سورة التحريم

Surat At-Tahrim kwa Kiswahili

Kuharamisha

Msahafu

Mishary Rashid AlafasyPakua MP3Pakua PDF

Surat At-Tahrim (التحريم) ni sura ya 66 katika Qur’ani na ina aya 12. Jina lake lina maana ya “Kuharamisha”. Ni sura ya Madina, iliyoteremshwa Madina baada ya Hijra, na iko katika juzuu ya 28.

Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat At-Tahrim yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.

Surat At-Tahrim kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

  1. يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِىُّ لِمَ تُحَرِّمُ مَآ أَحَلَّ ٱللَّهُ لَكَ ۖ تَبْتَغِى مَرْضَاتَ أَزْوَٰجِكَ ۚ وَٱللَّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ۝١

    Ya ayyuha alnnabiyyu lima tuharrimu ma ahalla Allahu laka tabtaghee mardata azwajika waAllahu ghafoorun raheemun

    Ewe Nabii! Kwa nini unaharimisha alicho kuhalilishia Mwenyezi Mungu? Unatafuta kuwaridhi wake zako. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.1

    Maelezo
    [1] Ewe Nabii! Kwa nini unajikhini nafsi yako alicho kuhalalishia Mwenyezi Mungu? Unataka kuwaridhi wakezo, na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mkunjufu wa kurehemu.
  2. قَدْ فَرَضَ ٱللَّهُ لَكُمْ تَحِلَّةَ أَيْمَـٰنِكُمْ ۚ وَٱللَّهُ مَوْلَىٰكُمْ ۖ وَهُوَ ٱلْعَلِيمُ ٱلْحَكِيمُ۝٢

    Qad farada Allahu lakum tahillata aymanikum waAllahu mawlakum wahuwa alʿaleemu alhakeemu

    Hakika Mwenyezi Mungu kakupeni Sharia ya kufungua viapo vyenu, na Mwenyezi Mungu ni Mola wenu. Na Yeye ni Mwenye kujua, Mwenye hikima.2

    Maelezo
    [2] Amekuwekeeni Sharia ya kuondoa viapo vyenu kwa kafara. Na Mwenyezi Mungu ni Bwana wenu, Mwenye kutawala mambo yenu, na Yeye ni Mtimilivu wa ujuzi, basi anakuwekeeni Sharia zenye kheri yenu, naye ni Mwenye hikima katika kuweka Sharia zake.
  3. وَإِذْ أَسَرَّ ٱلنَّبِىُّ إِلَىٰ بَعْضِ أَزْوَٰجِهِۦ حَدِيثًا فَلَمَّا نَبَّأَتْ بِهِۦ وَأَظْهَرَهُ ٱللَّهُ عَلَيْهِ عَرَّفَ بَعْضَهُۥ وَأَعْرَضَ عَنۢ بَعْضٍ ۖ فَلَمَّا نَبَّأَهَا بِهِۦ قَالَتْ مَنْ أَنۢبَأَكَ هَـٰذَا ۖ قَالَ نَبَّأَنِىَ ٱلْعَلِيمُ ٱلْخَبِيرُ۝٣

    Waith asarra alnnabiyyu ila baʿdi azwajihi hadeethan falamma nabbaat bihi waathharahu Allahu ʿalayhi ʿarrafa baʿdahu waaʿrada ʿan baʿdin falamma nabbaaha bihi qalat man anbaaka hatha qala nabbaaniya alʿaleemu alkhabeeru

    Na Nabii alipo mwambia mmoja wa wake zake jambo la siri. Basi alipo litangaza yule mke, na Mwenyezi Mungu akamdhihirishia Mtume, alimjuvya sehemu na akaacha sehemu nyengine. Alipo mwambia hayo, huyo mke akasema: Nani aliye kwambia haya? Mtume akasema: Kaniambia Mjuzi Mwenye khabari zote!3

