سورة الصف

Surat As-Saff kwa Kiswahili

Safu

Msahafu

Mishary Rashid AlafasyPakua MP3Pakua PDF

Surat As-Saff (الصف) ni sura ya 61 katika Qur’ani na ina aya 14. Jina lake lina maana ya “Safu”. Ni sura ya Madina, iliyoteremshwa Madina baada ya Hijra, na iko katika juzuu ya 28.

Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat As-Saff yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.

Surat As-Saff kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

  1. سَبَّحَ لِلَّهِ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَمَا فِى ٱلْأَرْضِ ۖ وَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلْحَكِيمُ۝١

    Sabbaha lillahi ma fee alssamawati wama fee alardi wahuwa alʿazeezu alhakeemu

    Vinamtakasa Mwenyezi Mungu viliomo katika mbingu na katika ardhi. Na Yeye ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima.1

    Maelezo
    [1] Kila kiliomo katika mbingu na kiliomo katika ardhi kinamtakasa Mwenyezi Mungu na kila kisicho kuwa ni laiki yake. Na Yeye peke yake ndiye Mwenye kuvishinda vitu vyote, Mwenye hikima iliyo fika ukomo.
  2. يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لِمَ تَقُولُونَ مَا لَا تَفْعَلُونَ۝٢

    Ya ayyuha allatheena amanoo lima taqooloona ma la tafʿaloona

    Enyi mlio amini! Kwa nini mnasema msiyo yatenda?2

    Maelezo
    [2] Enyi mlio amini! Kwa ajili ya nini mnasema kwa ndimi zenu yasiyo hakikishwa na vitendo vyenu?
  3. كَبُرَ مَقْتًا عِندَ ٱللَّهِ أَن تَقُولُوا۟ مَا لَا تَفْعَلُونَ۝٣

    Kabura maqtan ʿinda Allahi an taqooloo ma la tafʿaloona

    Yanachukiza vikubwa mno kwa Mwenyezi Mungu kuwa mnasema msiyo yatenda.3

    Maelezo
    [3] Mwenyezi Mungu anachukia mno kuwa nyinyi mnasema msiyo yatenda.
  4. إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلَّذِينَ يُقَـٰتِلُونَ فِى سَبِيلِهِۦ صَفًّا كَأَنَّهُم بُنْيَـٰنٌ مَّرْصُوصٌ۝٤

    Inna Allaha yuhibbu allatheena yuqatiloona fee sabeelihi saffan kaannahum bunyanun marsoosun

    Kwa hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wanao pigana katika Njia yake kwa safu kama jengo lilio kamatana.4

    Maelezo
    [4] Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wanao pigania kutaka kulinyanyua Neno lake nao wameshikamana kitu kimoja, kama kwamba wao ni jengo lilio simama imara.
  5. وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِۦ يَـٰقَوْمِ لِمَ تُؤْذُونَنِى وَقَد تَّعْلَمُونَ أَنِّى رَسُولُ ٱللَّهِ إِلَيْكُمْ ۖ فَلَمَّا زَاغُوٓا۟ أَزَاغَ ٱللَّهُ قُلُوبَهُمْ ۚ وَٱللَّهُ لَا يَهْدِى ٱلْقَوْمَ ٱلْفَـٰسِقِينَ۝٥

    Waith qala moosa liqawmihi ya qawmi lima tuthoonanee waqad taʿlamoona annee rasoolu Allahi ilaykum falamma zaghoo azagha Allahu quloobahum waAllahu la yahdee alqawma alfasiqeena

    Na Musa alipo waambia watu wake: Enyi watu wangu! Kwa nini mnaniudhi, nanyi mnajua kuwa hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu niliye tumwa kwenu? Walipo potoka, Mwenyezi Mungu aliziachia nyoyo zao zipotoke. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wapotovu.5

