سورة الدخان

Surat Ad-Dukhan kwa Kiswahili

Moshi

Msahafu

Mishary Rashid AlafasyPakua MP3Pakua PDF

Surat Ad-Dukhan (الدخان) ni sura ya 44 katika Qur’ani na ina aya 59. Jina lake lina maana ya “Moshi”. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na iko katika juzuu ya 25.

Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat Ad-Dukhan yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.

Surat Ad-Dukhan kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

  1. حمٓ۝١

    Hameem

    H'a Mim .1

    Maelezo
    [1] H'a Mim. Imeanzia Sura hii kwa baadhi ya harufi za kutamkwa kama ilivyo ada ya Qur'ani katika kufungulia Sura nyingi kwa harufi kama hizi.
  2. وَٱلْكِتَـٰبِ ٱلْمُبِينِ۝٢

    Waalkitabi almubeeni

    Naapa kwa Kitabu kinacho bainisha!2

    Maelezo
    [2] Mwenyezi Mungu anaapa kwa Qur'ani yenye kuweka wazi Dini ya Haki, yenye kuwabainishia watu yaliyo na maslaha ya dunia yao na Akhera yao, ili kujuulisha utukufu wa cheo chake.
  3. إِنَّآ أَنزَلْنَـٰهُ فِى لَيْلَةٍ مُّبَـٰرَكَةٍ ۚ إِنَّا كُنَّا مُنذِرِينَ۝٣

    Inna anzalnahu fee laylatin mubarakatin inna kunna munthireena

    Hakika tumekiteremsha katika usiku ulio barikiwa. Hakika Sisi ni Waonyaji.3

    Maelezo
    [3] Hakika Sisi tumeanza kuiteremsha Qur'ani katika usiku ulio jaa kheri, wenye baraka nyingi, kwani ni mwendo wetu kuonya kwa kuwatuma Mitume na kuteremsha Vitabu.
  4. فِيهَا يُفْرَقُ كُلُّ أَمْرٍ حَكِيمٍ۝٤

    Feeha yufraqu kullu amrin hakeemin

    Katika usiku huu hubainishwa kila jambo la hikima!4

    Maelezo
    [4] Katika usiku huu wenye baraka hupambanuliwa baina ya mambo yote yenye hikima, na Qur'ani ndio kilele cha hikima, na ndio pambanuo baina ya kweli na uwongo. Na kwa hivyo ndio ikateremshwa katika usiku huo.
  5. أَمْرًا مِّنْ عِندِنَآ ۚ إِنَّا كُنَّا مُرْسِلِينَ۝٥

    Amran min ʿindina inna kunna mursileena

    Jambo litokalo kwetu. Hakika Sisi ndio wenye kutuma.5

    Maelezo
    [5] Nakusudia kwa jambo hili, yaani jambo kuu lenye kutoka kwetu kama ilivyo kwisha pita hukumu ya mpango wetu. Kwani ni shani yetu kutuma Mitume kwa Vitabu ili kuwafikishia waja wetu.
  6. رَحْمَةً مِّن رَّبِّكَ ۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلْعَلِيمُ۝٦

    Rahmatan min rabbika innahu huwa alssameeʿu alʿaleemu

    Ni rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia Mwenye kujua.6

    Maelezo
    [6] Kwa ajili ya rehema ya Mola wako Mlezi kwa waja wake, amewatuma Mitume kwa watu wawafikishie uwongofu wake, kwani hakika Yeye peke yake, ndiye Mwenye kusikia kila cha kusikiwa, Mwenye kujua kila cha kujuulikana.
  7. رَبِّ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَآ ۖ إِن كُنتُم مُّوقِنِينَ۝٧

    Rabbi alssamawati waalardi wama baynahuma in kuntum mooqineena

    Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilio baina yao, ikiwa nyinyi mna yakini.7

    Maelezo
    [7] Yeye ndiye Muumba mbingu na ardhi na vilio baina yao, ikiwa nyinyi mna yakini na haki, na mnaifuata, na mnaamini kuwa hakika ndio Yeye Mwenye kuteremsha Qur'ani kuwa ni rehema na uwongofu.
  8. لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ يُحْىِۦ وَيُمِيتُ ۖ رَبُّكُمْ وَرَبُّ ءَابَآئِكُمُ ٱلْأَوَّلِينَ۝٨

