سورة الحجرات

Surat Al-Hujurat kwa Kiswahili

Vyumba

Msahafu

Mishary Rashid AlafasyPakua MP3Pakua PDF

Surat Al-Hujurat (الحجرات) ni sura ya 49 katika Qur’ani na ina aya 18. Jina lake lina maana ya “Vyumba”. Ni sura ya Madina, iliyoteremshwa Madina baada ya Hijra, na iko katika juzuu ya 26.

Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat Al-Hujurat yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.

Surat Al-Hujurat kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

  1. يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا تُقَدِّمُوا۟ بَيْنَ يَدَىِ ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ ۖ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ۝١

    Ya ayyuha allatheena amanoo la tuqaddimoo bayna yadayi Allahi warasoolihi waittaqoo Allaha inna Allaha sameeʿun ʿaleemun

    Enyi mlio amini! Msitangulie mbele ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.1

    Maelezo
    [1] Enyi mlio amini! Msitangulie na kulikata jambo lolote la kidini na la kidunia bila ya kukuamrisheni Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na jiwekeeni kinga ya nafsi zenu isikupateni adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa kufuata sharia yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia baraabara yote mnayo yasema, ni Mwenye kuyajua vilivyo mambo yote.
  2. يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا تَرْفَعُوٓا۟ أَصْوَٰتَكُمْ فَوْقَ صَوْتِ ٱلنَّبِىِّ وَلَا تَجْهَرُوا۟ لَهُۥ بِٱلْقَوْلِ كَجَهْرِ بَعْضِكُمْ لِبَعْضٍ أَن تَحْبَطَ أَعْمَـٰلُكُمْ وَأَنتُمْ لَا تَشْعُرُونَ۝٢

    Ya ayyuha allatheena amanoo la tarfaʿoo aswatakum fawqa sawti alnnabiyyi wala tajharoo lahu bialqawli kajahri baʿdikum libaʿdin an tahbata aʿmalukum waantum la tashʿuroona

    Enyi mlio amini! Msinyanyue sauti zenu kuliko sauti ya Nabii, wala msiseme naye kwa kelele kama mnavyo semezana nyinyi kwa nyinyi, visije vitendo vyenu vikaharibika, na hali hamtambui.2

    Maelezo
    [2] Enyi mlio amini! Msinyanyue sauti zenu juu ya sauti ya Nabii anapo sema na nyinyi mnasema. Wala msipambanishe sauti zenu na sauti yake, kama mnapo semezana nyinyi kwa nyinyi, kwa kuchelea visiharibike vitendo vyenu bila ya nyinyi wenyewe kutambua.
  3. إِنَّ ٱلَّذِينَ يَغُضُّونَ أَصْوَٰتَهُمْ عِندَ رَسُولِ ٱللَّهِ أُو۟لَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ ٱمْتَحَنَ ٱللَّهُ قُلُوبَهُمْ لِلتَّقْوَىٰ ۚ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَأَجْرٌ عَظِيمٌ۝٣

    Inna allatheena yaghuddoona aswatahum ʿinda rasooli Allahi olaika allatheena imtahana Allahu quloobahum lilttaqwa lahum maghfiratun waajrun ʿatheemun

    Kwa hakika wanao teremsha sauti zao mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, hao ndio Mwenyezi Mungu amezisafisha nyoyo zao kwa uchamngu. Hao watakuwa na maghfira na ujira mkubwa.3

    Maelezo
    [3] Hakika wanao teremsha sauti zao katika baraza ya Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa kumtukuza yeye, hao peke yao ndio Mwenyezi Mungu amezisafisha nyoyo zao kwa uchamngu. Kwa wengineo si hivyo. Nao watapata msamaha mkubwa kufutiwa madhambi yao, na thawabu zilizo fika ukomo wa kufika kwake.
  4. إِنَّ ٱلَّذِينَ يُنَادُونَكَ مِن وَرَآءِ ٱلْحُجُرَٰتِ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْقِلُونَ۝٤