    Maelezo
    [5] Ewe Muhammad! Kumbuka pale Musa alipo waambia watu wake: Enyi watu wangu! Kwa nini mnaniudhi mimi, na hali nyinyi mnajua kwamba hakika mimi ni Mjumbe niliye tumwa na Mwenyezi Mungu nije kwenu? Walipo endelea na kuiacha Haki, Mwenyezi Mungu alizipotoa nyoyo zao zisipokee uwongofu. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu walio toka kwenye ut'iifu wake.
  6. وَإِذْ قَالَ عِيسَى ٱبْنُ مَرْيَمَ يَـٰبَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ إِنِّى رَسُولُ ٱللَّهِ إِلَيْكُم مُّصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَىَّ مِنَ ٱلتَّوْرَىٰةِ وَمُبَشِّرًۢا بِرَسُولٍ يَأْتِى مِنۢ بَعْدِى ٱسْمُهُۥٓ أَحْمَدُ ۖ فَلَمَّا جَآءَهُم بِٱلْبَيِّنَـٰتِ قَالُوا۟ هَـٰذَا سِحْرٌ مُّبِينٌ۝٦

    Waith qala ʿeesa ibnu maryama ya banee israeela innee rasoolu Allahi ilaykum musaddiqan lima bayna yadayya mina alttawrati wamubashshiran birasoolin yatee min baʿdee ismuhu ahmadu falamma jaahum bialbayyinati qaloo hatha sihrun mubeenun

    Na Isa bin Mariamu alipo sema: Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, ninaye thibitisha yaliyo kuwa kabla yangu katika Taurati, na mwenye kubashiria kuja Mtume atakaye kuja baada yangu; jina lake ni Ahmad! Lakini alipo waletea hoja zilizo wazi, walisema: Huu ni uchawi ulio dhaahiri!6

    Maelezo
    [6] Na kumbuka pale Isa bin Mariamu alipo sema: Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume nimetumwa kwenu, mwenye kusadikisha yaliyo nitangulia yaliomo katika Taurati, na kukupeni bishara ya Mtume atakaye kuja baada yangu. Jina lake ni Ahmad. Alipo kuja huyo Mtume aliye bashiriwa kwa Ishara zilizo wazi wakasema: Haya uliyo tujia nayo ni uchawi dhaahiri! (Kwa ushahidi wa kubashiriwa Nabii Muhammad s.a.w. katika vitabu vya Kikristo na Kiyahudi, tazama: Kumbukumbu la Torati 18.19-22, na Injili ya Yohana 16.5-14.)
  7. وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ ٱفْتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ ٱلْكَذِبَ وَهُوَ يُدْعَىٰٓ إِلَى ٱلْإِسْلَـٰمِ ۚ وَٱللَّهُ لَا يَهْدِى ٱلْقَوْمَ ٱلظَّـٰلِمِينَ۝٧

    Waman athlamu mimmani iftara ʿala Allahi alkathiba wahuwa yudʿa ila alislami waAllahu la yahdee alqawma alththalimeena

    Na ni nani mwenye kudhulumu zaidi kuliko yule anaye mzulia Mwenyezi Mungu uwongo, naye anaitwa kwenye Uislamu? Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhaalimu.7

    Maelezo
    [7] Na nani aliye zidi kwa udhaalimu kuliko huyo aliye mzulia uwongo Mwenyezi Mungu, naye anaitwa aingie katika Dini ya Kiislamu, Dini ya haki na kheri? Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu walio shikilia dhulma.
  8. يُرِيدُونَ لِيُطْفِـُٔوا۟ نُورَ ٱللَّهِ بِأَفْوَٰهِهِمْ وَٱللَّهُ مُتِمُّ نُورِهِۦ وَلَوْ كَرِهَ ٱلْكَـٰفِرُونَ۝٨

    Yureedoona liyutfioo noora Allahi biafwahihim waAllahu mutimmu noorihi walaw kariha alkafiroona

    Wanataka kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao. Na Mwenyezi Mungu atakamilisha nuru yake ijapo kuwa makafiri watachukia.8

