سورة النمل

Surat An-Naml kwa Kiswahili

Wadudu Chungu

Msahafu

Mishary Rashid AlafasyPakua MP3Pakua PDF

Surat An-Naml (النمل) ni sura ya 27 katika Qur’ani na ina aya 93. Jina lake lina maana ya “Wadudu Chungu”. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na inaenea katika juzuu za 19 na 20.

Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat An-Naml yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.

Surat An-Naml kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

  1. طسٓ ۚ تِلْكَ ءَايَـٰتُ ٱلْقُرْءَانِ وَكِتَابٍ مُّبِينٍ۝١

    Taseen tilka ayatu alqurani wakitabin mubeenin

    T'aa Siin. (T'.S.), Hizi ni Aya za Qur'ani na Kitabu kinacho bainisha; .1

    Maelezo
    [1] T'aa Siin, (T' na S) harufi mbili za kutamkwa, ni harufi za alifbete, ndizo zimeanzia Sura hii, ili kunabihisha siri ya muujiza wa Qur'ani pamoja na kuashiria kuwa imeundwa kwa jinsi ya harufi hizi hizi mnazo zitumia katika kusema, na pia kuzindua akili ziisikilize hii Qur'ani inapo somwa. Hizi Aya zilizo teremka kwa kusomwa, na ni Kitabu chenye kubainisha mambo yaliyo kuja ndani yake.
  2. هُدًى وَبُشْرَىٰ لِلْمُؤْمِنِينَ۝٢

    Hudan wabushra lilmumineena

    Uwongofu na bishara kwa Waumini!2

    Maelezo
    [2] Na hii Qur'ani ni Uwongofu wa kuwaahidi Waumini waifuate njia ya kheri, na kufuzu duniani na Akhera, na inawabashiria kuwa watapata malipo mazuri.
  3. ٱلَّذِينَ يُقِيمُونَ ٱلصَّلَوٰةَ وَيُؤْتُونَ ٱلزَّكَوٰةَ وَهُم بِٱلْـَٔاخِرَةِ هُمْ يُوقِنُونَ۝٣

    Allatheena yuqeemoona alssalata wayutoona alzzakata wahum bialakhirati hum yooqinoona

    Ambao wanashika Swala, na wanatoa Zaka, na Akhera wana yakini nayo.3

    Maelezo
    [3] Waumini hao ndio wanao ishika Swala kwa unyenyekevu na kutimiliza nguzo, na wanatoa Zaka kwa nyakati zake, nao wana yakini ya maisha ya baadaye Akhera, na yatayo kuwa huko ya adhabu na thawabu.
  4. إِنَّ ٱلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِٱلْـَٔاخِرَةِ زَيَّنَّا لَهُمْ أَعْمَـٰلَهُمْ فَهُمْ يَعْمَهُونَ۝٤

    Inna allatheena la yuminoona bialakhirati zayyanna lahum aʿmalahum fahum yaʿmahoona

    Kwa hakika wale wasio iamini Akhera tumewapambia vitendo vyao, kwa hivyo wanatangatanga ovyo.4

    Maelezo
    [4] Hakika wale ambao hawaiamini Akhera, Sisi tumewapambia vitendo vyao kwa kuwaumbia matamanio ndani yake. Kwa hivyo wao wanababaika humo katika upotovu wao.
  5. أُو۟لَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ لَهُمْ سُوٓءُ ٱلْعَذَابِ وَهُمْ فِى ٱلْـَٔاخِرَةِ هُمُ ٱلْأَخْسَرُونَ۝٥

    Olaika allatheena lahum sooo alʿathabi wahum fee alakhirati humu alakhsaroona

    Hao ndio watapata adhabu mbaya kabisa, na hao katika Akhera ndio watapata khasara zaidi.5

    Maelezo
    [5] Hao ndio watapata adhabu mbaya kabisa, na Akhera ndio watakuwa khasarani kushinda wote.
  6. وَإِنَّكَ لَتُلَقَّى ٱلْقُرْءَانَ مِن لَّدُنْ حَكِيمٍ عَلِيمٍ۝٦

    Wainnaka latulaqqa alqurana min ladun hakeemin ʿaleemin

    Na hakika wewe unafundishwa Qur'ani inayo tokana kwake Mwenye hikima Mwenye kujua.6

    Maelezo
    [6] Ewe Nabii! Wewe unapokea Qur'ani hii unayo teremshiwa kutokana na Yeye ambaye hapana anaye mkaribia kwa hikima yake, naye anajua kila kitu.
  7. إِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِأَهْلِهِۦٓ إِنِّىٓ ءَانَسْتُ نَارًا سَـَٔاتِيكُم مِّنْهَا بِخَبَرٍ أَوْ ءَاتِيكُم بِشِهَابٍ قَبَسٍ لَّعَلَّكُمْ تَصْطَلُونَ۝٧

    Ith qala moosa liahlihi innee anastu naran saateekum minha bikhabarin aw ateekum bishihabin qabasin laʿallakum tastaloona

    (Kumbuka) Musa alipo waambia ahali zake: Hakika nimeona moto, nitakwenda nikuleteeni khabari, au nitakuleteeni kijinga kinacho waka ili mpate kuota moto.7

    Maelezo
    [7] Kumbuka pale Musa alipo mwambia mkewe na walio pamoja naye na yeye ndio anarejea Misri: Mimi nimeona moto. Nitakwenda kuleteeni khabari ya njia, au nitapata kijinga cha moto, kitacho kufaeni kwa kuota moto kwa hii baridi.
  8. فَلَمَّا جَآءَهَا نُودِىَ أَنۢ بُورِكَ مَن فِى ٱلنَّارِ وَمَنْ حَوْلَهَا وَسُبْحَـٰنَ ٱللَّهِ رَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ۝٨

    Falamma jaaha noodiya an boorika man fee alnnari waman hawlaha wasubhana Allahi rabbi alʿalameena

    Basi alipo fika ilinadiwa: Amebarikiwa aliomo katika moto huu na walioko pembezoni mwake. Na ametakasika Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.8

    Maelezo
    [8] Alipo fika huko paliitwa: Wamebarikiwa waliomo katika moto huu na walioko pembezoni mwake, yaani karibu yake. Nao ni Malaika na Musa. Na Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote ametakasika na kila kisicho kuwa laiki naye.
  9. يَـٰمُوسَىٰٓ إِنَّهُۥٓ أَنَا ٱللَّهُ ٱلْعَزِيزُ ٱلْحَكِيمُ۝٩

    Ya moosa innahu ana Allahu alʿazeezu alhakeemu

    Ewe Musa! Hakika Mimi ndiye Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye hikima.9

    Maelezo
    [9] Ewe Musa! Hakika Mimi ni Mwenyezi Mungu, Mwenye kustahiki kuabudiwa pekee, Mwenye kushinda kila kitu, Mwenye kuweka kila kitu pahala pake.
  10. وَأَلْقِ عَصَاكَ ۚ فَلَمَّا رَءَاهَا تَهْتَزُّ كَأَنَّهَا جَآنٌّ وَلَّىٰ مُدْبِرًا وَلَمْ يُعَقِّبْ ۚ يَـٰمُوسَىٰ لَا تَخَفْ إِنِّى لَا يَخَافُ لَدَىَّ ٱلْمُرْسَلُونَ۝١٠

    Waalqi ʿasaka falamma raaha tahtazzu kaannaha jannun walla mudbiran walam yuʿaqqib ya moosa la takhaf innee la yakhafu ladayya almursaloona

    Na itupe fimbo yako! Alipo iona ikitikisika kama nyoka, aligeuka nyuma wala hakungoja. Ewe Musa! Usikhofu! Hakika hawakhofu mbele yangu Mitume.10

    Maelezo
    [10] Na katika njia ya kufikisha wito wako, tupa fimbo yako na utaiona inatikisika kama kijoka jepesi kinakwenda mbio. Yeye akarudi nyuma, wala hakurejea baada ya kurudi nyuma. Mwenyezi Mungu Mtukufu akamtuza kwa kauli yake: Usiogope. Mbele yangu hawaogopi. Mitume ninapo sema nao. Kisa cha Musa kimetajwa zaidi ya mara moja katika Qur'ani. Pengine hutolewa yasiyo tajwa penginepo. Na kila sehemu ina mnasaba wake. Katika sehemu hii makusudio ni kuondoa yale mastaajabu ya kuwa Nabii Muhammad s.a.w. kapata Ufunuoa (Wahyi) vile vile.
  11. إِلَّا مَن ظَلَمَ ثُمَّ بَدَّلَ حُسْنًۢا بَعْدَ سُوٓءٍ فَإِنِّى غَفُورٌ رَّحِيمٌ۝١١

    Illa man thalama thumma baddala husnan baʿda sooin fainnee ghafoorun raheemun

    Lakini aliye dhulumu, kisha akabadilisha wema baada ya ubaya, basi Mimi ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.11

    Maelezo
    [11] Lakini mwenye kutenda asicho ruhusiwa, na kisha akaleta wema baada ya kuteleza kwake, basi Mimi ni Mwingi wa kusamehe, Mkubwa wa kurehemu.
  12. وَأَدْخِلْ يَدَكَ فِى جَيْبِكَ تَخْرُجْ بَيْضَآءَ مِنْ غَيْرِ سُوٓءٍ ۖ فِى تِسْعِ ءَايَـٰتٍ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَقَوْمِهِۦٓ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا۟ قَوْمًا فَـٰسِقِينَ۝١٢

    Waadkhil yadaka fee jaybika takhruj baydaa min ghayri sooin fee tisʿi ayatin ila firʿawna waqawmihi innahum kanoo qawman fasiqeena

    Na ingiza mkono wako katika mfuko wako, utatoka mweupe bila ya maradhi. Ni katika Ishara tisa za kumpelekea Firauni na kaumu yake. Hakika hao walikuwa watu waovu.12

    Maelezo
    [12] Na utie mkono wako katika mfuko wa nguo zako, utatoka mweupe wala si kwa balanga. Hayo ni katika Ishara tisa za kumpelekea Firauni na kaumu yake. Hakika hao walikuwa watu walio tokana na amri ya Mwenyezi Mungu, ni makafiri. Hizo Ishara tisa ni:- Kupasuka bahari, T'ufani (Kimbunga), Nzige, Chawa, Vyura, Damu, Ukame, Fimbo, Kutoka mkono mweupe bila ya maradhi.
  13. فَلَمَّا جَآءَتْهُمْ ءَايَـٰتُنَا مُبْصِرَةً قَالُوا۟ هَـٰذَا سِحْرٌ مُّبِينٌ۝١٣

    Falamma jaathum ayatuna mubsiratan qaloo hatha sihrun mubeenun

    Basi zilipo wafikia Ishara zetu hizo zenye kuonyesha, wakasema: Huu ni uchawi dhaahiri.13

    Maelezo
    [13] Ilipo kuja miujiza hii kwa uwazi na dhaahiri wakasema: Huu ni uchawi wazi!
  14. وَجَحَدُوا۟ بِهَا وَٱسْتَيْقَنَتْهَآ أَنفُسُهُمْ ظُلْمًا وَعُلُوًّا ۚ فَٱنظُرْ كَيْفَ كَانَ عَـٰقِبَةُ ٱلْمُفْسِدِينَ۝١٤

    Wajahadoo biha waistayqanatha anfusuhum thulman waʿuluwwan faonthur kayfa kana ʿaqibatu almufsideena

    Na wakazikataa kwa dhulma na kujivuna, na hali ya kuwa nafsi zao zina yakini nazo. Basi angalia ulikuwaje mwisho wa mafisadi!14

    Maelezo
    [14] Wakaikadhibisha miujiza wakikataa kuwa inaonyesha dalili ya Utume. Na hakika yakini ilikwisha waingia katika nyoyo zao, lakini hawakusalimu amri kwa kuwa walikwisha tangaza kufuata upotovu na kushika uasi. Basi ewe Nabii! Hebu angalia vipi yalikuwa matokeo ya walio shikilia ufisadi, wakaikanya miujiza nayo iko wazi.
  15. وَلَقَدْ ءَاتَيْنَا دَاوُۥدَ وَسُلَيْمَـٰنَ عِلْمًا ۖ وَقَالَا ٱلْحَمْدُ لِلَّهِ ٱلَّذِى فَضَّلَنَا عَلَىٰ كَثِيرٍ مِّنْ عِبَادِهِ ٱلْمُؤْمِنِينَ۝١٥

