سورة الجمعة

Surat Al-Jumu’a kwa Kiswahili

Ijumaa

Msahafu

Mishary Rashid AlafasyPakua MP3Pakua PDF

Surat Al-Jumu’a (الجمعة) ni sura ya 62 katika Qur’ani na ina aya 11. Jina lake lina maana ya “Ijumaa”. Ni sura ya Madina, iliyoteremshwa Madina baada ya Hijra, na iko katika juzuu ya 28.

Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat Al-Jumu’a yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.

Surat Al-Jumu’a kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

  1. يُسَبِّحُ لِلَّهِ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَمَا فِى ٱلْأَرْضِ ٱلْمَلِكِ ٱلْقُدُّوسِ ٱلْعَزِيزِ ٱلْحَكِيمِ۝١

    Yusabbihu lillahi ma fee alssamawati wama fee alardi almaliki alquddoosi alʿazeezi alhakeemi

    Viliomo mbinguni na viliomo katika ardhi vinamtakasa Mwenyezi Mungu, Mfalme, Mtakatifu, Mwenye nguvu, Mwenye hikima.1

    Maelezo
    [1] Vitu vyote viliomo katika mbingu na viliomo katika ardhi vinamsabihi na kumtakasa Mwenyezi Mungu na kila kisicho kuwa laiki, Yeye ndiye Mfalme wa kila kitu, Mwenye kuendesha atakavyo bila ya mpinzani, Mwenye kutakasika kwa ukamilifu na kila cha upungufu, Mwenye kushinda kila kitu, Mwenye hikima ya kufika mwisho.
  2. هُوَ ٱلَّذِى بَعَثَ فِى ٱلْأُمِّيِّـۧنَ رَسُولًا مِّنْهُمْ يَتْلُوا۟ عَلَيْهِمْ ءَايَـٰتِهِۦ وَيُزَكِّيهِمْ وَيُعَلِّمُهُمُ ٱلْكِتَـٰبَ وَٱلْحِكْمَةَ وَإِن كَانُوا۟ مِن قَبْلُ لَفِى ضَلَـٰلٍ مُّبِينٍ۝٢

    Huwa allathee baʿatha fee alommiyyeena rasoolan minhum yatloo ʿalayhim ayatihi wayuzakkeehim wayuʿallimuhumu alkitaba waalhikmata wain kanoo min qablu lafee dalalin mubeenin

    Yeye ndiye aliye mpeleka Mtume kwenye watu wasio jua kusoma, awasomee Aya zake na awatakase, na awafunze Kitabu na hikima, ijapo kuwa kabla ya haya walikuwa katika upotofu ulio dhaahiri.2

    Maelezo
    [2] Mwenyezi Mungu ndiye aliye mtuma Mtume kwa watu wasio jua kuandika, naye ni katika wao wenyewe, anawasomea Aya zake Mwenyezi Mungu, na anawasafisha na mambo machafu ya itikadi na tabia, na anawafundisha Qur'ani na kuijua Dini. Na wao kabla ya kuletwa yeye walikuwa wamepotoka kabisa kuiacha haki.
  3. وَءَاخَرِينَ مِنْهُمْ لَمَّا يَلْحَقُوا۟ بِهِمْ ۚ وَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلْحَكِيمُ۝٣

    Waakhareena minhum lamma yalhaqoo bihim wahuwa alʿazeezu alhakeemu

    Na kwa wengine ambao bado hawajaungana nao. Na Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima.3

    Maelezo
    [3] Na pia Mwenyezi Mungu amempeleka Muhammad kwa watu wenginewe, ambao hawajaja bado, lakini watakuja. Na Mwenyezi Mungu peke yake ndiye Mwenye kushinda kila kitu, Mwenye hikima ya kufikia ukomo katika vitendo vyake.
  4. ذَٰلِكَ فَضْلُ ٱللَّهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَآءُ ۚ وَٱللَّهُ ذُو ٱلْفَضْلِ ٱلْعَظِيمِ۝٤

    Thalika fadlu Allahi yuteehi man yashao waAllahu thoo alfadli alʿatheemi

    Hiyo ni fadhila ya Mwenyezi Mungu anayo mpa amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kubwa.4

    Maelezo
    [4] Kuletwa Mtume huko ni fadhila inayo toka kwa Mwenyezi Mungu. Anamkirimu kwayo aliye mkhitari katika waja wake. Na Mwenyezi Mungu peke yake, ndiye Mwenye fadhila kubwa.
  5. مَثَلُ ٱلَّذِينَ حُمِّلُوا۟ ٱلتَّوْرَىٰةَ ثُمَّ لَمْ يَحْمِلُوهَا كَمَثَلِ ٱلْحِمَارِ يَحْمِلُ أَسْفَارًۢا ۚ بِئْسَ مَثَلُ ٱلْقَوْمِ ٱلَّذِينَ كَذَّبُوا۟ بِـَٔايَـٰتِ ٱللَّهِ ۚ وَٱللَّهُ لَا يَهْدِى ٱلْقَوْمَ ٱلظَّـٰلِمِينَ۝٥