    Maelezo
    [8] Wana wa Israili wanamzulia Mwenyezi Mungu uwongo, ili ati wapate kuizima nuru ya Dini yake kwa vinywa vyao, kama anaye taka kuizima nuru ya jua kwa kuipulizia. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuikamilisha nuru yake kwa kuitimiza Dini yake hata hao makafiri wakiudhika.
  9. هُوَ ٱلَّذِىٓ أَرْسَلَ رَسُولَهُۥ بِٱلْهُدَىٰ وَدِينِ ٱلْحَقِّ لِيُظْهِرَهُۥ عَلَى ٱلدِّينِ كُلِّهِۦ وَلَوْ كَرِهَ ٱلْمُشْرِكُونَ۝٩

    Huwa allathee arsala rasoolahu bialhuda wadeeni alhaqqi liyuthhirahu ʿala alddeeni kullihi walaw kariha almushrikoona

    Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya haki ili ipate kuzishinda dini zote, ijapo kuwa washirikina watachukia.9

    Maelezo
    [9] Mwenyezi Mungu ndiye aliye mtuma Mtume wake, Muhammad, pamoja na Qur'ani ambayo ni uwongofu kwa watu wote, na Uislamu ambao ndio Dini ya haki, ili autukuze juu ya dini zote, ijapo kuwa washirikina wataudhika.
  10. يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ هَلْ أَدُلُّكُمْ عَلَىٰ تِجَـٰرَةٍ تُنجِيكُم مِّنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ۝١٠

    Ya ayyuha allatheena amanoo hal adullukum ʿala tijaratin tunjeekum min ʿathabin aleemin

    Enyi mlio amini! Nikuonyesheni biashara itakayo kuokoeni na adhabu iliyo chungu?10

    Maelezo
    [10] Enyi mlio amini! Nikuongozeni kwenye biashara kubwa ambayo itakuokoeni na adhabu yenye machungu makali?
  11. تُؤْمِنُونَ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ وَتُجَـٰهِدُونَ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ بِأَمْوَٰلِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ ۚ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ۝١١

    Tuminoona biAllahi warasoolihi watujahidoona fee sabeeli Allahi biamwalikum waanfusikum thalikum khayrun lakum in kuntum taʿlamoona

    Muaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na piganeni Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali yenu na nafsi zenu. Haya ni bora kwenu, ikiwa nyinyi mnajua.11

    Maelezo
    [11] Biashara hii ni kuwa mumuamini Mwenyezi Mungu, na Mtume wake, na mpigane Jihadi katika Njia ya MwenyeziMungu kwa mali zenu na nafsi zenu. Hayo aliyo kuonyesheni ndiyo kheri yenu ikiwa nyinyi mnajua.
  12. يَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ وَيُدْخِلْكُمْ جَنَّـٰتٍ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَـٰرُ وَمَسَـٰكِنَ طَيِّبَةً فِى جَنَّـٰتِ عَدْنٍ ۚ ذَٰلِكَ ٱلْفَوْزُ ٱلْعَظِيمُ۝١٢

    Yaghfir lakum thunoobakum wayudkhilkum jannatin tajree min tahtiha alanharu wamasakina tayyibatan fee jannati ʿadnin thalika alfawzu alʿatheemu

    Atakusameheni dhambi zenu, na atakutieni katika Mabustani yapitiwayo na mito kati yake, na maskani nzuri nzuri katika Bustani za milele. Huko ndio kufuzu kukubwa.12

    Maelezo
    [12] Muamini na mpigane Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, ili akusameheni madhambi yenu, na akutieni katika Bustani zinazo pita kati yake mito, na maskani nzuri katika Bustani za milele. Hayo ndiyo malipo makubwa.
  13. وَأُخْرَىٰ تُحِبُّونَهَا ۖ نَصْرٌ مِّنَ ٱللَّهِ وَفَتْحٌ قَرِيبٌ ۗ وَبَشِّرِ ٱلْمُؤْمِنِينَ۝١٣

    Waokhra tuhibboonaha nasrun mina Allahi wafathun qarreebun wabashshiri almumineena

