سورة الطور

Surat At-Tur kwa Kiswahili

Mlima

Msahafu

Mishary Rashid AlafasyPakua MP3Pakua PDF

Surat At-Tur (الطور) ni sura ya 52 katika Qur’ani na ina aya 49. Jina lake lina maana ya “Mlima”. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na iko katika juzuu ya 27.

Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat At-Tur yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.

Surat At-Tur kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

  1. وَٱلطُّورِ۝١

    Waalttoori

    Naapa kwa mlima wa T'ur!1

    Maelezo
    [1] Ninaapa kwa mlima wa T'ur ulioko katika Sinai. Kwenye mlima huo ndio Nabii Musa a.s. alisemezwa.
  2. وَكِتَـٰبٍ مَّسْطُورٍ۝٢

    Wakitabin mastoorin

    Na Kitabu kilicho andikwa .2

    Maelezo
    [2] Ninaapa kwa mlima wa T'ur ulioko katika Sinai. Kwenye mlima huo ndio Nabii Musa a.s.
  3. فِى رَقٍّ مَّنشُورٍ۝٣

    Fee raqqin manshoorin

    Katika ngozi iliyo kunjuliwa!3

    Maelezo
    [3] Kilicho andikwa katika kurasa zilio nyepesi kuzisoma,
  4. وَٱلْبَيْتِ ٱلْمَعْمُورِ۝٤

    Waalbayti almaʿmoori

    Na kwa Nyumba iliyo jengwa!4

    Maelezo
    [4] Na kwa Nyumba iliyo jengwa kwa sababu ya wenye kuizunguka kwa ibada na wenye kusimama na kurukuu na kusujudu kwa Swala,
  5. وَٱلسَّقْفِ ٱلْمَرْفُوعِ۝٥

    Waalssaqfi almarfooʿi

    Na kwa dari iliyo nyanyuliwa!5

    Maelezo
    [5] Na naapa kwa mbingu iliyo nyanyuliwa bila ya nguzo, na bahari iliyo jaa.
  6. وَٱلْبَحْرِ ٱلْمَسْجُورِ۝٦

    Waalbahri almasjoori

    Na kwa bahari iliyo jazwa!6

    Maelezo
    [6] Na bahari iliyo jaa.
  7. إِنَّ عَذَابَ رَبِّكَ لَوَٰقِعٌ۝٧

    Inna ʿathaba rabbika lawaqiʿun

    Hakika adhabu ya Mola wako Mlezi hapana shaka itatokea.7

    Maelezo
    [7] Hakika adhabu ya Mola wako Mlezi waliyo ahidiwa makafiri bila ya shaka itawateremkia hapana hivi wala hivi.
  8. مَّا لَهُۥ مِن دَافِعٍ۝٨

    Ma lahu min dafiʿin

    Hapana wa kuizuia.8

    Maelezo
    [8] Hapana wa kuizuia isiwafikilie.
  9. يَوْمَ تَمُورُ ٱلسَّمَآءُ مَوْرًا۝٩

    Yawma tamooru alssamao mawran

    Siku zitakapo tikisika mbingu kwa mtikiso!9

    Maelezo
    [9] Siku mbingu itapo tikisika kwa mtikiso mkubwa.
  10. وَتَسِيرُ ٱلْجِبَالُ سَيْرًا۝١٠

    Wataseeru aljibalu sayran

    Na milima iwe inakwenda kwa mwendo mkubwa.10

    Maelezo
    [10] Na milima itapo ng'oka kutoka hapo ilipo kwa kuonekana khasa.
  11. فَوَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ۝١١

    Fawaylun yawmaithin lilmukaththibeena

    Basi ole wao siku hiyo hao wanao kadhibisha,11

    Maelezo
    [11] Maangamio makubwa yatawapata siku hiyo hao wanao kadhibisha Haki.
  12. ٱلَّذِينَ هُمْ فِى خَوْضٍ يَلْعَبُونَ۝١٢

    Allatheena hum fee khawdin yalʿaboona

    Ambao wanacheza katika mambo ya upuuzi.12

    Maelezo
    [12] Ambao katika upotovu ndio mchezo wao wanapo chezea.
  13. يَوْمَ يُدَعُّونَ إِلَىٰ نَارِ جَهَنَّمَ دَعًّا۝١٣