    La ilaha illa huwa yuhyee wayumeetu rabbukum warabbu abaikumu alawwaleena

    Hakuna mungu ila Yeye; anahuisha na anafisha- Mola Mlezi wenu na Mola Mlezi wa baba zenu wa mwanzo.8

    Maelezo
    [8] Hapana Mungu isipo kuwa Yeye anaye stahiki kuabudiwa, Yeye peke yake, Mwenye kuhuisha na kufisha. Na Yeye peke yake, ndiye aliye kuumbeni nyinyi na kawaumba baba zenu wa mwanzo.
  9. بَلْ هُمْ فِى شَكٍّ يَلْعَبُونَ۝٩

    Bal hum fee shakkin yalʿaboona

    Lakini wao wanacheza katika shaka.9

    Maelezo
    [9] Lakini makafiri wana shaka na ukweli huu, wamo wakifuata pumbao lao. Na huo ndio mtindo wa watu wa pumbao na michezo, sio mwendo wa watu wa ilimu na yakini.
  10. فَٱرْتَقِبْ يَوْمَ تَأْتِى ٱلسَّمَآءُ بِدُخَانٍ مُّبِينٍ۝١٠

    Fairtaqib yawma tatee alssamao bidukhanin mubeenin

    Basi ingoje siku ambayo mbingu zitakapo leta moshi ulio dhaahiri,10

    Maelezo
    [10] Basi ewe Mtume! Ngojea ukame utapo wateremkia, wakasibiwa na kukonda na udhaifu wa kuona, ikawa mtu huwa anaona baina ya mbingu na ardhi moshi dhaahiri shaahiri, akawa anasikia mvumo wake wala hauoni.
  11. يَغْشَى ٱلنَّاسَ ۖ هَـٰذَا عَذَابٌ أَلِيمٌ۝١١

    Yaghsha alnnasa hatha ʿathabun aleemun

    Utakao wafunika watu: Hii ni adhabu chungu!11

    Maelezo
    [11] Moshi huu utawazunguka wale wanao kadhibisha walio sibiwa na ukame, watasema kwa wingi wa kitisho: Hii ni adhabu kali na chungu!
  12. رَّبَّنَا ٱكْشِفْ عَنَّا ٱلْعَذَابَ إِنَّا مُؤْمِنُونَ۝١٢

    Rabbana ikshif ʿanna alʿathaba inna muminoona

    Mola wetu Mlezi! Tuondolee adhabu hii. Hakika tutaamini.12

    Maelezo
    [12] Kama pia watavyo sema kwa kuomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu: Hakika sisi tutaamini ukituondolea adhabu ya njaa na dhiki.
  13. أَنَّىٰ لَهُمُ ٱلذِّكْرَىٰ وَقَدْ جَآءَهُمْ رَسُولٌ مُّبِينٌ۝١٣

    Anna lahumu alththikra waqad jaahum rasoolun mubeenun

    Nini faida ya kukumbuka kwao? Na alikwisha wafikia Mtume mwenye kubainisha.13

    Maelezo
    [13] Watu hawa watawaidhika vipi, hata watimize hiyo Imani wanayo iahidi wakiondolewa adhabu, na hali Mtume mwenye ujumbe ulio wazi kesha wajia na miujiza yenye kuonyesha ukweli wake, na hayo ndiyo mawaidha makubwa kabisa?
  14. ثُمَّ تَوَلَّوْا۟ عَنْهُ وَقَالُوا۟ مُعَلَّمٌ مَّجْنُونٌ۝١٤

    Thumma tawallaw ʿanhu waqaloo muʿallamun majnoonun

    Na wao wakamgeuzia uso, na wakasema: Huyu amefunzwa, naye ni mwendawazimu.14

    Maelezo
    [14] Kisha wakaacha kumsadiki Mtume aliye tiliwa nguvu na miujiza iliyo wazi, na wakamwambia: Huo uwongo na uzushi! Mara nyengine wakimsingizia kuwa amefunzwa hayo na mtu, na mara nyengine kuwa akili yake imekorogeka.
  15. إِنَّا كَاشِفُوا۟ ٱلْعَذَابِ قَلِيلًا ۚ إِنَّكُمْ عَآئِدُونَ۝١٥

