سورة الأنبياء

Surat Al-Anbiya kwa Kiswahili

Manabii

Msahafu

Mishary Rashid AlafasyPakua MP3Pakua PDF

Surat Al-Anbiya (الأنبياء) ni sura ya 21 katika Qur’ani na ina aya 112. Jina lake lina maana ya “Manabii”. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na iko katika juzuu ya 17.

Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat Al-Anbiya yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.

Surat Al-Anbiya kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

  1. ٱقْتَرَبَ لِلنَّاسِ حِسَابُهُمْ وَهُمْ فِى غَفْلَةٍ مُّعْرِضُونَ۝١

    Iqtaraba lilnnasi hisabuhum wahum fee ghaflatin muʿridoona

    IMEWAKARIBIA watu hisabu yao, nao wamo katika mghafala wanapuuza.1

    Maelezo
    [1] Umewakaribia washirikina wakati wao wa kuhisabiwa Siku ya Kiyama, nao hali wameghafilika na kitisho chake, wanapuuza kuiamini.
  2. مَا يَأْتِيهِم مِّن ذِكْرٍ مِّن رَّبِّهِم مُّحْدَثٍ إِلَّا ٱسْتَمَعُوهُ وَهُمْ يَلْعَبُونَ۝٢

    Ma yateehim min thikrin min rabbihim muhdathin illa istamaʿoohu wahum yalʿaboona

    Hayawafikilii mawaidha mapya kutoka kwa Mola wao Mlezi ila huyasikiliza na huku wanafanya mchezo.2

    Maelezo
    [2] Haiwajii Qur'ani kutokana na Mola wao Mlezi pale inapoteremka kuwakumbusha ya kuwanufaisha, ila wao huisikiliza na hali wao wameshughulika na mengine yasiyo na faida nao, wakicheza kama wachezavyo watoto wadogo.
  3. لَاهِيَةً قُلُوبُهُمْ ۗ وَأَسَرُّوا۟ ٱلنَّجْوَى ٱلَّذِينَ ظَلَمُوا۟ هَلْ هَـٰذَآ إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ ۖ أَفَتَأْتُونَ ٱلسِّحْرَ وَأَنتُمْ تُبْصِرُونَ۝٣

    Lahiyatan quloobuhum waasarroo alnnajwa allatheena thalamoo hal hatha illa basharun mithlukum afatatoona alssihra waantum tubsiroona

    Zimeghafilika nyoyo zao. Na wale walio dhulumu hunong'onezana kwa siri: Ni nani ati huyu isipo kuwa ni binaadamu tu kama nyinyi! Mnauwendea uchawi hali nanyi mnaona?3

    Maelezo
    [3] Nyoyo zao zimo katika pumbao, hazizingatii, wameshikilia kuficha njama zao za kumpinga Nabii na Qur'ani, wakiambizana wenyewe kwa wenyewe: Huyu Muhammad si chochote ila ni mtu tu kama nyinyi. Na Mtume hawi ila Malaika. Basi, je! Mnamsadiki Muhammad na mnahudhuria baraza za uchawi na hali nyinyi mnaona kuwa hakika huo ni uchawi?
  4. قَالَ رَبِّى يَعْلَمُ ٱلْقَوْلَ فِى ٱلسَّمَآءِ وَٱلْأَرْضِ ۖ وَهُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلْعَلِيمُ۝٤

    Qala rabbee yaʿlamu alqawla fee alssamai waalardi wahuwa alssameeʿu alʿaleemu

    Alisema: Mola wangu Mlezi anayajua yasemwayo mbinguni na katika ardhi. Na Yeye ni Mwenye kusikia Mwenye kujua.4

    Maelezo
    [4] Mtume, kwa kuwa Mwenyezi Mungu kamjuulisha waliyo kuwa wakiyasema kwa siri, aliwaambia: Mola wangu Mlezi anayajua yote yanayo semwa katika mbingu na katika ardhi, na Yeye ndiye anaye sikia kila linalo sikiwa; na anajua kila linalo tokea..
  5. بَلْ قَالُوٓا۟ أَضْغَـٰثُ أَحْلَـٰمٍۭ بَلِ ٱفْتَرَىٰهُ بَلْ هُوَ شَاعِرٌ فَلْيَأْتِنَا بِـَٔايَةٍ كَمَآ أُرْسِلَ ٱلْأَوَّلُونَ۝٥

    Bal qaloo adghathu ahlamin bali iftarahu bal huwa shaʿirun falyatina biayatin kama orsila alawwaloona

    Lakini wao walisema: Hizo ni ndoto za ovyo ovyo, bali amezizua tu, bali huyo ni mtunga mashairi. Basi atuletee miujiza kama walivyo tumwa wale wa mwanzo.5

    Maelezo
    [5] Bali wao wakasema: Hizi ni mchanganyiko wa ndoto alizo ziota (Muhammad); bali kazua tu na akamsingizia Mwenyezi Mungu kwa uwongo. Kisha wakaacha hayo na wakasema: Bali huyu ni mtunga mashairi anaziteka nafsi za wenye kumsikiliza. Kama kweli, basi na atuletee muujiza khasa wa kuonyesha ukweli wake, kama walivyo tumwa Manabii wa zamani wakitiwa nguvu kwa miujiza mbali mbali.
  6. مَآ ءَامَنَتْ قَبْلَهُم مِّن قَرْيَةٍ أَهْلَكْنَـٰهَآ ۖ أَفَهُمْ يُؤْمِنُونَ۝٦

    Ma amanat qablahum min qaryatin ahlaknaha afahum yuminoona

    Hawakuamini kabla yao watu wa mji tulio uangamiza. Basi, je, wataamini hawa?6

    Maelezo
    [6] Hizo kaumu tulizo ziangamiza baada ya kukadhibisha hiyo miujiza hazikuamini. Basi, je! Watakuja amini hawa yatapo wajia hayo wayatakayo?
  7. وَمَآ أَرْسَلْنَا قَبْلَكَ إِلَّا رِجَالًا نُّوحِىٓ إِلَيْهِمْ ۖ فَسْـَٔلُوٓا۟ أَهْلَ ٱلذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ۝٧

    Wama arsalna qablaka illa rijalan noohee ilayhim faisaloo ahla alththikri in kuntum la taʿlamoona

    Na kabla yako hatukuwatuma ila watu wanaume tulio wapa wahyi (ufunuo). Basi waulizeni wenye ilimu ikiwa nyinyi hamjui.7

    Maelezo
    [7] Ewe Nabii! Kabla yako wewe hatukuwatumia watu ila watu wa kibinaadamu vile vile, ambao tuliwafunulia Dini waifikishe kwa watu. Basi, enyi mnao kataa! Waulizeni wanazuoni wajuao ilimu za Vitabu vilivyo teremka, ikiwa nyinyi hamyajui hayo.
  8. وَمَا جَعَلْنَـٰهُمْ جَسَدًا لَّا يَأْكُلُونَ ٱلطَّعَامَ وَمَا كَانُوا۟ خَـٰلِدِينَ۝٨

    Wama jaʿalnahum jasadan la yakuloona alttaʿama wama kanoo khalideena

    Wala hatukuwafanya miili isiyo kula chakula, wala hawakuwa wenye kuishi milele.8

    Maelezo
    [8] Wala Sisi hatukuwajaalia Mitume kuwa na miili inayo khitalifiana na miili ya wanaadamu wengine, wakawa wanaishi bila ya chakula, na wakabaki siku zote, na wala hawakuwa wanaishi daima milele.
  9. ثُمَّ صَدَقْنَـٰهُمُ ٱلْوَعْدَ فَأَنجَيْنَـٰهُمْ وَمَن نَّشَآءُ وَأَهْلَكْنَا ٱلْمُسْرِفِينَ۝٩

    Thumma sadaqnahumu alwaʿda faanjaynahum waman nashao waahlakna almusrifeena

    Kisha tukawatimizia miadi, na tukawaokoa wao na tulio wataka, na tukawateketeza walio pita mipaka.9

    Maelezo
    [9] Kisha tukawatimizia na tukawahakikishia ahadi, na tukawaokoa wao na pamoja nao tukawaokoa tulio taka kuwaokoa miongoni mwa Waumini. Na makafiri walio vuka mipaka tuliwaangamiza kwa kukadhibisha kwao na kuukataa Ujumbe wa Manabii wao.
  10. لَقَدْ أَنزَلْنَآ إِلَيْكُمْ كِتَـٰبًا فِيهِ ذِكْرُكُمْ ۖ أَفَلَا تَعْقِلُونَ۝١٠

    Laqad anzalna ilaykum kitaban feehi thikrukum afala taʿqiloona

    Na hakika tumekuteremshieni Kitabu ambacho ndani yake yamo makumbusho yenu. Je! Hamzingatii?10

    Maelezo
    [10] Sisi hakika tumekuteremshieni Kitabu. Ndani yake yamo mawaidha ya kuwakumbusheni ikiwa mtakisoma na mtayatenda yaliyomo ndani yake. Basi huwaje mkakipuuza na mkakikataa? Je, inda na upumbavu umefika hadi ya kukufikisheni hali hii mlio nayo, mkawa hamuelewi lipi lenye manufaa nanyi mkalikimbilia?
  11. وَكَمْ قَصَمْنَا مِن قَرْيَةٍ كَانَتْ ظَالِمَةً وَأَنشَأْنَا بَعْدَهَا قَوْمًا ءَاخَرِينَ۝١١

    Wakam qasamna min qaryatin kanat thalimatan waanshana baʿdaha qawman akhareena

    Na mingapi katika miji iliyo kuwa ikidhulumu tumeiteketeza, na tukawasimamisha baada yao watu wengine.11

    Maelezo
    [11] Na wengi katika watu wa miji tuliyo iteketeza kwa sababu ya ukafiri wao na kuwakadhibisha Manabii, na baada yao tukasimamisha kaumu nyengine zenye hali bora na mwisho mwema kuliko hao.
  12. فَلَمَّآ أَحَسُّوا۟ بَأْسَنَآ إِذَا هُم مِّنْهَا يَرْكُضُونَ۝١٢

    Falamma ahassoo basana itha hum minha yarkudoona

    Basi walipo ihisi adhabu yetu, mara wakaanza kukimbia.12

    Maelezo
    [12] Na tulipo taka kuwateketeza, na wakahisi ukali wa adhabu yetu na uwezo wetu wa kuwateremshia hayo yatakayo wapata, wakafanya haraka kukimbia, kama wanyama hayawani, ati kutafuta kuokoka!
  13. لَا تَرْكُضُوا۟ وَٱرْجِعُوٓا۟ إِلَىٰ مَآ أُتْرِفْتُمْ فِيهِ وَمَسَـٰكِنِكُمْ لَعَلَّكُمْ تُسْـَٔلُونَ۝١٣

    La tarkudoo wairjiʿoo ila ma otriftum feehi wamasakinikum laʿallakum tusaloona

    Msikimbie! Na rejeeni kwenye zile zile starehe zenu, na maskani zenu, mpate kusailiwa!13

    Maelezo
    [13] Enyi wapinzani! Msikimbie! Hapana kitu chochote kitacho kulindeni na adhabu ya Mwenyezi Mungu. Rudini kwenye zile zile neema na majumba mliyo kuwa nayo, huenda watumishi wenu na wenzenu watakutakeni msaada na rai kama ilivyo kuwa ada yenu. Wapi! Hamtoweza!
  14. قَالُوا۟ يَـٰوَيْلَنَآ إِنَّا كُنَّا ظَـٰلِمِينَ۝١٤

    Qaloo ya waylana inna kunna thalimeena

    Wakasema: Ole wetu! Hakika sisi tulikuwa madhaalimu.14

    Maelezo
    [14] Kwa kuwa hao makafiri wamekwisha sikia wanavyo kejeliwa na wanavyo itwa kwenda teketezwa na wana yakini nako, basi watasema: Hakika kweli sisi tulikuwa ni wenye kudhulumu tulipo yaacha yanayo tunafiisha, na tusiziamini Ishara za Mola wetu Mlezi.
  15. فَمَا زَالَت تِّلْكَ دَعْوَىٰهُمْ حَتَّىٰ جَعَلْنَـٰهُمْ حَصِيدًا خَـٰمِدِينَ۝١٥

    Fama zalat tilka daʿwahum hatta jaʿalnahum haseedan khamideena

    Hakikuacha hicho kuwa kilio chao mpaka tukawafanya kama walio fyekwa, wamezimika.15

    Maelezo
    [15] Maneno hayo hawaachi kuyakariri na kuyapigia makelele mpaka kwa adhabu yetu tukawafanya kama mimea iliyo fyekwa, na moto ulio zimika, hawana tena uhai.
  16. وَمَا خَلَقْنَا ٱلسَّمَآءَ وَٱلْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا لَـٰعِبِينَ۝١٦

    Wama khalaqna alssamaa waalarda wama baynahuma laʿibeena

    Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yao kwa mchezo.16

    Maelezo
    [16] Wala hatukuziumba mbingu na ardhi na viliomo baina yao kwa mpango huu wa hikima, na muundo huu wa namna peke yake, kwa mchezo. Bali tumefanya yote haya kwa hikima ya juu ambayo wanaifahamu wenye kuzingatia.
  17. لَوْ أَرَدْنَآ أَن نَّتَّخِذَ لَهْوًا لَّٱتَّخَذْنَـٰهُ مِن لَّدُنَّآ إِن كُنَّا فَـٰعِلِينَ۝١٧