    Inna allatheena yunadoonaka min warai alhujurati aktharuhum la yaʿqiloona

    Hakika hao wanao kuita nawe uko nyuma ya vyumba, wengi wao hawana akili.4

    Maelezo
    [4] Hakika hao wanao kuita kwa makelele nawe uko vyumbani mwako wengi wao hawafahamu yanayo takikakana kukuhishimu na kukutukuza kwa makamo yako.
  5. وَلَوْ أَنَّهُمْ صَبَرُوا۟ حَتَّىٰ تَخْرُجَ إِلَيْهِمْ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُمْ ۚ وَٱللَّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ۝٥

    Walaw annahum sabaroo hatta takhruja ilayhim lakana khayran lahum waAllahu ghafoorun raheemun

    Na lau wao wangeli ngojea mpaka uwatokee ingeli kuwa kheri kwao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira, Mwenye kurehemu.5

    Maelezo
    [5] Na lau kuwa hao wangeli ngojea, kwa kukufanyia adabu, mpaka ukatoka, bila ya shaka ingeli kuwa ni bora zaidi katika Dini yao. Na Mwenyezi Mungu ni Mkubwa wa kusamehe, Mwenye rehema kunjufu.
  6. يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِن جَآءَكُمْ فَاسِقٌۢ بِنَبَإٍ فَتَبَيَّنُوٓا۟ أَن تُصِيبُوا۟ قَوْمًۢا بِجَهَـٰلَةٍ فَتُصْبِحُوا۟ عَلَىٰ مَا فَعَلْتُمْ نَـٰدِمِينَ۝٦

    Ya ayyuha allatheena amanoo in jaakum fasiqun binabain fatabayyanoo an tuseeboo qawman bijahalatin fatusbihoo ʿala ma faʿaltum nadimeena

    Enyi mlio amini! Akikujieni mpotovu na khabari yoyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kuto jua, na mkawa tena wenye kujuta kwa mliyo yatenda.6

    Maelezo
    [6] Enyi mlio amini! Akikujieni mtu ambaye yuko nje ya sharia ya Mwenyezi Mungu akakupeni khabari yoyote, basi chungueni mjue ukweli wake, kwa kuchelea msije mkawaletea watu madhara, kwa kutojua hali yao. Hapo tena baada ya kwisha dhihiri kuwa hawana makosa mkaingia katika majuto ya daima, mkatamani yasingeli kuwa.
  7. وَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّ فِيكُمْ رَسُولَ ٱللَّهِ ۚ لَوْ يُطِيعُكُمْ فِى كَثِيرٍ مِّنَ ٱلْأَمْرِ لَعَنِتُّمْ وَلَـٰكِنَّ ٱللَّهَ حَبَّبَ إِلَيْكُمُ ٱلْإِيمَـٰنَ وَزَيَّنَهُۥ فِى قُلُوبِكُمْ وَكَرَّهَ إِلَيْكُمُ ٱلْكُفْرَ وَٱلْفُسُوقَ وَٱلْعِصْيَانَ ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلرَّٰشِدُونَ۝٧

    Waiʿlamoo anna feekum rasoola Allahi law yuteeʿukum fee katheerin mina alamri laʿanittum walakinna Allaha habbaba ilaykumu aleemana wazayyanahu fee quloobikum wakarraha ilaykumu alkufra waalfusooqa waalʿisyana olaika humu alrrashidoona

    Na jueni kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu yuko nanyi. Lau angeli kut'iini katika mambo mengi, bila ya shaka mngeli taabika. Lakini Mwenyezi Mungu amekupendezeeni Imani, na akaipamba katika nyoyo zenu, na amekufanyeni muuchukie ukafiri, na upotovu, na uasi. Hao ndio walio ongoka!7

    Maelezo
    [7] Na jueni, enyi Waumini, kwamba Mtume yuko nanyi. Basi mkadirieni kama anavyo stahiki kadiri yake, na msadikini. Lau yeye angeli wafuata walio wachache wa Imani kati yenu katika mambo mengi, basi hapana shaka mngeli ingia katika mashaka na hilaki. Lakini Mwenyezi Mungu amewapendezesha Imani wale walio kamilika katika nyinyi, na akaipamba katika nyoyo zenu. Basi jilindeni na kujipamba na yasiyo takikana. Na amekufanyeni mchukie kukufuru neema za Mwenyezi Mungu, na kutokana na sharia zake, na kwenda kinyume na amri zake. Hao tu, peke yao, ndio wanao ijua njia ya uwongofu na wameishikilia.
  8. فَضْلًا مِّنَ ٱللَّهِ وَنِعْمَةً ۚ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ۝٨