    Walaqad atayna dawooda wasulaymana ʿilman waqala alhamdu lillahi allathee faddalana ʿala katheerin min ʿibadihi almumineena

    Na hakika tuliwapa Daudi na Sulaiman ilimu, na wakasema: Alhamdu Lillahi, Kuhimidiwa kote ni kwa Mwenyezi Mungu aliye tufadhilisha kuliko wengi katika waja wake Waumini.15

    Maelezo
    [15] Hizo ndizo jeuri za Firauni kwa sababu ya ufalme wake. Hebu sasa angalia utawala muadilifu, utawala wa hukumu, utawala wa unabii wa Daudi na mwanawe, Sulaiman, Mwenyezi Mungu awape amani. Sisi tuliwapa ilimu nyingi za sharia na mazoezi ya kuhukumu. Wakasimamisha uadilifu, na wakamhimidi Mwenyezi Mungu aliye wapa fadhila kushinda wengi katika waja wake wenye kusadiki, na kuifuata Haki.
  16. وَوَرِثَ سُلَيْمَـٰنُ دَاوُۥدَ ۖ وَقَالَ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ عُلِّمْنَا مَنطِقَ ٱلطَّيْرِ وَأُوتِينَا مِن كُلِّ شَىْءٍ ۖ إِنَّ هَـٰذَا لَهُوَ ٱلْفَضْلُ ٱلْمُبِينُ۝١٦

    Wawaritha sulaymanu dawooda waqala ya ayyuha alnnasu ʿullimna mantiqa alttayri waooteena min kulli shayin inna hatha lahuwa alfadlu almubeenu

    Na Sulaiman alimrithi Daudi, na akasema: Enyi watu! Tumefunzwa usemi wa ndege, na tumepewa kila kitu. Hakika hii ni fadhila iliyo dhaahiri.16

    Maelezo
    [16] Ufalme na hukumu ukatoka kwa Daudi ukenda kwa mwanawe, Sulaiman; naye akasema: Enyi watu! Sisi tumefunzwa lugha ya ndege, na tumepewa mengi tunayo yahitajia katika utawala wetu. Hakika neema hizi ni fadhila iliyo wazi aliyo tukhusisha sisi Mwenyezi Mungu, "Na Sulaiman alimrithi Daudi, na akasema: Enyi watu! Tumefunzwa usemi wa ndege, na tumepewa kila kitu. Hakika hii ni fadhila iliyo dhaahiri." Sulaiman a.s. ni mwana wa Daudi, naye ni Nabii na Mfalme kama yeye. Aliishi mnamo mwaka 974 mpaka 937 K.K. (yaani Kabla ya Kuzaliwa Nabii Isa). Mwenyezi Mungu alimjaalia kumjuvya kufahamu maneno ya ndege. Uchunguzi wa kisasa umeonyesha kwamba kila namna ya ndege wana njia zao za kufahamiana wao kwa wao. Katika njia hizo ni kwa kugusa, na sauti, na ishara.
  17. وَحُشِرَ لِسُلَيْمَـٰنَ جُنُودُهُۥ مِنَ ٱلْجِنِّ وَٱلْإِنسِ وَٱلطَّيْرِ فَهُمْ يُوزَعُونَ۝١٧

    Wahushira lisulaymana junooduhu mina aljinni waalinsi waalttayri fahum yoozaʿoona

    Na alikusanyiwa Sulaiman majeshi yake ya majini, na watu, na ndege; nayo yakapangwa kwa nidhamu.17

    Maelezo
    [17] Na Sulaiman alikusanya majeshi yake ya majini, watu, na ndege, kwenye uwanja mmoja. Na wao wakawa jeshi moja lenye nidhamu kwa vile kudhibitiwa wa mwanzo mpaka mwisho.
  18. حَتَّىٰٓ إِذَآ أَتَوْا۟ عَلَىٰ وَادِ ٱلنَّمْلِ قَالَتْ نَمْلَةٌ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّمْلُ ٱدْخُلُوا۟ مَسَـٰكِنَكُمْ لَا يَحْطِمَنَّكُمْ سُلَيْمَـٰنُ وَجُنُودُهُۥ وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ۝١٨

    Hatta itha ataw ʿala wadi alnnamli qalat namlatun ya ayyuha alnnamlu odkhuloo masakinakum la yahtimannakum sulaymanu wajunooduhu wahum la yashʿuroona

    Mpaka walipo fika kwenye bonde la wadudu chungu, alisema mdudu chungu mmoja: Enyi wadudu chungu! Ingieni majumbani mwenu, asikupondeni Sulaiman na majeshi yake bila ya wao kutambua.18

    Maelezo
    [18] Hata walipo fika kwenye bonde la wadudu chungu, mdudu chungu mmoja akasema: Enyi wadudu chungu! Ingieni vishimoni mwenu, asije Sulaiman na askari wake wakakuuweni na wao wala hawahisi kuwa nyinyi mpo. "Mpaka walipo fika kwenye bonde la wadudu chungu, alisema mdudu chungu mmoja: Enyi wadudu chungu! Ingieni majumbani mwenu, asikupondeni Sulaiman na majeshi yake bila ya wao kutambua." Inafahamikana wazi katika Aya hii kuwa wadudu chungu wanaishi kwa makundi, yaani wana umoja, na moja katika sifa zao ni kuwa macho na kutahadhari. Na inajuulikana tangu zamani kuwa wadudu chungu wana sifa kadhaa wa kadhaa makhsusi ambazo zinaonyesha kuwa wana umoja wenye nidhamu madhubuti katika hukumu, na wana kiasi kikubwa cha akili, na werevu, na nguvu za kukumbuka, na kupenda kazi na kukakamia, na juhudi isiyo jua kunyong'onyea wala kukata tamaa. Kama wanavyo juulikana kuwa wana wingi wa hila za kuendesha kazi zao. Na dalili ya hayo ni kuwa jamaa wa wadudu chungu ni peke yao baada ya binaadamu ndio wanao zika maiti wao. Na makundi mbali mbali yao yanashughulikia kukutana pahala pamoja kwa nyakati maalumu. Kwa ajili ya hayo zimewekwa siku makhsusi za kusimamisha soko wanapo kusanyika makundi yote kwa kubadilishana bidhaa na kujuana. Na makundi haya yanapo kutana hutokea mazungumzo kwa hima kubwa, na huulizana masuala yaliyo khusiana na mambo yao. Katika yanayo onekana yaliyo fungamana na mikusanyiko hiyo ni kuzuka mashauri yaliyo khusu umma wao, kama kutengeneza barabara ndefu, kwa subira na kukakamia kunako staajabisha. Wala makundi haya hayatosheki na kufanya kazi mchana tu, bali huendeleza kazi zao katika masiku ya mbaamwezi; ama masiku ya kiza hubaki mwahala mwao. Na jamaa wa makundi haya wana njia za pekee za kukusanya na kubeba na kuhifadhi vifaa vyao vya kula. Akishindwa mdudu kuchukua chakula alicho kikusanya kwa mdomo wake hukisukuma kwa miguu yake ya nyuma, na akakinyanyua kwa mikono yake. Na katika mtindo wao ni kuzing'ong'ona mbegu, na kuzipasua baadhi ya nafaka kabla ya kuzirindika ili zisije kuchipua. Na mbegu kubwa kubwa huzigawa vipande vipande ili iwe wepesi kuziingiza katika ghala zao. Na pindi zikiroana kwa mvua huzitoa zipate upepo na jua zikauke.
  19. فَتَبَسَّمَ ضَاحِكًا مِّن قَوْلِهَا وَقَالَ رَبِّ أَوْزِعْنِىٓ أَنْ أَشْكُرَ نِعْمَتَكَ ٱلَّتِىٓ أَنْعَمْتَ عَلَىَّ وَعَلَىٰ وَٰلِدَىَّ وَأَنْ أَعْمَلَ صَـٰلِحًا تَرْضَىٰهُ وَأَدْخِلْنِى بِرَحْمَتِكَ فِى عِبَادِكَ ٱلصَّـٰلِحِينَ۝١٩

    Fatabassama dahikan min qawliha waqala rabbi awziʿnee an ashkura niʿmataka allatee anʿamta ʿalayya waʿala walidayya waan aʿmala salihan tardahu waadkhilnee birahmatika fee ʿibadika alssaliheena

    Basi (Sulaiman) akatabasamu akacheka kwa neno hili, na akasema: Ee Mola wangu Mlezi! Nizindue niishukuru neema yako uliyo nineemesha mimi na wazazi wangu, na nipate kutenda mema uyapendayo, na uniingize kwa rehema yako katika waja wako wema.19

    Maelezo
    [19] Sulaiman akatabasamu akicheka kwa ile kauli ya mdudu chungu yenye kushughulikia maslaha yao, na akahisi neema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu iliyo juu yake. Akasema: Ewe Uliye niumba! Nijaalie niwe na shukrani kwako kwa neema ulizo nineemesha mimi na wazazi wangu, na niwezeshe nitende vitendo vyema unavyo viridhia, na unitie kwenye rehema yako iliyo timia.
  20. وَتَفَقَّدَ ٱلطَّيْرَ فَقَالَ مَا لِىَ لَآ أَرَى ٱلْهُدْهُدَ أَمْ كَانَ مِنَ ٱلْغَآئِبِينَ۝٢٠

    Watafaqqada alttayra faqala ma liya la ara alhudhuda am kana mina alghaibeena

    Na akawakagua ndege, na akasema: Imekuwaje, mbona simwoni Hud-hud, au amekuwa miongoni mwa walio ghibu?20

    Maelezo
    [20] Akalikagua jeshi lake la ndege asimwone Hud-hud. Akastaajabu, akasema: Mbona simwoni Hud-hud! Yupo hapa na mimi simwoni, au ameghibu hayupo miongoni mwetu?
  21. لَأُعَذِّبَنَّهُۥ عَذَابًا شَدِيدًا أَوْ لَأَا۟ذْبَحَنَّهُۥٓ أَوْ لَيَأْتِيَنِّى بِسُلْطَـٰنٍ مُّبِينٍ۝٢١

    Laoʿaththibannahu ʿathaban shadeedan aw laathbahannahu aw layatiyannee bisultanin mubeenin

    Kwa yakini nitamuadhibu kwa adhabu kali, au nitamchinja, au aniletee hoja ya kutosha.21

    Maelezo
    [21] Wallahi! Nitampatisha adhabu kali ya kumshikisha adabu, au nitamchinja ikiwa kosa lake ni kubwa! Ila aniletee hoja madhubuti ya kumtoa makosani kwa kuto kuwepo mbele yangu.
  22. فَمَكَثَ غَيْرَ بَعِيدٍ فَقَالَ أَحَطتُ بِمَا لَمْ تُحِطْ بِهِۦ وَجِئْتُكَ مِن سَبَإٍۭ بِنَبَإٍ يَقِينٍ۝٢٢

    Famakatha ghayra baʿeedin faqala ahattu bima lam tuhit bihi wajituka min sabain binabain yaqeenin

    Basi (Hud-hud) akakaa si mbali na akasema: Nimegundua usilo gundua wewe, na ninakujia hivi kutoka nchi ya Sabai, na nakuletea khabari za yakini.22