    Law aradna an nattakhitha lahwan laittakhathnahu min ladunna in kunna faʿileena

    Kama tungeli taka kufanya mchezo tunge jifanyia Sisi wenyewe, lau kwamba tungeli kuwa ni wafanyao mchezo.17

    Maelezo
    [17] Lau kuwa tunataka kufanya mchezo na pumbao isingeli mkinika kuchukua ila yaliyo katika ufalme wetu, kwani hapana ufalme ila wetu - ingeli kuwa Sisi ni wa kufanya hayo. Wala nasi si wenye kufanya hayo, kwa kuwa si laiki ya haki yetu.
  18. بَلْ نَقْذِفُ بِٱلْحَقِّ عَلَى ٱلْبَـٰطِلِ فَيَدْمَغُهُۥ فَإِذَا هُوَ زَاهِقٌ ۚ وَلَكُمُ ٱلْوَيْلُ مِمَّا تَصِفُونَ۝١٨

    Bal naqthifu bialhaqqi ʿala albatili fayadmaghuhu faitha huwa zahiqun walakumu alwaylu mimma tasifoona

    Bali tunaitupa kweli juu ya uwongo ikauvunja na mara ukatoweka. Na ole wenu kwa mnayo yazua.18

    Maelezo
    [18] Lakini jambo linalo tuelekea Sisi kulifanya ni kuipambanisha kweli juu ya uwongo ipate kuuondoa. Na nyinyi makafiri mtahiliki kwa sababu ya kumzulia Mwenyezi Mungu na Mtume wake.
  19. وَلَهُۥ مَن فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۚ وَمَنْ عِندَهُۥ لَا يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِهِۦ وَلَا يَسْتَحْسِرُونَ۝١٩

    Walahu man fee alssamawati waalardi waman ʿindahu la yastakbiroona ʿan ʿibadatihi wala yastahsiroona

    Na ni vyake Yeye tu Mwenyezi Mungu vilivyomo mbinguni na katika ardhi. Na walioko kwake hawafanyi kiburi wakaacha kumuabudu, wala hawachoki.19

    Maelezo
    [19] Na ni vya Mwenyezi Mungu peke yake vyote viliomo mbinguni na katika ardhi, kwa kuviumba na kuvimiliki. Basi ni haki Yeye peke yake kuabudiwa. Na Malaika walio karibishwa kwake hawana kiburi cha kuwazuia kumuabudu na kumnyenyekea, wala hawaoni machofu na kunyong'onyea kwa ibada ya mchana na usiku.
  20. يُسَبِّحُونَ ٱلَّيْلَ وَٱلنَّهَارَ لَا يَفْتُرُونَ۝٢٠

    Yusabbihoona allayla waalnnahara la yafturoona

    Wanamtakasa usiku na mchana, wala hawanyong'onyei.20

    Maelezo
    [20] Wanamtakasa aliye tukuka shani yake na kila lisio muelekea. Kumtakasa huku hakusiti, bali huo ni mtakaso wa daima, hawana shughuli nyengine ya kuwashughulisha.
  21. أَمِ ٱتَّخَذُوٓا۟ ءَالِهَةً مِّنَ ٱلْأَرْضِ هُمْ يُنشِرُونَ۝٢١

    Ami ittakhathoo alihatan mina alardi hum yunshiroona

    Au wamepata miungu katika ardhi inayo fufua?21

    Maelezo
    [21] Washirikina hawafanyi wafanyavyo walio karibishwa katika kumsafishia ibada Mwenyezi Mungu, bali wao wamewaabudu wenginewe, na wakafanya miungu duniani isiyo stahiki kuabudiwa. Na huwaje kwenda kuabudu kitu kisicho kuwa Mwenyezi Mungu, ambacho hakiwezi kufufua?
  22. لَوْ كَانَ فِيهِمَآ ءَالِهَةٌ إِلَّا ٱللَّهُ لَفَسَدَتَا ۚ فَسُبْحَـٰنَ ٱللَّهِ رَبِّ ٱلْعَرْشِ عَمَّا يَصِفُونَ۝٢٢

    Law kana feehima alihatun illa Allahu lafasadata fasubhana Allahi rabbi alʿarshi ʿamma yasifoona

    Lau wangeli kuwamo humo miungu wengine isipo kuwa Mwenyezi Mungu basi bila ya shaka hizo mbingu na ardhi zingeli fisidika. Subahana 'Llah Ametakasika Mwenyezi Mungu, Bwana wa A'rshi (Kiti cha Enzi), na hayo wanayo yazua.22

    Maelezo
    [22] Lau kuwa mbinguni na duniani kuna miungu isipo kuwa Mwenyezi Mungu wanao endesha mambo yao, basi ingeli haribika nidhamu iliyo simamishiwa hizo mbingu na ardhi kwa kuumbwa, na ikafikilia mwisho wa mpango na hikima. Basi na atakasike Mwenyezi Mungu, Mwenye Ufalme wote, na yote wanayo msingizia washirikina.
  23. لَا يُسْـَٔلُ عَمَّا يَفْعَلُ وَهُمْ يُسْـَٔلُونَ۝٢٣

    La yusalu ʿamma yafʿalu wahum yusaloona

    Yeye hahojiwi kwa ayatendayo, na wao ndio wanao hojiwa kwa wayatendayo.23

    Maelezo
    [23] Yeye Subhanahu hahojiwi kwa anayo yatenda, kwani ni Yeye pekee mwenye utukufu na madaraka, Mwenye hikima na ujuzi. Hakosei katika kutenda chochote. Ni wao ndio watahisabiwa na kuhojiwa kwa wanayo yatenda, kwa kuwa wao hukosea kwa udhaifu wao na ujinga wao na kughilibiwa na matamanio.
  24. أَمِ ٱتَّخَذُوا۟ مِن دُونِهِۦٓ ءَالِهَةً ۖ قُلْ هَاتُوا۟ بُرْهَـٰنَكُمْ ۖ هَـٰذَا ذِكْرُ مَن مَّعِىَ وَذِكْرُ مَن قَبْلِى ۗ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ٱلْحَقَّ ۖ فَهُم مُّعْرِضُونَ۝٢٤

    Ami ittakhathoo min doonihi alihatan qul hatoo burhanakum hatha thikru man maʿiya wathikru man qablee bal aktharuhum la yaʿlamoona alhaqqa fahum muʿridoona

    Au wanawaabudu miungu mingine badala yake? Sema: Leteni ushahidi wenu! Haya ni ukumbusho wa hawa walio nami, na ukumbusho wa walio kabla yangu. Lakini wengi wao hawaijui kweli, na kwa hivyo wanapuuza.24

    Maelezo
    [24] Hawaujui waajibu wa Mwenyezi Mungu uliyo juu yao, ndio maana wakawa na miungu mingine isiyo kuwa Yeye wakaiabudu bila ya kuwa na ushahidi wowote wa kuingia akilini, wala uthibitisho wa kweli. Ewe Nabii! Waambie: Leteni uthibitisho wenu kama kweli Mwenyezi Mungu ana mshirika katika utawala hata akafaa kushirikishwa katika kuabudiwa. Hii Qur'ani iliyo kuja kuukumbusha umati wangu kwa linalo wajibikia, na hivi Vitabu vya Manabii wengine vilivyo kuja kukumbusha kaumu za kabla yangu, vyote hivyo vimesimama juu ya Tawhid, Upweke wa Mwenyezi Mungu. Lakini wengi wao hawajui yaliyo kuja ndani ya Vitabu hivyo, kwa sababu hawajishughulishi kuyazingatia yaliomo humo. Basi wao wamekuwa wenye kuipuuza Imani ya Mwenyezi Mungu.
  25. وَمَآ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رَّسُولٍ إِلَّا نُوحِىٓ إِلَيْهِ أَنَّهُۥ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّآ أَنَا۠ فَٱعْبُدُونِ۝٢٥

    Wama arsalna min qablika min rasoolin illa noohee ilayhi annahu la ilaha illa ana faoʿbudooni

    Na hatukumtuma kabla yako Mtume yeyote ila tulimfunulia ya kwamba hapana mungu isipo kuwa Mimi. Basi niabuduni Mimi tu.25

    Maelezo
    [25] Ewe Nabii! Sisi hatukumtuma Mtume yeyote kabla yako ila tulimpa wahyi (ufunuo) awafikishie watu wake kuwa hastahiki kuabudiwa isipo kuwa Mimi. Basi nisafieni ibada, iwe kwangu tu.
  26. وَقَالُوا۟ ٱتَّخَذَ ٱلرَّحْمَـٰنُ وَلَدًا ۗ سُبْحَـٰنَهُۥ ۚ بَلْ عِبَادٌ مُّكْرَمُونَ۝٢٦

    Waqaloo ittakhatha alrrahmanu waladan subhanahu bal ʿibadun mukramoona

    Na wanasema: Arrahman, Mwingi wa Rehema, ana mwana! Subhanahu, Ametakasika na hayo! Bali hao (wanao waita wana) ni watumwa walio tukuzwa.26

    Maelezo
    [26] Na baadhi ya makafiri wa Kiarabu walisema: Arrahman, Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema, ana mwana, kwa yale madai yao kuwa Malaika ni binti za Mwenyezi Mungu. Ametakasika na kuwa na mwana! Kwani hao Malaika ni waja wake walio tukuzwa tu kwa kuwakaribisha, na kwa wanavyo muabudu Yeye.
  27. لَا يَسْبِقُونَهُۥ بِٱلْقَوْلِ وَهُم بِأَمْرِهِۦ يَعْمَلُونَ۝٢٧

    La yasbiqoonahu bialqawli wahum biamrihi yaʿmaloona

    Hawamtangulii kwa neno, nao wanafanya amri zake.27

    Maelezo
    [27] Hawamtangulii Mwenyezi Mungu kwa kauli yao wainenayo kabla ya Yeye kuwapa ruhusa. Na wao hawatendi lolote ila kwa amri yake tu, wala hawapindukii mipaka ya amri anayo waamrisha.
  28. يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلَا يَشْفَعُونَ إِلَّا لِمَنِ ٱرْتَضَىٰ وَهُم مِّنْ خَشْيَتِهِۦ مُشْفِقُونَ۝٢٨

    Yaʿlamu ma bayna aydeehim wama khalfahum wala yashfaʿoona illa limani irtada wahum min khashyatihi mushfiqoona

    Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao. Wala hawamwombei yeyote ila yule anaye mridhia Yeye, nao kwa ajili ya kumwogopa wananyenyekea.28

    Maelezo
    [28] Mwenyezi Mungu anazijua hali zao zote na vitendo vyao vyote, walivyo vitanguliza na walivyo viakhirisha. Wala hawamwombei mtu kwake ila kwa aliye ridhia Mwenyezi Mungu. Na wao jinsi ya wingi wa khofu yao kumwogopa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kumtukuza Yeye, daima wana hadhari naye..
  29. ۞ وَمَن يَقُلْ مِنْهُمْ إِنِّىٓ إِلَـٰهٌ مِّن دُونِهِۦ فَذَٰلِكَ نَجْزِيهِ جَهَنَّمَ ۚ كَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلظَّـٰلِمِينَ۝٢٩

    Waman yaqul minhum innee ilahun min doonihi fathalika najzeehi jahannama kathalika najzee alththalimeena

    Na yeyote kati yao atakaye sema: Mimi ni mungu, badala yake, basi huyo tutamlipa malipo yake Jahannamu. Hivyo ndivyo tuwalipavyo wenye kudhulumu.29

    Maelezo
    [29] Na miongoni mwa Malaika atakaye sema: Mimi ni mungu wa kuabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu, huyo tutamlipa kwa kumtia Jahannamu. Mfano wa malipo hayo tunamlipa kila mwenye kupindukia mipaka ya haki, na wakajidhulumu nafsi zao kwa kudai Ungu na kuingia katika ushirikina.
  30. أَوَلَمْ يَرَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓا۟ أَنَّ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ كَانَتَا رَتْقًا فَفَتَقْنَـٰهُمَا ۖ وَجَعَلْنَا مِنَ ٱلْمَآءِ كُلَّ شَىْءٍ حَىٍّ ۖ أَفَلَا يُؤْمِنُونَ۝٣٠

    Awalam yara allatheena kafaroo anna alssamawati waalarda kanata ratqan fafataqnahuma wajaʿalna mina almai kulla shayin hayyin afala yuminoona

    Je! Hao walio kufuru hawakuona kwamba mbingu na ardhi zilikuwa zimeambatana, kisha Sisi tukazibabandua? Na tukajaalia kwa maji kila kilicho hai? Basi je, hawaamini?30

