سورة الذاريات
Surat Adh-Dhariyat kwa Kiswahili
Pepo Zinazotawanya
- 51
- Aya 60
- Sura ya Makka
- Juzuu 26–27
- Kurasa 520–523
Surat Adh-Dhariyat (الذاريات) ni sura ya 51 katika Qur’ani na ina aya 60. Jina lake lina maana ya “Pepo Zinazotawanya”. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na inaenea katika juzuu za 26 na 27.
Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat Adh-Dhariyat yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.
Surat Adh-Dhariyat kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
-
وَٱلذَّٰرِيَـٰتِ ذَرْوًا١
Waalththariyati tharwan
Naapa kwa pepo zinazo tawanya!1
Maelezo
[1] Ninaapa kwa pepo zinazo timua mawingu, zikayasukuma kwa nguvu, huku zikibeba mizigo mizito ya maji, zikawa zinakwenda kwa wepesi kwa amri ya Mwenyezi Mungu, zikawa zinagawanya riziki kwa ampendaye Mwenyezi Mungu. -
فَٱلْحَـٰمِلَـٰتِ وِقْرًا٢
Faalhamilati wiqran
Na zinazo beba mizigo!2
Maelezo
[2] Huku zikibeba mizigo mizito ya maji. -
فَٱلْجَـٰرِيَـٰتِ يُسْرًا٣
Faaljariyati yusran
Na zinazo kwenda kwa wepesi.3
Maelezo
[3] Zikawa zinakwenda kwa wepesi kwa amri ya Mwenyezi Mungu. -
فَٱلْمُقَسِّمَـٰتِ أَمْرًا٤
Faalmuqassimati amran
Na zinazo gawanya kwa amri!4
Maelezo
[4] Zikawa zinagawanya riziki kwa ampendaye Mwenyezi Mungu. -
إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَصَادِقٌ٥
Innama tooʿadoona lasadiqun
Hakika mnayo ahidiwa bila ya shaka ni kweli!5
Maelezo
[5] Hakika hayo mnayo ahidiwa, nayo ya kufufuliwa na mengineyo, ni hakika ya kweli itakayo tokea. -
وَإِنَّ ٱلدِّينَ لَوَٰقِعٌ٦
Wainna alddeena lawaqiʿun
Na kwa hakika malipo bila ya shaka yatatokea.6
Maelezo
[6] Na kwamba kwa yakini malipo kwa vitendo vyenu yatakuwa tu hapana hivi wala hivi. -
وَٱلسَّمَآءِ ذَاتِ ٱلْحُبُكِ٧
Waalssamai thati alhubuki
Naapa kwa mbingu zenye njia!7
Maelezo
[7] Ninaapa kwa mbingu zenye njia zilizo wekwa baraabara. -
إِنَّكُمْ لَفِى قَوْلٍ مُّخْتَلِفٍ٨
Innakum lafee qawlin mukhtalifin
Hakika nyinyi bila ya shaka mmo katika kauli inayo khitalifiana.8
Maelezo
[8] Kwamba nyinyi msemapo mnayo yasema ni maneno ya kugongana. -
يُؤْفَكُ عَنْهُ مَنْ أُفِكَ٩
Yufaku ʿanhu man ofika
Anageuzwa kutokana na haki mwenye kugeuzwa.9
Maelezo
[9] Huacha kuamini hiyo ahadi ya kweli na malipo yatakayo kuwa huyo anaye acha, kwa sababu amekhiari kufuata pumbao la nafsi yake kuliko akili yake. -
قُتِلَ ٱلْخَرَّٰصُونَ١٠
Qutila alkharrasoona
Wazushi wameangamizwa.10
Maelezo
[10] Wameteketea waongo wanao sema katika khabari za Kiyama kuwa ni mambo ya dhana na kukisia tu, ambao kwamba wamezamishwa katika ujinga, wameghafilika na dalili za yakini. -
