سورة الطلاق

Surat At-Talaq kwa Kiswahili

Talaka

Msahafu

Mishary Rashid AlafasyPakua MP3Pakua PDF

Surat At-Talaq (الطلاق) ni sura ya 65 katika Qur’ani na ina aya 12. Jina lake lina maana ya “Talaka”. Ni sura ya Madina, iliyoteremshwa Madina baada ya Hijra, na iko katika juzuu ya 28.

Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat At-Talaq yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.

Surat At-Talaq kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

  1. يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِىُّ إِذَا طَلَّقْتُمُ ٱلنِّسَآءَ فَطَلِّقُوهُنَّ لِعِدَّتِهِنَّ وَأَحْصُوا۟ ٱلْعِدَّةَ ۖ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ رَبَّكُمْ ۖ لَا تُخْرِجُوهُنَّ مِنۢ بُيُوتِهِنَّ وَلَا يَخْرُجْنَ إِلَّآ أَن يَأْتِينَ بِفَـٰحِشَةٍ مُّبَيِّنَةٍ ۚ وَتِلْكَ حُدُودُ ٱللَّهِ ۚ وَمَن يَتَعَدَّ حُدُودَ ٱللَّهِ فَقَدْ ظَلَمَ نَفْسَهُۥ ۚ لَا تَدْرِى لَعَلَّ ٱللَّهَ يُحْدِثُ بَعْدَ ذَٰلِكَ أَمْرًا۝١

    Ya ayyuha alnnabiyyu itha tallaqtumu alnnisaa fatalliqoohunna liʿiddatihinna waahsoo alʿiddata waittaqoo Allaha rabbakum la tukhrijoohunna min buyootihinna wala yakhrujna illa an yateena bifahishatin mubayyinatin watilka hudoodu Allahi waman yataʿadda hudooda Allahi faqad thalama nafsahu la tadree laʿalla Allaha yuhdithu baʿda thalika amran

    Ewe Nabii! Mtakapo wapa talaka wanawake, basi wapeni talaka katika wakati wa eda zao. Na fanyeni hisabu ya eda. Na mcheni Mwenyezi Mungu, Mola wenu Mlezi. Msiwatoe katika nyumba zao, wala wasitoke wenyewe, ila wakifanya jambo la uchafu ulio wazi. Hiyo ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu, msiikiuke. Na mwenye kuikiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu, basi amejidhulumu nafsi yake. Hujui; labda Mwenyezi Mungu ataleta jambo jengine baada ya haya.1

    Maelezo
    [1] Ewe Nabii! Mkitaka kuwapa talaka wanawake, basi wapeni talaka kwa kukabiliana na eda zao, (yaani wakati wa tahara kabla ya kuwaingilia), na idhibitini eda, na mcheni Mwenyezi Mungu, Mola wenu Mlezi. Msiwatoe watalaka katika nyumba zao walimo pewa talaka. Wasitoke humo ila ikiwa wamefanya kitendo kichafu wazi. Hukumu hizo zilizo tangulia ni alama za Mwenyezi Mungu amezifanya ni sharia kwa waja wake. Na Mwenye kukiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu basi amejidhulumu nafsi yake. Hujui pengine Mwenyezi Mungu labda ataleta jambo usilo litaraji baada ya talaka hiyo, na wakapendana.
  2. فَإِذَا بَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَأَمْسِكُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ أَوْ فَارِقُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ وَأَشْهِدُوا۟ ذَوَىْ عَدْلٍ مِّنكُمْ وَأَقِيمُوا۟ ٱلشَّهَـٰدَةَ لِلَّهِ ۚ ذَٰلِكُمْ يُوعَظُ بِهِۦ مَن كَانَ يُؤْمِنُ بِٱللَّهِ وَٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ ۚ وَمَن يَتَّقِ ٱللَّهَ يَجْعَل لَّهُۥ مَخْرَجًا۝٢

    Faitha balaghna ajalahunna faamsikoohunna bimaʿroofin aw fariqoohunna bimaʿroofin waashhidoo thaway ʿadlin minkum waaqeemoo alshshahadata lillahi thalikum yooʿathu bihi man kana yuminu biAllahi waalyawmi alakhiri waman yattaqi Allaha yajʿal lahu makhrajan