    Maelezo
    [30] Wenye kukufuru wamepofuka, na hawaoni kuwa mbingu na ardhi hapo mwanzo zilikuwa zimeshikamana. Kwa uwezo wetu tukazibambandua mbali mbali. Na tukajaalia kutokana na maji, ambayo hayo si kitu hai, kila chenye uhai kutokana na hayo hayo. Basi je! Baada ya yote haya wangali kupuuza tu, na hawaamini kuwa bila ya shaka yoyote hapana mungu isipo kuwa Sisi? "Je! Hao walio kufuru hawakuona kwamba mbingu na ardhi zilikuwa zimeambatana, kisha Sisi tukazibabandua? Na tukajaalia kwa maji kila kilicho hai? Basi je, hawaamini?" Aya hii ina maana ya kisayansi yenye kutilia nguvu nadhariya ya ilimu za kisasa katika kuumbwa sayari na ardhi. Nayo ni kuwa mbingu na ardhi asili yao zilikuwa zimeshikamana. Na ukweli wa sayansi zinazo kubaliwa ni kuwa hakika ziliambatana, na sayansi mbali mbali zinathibitisha hayo. Na zipo nadhariya nyengine kadhaa wa kadhaa ambazo kwazo zaweza kuelezea dhaahiri ya mambo haya. Lakini bado kuthibiti nadhariya mojapo kwa njia ya mkato kwa wanazuoni kwa kuwafikiana wote. Kwa kuonyesha mfano tutaja nadhariya mbili: Nadhariya ya Kwanza: Imekhusu kuumbwa kwa mfumo wa jua (Solar System). Kwa mfano imethibiti kuwa mawingu au umande ulio zunguka jua ulianza kuenea kwenye anga lilio baridi, na chembechembe za gasi zinazo fanya hayo mawingu au moshi zikakusanyika kwenye chembechembe za vumbi linalo kwenda kwa kasi kubwa. Kisha chembechembe hizo zikawa zinagongana na zinarindika, na huku ndani yake zikawamo gasi nzito, na kukazidi kurindika na kujumuika kwa kupita mamilioni na mamilioni ya makarne mpaka zikafanyika sayari na mwezi na ardhi kwa umbali unao stahiki. Na yajuulikana kuwa huko kukusanyika na kurindika huzidisha mbinyo (Pressure), na huo huzidisha joto. Na gamba la ardhi lilipo ingia kupoa, na wakati zilipo ripuka volkano ardhi ikapata mvuke wa maji na gasi ya Carbon dioxide ilio tokana na miripuko ya volkano...na katika iliyo saidia kupatikana Oxygen katika hewa baada ya hapo ni nishati na nguvu za miyale ya jua kwa njia ya mwanga juu ya mimea na majani ya mwanzo. Ama Nadhariya ya Pili: Imekhusiana na uumbaji wa ulimwengu kwa jumla, ambao kwa mukhtasari unaelezwa na kauli yake Mtukufu: "Zilikuwa zimeambatana", yaani zimeshikamana na kuwa kitu kimoja. Na hayo ndiyo yaliyo fikilia mwishoni ilimu za sayansi katika uumbaji wa ulimwengu. Nayo ni kwamba kabla ya kufikilia sura yake hii ya sasa ulikuwa kama donge lilio kusanyika lenye kutisha, la mkusanyiko wa chembechembe zenye kuambatana chini ya mbinyo pressure, hata akili haiwezi kuifikiria. Na hizi sayari zote na nyota zilioko mbinguni hivi leo tunazo ziita mfumo wa jua solar system zilikuwa ni mkusanyiko wa donge moja lisilo zidi 1/2 diameter yake maili milioni tatu. Na neno lake Mwenyezi Mungu: "Tukazibambandua" linafahamisha ule mripuko mkubwa wa mwanzo wa ki-nuclear ukazalisha uumbaji wa anga na sayari za namna mbali mbali tunazo ziita kwa pamoja "Mfumo wa Jua" au Solar System. "Na tukajaalia kwa maji kila kilicho hai": Aya hii imethibitisha uhakika wa kisayansi ulio thibitishwa na ncha mbali mbali za ilimu. Imethibitisha Cytology, sayansi ya "cells", (khalaya), kwamba maji ni muhimu kabisa katika ujengaji wa "cells" zote za vitu vilivyo hai, ikiwa mimea au wanyama. Na ilimu ya "Kimyaa", Chemistry kwamba maji ni lazima yapatikane katika vitendo na mageuko yoyote katika viumbe vilivyo hai. Basi hayo maji ama yawe ni kiungo, kitu cha kusaidia, au cha kuwamo ndani ya kitendo, au ni matokeo yake. Na imethibitisha ilimu ya viungo physiology kwamba maji ni dharura kwa viungo kufanya kazi yao. Bila ya hayo maji hautodhihiri uhai katika viungo.
  31. وَجَعَلْنَا فِى ٱلْأَرْضِ رَوَٰسِىَ أَن تَمِيدَ بِهِمْ وَجَعَلْنَا فِيهَا فِجَاجًا سُبُلًا لَّعَلَّهُمْ يَهْتَدُونَ۝٣١

    Wajaʿalna fee alardi rawasiya an tameeda bihim wajaʿalna feeha fijajan subulan laʿallahum yahtadoona

    Na tukaweka katika ardhi milima iliyo thibiti ili isiwayumbishe, na tukaweka humo njia pana ili wapate kuongoka.31

    Maelezo
    [31] Na katika dalili za uweza wetu ni kuwa tumeifanya milima imesimama imara kwenye ardhi ili isiyumbeyumbe nao watu, na tumefanya humo njia pana, za kupitia kwa wasaa, ili waweze kuongoza njia humo kwa makusudio yao. Maoni ya wataalamu juu ya Aya ya 31: "Na tukaweka katika ardhi milima iliyo thibiti ili isiwayumbishe, na tukaweka humo njia pana ili wapate kuongoka." Ilivyo kuwa ndani ya ardhi kila kitu kimeyayuka, na lau kuwa milima imewekwa tu katika baadhi ya sehemu za huu mpira wa dunia kama majabali yaliyo nyanyuka juu tu, uzito wao ungeli sabibisha gamba la dunia liyumbe, au lipindane na kupasuka. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu kwa utukufu wa shani yake ameifanya milima isimame imara kwa kuwa na mizizi iliyo zama kwenye gamba la ardhi mpaka chini kwenye kina kirefu kulingana na urefu wake kwendea juu. Kwa hivyo imekuwa hiyo milima kama vigingi, kama alivyo jaalia eneo la minyanyuka hii na mizizi ni duni kuliko maeneo ya gamba lilio zunguka. Yote haya ni kwa ajili ya kueneza sawa uzito wa juu ya gamba kwa pande zote ili pasiwepo kuyumbayumba na kupasuka. Kwani hakika kuenezwa kwa uzito juu ya uso wa dunia yakaribia kuwa hakuleti athari kubwa ya kutajika. Na ilimu za kisasa zimethibitisha kuwa kuenezwa kwa nchi kavu na maji juu ya ardhi, na kuwepo mfululizo wa milima juu yake ni katika yanayo hakikisha hali ilivyo ardhi, na imethibitika kuwa chini ya milima mizito kuna vitu vyepesi kubungunyika, na chini ya maji ya bahari kuu vipo vitu vizito. Kwa kuenezwa uzani wa namna hiyo mbali mbali katika dunia, na mgawanyo huu wa milima, makusudio yake ni kusawizisha uzani wa mpira huu wa ardhi. Na ilivyo nyanyuka milima zikatokea nyanda na mabonde na njia baina ya milima na mwambao na bahari na minyanyuko, na zikawa njia.
  32. وَجَعَلْنَا ٱلسَّمَآءَ سَقْفًا مَّحْفُوظًا ۖ وَهُمْ عَنْ ءَايَـٰتِهَا مُعْرِضُونَ۝٣٢

    Wajaʿalna alssamaa saqfan mahfoothan wahum ʿan ayatiha muʿridoona

    Na tukaifanya mbingu kuwa dari iliyo hifadhiwa, lakini wanazipuuza Ishara zake.32

    Maelezo
    [32] Na tumeifanya mbingu kama dari iliyo nyanyuliwa, na tukailinda isianguke, au visianguke viliomo humo. Na juu ya hayo, wao hawazioni wala hawaziingatii Ishara zetu zenye kuonyesha uweza wetu na hikima yetu na rehema yetu. Maoni ya wataalamu juu ya Aya 32: "Na tukaifanya mbingu kuwa dari iliyo hifadhiwa lakini wanazipuuza Ishara zake. ": Aya hii tukufu imethibitisha kuwa mbingu na vyote viliomo ndani yake vimehifadhiwa visiwe na ila yoyote, na vimehifadhiwa visidondoke juu ya ardhi. Na mbingu ni kila kilicho juu yetu, kuanzia kifuniko hichi cha hewa inayo walinda walioko juu ya ardhi na khatari nyingi za angani ambazo zinazuia maisha, mfano wa vimondo vya nyota za mkia, na miyale. Na juu ya ardhi pana kifuniko cha hewa kinacho linda ardhi kwa nguvu za mvutano, na haifai kukosekana hivyo bila ya maangamizo kabisa. Na juu ya kifuniko cha hewa ndio kuna hizo sayari za mbinguni, na zipo kwa umbali mbali mbali kufuatana na nyendo zao tangu mwanzo. "Na tukaifanya mbingu kuwa dari iliyo hifadhiwa" yaani hizo sayari na vyote vilio mbinguni vyaonekana kwa nadhari yetu kama kwamba ni dari, na tunaona vilio juu ya vichwa vyetu kama ni vidogo kuliko vilioko upeo wa macho. Na hayo ni kiini macho tu, kama tunapo liona jua kubwa wakati wa kuchomoza na kuchwa kuliko adhuhuri. Na hili qubba la mbingu lina sifa zake, zinazo khitalifiana kila ukizidi mnyanyuko wa ardhi, kama hizo sayari za mbinguni kwa mujibu wa jicho linavyo ona katika qubba la mbingu.
  33. وَهُوَ ٱلَّذِى خَلَقَ ٱلَّيْلَ وَٱلنَّهَارَ وَٱلشَّمْسَ وَٱلْقَمَرَ ۖ كُلٌّ فِى فَلَكٍ يَسْبَحُونَ۝٣٣

    Wahuwa allathee khalaqa allayla waalnnahara waalshshamsa waalqamara kullun fee falakin yasbahoona

    Na Yeye ndiye aliye umba usiku na mchana na jua na mwezi, vyote katika anga vinaogelea.33

    Maelezo
    [33] Na Mwenyezi Mungu ndiye aliye umba usiku na mchana, na jua na mwezi. Vyote hivyo vinakwenda katika njia zake kama alivyo zijaalia Mwenyezi Mungu, na zinamtakasa bila ya kupotea. Maoni ya wataalamu juu ya Aya 33: "Na Yeye ndiye aliye umba usiku na mchana na jua na mwezi, vyote katika anga vinaogelea." Kila sayari ya mbinguni ina mzunguko wake makhsusi inayo ogelea kuufuata. Na zote hizo hazisiti, na zinakwenda kwa mwendo wao maalumu katika anga. Na sisi tunaona hayo kwa hakika kwa kutazama mwendo wa jua na mwezi. Kama kadhaalika mzunguko wa ardhi wake wenyewe ndio unao leta usiku na mchana kwa zamu, kama kwamba unaogelea.
  34. وَمَا جَعَلْنَا لِبَشَرٍ مِّن قَبْلِكَ ٱلْخُلْدَ ۖ أَفَإِي۟ن مِّتَّ فَهُمُ ٱلْخَـٰلِدُونَ۝٣٤

    Wama jaʿalna libasharin min qablika alkhulda afain mitta fahumu alkhalidoona

    Nasi hatukumjaalia mwanaadamu yeyote kabla yako kuwa na maisha ya milele. Basi je! Ukifa wewe, wao wataishi milele?34

    Maelezo
    [34] Ewe Nabii! Hatukumjaalia mwanaadamu yeyote kabla yako wewe aishi milele, hata ikawa hao makafiri wakawa wanakutamania ufe wewe. Vipi wanakutamania mauti wewe na hali na wao vile vile watakufa kama wewe? Ukifa wewe, je, ndio wao watabakia kushinda wanaadamu wote?
  35. كُلُّ نَفْسٍ ذَآئِقَةُ ٱلْمَوْتِ ۗ وَنَبْلُوكُم بِٱلشَّرِّ وَٱلْخَيْرِ فِتْنَةً ۖ وَإِلَيْنَا تُرْجَعُونَ۝٣٥

    Kullu nafsin thaiqatu almawti wanablookum bialshsharri waalkhayri fitnatan wailayna turjaʿoona

    Kila nafsi itaonja mauti; na tunakujaribuni kwa mtihani wa shari na kheri. Na kwetu Sisi mtarejeshwa.35

    Maelezo
    [35] Kila nafsi haina budi kuonja mauti. Na Sisi tunakufanyieni hapa duniani kama wenye kukupeni mtihani, kwa kukupeni yenye manufaa yenu na yenye madhara pia, ili abagulike mwenye kushukuru kwa kupewa kheri na kuvumilia balaa, na yule asiye na fadhila kwa neema aipatayo na anapapatika akipata misiba. Nanyi mtarejeshwa kwetu, na hapo tutakuhisabieni vitendo vyenu.
  36. وَإِذَا رَءَاكَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓا۟ إِن يَتَّخِذُونَكَ إِلَّا هُزُوًا أَهَـٰذَا ٱلَّذِى يَذْكُرُ ءَالِهَتَكُمْ وَهُم بِذِكْرِ ٱلرَّحْمَـٰنِ هُمْ كَـٰفِرُونَ۝٣٦

    Waitha raaka allatheena kafaroo in yattakhithoonaka illa huzuwan ahatha allathee yathkuru alihatakum wahum bithikri alrrahmani hum kafiroona

    Na wakikuona walio kufuru hawakufanyi wewe ila ni kitu cha maskhara tu, (wakisema): Je! Ndiye huyu anaye itaja miungu yenu? Na hali wao wanakataa kumkumbuka Arrahman, Mwingi wa Rehema!36

    Maelezo
    [36] Na wakikuona, ewe Nabii, wale walio mkataa Mwenyezi Mungu na ulio kuja nayo wewe, hawakufanyii wewe ila maskhara na kejeli. Huambiana wao kwa wao: Ndiye huyu anaye watia aibu miungu yenu? Na hali wao hawasadiki kumdhukuru Mwenyezi Mungu ambaye ndiye aliye waeneza rehema yake!
  37. خُلِقَ ٱلْإِنسَـٰنُ مِنْ عَجَلٍ ۚ سَأُو۟رِيكُمْ ءَايَـٰتِى فَلَا تَسْتَعْجِلُونِ۝٣٧