    Inna kashifoo alʿathabi qaleelan innakum ʿaidoona

    Hakika sisi tutaiondoa adhabu kidogo, lakini nyinyi kwa yakini mtarejea vile vile!15

    Maelezo
    [15] Mwenyezi Mungu anawarudi: Sisi hakika tutakuondoleeni adhabu wakati wa duniani, nao ni wakati mchache, lakini nyinyi mtarejea tu, bila ya shaka, yale yale mliyo kuwa mkiyatenda.
  16. يَوْمَ نَبْطِشُ ٱلْبَطْشَةَ ٱلْكُبْرَىٰٓ إِنَّا مُنتَقِمُونَ۝١٦

    Yawma nabtishu albatshata alkubra inna muntaqimoona

    Siku tutayo yashambulia mashambulio makubwa, bila ya shaka Sisi ni wenye kutesa.16

    Maelezo
    [16] Ewe Mtume! Watajie ile siku tutapo washika kwa mshiko mkubwa, wa nguvu. Nasi kwa mshiko huu ndio tunawatesa.
  17. ۞ وَلَقَدْ فَتَنَّا قَبْلَهُمْ قَوْمَ فِرْعَوْنَ وَجَآءَهُمْ رَسُولٌ كَرِيمٌ۝١٧

    Walaqad fatanna qablahum qawma firʿawna wajaahum rasoolun kareemun

    Na hakika kabla ya hawa tuliwafanyia mtihani watu wa Firauni, na aliwafikia Mtume Mtukufu.17

    Maelezo
    [17] Na bila ya shaka tulikwisha wafanyia mtihani, kabla ya makafiri wa Makka, kaumu ya Firauni kwa kuwaitia kwenye Imani, na akawajia Musa, Mtume Mtukufu kwa Mwenyezi Mungu. Wakamkataa kwa inda tu. Na huo ndio mtindo wa hawa washirikina.
  18. أَنْ أَدُّوٓا۟ إِلَىَّ عِبَادَ ٱللَّهِ ۖ إِنِّى لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ۝١٨

    An addoo ilayya ʿibada Allahi innee lakum rasoolun ameenun

    Akasema: Nipeni waja wa Mwenyezi Mungu; kwa hakika mimi kwenu ni Mtume Muaminifu.18

    Maelezo
    [18] Mtume Mtukufu aliwaambia: Nipeni enyi waja wa Mwenyezi Mungu lilio waajibu juu yenu, nalo ni kuitikia wito wangu, kwani mimi ni Mtume nimetumwa makhsusi kwenu, na ni muaminifu katika ujumbe wangu.
  19. وَأَن لَّا تَعْلُوا۟ عَلَى ٱللَّهِ ۖ إِنِّىٓ ءَاتِيكُم بِسُلْطَـٰنٍ مُّبِينٍ۝١٩

    Waan la taʿloo ʿala Allahi innee ateekum bisultanin mubeenin

    Na msimfanyie kiburi Mwenyezi Mungu; hakika mimi nitakuleteeni uthibitisho ulio wazi.19

    Maelezo
    [19] Wala msimfanyie kiburi Mwenyezi Mungu kwa kumkadhibisha Mtume wake, kwani mimi nakuleteeni muujiza ulio wazi wa kubainisha ukweli wa Unabii wangu na Utume wangu.
  20. وَإِنِّى عُذْتُ بِرَبِّى وَرَبِّكُمْ أَن تَرْجُمُونِ۝٢٠

    Wainnee ʿuthtu birabbee warabbikum an tarjumooni

    Nami najikinga kwa Mola wangu Mlezi na ndiye Mola wenu Mlezi pia, ili msinipige mawe.20

    Maelezo
    [20] Na mimi najilinda na Mwenye kuniumba msiweze kuniuwa kwa kunipiga mawe.
  21. وَإِن لَّمْ تُؤْمِنُوا۟ لِى فَٱعْتَزِلُونِ۝٢١

    Wain lam tuminoo lee faiʿtazilooni

    Na ikiwa hamniamini, basi jitengeni nami.21

    Maelezo
    [21] Na ikiwa hamnisadiki basi jitengeni nami, wala msiniudhi.
  22. فَدَعَا رَبَّهُۥٓ أَنَّ هَـٰٓؤُلَآءِ قَوْمٌ مُّجْرِمُونَ۝٢٢