    Yawma yudaʿʿoona ila nari jahannama daʿʿan

    Siku watapo sukumwa kwenye Moto kwa msukumo wa nguvu,13

    Maelezo
    [13] Siku watakapo sukumwa kuingizwa Motoni kwa nguvu.
  14. هَـٰذِهِ ٱلنَّارُ ٱلَّتِى كُنتُم بِهَا تُكَذِّبُونَ۝١٤

    Hathihi alnnaru allatee kuntum biha tukaththiboona

    (Waambiwe): Huu ndio ule Moto mlio kuwa mkiukanusha!14

    Maelezo
    [14] Wataambiwa: Huu ndio Moto mlio kuwa mkiukanusha duniani.
  15. أَفَسِحْرٌ هَـٰذَآ أَمْ أَنتُمْ لَا تُبْصِرُونَ۝١٥

    Afasihrun hatha am antum la tubsiroona

    Je! Huu ni uchawi, au hamwoni tu?15

    Maelezo
    [15] Je! Bado mnaendelea kuukanya. Huu Moto mnao uona ni uchawi, au hamwoni tu?
  16. ٱصْلَوْهَا فَٱصْبِرُوٓا۟ أَوْ لَا تَصْبِرُوا۟ سَوَآءٌ عَلَيْكُمْ ۖ إِنَّمَا تُجْزَوْنَ مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ۝١٦

    Islawha faisbiroo aw la tasbiroo sawaon ʿalaykum innama tujzawna ma kuntum taʿmaloona

    Uingieni, mkistahamili au msistahamili - ni mamoja kwenu. Hakika mnalipwa kwa mliyo kuwa mkiyatenda.16

    Maelezo
    [16] Uingieni, mpate kuonja vukuto lake. Mkivumilia shida zake, au mkitovumilia, kwenu ni mamoja. Hakika leo mtayakuta mliyo kuwa mkiyatenda duniani.
  17. إِنَّ ٱلْمُتَّقِينَ فِى جَنَّـٰتٍ وَنَعِيمٍ۝١٧

    Inna almuttaqeena fee jannatin wanaʿeemin

    Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na neema,17

    Maelezo
    [17] Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani yenye wasaa, hapana awezae kuyaeleza yalivyo, na neema kubwa kadhaalika.
  18. فَـٰكِهِينَ بِمَآ ءَاتَىٰهُمْ رَبُّهُمْ وَوَقَىٰهُمْ رَبُّهُمْ عَذَابَ ٱلْجَحِيمِ۝١٨

    Fakiheena bima atahum rabbuhum wawaqahum rabbuhum ʿathaba aljaheemi

    Wakifurahi kwa yale aliyo wapa Mola wao Mlezi. Na Mola wao Mlezi atawalinda na adhabu ya Motoni.18

    Maelezo
    [18] Wakistarehe na neema alizo wapa Mola wao Mlezi, na Mola wao Mlezi akawalinda na adhabu ya Moto.
  19. كُلُوا۟ وَٱشْرَبُوا۟ هَنِيٓـًٔۢا بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ۝١٩

    Kuloo waishraboo haneean bima kuntum taʿmaloona

    Kuleni na kunyweni kwa raha kabisa kwa sababu ya mliyo kuwa mkiyatenda.19

    Maelezo
    [19] Wataambiwa: Kuleni chakula mpendacho, na kunyweni kwa raha, kuwa ni malipo ya vitendo mlivyo vitenda duniani.
  20. مُتَّكِـِٔينَ عَلَىٰ سُرُرٍ مَّصْفُوفَةٍ ۖ وَزَوَّجْنَـٰهُم بِحُورٍ عِينٍ۝٢٠

    Muttakieena ʿala sururin masfoofatin wazawwajnahum bihoorin ʿeenin

    Watakuwa wameegemea juu ya viti vya enzi vilivyo pangwa kwa safu. Na tutawaoza mahuru-l-aini.20

    Maelezo
    [20] Wakikaa nao wameegema juu ya makochi yaliyo pangwa kwa safu. Na tutawaoza wake weupe wenye macho ya vikombe wazuri.
  21. وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَٱتَّبَعَتْهُمْ ذُرِّيَّتُهُم بِإِيمَـٰنٍ أَلْحَقْنَا بِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ وَمَآ أَلَتْنَـٰهُم مِّنْ عَمَلِهِم مِّن شَىْءٍ ۚ كُلُّ ٱمْرِئٍۭ بِمَا كَسَبَ رَهِينٌ۝٢١

    Waallatheena amanoo waittabaʿathum thurriyyatuhum bieemanin alhaqna bihim thurriyyatahum wama alatnahum min ʿamalihim min shayin kullu imriin bima kasaba raheenun