    Khuliqa alinsanu min ʿajalin saoreekum ayatee fala tastaʿjiloona

    Mwanaadamu ameumbwa na haraka. Nitakuonyesheni Ishara zangu. Basi msinihimize.37

    Maelezo
    [37] Na ikiwa wao wanataka waletewe adhabu kwa upesi, basi ndio tabia ya binaadamu kutaka kila jambo kwa haraka. Basi enyi wenye haraka! Nitakuonesheni neema yangu duniani, na adhabu yangu Akhera. Msijishughulishe kuhimiza kitu ambacho hakina budi kuwa. Maoni ya wataalamu juu ya Aya 37: "Mwanaadamu ameumbwa na haraka. Nitakuonyesheni Ishara zangu. Basi msinihimize." Makusudio ya kauli ya "Ishara" ni ishara za maumbile zenye kuonyesha kuwepo kwa Mwenyezi Mungu na uweza wake. Na ujuzi wa ilimu za sayansi utavumbua kwa mujibu wa itavyo nyanyuka akili ya binaadamu. Na hayo ni kwa mujibu wa miadi ilio wekwa kwa wakati wake. Kila ukifika wakati maalumu Mwenyezi Mungu hudhihirisha Ishara yake, au huwasahilishia wanaadamu njia za kuzifikilia Ishara hizo.
  38. وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَـٰذَا ٱلْوَعْدُ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ۝٣٨

    Wayaqooloona mata hatha alwaʿdu in kuntum sadiqeena

    Na wanasema: Ahadi hii itatokea lini, ikiwa nyinyi mnasema kweli?38

    Maelezo
    [38] Na makafiri wanaohimiza adhabu, na huku wanaona haiwi, wanasema: Lini yatakuwa hayo munatuahidi enyi Waumini kama kweli hayo muyasemayo
  39. لَوْ يَعْلَمُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ حِينَ لَا يَكُفُّونَ عَن وُجُوهِهِمُ ٱلنَّارَ وَلَا عَن ظُهُورِهِمْ وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ۝٣٩

    Law yaʿlamu allatheena kafaroo heena la yakuffoona ʿan wujoohihimu alnnara wala ʿan thuhoorihim wala hum yunsaroona

    Lau wangeli jua wale walio kufuru wakati ambao hawatauzuia Moto kwenye nyuso zao wala migongo yao, na wala hawatanusuriwa!39

    Maelezo
    [39] Lau kuwa hao walio mkufuru Mwenyezi Mungu wangeli ijua hali yao wakati watapo kuwa hawawezi kuuondoa Moto kwenye nyuso zao na migongo yao, na wala hawampati wa kuwasaidia kuuondoa, wasingeli sema wayasemayo.
  40. بَلْ تَأْتِيهِم بَغْتَةً فَتَبْهَتُهُمْ فَلَا يَسْتَطِيعُونَ رَدَّهَا وَلَا هُمْ يُنظَرُونَ۝٤٠

    Bal tateehim baghtatan fatabhatuhum fala yastateeʿoona raddaha wala hum yuntharoona

    Bali utawafikia kwa ghafla, na utawashitua na wala hawataweza kuurudisha, wala hawatapewa muhula!40

    Maelezo
    [40] Kiyama hakiwajii kwa kukitarajia kutokea kwake, bali kitawazukia kwa ghafla tu kiwababaishe, wasiweze kukirudisha, wala wao hawatapewa muhula wa kutubia na kutafuta udhuru kwa waliyo kwisha yatenda..
  41. وَلَقَدِ ٱسْتُهْزِئَ بِرُسُلٍ مِّن قَبْلِكَ فَحَاقَ بِٱلَّذِينَ سَخِرُوا۟ مِنْهُم مَّا كَانُوا۟ بِهِۦ يَسْتَهْزِءُونَ۝٤١

    Walaqadi istuhzia birusulin min qablika fahaqa biallatheena sakhiroo minhum ma kanoo bihi yastahzioona

    Na Mitume walio kabla yako walikwisha dhihakiwa. Kwa hivyo wale walio wafanyia maskhara yaliwafika yale waliyo kuwa wakiyafanyia dhihaka.41

    Maelezo
    [41] Na Mitume wa kabla yako yaliwapata vile vile ya kufanyiwa kejeli na makafiri katika kaumu zao. Ikawateremkia hao walio wakataa Mitume na kuwafanyia maskhara adhabu hiyo hiyo ambayo wao waliifanyia maskhara na kejeli.
  42. قُلْ مَن يَكْلَؤُكُم بِٱلَّيْلِ وَٱلنَّهَارِ مِنَ ٱلرَّحْمَـٰنِ ۗ بَلْ هُمْ عَن ذِكْرِ رَبِّهِم مُّعْرِضُونَ۝٤٢

    Qul man yaklaokum biallayli waalnnahari mina alrrahmani bal hum ʿan thikri rabbihim muʿridoona

    Sema: Nani anaye kulindeni usiku na mchana na Arrahmani Mwingi wa Rehema? Bali wao wanapuuza kumkumbuka Mola wao Mlezi.42

    Maelezo
    [42] Ewe Nabii! Waambie: Ni nani anaye kuhifadhini na nakama zake wakati wa usiku na mchana, na akakurehemuni na kukuneemesheni? Hapana awezae hayo. Lakini wao wanaipuuza Qur'ani ambayo ndiyo inawakumbusha ya kuwafaa na kuwalinda na adhabu.
  43. أَمْ لَهُمْ ءَالِهَةٌ تَمْنَعُهُم مِّن دُونِنَا ۚ لَا يَسْتَطِيعُونَ نَصْرَ أَنفُسِهِمْ وَلَا هُم مِّنَّا يُصْحَبُونَ۝٤٣

    Am lahum alihatun tamnaʿuhum min doonina la yastateeʿoona nasra anfusihim wala hum minna yushaboona

    Au wao wanao miungu watao weza kuwakinga nasi? Hao hawawezi kujinusuru nafsi zao, wala hawatalindwa nasi!43

    Maelezo
    [43] Kwani wao wanao miungu wa kuwalinda na adhabu itokayo kwetu? Hasha! Hiyo miungu yao haiwezi kujilinda wenyewe, licha kumlinda mwenginewe. Wala hapana yeyote awezae kumlinda yeyote kati yao karibu yake au pamoja naye pindi tukitaka kumuadhibu na kumteketeza.
  44. بَلْ مَتَّعْنَا هَـٰٓؤُلَآءِ وَءَابَآءَهُمْ حَتَّىٰ طَالَ عَلَيْهِمُ ٱلْعُمُرُ ۗ أَفَلَا يَرَوْنَ أَنَّا نَأْتِى ٱلْأَرْضَ نَنقُصُهَا مِنْ أَطْرَافِهَآ ۚ أَفَهُمُ ٱلْغَـٰلِبُونَ۝٤٤

    Bal mattaʿna haolai waabaahum hatta tala ʿalayhimu alʿumuru afala yarawna anna natee alarda nanqusuha min atrafiha afahumu alghaliboona

    Bali tuliwastarehesha hawa na baba zao mpaka umri ukawa mrefu kwao. Je, hawaoni ya kwamba Sisi tunaifikia ardhi tukiipunguza ncha zake? Basi je! Hao ni wenye kushinda?44

    Maelezo
    [44] Sisi hatufanyi haraka kuwaadhibu hawa kwa ukafiri wao, lakini tunawapururia na kuwastarehesha katika uhai wa dunia, kama tulivyo wastarehesha baba zao kabla yao, mpaka umri ukawa mrefu kwao. Je! Wanajitia upofu hawaoni yanao wazunguka wakaona kuwa Sisi tunaiendea nchi na tukaipunguza ncha zake kwa ushindi wa Waumini? Ni wao ndio wenye kushinda au Waumini ambao Mwenyezi Mungu amewaahidi kuwasaidia na kuwaunga mkono? Maoni ya wataalamu juu ya Aya 44: "Je, hawaoni ya kwamba Sisi tunaifikia ardhi tukiipunguza mipaka yake? Basi je! Hao ni wenye kushinda?": Aya hii ni katika Aya za miujiza ya kisayansi katika Qur'ani Tukufu. Hii inaonyesha kuwa dunia si mduwara kaamili. Na wataalamu wa sayansi hawakutamakani kupima masafa ya dunia baraabara mpaka kiasi ya miaka 250 tu takriban, walipo ingia kikundi cha mabingwa walio khusika na ilimu ya kupima marefu baina ya daraja mbili za urefu longitudes. Na hayo kwa pahala mbali mbali duniani. Katika kupima huku ikadhihiri kuwa nusu ya kati ya dunia kwenye equator inazidi kuliko nusu ya poles kwa takriban kilomita 21.5. Yaani dunia imepungua katika ncha zake, yaani katika poles. Na inajuulikana maalumu kuwa sura ya dunia na masafa yake ndio msingi katika kuchorwa kwa ramani.
  45. قُلْ إِنَّمَآ أُنذِرُكُم بِٱلْوَحْىِ ۚ وَلَا يَسْمَعُ ٱلصُّمُّ ٱلدُّعَآءَ إِذَا مَا يُنذَرُونَ۝٤٥

    Qul innama onthirukum bialwahyi wala yasmaʿu alssummu aldduʿaa itha ma yuntharoona

    Sema: Mimi nakuonyeni kwa Wahyi. Na viziwi hawasikii wito wanapo onywa.45

    Maelezo
    [45] Ewe Nabii! Sema: Sikuhadharisheni kwa maneno yanayo tokana nami. Lakini nakuhadharisheni kwa Wahyi (Ufunuo) unao tokana na Mwenyezi Mungu Mtukufu ulio nijia mimi. Na huo ni wa Haki na kweli. Lakini hao kwa sababu ya kupuuza kwao kurefu kuipuuza Sauti ya Haki, Mwenyezi Mungu ameyaziba masikio yao mpaka wakawa kama viziwi. Na kiziwi hasikii Wito anapo hadharishwa na adhabu!
  46. وَلَئِن مَّسَّتْهُمْ نَفْحَةٌ مِّنْ عَذَابِ رَبِّكَ لَيَقُولُنَّ يَـٰوَيْلَنَآ إِنَّا كُنَّا ظَـٰلِمِينَ۝٤٦

    Walain massathum nafhatun min ʿathabi rabbika layaqoolunna ya waylana inna kunna thalimeena

    Na wanapo guswa na mpulizo mmoja tu wa adhabu itokayo kwa Mola wako Mlezi, bila ya shaka wao husema: Ole wetu! Hakika tulikuwa wenye kudhulumu.46

    Maelezo
    [46] Na kuwa na yakini kuwa nao wakisibiwa hata na chembe ya adhabu ndogo wanayo ifanyia maskhara, hupiga kelele kwa khofu wakisema: Ole wetu! Hakika sisi tulikuwa tunajidhulumu nafsi zetu, na tukiwadhulumu wenginewe, tulipo yakataa tuliyo ambiwa.
  47. وَنَضَعُ ٱلْمَوَٰزِينَ ٱلْقِسْطَ لِيَوْمِ ٱلْقِيَـٰمَةِ فَلَا تُظْلَمُ نَفْسٌ شَيْـًٔا ۖ وَإِن كَانَ مِثْقَالَ حَبَّةٍ مِّنْ خَرْدَلٍ أَتَيْنَا بِهَا ۗ وَكَفَىٰ بِنَا حَـٰسِبِينَ۝٤٧

    Wanadaʿu almawazeena alqista liyawmi alqiyamati fala tuthlamu nafsun shayan wain kana mithqala habbatin min khardalin atayna biha wakafa bina hasibeena

    Nasi tutaweka mizani za uadilifu kwa Siku ya Kiyama. Basi nafsi haitadhulumiwa kitu chochote. Hata ikiwa ni uzito wa chembe ya khardali tutaileta. Nasi tunatosha kuwa washika hisabu.47

    Maelezo
    [47] Na Sisi tunaweka mizani ya kupimiwa kwa uadilifu Siku ya Kiyama. Basi hadhulumiwi mtu kwa kupunguziwa wema wake au kuongezewa maovu yake. Hata ikiwa ni kiasi ya uzani wa chembe ndogo hii tutaileta na tutaihisabu. Na yatosha kuwa ni Sisi ndio wa kuhisabu. Basi hapana atakaye dhulumiwa kitu. Maoni ya wataalamu juu ya Aya ya 47: "Nasi tutaweka mizani za uadilifu kwa Siku ya Kiyama. Basi nafsi haitadhulumiwa kitu chochote. Hata ikiwa ni uzito wa chembe ya khardali tutaileta. Nasi tunatosha kuwa washika hisabu.": Aya hii tukufu inaonyesha kuwa chembe ya khardali ni hadi ya udogo katika mizani. Imethibitika kwa majaribio ya sayansi kuwa Kilogram ya chembe za khardali ni chembe 913,000. Kwa hivyo chembe moja ya khardali ni takriban sehemu moja katika elfu ya gram, yaani ni takriban sawa na Miligram moja. Na huu ni uzito mdogo kabisa unao juulikana katika mbegu za mimea mpaka sasa. Kwa hivyo hutumiwa katika kupimiwa vitu vidogo vidogo kabisa.
  48. وَلَقَدْ ءَاتَيْنَا مُوسَىٰ وَهَـٰرُونَ ٱلْفُرْقَانَ وَضِيَآءً وَذِكْرًا لِّلْمُتَّقِينَ۝٤٨