    Basi wanapo fikia muda wao, ima warejeeni muwaweke kwa wema, au farikianeni nao kwa wema. Na mshuhudishe mashahidi wawili waadilifu miongoni mwenu. Na simamisheni ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Hivyo ndivyo anavyo agizwa anaye muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na anaye mcha Mwenyezi Mungu humtengezea njia ya kutokea.2

    Maelezo
    [2] Wakikaribia walio achwa mwisho wa eda zao warejeeni mkae nao kwa wema na ihsani, au farikianeni nao bila ya madhara. Na washuhudisheni kuwarejea na kufarikiana watu wawili waadilifu miongoni mwenu, na toeni ushahidi kwa mujibu wake kwa kumsafia Mwenyezi Mungu. Hayo mliyo amrishwa ndiyo anayo waidhiwa mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na mwenye kumkhofu Mwenyezi Mungu akazishika amri zake na akaepuka makatazo yake atamjaalia njia ya kutokana na kila dhiki.
  3. وَيَرْزُقْهُ مِنْ حَيْثُ لَا يَحْتَسِبُ ۚ وَمَن يَتَوَكَّلْ عَلَى ٱللَّهِ فَهُوَ حَسْبُهُۥٓ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ بَـٰلِغُ أَمْرِهِۦ ۚ قَدْ جَعَلَ ٱللَّهُ لِكُلِّ شَىْءٍ قَدْرًا۝٣

    Wayarzuqhu min haythu la yahtasibu waman yatawakkal ʿala Allahi fahuwa hasbuhu inna Allaha balighu amrihi qad jaʿala Allahu likulli shayin qadran

    Na humruzuku kwa jiha asiyo tazamia. Na anaye mtegemea Mwenyezi Mungu Yeye humtosha. Hakika Mwenyezi Mungu anatimiza amri yake. Mwenyezi Mungu kajaalia kila kitu na kipimo chake.3

    Maelezo
    [3] Na atamtengezea sababu za kupata riziki kwa jiha ambazo hata hazimpitikii katika fikra zake. Na mwenye kumwachia mambo yake yote Mwenyezi Mungu basi Yeye ni Mwenye kumtosha, hana haja ya mwengine. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kutimiza alitakalo, ni Mwenye kutekeleza alipendalo. Amejaalia kila kitu na wakati wake, wala haupitikii, na kipimo hakivuki.
  4. وَٱلَّـٰٓـِٔى يَئِسْنَ مِنَ ٱلْمَحِيضِ مِن نِّسَآئِكُمْ إِنِ ٱرْتَبْتُمْ فَعِدَّتُهُنَّ ثَلَـٰثَةُ أَشْهُرٍ وَٱلَّـٰٓـِٔى لَمْ يَحِضْنَ ۚ وَأُو۟لَـٰتُ ٱلْأَحْمَالِ أَجَلُهُنَّ أَن يَضَعْنَ حَمْلَهُنَّ ۚ وَمَن يَتَّقِ ٱللَّهَ يَجْعَل لَّهُۥ مِنْ أَمْرِهِۦ يُسْرًا۝٤

    Waallaee yaisna mina almaheedi min nisaikum ini irtabtum faʿiddatuhunna thalathatu ashhurin waallaee lam yahidna waolatu alahmali ajaluhunna an yadaʿna hamlahunna waman yattaqi Allaha yajʿal lahu min amrihi yusran

    Na wale walio sita hedhi miongoni mwa wanawake wenu, ikiwa mnayo shaka, basi muda wa eda yao ni miezi mitatu, pamoja na ambao hawapati hedhi. Na wenye mimba eda yao mpaka watakapo zaa. Na anaye mcha Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu humfanyia mambo yake kuwa mepesi.4

