Surat Al-Qiyama (القيامة) ni sura ya 75 katika Qur’ani na ina aya 40. Jina lake lina maana ya “Kiyama”. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na iko katika juzuu ya 29.
Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat Al-Qiyama yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.
Surat Al-Qiyama kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
-
لَآ أُقْسِمُ بِيَوْمِ ٱلْقِيَـٰمَةِ١
La oqsimu biyawmi alqiyamati
Ninaapa kwa Siku ya Kiyama!1
Maelezo
[1] Ninaapa na natilia mkazo kiapo hichi kwa Siku ya Kiyama, na hiyo ni kweli iliyo thibiti; -
وَلَآ أُقْسِمُ بِٱلنَّفْسِ ٱللَّوَّامَةِ٢
Wala oqsimu bialnnafsi allawwamati
Na ninaapa kwa nafsi inayo jilaumu!2
Maelezo
[2] Na ninaapa na natilia mkazo kiapo hichi kwa nafsi inayo mlaumu mtu kwa dhambi zake na upungufu wake, ya kwamba bila ya shaka yoyote mtafufuliwa baada ya kukusanywa mafupa yenu yaliyo tawanyika. -
أَيَحْسَبُ ٱلْإِنسَـٰنُ أَلَّن نَّجْمَعَ عِظَامَهُۥ٣
Ayahsabu alinsanu allan najmaʿa ʿithamahu
Anadhani mtu kuwa Sisi hatutaikusanya mifupa yake?3
Maelezo
[3] Hivyo mtu anadhani baada ya kuwa Sisi tulimuumba naye hakuwa kitu chochote, tutakuja shindwa kuyakusanya mafupa yake yaliyooza na yakatapanyika? -
بَلَىٰ قَـٰدِرِينَ عَلَىٰٓ أَن نُّسَوِّىَ بَنَانَهُۥ٤
Bala qadireena ʿala an nusawwiya bananahu
Kwani! Sisi tunaweza hata kuziweka sawa sawa ncha za vidole vyake!4
Maelezo
[4] Hasha! Sisi tuna uweza wa kuviweka sawa hata vifupa vya vidole vyake vilivyo vurugika, wachilia mbali mafupa yake makubwa makubwa ya mwili wake. -
بَلْ يُرِيدُ ٱلْإِنسَـٰنُ لِيَفْجُرَ أَمَامَهُۥ٥
Bal yureedu alinsanu liyafjura amamahu
Lakini mtu anataka tu kuendelea na maasi kwa siku zilioko mbele yake.5
Maelezo
[5] Hivyo mtu anakanya kufufuliwa? Anataka abakie katika uasi wake katika siku zote zilizo mbakilia katika umri wake ulio salia? -
يَسْـَٔلُ أَيَّانَ يَوْمُ ٱلْقِيَـٰمَةِ٦
Yasalu ayyana yawmu alqiyamati
Anauliza: Lini itakuwa hiyo Siku ya Kiyama?6
Maelezo
[6] Anauliza kwa kuona haiwezi kutokea saa ya Kiyama: Lini itakuwa hiyo Siku ya Kiyama? -
فَإِذَا بَرِقَ ٱلْبَصَرُ٧
Faitha bariqa albasaru
Basi jicho litapo dawaa!7
Maelezo
[7] Jicho litapo tahayari kwa kufazaika na kushtuka, -
وَخَسَفَ ٱلْقَمَرُ٨
Wakhasafa alqamaru
Na mwezi utapo patwa!8
Maelezo
[8] Na mwangaza wa mwezi ukapotea, -
وَجُمِعَ ٱلشَّمْسُ وَٱلْقَمَرُ٩
Wajumiʿa alshshamsu waalqamaru
Na likakusanywa jua na mwezi!9
Maelezo
[9] Na jua likakusanyika na mwezi kuchomoza magharibi, -
يَقُولُ ٱلْإِنسَـٰنُ يَوْمَئِذٍ أَيْنَ ٱلْمَفَرُّ١٠
Yaqoolu alinsanu yawmaithin ayna almafarru