    Maelezo
    [3] Na taja pale Nabii alipo msimulia jambo kwa siri mmoja katika wake zake, na alipo ifichua. Na Mwenyezi Mungu akamjuvya Nabii wake kuwa imefichuliwa. Akamjuvya baadhi, na akamzuilia - kwa staha - baadhi nyengine. Alipo mjuvya, akasema yule mke: Nani aliye kwambia haya? Akasema Nabii: Ameniambia Mwenye kujua kila kitu, asiye fichika kitu.
  4. إِن تَتُوبَآ إِلَى ٱللَّهِ فَقَدْ صَغَتْ قُلُوبُكُمَا ۖ وَإِن تَظَـٰهَرَا عَلَيْهِ فَإِنَّ ٱللَّهَ هُوَ مَوْلَىٰهُ وَجِبْرِيلُ وَصَـٰلِحُ ٱلْمُؤْمِنِينَ ۖ وَٱلْمَلَـٰٓئِكَةُ بَعْدَ ذَٰلِكَ ظَهِيرٌ۝٤

    In tatooba ila Allahi faqad saghat quloobukuma wain tathahara ʿalayhi fainna Allaha huwa mawlahu wajibreelu wasalihu almumineena waalmalaikatu baʿda thalika thaheerun

    Kama nyinyi wawili hamkutubia kwa Mwenyezi Mungu, basi nyoyo zenu zimekwisha elekea huko. Na mkisaidiana dhidi yake (Mtume), basi hakika Mwenyezi Mungu ndiye kipenzi chake, na Jibrili, na Waumini wema, na zaidi ya hayo Malaika pia watasaidia.4

    Maelezo
    [4] Mkirejea nyinyi wawili kwa Mwenyezi Mungu nanyi mmejuta basi itakuwa mmefanya waajibu wenu wa kutubu, kwa sababu nyoyo zenu zilikuwa zimeacha jambo analo lipenda Mtume wa Mwenyezi Mungu, nalo ni kuweka siri. Na ikiwa mtasaidiana kinyume chake kwa mambo ya kumuudhi, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Msaidizi wake, na Jibrili, na Waumini wanao sifika kwa wema, na Malaika baada ya msaada wa Mwenyezi Mungu nao ni wenye kumsaidia.
  5. عَسَىٰ رَبُّهُۥٓ إِن طَلَّقَكُنَّ أَن يُبْدِلَهُۥٓ أَزْوَٰجًا خَيْرًا مِّنكُنَّ مُسْلِمَـٰتٍ مُّؤْمِنَـٰتٍ قَـٰنِتَـٰتٍ تَـٰٓئِبَـٰتٍ عَـٰبِدَٰتٍ سَـٰٓئِحَـٰتٍ ثَيِّبَـٰتٍ وَأَبْكَارًا۝٥

    ʿAsa rabbuhu in tallaqakunna an yubdilahu azwajan khayran minkunna muslimatin muminatin qanitatin taibatin ʿabidatin saihatin thayyibatin waabkaran

    Asaa Mola wake Mlezi, akikupeni talaka, akampa wake wengine badala yenu nyinyi, walio bora kuliko nyinyi, wanynyekevu, Waumini, wat'awa, walio tubu, wenye kushika ibada, wafanyao kheri, wajane na wanawari.5

    Maelezo
    [5] Asaa Mola wake Mlezi akikuacheni, enyi wakeze, atamwoza badala yenu wake wengine walio wanyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu kwa ut'iifu, wenye kusadiki kwa nyoyo zao, wanyonge mbele ya Mwenyezi Mungu, wenye kurejea kwa Mwenyezi Mungu kwa toba, wenye kumuabudu kwa kujidhalilisha kwake, wendao kila njia za ut'iifu kwa Mwenyezi Mungu, wajane na bikra.
  6. يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ قُوٓا۟ أَنفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَارًا وَقُودُهَا ٱلنَّاسُ وَٱلْحِجَارَةُ عَلَيْهَا مَلَـٰٓئِكَةٌ غِلَاظٌ شِدَادٌ لَّا يَعْصُونَ ٱللَّهَ مَآ أَمَرَهُمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ۝٦