    Fadaʿa rabbahu anna haolai qawmun mujrimoona

    Ndipo akamwomba Mola wake Mlezi: Hakika watu hawa ni wakosefu.22

    Maelezo
    [22] Musa akamwambia Mola wake Mlezi kwa kumshitakia watu wake alipo kata tamaa nao kuwa hawaamini: Hakika watu hawa shauri yao imekwisha fika ukomo katika ukafiri; basi Wewe wafanyie wanalo stahiki.
  23. فَأَسْرِ بِعِبَادِى لَيْلًا إِنَّكُم مُّتَّبَعُونَ۝٢٣

    Faasri biʿibadee laylan innakum muttabaʿoona

    Mwenyezi Mungu akasema: Basi nenda na waja wangu usiku. Kwa yakini mtafuatwa.23

    Maelezo
    [23] (Naye Musa akaambiwa:) Toka na Waumini usiku usiku kwa kificho, wasije kukupateni, kwani Firauni na askari wake watakufuateni pindi wakijua, wakukamateni.
  24. وَٱتْرُكِ ٱلْبَحْرَ رَهْوًا ۖ إِنَّهُمْ جُندٌ مُّغْرَقُونَ۝٢٤

    Waotruki albahra rahwan innahum jundun mughraqoona

    Na iache bahari vivyo hivyo imeachana, hakika wao hao ni jeshi litakalo zamishwa.24

    Maelezo
    [24] Na iache bahari imetulia kama ilivyo baada ya kwisha pigwa kwa fimbo, wapate kuingia hao wanao kanya; kwani wao watazama tu, hapana hivi wala hivi.
  25. كَمْ تَرَكُوا۟ مِن جَنَّـٰتٍ وَعُيُونٍ۝٢٥

    Kam tarakoo min jannatin waʿuyoonin

    Mabustani mangapi, na chemchem ngapi waliziacha!25

    Maelezo
    [25] Hao watu wa Firauni baada ya kuzama kwao waliacha mabustani mengi yenye kunawiri, na chemchem zinazo tiririka maji yake,
  26. وَزُرُوعٍ وَمَقَامٍ كَرِيمٍ۝٢٦

    Wazurooʿin wamaqamin kareemin

    Na mimea na vyeo vitukufu!26

    Maelezo
    [26] Na makulima ya namna kwa namna, na makaazi mazuri mazuri,
  27. وَنَعْمَةٍ كَانُوا۟ فِيهَا فَـٰكِهِينَ۝٢٧

    Wanaʿmatin kanoo feeha fakiheena

    Na neema walizo kuwa wakijistareheshea!27

    Maelezo
    [27] Na maisha ya raha na starehe, waliyo kuwa wakiyaonea utamu.
  28. كَذَٰلِكَ ۖ وَأَوْرَثْنَـٰهَا قَوْمًا ءَاخَرِينَ۝٢٨

    Kathalika waawrathnaha qawman akhareena

    Ndio hivyo! Na tukawarithisha haya watu wenginewe.28

    Maelezo
    [28] Mfano wa adhabu hiyo Mwenyezi Mungu humuadhibu mwenye kwenda kinyume na amri yake, na akatoka katika ut'iifu wake, na humwondolea neema yule mwenye nayo akawapa watu wenginewe wasio kuwa na makhusiano nao yoyote, la ya ujamaa wala dini.
  29. فَمَا بَكَتْ عَلَيْهِمُ ٱلسَّمَآءُ وَٱلْأَرْضُ وَمَا كَانُوا۟ مُنظَرِينَ۝٢٩

    Fama bakat ʿalayhimu alssamao waalardu wama kanoo munthareena

    La mbingu wala ardhi hazikuwalilia, wala hawakupewa muhula.29

    Maelezo
    [29] Basi la mbingu wala ardhi hazikuwahuzunukia ilipo wanyakua adhabu, jinsi ilivyo haribika hali yao; wala hawakungojewa watubu, wala hawakupewa muhula wapate kudiriki taksiri yao, kwa jinsi walivyo dharauliwa!
  30. وَلَقَدْ نَجَّيْنَا بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ مِنَ ٱلْعَذَابِ ٱلْمُهِينِ۝٣٠

