سورة ق

Surat Qaf kwa Kiswahili

Msahafu

Mishary Rashid AlafasyPakua MP3Pakua PDF

Surat Qaf (ق) ni sura ya 50 katika Qur’ani na ina aya 45. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na iko katika juzuu ya 26.

Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat Qaf yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.

Surat Qaf kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

  1. قٓ ۚ وَٱلْقُرْءَانِ ٱلْمَجِيدِ۝١

    Qaf waalqurani almajeedi

    Qaaf. Naapa kwa Qur'ani tukufu!1

    Maelezo
    [1] Qaaf. Hii ni harufi katika harufi za alifbete iliyo fungulia Sura hii kama ilivyo ada ya Qur'ani katika kufungulia Sura kadhaa wa kadhaa kwa harufi kama hii, ili kuwakabili makafiri kama wanaweza kuleta mfano wake, na pia kuwazindua watu wasikilize yanayo somwa. Ninaapa kwa Qur'ani yenye ubora, na utukufu, na hishima kwamba hakika Sisi tumekutuma wewe, ewe Muhammad, ili uwaonye watu kwa hii.
  2. بَلْ عَجِبُوٓا۟ أَن جَآءَهُم مُّنذِرٌ مِّنْهُمْ فَقَالَ ٱلْكَـٰفِرُونَ هَـٰذَا شَىْءٌ عَجِيبٌ۝٢

    Bal ʿajiboo an jaahum munthirun minhum faqala alkafiroona hatha shayon ʿajeebun

    Bali wanastaajabu kwamba amewafikia mwonyaji kutoka miongoni mwao, na wakasema makafiri: Hili ni jambo la ajabu!2

    Maelezo
    [2] Bali walistaajabu kutokea Mtume miongoni mwa jinsi yao akiwaonya kuwa watafufuliwa. Makafiri wakasema: Jambo hili hatulijui, na la ajabu!
  3. أَءِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا ۖ ذَٰلِكَ رَجْعٌۢ بَعِيدٌ۝٣

    Aitha mitna wakunna turaban thalika rajʿun baʿeedun

    Ati tukifa na tukawa udongo? Kurejea huko kuko mbali!3

    Maelezo
    [3] Ati baada ya kwisha kufa na tukawa udongo, tutafufuliwa tena? Huko kufufuliwa baada ya kufa ni marejeo yaliyo mbali, hayawi.
  4. قَدْ عَلِمْنَا مَا تَنقُصُ ٱلْأَرْضُ مِنْهُمْ ۖ وَعِندَنَا كِتَـٰبٌ حَفِيظٌۢ۝٤

    Qad ʿalimna ma tanqusu alardu minhum waʿindana kitabun hafeethun

    Hakika Sisi tunajua kiasi cha kila kinacho punguzwa na ardhi kutokana nao. Na kwetu kipo Kitabu kinacho hifadhi yote.4

    Maelezo
    [4] Sisi hakika tunajua vipi ardhi inavyo vimeza viwiliwili vyao baada ya kufa. Na Sisi tunacho Kitabu kinacho dhibiti na kuhifadhi kila kitu hata kidogo.
  5. بَلْ كَذَّبُوا۟ بِٱلْحَقِّ لَمَّا جَآءَهُمْ فَهُمْ فِىٓ أَمْرٍ مَّرِيجٍ۝٥

    Bal kaththaboo bialhaqqi lamma jaahum fahum fee amrin mareejin

    Lakini waliikanusha Haki ilipo wajia; kwa hivyo wamo katika mambo ya mkorogo.5

    Maelezo
    [5] Wao hawayazingatii aliyo kuja nayo Mtume, bali walimkadhibisha mara tu bila ya kuzingatia na kufikiri. Basi wao wamo katika hali ya kubabaika, hawana utulivu.
  6. أَفَلَمْ يَنظُرُوٓا۟ إِلَى ٱلسَّمَآءِ فَوْقَهُمْ كَيْفَ بَنَيْنَـٰهَا وَزَيَّنَّـٰهَا وَمَا لَهَا مِن فُرُوجٍ۝٦

    Afalam yanthuroo ila alssamai fawqahum kayfa banaynaha wazayyannaha wama laha min furoojin