    Maelezo
    [22] Na Hud-hud alikuwa kakaa si pahala mbali kwa muda usio kuwa mrefu. Kisha akamjia Sulaiman, akamwambia: Nimejua jambo ulilo kuwa wewe hujalijua, na nimekujia kutoka nchi ya Sabai na khabari muhimu sana, nayo ni ya kweli kwa yakini. "Basi hakukaa mbali, na akasema: Nimegundua usilo gundua wewe, na ninakujia hivi kutoka nchi ya Sabai, na nakuletea khabari za yakini. Hakika mimi nimemkuta mwanamke anawatawala, naye amepewa kila kitu, na anacho kiti cha enzi kikubwa.Nimemkuta yeye na watu wake wanalisujudia jua badala ya Mwenyezi Mungu; na Shetani amewapambia vitendo vyao na akawazuilia Njia. Kwa hivyo hawakuongoka." Hizi ndizo Aya khasa zilizo khusu Ufalme wa Sabai. Na hii Sabai ni moja katika falme za kusini ya Arabuni, inayo itwa Yaman, na ambayo zamani ilikuwa ni maarufu kwa jina la "Arabia Iliyo Neemeka". Na jina hili la mwisho linaonyesha maendeleo yake na utajiri wake. Kwani kwa hakika ilikuwa nchi hiyo ina ustaarabu wa juu tangu miaka elfu mbili kabla ya kuzaliwa Nabii Isa a.s. Ikitegemea makulima, kwa sababu ya rutuba ya ardhi yake, na uzuri wa hali yake ya hewa. Na pia ikitegemea biashara kwa kuwa ipo kati baina ya Bara Hindi, na Uhabeshi, na Somalia, na Sham, na Iraq. Na kwa hakika mahodhi yaliyo jengwa kuwekea maji na kuyatumia, na maarufu yao yote ni Hodhi Maa'rib (Tazama Aya 16 Surat Sabai) na miji iliyo jengewa ngome, na makasri, na mahekalu, yanashuhudia mpaka hii leo maendeleo ya kijamii ya utajiri ulio kuwako katika nchi hii. Na hakika nakshi walizo zinakishi watawala wao, na baina ya nakshi hizo zipo kanuni za kuendesha mambo ya ujenzi na mengineyo, yanaonyesha kwa kila dalili ukomo wa ustaarabu ulio nawiri walio ufikilia. Na huu ufalme wa Sabai ambao ulifikilia kilele cha kustawi kwake katika siku za Sulaiman a.s. kiasi ya karne kumi kabla ya kuzaliwa Nabii Isa a.s. ulikuwa ni ufalme kama wa kabla yake, yaani watoto wakiwarithi baba zao. Na kwa hivyo alikuwa akihukumu wakati wa Sulaiman a.s. Malkia. Wataalamu wa taarikhi wamekhitalifiana juu ya jina la Malkia huyo. Waarabu wakimwita Balqiis; akisaidiwa na wazee wahishimiwa kama ni Baraza la Mashauri lake. (Tazama Aya 28-33 katika Surat An-naml.) Wala haikuthibitisha taarikh (historia) kuwa Ufalme wa Sabai ulikuwa dola ya kuteka nchi, bali ulikuwa ufalme wa biashara, na misafara. Katika mabaki yake hatuoni kutajwa vita au kuteka nchi isipo kuwa kwa uchache. Na haya ni kuwa umuhimu wa majeshi yake ulikuwa ni kuhifadhi ngome zake na kuzihami, na kulinda misafara yake kwa aghlabu. Na wananchi wa Sabai walikuwa ni mapagani, makafiri, wakiliabudu jua, kama ilivyo kuja katika Aya tukufu nambari 24 katika Sura hii. Pia wakiabudu mwezi. Na hao ndio miungu yao muhimu kabisa. Na walikuwa wakiwatolea sadaka na wakifukiza ubani katika mahekalu yao.
  23. إِنِّى وَجَدتُّ ٱمْرَأَةً تَمْلِكُهُمْ وَأُوتِيَتْ مِن كُلِّ شَىْءٍ وَلَهَا عَرْشٌ عَظِيمٌ۝٢٣

    Innee wajadtu imraatan tamlikuhum waootiyat min kulli shayin walaha ʿarshun ʿatheemun

    Hakika mimi nimemkuta mwanamke anawatawala, naye amepewa kila kitu, na anacho kiti cha enzi kikubwa.23

    Maelezo
    [23] Hakika mimi nimewaona watu wa Sabai wanatawaliwa na mwanamke, na amepewa kila kheri za kidunia, naye ana kiti cha enzi kikubwa kinacho onyesha dalili ya utukufu wa ufalme na nguvu za madaraka yake.
  24. وَجَدتُّهَا وَقَوْمَهَا يَسْجُدُونَ لِلشَّمْسِ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَزَيَّنَ لَهُمُ ٱلشَّيْطَـٰنُ أَعْمَـٰلَهُمْ فَصَدَّهُمْ عَنِ ٱلسَّبِيلِ فَهُمْ لَا يَهْتَدُونَ۝٢٤

    Wajadtuha waqawmaha yasjudoona lilshshamsi min dooni Allahi wazayyana lahumu alshshaytanu aʿmalahum fasaddahum ʿani alssabeeli fahum la yahtadoona

    Nimemkuta yeye na watu wake wanalisujudia jua badala ya Mwenyezi Mungu; na Shet'ani amewapambia vitendo vyao na akawazuilia Njia. Kwa hivyo hawakuongoka24

    Maelezo
    [24] Nimemwona yeye na watu wake wanaabudu jua, wala hawamuabudu Mwenyezi Mungu. Na Shetani amewazainishia vitendo vyao na wenyewe wakaviona ni vizuri na hali ni viovu. Kwa hivyo amewapoteza Njia ya Haki, basi hawakuongoka.
  25. أَلَّا يَسْجُدُوا۟ لِلَّهِ ٱلَّذِى يُخْرِجُ ٱلْخَبْءَ فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَيَعْلَمُ مَا تُخْفُونَ وَمَا تُعْلِنُونَ۝٢٥

    Alla yasjudoo lillahi allathee yukhriju alkhabaa fee alssamawati waalardi wayaʿlamu ma tukhfoona wama tuʿlinoona

    Na hawamsujudii Mwenyezi Mungu ambaye huyatoa yaliyo fichikana katika mbingu na ardhi, na anayajua mnayo yaficha na mnayo yatangaza.25

    Maelezo
    [25] Hawamsujudii Mwenyezi Mungu Mtukufu, ambaye ndiye anayafichua yaliyo fichika katika mbingu na ardhi, na anajua mnayo fanya kwa siri na kwa dhaahiri.
  26. ٱللَّهُ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ رَبُّ ٱلْعَرْشِ ٱلْعَظِيمِ ۩۝٢٦

    Allahu la ilaha illa huwa rabbu alʿarshi alʿatheemi

    Mwenyezi Mungu - hapana mungu ila Yeye, Mola Mlezi wa A'rshi tukufu26

    Maelezo
    [26] Mwenyezi Mungu, ambaye hapana wa kuabudiwa kwa Haki isipo kuwa Yeye, ndiye Mwenye madaraka makuu yasio na ukomo juu ya kila kiumbe.
  27. ۞ قَالَ سَنَنظُرُ أَصَدَقْتَ أَمْ كُنتَ مِنَ ٱلْكَـٰذِبِينَ۝٢٧

    Qala sananthuru asadaqta am kunta mina alkathibeena

    Akasema (Sulaiman): Tutatazama umesema kweli au wewe ni miongoni mwa waongo.27

    Maelezo
    [27] Sulaiman akasema kumwambia Hud-hud: Tutaichungua khabari yako hii tujue kwamba umesema kweli au wewe ni miongoni mwa waongo.
  28. ٱذْهَب بِّكِتَـٰبِى هَـٰذَا فَأَلْقِهْ إِلَيْهِمْ ثُمَّ تَوَلَّ عَنْهُمْ فَٱنظُرْ مَاذَا يَرْجِعُونَ۝٢٨

    Ithhab bikitabee hatha faalqih ilayhim thumma tawalla ʿanhum faonthur matha yarjiʿoona

    Nenda na barua yangu hii na uwafikishie, kisha waache na utazame watarejesha nini.28

    Maelezo
    [28] Nenda na barua yangu hii umfikishie yeye na kaumu yake. Kisha jitenge nao ujifiche pahali karibu, uangalie wanarejesheana maneno gani.
  29. قَالَتْ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلْمَلَؤُا۟ إِنِّىٓ أُلْقِىَ إِلَىَّ كِتَـٰبٌ كَرِيمٌ۝٢٩

    Qalat ya ayyuha almalao innee olqiya ilayya kitabun kareemun

    (Malkia) akasema: Enyi wahishimiwa! Hakika nimeletewa barua tukufu.29

    Maelezo
    [29] Barua ikamfikia yule Malkia, naye basi akawakusanya wahishimiwa wa kaumu yake, na halmashauri wake. Naye akasema: Enyi wahishimiwa! Mimi hakika imenifikilia barua yenye shani kuu.
  30. إِنَّهُۥ مِن سُلَيْمَـٰنَ وَإِنَّهُۥ بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ۝٣٠

    Innahu min sulaymana wainnahu bismi Allahi alrrahmani alrraheemi

    Imetoka kwa Sulaiman nayo ni: Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.30

    Maelezo
    [30] Kisha akawasomea hiyo barua, nayo imeanzia kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwenye utukufu na neema zote, ambaye daima anawamiminia waja wake rehema zake.
  31. أَلَّا تَعْلُوا۟ عَلَىَّ وَأْتُونِى مُسْلِمِينَ۝٣١

    Alla taʿloo ʿalayya watoonee muslimeena

    Msinifanyie jeuri, na fikeni kwangu nanyi mmekwisha kuwa wenye kusalimu amri.31

    Maelezo
    [31] Msifanye kiburi juu yangu, na nijieni nanyi mmet'ii na wanyenyekevu.
  32. قَالَتْ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلْمَلَؤُا۟ أَفْتُونِى فِىٓ أَمْرِى مَا كُنتُ قَاطِعَةً أَمْرًا حَتَّىٰ تَشْهَدُونِ۝٣٢

    Qalat ya ayyuha almalao aftoonee fee amree ma kuntu qatiʿatan amran hatta tashhadoona

    Akasema: Enyi wahishimiwa! Nipeni shauri katika jambo langu hili, kwani mimi sikati shauri yoyote mpaka mhudhurie.32

    Maelezo
    [32] Akaiambia baraza ya washauri wake: Nibainishieni lifaalo katika haya mambo muhimu nilio wekewa mbele yangu. Kwani mimi sikati shauri juu ya jambo lolote mpaka muwe nyinyi mmehudhuria.
  33. قَالُوا۟ نَحْنُ أُو۟لُوا۟ قُوَّةٍ وَأُو۟لُوا۟ بَأْسٍ شَدِيدٍ وَٱلْأَمْرُ إِلَيْكِ فَٱنظُرِى مَاذَا تَأْمُرِينَ۝٣٣

    Qaloo nahnu oloo quwwatin waoloo basin shadeedin waalamru ilayki faonthuree matha tamureena

    Wakasema: Sisi ni wenye nguvu na wakali kwa vita; na amri iko kwako, basi tazama ni nini unaamrisha.33

    Maelezo
    [33] Wakamwambia nao wametua: Sisi ni watu wenye nguvu za mwili, na tuna moyo na mashujaa. Hatuogopi vita. Basi angalia wewe jambo unalo taka kutuamrisha nasi ni wenye kut'ii.
  34. قَالَتْ إِنَّ ٱلْمُلُوكَ إِذَا دَخَلُوا۟ قَرْيَةً أَفْسَدُوهَا وَجَعَلُوٓا۟ أَعِزَّةَ أَهْلِهَآ أَذِلَّةً ۖ وَكَذَٰلِكَ يَفْعَلُونَ۝٣٤

    Qalat inna almulooka itha dakhaloo qaryatan afsadooha wajaʿaloo aʿizzata ahliha athillatan wakathalika yafʿaloona

    Akasema: Hakika wafalme wanapo uingia mji wanauharibu, na wanawafanya wale watukufu wake kuwa wanyonge. Na hivyo ndivyo watendavyo.34

    Maelezo
    [34] Akasema kwa taratibu na kupendelea salama: Hakika watawala wakiingia katika miji mikubwa pamoja na majeshi yao huifisidi, wakaondoa matengenezo yake, wakateketeza makulima na roho, na wakawafanya walio watukufu katika watu wa hiyo miji kuwa ndio madhalili, na huo ndio mtindo wao daima.
  35. وَإِنِّى مُرْسِلَةٌ إِلَيْهِم بِهَدِيَّةٍ فَنَاظِرَةٌۢ بِمَ يَرْجِعُ ٱلْمُرْسَلُونَ۝٣٥

    Wainnee mursilatun ilayhim bihadiyyatin fanathiratun bima yarjiʿu almursaloona

    Lakini mimi nitawapelekea zawadi, nami nitangoja watakayo rudi nayo wajumbe.35

    Maelezo
    [35] Na mimi kwa kupendelea salama na uzima nitampelekea zawadi Sulaiman na kaumu yake, na nitatazama wajumbe watarejea na nini - wataikubali zawadi au watairudisha?
  36. فَلَمَّا جَآءَ سُلَيْمَـٰنَ قَالَ أَتُمِدُّونَنِ بِمَالٍ فَمَآ ءَاتَىٰنِۦَ ٱللَّهُ خَيْرٌ مِّمَّآ ءَاتَىٰكُم بَلْ أَنتُم بِهَدِيَّتِكُمْ تَفْرَحُونَ۝٣٦