    Na walio amini na dhuriya zao wakawafuata kwa Imani tutawakutanisha nao dhuriya zao, na wala hatutawapunja hata kidogo katika vitendo vyao. Kila mtu lazima atapata alicho kichuma.21

    Maelezo
    [21] Na walio amini, na wakastahiki vyeo vya juu, na vizazi vyao wakawafuata katika Imani, na wao hawajafikia daraja zile za baba zao, tutawakutanisha nao hao dhuriya zao, wapate kutulia nyoyo zao. Na wala hatuwapunguzii chochote katika thawabu za vitendo vyao. Wala wazazi hawatobeba chembe katika makosa ya dhuriya zao. Kwa sababu kila mtu amefungamana kwa rahani na vitendo vyake visio bebwa na mwenginewe.
  22. وَأَمْدَدْنَـٰهُم بِفَـٰكِهَةٍ وَلَحْمٍ مِّمَّا يَشْتَهُونَ۝٢٢

    Waamdadnahum bifakihatin walahmin mimma yashtahoona

    Na tutawapa matunda, na nyama kama watavyo penda.22

    Maelezo
    [22] Na tutawazidishia matunda mengi, na nyama kama waipendayo.
  23. يَتَنَـٰزَعُونَ فِيهَا كَأْسًا لَّا لَغْوٌ فِيهَا وَلَا تَأْثِيمٌ۝٢٣

    Yatanazaʿoona feeha kasan la laghwun feeha wala tatheemun

    Watapeana humo bilauri zisio na vinywaji vya kuleta maneno ya upuuzi wala dhambi.23

    Maelezo
    [23] Huko Peponi watakuwa wakipeana kwa mapenzi bilauri zilio jaa vinywaji visio leta maneno yasiyo na maana wala vitendo vya dhambi, yaani havilevi na kuondoa akili.
  24. ۞ وَيَطُوفُ عَلَيْهِمْ غِلْمَانٌ لَّهُمْ كَأَنَّهُمْ لُؤْلُؤٌ مَّكْنُونٌ۝٢٤

    Wayatoofu ʿalayhim ghilmanun lahum kaannahum luluon maknoonun

    Iwe wanawapitia watumishi wao kama kwamba ni lulu zilizomo katika chaza.24

    Maelezo
    [24] Na watakuwa wakiwapitia vijana walio wekwa kwa kuwatumikia, kwa weupe wao na usafi wao kama lulu iliomo ndani ya chaza.
  25. وَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَسَآءَلُونَ۝٢٥

    Waaqbala baʿduhum ʿala baʿdin yatasaaloona

    Wataelekeana wakiulizana.25

    Maelezo
    [25] Na watu wa Peponi watakabiliana wakiulizana wao kwa wao khabari za hayo mambo makuu wanayo yapata na sababu zake.
  26. قَالُوٓا۟ إِنَّا كُنَّا قَبْلُ فِىٓ أَهْلِنَا مُشْفِقِينَ۝٢٦

    Qaloo inna kunna qablu fee ahlina mushfiqeena

    Waseme: Tulikuwa zamani pamoja na ahali zetu tukiogopa;26

    Maelezo
    [26] Kabla ya neema hizi sisi tulikuwa pamoja na ahali zetu tukiiogopa adhabu ya Mwenyezi Mungu.
  27. فَمَنَّ ٱللَّهُ عَلَيْنَا وَوَقَىٰنَا عَذَابَ ٱلسَّمُومِ۝٢٧

    Famanna Allahu ʿalayna wawaqana ʿathaba alssamoomi

    Basi Mwenyezi Mungu akatufanyia hisani na akatulinda na adhabu ya upepo wa Moto.27

    Maelezo
    [27] Mwenyezi Mungu akatufadhili kwa rehema yake, na akatukinga na adhabu ya Moto.
  28. إِنَّا كُنَّا مِن قَبْلُ نَدْعُوهُ ۖ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلْبَرُّ ٱلرَّحِيمُ۝٢٨

    Inna kunna min qablu nadʿoohu innahu huwa albarru alrraheemu

    Hakika sisi zamani tulikuwa tukimwomba Yeye tu. Hakika Yeye ndiye Mwema Mwenye kurehemu.28

    Maelezo
    [28] Hakika sisi kabla ya haya tulikuwa duniani tukimuabudu Yeye tu. Yeye peke yake ndiye Mhisani Mkunjufu wa rehema.
  29. فَذَكِّرْ فَمَآ أَنتَ بِنِعْمَتِ رَبِّكَ بِكَاهِنٍ وَلَا مَجْنُونٍ۝٢٩