    Je! Hawaangalii mbingu zilizo juu yao! Vipi tulivyo zijenga, na tukazipamba. Wala hazina nyufa.6

    Maelezo
    [6] Wameghafilika hata hawaitazami mbingu ilivyo nyanyuliwa juu yao bila ya nguzo? Vipi tumetengeneza ujenzi wake, na tukaipamba kwa nyota, na haina nyufa za kuitia kombo! Mbingu ni kote kulio juu yetu, na ndani yake vimo vitu vya namna mbali mbali, vinaogelea katika njia zao, nyota na sayari. Na hayo ni kwa nidhamu ya uangalizi mkubwa, na mshikamano ulio timia, na vilevile zinafuata kwa mpango wake kuwafikiana na kanuni za mvutano, basi hazitelezi.
  7. وَٱلْأَرْضَ مَدَدْنَـٰهَا وَأَلْقَيْنَا فِيهَا رَوَٰسِىَ وَأَنۢبَتْنَا فِيهَا مِن كُلِّ زَوْجٍۭ بَهِيجٍ۝٧

    Waalarda madadnaha waalqayna feeha rawasiya waanbatna feeha min kulli zawjin baheejin

    Na ardhi tumeitandaza na tukaiwekea milima, na tukaiotesha mimea mizuri ya kila namna.7

    Maelezo
    [7] Na ardhi tumeikunjua na tukaisimamisha milima iliyo kaa imara na kuthibiti kwenda chini. Na tukaijaalia kumea kila namna ya mimea mizuri ya kuwafurahisha watazamao. Gamba lilio funika ardhi katika mwahali maalumu limetuna, ndio hiyo milima. Na pengine limedidimia ndio sakafu ya chini ya bahari. Na uzani wa vitu hivi vizito vinalingana wenyewe kwa wenyewe. Na ni katika uwezo wa Mwenyezi Mungu na hikima yake kupatikana kulingana huku kwa uzani, na ukawa umethibiti kwa kupenya madda za ardhi zilizo fanyika hilo gamba jembamba chini ya mat'abaka ya juu juu. Na hayo ni kutoka kuliko kuwa kuzito kwendea kuliko kwepesi.
  8. تَبْصِرَةً وَذِكْرَىٰ لِكُلِّ عَبْدٍ مُّنِيبٍ۝٨

    Tabsiratan wathikra likulli ʿabdin muneebin

    Yawe haya ni kifumbua macho na ukumbusho kwa kila mja mwenye kuelekea.8

    Maelezo
    [8] Tumejaalia hayo aone na akumbuke kila mja mwenye kurejea kwa Mola wake Mlezi, akafikiri Ishara za uwezo wake.
  9. وَنَزَّلْنَا مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءً مُّبَـٰرَكًا فَأَنۢبَتْنَا بِهِۦ جَنَّـٰتٍ وَحَبَّ ٱلْحَصِيدِ۝٩

    Wanazzalna mina alssamai maan mubarakan faanbatna bihi jannatin wahabba alhaseedi

    Na tumeteremsha kutoka mbinguni maji yaliyo barikiwa, na kwa hayo tukaotesha mabustani na nafaka za kuvunwa.9

    Maelezo
    [9] Na kutoka mbinguni tukateremsha maji yenye kheri nyingi na baraka, na kwa hayo tukaotesha mabustani yenye miti, na mauwa, na matunda, na tukatoa kwa hayo nafaka za makulima ya kuvunwa.
  10. وَٱلنَّخْلَ بَاسِقَـٰتٍ لَّهَا طَلْعٌ نَّضِيدٌ۝١٠

    Waalnnakhla basiqatin laha talʿun nadeedun

    Na mitende mirefu yenye makole yaliyo zaa kwa wingi,10

    Maelezo
    [10] Na mitende mirefu mirefu, yenye makole ya tende yaliyo pandana kwa wingi.
  11. رِّزْقًا لِّلْعِبَادِ ۖ وَأَحْيَيْنَا بِهِۦ بَلْدَةً مَّيْتًا ۚ كَذَٰلِكَ ٱلْخُرُوجُ۝١١