ٱلَّذِينَ هُمْ فِى غَمْرَةٍ سَاهُونَ١١
Allatheena hum fee ghamratin sahoona
Ambao wameghafilika katika ujinga.11
Maelezo
[11] Ambao kwamba wamezamishwa katika ujinga, wameghafilika na dalili za yakini. -
يَسْـَٔلُونَ أَيَّانَ يَوْمُ ٱلدِّينِ١٢
Yasaloona ayyana yawmu alddeeni
Wanauliza: Ni lini hiyo siku ya malipo?12
Maelezo
[12] Wanauliza kwa kejeli, kwa kuwa wanaona hayawi hayo: Lini itakuwa hiyo siku ya malipo? -
يَوْمَ هُمْ عَلَى ٱلنَّارِ يُفْتَنُونَ١٣
Yawma hum ʿala alnnari yuftanoona
Hiyo ni siku watakayo adhibiwa Motoni.13
Maelezo
[13] Siku watapo simamishwa Motoni wakichomwa! -
ذُوقُوا۟ فِتْنَتَكُمْ هَـٰذَا ٱلَّذِى كُنتُم بِهِۦ تَسْتَعْجِلُونَ١٤
Thooqoo fitnatakum hatha allathee kuntum bihi tastaʿjiloona
Onjeni adhabu yenu! Haya ndiyo mliyo kuwa mkiyahimiza.14
Maelezo
[14] Wataambiwa: Onjeni adhabu yenu hii ambayo duniani mlikuwa mkiihimiza iwe. -
إِنَّ ٱلْمُتَّقِينَ فِى جَنَّـٰتٍ وَعُيُونٍ١٥
Inna almuttaqeena fee jannatin waʿuyoonin
Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na chemchem.15
Maelezo
[15] Hakika walio mt'ii Mwenyezi Mungu na wakamkhofu watakuwa wananeemeka katika Mabustani na chemchem za Peponi ambazo haziwezi kusifika hakika yake. -
ءَاخِذِينَ مَآ ءَاتَىٰهُمْ رَبُّهُمْ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا۟ قَبْلَ ذَٰلِكَ مُحْسِنِينَ١٦
Akhitheena ma atahum rabbuhum innahum kanoo qabla thalika muhsineena
Wanapokea aliyo wapa Mola wao Mlezi. Kwa hakika hao walikuwa kabla ya haya wakifanya mema.16
Maelezo
[16] Wakipokea thawabu na takrima wanazo pewa na Mola wao Mlezi. Hakika hao kabla ya hapo walikuwa duniani ni wenye kufanya mambo mazuri kwa kutimiza waliyo takiwa wayafanye. -
كَانُوا۟ قَلِيلًا مِّنَ ٱلَّيْلِ مَا يَهْجَعُونَ١٧
Kanoo qaleelan mina allayli ma yahjaʿoona
Walikuwa wakilala kidogo tu usiku.17
Maelezo
[17] Walikuwa kulala kwao usiku ni kuchache, na wakikesha sana kwa ibada. -
وَبِٱلْأَسْحَارِ هُمْ يَسْتَغْفِرُونَ١٨
Wabialashari hum yastaghfiroona
Na kabla ya alfajiri wakiomba maghfira.18
Maelezo
[18] Na mwishoni mwa usiku walikuwa wakiomba maghfira. -
وَفِىٓ أَمْوَٰلِهِمْ حَقٌّ لِّلسَّآئِلِ وَٱلْمَحْرُومِ١٩
Wafee amwalihim haqqun lilssaili waalmahroomi
Na katika mali yao ipo haki ya mwenye kuomba na asiye omba.19
Maelezo
[19] Na katika mali yao wakiweka fungu maalumu lilio thibiti kwa ajili ya wenye haja, wanao omba na wanao jizuilia kuomba kwa kujiteta. -
وَفِى ٱلْأَرْضِ ءَايَـٰتٌ لِّلْمُوقِنِينَ٢٠
Wafee alardi ayatun lilmooqineena
Na katika ardhi zipo Ishara kwa wenye yakini.20
Maelezo
[20] Na katika ardhi zipo dalili nyingi zilizo wazi zinazo pelekea yakini, kwa mwenye kuitafuta njia. -