    Ya ayyuha allatheena amanoo qoo anfusakum waahleekum naran waqooduha alnnasu waalhijaratu ʿalayha malaikatun ghilathun shidadun la yaʿsoona Allaha ma amarahum wayafʿaloona ma yumaroona

    Enyi mlio amini! Jilindeni nafsi zenu na ahali zenu na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe. Wanausimamia Malaika wakali, wenye nguvu, hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa anayo waamrisha, na wanatenda wanayo amrishwa.6

    Maelezo
    [6] Enyi mlio amini! Jihifadhini nafsi zenu na ahali zenu na Moto, ambao kuni zake ni watu na mawe. Wanao simamia kazi yake na kuwaadhibu waliomo humo ni Malaika wakali, na wana nguvu katika muamala wao. Na wao hutekeleza lile wanalo amrishwa, wala hawakawilishi.
  7. يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لَا تَعْتَذِرُوا۟ ٱلْيَوْمَ ۖ إِنَّمَا تُجْزَوْنَ مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ۝٧

    Ya ayyuha allatheena kafaroo la taʿtathiroo alyawma innama tujzawna ma kuntum taʿmaloona

    Enyi mlio kufuru! Msilete udhuru leo. Hakika mnalipwa mliyo kuwa mkiyatenda.7

    Maelezo
    [7] Wataambiwa makafiri Siku ya Kiyama: Msitafute udhuru leo! Hapana shaka mnalipwa mliyo kuwa mkiyatenda.
  8. يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ تُوبُوٓا۟ إِلَى ٱللَّهِ تَوْبَةً نَّصُوحًا عَسَىٰ رَبُّكُمْ أَن يُكَفِّرَ عَنكُمْ سَيِّـَٔاتِكُمْ وَيُدْخِلَكُمْ جَنَّـٰتٍ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَـٰرُ يَوْمَ لَا يُخْزِى ٱللَّهُ ٱلنَّبِىَّ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ مَعَهُۥ ۖ نُورُهُمْ يَسْعَىٰ بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَبِأَيْمَـٰنِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَآ أَتْمِمْ لَنَا نُورَنَا وَٱغْفِرْ لَنَآ ۖ إِنَّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ۝٨

    Ya ayyuha allatheena amanoo tooboo ila Allahi tawbatan nasoohan ʿasa rabbukum an yukaffira ʿankum sayyiatikum wayudkhilakum jannatin tajree min tahtiha alanharu yawma la yukhzee Allahu alnnabiyya waallatheena amanoo maʿahu nooruhum yasʿa bayna aydeehim wabiaymanihim yaqooloona rabbana atmim lana noorana waighfir lana innaka ʿala kulli shayin qadeerun

    Enyi mlio amini! Tubuni kwa Mwenyezi Mungu toba iliyo ya kweli! Asaa Mola wenu Mlezi akakufutieni maovu yenu na akakuingizeni katika Pepo zipitazo mito kati yake, siku ambayo Mwenyezi Mungu hatamdhalilisha Nabii na walio amini pamoja naye. Nuru yao inakwenda mbele yao na pande zao za kulia, na huku wanasema: Mola wetu Mlezi! Tutimilizie nuru yetu, na utughufirie! Hakika Wewe ni Mwenye uweza juu ya kila kitu.8