    Rizqan lilʿibadi waahyayna bihi baldatan maytan kathalika alkhurooju

    Ili iwe ni riziki kwa waja wangu. Na tukaifufua kwa maji nchi iliyo kuwa imekufa. Kama hivyo ndivyo utakavyo kuwa ufufuaji.11

    Maelezo
    [11] Tumeotesha hiyo ili iwe ni riziki kwa waja wetu, na tukaihuisha kwa maji ardhi iliyo kauka mimea yake. Hali kadhaalika ndivyo kufufuliwa wafu kutoka makaburini.
  12. كَذَّبَتْ قَبْلَهُمْ قَوْمُ نُوحٍ وَأَصْحَـٰبُ ٱلرَّسِّ وَثَمُودُ۝١٢

    Kaththabat qablahum qawmu noohin waashabu alrrassi wathamoodu

    Kabla yao walikadhibisha kaumu ya Nuhu na wakaazi wa Rassi na Thamudi.12

    Maelezo
    [12] Kabla ya hawa, kaumu nyingi ziliwakadhibisha Mitume- kaumu ya Nuhu, na kaumu nyengine iliyo kuwa ikiitwa "Watu wa Rassi", na wa Thamudi, na wa A'di, na wa Firauni, na kaumu Lut'i, na kaumu iliyo kuwa maarufu kwa jina la "Watu wa Machakani", na kaumu ya Tubbaa' - wote hao waliwakadhibisha Mitume wao. Kwa hivyo wakastahiki maangamizo niliyo waahidi.
  13. وَعَادٌ وَفِرْعَوْنُ وَإِخْوَٰنُ لُوطٍ۝١٣

    Waʿadun wafirʿawnu waikhwanu lootin

    Na A'di na Firauni na kaumu ya Lut'i.13

    Maelezo
    [13] Na wa A'di, na wa Firauni, na kaumu Lut'i,
  14. وَأَصْحَـٰبُ ٱلْأَيْكَةِ وَقَوْمُ تُبَّعٍ ۚ كُلٌّ كَذَّبَ ٱلرُّسُلَ فَحَقَّ وَعِيدِ۝١٤

    Waashabu alaykati waqawmu tubbaʿin kullun kaththaba alrrusula fahaqqa waʿeedi

    Na wakaazi wa Machakani, na watu wa Tubbaa'. Wote hao waliwakanusha Mitume, kwa hivyo onyo likathibitika juu yao.14

    Maelezo
    [14] Na kaumu iliyo kuwa maarufu kwa jina la "Watu wa Machakani", na kaumu ya Tubbaa' - wote hao waliwakadhibisha Mitume wao. Kwa hivyo wakastahiki maangamizo niliyo waahidi.
  15. أَفَعَيِينَا بِٱلْخَلْقِ ٱلْأَوَّلِ ۚ بَلْ هُمْ فِى لَبْسٍ مِّنْ خَلْقٍ جَدِيدٍ۝١٥

    Afaʿayeena bialkhalqi alawwali bal hum fee labsin min khalqin jadeedin

    Kwani tulichoka kwa kuumba mara ya kwanza. Bali wao wamo katika shaka tu juu ya umbo jipya.15

    Maelezo
    [15] Kwani kutaka kwetu kulipungua, au uwezo wetu ulitetereka, hata tukashindwa kwa kule kuumba kwa mara ya kwanza, tusiweze tena kuwarejeza? Hasha! Hatukushindwa, nao wanatambua hayo. Bali wao wana shaka tu na wanadanganyikiwa na huku kuumbwa kupya baada ya kufa.
  16. وَلَقَدْ خَلَقْنَا ٱلْإِنسَـٰنَ وَنَعْلَمُ مَا تُوَسْوِسُ بِهِۦ نَفْسُهُۥ ۖ وَنَحْنُ أَقْرَبُ إِلَيْهِ مِنْ حَبْلِ ٱلْوَرِيدِ۝١٦

    Walaqad khalaqna alinsana wanaʿlamu ma tuwaswisu bihi nafsuhu wanahnu aqrabu ilayhi min habli alwareedi

    Na hakika tumemuumba mtu, nasi tunayajua yanayo mpitikia katika nafsi yake. Na Sisi tuko karibu naye kuliko mshipa wa shingoni mwake.16

