سورة المنافقون

Surat Al-Munafiqun kwa Kiswahili

Wanafiki

Msahafu

Mishary Rashid AlafasyPakua MP3Pakua PDF

Surat Al-Munafiqun (المنافقون) ni sura ya 63 katika Qur’ani na ina aya 11. Jina lake lina maana ya “Wanafiki”. Ni sura ya Madina, iliyoteremshwa Madina baada ya Hijra, na iko katika juzuu ya 28.

Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat Al-Munafiqun yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.

Surat Al-Munafiqun kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

  1. إِذَا جَآءَكَ ٱلْمُنَـٰفِقُونَ قَالُوا۟ نَشْهَدُ إِنَّكَ لَرَسُولُ ٱللَّهِ ۗ وَٱللَّهُ يَعْلَمُ إِنَّكَ لَرَسُولُهُۥ وَٱللَّهُ يَشْهَدُ إِنَّ ٱلْمُنَـٰفِقِينَ لَكَـٰذِبُونَ۝١

    Itha jaaka almunafiqoona qaloo nashhadu innaka larasoolu Allahi waAllahu yaʿlamu innaka larasooluhu waAllahu yashhadu inna almunafiqeena lakathiboona

    Wanapo kujia wanaafiki husema: Tunashuhudia ya kuwa wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anajua kuwa wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu anashuhudia ya kuwa hakika wanaafiki ni waongo.1

    Maelezo
    [1] Ewe Muhammad! Wanapo kujia wanaafiki, wanasema kwa ndimi zao: Tunashuhudia kuwa hakika wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anajua kwamba wewe ni Mtume wake; na Mwenyezi Mungu anashuhudia kwamba wanaafiki hapana shaka ni waongo katika kujidai kwao wanaamini, kwani hawasadiki katika nyoyo zao.
  2. ٱتَّخَذُوٓا۟ أَيْمَـٰنَهُمْ جُنَّةً فَصَدُّوا۟ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ ۚ إِنَّهُمْ سَآءَ مَا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ۝٢

    Ittakhathoo aymanahum junnatan fasaddoo ʿan sabeeli Allahi innahum saa ma kanoo yaʿmaloona

    Wamevifanya viapo vyao ni kinga, na wao wakajizuia kuifuata Njia ya Mwenyezi Mungu. Hakika ni mabaya kabisa waliyo kuwa wakiyafanya.2

    Maelezo
    [2] Wamezifanya yamini zao za uwongo ni kinga, au ngao za kujikingia ili wasichukuliwe kuwa ni makafiri. Basi wakajizuia wenyewe wasiishike Njia ya Mwenyezi Mungu Iliyo Nyooka. Hakika ni mabaya mno hayo wanayo yatenda ya unaafiki na kujitia imani ya uwongo.
  3. ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ ءَامَنُوا۟ ثُمَّ كَفَرُوا۟ فَطُبِعَ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ فَهُمْ لَا يَفْقَهُونَ۝٣

    Thalika biannahum amanoo thumma kafaroo fatubiʿa ʿala quloobihim fahum la yafqahoona

    Hayo ni kwa sababu ya kuwa waliamini, kisha wakakufuru; kwa hivyo umepigwa muhuri juu ya nyoyo zao. Kwa hivyo hawafahamu lolote.3

    Maelezo
    [3] Hayo waliyo yafanya ndiyo mazoea ya kudhihirisha yasiyo ya kweli, na kuapa yamini za uwongo, kwa sababu hao wameamini kwa ndimi zao, kisha wakakufuru katika nyoyo zao, basi nyoyo zao zimepigwa muhuri kwa ukafiri huu. Hao hawafahamu yepi ya kuwaokoa na adhabu za Mwenyezi Mungu.
  4. ۞ وَإِذَا رَأَيْتَهُمْ تُعْجِبُكَ أَجْسَامُهُمْ ۖ وَإِن يَقُولُوا۟ تَسْمَعْ لِقَوْلِهِمْ ۖ كَأَنَّهُمْ خُشُبٌ مُّسَنَّدَةٌ ۖ يَحْسَبُونَ كُلَّ صَيْحَةٍ عَلَيْهِمْ ۚ هُمُ ٱلْعَدُوُّ فَٱحْذَرْهُمْ ۚ قَـٰتَلَهُمُ ٱللَّهُ ۖ أَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ۝٤

    Waitha raaytahum tuʿjibuka ajsamuhum wain yaqooloo tasmaʿ liqawlihim kaannahum khushubun musannadatun yahsaboona kulla sayhatin ʿalayhim humu alʿaduwwu faihtharhum qatalahumu Allahu anna yufakoona

    Na unapo waona, miili yao inakupendeza, na wakisema, unasikiliza usemi wao. Lakini wao ni kama magogo yaliyo egemezwa. Wao hudhania kila ukelele unao pigwa ni kwa ajili yao. Hao ni maadui; tahadhari nao. Mwenyezi Mungu awaangamizilie mbali! Vipi wanapotoka na haki?4