    Maelezo
    [8] Enyi mlio amini! Rejeeni kwa Mwenyezi Mungu, muache madhambi yenu, mrejee kweli kweli kwa ikhlasi. Asaa Mola wenu Mlezi akakufutieni maovu yenu, na akakutieni Peponi kwenye kupita mito chini ya majumba yake na miti yake, Siku atakayo inyanyua Mwenyezi Mungu hadhi ya Nabii na walio amini pamoja naye. Nuru yao hao itakuwa inakwenda mbele yao, nayo itakuwa kuliani mwao, nao watakuwa wakisema kwa kujikaribisha kwa Mwenyezi Mungu: Ewe Bwana wetu, Mwenye kumiliki mambo yetu! Tutimizie nuru yetu, mpaka tuongoke kufikia Peponi. Na tusamehe dhambi zetu. Hakika Wewe ni Mtimilivu wa uweza juu ya kila kitu.
  9. يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِىُّ جَـٰهِدِ ٱلْكُفَّارَ وَٱلْمُنَـٰفِقِينَ وَٱغْلُظْ عَلَيْهِمْ ۚ وَمَأْوَىٰهُمْ جَهَنَّمُ ۖ وَبِئْسَ ٱلْمَصِيرُ۝٩

    Ya ayyuha alnnabiyyu jahidi alkuffara waalmunafiqeena waoghluth ʿalayhim wamawahum jahannamu wabisa almaseeru

    Ewe Nabii! Pambana na makafiri na wanaafiki, na kuwa mgumu kwao! Na makaazi yao ni Jahannamu. Na hayo ni marejeo mabaya.9

    Maelezo
    [9] Ewe Nabii! Pambana kwa Jihadi na hao walio tangaza ukafiri wao, na wanaafiki walio uficha ukafiri wao, kwa kila unacho kimiliki, nguvu na hoja. Na kuwa mkali juu ya makundi yote mawili hayo katika Jihadi yako. Na makaazi ya hao ni Jahannamu. Na marejeo maovu ni hayo marejeo yao!
  10. ضَرَبَ ٱللَّهُ مَثَلًا لِّلَّذِينَ كَفَرُوا۟ ٱمْرَأَتَ نُوحٍ وَٱمْرَأَتَ لُوطٍ ۖ كَانَتَا تَحْتَ عَبْدَيْنِ مِنْ عِبَادِنَا صَـٰلِحَيْنِ فَخَانَتَاهُمَا فَلَمْ يُغْنِيَا عَنْهُمَا مِنَ ٱللَّهِ شَيْـًٔا وَقِيلَ ٱدْخُلَا ٱلنَّارَ مَعَ ٱلدَّٰخِلِينَ۝١٠

    Daraba Allahu mathalan lillatheena kafaroo imraata noohin waimraata lootin kanata tahta ʿabdayni min ʿibadina salihayni fakhanatahuma falam yughniya ʿanhuma mina Allahi shayan waqeela odkhula alnnara maʿa alddakhileena

    Mwenyezi Mungu amewapigia mfano walio kufuru: mke wa Nuhu na mke wa Lut'i. Walikuwa chini ya waja wetu wema wawili miongoni mwa waja wetu. Lakini wakawakhuni waume zao, nao wasiwafae kitu. Na ikasemwa: Ingieni Motoni pamoja na wanao ingia!10

    Maelezo
    [10] Mwenyezi Mungu ametaja hali ya ajabu inayo juulikana kuwa ni hali zinazo fanana kwa wanao kufuru. Nayo ni hali ya mke wa Nuhu na mke wa Lut'i. Hao walikuwa chini ya ulinzi wa waja wawili katika waja wema. Nao wakawakhuni kwa kupanga njama dhidi yao, na kufichua siri zao kwenda wambia kaumu zao. Na waja wema wawili hawakuweza kuwakinga wake zao kwa lolote katika adhabu ya Mwenyezi Mungu. Na wakaambiwa hao wake wawili walipo angamizwa: Ingieni Motoni pamoja na wanao ingia!
  11. وَضَرَبَ ٱللَّهُ مَثَلًا لِّلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ٱمْرَأَتَ فِرْعَوْنَ إِذْ قَالَتْ رَبِّ ٱبْنِ لِى عِندَكَ بَيْتًا فِى ٱلْجَنَّةِ وَنَجِّنِى مِن فِرْعَوْنَ وَعَمَلِهِۦ وَنَجِّنِى مِنَ ٱلْقَوْمِ ٱلظَّـٰلِمِينَ۝١١