    Maelezo
    [16] Ninaapa: Bila ya shaka tumemuumba mtu, na Sisi tunajua hata anayo semezwa na nafsi yake. Na Sisi kwa kuzijua hali zake zote, ni karibu kuliko mshipa wake wa damu ulioko shingoni mwake. Na hicho ndicho kitu kilicho karibu mno naye.
  17. إِذْ يَتَلَقَّى ٱلْمُتَلَقِّيَانِ عَنِ ٱلْيَمِينِ وَعَنِ ٱلشِّمَالِ قَعِيدٌ۝١٧

    Ith yatalaqqa almutalaqqiyani ʿani alyameeni waʿani alshshimali qaʿeedun

    Wanapo pokea wapokeaji wawili, wanao kaa kuliani na kushotoni.17

    Maelezo
    [17] Watakapo kutana Malaika wawili walinzi, mmoja anakaa kuliani, na mwingine anakaa upande wa kushoto, wakiviandika vitendo vyake.
  18. مَّا يَلْفِظُ مِن قَوْلٍ إِلَّا لَدَيْهِ رَقِيبٌ عَتِيدٌ۝١٨

    Ma yalfithu min qawlin illa ladayhi raqeebun ʿateedun

    Hatamki neno ila karibu yake yupo mwangalizi tayari.18

    Maelezo
    [18] Halimtoki neno ila yuko karibu naye Malaika tayari kuandika neno lake.
  19. وَجَآءَتْ سَكْرَةُ ٱلْمَوْتِ بِٱلْحَقِّ ۖ ذَٰلِكَ مَا كُنتَ مِنْهُ تَحِيدُ۝١٩

    Wajaat sakratu almawti bialhaqqi thalika ma kunta minhu taheedu

    Na uchungu wa kutoka roho utamjia kwa haki. Hayo ndiyo uliyo kuwa ukiyakimbia.19

    Maelezo
    [19] Na yatapo kuja machungu ya kukata roho, kwa haki isiyo na shaka ndani yake, hilo ni jambo la kweli ulilo kuwa ukilikimbia.
  20. وَنُفِخَ فِى ٱلصُّورِ ۚ ذَٰلِكَ يَوْمُ ٱلْوَعِيدِ۝٢٠

    Wanufikha fee alssoori thalika yawmu alwaʿeedi

    Na litapulizwa baragumu. Hiyo ndiyo Siku ya Miadi.20

    Maelezo
    [20] Na baragumu litapulizwa kwa mpulizo wa kuwafufua watu. Kupulizwa huko kutakuwa siku hiyo ya kuteremka adhabu waliyo ahidiwa.
  21. وَجَآءَتْ كُلُّ نَفْسٍ مَّعَهَا سَآئِقٌ وَشَهِيدٌ۝٢١

    Wajaat kullu nafsin maʿaha saiqun washaheedun

    Na kila nafsi itakuja na pamoja nayo mchungaji na shahidi.21

    Maelezo
    [21] Na kila nafsi njema na mbaya, itakuja na pamoja nayo wa kuichunga kuipeleka kwenye mkusanyo, na wenye kuwatolea ushahidi wa vitendo vyao
  22. لَّقَدْ كُنتَ فِى غَفْلَةٍ مِّنْ هَـٰذَا فَكَشَفْنَا عَنكَ غِطَآءَكَ فَبَصَرُكَ ٱلْيَوْمَ حَدِيدٌ۝٢٢

    Laqad kunta fee ghaflatin min hatha fakashafna ʿanka ghitaaka fabasaruka alyawma hadeedun

    (Aambiwe): Kwa hakika ulikuwa umeghafilika na haya; basi leo tumekuondolea pazia lako, na kwa hivyo kuona kwako leo ni kukali.22

    Maelezo
    [22] Wataambiwa, kumtisha huyo mwenye kukadhibisha: Hakika wewe huko duniani ulikuwa umeghafilika kabisa na haya unayo sononeka nayo hivi sasa. Basi Sisi tumekuondolea pazia lilio kuwa likikuzuia usiyaone mambo ya Akhera. Basi jicho lako hii leo linaona kwa nguvu.
  23. وَقَالَ قَرِينُهُۥ هَـٰذَا مَا لَدَىَّ عَتِيدٌ۝٢٣