    Maelezo
    [4] Na wenye eda ya talaka miongoni mwa wanawake walio sita kuingia myezini kwa utu uzima, kama hawajui wahisabu vipi eda yao, basi eda yao ni miezi mitatu. Na wale ambao hawaingii hedhi kabisa ni kadhaalika. Na wenye mimba, eda yao inakwisha wanapo jifungua. Na mwenye kumcha Mwenyezi Mungu, na akazitimiza hukumu zake Mwenyezi Mungu atamsahilishia mambo yake.
  5. ذَٰلِكَ أَمْرُ ٱللَّهِ أَنزَلَهُۥٓ إِلَيْكُمْ ۚ وَمَن يَتَّقِ ٱللَّهَ يُكَفِّرْ عَنْهُ سَيِّـَٔاتِهِۦ وَيُعْظِمْ لَهُۥٓ أَجْرًا۝٥

    Thalika amru Allahi anzalahu ilaykum waman yattaqi Allaha yukaffir ʿanhu sayyiatihi wayuʿthim lahu ajran

    Hiyo ni amri ya Mwenyezi Mungu amekuteremshieni. Na anaye mcha Mwenyezi Mungu atamfutia maovu yake, na atampa ujira mkubwa.5

    Maelezo
    [5] Sharia hizo ni amri ya Mwenyezi Mungu, si ya mwenginewe. Amekuteremshieni Yeye. Na mwenye kumcha Mwenyezi Mungu kwa kuzihifadhi hukumu zake humfutia makosa yake, na akayafanya makubwa malipo yake.
  6. أَسْكِنُوهُنَّ مِنْ حَيْثُ سَكَنتُم مِّن وُجْدِكُمْ وَلَا تُضَآرُّوهُنَّ لِتُضَيِّقُوا۟ عَلَيْهِنَّ ۚ وَإِن كُنَّ أُو۟لَـٰتِ حَمْلٍ فَأَنفِقُوا۟ عَلَيْهِنَّ حَتَّىٰ يَضَعْنَ حَمْلَهُنَّ ۚ فَإِنْ أَرْضَعْنَ لَكُمْ فَـَٔاتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ ۖ وَأْتَمِرُوا۟ بَيْنَكُم بِمَعْرُوفٍ ۖ وَإِن تَعَاسَرْتُمْ فَسَتُرْضِعُ لَهُۥٓ أُخْرَىٰ۝٦

    Askinoohunna min haythu sakantum min wujdikum wala tudarroohunna litudayyiqoo ʿalayhinna wain kunna olati hamlin faanfiqoo ʿalayhinna hatta yadaʿna hamlahunna fain ardaʿna lakum faatoohunna ojoorahunna watamiroo baynakum bimaʿroofin wain taʿasartum fasaturdiʿu lahu okhra

    Wawekeni humo humo mnamo kaa nyinyi kwa kadiri ya pato lenu, wala msiwaletee madhara kwa kuwadhiki. Na wakiwa wana mimba, wagharimieni mpaka wajifungue. Na wakikunyonyesheeni, basi wapeni ujira wao, na shaurianeni kwa wema. Na mkiona uzito kati yenu, basi amnyonyeshee mwanamke mwengine.6

    Maelezo
    [6] Wawekeni wanawake waliomo edani humo humo katika nyumba zenu, kwa kadiri ya uwezo wenu. Wala msiwaletee madhara yoyote, kuwaletea dhiki katika maskani. Na ikiwa wana mimba basi watoleeni gharama za kuwakimu mpaka wazae. Wakikunyonyesheeni watoto wenu hao watalaka, basi wapeni ujira wao. Na amrishaneni mambo mazuri ya kusameheana na kuacha kutaabishana. Na ikitokea kati yenu dhiki na taabu, basi baba atafute mnyonyeshaji mwengine badala ya mama aliye achwa.
  7. لِيُنفِقْ ذُو سَعَةٍ مِّن سَعَتِهِۦ ۖ وَمَن قُدِرَ عَلَيْهِ رِزْقُهُۥ فَلْيُنفِقْ مِمَّآ ءَاتَىٰهُ ٱللَّهُ ۚ لَا يُكَلِّفُ ٱللَّهُ نَفْسًا إِلَّا مَآ ءَاتَىٰهَا ۚ سَيَجْعَلُ ٱللَّهُ بَعْدَ عُسْرٍ يُسْرًا۝٧