    Falamma jaa sulaymana qala atumiddoonani bimalin fama ataniya Allahu khayrun mimma atakum bal antum bihadiyyatikum tafrahoona

    Basi alipo fika (mjumbe) kwa Sulaiman, alisema (Sulaiman): Hivyo ndio nyinyi mnanisaidia kwa mali? Aliyo nipa Mwenyezi Mungu ni bora zaidi kuliko aliyo kupeni nyinyi. Lakini nyinyi mnafurahia hii zawadi yenu.36

    Maelezo
    [36] Wajumbe walifika kwa Sayyidina Sulaiman na zawadi zao. Huku anazijua neema za Mwenyezi Mungu Mtukufu zilio juu yake, Akawaambia naye ndio anamsemeza huyo Malkia na watu wake katika mkabala na wajumbe: Hivyo ndio mnanipa mimi mali? Aliyo nipa Mwenyezi Mungu ya Unabii, na ufalme, na neema, ni makubwa zaidi kuliko aliyo kupeni nyinyi. Bali nyinyi kwa hizi zawadi zenu na wingi wa mali yenu mnafurahi, sio kama mimi. Kwa sababu nyinyi hamjui ila yaliyo shikamana na dunia hii tu.
  37. ٱرْجِعْ إِلَيْهِمْ فَلَنَأْتِيَنَّهُم بِجُنُودٍ لَّا قِبَلَ لَهُم بِهَا وَلَنُخْرِجَنَّهُم مِّنْهَآ أَذِلَّةً وَهُمْ صَـٰغِرُونَ۝٣٧

    Irjiʿ ilayhim falanatiyannahum bijunoodin la qibala lahum biha walanukhrijannahum minha athillatan wahum saghiroona

    Rejea kwao! Kwa yakini sisi tutawajia kwa majeshi wasio yaweza kuyakabili. Na hakika tutawatoa humo na hali wao wamekuwa madhalili na wanyonge.37

    Maelezo
    [37] Akasema, akimsemeza yule msemaji kwa jina lao: Ewe mjumbe! Rejea kwao. Wallahi! tutawatokea kwa majeshi wasio yaweza kupambana nayo na kuyakabili. Na tutawatoa kwenye nchi ya Sabai nao wamepoteza utukufu wao, wamefanywa watumwa.
  38. قَالَ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلْمَلَؤُا۟ أَيُّكُمْ يَأْتِينِى بِعَرْشِهَا قَبْلَ أَن يَأْتُونِى مُسْلِمِينَ۝٣٨

    Qala ya ayyuha almalao ayyukum yateenee biʿarshiha qabla an yatoonee muslimeena

    Akasema: Enyi wahishimiwa! Ni nani kati yenu atakaye niletea kiti chake cha enzi kabla hawajanijia nao wamekwisha salimu amri.38

    Maelezo
    [38] Sulaiman akawaelekea binaadamu na majini aliyo dhalilishiwa na Mwenyezi Mungu kumtumikia, akawashitua kwa jambo geni. Akasema: Ni nani katika nyinyi anaweza kuniletea kiti chake cha enzi kikubwa kabla hawajanijia nao wamekwisha nyenyekea wanat'ii.
  39. قَالَ عِفْرِيتٌ مِّنَ ٱلْجِنِّ أَنَا۠ ءَاتِيكَ بِهِۦ قَبْلَ أَن تَقُومَ مِن مَّقَامِكَ ۖ وَإِنِّى عَلَيْهِ لَقَوِىٌّ أَمِينٌ۝٣٩

    Qala ʿifreetun mina aljinni ana ateeka bihi qabla an taqooma min maqamika wainne ʿalayhi laqawiyyun ameenun

    Akasema: Afriti, katika majini: Mimi nitakuletea kabla hujainuka pahala pako hapo. Na mimi kwa hakika nina nguvu na muaminifu.39

    Maelezo
    [39] Mmoja pandikizi la kijini lilisema: Mimi nitakuletea, na wewe umekaa katika baraza yako hii, kabla hujaondoka. Na mimi hakika naweza hayo, na muaminifu katika maneno yangu na vitendo vyangu.
  40. قَالَ ٱلَّذِى عِندَهُۥ عِلْمٌ مِّنَ ٱلْكِتَـٰبِ أَنَا۠ ءَاتِيكَ بِهِۦ قَبْلَ أَن يَرْتَدَّ إِلَيْكَ طَرْفُكَ ۚ فَلَمَّا رَءَاهُ مُسْتَقِرًّا عِندَهُۥ قَالَ هَـٰذَا مِن فَضْلِ رَبِّى لِيَبْلُوَنِىٓ ءَأَشْكُرُ أَمْ أَكْفُرُ ۖ وَمَن شَكَرَ فَإِنَّمَا يَشْكُرُ لِنَفْسِهِۦ ۖ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ رَبِّى غَنِىٌّ كَرِيمٌ۝٤٠

    Qala allathee ʿindahu ʿilmun mina alkitabi ana ateeka bihi qabla an yartadda ilayka tarfuka falamma raahu mustaqirran ʿindahu qala hatha min fadli rabbee liyabluwanee aashkuru am akfuru waman shakara fainnama yashkuru linafsihi waman kafara fainna rabbee ghaniyyun kareemun

    Akasema mwenye ilimu ya Kitabu: Mimi nitakuletea kabla ya kupepesa jicho lako. Basi alipo kiona kimewekwa mbele yake, akasema: Haya ni katika fadhila zake Mola wangu Mlezi, ili anijaribu nitashukuru au nitakufuru. Na mwenye kushukuru, kwa hakika, anashukuru kwa manufaa ya nafsi yake; na anaye kufuru, kwa hakika Mola wangu Mlezi ni Mkwasi na Karimu.40

    Maelezo
    [40] Akasema aliye pewa nguvu za kiroho, na ilimu ya Kitabu: Mimi nitakuletea hicho kiti cha enzi kabla jicho lako halijapepesa. Na akatimiza aliyo yasema. Sulaiman alipo kiona kiti kile kimetua mbele yake bila ya mtingisiko, alisema: Haya ni katika fadhila za Mwenyezi Mungu aliye niumba na akanipa kheri zake ili anifanyie mtihani, nitashukuru kwa neema hizi au sitoi haki yake? Na mwenye kumshukuru Mwenyezi Mungu basi huyo hakika amejiondolea nafsi yake mzigo wa waajibu. Na mwenye kuacha kushukuru kwa neema basi hakika Mola wangu Mlezi ni Mkwasi, si mwenye kuhitajia shukrani. Naye ni Karimu wa kuneemesha.
  41. قَالَ نَكِّرُوا۟ لَهَا عَرْشَهَا نَنظُرْ أَتَهْتَدِىٓ أَمْ تَكُونُ مِنَ ٱلَّذِينَ لَا يَهْتَدُونَ۝٤١

    Qala nakkiroo laha ʿarshaha nanthur atahtadee am takoonu mina allatheena la yahtadoona

    Akasema: Mgeuzieni kiti chake cha enzi hiki, tuone ataongoka, au atakuwa miongoni mwa wasio ongoka.41

    Maelezo
    [41] Sulaiman akawaambia watu wake: Kigeuzeni geuzeni hichi kiti cha enzi kwa baadhi ya mabadiliko ya nje, tupate kuona atakijua kwa kukiendea au hato kijua na kwa hivyo hato kiendea.
  42. فَلَمَّا جَآءَتْ قِيلَ أَهَـٰكَذَا عَرْشُكِ ۖ قَالَتْ كَأَنَّهُۥ هُوَ ۚ وَأُوتِينَا ٱلْعِلْمَ مِن قَبْلِهَا وَكُنَّا مُسْلِمِينَ۝٤٢

    Falamma jaat qeela ahakatha ʿarshuki qalat kaannahu huwa waooteena alʿilma min qabliha wakunna muslimeena

    Basi (Malkia) alipo fika akaambiwa: Je! Kiti chako cha enzi ni kama hiki? Akasema: Kama kwamba ndicho hichi. (Sulaiman na watu wake wakasema): Na sisi tumepewa ilimu kabla yake (Malkia), na tukawa Waislamu.42

    Maelezo
    [42] Alipo fika jicho lake lilipiga kwenye kiti chake cha enzi. Akaambiwa: Je! Kiti chako cha enzi ni mfano wa hiki? Akasema kwa vile kilivyo kamilika kufanana: Kama kwamba ndicho hichi. Na Sulaiman na walio pamoja naye wakasema: Sisi tulisha pewa ujuzi kumjua Mwenyezi Mungu na uwezo wake na ukweli wa yaliyo kuja kutoka kwake kama anavyo jua mwanamke huyu. Na sisi tangu hapo ni watu tulio mfuata Mwenyezi Mungu na tunamsafia Yeye ibada.
  43. وَصَدَّهَا مَا كَانَت تَّعْبُدُ مِن دُونِ ٱللَّهِ ۖ إِنَّهَا كَانَتْ مِن قَوْمٍ كَـٰفِرِينَ۝٤٣

    Wasaddaha ma kanat taʿbudu min dooni Allahi innaha kanat min qawmin kafireena

    Na yale aliyo kuwa akiyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu yalimzuilia. Hakika yeye (Malkia) alikuwa katika kaumu ya makafiri.43

    Maelezo
    [43] Na zile ibada za jua na mfano wake zilimzuia yule Malkia kumuabudu Mwenyezi Mungu. Kwani yeye alikuwa katika kaumu ya makafiri.
  44. قِيلَ لَهَا ٱدْخُلِى ٱلصَّرْحَ ۖ فَلَمَّا رَأَتْهُ حَسِبَتْهُ لُجَّةً وَكَشَفَتْ عَن سَاقَيْهَا ۚ قَالَ إِنَّهُۥ صَرْحٌ مُّمَرَّدٌ مِّن قَوَارِيرَ ۗ قَالَتْ رَبِّ إِنِّى ظَلَمْتُ نَفْسِى وَأَسْلَمْتُ مَعَ سُلَيْمَـٰنَ لِلَّهِ رَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ۝٤٤

    Qeela laha odkhulee alssarha falamma raathu hasibathu lujjatan wakashafat ʿan saqayha qala innahu sarhun mumarradun min qawareera qalat rabbi innee thalamtu nafsee waaslamtu maʿa sulaymana lillahi rabbi alʿalameena

    Akaambiwa: Liingie behewa la hili jumba. Alipo liona alidhani ni maji, na akapandisha nguo mpaka kwenye miundi yake. (Sulaiman) akasema: Hakika hilo ni behewa lilio sakafiwa kwa viyoo! Akasema (Malkia): Mola wangu Mlezi! Mimi nimejidhulumu nafsi yangu, na sasa nanyenyekea pamoja na Sulaiman kwa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.44

    Maelezo
    [44] Baada ya hao akaambiwa: Ingia katika jumba la Sulaiman. Na uwanja wake wa ndani ulikuwa umesakafiwa kwa kiyoo, na chini yake maji, na samaki wakiogelea humo. Kupandisha nguo miundi yake ya miguu ikaonekana, kwa kuwa alidhania ni maji. Sulaiman akamwambia hicho ni kiyoo, basi yakamuathiri yale madhaahiri ya kilimwengu, na akaona kuwa ufalme wake yeye haufai chochote mbele ya ufalme wa Nabii Sulaiman. Akasema: Mola Mlezi! Hakika mimi nimeidhulumu nafsi yangu kwa kughurika na ufalme wangu na ukafiri wangu. Na sasa ninanyenyekea pamoja na Sulaiman kumuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mwenye kuumba walimwengu wote na kuwalea na kuwasimamia.
  45. وَلَقَدْ أَرْسَلْنَآ إِلَىٰ ثَمُودَ أَخَاهُمْ صَـٰلِحًا أَنِ ٱعْبُدُوا۟ ٱللَّهَ فَإِذَا هُمْ فَرِيقَانِ يَخْتَصِمُونَ۝٤٥

    Walaqad arsalna ila thamooda akhahum salihan ani oʿbudoo Allaha faitha hum fareeqani yakhtasimoona

    . Na kwa kina Thamud tulimtuma ndugu yao Swaleh kuwaambia: Muabuduni Mwenyezi Mungu. Basi wakawa makundi mawili yanayo gombana.45