    Mathalu allatheena hummiloo alttawrata thumma lam yahmilooha kamathali alhimari yahmilu asfaran bisa mathalu alqawmi allatheena kaththaboo biayati Allahi waAllahu la yahdee alqawma alththalimeena

    Mfano wa walio bebeshwa Taurati kisha wasiibebe, ni mfano wa punda anaye beba vitabu vikubwa vikubwa. Mfano muovu mno wa watu walio kadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhaalimu.5

    Maelezo
    [5] Mfano wa Mayahudi walio funzwa Taurati, na wakalazimishwa waifuate, na wao hawakuifuata kwa vitendo, ni mfano wa punda aliye beba vitabu ambavyo hajui ndani yake mna nini. Ni mbaya mno mfano wa watu wanao kadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu hawasaidii kufikilia uwongofu watu ambao kazi yao ni kudhulumu.
  6. قُلْ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ هَادُوٓا۟ إِن زَعَمْتُمْ أَنَّكُمْ أَوْلِيَآءُ لِلَّهِ مِن دُونِ ٱلنَّاسِ فَتَمَنَّوُا۟ ٱلْمَوْتَ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ۝٦

    Qul ya ayyuha allatheena hadoo in zaʿamtum annakum awliyao lillahi min dooni alnnasi fatamannawoo almawta in kuntum sadiqeena

    Sema: Enyi mlio Mayahudi! Ikiwa nyinyi mnadai kuwa ni vipenzi vya Mwenyezi Mungu pasipo kuwa watu wengine, basi yatamanini mauti, ikiwa mnasema kweli.6

    Maelezo
    [6] Ewe Muhammad! Sema: Enyi nyinyi mlio Mayahudi! Kama mnadai kwa uwongo kwamba nyinyi peke yenu ati ndio vipenzi vya Mwenyezi Mungu, basi takeni mauti kwa Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi mnasema kweli katika hayo madai ya kwamba Mwenyezi Mungu anakupendeni.
  7. وَلَا يَتَمَنَّوْنَهُۥٓ أَبَدًۢا بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ ۚ وَٱللَّهُ عَلِيمٌۢ بِٱلظَّـٰلِمِينَ۝٧

    Wala yatamannawnahu abadan bima qaddamat aydeehim waAllahu ʿaleemun bialththalimeena

    Wala hawatayatamani kabisa, kwa sababu ya iliyo kwisha yatanguliza mikono yao. Na Mwenyezi Mungu anawajua walio dhulumu.7

    Maelezo
    [7] Mwenyezi Mungu anasema: Wala Mayahudi hawatamani mauti milele kwa sababu ya ukafiri na vitendo viovu walio kwisha vitenda. Na Mwenyezi Mungu anawajua vyema walio dhulumu.
  8. قُلْ إِنَّ ٱلْمَوْتَ ٱلَّذِى تَفِرُّونَ مِنْهُ فَإِنَّهُۥ مُلَـٰقِيكُمْ ۖ ثُمَّ تُرَدُّونَ إِلَىٰ عَـٰلِمِ ٱلْغَيْبِ وَٱلشَّهَـٰدَةِ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ۝٨

    Qul inna almawta allathee tafirroona minhu fainnahu mulaqeekum thumma turaddoona ila ʿalimi alghaybi waalshshahadati fayunabbiokum bima kuntum taʿmaloona

    Sema: Hayo mauti mnayo yakimbia, bila ya shaka yatakukuteni. Kisha mtarudishwa kwa Mwenye kuyajua yaliyo fichikana na yanayo onekana. Hapo atakwambieni mliyo kuwa mkiyatenda.8

    Maelezo
    [8] Sema: Hayo mauti mnayo yakimbia hamwezi kuyakimbia, bila ya shaka yatakukuteni tu. Kisha mtarudishwa kwa Mwenye kujua ya siri na ya dhaahiri. Na Yeye atakwambieni mliyo kuwa mkiyatenda.
  9. يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِذَا نُودِىَ لِلصَّلَوٰةِ مِن يَوْمِ ٱلْجُمُعَةِ فَٱسْعَوْا۟ إِلَىٰ ذِكْرِ ٱللَّهِ وَذَرُوا۟ ٱلْبَيْعَ ۚ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ۝٩