    Maelezo
    [4] Na ukiwaona miili yao inakupendeza kwa uzuri wao, na wakizungumza unavutika kuwasikiliza kwa utamu wa maneno yao. Kumbe wao juu ya yote hayo nyoyo zao zitupu, hazina Imani ndani yake. Kama magogo yaliyo egemezwa, hayana uhai wowote. Wao hudhania kila linalo zuka basi linawalenga wao, kwa sababu wanaitambua hali yao ya unaafiki. Hao ndio maadui, basi tahadhari nao. Mwenyezi Mungu kesha wafukuza kwenye rehema yake. Vipi wanavyo iacha Haki wakauendea unaafiki wanao ushikilia?
  5. وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْا۟ يَسْتَغْفِرْ لَكُمْ رَسُولُ ٱللَّهِ لَوَّوْا۟ رُءُوسَهُمْ وَرَأَيْتَهُمْ يَصُدُّونَ وَهُم مُّسْتَكْبِرُونَ۝٥

    Waitha qeela lahum taʿalaw yastaghfir lakum rasoolu Allahi lawwaw ruoosahum waraaytahum yasuddoona wahum mustakbiroona

    Na wanapo ambiwa: Njooni ili Mtume wa Mwenyezi Mungu akuombeeni maghfira, huvigeuza vichwa vyao, na unawaona wanageuka nao wamejaa kiburi.5

    Maelezo
    [5] Na wakiambiwa: Jongeeni, apate Mtume wa Mwenyezi Mungu kukuombeeni msamaha, hutikisa vichwa vyao kwa kejeli, na utawaona wanageuka kwa kiburi hawataki kut'ii.
  6. سَوَآءٌ عَلَيْهِمْ أَسْتَغْفَرْتَ لَهُمْ أَمْ لَمْ تَسْتَغْفِرْ لَهُمْ لَن يَغْفِرَ ٱللَّهُ لَهُمْ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَهْدِى ٱلْقَوْمَ ٱلْفَـٰسِقِينَ۝٦

    Sawaon ʿalayhim astaghfarta lahum am lam tastaghfir lahum lan yaghfira Allahu lahum inna Allaha la yahdee alqawma alfasiqeena

    Sawa sawa kwao, ukiwatakia maghfira au hukuwatakia maghfira, Mwenyezi Mungu hatawaghufiria. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wapotovu.6

    Maelezo
    [6] Ni sawa kwa hawa wanaafiki, ukiwaombea msamaha, au ukito waombea. Kwa sababu hao hawauachi unaafiki wao. Basi Mwenyezi Mungu hatawasamehe kabisa. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongozi kuwapeleka kwenye Haki wale wanao kataa kufuata amri yake na kumuamini.
  7. هُمُ ٱلَّذِينَ يَقُولُونَ لَا تُنفِقُوا۟ عَلَىٰ مَنْ عِندَ رَسُولِ ٱللَّهِ حَتَّىٰ يَنفَضُّوا۟ ۗ وَلِلَّهِ خَزَآئِنُ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَلَـٰكِنَّ ٱلْمُنَـٰفِقِينَ لَا يَفْقَهُونَ۝٧

    Humu allatheena yaqooloona la tunfiqoo ʿala man ʿinda rasooli Allahi hatta yanfaddoo walillahi khazainu alssamawati waalardi walakinna almunafiqeena la yafqahoona

    Hao ndio wanao sema: Msitoe mali kwa ajili ya walioko kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, ili waondokelee mbali! Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye khazina za mbingu na ardhi, lakini wanaafiki hawafahamu.7

    Maelezo
    [7] Hao wanaafiki ndio wanao waambia watu wa Madina: Msitoe chochote kuwapa hao Waumini walio na Mtume wa Mwenyezi Mungu ili wapate kumwacha! Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye khazina zote za mbinguni na duniani, na riziki zote ziliomo humo. Lakini wanaafiki hawajui hayo.
  8. يَقُولُونَ لَئِن رَّجَعْنَآ إِلَى ٱلْمَدِينَةِ لَيُخْرِجَنَّ ٱلْأَعَزُّ مِنْهَا ٱلْأَذَلَّ ۚ وَلِلَّهِ ٱلْعِزَّةُ وَلِرَسُولِهِۦ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَلَـٰكِنَّ ٱلْمُنَـٰفِقِينَ لَا يَعْلَمُونَ۝٨

    Yaqooloona lain rajaʿna ila almadeenati layukhrijanna alaʿazzu minha alathalla walillahi alʿizzatu walirasoolihi walilmumineena walakinna almunafiqeena la yaʿlamoona

    Wanasema: Tukirejea Madina mwenye utukufu zaidi bila ya shaka atamfukuza aliye mnyonge. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye utukufu - Yeye, na Mtume wake, na Waumini. Lakini wanaafiki hawajui.8