وَفِىٓ أَنفُسِكُمْ ۚ أَفَلَا تُبْصِرُونَ٢١
Wafee anfusikum afala tubsiroona
Na pia katika nafsi zenu - Je! Hamwoni?21
Maelezo
[21] Na hali kadhaalika katika nafsi zenu zipo Ishara zilizo wazi. Je! Mmeghafilika nazo, hamzioni? -
وَفِى ٱلسَّمَآءِ رِزْقُكُمْ وَمَا تُوعَدُونَ٢٢
Wafee alssamai rizqukum wama tooʿadoona
Na katika mbingu ziko riziki zenu na mliyo ahidiwa.22
Maelezo
[22] Na katika mbingu ipo amri ya riziki zenu na kukadiriwa mnayo ahidiwa. -
فَوَرَبِّ ٱلسَّمَآءِ وَٱلْأَرْضِ إِنَّهُۥ لَحَقٌّ مِّثْلَ مَآ أَنَّكُمْ تَنطِقُونَ٢٣
Fawarabbi alssamai waalardi innahu lahaqqun mithla ma annakum tantiqoona
Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, hakika haya ni kweli kama ilivyo kweli kuwa nyinyi mnasema.23
Maelezo
[23] Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mbingu na ardhi kwamba hakika yote hayo mnayo yakanya kuwa, yaani kufufuliwa, kulipwa, kuadhibiwa wanao kadhibisha, na kuwalipa thawabu wachamngu, yote hayo bila ya shaka ni ya kweli thaabiti kama hivyo kusema kwenu ambako hamna shaka nako kuwa mnasema. -
هَلْ أَتَىٰكَ حَدِيثُ ضَيْفِ إِبْرَٰهِيمَ ٱلْمُكْرَمِينَ٢٤
Hal ataka hadeethu dayfi ibraheema almukrameena
Je! Imekufikia hadithi ya wageni wa Ibrahim wanao hishimiwa?24
Maelezo
[24] Unakijua kisa cha Malaika, wageni wa hishima wa Ibrahim? Pale walipo ingia kwake na wakamtolea Salamu, na yeye akawajibu kwa Salamu, na kuwambia kuwa ni watu asio wajua. -
إِذْ دَخَلُوا۟ عَلَيْهِ فَقَالُوا۟ سَلَـٰمًا ۖ قَالَ سَلَـٰمٌ قَوْمٌ مُّنكَرُونَ٢٥
Ith dakhaloo ʿalayhi faqaloo salaman qala salamun qawmun munkaroona
Walipo ingia kwake wakasema: Salama! Na yeye akasema: Salama! Nyinyi ni watu nisio kujueni.25
Maelezo
[25] Pale walipo ingia kwake na wakamtolea Salamu, na yeye akawajibu kwa Salamu, na kuwambia kuwa ni watu asio wajua. -
فَرَاغَ إِلَىٰٓ أَهْلِهِۦ فَجَآءَ بِعِجْلٍ سَمِينٍ٢٦
Faragha ila ahlihi fajaa biʿijlin sameenin
Akenda kwa ahali yake na akaja na ndama aliye nona.26
Maelezo
[26] Akenda kwa mkewe naye ana khofu, akaja na ndama aliye nona. -
فَقَرَّبَهُۥٓ إِلَيْهِمْ قَالَ أَلَا تَأْكُلُونَ٢٧
Faqarrabahu ilayhim qala ala takuloona
Akawakaribisha, akasema: Mbona hamli?27
Maelezo
[27] Akawakaribisha, nao hawakula. Akasema kwa kuto wajua hakika yao: Mbona hamli? -
فَأَوْجَسَ مِنْهُمْ خِيفَةً ۖ قَالُوا۟ لَا تَخَفْ ۖ وَبَشَّرُوهُ بِغُلَـٰمٍ عَلِيمٍ٢٨
Faawjasa minhum kheefatan qaloo la takhaf wabashsharoohu bighulamin ʿaleemin
Akahisi kuwaogopa katika nafsi yake. Wakasema: Usiwe na khofu, nao wakambashiria kupata kijana mwenye ilimu.28
Maelezo