Siku hiyo mtu atasema: Yako wapi makimbilio?10
Maelezo
[10] Mtu hapo atasema: Yako wapi makimbilio kuikimbia hii adhabu? -
كَلَّا لَا وَزَرَ١١
Kalla la wazara
La! Hapana pa kukimbilia!11
Maelezo
[11] Huachi, ewe mtu, kutafuta makimbilio? Leo huna pa kukimbilia wewe, -
إِلَىٰ رَبِّكَ يَوْمَئِذٍ ٱلْمُسْتَقَرُّ١٢
Ila rabbika yawmaithin almustaqarru
Siku hiyo pa kutua ni kwa Mola wako Mlezi tu.12
Maelezo
[12] ila kwa Mola wako Mlezi peke yake, ndipo penye matulivu ya waja, Peponi au Motoni. -
يُنَبَّؤُا۟ ٱلْإِنسَـٰنُ يَوْمَئِذٍۭ بِمَا قَدَّمَ وَأَخَّرَ١٣
Yunabbao alinsanu yawmaithin bima qaddama waakhkhara
Siku hiyo ataambiwa aliyo yatanguliza na aliyo yaakhirisha.13
Maelezo
[13] Siku hiyo mtu ataambiwa vitendo vyake alivyo vitanguliza na alivyo viakhirisha. -
بَلِ ٱلْإِنسَـٰنُ عَلَىٰ نَفْسِهِۦ بَصِيرَةٌ١٤
Bali alinsanu ʿala nafsihi baseeratun
Bali mtu ni hoja juu ya nafsi yake.14
Maelezo
[14] Bali mtu yeye mwenyewe ni hoja iliyo wazi juu ya nafsi yake inayo mkazania kwa anayo yatenda na anayo yaacha. -
وَلَوْ أَلْقَىٰ مَعَاذِيرَهُۥ١٥
Walaw alqa maʿatheerahu
Na ingawa atatoa chungu ya udhuru.15
Maelezo
[15] Na ijapo kuwa atajitolea chungu nzima ya udhuru na akazieneza, hawezi kabisa kuepukana na hoja hizo. -
لَا تُحَرِّكْ بِهِۦ لِسَانَكَ لِتَعْجَلَ بِهِۦٓ١٦
La tuharrik bihi lisanaka litaʿjala bihi
Usiutikisie huu wahyi ulimi wako kwa kuufanyia haraka.16
Maelezo
[16] Usiuharikishe ulimi wako kwa kuisoma Qur'ani na kujaribu kuihifadhi kwa haraka pale unapo teremshiwa kwa Wahyi. -
إِنَّ عَلَيْنَا جَمْعَهُۥ وَقُرْءَانَهُۥ١٧
Inna ʿalayna jamʿahu waquranahu
Hakika ni juu yetu kuukusanya na kuusomesha.17
Maelezo
[17] Hakika ni juu yetu Sisi kuikusanya hiyo katika kifua chako, na kuithibitisha katika ulimi wako. -
فَإِذَا قَرَأْنَـٰهُ فَٱتَّبِعْ قُرْءَانَهُۥ١٨
Faitha qaranahu faittabiʿ quranahu
Tunapo usoma, basi nawe fuatiliza kusoma kwake.18
Maelezo
[18] Akikusomea Mjumbe wetu (Jibril) basi nawe ifuatilize kama unavyo isikia. -
ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا بَيَانَهُۥ١٩
Thumma inna ʿalayna bayanahu
Kisha ni juu yetu kuubainisha.19
Maelezo
[19] Kisha baada ya hayo ni juu yetu kuibainisha ikiingia tatizo lolote juu yako. -
كَلَّا بَلْ تُحِبُّونَ ٱلْعَاجِلَةَ٢٠
Kalla bal tuhibboona alʿajilata
Hasha! Bali nyinyi mnapenda maisha ya duniani,20
Maelezo
[20] Wacheni kukanya kufufuliwa, na hilo ni jambo la kweli. Lakini nyinyi mnaipenda dunia na starehe zake, -
وَتَذَرُونَ ٱلْـَٔاخِرَةَ٢١
Watatharoona alakhirata
Na mnaacha maisha ya Akhera.21
Maelezo
[21] Na mnaiacha Akhera na neema zake. -
وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ نَّاضِرَةٌ٢٢
Wujoohun yawmaithin nadiratun
Zipo nyuso siku hiyo zitao ng'ara,22
Maelezo
[22] Siku hiyo zitakuwapo nyuso nzuri, zenye kumwangalia Mola wao Mlezi bila ya kusema kwa sifa gani, wajihi gani, au masafa gani. -
إِلَىٰ رَبِّهَا نَاظِرَةٌ٢٣
Ila rabbiha nathiratun
Zinamwangallia Mola wao Mlezi.23
Maelezo
[23] Siku hiyo zitakuwapo nyuso nzuri, zenye kumwangalia Mola wao Mlezi bila ya kusema kwa sifa gani, wajihi gani, au masafa gani. -
وَوُجُوهٌ يَوْمَئِذٍۭ بَاسِرَةٌ٢٤
Wawujoohun yawmaithin basiratun
Na zipo nyuso siku hiyo zitakao kunjana.24
Maelezo
[24] Na nyuso nyengine zitakuwapo zimenuna, zimekunjana mno, zinangojea zitendewe jambo ambalo kwa kitisho chake linavunja uti wa mgongo. -
تَظُنُّ أَن يُفْعَلَ بِهَا فَاقِرَةٌ٢٥
Tathunnu an yufʿala biha faqiratun
Zitajua ya kuwa zitafikiwa na livunjalo uti wa mgongo.25
Maelezo
[25] Zinangojea zitendewe jambo ambalo kwa kitisho chake linavunja uti wa mgongo. -
كَلَّآ إِذَا بَلَغَتِ ٱلتَّرَاقِىَ٢٦
Kalla itha balaghati alttaraqiya
La, hasha! (Roho) itakapo fikia kwenye mafupa ya koo,26
Maelezo
[26] Mna nini na kuipenda dunia ambayo mnaifariki roho inapo fika katika mafupa ya kooni, -
وَقِيلَ مَنْ ۜ رَاقٍ٢٧
Waqeela man raqin
Na pakasemwa: Nani wa kumganga?27
Maelezo
[27] Na walio hudhuria wakasema: Yupo wa kumganga huyu kwa haya aliyo nayo? -
وَظَنَّ أَنَّهُ ٱلْفِرَاقُ٢٨
Wathanna annahu alfiraqu
Na mwenyewe akajua kwa hakika kuwa huko ndiko kufariki;28
Maelezo
[28] Akayakinisha yule yaliyo mfika mauti kama lililo mshukia ni kuiacha dunia inayo pendwa, na imekwisha mfika shida yake kikomo cha mwisho. -
وَٱلْتَفَّتِ ٱلسَّاقُ بِٱلسَّاقِ٢٩
Wailtaffati alssaqu bialssaqi
Na utapo ambatishwa muundi kwa muundi,29
Maelezo
[29] Na muundi wa mguu umekwisha ambatana na wa pili wakati wa kutoka roho. -
إِلَىٰ رَبِّكَ يَوْمَئِذٍ ٱلْمَسَاقُ٣٠
Ila rabbika yawmaithin almasaqu
Siku hiyo ndiyo kuchungwa kupelekwa kwa Mola wako Mlezi!30
Maelezo
[30] Kwa Mola wako Mlezi tu siku hiyo ndio machungio ya waja, ama Peponi au Motoni. -
فَلَا صَدَّقَ وَلَا صَلَّىٰ٣١
Fala saddaqa wala salla
Kwa sababu hakusadiki, wala hakuswali.31
Maelezo
[31] Binaadamu amekanya kufufuliwa, na kwa hivyo hakumsadiki Mtume wala Qur'ani. Wala hakumtimizia Mwenyezi Mungu faridha za Swala. -
وَلَـٰكِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ٣٢
Walakin kaththaba watawalla
Bali alikanusha, na akageuka.32
Maelezo
[32] Lakini aliikadhibisha Qur'ani, akaipuuza Imani, -
ثُمَّ ذَهَبَ إِلَىٰٓ أَهْلِهِۦ يَتَمَطَّىٰٓ٣٣
Thumma thahaba ila ahlihi yatamatta