    Walaqad atayna moosa waharoona alfurqana wadiyaan wathikran lilmuttaqeena

    Na kwa yakini tuliwapa Musa na Haaruni kipambanuzi, na mwangaza, na makumbusho kwa wachamngu,48

    Maelezo
    [48] Na Musa na Haaruni tuliwapa Taurati ya kupambanua baina ya kweli na uwongo, na halali na haramu. Na juu ya hivyo hiyo ni nuru ya kuwaongoa watu wafuate njia ya kheri na uwongozi mwema, na ni kumbusho la kuwafaa wachamngu...
  49. ٱلَّذِينَ يَخْشَوْنَ رَبَّهُم بِٱلْغَيْبِ وَهُم مِّنَ ٱلسَّاعَةِ مُشْفِقُونَ۝٤٩

    Allatheena yakhshawna rabbahum bialghaybi wahum mina alssaʿati mushfiqoona

    Ambao wanamkhofu Mola wao Mlezi faraghani, na wanaiogopa Saa ya Kiyama.49

    Maelezo
    [49] Ambao wanamkhofu Muumba wao Mwenye kumiliki mambo yao yote, juu ya kuwa wako mbali na watu, na wala hawamwoni mtu. Nao wamo katika khofu ya daima kuikhofu Siku ya Kiyama.
  50. وَهَـٰذَا ذِكْرٌ مُّبَارَكٌ أَنزَلْنَـٰهُ ۚ أَفَأَنتُمْ لَهُۥ مُنكِرُونَ۝٥٠

    Wahatha thikrun mubarakun anzalnahu afaantum lahu munkiroona

    Na haya ni makumbusho yaliyo barikiwa, tuliyo yateremsha. Basi je! Mnayakataa?50

    Maelezo
    [50] Na hii Qur'ani ni kumbusho, lenye kheri nyingi. Tumekuteremshieni kama tulivyo mteremshia Musa. Basi yawaje nyinyi muikatae, na hali nyinyi ndio mnao stahiki zaidi kuiamini kuliko watu wote!
  51. ۞ وَلَقَدْ ءَاتَيْنَآ إِبْرَٰهِيمَ رُشْدَهُۥ مِن قَبْلُ وَكُنَّا بِهِۦ عَـٰلِمِينَ۝٥١

    Walaqad atayna ibraheema rushdahu min qablu wakunna bihi ʿalimeena

    Na hakika tulikwisha mpa Ibrahim uwongofu wake zamani, na tulikuwa tunamjua.51

    Maelezo
    [51] Na hakika Sisi tulikwisha mpa Ibrahim uwongofu na fikra ya kutafuta Haki kwa usafi wa niya kabla ya Musa na Haaruni. Na Sisi ni Wenye kujua vyema hali yake na fadhila zake zilizo mfanya astahiki kuchukua Utume.
  52. إِذْ قَالَ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِۦ مَا هَـٰذِهِ ٱلتَّمَاثِيلُ ٱلَّتِىٓ أَنتُمْ لَهَا عَـٰكِفُونَ۝٥٢

    Ith qala liabeehi waqawmihi ma hathihi alttamatheelu allatee antum laha ʿakifoona

    Alipo mwambia baba yake na watu wake: Ni nini haya masanamu mnayo yashughulikia kuyaabudu?52

    Maelezo
    [52] Ewe Nabii! Kumbuka pale Ibrahim alipo mwambia baba yake na watu wake kuwaonya juu ya masanamu waliyo kuwa wakishughulikia kuyaabudu: Ni nini haya masanamu ambayo nyinyi mmeshika kuyaabudu?
  53. قَالُوا۟ وَجَدْنَآ ءَابَآءَنَا لَهَا عَـٰبِدِينَ۝٥٣

    Qaloo wajadna abaana laha ʿabideena

    Wakasema: Tumewakuta baba zetu wakiyaabudu.53

    Maelezo
    [53] Wakasema: Tumewakuta baba zetu wakiyatukuza na wameshika kuyaabudu. Nasi tukawafuata.
  54. قَالَ لَقَدْ كُنتُمْ أَنتُمْ وَءَابَآؤُكُمْ فِى ضَلَـٰلٍ مُّبِينٍ۝٥٤

    Qala laqad kuntum antum waabaokum fee dalalin mubeenin

    kasema: Bila ya shaka nyinyi na baba zenu mmekuwa katika upotofu ulio dhaahiri.54

    Maelezo
    [54] Yeye akasema: Nyinyi na baba zenu kabla yenu, ni wazi kuwa nyote mko mbali na Haki.
  55. قَالُوٓا۟ أَجِئْتَنَا بِٱلْحَقِّ أَمْ أَنتَ مِنَ ٱللَّـٰعِبِينَ۝٥٥

    Qaloo ajitana bialhaqqi am anta mina allaʿibeena

    Wakasema: Je! Umetujia kwa maneno ya kweli au wewe ni katika wachezao tu?55

    Maelezo
    [55] Wakasema: Je! Umetujia kwa haya uyasemayo na hakika ya kweli unayo iamini, au kwa maneno haya wewe ni katika wanao fanya pumbao na mchezo tu bila ya kuwa na maana yoyote?
  56. قَالَ بَل رَّبُّكُمْ رَبُّ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ٱلَّذِى فَطَرَهُنَّ وَأَنَا۠ عَلَىٰ ذَٰلِكُم مِّنَ ٱلشَّـٰهِدِينَ۝٥٦

    Qala bal rabbukum rabbu alssamawati waalardi allathee fatarahunna waana ʿala thalikum mina alshshahideena

    Akasema: Bali Mola wenu Mlezi ni Mola Mlezi wa mbingu na ardhi ambaye ndiye aliye ziumba. Na mimi ni katika wenye kuyashuhudia hayo.56

    Maelezo
    [56] Akasema: Hapana maskhara katika niyasemayo. Bali Mola wenu Mlezi anaye stahiki peke yake kutukuzwa na kuogopwa na kuabudiwa ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi, na akazileta bila ya kuwapo mfano wake wa kuigiza. Basi ni haki yake Yeye tu peke yake kuabudiwa. Na mimi kwa haya niyasemayo ni katika wenye hakika ambao hunena wanayo yashuhudia na wanayajua.
  57. وَتَٱللَّهِ لَأَكِيدَنَّ أَصْنَـٰمَكُم بَعْدَ أَن تُوَلُّوا۟ مُدْبِرِينَ۝٥٧

    WataAllahi laakeedanna asnamakum baʿda an tuwalloo mudbireena

    Na Wallahi! Nitayafanyia vitimbi masanamu yenu haya baada ya mkisha geuka kwenda zenu.57

    Maelezo
    [57] Na akasema moyoni mwake: Naapa kwa Mwenyezi Mungu, nitayafanyia vitimbi haya masanamu yenu niyavunje pale mtapo ondoka, ili mpate kuona upotovu wenu.
  58. فَجَعَلَهُمْ جُذَٰذًا إِلَّا كَبِيرًا لَّهُمْ لَعَلَّهُمْ إِلَيْهِ يَرْجِعُونَ۝٥٨

    Fajaʿalahum juthathan illa kabeeran lahum laʿallahum ilayhi yarjiʿoona

    Basi akayavunja vipande vipande, ila kubwa lao, ili wao walirudie.58

    Maelezo
    [58] Baada ya kwisha ondoka wale watu, Ibrahim aliwaendea masanamu akayavunja vipande vipande, isipokuwa sanamu kumbwa, hilo aliliacha ili wapate kuliregea waliulize yalio wasibu miungu yao nalo halikujibu kitu, kwa hivyo upotovu wa ibada yao ikabainika.
  59. قَالُوا۟ مَن فَعَلَ هَـٰذَا بِـَٔالِهَتِنَآ إِنَّهُۥ لَمِنَ ٱلظَّـٰلِمِينَ۝٥٩

    Qaloo man faʿala hatha bialihatina innahu lamina alththalimeena

    Wakasema: Nani aliye ifanyia haya miungu yetu? Hakika huyu ni katika walio dhulumu.59

    Maelezo
    [59] Baada ya kwisha ona yaliyo wapata miungu yao wakasema: Nani aliye itendea haya miungu yetu? Hakika mtu huyu hapana shaka ni katika walio jidhulumu wenyewe kwa adhabu itayo mpata..
  60. قَالُوا۟ سَمِعْنَا فَتًى يَذْكُرُهُمْ يُقَالُ لَهُۥٓ إِبْرَٰهِيمُ۝٦٠

    Qaloo samiʿna fatan yathkuruhum yuqalu lahu ibraheemu

    Wakasema: Tumemsikia kijana mmoja akiwataja. Anaitwa Ibrahim.60

    Maelezo
    [60] Wakasema baadhi yao: Tumemsikia kijana mmoja akiitaja kwa kuisubu (kuitukana) ; naye anaitwa Ibrahim.
  61. قَالُوا۟ فَأْتُوا۟ بِهِۦ عَلَىٰٓ أَعْيُنِ ٱلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَشْهَدُونَ۝٦١

    Qaloo fatoo bihi ʿala aʿyuni alnnasi laʿallahum yashhadoona

    Wakasema: Mleteni mbele ya macho ya watu, wapate kumshuhudia61

    Maelezo
    [61] Wakasema wakubwa wao: Nendeni mkamlete, ahukumiwe mbele ya macho ya watu, na washuhudie aliyo yatenda!
  62. قَالُوٓا۟ ءَأَنتَ فَعَلْتَ هَـٰذَا بِـَٔالِهَتِنَا يَـٰٓإِبْرَٰهِيمُ۝٦٢

    Qaloo aanta faʿalta hatha bialihatina ya ibraheemu

    Wakasema: Je! Wewe umeifanyia haya miungu yetu, ewe Ibrahim?62

    Maelezo
    [62] Baada ya kwisha mhudhurisha, wakasema: Ni wewe ulio itenda haya miungu yetu, ewe Ibrahim?
  63. قَالَ بَلْ فَعَلَهُۥ كَبِيرُهُمْ هَـٰذَا فَسْـَٔلُوهُمْ إِن كَانُوا۟ يَنطِقُونَ۝٦٣

    Qala bal faʿalahu kabeeruhum hatha faisaloohum in kanoo yantiqoona

    Akasema: Bali amefanya hayo huyu mkubwa wao. Basi waulizeni ikiwa wanaweza kutamka.63

    Maelezo
    [63] Kuwanabihisha upotovu wao, alisema kwa kuwakejeli: Hili kubwa lao ndilo lililo tenda hayo! Iulizeni hiyo miungu aliyo yatenda huyu, kama kweli inaweza kujibu suala yenu!
  64. فَرَجَعُوٓا۟ إِلَىٰٓ أَنفُسِهِمْ فَقَالُوٓا۟ إِنَّكُمْ أَنتُمُ ٱلظَّـٰلِمُونَ۝٦٤

    Farajaʿoo ila anfusihim faqaloo innakum antumu alththalimoona

    Basi wakajirudi nafsi zao, wakasema: Hakika nyinyi mlikuwa madhaalimu!64

    Maelezo
    [64] Wakazirejea nafsi zao wakiifikiria ile ibada yao kuabudu vitu visivyo mnufaisha yeyote wala haviwezi kujitetea wenyewe. Wakayaona makosa yao. Baadhi yao wakasema: Ibrahim si katika walio dhulumu, bali nyinyi ndio madhaalimu kwa kuabudu vitu visio stahiki kuabudiwa.
  65. ثُمَّ نُكِسُوا۟ عَلَىٰ رُءُوسِهِمْ لَقَدْ عَلِمْتَ مَا هَـٰٓؤُلَآءِ يَنطِقُونَ۝٦٥

    Thumma nukisoo ʿala ruoosihim laqad ʿalimta ma haolai yantiqoona

    Kisha wakarejea kwenye ule ule upotovu wao wakasema: Wewe unajua kwamba hawa hawesemi.65

    Maelezo
    [65] Kisha wakarejea tena, wakaacha uwongofu, wakarudia upotovu. Wakamwambia Ibrahim: Hakika wewe umekwisha jua kuwa haya masanamu tunayo yaabudu hayasemi kitu. Basi vipi unatutaka tuyaulize?
  66. قَالَ أَفَتَعْبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَنفَعُكُمْ شَيْـًٔا وَلَا يَضُرُّكُمْ۝٦٦

    Qala afataʿbudoona min dooni Allahi ma la yanfaʿukum shayan wala yadurrukum

    Akasema: Basi nyinyi mnawaabudu asiye kuwa Mwenyezi Mungu wasio kufaini kitu wala kukudhuruni?66

    Maelezo
    [66] Ibrahim akasema: Ikiwa hali yao haya masanamu ni hii, hayawezi kitu, na nyinyi ndio makhusiano yenu nao ni hivi, basi nyinyi mmekuwa mnaacha kumuabudu Mwenyezi Mungu, na badala yake mnaabudu vitu visivyo kupeni faida hata chembe mkiviabudu, wala havikudhuruni kwa lolote mkiviachilia mbali?
  67. أُفٍّ لَّكُمْ وَلِمَا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ ۖ أَفَلَا تَعْقِلُونَ۝٦٧

    Offin lakum walima taʿbudoona min dooni Allahi afala taʿqiloona

    Aibu yenu nyinyi na hivyo mnavyo viabudu badala ya Mwenyezi Mungu! Basi nyinyi hamtii akilini?67

    Maelezo
    [67] Aibu yenu! Nyinyi na miungu yenu mmelaanika! Mnaacha fikra zenu zipotee, na mnapuuza kuzingatia? Bila ya shaka haya masanamu hayafai kuabudiwa!
  68. قَالُوا۟ حَرِّقُوهُ وَٱنصُرُوٓا۟ ءَالِهَتَكُمْ إِن كُنتُمْ فَـٰعِلِينَ۝٦٨