    Fathakkir fama anta biniʿmati rabbika bikahin wala majnoonin

    Basi kumbusha! Kwani wewe, kwa neema ya Mola wako Mlezi, si kuhani wala mwendawazimu.29

    Maelezo
    [29] Wewe endelea na kukumbusha kama unavyo fanya. Kwani wewe, kwa neema ya Mwenyezi Mungu aliyo kuneemesha kukupa Unabii na akili iliyo timia, si kuhani anaye toa khabari za ghaibu bila ya ilimu, wala si mwendawazimu unaye sema usiyo yasadiki.
  30. أَمْ يَقُولُونَ شَاعِرٌ نَّتَرَبَّصُ بِهِۦ رَيْبَ ٱلْمَنُونِ۝٣٠

    Am yaqooloona shaʿirun natarabbasu bihi rayba almanooni

    Au wanasema: Huyu ni mtunga mashairi, tunamtarajia kupatilizwa na dahari.30

    Maelezo
    [30] Bali ati wanasema huyu ni mtunga mashairi, tunaye mngojea afikiwe na mauti!
  31. قُلْ تَرَبَّصُوا۟ فَإِنِّى مَعَكُم مِّنَ ٱلْمُتَرَبِّصِينَ۝٣١

    Qul tarabbasoo fainnee maʿakum mina almutarabbiseena

    Sema: Tarajieni, na mimi pia ni pamoja nanyi katika kutarajia.31

    Maelezo
    [31] Waambie kwa kuwatisha: Ngojeeni, na mimi nami ni katika wanao ngojea mwisho wa hali yangu na hali yenu!
  32. أَمْ تَأْمُرُهُمْ أَحْلَـٰمُهُم بِهَـٰذَآ ۚ أَمْ هُمْ قَوْمٌ طَاغُونَ۝٣٢

    Am tamuruhum ahlamuhum bihatha am hum qawmun taghoona

    Au hizo akili zao ndio zinawaamrisha haya, au wao basi ni watu majeuri tu?32

    Maelezo
    [32] Bali ndio akili zao zinawaamrisha waseme maneno hayo yanayo gongana. Kwani kohani na mtunga mashairi ni watu wenye fahamu na akili; na mwendawazimu hana akili. Lakini hawa ni watu walio pita mipaka katika inadi zao.
  33. أَمْ يَقُولُونَ تَقَوَّلَهُۥ ۚ بَل لَّا يُؤْمِنُونَ۝٣٣

    Am yaqooloona taqawwalahu bal la yuminoona

    Au ndio wanasema: Ameitunga hii! Bali basi tu hawaamini!33

    Maelezo
    [33] Bali ati wanasema: Muhammad ameizua hii Qur'ani! Bali hawa kwa ukaidi wao hawaamini tu.
  34. فَلْيَأْتُوا۟ بِحَدِيثٍ مِّثْلِهِۦٓ إِن كَانُوا۟ صَـٰدِقِينَ۝٣٤

    Falyatoo bihadeethin mithlihi in kanoo sadiqeena

    Basi nawalete masimulizi kama haya ikiwa wao wanasema kweli.34

    Maelezo
    [34] Basi nawalete masimulizi kama haya ya Qur'ani, ikiwa wao ni wasema kweli kuwa Muhammad kaizua.
  35. أَمْ خُلِقُوا۟ مِنْ غَيْرِ شَىْءٍ أَمْ هُمُ ٱلْخَـٰلِقُونَ۝٣٥

    Am khuliqoo min ghayri shayin am humu alkhaliqoona

    Au wao wameumbwa pasipo kutokana na kitu chochote, au ni wao ndio waumbaji?35

    Maelezo
    [35] Kwani wao wameumbwa bila ya kuweko Muumbaji, au wao wamejiumba wenyewe, basi kwa hivyo ati ndio hawamtambui Muumbaji wa kumuabudu?
  36. أَمْ خَلَقُوا۟ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ ۚ بَل لَّا يُوقِنُونَ۝٣٦

    Am khalaqoo alssamawati waalarda bal la yooqinoona

    Au wao wameziumba mbingu na ardhi? Bali hawana na yakini.36

    Maelezo
    [36] Kwani wao ndio walio ziumba mbingu na ardhi kwa uumbaji mzuri wa pekee wa namna hii? Bali wao hawana na yakini na lolote lilio mwajibikia Muumbaji. Na kwa hivyo ndio wanamshirikisha.
  37. أَمْ عِندَهُمْ خَزَآئِنُ رَبِّكَ أَمْ هُمُ ٱلْمُصَۣيْطِرُونَ۝٣٧