    Maelezo
    [45] Na tuliwapelekea Thamud ndugu yao Swaleh kuwafunza wamuamini Mwenyezi Mungu pekee. Wao wakakimbilia kugombana na kukhitalifiana. Wakawa makundi mawili. Moja lenye kuamini, na moja la kikafiri.
  46. قَالَ يَـٰقَوْمِ لِمَ تَسْتَعْجِلُونَ بِٱلسَّيِّئَةِ قَبْلَ ٱلْحَسَنَةِ ۖ لَوْلَا تَسْتَغْفِرُونَ ٱللَّهَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ۝٤٦

    Qala ya qawmi lima tastaʿjiloona bialssayyiati qabla alhasanati lawla tastaghfiroona Allaha laʿallakum turhamoona

    Akasema: Enyi watu wangu! Kwa nini mnauhimiza uwovu kabla ya wema? Kwa nini hamuombi msamaha kwa Mwenyezi Mungu ili mrehemewe?46

    Maelezo
    [46] Swaleh akasema nao kuwanasihi: Enyi watu! Mbona mnaihimiza adhabu mlio ahidiwa kabla ya kutubu? Kwa nini hamwombi msamaha kwa Mola wenu Mlezi, mkamuamini Yeye kwa kutaraji akurehemuni?
  47. قَالُوا۟ ٱطَّيَّرْنَا بِكَ وَبِمَن مَّعَكَ ۚ قَالَ طَـٰٓئِرُكُمْ عِندَ ٱللَّهِ ۖ بَلْ أَنتُمْ قَوْمٌ تُفْتَنُونَ۝٤٧

    Qaloo ittayyarna bika wabiman maʿaka qala tairukum ʿinda Allahi bal antum qawmun tuftanoona

    Wakasema: Tuna kisirani nawe na wale walio pamoja nawe. Yeye akasema: Uaguzi wa ukorofi wenu uko kwa Mwenyezi Mungu; lakini nyinyi ni watu mnao jaribiwa.47

    Maelezo
    [47] Wakasema: Sisi tunakuona wewe na hao walio nawe ni wakorofi, ndio tukapatilizwa na ukame. Yeye akasema: Sababu za kheri na shari zinazo kuteremkieni bila ya shaka yoyote zinatoka kwa Mwenyezi Mungu. Bali nyinyi ni watu mnao pewa mitihani ya neema na nakama, ili mpate kuamini.
  48. وَكَانَ فِى ٱلْمَدِينَةِ تِسْعَةُ رَهْطٍ يُفْسِدُونَ فِى ٱلْأَرْضِ وَلَا يُصْلِحُونَ۝٤٨

    Wakana fee almadeenati tisʿatu rahtin yufsidoona fee alardi wala yuslihoona

    Na walikuwamo mjini watu tisa wakifanya ufisadi katika nchi wala hawafanyi la maslaha.48

    Maelezo
    [48] Na waongozi wa shari kati yao walikuwa ni tisa, kazi yao ni kufisidi katika nchi kwa maoni yao na madai yao. Wala haukuwa mtindo wao kutenda jema lolote.
  49. قَالُوا۟ تَقَاسَمُوا۟ بِٱللَّهِ لَنُبَيِّتَنَّهُۥ وَأَهْلَهُۥ ثُمَّ لَنَقُولَنَّ لِوَلِيِّهِۦ مَا شَهِدْنَا مَهْلِكَ أَهْلِهِۦ وَإِنَّا لَصَـٰدِقُونَ۝٤٩

    Qaloo taqasamoo biAllahi lanubayyitannahu waahlahu thumma lanaqoolanna liwaliyyihi ma shahidna mahlika ahlihi wainna lasadiqoona

    Wakasema: Apishaneni kwa Mwenyezi Mungu tutamshambulia usiku yeye na ahali zake; kisha tutamwambia mrithi wake: Sisi hatukuona maangamizo ya watu wake, na sisi bila ya shaka tunasema kweli.49

    Maelezo
    [49] Wale washirikina wakaambizana wenyewe kwa wenyewe: Apishaneni kwa jina la Mwenyezi Mungu, kwamba kwa yakini tutamshambulia yeye na ahali zake, na tutawauwa. Kisha tutamwambia jamaa yao wa damu kwamba sisi hatukayaona mauwaji yake wala ya ahali zake. Na hakika sisi ni wasema kweli kwa haya tuliyo yataja.
  50. وَمَكَرُوا۟ مَكْرًا وَمَكَرْنَا مَكْرًا وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ۝٥٠

    Wamakaroo makran wamakarna makran wahum la yashʿuroona

    Basi wakapanga mipango yao, na Sisi tukapanga mipango yetu, na wao hawatambui.50

    Maelezo
    [50] Walipanga kumuuwa Swaleh na ahali zake, na Mwenyezi Mungu nyuma yao kapanga kumwokoa Nabii wake na ahali zake, na kuwateketeza wao, na hali wao hata hawatambui.
  51. فَٱنظُرْ كَيْفَ كَانَ عَـٰقِبَةُ مَكْرِهِمْ أَنَّا دَمَّرْنَـٰهُمْ وَقَوْمَهُمْ أَجْمَعِينَ۝٥١

    Faonthur kayfa kana ʿaqibatu makrihim anna dammarnahum waqawmahum ajmaʿeena

    Basi angalia ulivyo kuwa mwisho wa mipango yao, ya kwamba tuliwaangamiza wao pamoja na watu wao wote.51

    Maelezo
    [51] Ewe Nabii! Hebu tazama vipi yalikuwa matokeo ya mipango yao na mipango yetu. Sisi tuliwaangamiza wote hao wao na kaumu yao.
  52. فَتِلْكَ بُيُوتُهُمْ خَاوِيَةًۢ بِمَا ظَلَمُوٓا۟ ۗ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةً لِّقَوْمٍ يَعْلَمُونَ۝٥٢

    Fatilka buyootuhum khawiyatan bima thalamoo inna fee thalika laayatan liqawmin yaʿlamoona

    Basi hizo nyumba zao ni tupu kwa sababu ya walivyo dhulumu. Hakika bila ya shaka katika hayo ipo Ishara kwa watu wanao jua.52

    Maelezo
    [52] Na hebu yatazame mabaki yao. Utakuta nyumba zao zimeanguka, zimevurugika, kwa sababu ya udhalimu wao na kufru zao, na kumtakia shari Nabii wao. Hakika kwa walio fanyiwa kina Thamud ipo Ishara kwa watu wanao ujua uwezo wetu na wakawaidhika.
  53. وَأَنجَيْنَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَكَانُوا۟ يَتَّقُونَ۝٥٣

    Waanjayna allatheena amanoo wakanoo yattaqoona

    Na tukawaokoa wale walio amini na walio kuwa wanamchamngu.53

    Maelezo
    [53] Na Sisi tukakiokoa kikundi kilicho muamini Saleh kutokana na hilaki hii, na wakawa wanao gopa kuziacha amri zake.
  54. وَلُوطًا إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِۦٓ أَتَأْتُونَ ٱلْفَـٰحِشَةَ وَأَنتُمْ تُبْصِرُونَ۝٥٤

    Walootan ith qala liqawmihi atatoona alfahishata waantum tubsiroona

    Na Luut'i alipo waambia watu wake: Je! Mnafanya uchafu nanyi mnaona?54

    Maelezo
    [54] Ewe Nabii! Mtaje Luut'i na khabari zake pamoja na kaumu ya watendao uchafu, pale alipo waambia: Je! Mnafanya dhambi hizi ambazo zimepita hadi ya uchafu na kinyume na maumbile, na hali nyinyi mnaona na mnaangalia uovu wa haya mliyo yashikilia?
  55. أَئِنَّكُمْ لَتَأْتُونَ ٱلرِّجَالَ شَهْوَةً مِّن دُونِ ٱلنِّسَآءِ ۚ بَلْ أَنتُمْ قَوْمٌ تَجْهَلُونَ۝٥٥

    Ainnakum latatoona alrrijala shahwatan min dooni alnnisai bal antum qawmun tajhaloona

    Hivyo nyinyi mnawaingilia wanaume kwa matamanio badala ya wanawake? Hakika nyinyi ni watu mnao fanya ujinga kabisa!55

    Maelezo
    [55] Hivyo inaelekea katika nadhari ya akili zenu na maumbile kuwaingilia wanaume kwa matamanio yenu, na mkwawacha wanawake? Ama kweli nyinyi mmesibiwa na upumbavu na ujinga wa kufudikiza, hata imekuwa hamwezi tena kuteuwa baina ya kiovu na chema.
  56. ۞ فَمَا كَانَ جَوَابَ قَوْمِهِۦٓ إِلَّآ أَن قَالُوٓا۟ أَخْرِجُوٓا۟ ءَالَ لُوطٍ مِّن قَرْيَتِكُمْ ۖ إِنَّهُمْ أُنَاسٌ يَتَطَهَّرُونَ۝٥٦

    Fama kana jawaba qawmihi illa an qaloo akhrijoo ala lootin min qaryatikum innahum onasun yatatahharoona

    Basi haikuwa jawabu ya watu wake ila ni kusema: Wafukuzeni wafwasi wa Luut'i katika mji wenu. Hao ni watu wanao jitia usafi.56

    Maelezo
    [56] Haikuwa jawabu ya watu wake alipo wakataza ila ni kusema: Mtoleeni mbali Luut'i na wafwasi wake katika mji huu. Kwani wao wanajitakasa hawataki kushirikiana nasi katika haya tuyatendayo.
  57. فَأَنجَيْنَـٰهُ وَأَهْلَهُۥٓ إِلَّا ٱمْرَأَتَهُۥ قَدَّرْنَـٰهَا مِنَ ٱلْغَـٰبِرِينَ۝٥٧

    Faanjaynahu waahlahu illa imraatahu qaddarnaha mina alghabireena

    Basi tukamwokoa yeye na ahali zake, isipo kuwa mkewe; tukamkadiria katika walio baki nyuma.57

    Maelezo
    [57] Basi Sisi tukamwokoa yeye na ahali zake na ile adhabu walio pelekewa wale watu, isipo kuwa mkewe. Mwenyezi Mungu alimkadiria awe na walio baki nyuma ili apate kuangamia kwa adhabu pamoja na makafiri.
  58. وَأَمْطَرْنَا عَلَيْهِم مَّطَرًا ۖ فَسَآءَ مَطَرُ ٱلْمُنذَرِينَ۝٥٨

    Waamtarna ʿalayhim mataran fasaa mataru almunthareena

    Na tukawanyeshea mvua. Ni ovu kweli kweli hiyo mvua ya walio kwisha onywa.58

    Maelezo
    [58] Na Sisi tukawanyeshea mvua hao mafisadi, mvua ya adhabu na nakama. Ilikuwa mvua ya kuwahiliki walio onywa kuwa watapata adhabu chungu, na wala wasisikie.
  59. قُلِ ٱلْحَمْدُ لِلَّهِ وَسَلَـٰمٌ عَلَىٰ عِبَادِهِ ٱلَّذِينَ ٱصْطَفَىٰٓ ۗ ءَآللَّهُ خَيْرٌ أَمَّا يُشْرِكُونَ۝٥٩

    Quli alhamdu lillahi wasalamun ʿala ʿibadihi allatheena istafa allahu khayrun amma yushrikoona

    Sema: Alhamdu Lillahi! Kuhimidiwa ni kwa Mwenyezi Mungu! Na amani ishuke juu ya waja wake alio wateuwa. Je! Mwenyezi Mungu ni bora, au wale wanao washirikisha naye?59

    Maelezo
    [59] Ewe Mtume! Sema: Hakika mimi namhimidi Mwenyezi Mungu na namsifu Yeye peke yake. Na namwomba Mwenyezi Mungu salama na maamkio kwa waja wake alio wateuwa kwa kuwapa Ujumbe wake. Na ewe Mtume! Waambie washirikina: Je! Kumuamini Mwenyezi Mungu Mmoja, Aliye Mpweke, ni bora kwa mwenye kuamini, au kuabudu masanamu mnayo mshirikisha naye, nayo hayawezi kukudhuruni wala kukufaeni?
  60. أَمَّنْ خَلَقَ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ وَأَنزَلَ لَكُم مِّنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءً فَأَنۢبَتْنَا بِهِۦ حَدَآئِقَ ذَاتَ بَهْجَةٍ مَّا كَانَ لَكُمْ أَن تُنۢبِتُوا۟ شَجَرَهَآ ۗ أَءِلَـٰهٌ مَّعَ ٱللَّهِ ۚ بَلْ هُمْ قَوْمٌ يَعْدِلُونَ۝٦٠