    Wadaraba Allahu mathalan lillatheena amanoo imraata firʿawna ith qalat rabbi ibni lee ʿindaka baytan fee aljannati wanajjinee min firʿawna waʿamalihi wanajjinee mina alqawmi alththalimeena

    Na Mwenyezi Mungu amewapigia mfano walio amini - mkewe Firauni, alipo sema: Mola wangu Mlezi! Nijengee kwako nyumba Peponi, na uniokoe na Firauni na vitendo vyake, na uniokoe na watu madhaalimu.11

    Maelezo
    [11] Na Mwenyezi Mungu amepiga mfano kwa Waumini kisa cha mke wa Firauni alipo sema: Mola wangu Mlezi! Nijengee kwako nyumba karibu na rehema yako Peponi, na uniokoe na utawala wa Firauni na vitendo vyake vilivyo pita mipaka katika dhulma, na uniokoe na kaumu ya wanao fanya uadui!
  12. وَمَرْيَمَ ٱبْنَتَ عِمْرَٰنَ ٱلَّتِىٓ أَحْصَنَتْ فَرْجَهَا فَنَفَخْنَا فِيهِ مِن رُّوحِنَا وَصَدَّقَتْ بِكَلِمَـٰتِ رَبِّهَا وَكُتُبِهِۦ وَكَانَتْ مِنَ ٱلْقَـٰنِتِينَ۝١٢

    Wamaryama ibnata ʿimrana allatee ahsanat farjaha fanafakhna feehi min roohina wasaddaqat bikalimati rabbiha wakutubihi wakanat mina alqaniteena

    Na Mariamu binti wa Imrani, aliye linda ubikira wake, na tukampulizia humo kutoka roho yetu, na akayasadiki maneno ya Mola wake Mlezi na Vitabu vyake, na alikuwa miongoni mwa wat'iifu.12

    Maelezo
    [12] Na Mwenyezi Mungu amewapigia Waumini mfano wa Mariamu binti wa Imrani, ambaye amehifadhi utupu wake, tukampulizia humo katika roho yetu, akashika mimba ya Isa. Naye akayasadiki maneno ya Mwenyezi Mungu, nayo ni amri zake, na makatazo yake, na Vitabu vilivyo teremshwa juu ya Mitume wake. Na yeye alikuwa miongoni mwa idadi walio dumu juu ya ut'iifu wa Mwenyezi Mungu. (Huku kupuliziwa Mariamu roho ya Mwenyezi Mungu si kiroja, kwani wanaadamu wote wamepuliziwa kadhaalika. Soma Surat Al-H'ijr Aya 28-29 inapo simuliwa alipo umbwa mtu na akapuliziwa kutokana na roho ya Mwenyezi Mungu.)

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Surat At-Tahrim maana yake ni nini?

At-Tahrim maana yake ni “Kuharamisha”.

Surat At-Tahrim iko katika juzuu ya ngapi?

Surat At-Tahrim iko katika juzuu ya 28.

Surat At-Tahrim ina aya ngapi?

Surat At-Tahrim ina aya 12.

Surat At-Tahrim ni ya Makka au ya Madina?

Surat At-Tahrim ni sura ya Madina.

Surat At-Tahrim ni sura ya ngapi katika Qur’ani?

Ni sura ya 66 katika Qur’ani.

Vyanzo

  • Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
  • Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
  • Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
  • Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
  • Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
  • Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.

Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.

Mipangilio ya kusoma

Fonti ya Qur’ani
Ukubwa wa Kiarabu
100%
Ukubwa wa tafsiri
100%
Mandhari

Ongeza kwenye skrini ya kwanza

ReadSurahFungua ReadSurah kutoka skrini ya kwanza, kwa skrini nzima. Sura ulizosoma hufunguka hata bila intaneti.

  1. Katika Safari, gusa kitufe cha kushiriki (Share). Kwenye iPhone mpya kiko kwenye menyu ya •••.
  2. Gusa “Add to Home Screen”. Huenda ukahitaji kusogeza chini.
  3. Gusa “Add”.