    Am ʿindahum khazainu rabbika am humu almusaytiroona

    Au wanazo khazina za Mola wako Mlezi au wao ndio wenye madaraka?37

    Maelezo
    [37] Kwani wao wanazo khazina za Mola wako Mlezi wanazo zisarifu watakavyo? Au wana nguvu za kutenda watakavyo, na kupanga mambo kama wapendavyo?
  38. أَمْ لَهُمْ سُلَّمٌ يَسْتَمِعُونَ فِيهِ ۖ فَلْيَأْتِ مُسْتَمِعُهُم بِسُلْطَـٰنٍ مُّبِينٍ۝٣٨

    Am lahum sullamun yastamiʿoona feehi falyati mustamiʿuhum bisultanin mubeenin

    Au wanazo ngazi za kusikilizia? Basi huyo msikilizaji wao na alete hoja ilio wazi!38

    Maelezo
    [38] Bali wanacho kipandio cha kupandia mpaka mbinguni wakasikiliza anayo yahukumia Mwenyezi Mungu? Kama hivyo, basi nawamlete huyo mtu wao anaye sikiliza atoe hoja iliyo wazi kuthibitisha madai yake.
  39. أَمْ لَهُ ٱلْبَنَـٰتُ وَلَكُمُ ٱلْبَنُونَ۝٣٩

    Am lahu albanatu walakumu albanoona

    Au Yeye Mwenyezi Mungu ana wasichana, na nyinyi ndio mna wavulana?39

    Maelezo
    [39] Ati Mwenyezi Mungu ndiye mwenye mabinti, kama mnavyo zua, na nyinyi ndio mna watoto wa kiume kama ndio mnavyo penda?
  40. أَمْ تَسْـَٔلُهُمْ أَجْرًا فَهُم مِّن مَّغْرَمٍ مُّثْقَلُونَ۝٤٠

    Am tasaluhum ajran fahum min maghramin muthqaloona

    Au wewe unawaomba ujira, na kwa hivyo ndio wanaelemewa na uzito wa gharama?40

    Maelezo
    [40] Kwani wewe unawaomba chochote kuwa ni ujira wa kuwafikishia Ujumbe wako, ndio wamethakilika na hizo gharama wakalalimika?
  41. أَمْ عِندَهُمُ ٱلْغَيْبُ فَهُمْ يَكْتُبُونَ۝٤١

    Am ʿindahumu alghaybu fahum yaktuboona

    Au wanayo ilimu ya ghaibu, nao wameandika?41

    Maelezo
    [41] Bali kwani wao wanao ujuzi kujua mambo ya ghaibu, yaliyo fichikana, na hivyo wanaandika kutoka hayo wayatakayo?
  42. أَمْ يُرِيدُونَ كَيْدًا ۖ فَٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ هُمُ ٱلْمَكِيدُونَ۝٤٢

    Am yureedoona kaydan faallatheena kafaroo humu almakeedoona

    Au wanataka kufanya vitimbi tu? Lakini hao walio kufuru ndio watakao tegeka.42

    Maelezo
    [42] Au wanataka kukufanyia vitimbi tu na kuuharibu Ujumbe wako? Basi hao walio kufuru ndio wanao stahiki kutumbukia katika vitimbi vyao.
  43. أَمْ لَهُمْ إِلَـٰهٌ غَيْرُ ٱللَّهِ ۚ سُبْحَـٰنَ ٱللَّهِ عَمَّا يُشْرِكُونَ۝٤٣

    Am lahum ilahun ghayru Allahi subhana Allahi ʿamma yushrikoona

    Au wanae mungu asiye kuwa Mwenyezi Mungu? Subhanallah! Ametaksika Mwenyezi Mungu na hao wanao washirikisha naye.43

    Maelezo
    [43] Au wao wanae mungu wa kuabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu atakae walinda na adhabu ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu ametakasika na hayo wanayo mshirikisha naye!
  44. وَإِن يَرَوْا۟ كِسْفًا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ سَاقِطًا يَقُولُوا۟ سَحَابٌ مَّرْكُومٌ۝٤٤

    Wain yaraw kisfan mina alssamai saqitan yaqooloo sahabun markoomun

    Na hata wange ona pande linatoka mbinguni linaanguka wange sema: Ni mawingu yaliyo bebana.44