[28] Akahisi katika nafsi yake khofu kuwaogopa. Wakasema: Usiogope. Na wakampa bishara kuwa atapata mwana mwenye ilimu nzuri. -
فَأَقْبَلَتِ ٱمْرَأَتُهُۥ فِى صَرَّةٍ فَصَكَّتْ وَجْهَهَا وَقَالَتْ عَجُوزٌ عَقِيمٌ٢٩
Faaqbalati imraatuhu fee sarratin fasakkat wajhaha waqalat ʿajoozun ʿaqeemun
Ndipo mkewe akawaelekea, na huku anasema na akijipiga usoni kwa mastaajabu, na kusema: Mimi ni kikongwe na tasa!29
Maelezo
[29] Akatokea mkewe akipiga kelele alipo isikia ile bishara, akijipiga uso wake kwa mkono wake, kwa kuona muhali hayo na kustaajabu, na akasema: Mimi ni kizee, na tasa. Itakuwaje nizae? -
قَالُوا۟ كَذَٰلِكِ قَالَ رَبُّكِ ۖ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلْحَكِيمُ ٱلْعَلِيمُ٣٠
Qaloo kathaliki qala rabbuki innahu huwa alhakeemu alʿaleemu
Wakasema: Ndivyo vivyo hivyo alivyo sema Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye hikima na Mwenye kujua.30
Maelezo
[30] Wakasema: Hivyo ndivyo alivyo kwisha hukumu Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye hikima katika kila anayo hukumu, ni Mwenye ujuzi ambaye hapana linalo fichikana kwake lolote. -
۞ قَالَ فَمَا خَطْبُكُمْ أَيُّهَا ٱلْمُرْسَلُونَ٣١
Qala fama khatbukum ayyuha almursaloona
AKASEMA: Basi ujumbe wenu ni nini, enyi mlio tumwa?31
Maelezo
[31] Ibrahim akasema: Mna kazi gani tena baada ya khabari hii nzuri, enyi wajumbe? -
قَالُوٓا۟ إِنَّآ أُرْسِلْنَآ إِلَىٰ قَوْمٍ مُّجْرِمِينَ٣٢
Qaloo inna orsilna ila qawmin mujrimeena
Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwa watu wakosefu,32
Maelezo
[32] Wakasema: Kwa hakika sisi tumetumwa kwa kaumu iliyo pita kiasi katika uasi, -
لِنُرْسِلَ عَلَيْهِمْ حِجَارَةً مِّن طِينٍ٣٣
Linursila ʿalayhim hijaratan min teenin
Tuwatupie mawe ya udongo,33
Maelezo
[33] Tuwatupie mawe ya udongo, ambayo hapana anaye yajua yalivyo ila Mwenyezi Mungu. -
مُّسَوَّمَةً عِندَ رَبِّكَ لِلْمُسْرِفِينَ٣٤
Musawwamatan ʿinda rabbika lilmusrifeena
Yaliyo tiwa alama kutoka kwa Mola wako Mlezi kwa ajili ya wanao pindukia mipaka.34
Maelezo
[34] Mawe hayo ni makhsusi na maalumu kwa Mola wako Mlezi kwa ajili ya wanao pindukia mipaka katika mambo machafu. -
فَأَخْرَجْنَا مَن كَانَ فِيهَا مِنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ٣٥
Faakhrajna man kana feeha mina almumineena
Kwa hivyo tutawatoa katika hao wale walio amini.35
Maelezo
[35] Basi tukahukumu tuwatoea kwenye mji huo walio amini. -
فَمَا وَجَدْنَا فِيهَا غَيْرَ بَيْتٍ مِّنَ ٱلْمُسْلِمِينَ٣٦
Fama wajadna feeha ghayra baytin mina almuslimeena
Lakini hatukupata humo ila nyumba moja tu yenye Waislamu!36
Maelezo
[36] Lakini hatukukuta ila nyumba moja tu ndiyo ya Waislamu. -