    Walaqad najjayna banee israeela mina alʿathabi almuheeni

    Na bila ya shaka tuliwaokoa Wana wa Israili katika adhabu ya kuwadhalilisha,30

    Maelezo
    [30] Na kwa hakika Mwenyezi Mungu aliwaokoa Wana wa Israili na adhabu ya kuwadhalilisha.
  31. مِن فِرْعَوْنَ ۚ إِنَّهُۥ كَانَ عَالِيًا مِّنَ ٱلْمُسْرِفِينَ۝٣١

    Min firʿawna innahu kana ʿaliyan mina almusrifeena

    Ya Firauni. Hakika yeye alikuwa jeuri katika wenye kupindukia mipaka.31

    Maelezo
    [31] Aliwaokoa kwa Firauni. Hakika Firauni alikuwa jeuri kwa watu wake, amepita mipaka kwa shari na uasi.
  32. وَلَقَدِ ٱخْتَرْنَـٰهُمْ عَلَىٰ عِلْمٍ عَلَى ٱلْعَـٰلَمِينَ۝٣٢

    Walaqadi ikhtarnahum ʿala ʿilmin ʿala alʿalameena

    Na tuliwakhiari kwa ujuzi wetu kuliko walimwengu wenginewe.32

    Maelezo
    [32] Ninaapa: Tuliwakhiari Wana wa Israili kwa kuwa tuliwajua kwamba wao wana stahiki kuteuliwa kuliko watu wengine wote wa zama zao. Kwa hivyo tukawatuma miongoni mwao Manabii wengi kwa kuwa tulijua hali zao.
  33. وَءَاتَيْنَـٰهُم مِّنَ ٱلْـَٔايَـٰتِ مَا فِيهِ بَلَـٰٓؤٌا۟ مُّبِينٌ۝٣٣

    Waataynahum mina alayati ma feehi balaon mubeenun

    Na tukawapa katika ishara zenye majaribio yaliyo wazi.33

    Maelezo
    [33] Na Mwenyezi Mungu akawaletea katika mkono wa Musa dalili kadhaa wa kadhaa za kuwatia wao katika mitihani iliyo wazi.
  34. إِنَّ هَـٰٓؤُلَآءِ لَيَقُولُونَ۝٣٤

    Inna haolai layaqooloona

    Hakika hawa wanasema:34

    Maelezo
    [34] Hakika hawa wanao kadhibisha kufufuliwa bila ya shaka wanasema: Hapana kufa ila kwa haya haya mauti yetu ya kwanza ya duniani, wala sisi hatutafufuliwa tena.
  35. إِنْ هِىَ إِلَّا مَوْتَتُنَا ٱلْأُولَىٰ وَمَا نَحْنُ بِمُنشَرِينَ۝٣٥

    In hiya illa mawtatuna aloola wama nahnu bimunshareena

    Hapana ila kufa kwetu mara ya kwanza tu, wala sisi hatufufuliwi.35

    Maelezo
    [35] Hakika hawa wanao kadhibisha kufufuliwa bila ya shaka wanasema: Hapana kufa ila kwa haya haya mauti yetu ya kwanza ya duniani, wala sisi hatutafufuliwa tena.
  36. فَأْتُوا۟ بِـَٔابَآئِنَآ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ۝٣٦

    Fatoo biabaina in kuntum sadiqeena

    Basi warudisheni baba zetu, ikiwa nyinyi mnasema kweli.36

    Maelezo
    [36] Na wao humwambia Mtume wa Mwenyezi Mungu na Waumini: Ikiwa nyinyi mnasema kweli katika madai yenu kwamba Mola wenu Mlezi anahuisha wafu kwa ajili ya hisabu katika Akhera, basi upesi upesi tufufulieni baba zetu walio kwisha kufa, kwa kumwomba huyo Mola wenu Mlezi!
  37. أَهُمْ خَيْرٌ أَمْ قَوْمُ تُبَّعٍ وَٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ أَهْلَكْنَـٰهُمْ ۖ إِنَّهُمْ كَانُوا۟ مُجْرِمِينَ۝٣٧

    Ahum khayrun am qawmu tubbaʿin waallatheena min qablihim ahlaknahum innahum kanoo mujrimeena

    Je! Ni wao bora au watu wa Tubbaa' na walio kuwa kabla yao? Tuliwaangamiza. Hakika hao walikuwa wakosefu.37