    Waqala qareenuhu hatha ma ladayya ʿateedun

    Na mwenzake atasema: Huyu niliye naye mimi kesha tayarishwa.23

    Maelezo
    [23] Na Shetani wake aliye kuwa mwongozi wake duniani, atasema: Kafiri huyu alioko kwangu yuko tayari kuingia Jahannamu kwa kupotezwa nami.
  24. أَلْقِيَا فِى جَهَنَّمَ كُلَّ كَفَّارٍ عَنِيدٍ۝٢٤

    Alqiya fee jahannama kulla kaffarin ʿaneedin

    Mtupeni katika Jahannamu kila kafiri mwenye inda,24

    Maelezo
    [24] Malaika wawili wataambiwa: Watieni katika Jahannamu kila aliye pita mipaka kwa ukafiri, na aliye pita mipaka kwa inadi, na akaacha kuifuata Haki,
  25. مَّنَّاعٍ لِّلْخَيْرِ مُعْتَدٍ مُّرِيبٍ۝٢٥

    Mannaʿin lilkhayri muʿtadin mureebin

    Akatazaye kheri, arukaye mipaka, mwenye kutia shaka,25

    Maelezo
    [25] Na akapita mipaka kuzuia kheri, mwenye kudhulumu akaipindukia Haki, mwenye kumtilia shaka Mwenyezi Mungu Mtukufu na aliyo yateremsha.
  26. ٱلَّذِى جَعَلَ مَعَ ٱللَّهِ إِلَـٰهًا ءَاخَرَ فَأَلْقِيَاهُ فِى ٱلْعَذَابِ ٱلشَّدِيدِ۝٢٦

    Allathee jaʿala maʿa Allahi ilahan akhara faalqiyahu fee alʿathabi alshshadeedi

    Aliye weka mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu. Basi mtupeni katika adhabu kali.26

    Maelezo
    [26] Aliye mfanya mungu mwengine wa kumuabudu pamoja na Mwenyezi Mungu. Basi mtupeni huyo katika adhabu yenye mwisho wa ukali.
  27. ۞ قَالَ قَرِينُهُۥ رَبَّنَا مَآ أَطْغَيْتُهُۥ وَلَـٰكِن كَانَ فِى ضَلَـٰلٍۭ بَعِيدٍ۝٢٧

    Qala qareenuhu rabbana ma atghaytuhu walakin kana fee dalalin baʿeedin

    Mwenzake aseme: Ee Mola wetu Mlezi! Sikumpoteza mimi, bali yeye mwenyewe alikuwa katika upotovu wa mbali.27

    Maelezo
    [27] Shetani atasema kumrudi yule kafiri: Ewe Mola wangu Mlezi! Mimi siye niliye mfanya awe mwenye kua'si, lakini yeye mwenyewe alikuwa katika upotovu wa mbali na haki. Na mimi nilimsaidia tu kwa kumpotoa.
  28. قَالَ لَا تَخْتَصِمُوا۟ لَدَىَّ وَقَدْ قَدَّمْتُ إِلَيْكُم بِٱلْوَعِيدِ۝٢٨

    Qala la takhtasimoo ladayya waqad qaddamtu ilaykum bialwaʿeedi

    (Mwenyezi Mungu) aseme: Msigombane mbele yangu. Nilikuleteeni mbele onyo langu.28

    Maelezo
    [28] Mwenyezi Mungu Mtukufu atawaambia makafiri na wenzi wao: Msigombane mbele yangu hapa pahala pa hisabu na malipo. Na Mimi nilikuleteeni mbele duniani onyo juu ya kukufuru kwenu kuukataa Ujumbe wangu niliyo utuma kwenu. Nanyi hamkuamini.
  29. مَا يُبَدَّلُ ٱلْقَوْلُ لَدَىَّ وَمَآ أَنَا۠ بِظَلَّـٰمٍ لِّلْعَبِيدِ۝٢٩