    Qaloo harriqoohu waonsuroo alihatakum in kuntum faʿileena

    Wakasema: Mchomeni moto, na muinusuru miungu yenu, ikiwa nyinyi ni watendao jambo!68

    Maelezo
    [68] Wakaambiana wenyewe kwa wenyewe: Mchomeni moto mpate kuinusuru miungu yenu kwa mateso haya, ikiwa nyinyi mnataka kufanya kitu cha kuiunusuru miungu yenu.
  69. قُلْنَا يَـٰنَارُ كُونِى بَرْدًا وَسَلَـٰمًا عَلَىٰٓ إِبْرَٰهِيمَ۝٦٩

    Qulna ya naru koonee bardan wasalaman ʿala ibraheema

    Sisi tukasema: Ewe moto! Kuwa baridi na salama kwa Ibrahim!69

    Maelezo
    [69] Sisi tukaufanya moto ule uwe baridi na salama, hauna madhara yoyote, kwa Ibrahim.
  70. وَأَرَادُوا۟ بِهِۦ كَيْدًا فَجَعَلْنَـٰهُمُ ٱلْأَخْسَرِينَ۝٧٠

    Waaradoo bihi kaydan fajaʿalnahumu alakhsareena

    Wao walimkusudia maovu, lakini Sisi tukawafanya wao ndio walio khasiri.70

    Maelezo
    [70] Wao walitaka kumuangamiza, lakini Sisi tukamwokoa, na tukawafanya wao ndio watu walio khasiri mno.
  71. وَنَجَّيْنَـٰهُ وَلُوطًا إِلَى ٱلْأَرْضِ ٱلَّتِى بَـٰرَكْنَا فِيهَا لِلْعَـٰلَمِينَ۝٧١

    Wanajjaynahu walootan ila alardi allatee barakna feeha lilʿalameena

    Na tukamwokoa yeye na Luut'i tukawapeleka kwenye nchi tulio ibariki kwa ajili ya walimwengu wote.71

    Maelezo
    [71] Na tukamwokoa yeye na Luut'i na njama zilizo pangwa, wakaelekea kwenye nchi tuliyo ijaalia kheri nyingi kwa watu wote, na tukawapeleka huko Manabii wengi.
  72. وَوَهَبْنَا لَهُۥٓ إِسْحَـٰقَ وَيَعْقُوبَ نَافِلَةً ۖ وَكُلًّا جَعَلْنَا صَـٰلِحِينَ۝٧٢

    Wawahabna lahu ishaqa wayaʿqooba nafilatan wakullan jaʿalna saliheena

    Naye tukampa Is-haq, na Yaaqub kuwa ni ziada. Na wote tukawajaalia wawe watu wema.72

    Maelezo
    [72] Na tukampa Ibrahim mtoto Is-haq, na kutokana na Is-haq tukampa Yaaqubu, zaidi kuliko aliyo taka. Na wote wawili, Is-haq na Yaaqubu tuliwajaalia kuwa ni watu wema.
  73. وَجَعَلْنَـٰهُمْ أَئِمَّةً يَهْدُونَ بِأَمْرِنَا وَأَوْحَيْنَآ إِلَيْهِمْ فِعْلَ ٱلْخَيْرَٰتِ وَإِقَامَ ٱلصَّلَوٰةِ وَإِيتَآءَ ٱلزَّكَوٰةِ ۖ وَكَانُوا۟ لَنَا عَـٰبِدِينَ۝٧٣

    Wajaʿalnahum aimmatan yahdoona biamrina waawhayna ilayhim fiʿla alkhayrati waiqama alssalati waeetaa alzzakati wakanoo lana ʿabideena

    Na tukawafanya maimamu wakiongoa watu kwa amri yetu. Na tukawafunulia watende kheri, na washike Swala, na watoe Zaka; na walikuwa wanatuabudu Sisi tu.73

    Maelezo
    [73] Na tukawafanya ni Manabii wakiwaendea watu, wakiwaongoa kwenye kheri kwa mujibu wa tulivyo waamrisha. Na tukawaonyesha vitendo vyema, na kudumisha Swala kama inavyo faa, na kutoa Zaka. Na wakawa wanatunyenyekea na kutusafia ibada Sisi tu.
  74. وَلُوطًا ءَاتَيْنَـٰهُ حُكْمًا وَعِلْمًا وَنَجَّيْنَـٰهُ مِنَ ٱلْقَرْيَةِ ٱلَّتِى كَانَت تَّعْمَلُ ٱلْخَبَـٰٓئِثَ ۗ إِنَّهُمْ كَانُوا۟ قَوْمَ سَوْءٍ فَـٰسِقِينَ۝٧٤

    Walootan ataynahu hukman waʿilman wanajjaynahu mina alqaryati allatee kanat taʿmalu alkhabaitha innahum kanoo qawma sawin fasiqeena

    Na Luut'i tukampa hukumu na ilimu na tukamwokoa na ule mji ulio kuwa ukifanya maovu. Hakika hao walikuwa watu wabaya, wachafu.74

    Maelezo
    [74] Luut'i tukampa kauli ya kukata na madhubuti katika hukumu na ilimu yenye manufaa. Na tukamwokoa kutokana na mji ambao watu wake wanafanya kitendo cha namna ya peke yake katika uovu. Hakika hao walikuwa watu walio shikilia kufanya maovu, walio toka kwenye ut'iifu wa Mwenyezi Mungu na tabia iliyo zowewa.
  75. وَأَدْخَلْنَـٰهُ فِى رَحْمَتِنَآ ۖ إِنَّهُۥ مِنَ ٱلصَّـٰلِحِينَ۝٧٥

    Waadkhalnahu fee rahmatina innahu mina alssaliheena

    Na tukamuingiza katika rehema yetu. Hakika yeye ni miongoni mwa watenda mema.75

    Maelezo
    [75] Tukampeleka njia ya watu wa rehema yetu. Hakika huyo alikuwa miongoni mwa watu wema alio wakusanya Mwenyezi Mungu katika rehema yake na akawakunjulia msaada wake.
  76. وَنُوحًا إِذْ نَادَىٰ مِن قَبْلُ فَٱسْتَجَبْنَا لَهُۥ فَنَجَّيْنَـٰهُ وَأَهْلَهُۥ مِنَ ٱلْكَرْبِ ٱلْعَظِيمِ۝٧٦

    Wanoohan ith nada min qablu faistajabna lahu fanajjaynahu waahlahu mina alkarbi alʿatheemi

    Na Nuhu alipo ita zamani, nasi tukamuitikia, na tukamwokoa yeye na watu wake kutokana na shida kubwa.76

    Maelezo
    [76] Na hapa tumjaje Nu'h kabla ya Ibrahim na Luu't, pale alipo muomba Mola wake Mlezi, aisafishe nchi kwa kuondoa waovu tukamuitikia ombi lake, tukamuokowa yeye na wale walioamini katika watu wake, kutokana na shakawa (shida) ya kimbunga kikubwa.
  77. وَنَصَرْنَـٰهُ مِنَ ٱلْقَوْمِ ٱلَّذِينَ كَذَّبُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَآ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا۟ قَوْمَ سَوْءٍ فَأَغْرَقْنَـٰهُمْ أَجْمَعِينَ۝٧٧

    Wanasarnahu mina alqawmi allatheena kaththaboo biayatina innahum kanoo qawma sawin faaghraqnahum ajmaʿeena

    Na tukamnusuru na watu walio zikanusha Ishara zetu. Hakika hao walikuwa watu wabaya. Basi tukawazamisha wote.77

    Maelezo
    [77] Tukamlinda kwa nusura yetu na vitimbi vya kaumu yake walio zikanusha Ishara zetu zenye kuthibitisha Utume wake. Hakika hao walikuwa watu wa shari. Basi tukawagharikisha wote!
  78. وَدَاوُۥدَ وَسُلَيْمَـٰنَ إِذْ يَحْكُمَانِ فِى ٱلْحَرْثِ إِذْ نَفَشَتْ فِيهِ غَنَمُ ٱلْقَوْمِ وَكُنَّا لِحُكْمِهِمْ شَـٰهِدِينَ۝٧٨

    Wadawooda wasulaymana ith yahkumani fee alharthi ith nafashat feehi ghanamu alqawmi wakunna lihukmihim shahideena

    Na Daud na Suleiman walipo kata hukumu katika kadhiya ya konde walipo lisha humo mbuzi wa watu usiku. Na Sisi tulikuwa wenye kushuhudia hukumu yao hiyo.78

    Maelezo
    [78] Ewe Nabii! Wataje Daud na Suleiman walipo toa hukumu katika kesi ya konde, ilio ingiliwa na mbuzi wa watu mbali usiku na wakala mazao yake. Na Sisi tulikuwa tunaijua hukumu iliyo khusiana na kesi hiyo. Kisa cha hiyo hukumu: Mbuzi waliingia usiku mmoja katika konde ya mtu, wasibakishe kitu. Daud akahukumu kuwa wale mbuzi wawe wa mwenye konde kulipia khasara yake. Suleiman akatoa hukumu nyengine, akasema: Mbuzi wale wabakie mkononi mwa mwenye konde mpaka itapo mea tena mazao yake, na avumilie kwa yaliyo mpata. Na baada yake warejesheane.
  79. فَفَهَّمْنَـٰهَا سُلَيْمَـٰنَ ۚ وَكُلًّا ءَاتَيْنَا حُكْمًا وَعِلْمًا ۚ وَسَخَّرْنَا مَعَ دَاوُۥدَ ٱلْجِبَالَ يُسَبِّحْنَ وَٱلطَّيْرَ ۚ وَكُنَّا فَـٰعِلِينَ۝٧٩

    Fafahhamnaha sulaymana wakullan atayna hukman waʿilman wasakhkharna maʿa dawooda aljibala yusabbihna waalttayra wakunna faʿileena

    Tukamfahamisha Suleiman. Na kila mmoja wao tulimpa hukumu na ilimu. Na tuliifanya milima na ndege kuwa pamoja na Daud imnyenyekee na imtakase Mwenyezi Mungu. Na Sisi ndio tulio fanya hayo.79

    Maelezo
    [79] Basi tulimfahamisha Suleiman hiyo fatwa. Na wote wawili tuliwapa hikima na ilimu ya maisha na mambo yake. Na tulimfanyia Daud pamoja na milima it'ii na imtakase Mwenyezi Mungu kama alivyo kuwa anamtakasa yeye Daud na kila lisio kuwa linamwelekea Mwenyezi Mungu. Na kadhaalika tuliwafanya ndege hivyo hivyo wamsabihi Mwenyezi Mungu pamoja naye. Na tulifanya hayo kwa uweza wetu usio shindika.
  80. وَعَلَّمْنَـٰهُ صَنْعَةَ لَبُوسٍ لَّكُمْ لِتُحْصِنَكُم مِّنۢ بَأْسِكُمْ ۖ فَهَلْ أَنتُمْ شَـٰكِرُونَ۝٨٠

    Waʿallamnahu sanʿata laboosin lakum lituhsinakum min basikum fahal antum shakiroona

    Na tukamfundisha kuunda mavazi ya vita kwa ajili yenu ili yakuhifadhini katika kupigana kwenu. Je! Mtakuwa wenye kushukuru?80

    Maelezo
    [80] Tukamfundisha Daud kufuma nguo za chuma, ili zikulindeni katika vita vyenu. Basi mshukuruni Mwenyezi Mungu kwa neema hii aliyo kuneemesheni.
  81. وَلِسُلَيْمَـٰنَ ٱلرِّيحَ عَاصِفَةً تَجْرِى بِأَمْرِهِۦٓ إِلَى ٱلْأَرْضِ ٱلَّتِى بَـٰرَكْنَا فِيهَا ۚ وَكُنَّا بِكُلِّ شَىْءٍ عَـٰلِمِينَ۝٨١

    Walisulaymana alrreeha ʿasifatan tajree biamrihi ila alardi allatee barakna feeha wakunna bikulli shayin ʿalimeena

    Na tukamsahilishia Suleiman upepo wa kimbunga wendao kwa amri yake kwenye ardhi tuliyo ibarikia. Na Sisi ndio tunao jua kila kitu.81

    Maelezo
    [81] Na tulimsahilishia Suleiman upepo unao vuma kwa nguvu umtumikie, nao huo ulikuwa unakwenda kwa kufuata amri yake mpaka kwenye nchi tuliyo izidishia kheri yake. Nasi ni wenye kuyajua yote hayo. Halitupotei kubwa wala dogo.
  82. وَمِنَ ٱلشَّيَـٰطِينِ مَن يَغُوصُونَ لَهُۥ وَيَعْمَلُونَ عَمَلًا دُونَ ذَٰلِكَ ۖ وَكُنَّا لَهُمْ حَـٰفِظِينَ۝٨٢

    Wamina alshshayateeni man yaghoosoona lahu wayaʿmaloona ʿamalan doona thalika wakunna lahum hafitheena

    Na pia mashet'ani wanao mpigia mbizi na kufanya kazi nyenginezo. Na Sisi tulikuwa walinzi wao.82