    Maelezo
    [37] Je! Makafiri wa Makka wanawashinda kaumu ya Tubbaa' na walio watangulia kwa nguvu, na ulinzi, na utawala, na mambo yote ya kidunia? Ewe Muhammad! Hao washirikina wa kaumu yako hawawashindi hao kwa nguvu, na hao Sisi tuliwateketeza katika dunia kwa ukafiri wao na madhambi yao. Basi nawawazingatie!
  38. وَمَا خَلَقْنَا ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا لَـٰعِبِينَ۝٣٨

    Wama khalaqna alssamawati waalarda wama baynahuma laʿibeena

    Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyomo baina yake kwa mchezo.38

    Maelezo
    [38] Na Mwenyezi Mungu hakuumba mbingu na ardhi na viliomo baina yao bila ya hikima.
  39. مَا خَلَقْنَـٰهُمَآ إِلَّا بِٱلْحَقِّ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ۝٣٩

    Ma khalaqnahuma illa bialhaqqi walakinna aktharahum la yaʿlamoona

    Hatukuviumba hivyo ila kwa Haki, lakini wengi wao hawajui.39

    Maelezo
    [39] Hatukuziumba hizo ila kwa umbo lilio ambatana na hikima, kwa nidhamu iliyo thibiti yenye kuonyesha ushahidi wa kuwepo Mwenyezi Mungu wa pekee, Mwenye uwezo. Lakini wengi wa hawa wameghafilika, wamo katika upofu, hawazioni dalili hizi.
  40. إِنَّ يَوْمَ ٱلْفَصْلِ مِيقَـٰتُهُمْ أَجْمَعِينَ۝٤٠

    Inna yawma alfasli meeqatuhum ajmaʿeena

    Hakika siku ya Uamuzi ni wakati ulio wekwa kwa wao wote.40

    Maelezo
    [40] Hakika siku ya hukumu kupambanua baina ya mwenye haki na asiye na haki, ni wakati walio ahidiwa wote.
  41. يَوْمَ لَا يُغْنِى مَوْلًى عَن مَّوْلًى شَيْـًٔا وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ۝٤١

    Yawma la yughnee mawlan ʿan mawlan shayan wala hum yunsaroona

    Siku ambayo rafiki hatamfaa rafiki yake kwa chochote, wala hawatanusuriwa.41

    Maelezo
    [41] Siku ambayo jamaa hawezi kumtetea jamaa yake, wala rafiki kumtetea rafiki yake kwa lolote, hata kwa uchache wa adhabu. Wala wao hawatanusuriwa nafsi zao mbele ya Mwenyezi Mungu.
  42. إِلَّا مَن رَّحِمَ ٱللَّهُ ۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ۝٤٢

    Illa man rahima Allahu innahu huwa alʿazeezu alrraheemu

    Isipo kuwa atakaye mrehemu Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu.42

    Maelezo
    [42] Lakini wale ambao Mwenyezi Mungu amewarehemu, miongoni mwa Waumini, Mwenyezi Mungu atawasamehe, na atawapa ruhusa ya uombezi waweze kuwaombea wenginewe. Hakika Yeye ndiye Mwenye kushinda kila kitu, Mwenye kuwarehemu waja wake Waumini.
  43. إِنَّ شَجَرَتَ ٱلزَّقُّومِ۝٤٣

    Inna shajarata alzzaqqoomi

    Hakika Mti wa Zaqqum,43

    Maelezo
    [43] Hakika mti wa Zaqqumu unao juulikana kwa ubaya wa sura yake, na ukarihi kuula kwake, na harufu yake, ni chakula cha wakosefu wenye madhambi mengi.
  44. طَعَامُ ٱلْأَثِيمِ۝٤٤

    Taʿamu alatheemi

    Ni chakula cha mwenye dhambi.44

    Maelezo
    [44] Hakika mti wa Zaqqumu unao juulikana kwa ubaya wa sura yake, na ukarihi kuula kwake, na harufu yake, ni chakula cha wakosefu wenye madhambi mengi.
  45. كَٱلْمُهْلِ يَغْلِى فِى ٱلْبُطُونِ۝٤٥

    Kaalmuhli yaghlee fee albutooni

    Kama shaba iliyo yayushwa, hutokota matumboni45

    Maelezo
    [45] Utamu wake kama maadeni iliyo yayushwa kwa moto, inatokota matumboni kama yanavyo tokota maji yanayo chemshwa.
  46. كَغَلْىِ ٱلْحَمِيمِ۝٤٦