    Amman khalaqa alssamawati waalarda waanzala lakum mina alssamai maan faanbatna bihi hadaiqa thata bahjatin ma kana lakum an tunbitoo shajaraha ailahun maʿa Allahi bal hum qawmun yaʿdiloona

    AU NANI yule aliye ziumba mbingu na ardhi, na akakuteremshieni maji kutoka mbinguni, na kwa hayo tukaziotesha bustani zenye kupendeza? Nyinyi hamna uwezo wa kuiotesha miti yake. Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Bali hao ni watu walio potoka.60

    Maelezo
    [60] Bali, ewe Mtume, waulize: Ni nani aliye ziumba mbingu na ardhi na viliomo ndani yake, na akakuteremshieni kutoka mbinguni mvua yenye manufaa, na kwa hiyo akakuotesheeni bustani nzuri zenye kupendeza. Msingeli weza nyinyi kuiotesha miti yake ya namna mbali mbali, na rangi mbali mbali, na matunda mbali mbali! Mipango hii iliyo umana sawa katika uumbaji inathibitisha kuwa hapana mungu pamoja na Mwenyezi Mungu. Lakini makafiri ni watu walio potoka wakaiacha Haki na Imani, na wameelekea kwenye upotovu na ushirikina.
  61. أَمَّن جَعَلَ ٱلْأَرْضَ قَرَارًا وَجَعَلَ خِلَـٰلَهَآ أَنْهَـٰرًا وَجَعَلَ لَهَا رَوَٰسِىَ وَجَعَلَ بَيْنَ ٱلْبَحْرَيْنِ حَاجِزًا ۗ أَءِلَـٰهٌ مَّعَ ٱللَّهِ ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ۝٦١

    Amman jaʿala alarda qararan wajaʿala khilalaha anharan wajaʿala laha rawasiya wajaʿala bayna albahrayni hajizan ailahun maʿa Allahi bal aktharuhum la yaʿlamoona

    Au nani yule aliye ifanya ardhi mahali pa kutua, na akajaalia ndani yake mito, na akaweka milima? Na akaweka baina ya bahari mbili kiziwizi? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Bali wengi wao hawajui.61

    Maelezo
    [61] Bali waulize, ewe Mtume: Nani aliye itengeneza ardhi hata ikafaa kukaliwa na watu wakatulia humo, na akaumba mito kati yake, na juu yake akaumba milima kuizuilia isiyumbe yumbe, na akayatenganisha maji matamu na maji ya chumvi hata yasichanganyike? Hapana mungu pamoja na Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mwenye kuumba peke yake. Lakini wengi wa watu hawanafiiki na ujuzi wa Haki kama ilivyo. Wamekuwa kama kwamba hawajui kitu.
  62. أَمَّن يُجِيبُ ٱلْمُضْطَرَّ إِذَا دَعَاهُ وَيَكْشِفُ ٱلسُّوٓءَ وَيَجْعَلُكُمْ خُلَفَآءَ ٱلْأَرْضِ ۗ أَءِلَـٰهٌ مَّعَ ٱللَّهِ ۚ قَلِيلًا مَّا تَذَكَّرُونَ۝٦٢

    Amman yujeebu almudtarra itha daʿahu wayakshifu alssooa wayajʿalukum khulafaa alardi ailahun maʿa Allahi qaleelan ma tathakkaroona

    Au nani yule anaye mjibu mwenye shida pale anapo mwomba, na akaiondoa dhiki, na akakufanyeni warithi wa ardhi? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Ni machache mnayo yazingatia.62

    Maelezo
    [62] Bali waulize, ewe Mtume: Nani anaye muitikia aliye shikwa na shida katika maombi yake, pale anapo shikwa na shida, akamtegemea Mwenyezi Mungu kwa unyonge na unyenyekevu, naye akamwondolea huyo mtu karaha iliyo msibu, na akakufanyeni warithi wa walio kutangulieni katika nchi? Hapana mungu pamoja na Mwenyezi Mungu wa kukupeni neema zote hizi. Lakini nyinyi makafiri, ni kuchache kabisa kuwaidhika kwenu.
  63. أَمَّن يَهْدِيكُمْ فِى ظُلُمَـٰتِ ٱلْبَرِّ وَٱلْبَحْرِ وَمَن يُرْسِلُ ٱلرِّيَـٰحَ بُشْرًۢا بَيْنَ يَدَىْ رَحْمَتِهِۦٓ ۗ أَءِلَـٰهٌ مَّعَ ٱللَّهِ ۚ تَعَـٰلَى ٱللَّهُ عَمَّا يُشْرِكُونَ۝٦٣

    Amman yahdeekum fee thulumati albarri waalbahri waman yursilu alrriyaha bushran bayna yaday rahmatihi ailahun maʿa Allahi taʿala Allahu ʿamma yushrikoona

    Au nani yule anaye kuongoeni katika giza la bara na bahari, na akazipeleka pepo kuleta bishara kabla ya rehema zake? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Ametukuka Mwenyezi Mungu juu ya wanao washirikisha naye.63

    Maelezo
    [63] Bali waulize, ewe Mtume: Nani anaye waongoza katika nyendo za katika giza la usiku katika safari za nchi kavu na baharini? Na nani anaye zipeleka pepo zinazo bashiria mvua, nayo ni rehema itokayo kwa Mwenyezi Mungu? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu anaye fanya hayo? Mwenyezi Mungu Subhanahu ametakasika kuwa na mshirika.
  64. أَمَّن يَبْدَؤُا۟ ٱلْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُۥ وَمَن يَرْزُقُكُم مِّنَ ٱلسَّمَآءِ وَٱلْأَرْضِ ۗ أَءِلَـٰهٌ مَّعَ ٱللَّهِ ۚ قُلْ هَاتُوا۟ بُرْهَـٰنَكُمْ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ۝٦٤

    Amman yabdao alkhalqa thumma yuʿeeduhu waman yarzuqukum mina alssamai waalardi ailahun maʿa Allahi qul hatoo burhanakum in kuntum sadiqeena

    Au nani anaye uanzisha uumbaji, kisha akaurejesha? Na nani anaye kuruzukuni kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Sema: Leteni hoja zenu kama nyinyi ni wasema kweli.64

    Maelezo
    [64] Bali waulize, ewe Mtume: Nani anaye anzisha uumbaji tangu mwanzo, na kisha baada ya kupotea kwake akaurejesha kama ulivyo kuwa? Na nani anaye kuteremshieni riziki kutoka mbinguni, na akaitoa kwenye ardhi? Hakuna mungu pamoja na Mwenyezi Mungu atendaye hayo. Sema, ewe Mtume, kuwatahayarisha na kuwakanya: Kama nyinyi mnaye mungu asiye kuwa Mwenyezi Mungu basi tupeni hoja ya hayo, ikiwa mnadai kuwa nyinyi ni wasema kweli. Na wala hayataweza kuwa hayo kwenu.
  65. قُل لَّا يَعْلَمُ مَن فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ٱلْغَيْبَ إِلَّا ٱللَّهُ ۚ وَمَا يَشْعُرُونَ أَيَّانَ يُبْعَثُونَ۝٦٥

    Qul la yaʿlamu man fee alssamawati waalardi alghayba illa Allahu wama yashʿuroona ayyana yubʿathoona

    Sema: Hapana katika mbingu na ardhi ajuaye ya ghaibu isipo kuwa Mwenyezi Mungu. Wala wao hawajui lini watafufuliwa.65

    Maelezo
    [65] Sema, ewe Mtume: Hakika mwenye kutenda yote haya peke yake ndiye Yeye Subhanahu aliye tengeka peke yake kwa kuyajua mambo ya ghaibu yalioko mbinguni na duniani. Na Yeye huyo ndiye Mwenyezi Mungu wa pekee. Wala watu hawajui wakati gani watafufuliwa kutoka makaburini kwao kwa ajili ya kuhisabiwa na kulipwa.
  66. بَلِ ٱدَّٰرَكَ عِلْمُهُمْ فِى ٱلْـَٔاخِرَةِ ۚ بَلْ هُمْ فِى شَكٍّ مِّنْهَا ۖ بَلْ هُم مِّنْهَا عَمُونَ۝٦٦

    Bali iddaraka ʿilmuhum fee alakhirati bal hum fee shakkin minha bal hum minha ʿamoona

    Kwani huo ujuzi wao umefikilia kuijua Akhera? Bali wao wamo katika shaka nayo tu, bali wao ni vipofu nayo.66

    Maelezo
    [66] Ujuzi wao wa Akhera umefuatana na ujinga, na huo ukawapelekea kuitilia shaka. Nao wamekuwa vipofu hawaitambui Haki katika jambo lolote, kwa sababu upotovu umefisidi fahamu zao.
  67. وَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓا۟ أَءِذَا كُنَّا تُرَٰبًا وَءَابَآؤُنَآ أَئِنَّا لَمُخْرَجُونَ۝٦٧

    Waqala allatheena kafaroo aitha kunna turaban waabaona ainna lamukhrajoona

    Na wakasema walio kufuru: Tutapo kuwa mchanga, sisi na baba zetu, hivyo kweli tutakuja tolewa?67

    Maelezo
    [67] Wakasema makafiri kwa kukanya kufufuliwa: Hivyo sisi tukisha kuwa mchanga, na ikisha oza miili yetu na ya baba zetu walio tutangulia, ndio tutarejeshwa tutolewe upya tuwe wahai?
  68. لَقَدْ وُعِدْنَا هَـٰذَا نَحْنُ وَءَابَآؤُنَا مِن قَبْلُ إِنْ هَـٰذَآ إِلَّآ أَسَـٰطِيرُ ٱلْأَوَّلِينَ۝٦٨

    Laqad wuʿidna hatha nahnu waabaona min qablu in hatha illa asateeru alawwaleena

    Haya haya tuliahidiwa sisi na baba zetu zamani. Hayakuwa haya ila ni hadithi za uwongo za watu wa kale.68

    Maelezo
    [68] Muhammad ametuahidi kuwa tutafufuliwa, kama Mitume walio tangulia walivyo waahidi baba zetu. Ingeli kuwa hayo ni kweli, basi yangeli kwisha kuwa. Haya si chochote ila ni uwongo tu wa watu wa kale.
  69. قُلْ سِيرُوا۟ فِى ٱلْأَرْضِ فَٱنظُرُوا۟ كَيْفَ كَانَ عَـٰقِبَةُ ٱلْمُجْرِمِينَ۝٦٩

    Qul seeroo fee alardi faonthuroo kayfa kana ʿaqibatu almujrimeena

    Sema: Nendeni katika ardhi, na tazameni ulikuwaje mwisho wa wakosefu.69

    Maelezo
    [69] Ewe Mtume! Waambie: Tembeeni duniani, na mtazame mabaki ya yaliyo wapata walio kadhibisha, nayo ni adhabu ya Mwenyezi Mungu. Huenda labda mkayazingatia haya, na mkaikhofu adhabu ya Akhera.
  70. وَلَا تَحْزَنْ عَلَيْهِمْ وَلَا تَكُن فِى ضَيْقٍ مِّمَّا يَمْكُرُونَ۝٧٠

    Wala tahzan ʿalayhim wala takun fee dayqin mimma yamkuroona

    Wala usiwahuzunukie wala usiwe katika dhiki kwa sababu ya hila zao wanazo zifanya.70

    Maelezo
    [70] Ewe Mtume! Usiwahuzunukie makafiri wasio kufuata. Kwani kwa hakika waajibu wako ni kufikisha Ujumbe tu. Wala usiwe na dhiki kifuani mwako kwa sababu ya hila zao na vitimbi vyao. Kwani hakika Mwenyezi Mungu atakupa ushindi juu yao.
  71. وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَـٰذَا ٱلْوَعْدُ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ۝٧١

    Wayaqooloona mata hatha alwaʿdu in kuntum sadiqeena

    Na wanasema: Ahadi hii itatokea lini, ikiwa mnasema kweli?71

    Maelezo
    [71] Na makafiri wanafanya ukomo wa juhudi yao kukanusha, na wanaihimiza adhabu kwa kusema: Lini, basi, itakuwa hiyo adhabu ambayo mnatutishia kuwa itakuja, ikiwa nyinyi mnasema kweli kuwa adhabu itawashukia wanao kanusha?
  72. قُلْ عَسَىٰٓ أَن يَكُونَ رَدِفَ لَكُم بَعْضُ ٱلَّذِى تَسْتَعْجِلُونَ۝٧٢