وَتَرَكْنَا فِيهَآ ءَايَةً لِّلَّذِينَ يَخَافُونَ ٱلْعَذَابَ ٱلْأَلِيمَ٣٧
Watarakna feeha ayatan lillatheena yakhafoona alʿathaba alaleema
Na tukaacha humo Ishara kwa ajili ya wanao iogopa adhabu chungu.37
Maelezo
[37] Na katika mji huo tumeacha alama ya maangamizo ya watu wake, ili wapate kuzingatia wanayo ikhofu adhabu chungu. -
وَفِى مُوسَىٰٓ إِذْ أَرْسَلْنَـٰهُ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ بِسُلْطَـٰنٍ مُّبِينٍ٣٨
Wafee moosa ith arsalnahu ila firʿawna bisultanin mubeenin
Na katika khabari za Musa, tulipo mtuma kwa Firauni na hoja wazi.38
Maelezo
[38] Na katika kisa cha Musa yapo mawaidha. Tulipo mtuma kwa Firauni, na tukatilia nguvu kwa kumpa ushahidi ulio wazi. -
فَتَوَلَّىٰ بِرُكْنِهِۦ وَقَالَ سَـٰحِرٌ أَوْ مَجْنُونٌ٣٩
Fatawalla biruknihi waqala sahirun aw majnoonun
Lakini alipuuza kwa sababu ya nguvu zake na akasema: Huyu ni mchawi au mwendawazimu!39
Maelezo
[39] Firauni akapuuza kumuamini Musa kwa kutegemea ati nguvu zake. Akasema: Huyu ni mchawi au mwendawazimu! -
فَأَخَذْنَـٰهُ وَجُنُودَهُۥ فَنَبَذْنَـٰهُمْ فِى ٱلْيَمِّ وَهُوَ مُلِيمٌ٤٠
Faakhathnahu wajunoodahu fanabathnahum fee alyammi wahuwa muleemun
Basi tukamkamata yeye na majeshi yake na tukawatupa baharini, na yeye ndiye wa kulaumiwa.40
Maelezo
[40] Tukamchukua yeye na hao anao jitapia kwao, tukawatumbukiza baharini, naye ni mwenye kuyatenda hayo ya ukafiri na inda anayo laumiwa kwayo. -
وَفِى عَادٍ إِذْ أَرْسَلْنَا عَلَيْهِمُ ٱلرِّيحَ ٱلْعَقِيمَ٤١
Wafee ʿadin ith arsalna ʿalayhimu alrreeha alʿaqeema
Na katika khabari za A'di tulipo wapelekea upepo wa kukata uzazi.41
Maelezo
[41] Na katika kisa cha A'di yamo mawaidha pia. Tulipo wapelekea upepo usio kuwa na kheri yoyote. -
مَا تَذَرُ مِن شَىْءٍ أَتَتْ عَلَيْهِ إِلَّا جَعَلَتْهُ كَٱلرَّمِيمِ٤٢
Ma tatharu min shayin atat ʿalayhi illa jaʿalathu kaalrrameemi
Haukuacha chochote ulicho kifikia ila ulikifanya kama kilio nyambuka.42
Maelezo
[42] Upepo huo haupiti kwa kitu chochote ila hukiacha kama fupa lilio nyambuka. -
وَفِى ثَمُودَ إِذْ قِيلَ لَهُمْ تَمَتَّعُوا۟ حَتَّىٰ حِينٍ٤٣
Wafee thamooda ith qeela lahum tamattaʿoo hatta heenin
Na katika khabari za Thamudi walipo ambiwa: Jifurahisheni kwa muda mdogo tu.43
Maelezo
[43] Na katika kisa cha Thamudi ipo Ishara. Walipo ambiwa: Stareheni katika majumba yenu kwa muda maalumu. -
فَعَتَوْا۟ عَنْ أَمْرِ رَبِّهِمْ فَأَخَذَتْهُمُ ٱلصَّـٰعِقَةُ وَهُمْ يَنظُرُونَ٤٤
Faʿataw ʿan amri rabbihim faakhathathumu alssaʿiqatu wahum yanthuroona
Wakaasi amri ya Mola wao Mlezi. Basi uliwanyakua moto wa radi nao wanaona.44
Maelezo