    Kaghalyi alhameemi

    Kama kutokota kwa maji ya moto.46

    Maelezo
    [46] Utamu wake kama maadeni iliyo yayushwa kwa moto, inatokota matumboni kama yanavyo tokota maji yanayo chemshwa.
  47. خُذُوهُ فَٱعْتِلُوهُ إِلَىٰ سَوَآءِ ٱلْجَحِيمِ۝٤٧

    Khuthoohu faiʿtiloohu ila sawai aljaheemi

    (Itasemwa:) Mkamateni na mtupeni katikati ya Jahannamu!47

    Maelezo
    [47] Enyi Mazabania wa Jahannamu (Walinzi wa Motoni)! Mkamateni huyu mkosefu, mwenye dhambi, mumtokomeze kwa nguvu na ukali mpaka katikati ya Jahannamu!
  48. ثُمَّ صُبُّوا۟ فَوْقَ رَأْسِهِۦ مِنْ عَذَابِ ٱلْحَمِيمِ۝٤٨

    Thumma subboo fawqa rasihi min ʿathabi alhameemi

    Kisha mmwagieni juu ya kichwa chake adhabu ya maji yanayo chemka.48

    Maelezo
    [48] Kisha mmiminieni juu ya kichwa chake maji ya moto makali kuzidi kumuadhibu na kumtesa.
  49. ذُقْ إِنَّكَ أَنتَ ٱلْعَزِيزُ ٱلْكَرِيمُ۝٤٩

    Thuq innaka anta alʿazeezu alkareemu

    Onja! Ati wewe ndiye mwenye nguvu, mtukufu!49

    Maelezo
    [49] Ataambiwa kwa kejeli na maskhara: Onja hii adhabu kali, kwani ati wewe si ndiye mtukufu mwenye nguvu katika kaumu yako, ndiye mheshimiwa unavyo jiona mwenyewe!
  50. إِنَّ هَـٰذَا مَا كُنتُم بِهِۦ تَمْتَرُونَ۝٥٠

    Inna hatha ma kuntum bihi tamtaroona

    Hakika haya ndiyo mliyo kuwa mkiyatilia shaka.50

    Maelezo
    [50] Hapana shaka hii adhabu mnayo ipata ni kweli yenye kuwa, na ndiyo mliyo kuwa mkiibisha duniani, na mkiitilia shaka kuwa haiwi.
  51. إِنَّ ٱلْمُتَّقِينَ فِى مَقَامٍ أَمِينٍ۝٥١

    Inna almuttaqeena fee maqamin ameenin

    Hakika wachamngu watakuwa katika mahali pa amani,51

    Maelezo
    [51] Hakika hao ambao wamejikinga nafsi zao na maasi kwa kufuata ut'iifu wa Mwenyezi Mungu wapo pahala patukufu ambapo ndani yake wao wanajipatia amani kwa nafsi zao.
  52. فِى جَنَّـٰتٍ وَعُيُونٍ۝٥٢

    Fee jannatin waʿuyoonin

    Katika mabustani na chemchem,52

    Maelezo
    [52] Katika mabustani watapo kuwa ndani yake wanastarehe, na chemchem za maji yanayo pita chini yao, kwa sababu ya kuwakirimu wao kwa kutukuza hizo neema zao.
  53. يَلْبَسُونَ مِن سُندُسٍ وَإِسْتَبْرَقٍ مُّتَقَـٰبِلِينَ۝٥٣

    Yalbasoona min sundusin waistabraqin mutaqabileena

    Watavaa hariri nyepesi na hariri nzito wakikabiliana,53

    Maelezo
    [53] Wakivaa humo hariri nyepesi na nzito kuzidi kuongeza mapambo yao, nao wakielekeana katika majlisi zao, ili kutimiza starehe.
  54. كَذَٰلِكَ وَزَوَّجْنَـٰهُم بِحُورٍ عِينٍ۝٥٤

    Kathalika wazawwajnahum bihoorin ʿeenin

    Hivi ndivyo itakavyo kuwa, na tutawaoza mahurilaini.54

    Maelezo
    [54] Na pamoja na malipo haya tutawaoza huko Peponi mahurulaini, ambao huwezi kuwachanganyia jicho kwa hadi ya uzuri wao na ukubwa wa macho yao.
  55. يَدْعُونَ فِيهَا بِكُلِّ فَـٰكِهَةٍ ءَامِنِينَ۝٥٥