    Liyunfiq thoo saʿatin min saʿatihi waman qudira ʿalayhi rizquhu falyunfiq mimma atahu Allahu la yukallifu Allahu nafsan illa ma ataha sayajʿalu Allahu baʿda ʿusrin yusran

    Mwenye wasaa atoe kadiri ya wasaa wake, na mwenye dhiki atoe katika alicho mpa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu hamkalifishi mtu ila kwa kadiri ya alicho mpa. Mwenyezi Mungu atajaalia baada ya dhiki faraji.7

    Maelezo
    [7] Atoe mwenye nafasi nzuri ya riziki kwa mujibu alicho kunjuliwa na Mwenyezi Mungu, na mwenye dhiki ya pato atoe kwa kadiri alicho mpa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu hamkalifishi mtu ila kwa mujibu alicho mpa. Mwenyezi Mungu atajaalia baada ya dhiki faraji.
  8. وَكَأَيِّن مِّن قَرْيَةٍ عَتَتْ عَنْ أَمْرِ رَبِّهَا وَرُسُلِهِۦ فَحَاسَبْنَـٰهَا حِسَابًا شَدِيدًا وَعَذَّبْنَـٰهَا عَذَابًا نُّكْرًا۝٨

    Wakaayyin min qaryatin ʿatat ʿan amri rabbiha warusulihi fahasabnaha hisaban shadeedan waʿaththabnaha ʿathaban nukran

    Na miji mingapi iliyo vunja amri ya Mola wake Mlezi na Mitume wake, basi tuliihisabia hisabu ngumu na tukaiadhibu kwa adhabu kali.8

    Maelezo
    [8] Na miji mingi ambayo watu wake wamefanya ujabari na wakapuuza amri ya Mola wao Mlezi na Mitume wake, tukaihisabia kwa hisabu kali kwa kuchungua kila walilo litenda na kujadiliana nao, na tukawaadhibu adhabu ya kuchusha iliyo mbaya, wakagugumia malipo maovu ya mambo yao. Na ukawa mwisho wa mambo yao ni kukhasiri kukubwa mno.
  9. فَذَاقَتْ وَبَالَ أَمْرِهَا وَكَانَ عَـٰقِبَةُ أَمْرِهَا خُسْرًا۝٩

    Fathaqat wabala amriha wakana ʿaqibatu amriha khusran

    Basi ikauonja ubaya wa mambo yake; na mwisho wa mambo yao ilikuwa khasara.9

    Maelezo
    [9] Wakagugumia malipo maovu ya mambo yao. Na ukawa mwisho wa mambo yao ni kukhasiri kukubwa mno.
  10. أَعَدَّ ٱللَّهُ لَهُمْ عَذَابًا شَدِيدًا ۖ فَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ يَـٰٓأُو۟لِى ٱلْأَلْبَـٰبِ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ۚ قَدْ أَنزَلَ ٱللَّهُ إِلَيْكُمْ ذِكْرًا۝١٠

    aʿadda Allahu lahum ʿathaban shadeedan faittaqoo Allaha ya olee alalbabi allatheena amanoo qad anzala Allahu ilaykum thikran

    Mwenyezi Mungu aliwaandalia adhabu kali. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, enyi wenye akili, mlio amini! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteremshieni Ukumbusho,10

    Maelezo
    [10] Mwenyezi Mungu amewaandalia watu wa miji ya watu walio fanya ujabari adhabu ya mwisho wa ukali. Basi tahadharini na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, enyi wenye akili sawa, ambao mnasifika kwa Imani. Amekuteremshieni mtu mwenye utukufu na cheo,
  11. رَّسُولًا يَتْلُوا۟ عَلَيْكُمْ ءَايَـٰتِ ٱللَّهِ مُبَيِّنَـٰتٍ لِّيُخْرِجَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ مِنَ ٱلظُّلُمَـٰتِ إِلَى ٱلنُّورِ ۚ وَمَن يُؤْمِنۢ بِٱللَّهِ وَيَعْمَلْ صَـٰلِحًا يُدْخِلْهُ جَنَّـٰتٍ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَـٰرُ خَـٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدًا ۖ قَدْ أَحْسَنَ ٱللَّهُ لَهُۥ رِزْقًا۝١١