[44] Na katika kisa cha Thamudi ipo Ishara. Walipo ambiwa: Stareheni katika majumba yenu kwa muda maalumu. Wakajivuna na wakatakabari wasifuate amri ya Mola wao Mlezi. Basi radi ikawaangamiza nao wanaiona kwa macho yao inavyo tokea. -
فَمَا ٱسْتَطَـٰعُوا۟ مِن قِيَامٍ وَمَا كَانُوا۟ مُنتَصِرِينَ٤٥
Fama istataʿoo min qiyamin wama kanoo muntasireena
Basi hawakuweza kusimama wala hawakuwa wenye kujitetea.45
Maelezo
[45] Basi hawakuweza kuinuka. Wala hawakuweza kujipigania kuijikinga na adhabu. -
وَقَوْمَ نُوحٍ مِّن قَبْلُ ۖ إِنَّهُمْ كَانُوا۟ قَوْمًا فَـٰسِقِينَ٤٦
Waqawma noohin min qablu innahum kanoo qawman fasiqeena
Na kaumu ya Nuhu hapo mbele. Hakika hao walikuwa watu wapotovu.46
Maelezo
[46] Na kaumu ya Nuhu tuliihiliki kabla ya hawa. Hakika hao walikuwa watu walio toka nje ya ut'iifu wa Mwenyezi Mungu. -
وَٱلسَّمَآءَ بَنَيْنَـٰهَا بِأَيْي۟دٍ وَإِنَّا لَمُوسِعُونَ٤٧
Waalssamaa banaynaha biaydin wainna lamoosiʿoona
Na mbingu tumezifanya kwa nguvu na uwezo na hakika Sisi bila ya shaka ndio twenye uwezo wa kuzitanua.47
Maelezo
[47] Na mbingu tumeipanga kwa nguvu, na bila ya shaka Sisi ni waweza zaidi ya hayo. -
وَٱلْأَرْضَ فَرَشْنَـٰهَا فَنِعْمَ ٱلْمَـٰهِدُونَ٤٨
Waalarda farashnaha faniʿma almahidoona
Na ardhi tumeitandaza; basi watandazaji wazuri namna gani Sisi!48
Maelezo
[48] Na ardhi tumeikunjua, na Sisi ni wenye kuitengeneza vizuri kama kitanda. Aya hii tukufu inaashiria maana za kitaalamu nyingi; miongoni mwazo ni kwamba Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taa'la ameumba ulimwengu huu mkunjufu kwa nguvu. Na Yeye ni Muweza kwa atakayo. Na maana ya mbingu katika Aya hii ni kila kilicho juu ya kitu na kikakifunika. Basi kila kilicho zunguka sayari na nyota na mkusanyiko wa jua katika sehemu hii inayo onekana ya ulimwengu kimetanda kupita inavyo kadirika na akili, wala haiwezi kupimika. Kwani masafa yao hukisiwa kwa mamilioni ya miaka ya mwangaza. Na mwaka mmoja wa mwangaza kwa ilivyo thibiti kwa ilimu za kisasa katika karne hii ya ishirini ni masafa yanayo kwenda mwangaza kwa mbio za kilomita 300,000 kwa nukta moja ya dakika. Na ibara ya Aya tukufu (Na hakika Sisi ndio twenye kuutanua) inaashiria hayo, yaani kutanda huko kwa ulimwengu kunako staajabisha tangu kuumbwa kwake. Kama vile vile kuwa kukunjuka huko kungali kunaendelea, na hayo sayansi ya sasa imethibitisha vile vile. Na imejuulikana kwa nadhariya ya kutanda ambayo katika mwanzo mwanzo wa karne hii imethibiti kuwa ni kweli kiilimu, na ufupi wake ni kuwa ulimwengu unaendelea kukua na kupanuka, na kila sayari za mbinguni zinajitenga wenyewe kwa wenyewe. -
وَمِن كُلِّ شَىْءٍ خَلَقْنَا زَوْجَيْنِ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ٤٩