    Maelezo
    [82] Na tukawafanya mashetani wamtumikie kwa kuzamia chini baharini kumletea lulu na marijani; na wakifanya kazi nyenginezo, kama kujenga ngome na majumba ya kifalme. Na Sisi tulikuwa tukiwaangalia katika kazi zao hizo, basi hapana hata mmoja wao aliye pata shida, wala hawakuvunja amri ya Suleiman.
  83. ۞ وَأَيُّوبَ إِذْ نَادَىٰ رَبَّهُۥٓ أَنِّى مَسَّنِىَ ٱلضُّرُّ وَأَنتَ أَرْحَمُ ٱلرَّٰحِمِينَ۝٨٣

    Waayyooba ith nada rabbahu annee massaniya alddurru waanta arhamu alrrahimeena

    Na Ayyubu, alipo mwita Mola wake Mlezi, akasema: Mimi yamenipata madhara. Na Wewe ndiye unaye rehemu kuliko wote wanao rehemu.83

    Maelezo
    [83] Ewe Nabii! Mtaje Ayyubu, pale alipo mwita Mola wake Mlezi, na maradhi yalikwisha mdhoofisha, na akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Hakika nimesibiwa na madhara na yananiuma! Na Wewe ni Mbora wa wanao rehemu..
  84. فَٱسْتَجَبْنَا لَهُۥ فَكَشَفْنَا مَا بِهِۦ مِن ضُرٍّ ۖ وَءَاتَيْنَـٰهُ أَهْلَهُۥ وَمِثْلَهُم مَّعَهُمْ رَحْمَةً مِّنْ عِندِنَا وَذِكْرَىٰ لِلْعَـٰبِدِينَ۝٨٤

    Faistajabna lahu fakashafna ma bihi min durrin waataynahu ahlahu wamithlahum maʿahum rahmatan min ʿindina wathikra lilʿabideena

    Basi tukamwitikia, na tukamwondolea madhara aliyo kuwa nayo, na tukampa watu wake na mfano wao pamoja nao kuwa ni rehema inayo toka kwetu, na ukumbusho kwa wafanyao ibada.84

    Maelezo
    [84] Tukamwitikia kwa aliyo yaomba, tukamwondolea madhara, na tukampa watoto kwa kadri ya waliyo kwisha kufa. Na tukamwongezea mfano wa wale, kuwa ni rehema iliyo tokana na fadhila yetu, na pia ni kuwa ni kumbusho kwa wenginewe wanao tuabudu ili wapate nao kusubiri kama alivyo subiri yeye, na watumai kupata rehema ya Mwenyezi Mungu kama alivyo tumai yeye.
  85. وَإِسْمَـٰعِيلَ وَإِدْرِيسَ وَذَا ٱلْكِفْلِ ۖ كُلٌّ مِّنَ ٱلصَّـٰبِرِينَ۝٨٥

    Waismaʿeela waidreesa watha alkifli kullun mina alssabireena

    Na Ismail, na Idris, na Dhulkifli - wote walikuwa miongoni mwa wanao subiri.85

    Maelezo
    [85] Ewe Nabii! Watajie watu wako khabari za Ismail, na Idris, na Dhulkifli. Wote hao ni miongoni wanao subiri wakahimili taklifa na shida.
  86. وَأَدْخَلْنَـٰهُمْ فِى رَحْمَتِنَآ ۖ إِنَّهُم مِّنَ ٱلصَّـٰلِحِينَ۝٨٦

    Waadkhalnahum fee rahmatina innahum mina alssaliheena

    Na tukawaingiza katika rehema yetu. Hakika wao walikuwa katika watu wema.86

    Maelezo
    [86] Na tukawajaalia miongoni mwa watu wa kupata rehema yetu. Hakika hao ni katika waja wetu wema.
  87. وَذَا ٱلنُّونِ إِذ ذَّهَبَ مُغَـٰضِبًا فَظَنَّ أَن لَّن نَّقْدِرَ عَلَيْهِ فَنَادَىٰ فِى ٱلظُّلُمَـٰتِ أَن لَّآ إِلَـٰهَ إِلَّآ أَنتَ سُبْحَـٰنَكَ إِنِّى كُنتُ مِنَ ٱلظَّـٰلِمِينَ۝٨٧

    Watha alnnooni ith thahaba mughadiban fathanna an lan naqdira ʿalayhi fanada fee alththulumati an la ilaha illa anta subhanaka innee kuntu mina alththalimeena

    Na Dhun-Nun alipoondoka hali ameghadhibika, na akadhani ya kwamba hatutakuwa na uwezo juu yake. Basi aliita katika giza: Hapana mungu isipo kuwa Wewe Subhanaka Uliye takasika. Hakika mimi nilikuwa miongoni mwa wenye kudhulumu.87

    Maelezo
    [87] Ewe Nabii! Taja kisa cha Yunus, aliye mezwa na samaki..Pale alipoona dhiki kwa vile watu wake walipo puuza wito wake, naye akawahama akenda mbali nao na huku amewakasirikia. Akadhani ya kuwa Mwenyezi Mungu amemruhusu kuwahama, na kwamba haitopita hukumu juu yake. Samaki akammeza, na akaishi katika kiza cha bahari. Akamwita Mola wake Mlezi kwa kumnyenyekea, na kuungama aliyo kuwa nayo, akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Hapana wa kuabudiwa kwa haki ila Wewe. Ninakutakasa na kila lisio kuelekea Wewe. Ninaungama kuwa hakika mimi nilikuwa miongoni mwa walio dhulumu nafsi zao kwa kutenda yasio kupendeza.
  88. فَٱسْتَجَبْنَا لَهُۥ وَنَجَّيْنَـٰهُ مِنَ ٱلْغَمِّ ۚ وَكَذَٰلِكَ نُـۨجِى ٱلْمُؤْمِنِينَ۝٨٨

    Faistajabna lahu wanajjaynahu mina alghammi wakathalika nunjee almumineena

    Basi tukamwitikia na tukamwokoa kutokana na dhiki. Na hivyo ndivyo tunavyo waokoa Waumini.88

    Maelezo
    [88] Tukamwitikia kwa aliyo kuwa akiyaomba, na tukamvua na dhiki aliyo kuwa nayo. Na mfano wa hivi ndivyo tunavyo waokoa Waumini wanao ungama makosa yao, na wakatuomba kwa usafi wa moyo.
  89. وَزَكَرِيَّآ إِذْ نَادَىٰ رَبَّهُۥ رَبِّ لَا تَذَرْنِى فَرْدًا وَأَنتَ خَيْرُ ٱلْوَٰرِثِينَ۝٨٩

    Wazakariyya ith nada rabbahu rabbi la tatharnee fardan waanta khayru alwaritheena

    Na Zakariya alipo mwita Mola wake Mlezi: Mola wangu Mlezi! Usiniache peke yangu, na Wewe ndiye Mbora wa wanao rithi.89

    Maelezo
    [89] Na kitaje kisa cha Zakariya alipo mwita Mola wake Mlezi baada ya kwisha ona uweza wake Subhanahu kwa alivyo mtia katika nafsi yake matarajio ya rehema yake. Alisema: Ewe Mola wangu Mlezi! Usiniache mpweke bila ya kuwa na mrithi, na Wewe ndiye Mbora wa wanao rithi. Kwani Wewe ndiye utakaye baki baada ya kumalizika viumbe vyote.
  90. فَٱسْتَجَبْنَا لَهُۥ وَوَهَبْنَا لَهُۥ يَحْيَىٰ وَأَصْلَحْنَا لَهُۥ زَوْجَهُۥٓ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا۟ يُسَـٰرِعُونَ فِى ٱلْخَيْرَٰتِ وَيَدْعُونَنَا رَغَبًا وَرَهَبًا ۖ وَكَانُوا۟ لَنَا خَـٰشِعِينَ۝٩٠

    Faistajabna lahu wawahabna lahu yahya waaslahna lahu zawjahu innahum kanoo yusariʿoona fee alkhayrati wayadʿoonana raghaban warahaban wakanoo lana khashiʿeena

    Na mwanamke aliye linda uke wake, na tukampulizia katika roho yetu, na tukamfanya yeye na mwanawe kuwa ni Ishara kwa walimwengu.90

    Maelezo
    [90] Tukamtimizia matumaini yake, na tukamwitikia dua yake, na tukamtunukia juu ya ukongwe mwanawe, Yahya, tukamfanya mkewe tasa aweze kuzaa. Hakika wasafi hao Manabii walikuwa wepesi wa kutenda kheri tunayo waitaka waitende, na wanatuomba kwa kutumai rehema yetu, na kuikhofu adhabu yetu. Na walikuwa hawamtukuzi mtu wala hawamwogopi mtu isipo kuwa Sisi tu.
  91. وَٱلَّتِىٓ أَحْصَنَتْ فَرْجَهَا فَنَفَخْنَا فِيهَا مِن رُّوحِنَا وَجَعَلْنَـٰهَا وَٱبْنَهَآ ءَايَةً لِّلْعَـٰلَمِينَ۝٩١

    Waallatee ahsanat farjaha fanafakhna feeha min roohina wajaʿalnaha waibnaha ayatan lilʿalameena

    Na mwanamke aliye linda uke wake, na tukampulizia katika roho yetu, na tukamfanya yeye na mwanawe kuwa ni Ishara kwa walimwengu.91

    Maelezo
    [91] Pamoja na hawa simulia kisa cha Maryamu aliye ulinda uke wake, nasi tukamfikishia siri katika siri zetu. Tukamjaalia achukue mimba bila ya mume, na tukamjaalia mwanawe azaliwe bila ya baba. Akawa yeye na mwanawe dalili iliyo wazi ya uweza wetu kugeuza sababu na vinavyo sabibishwa. Na hakika Sisi ni waweza wa kila kitu.
  92. إِنَّ هَـٰذِهِۦٓ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَٰحِدَةً وَأَنَا۠ رَبُّكُمْ فَٱعْبُدُونِ۝٩٢

    Inna hathihi ommatukum ommatan wahidatan waana rabbukum faoʿbudooni

    Kwa hakika huu umma wenu ni umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu Mlezi. Kwa hivyo niabuduni Mimi.92

    Maelezo
    [92] Hakika mila hii, nayo ndiyo Uislamu, ndiyo mila iliyo sahihi inayo kupasini kuilinda, kwa kuwa ni mila moja iliyo shikamana wala haikukhitalifiana baina ya hukumu zake. Basi nanyi msifarikiene katika mila hii kwa makundi na vyama. Na Mimi ndiye Muumba wenu, na Mwenye kumiliki mambo yenu yote. Basi niabuduni Mimi tu, wala msinishirikishe na mwengine.
  93. وَتَقَطَّعُوٓا۟ أَمْرَهُم بَيْنَهُمْ ۖ كُلٌّ إِلَيْنَا رَٰجِعُونَ۝٩٣

    Wataqattaʿoo amrahum baynahum kullun ilayna rajiʿoona

    Nao wakalikata jambo lao hili mapande mapande baina yao. Wote watarudi kwetu.93

    Maelezo
    [93] Na juu ya kuwepo uwongozi huu aghlabu ya watu wamegawanyika kwa mujibu wa matamanio yao, wakafanya mambo yao ya Dini mapande mapande, wakawa makundi mbali mbali. Na kila kundi litaturejea Sisi tulihisabie vitendo vyake.
  94. فَمَن يَعْمَلْ مِنَ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَا كُفْرَانَ لِسَعْيِهِۦ وَإِنَّا لَهُۥ كَـٰتِبُونَ۝٩٤

    Faman yaʿmal mina alssalihati wahuwa muminun fala kufrana lisaʿyihi wainna lahu katiboona

    Na atendaye mema naye ni Muumini basi haitakataliwa juhudi yake. Na hakika Sisi tunamwandikia.94

    Maelezo
    [94] Basi mwenye kutenda vitendo vyake vyema, naye ni mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Dini yake aliyo iridhia, hatopunguziwa kitu katika juhudi yake. Bali atalipwa malipo kaamili. Na Sisi ni wenye kuiandika hiyo juhudi yake. Basi hakitopotea kitu.
  95. وَحَرَٰمٌ عَلَىٰ قَرْيَةٍ أَهْلَكْنَـٰهَآ أَنَّهُمْ لَا يَرْجِعُونَ۝٩٥

    Waharamun ʿala qaryatin ahlaknaha annahum la yarjiʿoona

    Na haiwi kwa wana-mji tulio uangamiza, ya kwamba hawatarejea,95

    Maelezo
    [95] Na haitakuwa kwa watu wa mji tulio uteketeza kwa sababu ya dhulma yao kwamba hawatarejea kwetu Siku ya Kiyama, bali hapana budi kuwa watarejea na tutawahisabia vitendo vyao viovu.
  96. حَتَّىٰٓ إِذَا فُتِحَتْ يَأْجُوجُ وَمَأْجُوجُ وَهُم مِّن كُلِّ حَدَبٍ يَنسِلُونَ۝٩٦

    Hatta itha futihat yajooju wamajooju wahum min kulli hadabin yansiloona

    Mpaka watapo funguliwa Juju na Maajuju wakawa wanateremka kutoka kila mlima;96

    Maelezo
    [96] Mpaka itapo funguliwa milango ya shari na ufisadi, wakaingia wana wa Juju na Maajuju wakikimbizana kuteremka milimani na majiani kwa kufanya vitendo vya fujo na rabsha.
  97. وَٱقْتَرَبَ ٱلْوَعْدُ ٱلْحَقُّ فَإِذَا هِىَ شَـٰخِصَةٌ أَبْصَـٰرُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ يَـٰوَيْلَنَا قَدْ كُنَّا فِى غَفْلَةٍ مِّنْ هَـٰذَا بَلْ كُنَّا ظَـٰلِمِينَ۝٩٧