    Ma yubaddalu alqawlu ladayya wama ana bithallamin lilʿabeedi

    Mbele yangu haibadilishwi kauli, wala Mimi siwadhulumu waja wangu.29

    Maelezo
    [29] Hapana la kugeuza kauli ilioko kwangu na onyo langu kuwatia makafiri Motoni, wala Mimi si Mwenye kuwadhulumu waja. Kwani simuadhibu mja yeyote bila ya makosa.
  30. يَوْمَ نَقُولُ لِجَهَنَّمَ هَلِ ٱمْتَلَأْتِ وَتَقُولُ هَلْ مِن مَّزِيدٍ۝٣٠

    Yawma naqoolu lijahannama hali imtalati wataqoolu hal min mazeedin

    Siku tutapo iambia Jahannamu: Je! Umejaa? Nayo itasema: Je! Kuna ziada?30

    Maelezo
    [30] Siku tutapo iambia Jahannamu kwa kuwatia kiwewe makafiri: Je! Umejaa? Nayo Jahannamu iseme kwa kuwaghadhibikia: Wapo wengine zaidi wa kuwaongeza katika hawa wenye kudhulumu?
  31. وَأُزْلِفَتِ ٱلْجَنَّةُ لِلْمُتَّقِينَ غَيْرَ بَعِيدٍ۝٣١

    Waozlifati aljannatu lilmuttaqeena ghayra baʿeedin

    Na Pepo italetwa karibu kwa ajili ya wachamngu, haitakuwa mbali.31

    Maelezo
    [31] Na Pepo iliyo pambwa italetwa karibu kwa ajili ya wenye kumcha Mola wao Mlezi, kwa kufuata amri zake na kuyaepuka makatazo yake, iletwe pahala pasipo kuwa mbali nao.
  32. هَـٰذَا مَا تُوعَدُونَ لِكُلِّ أَوَّابٍ حَفِيظٍ۝٣٢

    Hatha ma tooʿadoona likulli awwabin hafeethin

    Haya ndiyo mnayo ahidiwa kwa kila mwenye kurejea kwa Mwenyezi Mungu na akajilinda.32

    Maelezo
    [32] Haya ndiyo malipo ya kila mwenye kurejea kwa Mwenyezi Mungu, aliye mwingi wa kuhifadhi sharia zake.
  33. مَّنْ خَشِىَ ٱلرَّحْمَـٰنَ بِٱلْغَيْبِ وَجَآءَ بِقَلْبٍ مُّنِيبٍ۝٣٣

    Man khashiya alrrahmana bialghaybi wajaa biqalbin muneebin

    Mwenye kumwogopa Mwingi wa Rehema hali kuwa hamwoni, na akaja kwa moyo ulio elekea33

    Maelezo
    [33] Mwenye kukhofu adhabu ya Mwenyezi Mungu ambaye rehema yake imeenea juu ya kila kitu, na Yeye haonekani, na akaja Akhera na moyo wa aliye kwisha rejea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  34. ٱدْخُلُوهَا بِسَلَـٰمٍ ۖ ذَٰلِكَ يَوْمُ ٱلْخُلُودِ۝٣٤

    Odkhulooha bisalamin thalika yawmu alkhuloodi

    (Ataambiwa) ingieni kwa salama. Hiyo ndiyo siku ya daima dawamu.34

    Maelezo
    [34] Itasemwa kwa hishima yao: Ingieni Peponi kwa amani. Hiyo siku mtakapo ingia Peponi ndiyo siku ya kubakia milele isiyo na mwisho.
  35. لَهُم مَّا يَشَآءُونَ فِيهَا وَلَدَيْنَا مَزِيدٌ۝٣٥

    Lahum ma yashaoona feeha waladayna mazeedun

    Humo watapata wakitakacho, na kwetu yako ya ziada.35

    Maelezo
    [35] Hao wachamngu watapata kila wakitakacho huko Peponi. Na Sisi tunazo neema za kuzidi kuliko yanayo mpitikia mtu kuyawaza.
  36. وَكَمْ أَهْلَكْنَا قَبْلَهُم مِّن قَرْنٍ هُمْ أَشَدُّ مِنْهُم بَطْشًا فَنَقَّبُوا۟ فِى ٱلْبِلَـٰدِ هَلْ مِن مَّحِيصٍ۝٣٦