    Na kinginecho mkipendacho, nacho ni nusura itokayo kwa Mwenyezi Mungu, na ushindi ulio karibu! Na wabashirieni Waumini!13

    Maelezo
    [13] Na neema nyengine ambazo Waumini Mujahidina wanazo zipenda, ni msaada utokao kwa Mwenyezi Mungu na ushindi wa karibu utakao kuleteeni kheri zake. Na ewe Muhammad! Wabashirie Waumini kuwa watapata malipo haya.
  14. يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ كُونُوٓا۟ أَنصَارَ ٱللَّهِ كَمَا قَالَ عِيسَى ٱبْنُ مَرْيَمَ لِلْحَوَارِيِّـۧنَ مَنْ أَنصَارِىٓ إِلَى ٱللَّهِ ۖ قَالَ ٱلْحَوَارِيُّونَ نَحْنُ أَنصَارُ ٱللَّهِ ۖ فَـَٔامَنَت طَّآئِفَةٌ مِّنۢ بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ وَكَفَرَت طَّآئِفَةٌ ۖ فَأَيَّدْنَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ عَلَىٰ عَدُوِّهِمْ فَأَصْبَحُوا۟ ظَـٰهِرِينَ۝١٤

    Ya ayyuha allatheena amanoo koonoo ansara Allahi kama qala ʿeesa ibnu maryama lilhawariyyeena man ansaree ila Allahi qala alhawariyyoona nahnu ansaru Allahi faamanat taifatun min banee israeela wakafarat taifatun faayyadna allatheena amanoo ʿala ʿaduwwihim faasbahoo thahireena

    Enyi mlio amini! Kuweni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu, kama alivyo sema Isa bin Mariamu kuwaambia wanafunzi wake: Nani wasaidizi wangu kwa Mwenyezi Mungu? Wakasema wanafunzi: Sisi ni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu! Basi taifa moja la Wana wa Israili liliamini, na taifa jingine lilikufuru. Basi tukawaunga mkono walio amini dhidi ya maadui zao, wakawa wenye kushinda.14

    Maelezo
    [14] Enyi mlio amini! Kuweni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu anapo kutakeni Mtume wa Mwenyezi Mungu muwe wasaidizi wake. Kama walivyo kuwa masahaba wa Isa wasaidizi wa Mwenyezi Mungu alipo sema: Nani wa kunisaidia mimi kwa Mwenyezi Mungu? Basi kundi moja katika Wana wa Israili lilimuamini Isa, na kundi jengine likamkataa. Sisi tukawapa nguvu walio amini juu ya maadui zao walio kufuru. Basi kwa kuwapa nguvu kwetu wakawa ni wenye kushinda.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Surat As-Saff maana yake ni nini?

As-Saff maana yake ni “Safu”.

Surat As-Saff iko katika juzuu ya ngapi?

Surat As-Saff iko katika juzuu ya 28.

Surat As-Saff ina aya ngapi?

Surat As-Saff ina aya 14.

Surat As-Saff ni ya Makka au ya Madina?

Surat As-Saff ni sura ya Madina.

Surat As-Saff ni sura ya ngapi katika Qur’ani?

Ni sura ya 61 katika Qur’ani.

Vyanzo

  • Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
  • Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
  • Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
  • Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
  • Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
  • Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.

Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.

Mipangilio ya kusoma

Fonti ya Qur’ani
Ukubwa wa Kiarabu
100%
Ukubwa wa tafsiri
100%
Mandhari

Ongeza kwenye skrini ya kwanza

ReadSurahFungua ReadSurah kutoka skrini ya kwanza, kwa skrini nzima. Sura ulizosoma hufunguka hata bila intaneti.

  1. Katika Safari, gusa kitufe cha kushiriki (Share). Kwenye iPhone mpya kiko kwenye menyu ya •••.
  2. Gusa “Add to Home Screen”. Huenda ukahitaji kusogeza chini.
  3. Gusa “Add”.