    Rasoolan yatloo ʿalaykum ayati Allahi mubayyinatin liyukhrija allatheena amanoo waʿamiloo alssalihati mina alththulumati ila alnnoori waman yumin biAllahi wayaʿmal salihan yudkhilhu jannatin tajree min tahtiha alanharu khalideena feeha abadan qad ahsana Allahu lahu rizqan

    Mtume anaye kusomeeni Aya za Mwenyezi Mungu zinazo bainisha, ili kuwatoa walio amini na wakatenda mema kutoka gizani kuwapeleka kwenye nuru. Na mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu, na akatenda mema, atamwingiza katika Bustani zipitazo mito kati yake, wadumu humo milele. Mwenyezi Mungu amekwisha mpa riziki nzuri.11

    Maelezo
    [11] Mtume anaye kusomeeni Aya za Mwenyezi Mungu zenye kukubainishieni baina yaliyo kweli na ya uwongo, ili awatoe walio amini na wakatenda mema kutoka kwenye giza la upotovu kwenda kwenye mwangaza wa hidaya. Na mwenye kumsadiki Mwenyezi Mungu, na akatenda vitendo vyema atamtia katika Bustani zinazo pita kati yake mito. Watakaa humo milele. Mwenyezi Mungu kamfanyia ihsani Muumini mwema kwa kumpa riziki iliyo njema.
  12. ٱللَّهُ ٱلَّذِى خَلَقَ سَبْعَ سَمَـٰوَٰتٍ وَمِنَ ٱلْأَرْضِ مِثْلَهُنَّ يَتَنَزَّلُ ٱلْأَمْرُ بَيْنَهُنَّ لِتَعْلَمُوٓا۟ أَنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ وَأَنَّ ٱللَّهَ قَدْ أَحَاطَ بِكُلِّ شَىْءٍ عِلْمًۢا۝١٢

    Allahu allathee khalaqa sabʿa samawatin wamina alardi mithlahunna yatanazzalu alamru baynahunna litaʿlamoo anna Allaha ʿala kulli shayin qadeerun waanna Allaha qad ahata bikulli shayin ʿilman

    Mwenyezi Mungu ni yule ambaye ameziumba mbingu saba, na ardhi kwa mfano wa hizo. Amri zake zinashuka baina yao, ili mjue kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu, na kwamba Mwenyezi Mungu amekizunguka kila kitu kukijua vilivyo kwa ilimu yake.12

    Maelezo
    [12] Mwenyezi Mungu peke yake ndiye aliye umba mbingu saba, na ardhi mfano wa hizo. Amri yake inapita kote, ili mjue kwamba Mwenyezi Mungu ni mtimilivu wa uweza, na kwamba Mwenyezi Mungu amevizunguka vitu vyote kwa ujuzi wake.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Surat At-Talaq maana yake ni nini?

At-Talaq maana yake ni “Talaka”.

Surat At-Talaq iko katika juzuu ya ngapi?

Surat At-Talaq iko katika juzuu ya 28.

Surat At-Talaq ina aya ngapi?

Surat At-Talaq ina aya 12.

Surat At-Talaq ni ya Makka au ya Madina?

Surat At-Talaq ni sura ya Madina.

Surat At-Talaq ni sura ya ngapi katika Qur’ani?

Ni sura ya 65 katika Qur’ani.

Vyanzo

  • Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
  • Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
  • Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
  • Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
  • Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
  • Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.

Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.

Mipangilio ya kusoma

Fonti ya Qur’ani
Ukubwa wa Kiarabu
100%
Ukubwa wa tafsiri
100%
Mandhari

Ongeza kwenye skrini ya kwanza

ReadSurahFungua ReadSurah kutoka skrini ya kwanza, kwa skrini nzima. Sura ulizosoma hufunguka hata bila intaneti.

  1. Katika Safari, gusa kitufe cha kushiriki (Share). Kwenye iPhone mpya kiko kwenye menyu ya •••.
  2. Gusa “Add to Home Screen”. Huenda ukahitaji kusogeza chini.
  3. Gusa “Add”.