    Wakam ahlakna qablahum min qarnin hum ashaddu minhum batshan fanaqqaboo fee albiladi hal min maheesin

    Na kaumu ngapi tuliziangamiza kabla yao walio kuwa na nguvu zaidi kuliko hawa! Nao walitanga tanga katika nchi nyingi. Je! Walipata pa kukimbilia?36

    Maelezo
    [36] Na wengi tumekwisha wateketeza kabla ya hawa wanao kadhibisha katika mataifa yaliyo kwisha pita. Wao walikuwa na nguvu na madaraka zaidi kuliko hawa. Wakaizunguka miji wakishughulika kuchungua na kutafuta. Je! Walipata pa kukimbilia wasiangamizwe?
  37. إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَذِكْرَىٰ لِمَن كَانَ لَهُۥ قَلْبٌ أَوْ أَلْقَى ٱلسَّمْعَ وَهُوَ شَهِيدٌ۝٣٧

    Inna fee thalika lathikra liman kana lahu qalbun aw alqa alssamʿa wahuwa shaheedun

    Hakika katika hayo upo ukumbusho kwa mwenye moyo au akatega sikio naye yupo anashuhudia.37

    Maelezo
    [37] Hakika kwa waliyo tendewa hao wa kaumu zilizo kwisha pita ni mawaidha kwa mwenye moyo wa kufahamu hakika ya mambo, au akasikiliza uwongofu naye akili zake anazo.
  38. وَلَقَدْ خَلَقْنَا ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِى سِتَّةِ أَيَّامٍ وَمَا مَسَّنَا مِن لُّغُوبٍ۝٣٨

    Walaqad khalaqna alssamawati waalarda wama baynahuma fee sittati ayyamin wama massana min lughoobin

    Na bila ya shaka Sisi tumeziumba mbingu na ardhi na vilio baina yao mnamo siku sita; na wala hayakutugusa machofu.38

    Maelezo
    [38] Ninaapa: Hakika tumeziumba mbingu na ardhi na viumbe viliomo baina yao katika siku sita. Na hatukupata kuchoka. Rejea mambo yaliyo khusu maana ya neno "Siku" za uumbaji katika maelezo ya kitaalamu juu ya Aya za idadi 9 mpaka 12 katika Sura ya "Fuss'ilat". 41:9-12
  39. فَٱصْبِرْ عَلَىٰ مَا يَقُولُونَ وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ قَبْلَ طُلُوعِ ٱلشَّمْسِ وَقَبْلَ ٱلْغُرُوبِ۝٣٩

    Faisbir ʿala ma yaqooloona wasabbih bihamdi rabbika qabla tulooʿi alshshamsi waqabla alghuroobi

    Basi vumilia kwa hayo wasemayo, na mtakase kwa kumsifu Mola wako Mlezi kabla ya kuchomoza jua na kabla ya kuchwa.39

    Maelezo
    [39] Ikiwa haya yamebainika, basi, ewe Mtume, yastahamilie hayo wayasemayo hao wanao kanusha, ya uwongo na uzushi kukhusu Utume wako. Nawe mtakasishe, Msabbih, Muumba wako na Mlezi wako na kila upungufu, ukimhimidi wakati wa alfajiri, na wakati wa alasiri, kwani ibada nyakati hizo ni jambo kuu.
  40. وَمِنَ ٱلَّيْلِ فَسَبِّحْهُ وَأَدْبَـٰرَ ٱلسُّجُودِ۝٤٠

    Wamina allayli fasabbihhu waadbara alssujoodi

    Na katika usiku pia mtakase, na baada ya kusujudu.40

    Maelezo
    [40] Na pia mtakasishe, Msabbih, katika saa za usiku, na baada ya Swala.
  41. وَٱسْتَمِعْ يَوْمَ يُنَادِ ٱلْمُنَادِ مِن مَّكَانٍ قَرِيبٍ۝٤١

