele,33
Maelezo
[33] Basi utakapo kuja ukelele wa Kiyama utakao tia uziwi masikio, -
يَوْمَ يَفِرُّ ٱلْمَرْءُ مِنْ أَخِيهِ٣٤
Yawma yafirru almaro min akheehi
Siku ambayo mtu atamkimbia nduguye,34
Maelezo
[34] Siku mtu atakapo mkimbia ndugu yake, -
وَأُمِّهِۦ وَأَبِيهِ٣٥
Waommihi waabeehi
Na mamaye na babaye,35
Maelezo
[35] Na mama yake, na baba yake, -
وَصَـٰحِبَتِهِۦ وَبَنِيهِ٣٦
Wasahibatihi wabaneehi
Na mkewe na wanawe.36
Maelezo
[36] Na mkewe, na wanawe! -
لِكُلِّ ٱمْرِئٍ مِّنْهُمْ يَوْمَئِذٍ شَأْنٌ يُغْنِيهِ٣٧
Likulli imriin minhum yawmaithin shanun yughneehi
Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na lake la kumtosha37
Maelezo
[37] Kila mmojapo katika hawa atakuwa na jambo lake la kumshughulisha! -
وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ مُّسْفِرَةٌ٣٨
Wujoohun yawmaithin musfiratun
Siku hiyo ziko nyuso zitazo nawiri,38
Maelezo
[38] Zipo nyuso siku hii zenye mwangaza, -
ضَاحِكَةٌ مُّسْتَبْشِرَةٌ٣٩
Dahikatun mustabshiratun
Zitacheka, zitachangamka;39
Maelezo
[39] Zenye kung'ara na kufurahi kwa neema za Mwenyezi Mungu. -
وَوُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ عَلَيْهَا غَبَرَةٌ٤٠
Wawujoohun yawmaithin ʿalayha ghabaratun
Na nyuso siku hiyo zitakuwa na mavumbi,40
Maelezo
[40] Na nyuso nyengine siku hii zina vumbi zimesawijika. -
تَرْهَقُهَا قَتَرَةٌ٤١
Tarhaquha qataratun
Giza totoro litazifunika,41
Maelezo
[41] Zimegubikwa na kiza na weusi. -
أُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْكَفَرَةُ ٱلْفَجَرَةُ٤٢
Olaika humu alkafaratu alfajaratu
Hao ndio makafiri watenda maovu42
Maelezo
[42] Wenye nyuso hizi ni makafiri wapotovu, ambao walio kuwa hawabali maasi waliyo kuwa wakiyatenda.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Surat Abasa maana yake ni nini?
Abasa maana yake ni “Alikunja Uso”.
Surat Abasa iko katika juzuu ya ngapi?
Surat Abasa iko katika juzuu ya 30.
Surat Abasa ina aya ngapi?
Surat Abasa ina aya 42.
Surat Abasa ni ya Makka au ya Madina?
Surat Abasa ni sura ya Makka.
Surat Abasa ni sura ya ngapi katika Qur’ani?
Ni sura ya 80 katika Qur’ani.
Vyanzo
- Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
- Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
- Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
- Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
- Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
- Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.
Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.