    Fadlan mina Allahi waniʿmatan waAllahu ʿaleemun hakeemun

    Kwa fadhila za Mwenyezi Mungu na neema zake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hikima.8

    Maelezo
    [8] Na hiyo ni fadhila tukufu na neema kubwa ya Mwenyezi Mungu juu yao. Na Mwenyezi Mungu amekizunguka kila kitu kwa ujuzi wake, ni Mwenye hikima ya kupita mpaka katika kuendesha kila jambo.
  9. وَإِن طَآئِفَتَانِ مِنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ ٱقْتَتَلُوا۟ فَأَصْلِحُوا۟ بَيْنَهُمَا ۖ فَإِنۢ بَغَتْ إِحْدَىٰهُمَا عَلَى ٱلْأُخْرَىٰ فَقَـٰتِلُوا۟ ٱلَّتِى تَبْغِى حَتَّىٰ تَفِىٓءَ إِلَىٰٓ أَمْرِ ٱللَّهِ ۚ فَإِن فَآءَتْ فَأَصْلِحُوا۟ بَيْنَهُمَا بِٱلْعَدْلِ وَأَقْسِطُوٓا۟ ۖ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلْمُقْسِطِينَ۝٩

    Wain taifatani mina almumineena iqtataloo faaslihoo baynahuma fain baghat ihdahuma ʿala alokhra faqatiloo allatee tabghee hatta tafeea ila amri Allahi fain faat faaslihoo baynahuma bialʿadli waaqsitoo inna Allaha yuhibbu almuqsiteena

    Na ikiwa makundi mawili katika Waumini yanapigana, basi yapatanisheni. Na likiwa moja la hao linamdhulumu mwenzie, basi lipigeni linalo dhulumu mpaka lirejee kwenye amri ya Mwenyezi Mungu. Na likirudi basi yapatanisheni kwa uadilifu. Na hukumuni kwa haki. Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wanao hukumu kwa haki.9

    Maelezo
    [9] Na ikiwa makundi mawili ya Waumini yanapigana, basi enyi Waumini, yapatanisheni. Ikiwa moja ndilo linalishambulia la pili, na likakataa kupatanishwa, basi lipigeni hilo linalo shambulia, mpaka lirejee kwenye hukumu ya Mwenyezi Mungu. Likirejea basi wapatanisheni kwa insafu. Na fanyeni uadilifu baina ya watu wote katika kila jambo. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wenye kufanya uadilifu.
  10. إِنَّمَا ٱلْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ فَأَصْلِحُوا۟ بَيْنَ أَخَوَيْكُمْ ۚ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ۝١٠

    Innama almuminoona ikhwatun faaslihoo bayna akhawaykum waittaqoo Allaha laʿallakum turhamoona

    Hakika Waumini ni ndugu, basi patanisheni baina ya ndugu zenu, na mcheni Mwenyezi Mungu ili mrehemewe.10

    Maelezo
    [10] Hakika wote wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake ni ndugu, Imani imezifanya nyoyo zao pamoja. Basi patanisheni baina ya ndugu zenu kwa kufuata udugu wa Imani. Na jiwekeeni nafsi zenu kinga cha kukinga adhabu ya Mwenyezi Mungu, kwa kufuata amri yake, na kuepuka anayo yakataza, na huku mkitaraji Mwenyezi Mungu akurehemuni kwa uchamngu wenu.
  11. يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا يَسْخَرْ قَوْمٌ مِّن قَوْمٍ عَسَىٰٓ أَن يَكُونُوا۟ خَيْرًا مِّنْهُمْ وَلَا نِسَآءٌ مِّن نِّسَآءٍ عَسَىٰٓ أَن يَكُنَّ خَيْرًا مِّنْهُنَّ ۖ وَلَا تَلْمِزُوٓا۟ أَنفُسَكُمْ وَلَا تَنَابَزُوا۟ بِٱلْأَلْقَـٰبِ ۖ بِئْسَ ٱلِٱسْمُ ٱلْفُسُوقُ بَعْدَ ٱلْإِيمَـٰنِ ۚ وَمَن لَّمْ يَتُبْ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلظَّـٰلِمُونَ۝١١

    Ya ayyuha allatheena amanoo la yaskhar qawmun min qawmin ʿasa an yakoonoo khayran minhum wala nisaon min nisain ʿasa an yakunna khayran minhunna wala talmizoo anfusakum wala tanabazoo bialalqabi bisa alismu alfusooqu baʿda aleemani waman lam yatub faolaika humu alththalimoona

    Enyi mlio amini! Wanaume wasiwadharau wanaume wenzao, wala wanawake wasiwadharau wanawake wenzao. Huenda hao wakawa bora kuliko wao. Wala msivunjiane hishima, wala msiitane kwa majina ya kejeli. Ni uovu kutumia jina baya baada ya kwisha amini. Na wasio tubu, hao ndio wenye kudhulumu.11

    Maelezo
    [11] Enyi mlio amini! Wanaume katika nyinyi wasiwadharau wanaume wenginewe, huenda hao mbele ya Mwenyezi Mungu wakawa bora kuliko wao. Wala wanawake Waumini wasiwadharau wanawake wenzao, huenda pengine wakawa hao ni bora kwa Mwenyezi Mungu kuliko wao. Wala msifanye kuaibishana nyinyi kwa nyinyi, wala mtu asimwite mwenzie kwa jina la kumuudhi. Ni uovu mno kwa Waumini kutajwa kwa upotovu baada ya kwisha sifika kwa Imani. Na wasio rudi wakaacha waliyo katazwa, basi hao peke yao ndio walio jidhulumu nafsi zao na wakawadhulumu wengineo.
  12. يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ٱجْتَنِبُوا۟ كَثِيرًا مِّنَ ٱلظَّنِّ إِنَّ بَعْضَ ٱلظَّنِّ إِثْمٌ ۖ وَلَا تَجَسَّسُوا۟ وَلَا يَغْتَب بَّعْضُكُم بَعْضًا ۚ أَيُحِبُّ أَحَدُكُمْ أَن يَأْكُلَ لَحْمَ أَخِيهِ مَيْتًا فَكَرِهْتُمُوهُ ۚ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ تَوَّابٌ رَّحِيمٌ۝١٢

    Ya ayyuha allatheena amanoo ijtaniboo katheeran mina alththanni inna baʿda alththanni ithmun wala tajassasoo wala yaghtab baʿdukum baʿdan ayuhibbu ahadukum an yakula lahma akheehi maytan fakarihtumoohu waittaqoo Allaha inna Allaha tawwabun raheemun

    Enyi mlio amini! Jiepusheni na dhana nyingi, kwani baadhi ya dhana ni dhambi. Wala msipelelezane, wala msisengenyane nyinyi kwa nyinyi. Je! Yupo katika nyinyi anaye penda kuila nyama ya nduguye aliye kufa? Mnalichukia hilo! Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupokea toba, Mwenye kurehemu.12

    Maelezo
    [12] Enyi mlio amini, jitengeni mbali na wingi wa kudhania dhana mbovu kwa watu wa kheri. Kwani hakika baadhi ya dhana ni dhambi zinazo stahiki adhabu. Wala msiwe mkitafuta aibu za Waislamu. Wala msisengenyane, yaani kumsema mtu nyuma yake kwa jambo linalo muudhi. Hebu yupo yeyote kati yenu anaye penda kula nyama ya nduguye aliye kufa? Bila ya shaka hayo yanakuchukizeni! Basi ichukieni pia tabia ya kusengenyana na kusemana, kwani haya nayo ni mfano wa hayo. Na zikingeni nafsi zenu na adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa kufuata amri zake, na kuyaepuka ayakatazayo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkubwa wa kukubali toba ya wenye kutubia, Mwenye rehema kunjufu kwa walimwengu wote.
  13. يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَـٰكُم مِّن ذَكَرٍ وَأُنثَىٰ وَجَعَلْنَـٰكُمْ شُعُوبًا وَقَبَآئِلَ لِتَعَارَفُوٓا۟ ۚ إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِندَ ٱللَّهِ أَتْقَىٰكُمْ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ۝١٣