Wamin kulli shayin khalaqna zawjayni laʿallakum tathakkaroona
Na katika kila kitu tumeumba kwa jozi ili mzingatie.49
Maelezo
[49] Na kila kitu tumekiumba namna mbili, yaani kwa jozi, ili mpate kukumbuka muuamini uwezo wetu. -
فَفِرُّوٓا۟ إِلَى ٱللَّهِ ۖ إِنِّى لَكُم مِّنْهُ نَذِيرٌ مُّبِينٌ٥٠
Fafirroo ila Allahi innee lakum minhu natheerun mubeenun
Basi kimbilieni kwa Mwenyezi Mungu, hakika mimi ni mwonyaji kwenu wa kubainisha nitokae kwake.50
Maelezo
[50] Basi fanyeni haraka kuendea kwenye ut'iifu wa Mwenyezi Mungu. -
وَلَا تَجْعَلُوا۟ مَعَ ٱللَّهِ إِلَـٰهًا ءَاخَرَ ۖ إِنِّى لَكُم مِّنْهُ نَذِيرٌ مُّبِينٌ٥١
Wala tajʿaloo maʿa Allahi ilahan akhara innee lakum minhu natheerun mubeenun
Wala msifanye kuwa kuna mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu. Hakika mimi ni mwonyaji kwenu wa kubainisha nitokae kwake.51
Maelezo
[51] Wala msimfanye mungu mwengine kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu. Hakika mimi nimekujieni kwa amri ya Mwenyezi Mungu kukuonyeni kwa uwazi matokeo ya ushirikina. -
كَذَٰلِكَ مَآ أَتَى ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِم مِّن رَّسُولٍ إِلَّا قَالُوا۟ سَاحِرٌ أَوْ مَجْنُونٌ٥٢
Kathalika ma ata allatheena min qablihim min rasoolin illa qaloo sahirun aw majnoonun
Basi ndio hivyo hivyo, hakuwajia kabla yao Mtume ila walisema: Huyu ni mchawi au mwendawazimu.52
Maelezo
[52] Hivyo ndivyo ilivyo kuwa hali ya mataifa yote kwa Mitume wao. Hakuja Mtume kwa watu wa kabla ya kaumu yako ila walimwita: Mchawi au mwendawazimu. -
أَتَوَاصَوْا۟ بِهِۦ ۚ بَلْ هُمْ قَوْمٌ طَاغُونَ٥٣
Atawasaw bihi bal hum qawmun taghoona
Je! Wameambizana kwa haya? Bali hawa ni watu waasi.53
Maelezo
[53] Je! Mmeusiana, mmeambizana, nyinyi kwa nyinyi kusema hivyo ndio maana mnalirejea hilo kwa hilo? Bali hao ni watu walio pindukia mipaka, ndio wakawafikiana katika kuwashutumu Mitume! -
فَتَوَلَّ عَنْهُمْ فَمَآ أَنتَ بِمَلُومٍ٥٤
Fatawalla ʿanhum fama anta bimaloomin
Basi waachilie mbali, nawe hulaumiwi.54
Maelezo
[54] Basi wapuuzilie mbali hawa wenye inda! Wewe hulaumiki usipo wajibu kitu. -
وَذَكِّرْ فَإِنَّ ٱلذِّكْرَىٰ تَنفَعُ ٱلْمُؤْمِنِينَ٥٥
Wathakkir fainna alththikra tanfaʿu almumineena
Na kumbusha, kwani ukumbusho huwafaa Waumini.55
Maelezo
[55] Wewe dumisha kukumbusha, kwani ukumbusho huwazidisha Waumini kufumbua macho na kuwa na nguvu za yakini. -
وَمَا خَلَقْتُ ٱلْجِنَّ وَٱلْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ٥٦
Wama khalaqtu aljinna waalinsa illa liyaʿbudooni
Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi.56
Maelezo