    Qul ʿasa an yakoona radifa lakum baʿdu allathee tastaʿjiloona

    Sema: Asaa ni karibu kukufikieni sehemu ya yale mnayo yahimiza.72

    Maelezo
    [72] Ewe Mtume! Sema: Huenda ikakukuteni, na imekukaribieni baadhi ya adhabu mnayo ihimiza.
  73. وَإِنَّ رَبَّكَ لَذُو فَضْلٍ عَلَى ٱلنَّاسِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَشْكُرُونَ۝٧٣

    Wainna rabbaka lathoo fadlin ʿala alnnasi walakinna aktharahum la yashkuroona

    Na hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye fadhila kwa watu, lakini wengi wao hawashukuru.73

    Maelezo
    [73] Na hakika Mwenyezi Mungu Mola wako Mlezi, ewe Mtume, ni Mwenye neema na hisani kwa watu wote. Na katika rehema zake ni kuakhirisha hiyo adhabu kwa hao wanao kadhibisha. Lakini watu wengi hawaelewi fadhila za Mwenyezi Mungu wala hawamshukuru.
  74. وَإِنَّ رَبَّكَ لَيَعْلَمُ مَا تُكِنُّ صُدُورُهُمْ وَمَا يُعْلِنُونَ۝٧٤

    Wainna rabbaka layaʿlamu ma tukinnu sudooruhum wama yuʿlinoona

    Na hakika Mola wako Mlezi anayajua yanayo ficha vifua vyao na wanayo yatangaza.74

    Maelezo
    [74] Ewe Mtume! Hakika Mwenyezi Mungu, Mola wako Mlezi, hapana shaka anajua kila wanalo lificha na wanalo litangaza, ikiwa maneno au vitendo viovu. Naye atakuja walipa kwayo.
  75. وَمَا مِنْ غَآئِبَةٍ فِى ٱلسَّمَآءِ وَٱلْأَرْضِ إِلَّا فِى كِتَـٰبٍ مُّبِينٍ۝٧٥

    Wama min ghaibatin fee alssamai waalardi illa fee kitabin mubeenin

    Na hakuna siri katika mbingu na ardhi ila imo katika Kitabu kinacho bainisha.75

    Maelezo
    [75] Na hapana kilicho fichikana cha ghaibu, na kiwe kidogo vipi au duni, mbinguni au katika ardhi ila Mwenyezi Mungu anakijua, na amekidhibiti katika Kitabu cha Haki kilioko kwake.
  76. إِنَّ هَـٰذَا ٱلْقُرْءَانَ يَقُصُّ عَلَىٰ بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ أَكْثَرَ ٱلَّذِى هُمْ فِيهِ يَخْتَلِفُونَ۝٧٦

    Inna hatha alqurana yaqussu ʿala banee israeela akthara allathee hum feehi yakhtalifoona

    Hakika Qur'ani hii inawasimulia Wana wa Israili mengi wanayo khitalifiana nayo.76

    Maelezo
    [76] Hakika Kitabu hiki alicho teremshiwa Muhammad kinawawekea wazi Wana wa Israili ukweli wa yaliyo kuja katika Taurati, katika mambo ya itikadi na hukumu na hadithi. Na kinawarudisha kwenye kweli katika mambo waliyo khitalifiana kwayo.
  77. وَإِنَّهُۥ لَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِّلْمُؤْمِنِينَ۝٧٧

    Wainnahu lahudan warahmatun lilmumineena

    Nayo hakika ni Uwongofu na Rehema kwa Waumini.77

    Maelezo
    [77] Hakika Kitabu hichi ni Uwongofu wa kuokoa watu wasipotee, na ni Rehema ya kuwakinga na adhabu wote wenye kukiamini.
  78. إِنَّ رَبَّكَ يَقْضِى بَيْنَهُم بِحُكْمِهِۦ ۚ وَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلْعَلِيمُ۝٧٨

    Inna rabbaka yaqdee baynahum bihukmihi wahuwa alʿazeezu alʿaleemu

    Hakika Mola wako Mlezi atawahukumu kwa hukumu yake, naye ni Mwenye nguvu Mjuzi.78

    Maelezo
    [78] Ewe Mtume! Hakika Mola wako Mlezi atawapambanua watu wote Siku ya Kiyama kwa uadilifu wake. Naye ndiye Mwenye nguvu za kushinda, basi hapana wa kuipinga hukumu yake. Yeye ni Mjuzi wa kila kitu, basi mbele yake kweli haiwezi kuchanganyika na uwongo.
  79. فَتَوَكَّلْ عَلَى ٱللَّهِ ۖ إِنَّكَ عَلَى ٱلْحَقِّ ٱلْمُبِينِ۝٧٩

    Fatawakkal ʿala Allahi innaka ʿala alhaqqi almubeeni

    Basi mtegemee Mweneyezi Mungu; hakika wewe uko juu ya Haki iliyo wazi.79

    Maelezo
    [79] Basi, ewe Mtume, mtegemezee mambo yako Mwenyezi Mungu, na shikilia wito wako kwa kuamini kuwa utashinda tu, kwa sababu wewe uko juu ya Haki iliyo wazi, na mapuuza ya makafiri kukupuuza wewe hakutakudhuru kitu.
  80. إِنَّكَ لَا تُسْمِعُ ٱلْمَوْتَىٰ وَلَا تُسْمِعُ ٱلصُّمَّ ٱلدُّعَآءَ إِذَا وَلَّوْا۟ مُدْبِرِينَ۝٨٠

    Innaka la tusmiʿu almawta wala tusmiʿu alssumma aldduʿaa itha wallaw mudbireena

    Kwa hakika wewe huwezi kuwafanya maiti wasikie, wala kuwafanya viziwi wasikie wito, wanapo kwisha geuka kwenda zao.80

    Maelezo
    [80] Ewe Mtume! Hakika wewe huwezi kuwaongoa hao, kwani hao ni kama maiti kwa kuto tambua kitu, na kama viziwi kwa kutosikia. Basi hao hawako tayari kuusikia wito wako kwa vile walivyo shikilia kukupuuza.
  81. وَمَآ أَنتَ بِهَـٰدِى ٱلْعُمْىِ عَن ضَلَـٰلَتِهِمْ ۖ إِن تُسْمِعُ إِلَّا مَن يُؤْمِنُ بِـَٔايَـٰتِنَا فَهُم مُّسْلِمُونَ۝٨١

    Wama anta bihadee alʿumyi ʿan dalalatihim in tusmiʿu illa man yuminu biayatina fahum muslimoona

    Wala huwezi kuwaongoa vipofu waache upotovu wao. Huwezi kuwafanya wasikie isipo kuwa wenye kuziamini Ishara zetu; na hao ndio wat'iifu.81

    Maelezo
    [81] Na wala huwezi kuwaongoa kwenye Haki wale ambao wamepofuka kuona kwao na kutambua kwao. Na huwezi kumfanya asikie ila mwenye kukubali kuziamini Ishara zetu. Hao ndio wenye kut'ii na wenye kuitikia.
  82. ۞ وَإِذَا وَقَعَ ٱلْقَوْلُ عَلَيْهِمْ أَخْرَجْنَا لَهُمْ دَآبَّةً مِّنَ ٱلْأَرْضِ تُكَلِّمُهُمْ أَنَّ ٱلنَّاسَ كَانُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَا لَا يُوقِنُونَ۝٨٢

    Waitha waqaʿa alqawlu ʿalayhim akhrajna lahum dabbatan mina alardi tukallimuhum anna alnnasa kanoo biayatina la yooqinoona

    Na itapo waangukia kauli juu yao, tutawatolea mnyama katika ardhi atakaye wasemeza, ya kuwa watu walikuwa hawana na yakini na Ishara zetu.82

    Maelezo
    [82] Na itapo karibia kutimia ahadi ya Mwenyezi Mungu kuileta Saa ya Kiyama na kuwateremshia makafiri adhabu, Mwenyezi Mungu atawatolea watu mnyama kwenye ardhi atakaye waambia miongoni mwa atakayo sema: Hakika makafiri walikuwa hawaiamini miujiza yetu yote, na pia Siku ya Mwisho. Na hayo waliyo kuwa wakiyakanusha sasa yamekwisha kuwa. Na hichi basi kitisho cha hiyo Saa na yanayo fuatia! Hii ndio tafsiri ya Aya hii kwa dhaahiri ya matamko yake. Na zipo tafsiri mbili nyengine ambazo za hii Aya zinazo weza kuwa: Kwanza ni kuwa makusudio ya "Dabbah" ni yeyote aendaye "yadibbu", katika watu au wengineo. Na hapa inachukuliwa kuwa ni watu, watao kuja kabla ya Kiyama. Na maana yake ni kuwa ikiwateremkia kauli juu yao na adhabu ikathibiti watakuja makundi ya Waumini wakiwaendea, wakienea kote kote, wakizitikisa nguzo za ukafiri. Tafsiri ya pili neno hilo "Dabbah" makusudio yake ni watu waovu, ambao kwa ujinga ni kama wanyama, kama alivyo sema Al As'fahan katika Muqarrarat yake. Na maana yake ni kuwa ikikaribia Siku ya Kiyama, uovu na ufisadi utazidi, na Kiyama wanacho kikanusha makafiri ndio kitakuja. Na hiyo kauli itakuwa, nayo si kauli ya kutamkwa kwa mdomo, lakini kwa kuwa hali yenyewe itakuwa hivyo ni kama iliyo semwa, kama maoni yaliyo kwisha tangulia.
  83. وَيَوْمَ نَحْشُرُ مِن كُلِّ أُمَّةٍ فَوْجًا مِّمَّن يُكَذِّبُ بِـَٔايَـٰتِنَا فَهُمْ يُوزَعُونَ۝٨٣

    Wayawma nahshuru min kulli ommatin fawjan mimman yukaththibu biayatina fahum yoozaʿoona

    Na Siku tutapo kusanya kutoka kila umma kundi katika wanao kadhibisha Ishara zetu, nao watagawanywa mafungu mafungu.83

    Maelezo
    [83] Na ewe Mtume! Kumbuka siku tutapo wakusanya kutoka kila kundi la wenye kukadhibisha Ishara zetu, nao ni hao waongozi wanao fuatwa. Basi hao watachungwa wawe mbele ya kaumu zao kuendea hisabu na malipo.
  84. حَتَّىٰٓ إِذَا جَآءُو قَالَ أَكَذَّبْتُم بِـَٔايَـٰتِى وَلَمْ تُحِيطُوا۟ بِهَا عِلْمًا أَمَّاذَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ۝٨٤

    Hatta itha jaoo qala akaththabtum biayatee walam tuheetoo biha ʿilman ammatha kuntum taʿmaloona

    Hata watakapo fika, atasema (Mwenyezi Mungu): Je! Nyinyi si mlizikanusha Ishara zangu pasipo kuzijua vyema? Au mlikuwa mkifanya nini?84

    Maelezo
    [84] Na pale watakapo simama mbele ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya hisabu, atasema Subhanahu kuwaambia kwa kuwadhili na kuwabinya: Nyinyi mlizikadhibisha Ishara zangu zote, na mkazikataa bila ya kuzingatia wala kufahamu. Na khasa mlikuwa mkitenda nini nanyi hamkuumbwa kwa upuuzi?
  85. وَوَقَعَ ٱلْقَوْلُ عَلَيْهِم بِمَا ظَلَمُوا۟ فَهُمْ لَا يَنطِقُونَ۝٨٥

    Wawaqaʿa alqawlu ʿalayhim bima thalamoo fahum la yantiqoona

    Na kauli itawaangukia juu yao kwa vile walivyo dhulumu. Basi hao hawatasema lolote.85

    Maelezo
    [85] Na adhabu itawateremkia kwa sababu ya kujidhulumu nafsi zao kwa ukafiri. Basi watakuwa hawawezi kujilinda wala kutaka udhuru.
  86. أَلَمْ يَرَوْا۟ أَنَّا جَعَلْنَا ٱلَّيْلَ لِيَسْكُنُوا۟ فِيهِ وَٱلنَّهَارَ مُبْصِرًا ۚ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَـٰتٍ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ۝٨٦