    Waiqtaraba alwaʿdu alhaqqu faitha hiya shakhisatun absaru allatheena kafaroo ya waylana qad kunna fee ghaflatin min hatha bal kunna thalimeena

    Na miadi ya haki ikakaribia. Hapo ndipo yatapo kodoka macho ya walio kufuru (na watasema:) Ole wetu! Bila ya shaka tulikuwa tumeghafilika na haya, bali tulikuwa wenye kudhulumu.97

    Maelezo
    [97] Na ikakaribia miadi iliyo haina budi kutimizwa, nayo ni Siku ya Kiyama, wakawa wale walio kufuru wanakutikana wakikodoa macho yao kwa wingi wa kitisho, wakipiga makelele kusema: Kitisho gani hichi cha kutuangamiza! Hakika sisi tulighafilika na Siku hii. Bali tulikuwa ni wenye kujidhulumu nafsi zetu kwa ukafiri na inda.
  98. إِنَّكُمْ وَمَا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ حَصَبُ جَهَنَّمَ أَنتُمْ لَهَا وَٰرِدُونَ۝٩٨

    Innakum wama taʿbudoona min dooni Allahi hasabu jahannama antum laha waridoona

    Hakika nyinyi na hao mnao waabudu badala ya Mwenyezi Mungu ni kuni za Jahannamu; huko mtaingia tu.98

    Maelezo
    [98] Wataambiwa makafiri hawa: Nyinyi na hiyo miungu mliyo kuwa mkiiabudu badala ya Mwenyezi Mungu ni kuni za Moto wa Jahannamu. Nyinyi mtaingia humo muadhibiwe!
  99. لَوْ كَانَ هَـٰٓؤُلَآءِ ءَالِهَةً مَّا وَرَدُوهَا ۖ وَكُلٌّ فِيهَا خَـٰلِدُونَ۝٩٩

    Law kana haolai alihatan ma waradooha wakullun feeha khalidoona

    Lau kuwa hawa ni miungu, wasingeli ingia. Na wote watadumu humo.99

    Maelezo
    [99] Lau kama hawa mlio waabudu badala ya Mwenyezi Mungu ni miungu inayo stahiki kuabudiwa, wasingeli ingia nanyi humo. Na nyote, wenye kuabudu na kuabudiwa, mtabaki Motoni, wala hamtatoka.
  100. لَهُمْ فِيهَا زَفِيرٌ وَهُمْ فِيهَا لَا يَسْمَعُونَ۝١٠٠

    Lahum feeha zafeerun wahum feeha la yasmaʿoona

    Lao wao humo ni kupiga mayowe, na wala hawatasikia (jenginelo).100

    Maelezo
    [100] Humo watatoa pumzi zitokazo vifuani kwa sauti kama ya mwenye kukabwa, kwa dhiki watayo pata, na hawatasikia la kuwafurahisha.
  101. إِنَّ ٱلَّذِينَ سَبَقَتْ لَهُم مِّنَّا ٱلْحُسْنَىٰٓ أُو۟لَـٰٓئِكَ عَنْهَا مُبْعَدُونَ۝١٠١

    Inna allatheena sabaqat lahum minna alhusna olaika ʿanha mubʿadoona

    Ama wale ambao wema wetu umewatangulia, hao watatenganishwa na hayo.101

    Maelezo
    [101] Hakika wale tulio wakubalia kwa kufuata kwao Haki na vitendo vya kheri, na tukawaahidi malipo mema, hao watawekwa mbali kabisa na Jahannamu na adhabu yake.
  102. لَا يَسْمَعُونَ حَسِيسَهَا ۖ وَهُمْ فِى مَا ٱشْتَهَتْ أَنفُسُهُمْ خَـٰلِدُونَ۝١٠٢

    La yasmaʿoona haseesaha wahum fee ma ishtahat anfusuhum khalidoona

    Hawatausikia mvumo wake, na wao watadumu katika yale zinayo yatamani nafsi zao.102

    Maelezo
    [102] Hawatasikia sauti ya Moto wake unavyo vuma. Nao huko watapata kila ambacho nafsi inatamani, daima milele.
  103. لَا يَحْزُنُهُمُ ٱلْفَزَعُ ٱلْأَكْبَرُ وَتَتَلَقَّىٰهُمُ ٱلْمَلَـٰٓئِكَةُ هَـٰذَا يَوْمُكُمُ ٱلَّذِى كُنتُمْ تُوعَدُونَ۝١٠٣

    La yahzunuhumu alfazaʿu alakbaru watatalaqqahumu almalaikatu hatha yawmukumu allathee kuntum tooʿadoona

    Hicho Kitisho Kikubwa hakito wahuzunisha. Na Malaika watawapokea (kwa kuwaambia): Hii ndiyo Siku yenu mliyo kuwa mkiahidiwa!.103

    Maelezo
    [103] Hawato huzunishwa na Kitisho Kikubwa kinacho wafazaisha makafiri. Na Malaika watawapokea kwa kuwapongeza kwa kusema: Hii ndiyo Siku yenu ya neema aliyo kuahidini Mola wenu Mlezi!
  104. يَوْمَ نَطْوِى ٱلسَّمَآءَ كَطَىِّ ٱلسِّجِلِّ لِلْكُتُبِ ۚ كَمَا بَدَأْنَآ أَوَّلَ خَلْقٍ نُّعِيدُهُۥ ۚ وَعْدًا عَلَيْنَآ ۚ إِنَّا كُنَّا فَـٰعِلِينَ۝١٠٤

    Yawma natwee alssamaa katayyi alssijlli lilkutubi kama badana awwala khalqin nuʿeeduhu waʿdan ʿalayna inna kunna faʿileena

    Siku tutakapo zikunja mbingu kama mkunjo wa karatasi za vitabu. Kama tulivyo anza umbo la mwanzo tutalirudisha tena. Ni ahadi iliyo juu yetu. Hakika Sisi ni watendao.104

    Maelezo
    [104] Siku tutapo zikunja mbingu kama zinavyo kunjwa karatasi katika kitabu. Na tutawarejeza viumbe kwa ajili ya hisabu na malipo. Wala hatushindwi kuwarejeza, kwani tuliwaumba mara ya kwanza. Na kama tulivyo waanza tutawarejeza. Ahadi yetu kwa hayo ni ahadi ya kweli. Daima Sisi tunatenda tunayo yaahidi.
  105. وَلَقَدْ كَتَبْنَا فِى ٱلزَّبُورِ مِنۢ بَعْدِ ٱلذِّكْرِ أَنَّ ٱلْأَرْضَ يَرِثُهَا عِبَادِىَ ٱلصَّـٰلِحُونَ۝١٠٥

    Walaqad katabna fee alzzaboori min baʿdi alththikri anna alarda yarithuha ʿibadiya alssalihoona

    Na hakika tulikwisha andika katika Zaburi baada ya Kumbukumbu, ya kwamba nchi watairithi waja wangu walio wema.105

    Maelezo
    [105] Na tulikwisha andika katika Zaburi - nacho ni Kitabu cha Daud baada ya Taurati - kwamba nchi watairithi waja wangu walio wema wapate kuitengeza, na kusahilisha njia za maisha bora humo. ("Bali wenye upole watairithi nchi"..Zaburi 37.11 "Wenye haki watairithi nchi, nao watakaa humo milele".. Zaburi 37.29)
  106. إِنَّ فِى هَـٰذَا لَبَلَـٰغًا لِّقَوْمٍ عَـٰبِدِينَ۝١٠٦

    Inna fee hatha labalaghan liqawmin ʿabideena

    Hakika katika haya yapo mawaidha kwa watu wafanyao ibada.106

    Maelezo
    [106] Hakika katika haya tuliyo yataja, khabari za Manabii pamoja na kaumu zao, na khabari za Pepo na Moto, yanatosha kuwakumbusha na kuwafanya wazingatie watu walio tayari kumuabudu Mwenyezi Mungu pekee na hawasalitiki na mapambo ya dunia.
  107. وَمَآ أَرْسَلْنَـٰكَ إِلَّا رَحْمَةً لِّلْعَـٰلَمِينَ۝١٠٧

    Wama arsalnaka illa rahmatan lilʿalameena

    Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote.107

    Maelezo
    [107] Na hatukukutuma, ewe Nabii, ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote.
  108. قُلْ إِنَّمَا يُوحَىٰٓ إِلَىَّ أَنَّمَآ إِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَٰحِدٌ ۖ فَهَلْ أَنتُم مُّسْلِمُونَ۝١٠٨

    Qul innama yooha ilayya annama ilahukum ilahun wahidun fahal antum muslimoona

    Sema: Hakika imefunuliwa kwangu ya kwamba hakika Mungu wenu ni Mungu Mmoja tu. Je! Mmesilimu?.108

    Maelezo
    [108] Ewe Nabii! Sema: Hakika kiini cha Wahyi aliyo nipa Mwenyezi Mungu ni kwamba hakika nyinyi hamna Mungu isipo kuwa Yeye. Na yote yaliyo bakia niliyo funuliwa yanafuata asili hii. Ikiwa mambo ni hivyo, basi inakuwajibikieni mjisalimishe na mnyenyekee kwa Mwenyezi Mungu peke yake.
  109. فَإِن تَوَلَّوْا۟ فَقُلْ ءَاذَنتُكُمْ عَلَىٰ سَوَآءٍ ۖ وَإِنْ أَدْرِىٓ أَقَرِيبٌ أَم بَعِيدٌ مَّا تُوعَدُونَ۝١٠٩

    Fain tawallaw faqul athantukum ʿala sawain wain adree aqareebun am baʿeedun ma tooʿadoona

    Na kama wakigeuka, basi sema: Nimekutangazieni sawa sawa, wala sijui yako karibu au mbali hayo mliyo ahidiwa.109

    Maelezo
    [109] Wakito ujali wito wako, basi waambie: Nimekufunzeni yote aliyo niamrisha Mola wangu Mlezi; na kwa hivyo tumekuwa sawa kwa kuyajua hayo. Wala mimi sijui hayo ya kufufuliwa na kuhisabiwa mliyo ahidiwa, yatakuwa karibu au mbali.
  110. إِنَّهُۥ يَعْلَمُ ٱلْجَهْرَ مِنَ ٱلْقَوْلِ وَيَعْلَمُ مَا تَكْتُمُونَ۝١١٠

    Innahu yaʿlamu aljahra mina alqawli wayaʿlamu ma taktumoona

    Hakika Yeye anajua kauli ya dhaahiri na anajua myafichayo.110

    Maelezo
    [110] Hakika Mwenyezi Mungu anayajua yote yasemwayo, mnayo yadhihirisha na mnayo yaficha.
  111. وَإِنْ أَدْرِى لَعَلَّهُۥ فِتْنَةٌ لَّكُمْ وَمَتَـٰعٌ إِلَىٰ حِينٍ۝١١١

    Wain adree laʿallahu fitnatun lakum wamataʿun ila heenin

    Wala sijui pengine huu ni mtihani tu kwenu na starehe mpaka muda kidogo.111

    Maelezo
    [111] Na sijui pengine huko kupewa muhula na kuakhirishiwa adhabu nyinyi ndio Mwenyezi Mungu anakufanyieni mtihani tu, na kukustarehesheni kwa ladha za maisha mpaka alipo kadiria Mwenyezi Mungu kukuhisabieni kwa hikima yake.
  112. قَـٰلَ رَبِّ ٱحْكُم بِٱلْحَقِّ ۗ وَرَبُّنَا ٱلرَّحْمَـٰنُ ٱلْمُسْتَعَانُ عَلَىٰ مَا تَصِفُونَ۝١١٢

    Qala rabbi ohkum bialhaqqi warabbuna alrrahmanu almustaʿanu ʿala ma tasifoona

    Sema: Mola wangu Mlezi! Hukumu kwa haki. Na Mola wetu Mlezi ni Mwingi wa Rehema, aombwaye msaada juu ya mnayo yazua;.112

    Maelezo
    [112] Ewe Nabii! Sema: Ewe Mola Mlezi! Tuhukumu baina yangu na hawa nilio wafikishia Wahyi kwa uadilifu ili wasiwe sawa Waumini na makafiri. Na Mola wetu Mlezi Mwenye kuneemesha kwa neema kubwa, Mwenye kustahiki kuhimidiwa na kushukuriwa, ndiye wa kutakiwa msaada kuvunja uzushi mnao zua, enyi makafiri.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Surat Al-Anbiya maana yake ni nini?

Al-Anbiya maana yake ni “Manabii”.

Surat Al-Anbiya iko katika juzuu ya ngapi?

Surat Al-Anbiya iko katika juzuu ya 17.

Surat Al-Anbiya ina aya ngapi?

Surat Al-Anbiya ina aya 112.

Surat Al-Anbiya ni ya Makka au ya Madina?

Surat Al-Anbiya ni sura ya Makka.

Surat Al-Anbiya ni sura ya ngapi katika Qur’ani?

Ni sura ya 21 katika Qur’ani.

Vyanzo

  • Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
  • Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
  • Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
  • Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
  • Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
  • Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.

Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.

Mipangilio ya kusoma

Fonti ya Qur’ani
Ukubwa wa Kiarabu
100%
Ukubwa wa tafsiri
100%
Mandhari

Ongeza kwenye skrini ya kwanza

ReadSurahFungua ReadSurah kutoka skrini ya kwanza, kwa skrini nzima. Sura ulizosoma hufunguka hata bila intaneti.

  1. Katika Safari, gusa kitufe cha kushiriki (Share). Kwenye iPhone mpya kiko kwenye menyu ya •••.
  2. Gusa “Add to Home Screen”. Huenda ukahitaji kusogeza chini.
  3. Gusa “Add”.