[56] Wala sikuwaumba majini na watu kwa jambo la kuniletea Mimi manufaa, bali ili waniabudu, na kuniabudu Mimi ni manufaa kwao. -
مَآ أُرِيدُ مِنْهُم مِّن رِّزْقٍ وَمَآ أُرِيدُ أَن يُطْعِمُونِ٥٧
Ma oreedu minhum min rizqin wama oreedu an yutʿimooni
Na sitaki kwao riziki, wala sitaki wanilishe.Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kuruzuku, Mwenye nguvu, Madhubuti.57
Maelezo
[57] Sitaki kwao riziki, kwani Mimi si mhitaji kwa walimwengu wote; wala sitaki wanilishe, kwani Mimi ndiye ninaye lisha, wala silishwi. -
إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلرَّزَّاقُ ذُو ٱلْقُوَّةِ ٱلْمَتِينُ٥٨
Inna Allaha huwa alrrazzaqu thoo alquwwati almateenu
Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kuruzuku, Mwenye nguvu, Madhubuti.58
Maelezo
[58] Hakika Mwenyezi Mungu peke yake, ndiye mdhamini wa kuwapa riziki waja wake, na Yeye ndiye Mwenye nguvu, Aliye imara, hashindiki. -
فَإِنَّ لِلَّذِينَ ظَلَمُوا۟ ذَنُوبًا مِّثْلَ ذَنُوبِ أَصْحَـٰبِهِمْ فَلَا يَسْتَعْجِلُونِ٥٩
Fainna lillatheena thalamoo thanooban mithla thanoobi ashabihim fala yastaʿjiloona
Hakika walio dhulumu wana fungu lao la adhabu kama fungu la wenzao. Basi wasinihimize.59
Maelezo
[59] Hakika hao walio jidhulumu nafsi zao kwa ukafiri na kukanusha wana fungu lao la adhabu mfano wa fungu la wenzao katika kaumu zilizo kwisha pita. Basi wasifanye haraka kuhimiza adhabu ishuke kabla ya wakati wake. -
فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ كَفَرُوا۟ مِن يَوْمِهِمُ ٱلَّذِى يُوعَدُونَ٦٠
Fawaylun lillatheena kafaroo min yawmihimu allathee yooʿadoona
Ole wao walio ikanusha siku yao waliyo ahidiwa.60
Maelezo
[60] Basi maangamio yatawapata wenye kuikataa siku yao waliyo ahidiwa, kwa sababu ya shida na vitisho viliomo katika siku hiyo.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Surat Adh-Dhariyat maana yake ni nini?
Adh-Dhariyat maana yake ni “Pepo Zinazotawanya”.
Surat Adh-Dhariyat iko katika juzuu ya ngapi?
Surat Adh-Dhariyat inaenea katika juzuu za 26 na 27.
Surat Adh-Dhariyat ina aya ngapi?
Surat Adh-Dhariyat ina aya 60.
Surat Adh-Dhariyat ni ya Makka au ya Madina?
Surat Adh-Dhariyat ni sura ya Makka.
Surat Adh-Dhariyat ni sura ya ngapi katika Qur’ani?
Ni sura ya 51 katika Qur’ani.
Vyanzo
- Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
- Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
- Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
- Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
- Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
- Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.
Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.