    Alam yaraw anna jaʿalna allayla liyaskunoo feehi waalnnahara mubsiran inna fee thalika laayatin liqawmin yuminoona

    Je! Hawaoni kwamba sisi tumeufanya usiku ili watulie, na mchana wa kuangaza. Hakika katika hayo zipo Ishara kwa watu wanao amini.86

    Maelezo
    [86] Bila ya shaka wameshuhudia kuwa Mwenyezi Mungu ameufanya usiku ili wapate kupumzika, na akaufanya mchana una mwangaza, wapate kushughulikia kutafuta maisha yao. Hakika katika hayo zipo dalili wazi za Ungu wa Mwenyezi Mungu, na Upweke wake, kwa watu wanao zingatia wakaamini.
  87. وَيَوْمَ يُنفَخُ فِى ٱلصُّورِ فَفَزِعَ مَن فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَمَن فِى ٱلْأَرْضِ إِلَّا مَن شَآءَ ٱللَّهُ ۚ وَكُلٌّ أَتَوْهُ دَٰخِرِينَ۝٨٧

    Wayawma yunfakhu fee alssoori fafaziʿa man fee alssamawati waman fee alardi illa man shaa Allahu wakullun atawhu dakhireena

    Na Siku litapo pulizwa baragumu, watahangaika waliomo mbinguni na katika ardhi, ila amtakaye Mwenyezi Mungu. Na wote watamfikia nao ni wanyonge.87

    Maelezo
    [87] Na taja, ewe Mtume, Siku atapo puliza Israfil baragumu kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na watapo ingiwa kiwewe walioko katika mbingu na katika ardhi kwa kitisho cha mpulizo huo, isipo kuwa huyo ambaye Mwenyezi Mungu atamtuliza na akamhifadhi na kitisho. Na viumbe vyote watakuja kwa Mola wao Mlezi nao ni madhalili.
  88. وَتَرَى ٱلْجِبَالَ تَحْسَبُهَا جَامِدَةً وَهِىَ تَمُرُّ مَرَّ ٱلسَّحَابِ ۚ صُنْعَ ٱللَّهِ ٱلَّذِىٓ أَتْقَنَ كُلَّ شَىْءٍ ۚ إِنَّهُۥ خَبِيرٌۢ بِمَا تَفْعَلُونَ۝٨٨

    Watara aljibala tahsabuha jamidatan wahiya tamurru marra alssahabi sunʿa Allahi allathee atqana kulla shayin innahu khabeerun bima tafʿaloona

    Na unaiona milima unaidhunia imetulia; nayo inakwenda kama mwendo wa mawingu. Huo ndio ufundi wa Mwenyezi Mungu aliye tengeneza vilivyo kila kitu. Hakika Yeye anazo khabari za yote myatendayo.88

    Maelezo
    [88] Na unaiona, ewe Mtume, milima na unadhani haitaharaki imetulia tu, lakini kwa hakika inakwenda mbio kama mawingu. Na haya ni katika uundaji wa Mwenyezi Mungu aliye umba kila kitu na akakizua. Hakika Yeye, Subhanahu, ni Mwenye kutimia ujuzi wake kwa yote wayatendayo watu, ya ut'iifu na maasi. Naye atawalipa kwayo. "Na unaiona milima unaidhunia imetulia; nayo inakwenda kama mwendo wa mawingu. Huo ndio ufundi wa Mwenyezi Mungu aliye tengeneza vilivyo kila kitu. Hakika Yeye anazo khabari za yote myatendayo." Aya hii inathibitisha kuwa vitu vyote vinavyo fuata mvutano wa ardhi, kama milima, bahari, na funiko la anga n.k. vinashirikiana na dunia katika mzunguko wake wa kila siku juu ya msumari-kati wake, na mzunguko wake wa kila mwaka kulizunguka jua. Lakini mzunguko huu hauonekani. Ni kama kwenda kwa mawingu angani. Wanao tazama wanayaona, lakini hawasikii sauti yao, wala hawayagusi. Inaonyesha Aya hii tukufu kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu aliye tukuka, ameumba ulimwengu na mipango yake ya kuiendeshea. Naye ni Muweza wa kuifanya hii dunia imetulia tu haizunguki juu ya msumari-kati wake, au akaifanya kuzunguka juu ya msumari-kati wake sawa sawa na kuzunguka kwake kulizunguka jua. Na kwa hivyo ingeli kuwa nusu ya dunia imo kizani totoro kwa muda wa miezi sita, na kwa muda wa miezi sita ikawa nusu ya pili imo katika mwangaza moja kwa moja wa mchana. Na haya yangeli pelekea kuharibika mizani ya joto katika dunia yote. Na kwa hivyo uhai ulioko ungeli toweka duniani. Na Mwenyezi Mungu, Subhanahu wa Taa'la, ndiye aliye panga mpango huu uliopo kwa rehema yake na huruma zake kwa waja wake. Na juu ya kuwa Aristakhoris, mtaalamu wa ilimu ya falaki wa Iskandaria (Alexandria) katika Misri, aliandika (310-230 K.K.) juu ya kuzunguka dunia wenyewe kwa wenyewe, maandishi haya ya kisayansi ya kale yalikuwa hayajawafikia Waarabu wakati wa Mtume Muhammad s.a.w. au kabla yake. Bali wa mwanzo wa kuashiria mambo haya katika wao alikuwa Albiruni katika mwaka 1000 B.K. (Baada ya Kuzaliwa Nabii Isa), baada ya kuingia kufasiriwa vitabu vya ilimu za zamani kwa lugha ya Kiarabu ulio kuweko katika enzi za Banul Abbas. Basi kutokea haya kwa ulimi wa Mtume Muhammad s.a.w. ambaye aliye kuwa hajapata ilimu hiyo, ni dalili kuwa haya yalifunuliwa kwake na Mwenyezi Mungu.
  89. مَن جَآءَ بِٱلْحَسَنَةِ فَلَهُۥ خَيْرٌ مِّنْهَا وَهُم مِّن فَزَعٍ يَوْمَئِذٍ ءَامِنُونَ۝٨٩

    Man jaa bialhasanati falahu khayrun minha wahum min fazaʿin yawmaithin aminoona

    Watakao kuja na mema, watapata bora kuliko hayo. Nao watasalimika na mahangaiko ya Siku hiyo.89

    Maelezo
    [89] Kila mwenye kuleta wema katika dunia, nayo ni Imani na usafi wa ut'iifu, atapata huko Akhera thawabu kubwa kabisa kwa ajili ya aliyo yatanguliza. Na wenye mema haya watasalimika na khofu na kufazaika Siku ya Kiyama.
  90. وَمَن جَآءَ بِٱلسَّيِّئَةِ فَكُبَّتْ وُجُوهُهُمْ فِى ٱلنَّارِ هَلْ تُجْزَوْنَ إِلَّا مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ۝٩٠

    Waman jaa bialssayyiati fakubbat wujoohuhum fee alnnari hal tujzawna illa ma kuntum taʿmaloona

    Na watakao kuja na uovu, basi zitasunukishwa nyuso zao Motoni. Je! Kwani mnalipwa isipo kuwa mliyo kuwa mkiyatenda?90

    Maelezo
    [90] Na kila mwenye kuleta uovu katika dunia - nao ni shirki na maasia - na akafa na hayo, basi malipo ya kundi hili ni kuwa Mwenyezi Mungu atawasukumiza juu ya nyuso zao katika Moto, na wataambiwa hapo kwa kuwatahayarisha: Hakika hii leo hamlipwi ila kwa sababu ya shirki yenu na maasi yenu.
  91. إِنَّمَآ أُمِرْتُ أَنْ أَعْبُدَ رَبَّ هَـٰذِهِ ٱلْبَلْدَةِ ٱلَّذِى حَرَّمَهَا وَلَهُۥ كُلُّ شَىْءٍ ۖ وَأُمِرْتُ أَنْ أَكُونَ مِنَ ٱلْمُسْلِمِينَ۝٩١

    Innama omirtu an aʿbuda rabba hathihi albaldati allathee harramaha walahu kullu shayin waomirtu an akoona mina almuslimeena

    Ama mimi nimeamrishwa nimuabudu Mola Mlezi wa mji huu aliye ufanya ni mtakatifu; na ni vyake Yeye tu vitu vyote. Na nimeamrishwa niwe miongoni mwa Waislamu, wenye kunyenyekea.91

    Maelezo
    [91] Ewe Mtume! Waambie watu: Sikuamrishwa nimuabudu yeyote isipo kuwa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa mji wa Makka aliye utukuza, na akaufanya mtakatifu wenye amani, usio faa kumwagwa damu ndani yake, wala kuwindwa wanyama wake, wala kukatwa miti yake. Na vitu vyote viliomo ulimwenguni ni vya Mwenyezi Mungu kuvimiliki na kuvitawala, na mimi nimeamrishwa niwe katika wanao mnyenyekea Mwenyezi Mungu.
  92. وَأَنْ أَتْلُوَا۟ ٱلْقُرْءَانَ ۖ فَمَنِ ٱهْتَدَىٰ فَإِنَّمَا يَهْتَدِى لِنَفْسِهِۦ ۖ وَمَن ضَلَّ فَقُلْ إِنَّمَآ أَنَا۠ مِنَ ٱلْمُنذِرِينَ۝٩٢

    Waan atluwa alqurana famani ihtada fainnama yahtadee linafsihi waman dalla faqul innama ana mina almunthireena

    Na niisome Qur'ani. Na mwenye kuongoka, basi ameongoka kwa faida ya nafsi yake; na aliye potea - basi sema: Hakika mimi ni miongoni mwa waonyaji.92

    Maelezo
    [92] Na nimeamrishwa nidumishe kuisoma Qur'ani, kwa ibada, na kuzingatia, na kuwaitia watu wafuate yaliomo humo. Basi mwenye kuongoka, akaiamini, na akakufuata wewe, basi kheri ya hayo na malipo yake ni kwa nafsi yake. Na mwenye kupotea asiifuate Haki, na asikufuate wewe, mwambie: Hakika mimi ni Mtume, naonya, na nafikisha Ujumbe tu.
  93. وَقُلِ ٱلْحَمْدُ لِلَّهِ سَيُرِيكُمْ ءَايَـٰتِهِۦ فَتَعْرِفُونَهَا ۚ وَمَا رَبُّكَ بِغَـٰفِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ۝٩٣

    Waquli alhamdu lillahi sayureekum ayatihi fataʿrifoonaha wama rabbuka bighafilin ʿamma taʿmaloona

    Na sema: Alhamdu Lillahi, Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu. Yeye atakuonyesheni Ishara zake, na mtazijua. Na Mola wako Mlezi si mwenye kughafilika na myatendayo.93

    Maelezo
    [93] Na sema, ewe Mtume: Alhamdu Lillahi, Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu kwa neema ya Unabii na Uwongofu. Mwenyezi Mungu atakuonyesheni hapa duniani athari za uwezo wake, na Akhera atakuonyesheni ukweli wa aliyo kwambieni, na mtayajua vilivyo. Wala Mwenyezi Mungu hashindwi kukuhisabieni wala haghafiliki na vitendo vyenu.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Surat An-Naml maana yake ni nini?

An-Naml maana yake ni “Wadudu Chungu”.

Surat An-Naml iko katika juzuu ya ngapi?

Surat An-Naml inaenea katika juzuu za 19 na 20.

Surat An-Naml ina aya ngapi?

Surat An-Naml ina aya 93.

Surat An-Naml ni ya Makka au ya Madina?

Surat An-Naml ni sura ya Makka.

Surat An-Naml ni sura ya ngapi katika Qur’ani?

Ni sura ya 27 katika Qur’ani.

Vyanzo

  • Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
  • Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
  • Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
  • Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
  • Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
  • Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.

Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.

Mipangilio ya kusoma

Fonti ya Qur’ani
Ukubwa wa Kiarabu
100%
Ukubwa wa tafsiri
100%
Mandhari

Ongeza kwenye skrini ya kwanza

ReadSurahFungua ReadSurah kutoka skrini ya kwanza, kwa skrini nzima. Sura ulizosoma hufunguka hata bila intaneti.

  1. Katika Safari, gusa kitufe cha kushiriki (Share). Kwenye iPhone mpya kiko kwenye menyu ya •••.
  2. Gusa “Add to Home Screen”. Huenda ukahitaji kusogeza chini.
  3. Gusa “Add”.