    Ya ayyuha allatheena amanoo itha noodiya lilssalati min yawmi aljumuʿati faisʿaw ila thikri Allahi watharoo albayʿa thalikum khayrun lakum in kuntum taʿlamoona

    Enyi mlio amini! Ikiadhiniwa Swala siku ya Ijumaa, nendeni upesi kwenye dhikri ya Mwenyezi Mungu, na wacheni biashara. Hayo ni bora kwenu, lau kama mnajua.9

    Maelezo
    [9] Enyi mlio amini! Ikiadhiniwa Swala siku ya Ijumaa, basi nendeni kwa hima na hamu kumkumbuka na kumtaja Mwenyezi Mungu, na wacheni biashara. Hayo mliyo amrishwa yana nafuu zaidi kwenu nyinyi, ikiwa mnajua.
  10. فَإِذَا قُضِيَتِ ٱلصَّلَوٰةُ فَٱنتَشِرُوا۟ فِى ٱلْأَرْضِ وَٱبْتَغُوا۟ مِن فَضْلِ ٱللَّهِ وَٱذْكُرُوا۟ ٱللَّهَ كَثِيرًا لَّعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ۝١٠

    Faitha qudiyati alssalatu faintashiroo fee alardi waibtaghoo min fadli Allahi waothkuroo Allaha katheeran laʿallakum tuflihoona

    Na itakapo kwisha Swala, tawanyikeni katika nchi mtafute fadhila za Mwenyezi Mungu, na mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi ili mpate kufanikiwa.10

    Maelezo
    [10] Mkisha maliza kuswali basi tawanyikeni katika nchi kwa ajili ya maslaha yenu, na mtake fadhila za Mwenyezi Mungu. Na mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa nyoyo zenu na ndimi zenu kwa wingi, ili asaa mkafuzu katika kheri za duniani na Akhera.
  11. وَإِذَا رَأَوْا۟ تِجَـٰرَةً أَوْ لَهْوًا ٱنفَضُّوٓا۟ إِلَيْهَا وَتَرَكُوكَ قَآئِمًا ۚ قُلْ مَا عِندَ ٱللَّهِ خَيْرٌ مِّنَ ٱللَّهْوِ وَمِنَ ٱلتِّجَـٰرَةِ ۚ وَٱللَّهُ خَيْرُ ٱلرَّٰزِقِينَ۝١١

    Waitha raaw tijaratan aw lahwan infaddoo ilayha watarakooka qaiman qul ma ʿinda Allahi khayrun mina allahwi wamina alttijarati waAllahu khayru alrraziqeena

    Na wanapo iona biashara au pumbao wanayakimbilia hayo na wakakuacha umesimama. Sema: Yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu ni bora kuliko pumbao na biashara. Na Mwenyezi Mungu ni Mbora wa watoa riziki.11

    Maelezo
    [11] Na wakiona bidhaa za biashara, au pumbao lolote hutawanyika kuendea hayo, na wakakuacha wewe umesimama unakhutubu! Waambie: Fadhila na thawabu zilioko kwa Mwenyezi Mungu zina nafuu zaidi kwenu kuliko pumbao na kuliko biashara. Na Mwenyezi Mungu ni Mbora wa wanao toa riziki. Basi itafuteni riziki yake kwa kumt'ii Yeye.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Surat Al-Jumu’a maana yake ni nini?

Al-Jumu’a maana yake ni “Ijumaa”.

Surat Al-Jumu’a iko katika juzuu ya ngapi?

Surat Al-Jumu’a iko katika juzuu ya 28.

Surat Al-Jumu’a ina aya ngapi?

Surat Al-Jumu’a ina aya 11.

Surat Al-Jumu’a ni ya Makka au ya Madina?

Surat Al-Jumu’a ni sura ya Madina.

Surat Al-Jumu’a ni sura ya ngapi katika Qur’ani?

Ni sura ya 62 katika Qur’ani.

Vyanzo

  • Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
  • Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
  • Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
  • Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
  • Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
  • Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.

Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.

Mipangilio ya kusoma

Fonti ya Qur’ani
Ukubwa wa Kiarabu
100%
Ukubwa wa tafsiri
100%
Mandhari

Ongeza kwenye skrini ya kwanza

ReadSurahFungua ReadSurah kutoka skrini ya kwanza, kwa skrini nzima. Sura ulizosoma hufunguka hata bila intaneti.

  1. Katika Safari, gusa kitufe cha kushiriki (Share). Kwenye iPhone mpya kiko kwenye menyu ya •••.
  2. Gusa “Add to Home Screen”. Huenda ukahitaji kusogeza chini.
  3. Gusa “Add”.