    Maelezo
    [44] Na wakiona kipande cha mbingu kinwaangukia kuwaadhibu wao husema, kwa inda tu: Ni mawingu yaliyo bebana!
  45. فَذَرْهُمْ حَتَّىٰ يُلَـٰقُوا۟ يَوْمَهُمُ ٱلَّذِى فِيهِ يُصْعَقُونَ۝٤٥

    Fatharhum hatta yulaqoo yawmahumu allathee feehi yusʿaqoona

    Basi waache mpaka wakutane na siku yao watakapo hilikishwa.45

    Maelezo
    [45] Waache bila ya kuwajali mpaka watakapo ikuta siku yao watapo angamizwa.
  46. يَوْمَ لَا يُغْنِى عَنْهُمْ كَيْدُهُمْ شَيْـًٔا وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ۝٤٦

    Yawma la yughnee ʿanhum kayduhum shayan wala hum yunsaroona

    Siku ambayo hila zao hazitawafaa hata kidogo, wala wao hawatanusuriwa.46

    Maelezo
    [46] Siku ambayo hila zao hazitawakinga hata na chembe ya adhabu, wala hawatapata wa kuwanusuru.
  47. وَإِنَّ لِلَّذِينَ ظَلَمُوا۟ عَذَابًا دُونَ ذَٰلِكَ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ۝٤٧

    Wainna lillatheena thalamoo ʿathaban doona thalika walakinna aktharahum la yaʿlamoona

    Na hakika walio dhulumu watapata adhabu nyengine isiyo kuwa hii, lakini wengi wao hawajui.47

    Maelezo
    [47] Na hakika hao walio dhulumu watapata adhabu mbali na hii waliyo teseka nayo hapa duniani, lakini wengi wao hawajui hayo.
  48. وَٱصْبِرْ لِحُكْمِ رَبِّكَ فَإِنَّكَ بِأَعْيُنِنَا ۖ وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ حِينَ تَقُومُ۝٤٨

    Waisbir lihukmi rabbika fainnaka biaʿyunina wasabbih bihamdi rabbika heena taqoomu

    Na ingojee hukumu ya Mola wako Mlezi. Kwani wewe hakika uko mbele ya macho yetu, na mtakase kwa kumsifu Mola wako Mlezi unapo simama,48

    Maelezo
    [48] Wewe isubirie hukumu ya Mola wako Mlezi ya kuwapa muhula hao, na wewe kupata maudhi yao. Kwani hakika wewe umo katika hifadhi yetu na ulinzi wetu. Basi vitimbi vyao havitokudhuru wewe. Na mtakase kwa kumsifu Mola wako Mlezi unapo amka.
  49. وَمِنَ ٱلَّيْلِ فَسَبِّحْهُ وَإِدْبَـٰرَ ٱلنُّجُومِ۝٤٩

    Wamina allayli fasabbihhu waidbara alnnujoomi

    Na usiku pia mtakase, na zinapo kuchwa nyota.49

    Maelezo
    [49] Na tafuta usiku usiku nafasi ya kumsabihi, yaani kumtakasa, Mwenyezi Mungu, na mtakase pia wakati zinapo kuchwa nyota, yaani alfajiri.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Surat At-Tur maana yake ni nini?

At-Tur maana yake ni “Mlima”.

Surat At-Tur iko katika juzuu ya ngapi?

Surat At-Tur iko katika juzuu ya 27.

Surat At-Tur ina aya ngapi?

Surat At-Tur ina aya 49.

Surat At-Tur ni ya Makka au ya Madina?

Surat At-Tur ni sura ya Makka.

Surat At-Tur ni sura ya ngapi katika Qur’ani?

Ni sura ya 52 katika Qur’ani.

Vyanzo

  • Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
  • Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
  • Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
  • Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
  • Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
  • Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.

Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.

Mipangilio ya kusoma

Fonti ya Qur’ani
Ukubwa wa Kiarabu
100%
Ukubwa wa tafsiri
100%
Mandhari

Ongeza kwenye skrini ya kwanza

ReadSurahFungua ReadSurah kutoka skrini ya kwanza, kwa skrini nzima. Sura ulizosoma hufunguka hata bila intaneti.

  1. Katika Safari, gusa kitufe cha kushiriki (Share). Kwenye iPhone mpya kiko kwenye menyu ya •••.
  2. Gusa “Add to Home Screen”. Huenda ukahitaji kusogeza chini.
  3. Gusa “Add”.