    Maelezo
    [8] Wanaafiki wanasema kwa kutoa ahadi: Tukirejea Madina hapana shaka kikundi chetu, ambacho ndicho chenye nguvu zaidi, kitakitoa kikundi cha Waumini ambao ni wanyonge! Nguvu anazo Mwenyezi Mungu, na Mtume wake, na Waumini; sio hawa wanao jitia kuahidi. Lakini wanaafiki hawajui kitu.
  9. يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا تُلْهِكُمْ أَمْوَٰلُكُمْ وَلَآ أَوْلَـٰدُكُمْ عَن ذِكْرِ ٱللَّهِ ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْخَـٰسِرُونَ۝٩

    Ya ayyuha allatheena amanoo la tulhikum amwalukum wala awladukum ʿan thikri Allahi waman yafʿal thalika faolaika humu alkhasiroona

    Enyi mlio amini! Yasikusahaulisheni mali yenu, wala watoto wenu, kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Na wenye kufanya hayo ndio walio khasiri.9

    Maelezo
    [9] Enyi mlio msadiki Mwenyezi Mungu na Mtume wake! Yasikuhangaisheni mali yenu, na watoto wenu, hata mkaacha kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kutekekeleza aliyo kuamrisheni kuyafanya. Na wenye kushughulishwa na mali zao na watoto wao wakaacha hayo, basi hao ndio watao kuwa wamekhasiri Siku ya Kiyama.
  10. وَأَنفِقُوا۟ مِن مَّا رَزَقْنَـٰكُم مِّن قَبْلِ أَن يَأْتِىَ أَحَدَكُمُ ٱلْمَوْتُ فَيَقُولَ رَبِّ لَوْلَآ أَخَّرْتَنِىٓ إِلَىٰٓ أَجَلٍ قَرِيبٍ فَأَصَّدَّقَ وَأَكُن مِّنَ ٱلصَّـٰلِحِينَ۝١٠

    Waanfiqoo min ma razaqnakum min qabli an yatiya ahadakumu almawtu fayaqoola rabbi lawla akhkhartanee ila ajalin qareebin faassaddaqa waakun mina alssaliheena

    Na toeni katika tulicho kupeni kabla hayajamfikia mmoja wenu mauti, tena hapo akasema: Mola wangu Mlezi! Huniakhirishi muda kidogo nipate kutoa sadaka, na niwe katika watu wema?10

    Maelezo
    [10] Enyi Waumini! Toeni katika mali tuliyo kuruzukuni upesi upesi kabla mmoja wenu hayajamfikia mauti akasema kwa majuto: Ewe Mola wangu Mlezi! Hebu hunipi muhula kidogo, nikapata kutoa sadaka, na nikawa miongoni wa watu wema watendao vitendo vyema?
  11. وَلَن يُؤَخِّرَ ٱللَّهُ نَفْسًا إِذَا جَآءَ أَجَلُهَا ۚ وَٱللَّهُ خَبِيرٌۢ بِمَا تَعْمَلُونَ۝١١

    Walan yuakhkhira Allahu nafsan itha jaa ajaluha waAllahu khabeerun bima taʿmaloona

    Wala Mwenyezi Mungu hataiakhirisha nafsi yoyote inapo fika ajali yake; na Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda.11

    Maelezo
    [11] Wala Mwenyezi Mungu hampi muhula mtu yeyote ukisha fika wakati wake wa kufa. Na Mwenyezi Mungu ni Mkamilifu wa kujua yote myatendayo, na Yeye atakulipeni kwa hayo.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Surat Al-Munafiqun maana yake ni nini?

Al-Munafiqun maana yake ni “Wanafiki”.

Surat Al-Munafiqun iko katika juzuu ya ngapi?

Surat Al-Munafiqun iko katika juzuu ya 28.

Surat Al-Munafiqun ina aya ngapi?

Surat Al-Munafiqun ina aya 11.

Surat Al-Munafiqun ni ya Makka au ya Madina?

Surat Al-Munafiqun ni sura ya Madina.

Surat Al-Munafiqun ni sura ya ngapi katika Qur’ani?

Ni sura ya 63 katika Qur’ani.

Vyanzo

  • Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
  • Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
  • Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
  • Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
  • Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
  • Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.

Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.

Mipangilio ya kusoma

Fonti ya Qur’ani
Ukubwa wa Kiarabu
100%
Ukubwa wa tafsiri
100%
Mandhari

Ongeza kwenye skrini ya kwanza

ReadSurahFungua ReadSurah kutoka skrini ya kwanza, kwa skrini nzima. Sura ulizosoma hufunguka hata bila intaneti.

  1. Katika Safari, gusa kitufe cha kushiriki (Share). Kwenye iPhone mpya kiko kwenye menyu ya •••.
  2. Gusa “Add to Home Screen”. Huenda ukahitaji kusogeza chini.
  3. Gusa “Add”.