    Ya ayyuha alnnasu inna khalaqnakum min thakarin waontha wajaʿalnakum shuʿooban waqabaila litaʿarafoo inna akramakum ʿinda Allahi atqakum inna Allaha ʿaleemun khabeerun

    Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari.13

    Maelezo
    [13] Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni nyinyi sawa sawa kutokana na asli moja, ya Adamu na Hawa. Na tukakufanyeni mkawa wengi kwa mataifa makubwa na makabila mengi, ili kutimie kujuana na kuawiniana baina yenu, sio kubaguana. Na hakika mwenye cheo cha juu miongoni mwenu kwa Mwenyezi Mungu duniani na Akhera ni yule anaye mcha Yeye zaidi. Hakika Mwenyezi Mungu amevizunguka vitu vyote kwa kuvijua, ni Mwenye khabari za dogo na kubwa la kila jambo.
  14. ۞ قَالَتِ ٱلْأَعْرَابُ ءَامَنَّا ۖ قُل لَّمْ تُؤْمِنُوا۟ وَلَـٰكِن قُولُوٓا۟ أَسْلَمْنَا وَلَمَّا يَدْخُلِ ٱلْإِيمَـٰنُ فِى قُلُوبِكُمْ ۖ وَإِن تُطِيعُوا۟ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ لَا يَلِتْكُم مِّنْ أَعْمَـٰلِكُمْ شَيْـًٔا ۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ۝١٤

    Qalati alaʿrabu amanna qul lam tuminoo walakin qooloo aslamna walamma yadkhuli aleemanu fee quloobikum wain tuteeʿoo Allaha warasoolahu la yalitkum min aʿmalikum shayan inna Allaha ghafoorun raheemun

    Mabedui wamesema: Tumeamini. Sema: Hamjaamini, lakini semeni: Tumesilimu. Kwani Imani haijaingia katika nyoyo zenu. Na mkimt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hatakupunguzieni chochote katika vitendo vyenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.14

    Maelezo
    [14] Wakaazi wa majangwani wamesema kwa ndimi zao: Tumeamini. Ewe Muhammad! Waambie: Bado hamjaamini; kwa sababu nyoyo zenu bado hazijasadiki hayo mnayo yatamka. Lakini nyinyi semeni: Tumefuata dhaahiri ya Ujumbe wako. Bado Imani haijaingia katika nyoyo zenu. Na mkimt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa kweli, hato kunyimeni hata chembe katika malipo ya vitendo vyenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkubwa wa kuwasamehe waja wake, ni Mwenye rehema kunjufu kwa kila kitu.
  15. إِنَّمَا ٱلْمُؤْمِنُونَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ ثُمَّ لَمْ يَرْتَابُوا۟ وَجَـٰهَدُوا۟ بِأَمْوَٰلِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلصَّـٰدِقُونَ۝١٥

    Innama almuminoona allatheena amanoo biAllahi warasoolihi thumma lam yartaboo wajahadoo biamwalihim waanfusihim fee sabeeli Allahi olaika humu alssadiqoona

    Hakika Waumini ni wale walio muamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake tena wasitie shaka kabisa, na wakapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali yao na nafsi zao. Hao ndio wakweli.15

    Maelezo
    [15] Hakika Waumini wa kweli ni wale ambao wanamuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kisha hapana shaka yoyote inayo ingia katika nyoyo zao kwa hayo wanayo yaamini; tena wakapigana Jihadi kwa kutoa mali yao na roho zao katika njia ya ut'iifu wa Mwenyezi Mungu. Hao peke yao ndio walio wakweli katika Imani yao.
  16. قُلْ أَتُعَلِّمُونَ ٱللَّهَ بِدِينِكُمْ وَٱللَّهُ يَعْلَمُ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَمَا فِى ٱلْأَرْضِ ۚ وَٱللَّهُ بِكُلِّ شَىْءٍ عَلِيمٌ۝١٦