    Waistamiʿ yawma yunadi almunadi min makanin qareebin

    Na sikiliza siku atapo nadi mwenye kunadi kutoka pahala karibu.41

    Maelezo
    [41] Na sikiliza khabari ninazo kwambia katika hadithi za Kiyama kwani shani yake ni kubwa. Siku atapo nadi Malaika wa kunadi kutoka pahala pa karibu na hao wanao itwa.
  42. يَوْمَ يَسْمَعُونَ ٱلصَّيْحَةَ بِٱلْحَقِّ ۚ ذَٰلِكَ يَوْمُ ٱلْخُرُوجِ۝٤٢

    Yawma yasmaʿoona alssayhata bialhaqqi thalika yawmu alkhurooji

    Siku watakapo sikia ukelele wa haki. Hiyo ndiyo siku ya kufufuka.42

    Maelezo
    [42] Siku watapo sikia mpulizo wa pili wa Haki, nao ni wa kufufuliwa watu. Hiyo ndiyo siku ya kutoka kwenye makaburi.
  43. إِنَّا نَحْنُ نُحْىِۦ وَنُمِيتُ وَإِلَيْنَا ٱلْمَصِيرُ۝٤٣

    Inna nahnu nuhyee wanumeetu wailayna almaseeru

    Hakika Sisi tunahuisha na tunafisha, na kwetu Sisi ndio marejeo.43

    Maelezo
    [43] Hakika Sisi, peke yetu, ndio tunao huisha viumbe vyote, na tunavifisha duniani. Na kwetu Sisi, peke yetu, ndio marejeo Akhera.
  44. يَوْمَ تَشَقَّقُ ٱلْأَرْضُ عَنْهُمْ سِرَاعًا ۚ ذَٰلِكَ حَشْرٌ عَلَيْنَا يَسِيرٌ۝٤٤

    Yawma tashaqqaqu alardu ʿanhum siraʿan thalika hashrun ʿalayna yaseerun

    Siku itapo wapasukia ardhi mbio mbio! Mkusanyo huo kwetu ni mwepesi.44

    Maelezo
    [44] Siku itakapo wapasukilia ardhi, na watoke humo mbio mbio wakikimbilia mkutanoni...Hilo jambo kuu la kuwakusanya wote ni dogo na jepesi kwetu.
  45. نَّحْنُ أَعْلَمُ بِمَا يَقُولُونَ ۖ وَمَآ أَنتَ عَلَيْهِم بِجَبَّارٍ ۖ فَذَكِّرْ بِٱلْقُرْءَانِ مَن يَخَافُ وَعِيدِ۝٤٥

    Nahnu aʿlamu bima yaqooloona wama anta ʿalayhim bijabbarin fathakkir bialqurani man yakhafu waʿeedi

    Sisi tunajua kabisa wayasemayo. Wala wewe si mwenye kuwatawalia kwa ujabari. Basi mkumbushe kwa Qur'ani anaye liogopa onyo.45

    Maelezo
    [45] Sisi tunajua kuliko yeyote hayo wayasemayo ya uwongo juu yaliyo khusu Utume wako. Wala wewe hukutumwa uwalazimishe kwa unayo yataka. Ila wewe ni mwonyaji basi mkumbushe kwa Qur'ani Muumini mwenye kuiogopa adhabu yangu ili ukumbusho umfae..

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Surat Qaf iko katika juzuu ya ngapi?

Surat Qaf iko katika juzuu ya 26.

Surat Qaf ina aya ngapi?

Surat Qaf ina aya 45.

Surat Qaf ni ya Makka au ya Madina?

Surat Qaf ni sura ya Makka.

Surat Qaf ni sura ya ngapi katika Qur’ani?

Ni sura ya 50 katika Qur’ani.

Vyanzo

  • Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
  • Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
  • Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
  • Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
  • Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
  • Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.

Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.

Mipangilio ya kusoma

Fonti ya Qur’ani
Ukubwa wa Kiarabu
100%
Ukubwa wa tafsiri
100%
Mandhari

Ongeza kwenye skrini ya kwanza

ReadSurahFungua ReadSurah kutoka skrini ya kwanza, kwa skrini nzima. Sura ulizosoma hufunguka hata bila intaneti.

  1. Katika Safari, gusa kitufe cha kushiriki (Share). Kwenye iPhone mpya kiko kwenye menyu ya •••.
  2. Gusa “Add to Home Screen”. Huenda ukahitaji kusogeza chini.
  3. Gusa “Add”.