    Yadʿoona feeha bikulli fakihatin amineena

    Humo watataka kila aina ya matunda, na wakae kwa amani.55

    Maelezo
    [55] Nao huko Peponi watataka kila tunda wanalo litamani, kwa kujua kuwa hayatawaletea vimbizi, wala hayatakwisha, wala hayataadimika.
  56. لَا يَذُوقُونَ فِيهَا ٱلْمَوْتَ إِلَّا ٱلْمَوْتَةَ ٱلْأُولَىٰ ۖ وَوَقَىٰهُمْ عَذَابَ ٱلْجَحِيمِ۝٥٦

    La yathooqoona feeha almawta illa almawtata aloola wawaqahum ʿathaba aljaheemi

    Humo hawataonja mauti ila mauti yale ya kwanza, na (Mwenyezi Mungu) atawalinda na adhabu ya Jahannamu,56

    Maelezo
    [56] Huko Peponi hawataonja mauti baada ya mauti ya kwanza waliyo kwisha yaonja duniani ulipo kwisha muda wao wa kuishi, na Mola wao Mlezi atawalinda na adhabu ya Motoni.
  57. فَضْلًا مِّن رَّبِّكَ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلْفَوْزُ ٱلْعَظِيمُ۝٥٧

    Fadlan min rabbika thalika huwa alfawzu alʿatheemu

    Kuwa ni fadhila zitokazo kwa Mola wako Mlezi. Huko ndiko kufuzu kukubwa.57

    Maelezo
    [57] Kuhifadhiwa kwao na adhabu ni fadhila na hisani ya Muumba wako. Kuhifadhiwa huko na adhabu na kuingizwa kwao Peponi ndio hadi ya mwisho ya kufuzu kulio kukubwa.
  58. فَإِنَّمَا يَسَّرْنَـٰهُ بِلِسَانِكَ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ۝٥٨

    Fainnama yassarnahu bilisanika laʿallahum yatathakkaroona

    Basi tumeifanya nyepesi hii Qur'ani kwa ulimi wako, ili wapate kukumbuka.58

    Maelezo
    [58] Basi hakika Sisi tumekufanyia wepesi kuisoma Qur'ani na kuifikisha kama ilivyo teremka kwa lugha yako, na lugha yao, ili wapate kuwaidhika, na waiamini, na watende kwa mujibu yaliomo ndani yake.
  59. فَٱرْتَقِبْ إِنَّهُم مُّرْتَقِبُونَ۝٥٩

    Fairtaqib innahum murtaqiboona

    Ngoja tu, na wao wangoje pia.59

    Maelezo
    [59] Basi wewe yangojee hayo yatakayo wafika, na wao pia wanangojea yatakayo kufika wewe na huo wito wako, mambo yakibadilika.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Surat Ad-Dukhan maana yake ni nini?

Ad-Dukhan maana yake ni “Moshi”.

Surat Ad-Dukhan iko katika juzuu ya ngapi?

Surat Ad-Dukhan iko katika juzuu ya 25.

Surat Ad-Dukhan ina aya ngapi?

Surat Ad-Dukhan ina aya 59.

Surat Ad-Dukhan ni ya Makka au ya Madina?

Surat Ad-Dukhan ni sura ya Makka.

Surat Ad-Dukhan ni sura ya ngapi katika Qur’ani?

Ni sura ya 44 katika Qur’ani.

Vyanzo

  • Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
  • Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
  • Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
  • Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
  • Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
  • Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.

Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.

Mipangilio ya kusoma

Fonti ya Qur’ani
Ukubwa wa Kiarabu
100%
Ukubwa wa tafsiri
100%
Mandhari

Ongeza kwenye skrini ya kwanza

ReadSurahFungua ReadSurah kutoka skrini ya kwanza, kwa skrini nzima. Sura ulizosoma hufunguka hata bila intaneti.

  1. Katika Safari, gusa kitufe cha kushiriki (Share). Kwenye iPhone mpya kiko kwenye menyu ya •••.
  2. Gusa “Add to Home Screen”. Huenda ukahitaji kusogeza chini.
  3. Gusa “Add”.