    Qul atuʿallimoona Allaha bideenikum waAllahu yaʿlamu ma fee alssamawati wama fee alardi waAllahu bikulli shayin ʿaleemun

    Sema: Ati ndio mnamfundisha Mwenyezi Mungu Dini yenu, na hali Mwenyezi Mungu anayajua ya katika mbingu na ardhi, na Mwenyezi Mungu anajua kila kitu?16

    Maelezo
    [16] Ewe Muhammad! Waambie kwa kuwakanusha ile kauli yao kuwa wameamini: Ndio hivyo ati mnampa khabari Mwenyezi Mungu kuwa nyoyo zenu zimesadiki? Na Mwenyezi Mungu peke yake anajua kila kiliomo katika mbingu na katika ardhi. Na Mwenyezi Mungu amevizunguka vitu vyote kwa ujuzi wake.
  17. يَمُنُّونَ عَلَيْكَ أَنْ أَسْلَمُوا۟ ۖ قُل لَّا تَمُنُّوا۟ عَلَىَّ إِسْلَـٰمَكُم ۖ بَلِ ٱللَّهُ يَمُنُّ عَلَيْكُمْ أَنْ هَدَىٰكُمْ لِلْإِيمَـٰنِ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ۝١٧

    Yamunnoona ʿalayka an aslamoo qul la tamunnoo ʿalayya islamakum bali Allahu yamunnu ʿalaykum an hadakum lileemani in kuntum sadiqeena

    Wanakusimbulia kuwa wamesilimu! Sema: Msinisimbulie kwa kusilimu kwenu. Bali Mwenyezi Mungu ndiye aliye kufanyieni hisani kwa kukuongoeni kwenye Imani, ikiwa nyinyi ni wakweli.17

    Maelezo
    [17] Wanaona kuwa kusilimu kwao ni kukuunga mkono wewe, Muhammad, na hivyo inastahiki wewe uwashukuru. Sema: Msinisimbulie kusilimu kwenu; kwani kheri yake mnaipata nyinyi. Bali ni Mwenyezi Mungu peke yake ndiye aliye kufanyieni ihsani kwa kukuongoeni kwenye Imani, ikiwa nyinyi ni wakweli katika hayo madai yenu.
  18. إِنَّ ٱللَّهَ يَعْلَمُ غَيْبَ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۚ وَٱللَّهُ بَصِيرٌۢ بِمَا تَعْمَلُونَ۝١٨

    Inna Allaha yaʿlamu ghayba alssamawati waalardi waAllahu baseerun bima taʿmaloona

    Hakika Mwenyezi Mungu anajua siri za mbingu na ardhi. Na Mwenyezi Mungu anayaona myatendayo.18

    Maelezo
    [18] Hakika Mwenyezi Mungu anajua kila lilio fichikana katika mbingu na ardhi. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuona vyema yote myatendayo.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Surat Al-Hujurat maana yake ni nini?

Al-Hujurat maana yake ni “Vyumba”.

Surat Al-Hujurat iko katika juzuu ya ngapi?

Surat Al-Hujurat iko katika juzuu ya 26.

Surat Al-Hujurat ina aya ngapi?

Surat Al-Hujurat ina aya 18.

Surat Al-Hujurat ni ya Makka au ya Madina?

Surat Al-Hujurat ni sura ya Madina.

Surat Al-Hujurat ni sura ya ngapi katika Qur’ani?

Ni sura ya 49 katika Qur’ani.

Vyanzo

  • Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
  • Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
  • Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
  • Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
  • Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
  • Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.

Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.

Mipangilio ya kusoma

Fonti ya Qur’ani
Ukubwa wa Kiarabu
100%
Ukubwa wa tafsiri
100%
Mandhari

Ongeza kwenye skrini ya kwanza

ReadSurahFungua ReadSurah kutoka skrini ya kwanza, kwa skrini nzima. Sura ulizosoma hufunguka hata bila intaneti.

  1. Katika Safari, gusa kitufe cha kushiriki (Share). Kwenye iPhone mpya kiko kwenye menyu ya •••.
  2. Gusa “Add to Home Screen”. Huenda ukahitaji kusogeza chini.
  3. Gusa “Add”.