Kisha akenda kwa ahali zake kwa matao.33
Maelezo
[33] Na akatoka kwenda kwa watu wake wa nyumbani kwa maringo na kujitapa. -
أَوْلَىٰ لَكَ فَأَوْلَىٰ٣٤
Awla laka faawla
Ole wako, ole wako!34
Maelezo
[34] Ewe unaye kadhibisha, utaangamia! -
ثُمَّ أَوْلَىٰ لَكَ فَأَوْلَىٰٓ٣٥
Thumma awla laka faawla
Kisha Ole wako, ole wako!35
Maelezo
[35] Tena utaangamia! Na tena utaangamia, na utaangamia! -
أَيَحْسَبُ ٱلْإِنسَـٰنُ أَن يُتْرَكَ سُدًى٣٦
Ayahsabu alinsanu an yutraka sudan
Ati anadhani binaadamu kuwa ataachwa bure?36
Maelezo
[36] Hivyo anadhani huyu mtu anaye kanya kufufuliwa kuwa ataachwa hivi hivi akiringa tu katika maisha yake, na akisha kufa iwe basi, wala asifufuliwe akahisabiwa kwa vitendo vyake? -
أَلَمْ يَكُ نُطْفَةً مِّن مَّنِىٍّ يُمْنَىٰ٣٧
Alam yaku nutfatan min manayyin yumna
Kwani hakuwa yeye tone ya manii lilio shushwa?37
Maelezo
[37] Kwani yeye mtu hakuwa ni tone tu ya manii, ilio jaaliwa kuwemo katika tumbo la uzazi? -
ثُمَّ كَانَ عَلَقَةً فَخَلَقَ فَسَوَّىٰ٣٨
Thumma kana ʿalaqatan fakhalaqa fasawwa
Kisha akawa kidonge cha damu, tena Mwenyezi Mungu akamuumba na akamtengeneza vilivyo.38
Maelezo
[38] Kisha hiyo tone ikawa kipande cha damu iliyo ganda, na Mwenyezi Mungu akaiumba, akaisawazisha mpaka ikawa na umbo zuri? -
فَجَعَلَ مِنْهُ ٱلزَّوْجَيْنِ ٱلذَّكَرَ وَٱلْأُنثَىٰٓ٣٩
Fajaʿala minhu alzzawjayni alththakara waalontha
Kisha akamfanya namna mbili, mwanamume na mwanamke.39
Maelezo
[39] Akajaalia namna mbili, mwanamume na mwanamke? -
أَلَيْسَ ذَٰلِكَ بِقَـٰدِرٍ عَلَىٰٓ أَن يُحْـِۧىَ ٱلْمَوْتَىٰ٤٠
Alaysa thalika biqadirin ʿala an yuhyiya almawta
Je! Huyo hakuwa ni Muweza wa kufufua wafu?40
Maelezo
[40] Je! Huyo Muumba wa mwanzo aliye fanya yote haya, basi si muweza wa kuwahuisha maiti baada ya kuyakusanya mafupa yao?
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Surat Al-Qiyama maana yake ni nini?
Al-Qiyama maana yake ni “Kiyama”.
Surat Al-Qiyama iko katika juzuu ya ngapi?
Surat Al-Qiyama iko katika juzuu ya 29.
Surat Al-Qiyama ina aya ngapi?
Surat Al-Qiyama ina aya 40.
Surat Al-Qiyama ni ya Makka au ya Madina?
Surat Al-Qiyama ni sura ya Makka.
Surat Al-Qiyama ni sura ya ngapi katika Qur’ani?
Ni sura ya 75 katika Qur’ani.
Vyanzo
- Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
- Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
- Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
- Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
- Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
- Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.
Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.